11 – Dhambi
Haya ni maneno matakatifu ya Mungu Mwenyezi.
Hatupendi maneno ya wanadamu.
Kwa mtu yeyote anayempenda Mungu... hivi ndivyo Mungu anasema kuhusu: Dhambi.
Haya ni maneno matakatifu ya Mungu Mwenyezi.
Hatupendi maneno ya wanadamu.
Kwa mtu yeyote anayempenda Mungu... hivi ndivyo Mungu anasema kuhusu: Dhambi.
Kama tukiendelea kutenda dhambi kwa makusudi baada ya kupokea ufahamu wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi. Lakini kinachobaki ni kungoja kwa hofu hukumu ya moto uwakao utakaowaangamiza adui za Mungu.
”Hawakulishika Agano la Mungu na walikataa kuishi kwa sheria yake.
”Niliwaambia kuwa mtakufa katika dhambi zenu, kwa maana msipoamini ya kwamba ‘Mimi Ndiye,’ mtakufa katika dhambi zenu.”
”BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akamwambia, “Uko huru kula matunda ya mti wo wote katika bustani, lakini kamwe usile matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, kwa maana siku utakapokula matunda yake, hakika utakufa.”
”Mwanamke alipoona ya kuwa tunda la mti huo lilikuwa zuri kwa chakula na la kupendeza macho, tena linatamanika kwa kujipatia hekima, basi akachuma katika matunda yake, akala, pia akampa mumewe, aliyekuwa pamoja naye, naye akala.
”Ndipo macho yao wote wawili yakafumbuliwa, wakajiona kwamba walikuwa uchi; hivyo wakashona majani ya mtini, wakajifunika. Ndipo yule mwanaume na mkewe, waliposