10 – Ubatizo

Haya ni maneno matakatifu ya Mungu Mwenyezi.
Hatupendi maneno ya wanadamu.
Kwa mtu yeyote anayempenda Mungu... hivi ndivyo Mungu anasema kuhusu: Ubatizo.

Mistari 3 Muhimu Zaidi

Yesu akamwambia, “Amin, amin nakuambia, hakuna mtu ye yote anayeweza kuingia katika Ufalme wa Mungu isipokuwa amezaliwa kwa maji na kwa Roho. Mwili huzaa mwili, lakini Roho huzaa roho.

Petro akawajibu, “Tubuni, mkabatizwe kila mmoja wenu kwa jina la Yesu Kristo, ili mpate kusamehewa dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

(Watu wote hata watoza ushuru waliposikia maneno ya Yesu, walikubali kwamba mpango wa Mungu ni mwema, maana walikuwa wamebatizwa na Yohana. Lakini Mafarisayo na wataalamu wa sheria walikataa mpango wa Mungu kwao kwa kutokukubali kubatizwa na Yohana.)

Kila Mstari katika Mpangilio wa Biblia - 61 vifungu

Wakati huu Dunia ilikuwa haina umbo, tena ilikuwa tupu, giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji, naye Roho wa Mungu alikuwa ametanda juu ya maji.

Kwa hiyo tahirini mioyo yenu, na msiwe na shingo ngumu tena.

Unioshe na uovu wangu wote na unitakase dhambi yangu.

Unioshe kwa hisopo, nami nitakuwa safi, unisafishe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji.

jiosheni na mkajitakase. Yaondoeni matendo yenu maovu mbele zangu! Acheni kutenda mabaya,

Ee Yerusalemu, uusafishe uovu kutoka moyoni mwako na uokolewe. Utaendelea kuficha mawazo mapotovu mpaka lini?

Nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi, nitawatakasa kutoka katika uchafu wenu wote na kutoka katika sanamu zenu zote. Nitawapa moyo mpya na kuweka roho mpya ndani yenu, nitaondoa ndani yenu moyo wenu wa jiwe na kuwapa moyo wa nyama. Nami nitaweka Roho yangu ndani yenu na kuwafanya ninyi mfuate amri zangu na kuwafanya kuwa waangalifu kuzishika sheria zangu.

Watu walimwendea kutoka Yerusalemu, Uyahudi yote na nchi zote za kandokando ya Mto Yordani. Nao wakaziungama dhambi zao, akawabatiza katika Mto Yordani. Lakini alipowaona Mafarisayo na Masadukayo wengi wakija ili kubatizwa, aliwaambia, “Ninyi watoto wa nyoka! Ni nani aliyewaonya kuikimbia ghadhabu inayokuja? Basi zaeni matunda yastahiliyo toba.

Hata sasa shoka limekwisha kuwekwa tayari kwenye mizizi ya mti. Kila mti usiozaa matunda mazuri, hukatwa na kutupwa motoni. “Mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba. Lakini nyuma yangu anakuja yeye aliye na uwezo kuliko mimi, ambaye sistahili hata kuvichukua viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. Chombo chake cha kupuria kiko mkononi mwake, naye atasafisha sakafu yake ya kupuria, akiikusanya ngano yake ghalani na kuyachoma makapi kwa moto usiozimika.”

Kisha Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Mto Yordani ili Yohana ambatize. Lakini Yohana akajitahidi kumzuia, akimwambia, “Mimi ninahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu nikubatize?” Lakini Yesu akamjibu, “Kubali hivi sasa, kwa maana ndivyo itupasavyo kwa njia hii kuitimiza haki yote.” Hivyo Yohana akakubali. Naye Yesu alipokwisha kubatizwa, mara alipotoka ndani ya maji, ghafula mbingu zikamfungukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua na kutulia juu yake. Nayo sauti kutoka mbinguni ikasema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa, ambaye ninapendezwa sana naye.”

Yesu akawajibu, “Nami nitawauliza swali moja. Kama mkinijibu, mimi nitawaambia ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya. Ubatizo wa Yohana, ulitoka wapi? Je, ulitoka mbinguni au kwa wanadamu?” Wakaanza kuhojiana wao kwa wao na kusema, “Tukisema ulitoka mbinguni atatuuliza, ‘Mbona basi hamkumwamini?’ Lakini tukisema, ‘Ulitoka kwa wanadamu’, tunawaogopa hawa watu, maana wote wanamtambua Yohana kuwa ni nabii.” Kwa hiyo wakamjibu Yesu, “Sisi hatujui.” Ndipo akawaambia, “Wala mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani ninatenda mambo haya.”

Kwa sababu hii, enendeni ulimwenguni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, nanyi wafundisheni kuyashika mambo yote niliyowaamuru ninyi. Hakika mimi niko pamoja nanyi siku zote, hadi mwisho wa nyakati.” Amen.

Yohana alikuja, akibatiza huko nyikani, akihubiri ubatizo wa toba kwa ajili ya ondoleo la dhambi. Watu kutoka Uyahudi wote na sehemu zote za Yerusalemu walikuwa wakimwendea, naye akawabatiza katika Mto Yordani, wakitubu dhambi zao. Yohana alivaa mavazi yaliyotengenezwa kwa singa za ngamia na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu. Naye alihubiri akisema, “Baada yangu atakuja yeye aliye na uwezo kuliko mimi, ambaye sistahili hata kuinama na kulegeza kamba za viatu vyake. Mimi nawabatiza kwa maji, lakini yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu.”

Wakati huo Yesu akaja kutoka Nazareti ya Galilaya, naye akabatizwa na Yohana katika Mto Yordani. Yesu alipokuwa akitoka ndani ya maji, aliona mbingu zikifunguka na Roho akishuka juu yake kama hua. Nayo sauti kutoka mbinguni ikasema, “Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu, ambaye nimependezwa nawe.”

Yesu akawajibu, “Nitawauliza swali moja. Nijibuni, nami nitawaeleza ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya. Niambieni, ubatizo wa Yohana ulitoka mbinguni au kwa wanadamu?” Wakasemezana wao kwa wao, wakisema, “Kama tukisema, ‘Ulitoka mbinguni,’ atatuuliza, ‘Mbona hamkumwamini?’ Lakini tukisema, ‘Ulitoka kwa wanadamu,’…” (Waliwaogopa watu, kwa sababu kila mtu aliamini kwamba Yohana alikuwa nabii kweli kweli.) Kwa hiyo wakamjibu Yesu, “Hatujui.” Naye Yesu akawaambia, “Wala mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya.”

Akawaambia, “Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Ye yote aaminiye na kubatizwa ataokoka. Lakini ye yote asiyeamini atahukumiwa. Nazo ishara hizi zitafuatana na wale waaminio: Kwa Jina langu watatoa pepo wachafu, watasema kwa lugha mpya,

Akaenda katika nchi yote kandokando ya Mto Yordani, akihubiri ubatizo wa toba kwa ajili ya msamaha wa dhambi.

Yohana akauambia ule umati wa watu uliokuwa unakuja ili kubatizwa naye, “Enyi uzao wa nyoka! Ni nani aliyewaonya mwikimbie ghadhabu ijayo? Zaeni matunda yafananayo na toba yenu. Wala msianze kusema mioyoni mwenu kuwa ninyi ni uzao wa Abrahamu. Kwa maana nawaambia, Mungu anaweza kumwinulia Abrahamu watoto kutoka katika mawe haya. Hata sasa shoka limekwisha wekwa tayari kwenye shina la kila mti, basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni.”

Watoza ushuru nao wakaja ili wabatizwe, wakamwuliza, “Bwana na sisi inatupasa tufanyeje?”

Yohana akawajibu akawaambia, “Mimi nawabatiza kwa maji. Lakini atakuja aliye na nguvu kuliko mimi ambaye sistahili hata kufungua kamba ya viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. Pepeto lake liko mkononi, tayari kusafisha sakafu yake ya kupuria na kuikusanya ngano ghalani, lakini makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.”

Baada ya watu wote kubatizwa, Yesu naye akabatizwa. Naye alipokuwa akiomba, mbingu zilifunguka. Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa umbo kama la hua na sauti ikaja kutoka mbinguni ikisema: “Wewe ni Mwanangu mpendwa wangu, ninayependezwa nawe sana.”

(Watu wote hata watoza ushuru waliposikia maneno ya Yesu, walikubali kwamba mpango wa Mungu ni mwema, maana walikuwa wamebatizwa na Yohana. Lakini Mafarisayo na wataalamu wa sheria walikataa mpango wa Mungu kwao kwa kutokukubali kubatizwa na Yohana.)

Kisha Yohana akatoa ushuhuda huu: “Nilimwona Roho akishuka kutoka mbinguni kama hua, akakaa juu yake. Mimi nisingemtambua, lakini yeye aliyenituma nibatize kwa maji alikuwa ameniambia, ‘Yule mtu utakayemwona Roho akimshukia na kukaa juu yake, huyo ndiye atakayebatiza kwa Roho Mtakatifu.’ Mimi mwenyewe nimeona jambo hili na ninashuhudia kuwa huyu ndiye Mwana wa Mungu.”

Yesu akamjibu, “Amin, amin nakuambia, mtu hawezi kuuona Ufalme wa Mungu asipozaliwa mara ya pili.” Nikodemo akauliza, “Awezaje mtu kuzaliwa wakati akiwa mzee? Hakika hawezi kuingia mara ya pili kwenye tumbo la mama yake ili azaliwe!” Yesu akamwambia, “Amin, amin nakuambia, hakuna mtu ye yote anayeweza kuingia katika Ufalme wa Mungu isipokuwa amezaliwa kwa maji na kwa Roho. Mwili huzaa mwili, lakini Roho huzaa roho. Kwa hiyo usishangae ninapokuambia huna budi ‘kuzaliwa mara ya pili.’

Baada ya haya, Yesu na wanafunzi wake walikwenda katika nchi ya Uyahudi, nao wakakaa huko kwa muda na kubatiza. Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni karibu na Salimu kwa sababu huko kulikuwa na maji tele. Watu wazima wakamjia huko ili kubatizwa.

Mashindano yakazuka kati ya baadhi ya wanafunzi wa Yohana na Myahudi mmoja kuhusu suala la desturi ya kunawa. Wakamwendea Yohana wakamwambia, “Rabi, yule mtu aliyekuwa pamoja nawe ng'ambo ya pili ya Mto Yordani, yule uliyeshuhudia habari zake, sasa anabatiza na kila mtu anamwendea!” Yohana akawajibu, “Hakuna mtu ye yote awezaye kupata kitu cho chote isipokuwa kile tu alichopewa kutoka mbinguni.

Mafarisayo wakasikia kwamba Yesu alikuwa anapata na kubatiza wanafunzi wengi zaidi kuliko Yohana, ingawa kwa kweli si Yesu mwenyewe aliyekuwa akibatiza, ila ni wanafunzi wake. Bwana alipojua mambo haya, aliondoka Uyahudi akarudi tena Galilaya.

“Kama mnanipenda, mtazishika amri zangu.

Wakati mmoja alipokuwa pamoja nao, aliwapa amri hii, “Msitoke humu Yerusalemu, bali ingojeni ahadi ya Baba, ambayo mmenisikia nikisema habari zake. Yohana aliwabatiza kwa maji, lakini baada ya siku hizi chache mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.”

Ilipowadia siku ya Pentekoste, walikuwa wote mahali pamoja. Ghafula sauti kama mvumo mkubwa wa upepo uliotoka mbinguni, ukaijaza nyumba yote walimokuwa wameketi. Zikatokea ndimi kama za moto zilizogawanyika na kukaa juu ya kila mmoja wao. Wote wakajazwa na Roho Mtakatifu, wakaanza kunena kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia.

Petro akawajibu, “Tubuni, mkabatizwe kila mmoja wenu kwa jina la Yesu Kristo, ili mpate kusamehewa dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

Wale wote waliopokea ujumbe wa Petro kwa furaha wakabatizwa na siku ile waliongezeka watu wapatao 3,000. Nao wakawa wanadumu katika mafundisho ya mitume, katika ushirika, katika kumega mkate na katika kusali. Kila mtu akaingiwa na hofu ya Mungu, nayo miujiza mingi na ishara zikafanywa na mitume.

Lakini watu walipomwamini Filipo akihubiri habari njema za Ufalme wa Mungu na jina la Yesu Kristo, wakabatizwa wanaume na wanawake. Simoni naye akaamini na akabatizwa. Akamfuata Filipo kila mahali, akistaajabishwa na ishara kuu na miujiza aliyoiona.

Basi mitume waliokuwa Yerusalemu waliposikia kuwa Samaria wamelipokea neno la Mungu, wakawatuma Petro na Yohana waende huko. Nao walipofika wakawaombea ili wampokee Roho Mtakatifu, kwa sababu Roho Mtakatifu alikuwa bado hajawashukia hata mmoja ila wamebatizwa tu katika jina la Bwana Yesu. Ndipo Petro na Yohana wakaweka mikono yao juu ya wale waliobatizwa, nao wakapokea Roho Mtakatifu.

Walipokuwa wakiendelea na safari wakafika mahali palipokuwa na maji, yule towashi akamwambia Filipo, “Tazama, hapa kuna maji. Kitu gani kitanizuia nisibatizwe?” ( Filipo akamwambia, “Kama ukiamini kwa moyo wako wote unaweza kubatizwa.” Akajibu, “Naamini kuwa Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu).” Naye akaamuru lile gari lisimamishwe. Wakatelemka kwenye maji wote wawili, yule towashi na Filipo, naye Filipo akambatiza. Nao walipopanda kutoka kwenye maji, ghafula Roho wa Bwana akamnyakua Filipo, naye towashi hakumwona tena, lakini akaenda zake akifurahi. Filipo akajikuta yuko Azoto, akasafiri akihubiri injili katika miji yote mpaka alipofika Kaisaria.

Ghafula vitu kama magamba vikaanguka chini, kutoka machoni mwa Sauli, akapata kuona tena. Akasimama, akabatizwa.

“Je, kuna mtu ye yote anayeweza kuzuia watu hawa wasibatizwe kwa maji? Wamempokea Roho Mtakatifu kama sisi tulivyompokea.” Kwa hiyo akaamuru wabatizwe kwa jina la Yesu Kristo. Wakamsihi Petro akae nao kwa siku chache.

Nami nikakumbuka neno la Bwana alivyosema, ‘Yohana alibatiza kwa maji, lakini ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu.’ Basi ikiwa Mungu aliwapa hawa watu kipawa kile kile alichotupa sisi tuliomwamini Bwana Yesu, mimi ni nani hata nifikirie kuwa ningeweza kumpinga Mungu?” Waliposikia haya hawakuwa na la kupinga zaidi. Nao wakamwadhimisha Mungu wakisema, “Basi, Mungu amewapa hata watu Mataifa toba iletayo uzima wa milele.”

“Kutoka katika uzao wa mtu huyu, Mungu amewaletea Israeli Mwokozi Yesu, kama alivyoahidi. Kabla ya kuja kwa Yesu, Yohana alihubiri toba na ubatizo kwa watu wote wa Israeli.

Mmoja wa wale wanawake waliotusikiliza aliitwa Lidia, mfanya biashara wa nguo za zambarau, mwenyeji wa mji wa Thiatira, aliyekuwa mcha Mungu. Bwana akaufungua moyo wake akaupokea ujumbe wa Paulo. Basi alipokwisha kubatizwa yeye na watu wa nyumbani mwake, alitukaribisha nyumbani mwake akisema, “Kama mmeona kweli mimi nimemwamini Bwana, karibuni mkae nyumbani mwangu.” Naye akatushawishi.

Wakamjibu, “Mwamini Bwana Yesu Kristo, nawe utaokoka, pamoja na wa nyumbani mwako.” Wakamwambia neno la Bwana yeye pamoja na wote waliokuwako nyumbani mwake. Wakati ule ule yule mkuu wa gereza akawachukua akawaosha majeraha yao, kisha akabatizwa yeye pamoja na wote waliokuwa nyumbani mwake bila kuchelewa.

Kiongozi wa hilo sinagogi, aliyeitwa Krispo, akamwamini Bwana pamoja na wote wa nyumbani mwake, nao Wakorintho wengi waliomsikia Paulo wakaamini na kubatizwa.

akawauliza, “Je, mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini?” Wakajibu, “Hapana, hata hatukusikia kuwa kuna Roho Mtakatifu.” Ndipo Paulo akawauliza, “Je, mlibatizwa kwa ubatizo gani?” Wakajibu, “Kwa ubatizo wa Yohana.” Paulo akasema, “Ubatizo wa Yohana ulikuwa wa toba, aliwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja baada yake, yaani, Yesu.” Waliposikia haya, wakabatizwa katika jina la Yesu. Paulo alipoweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akawashukia, nao wakanena kwa lugha mpya na kutabiri.

Sasa basi, mbona unakawia? Inuka, ukabatizwe na dhambi zako zikasafishwe, ukiliita Jina lake.’

Au hamjui ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Kwa hiyo tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti, ili kama vile Kristo alivyofufuka kutoka kwa wafu kwa utukufu wa Baba, vivyo hivyo sisi nasi pia tupate kuenenda katika upya wa uzima. Kwa maana ikiwa tumeungana naye katika mauti yake, bila shaka tutaungana naye katika ufufuo wake. Kwa maana twajua kwamba utu wetu wa kale ulisulibiwa pamoja naye ili ule mwili wa dhambi upate kuangamizwa, nasi tusiendelee kuwa tena watumwa wa dhambi. Kwa maana mtu ye yote aliyekufa amewekwa huru mbali na dhambi. Basi ikiwa tulikufa pamoja na Kristo, tunaamini kwamba pia tutaishi pamoja naye.

Vivyo hivyo, jihesabuni wafu katika dhambi lakini mlio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu.

Lakini kama Kristo anakaa ndani yenu, miili yenu imekufa kwa sababu ya dhambi, lakini roho zenu zi hai kwa sababu ya haki.

Baadhi yenu mlikuwa kama hao. Lakini mlioshwa, mlitakaswa, mlihesabiwa haki kwa jina la Bwana Yesu Kristo na katika Roho wa Mungu wetu.

Kwa maana katika Roho mmoja wote tulibatizwa katika mwili mmoja, kama ni Wayahudi au Wayunani, kama ni watumwa au watu huru, nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.

Kwa hiyo kama mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita, tazama, yamekuwa mapya.

Kwa maana ninyi nyote mmekuwa watoto wa Mungu katika Kristo Yesu kwa njia ya imani. Kwa maana wote mliobatizwa ndani ya Kristo, mmemvaa Kristo.

Kwa habari zenu, mlikuwa wafu katika makosa na dhambi zenu,

hata tulipokuwa wafu kwa ajili ya makosa yetu, alitufanya tuwe hai pamoja na Kristo Yesu, yaani, mmeokolewa kwa neema. Mungu alitufufua pamoja na Kristo na kutuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho katika Kristo Yesu,

Kuna mwili mmoja na Roho mmoja, kama vile mlivyoitwa katika tumaini moja. Tena kuna Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja,

kusudi alifanye takatifu, akilitakasa kwa kuliosha kwa maji katika Neno lake, apate kujiletea Kanisa tukufu lisilo na doa wala kunyanzi au waa lo lote, bali takatifu lisilo na hatia.

Katika Kristo pia mlitahiriwa kwa kutengwa mbali na asili ya dhambi, si kwa tohara inayofanywa kwa mikono ya wanadamu bali kwa ile tohara iliyofanywa na Kristo, mkiwa mmezikwa pamoja naye katika ubatizo na kufufuliwa pamoja naye kwa njia ya imani yenu katika uweza wa Mungu aliyemfufua kutoka kwa wafu.

Kwa hiyo, tukiachana na mafundisho yale ya awali kuhusu Kristo na tusonge mbele ili tufikie utimilifu, si kuweka tena msingi wa mafundisho ya kuzitubia kazi zisizo na uhai na imani katika Mungu, yaani, mafundisho kuhusu aina za ubatizo, kuwekea watu mikono, ufufuo wa wafu na hukumu ya milele. Mungu akitujalia tutafanya hivyo.

Kwa hiyo, ndugu zangu, kwa kuwa tunao ujasiri wa kupaingia Patakatifu pa Patakatifu kwa damu ya Yesu, kwa njia mpya iliyo hai tuliyofunguliwa kwa ajili yetu kupitia kwenye lile pazia, yaani, mwili wake, basi kwa kuwa tunaye Kuhani Mkuu juu ya nyumba ya Mungu, sisi na tumkaribie Mungu kwa moyo mnyofu kwa imani timilifu, mioyo yetu ikiwa imenyunyizwa damu ya Kristo na kuwa safi kutokana na dhamiri mbaya nayo miili yetu ikiwa imeoshwa kwa maji safi.

Basi kwa kuwa mmejitakasa nafsi zenu kwa kuitii ile kweli kwa njia ya Roho kwa kuwapenda ndugu zenu kwa upendo wa kweli, pendaneni kwa dhati kutoka moyoni. Kwa maana mmezaliwa upya, si kwa mbegu ile iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika, kwa neno la Mungu lililo hai na linalodumu hata milele.

Nayo maji hayo ni kielelezo cha ubatizo ambao sasa unawaokoa ninyi pia, si kwa kuondoa uchafu kwenye mwili, bali kama ahadi ya dhamiri safi kwa Mungu, kwa njia ya ufufuo wa Yesu Kristo,

“Wamebarikiwa wale wafuao mavazi yao, ili wapate haki ya kuuendea huo mti wa uzima na kuuingia huo mji kupitia kwenye malango yake.

Swahili - Kiswahili - SW

NEN'2014 - Neno Bibilia Takatifu Kiswahili Contemporary Version - 2014

This Bible text is from Biblica Open Kiswahili Contemporary Version Neno 2015
https://open.bible/bibles/swahili-biblica-text-bible/
provided by: Biblica Inc, available by Creative Commons CC-BY-SA-4.0,
and this new compilation is shared as www.creativecommons.org/licenses/by-sa/4.0.
Languages are made available to you by www.ipedge.net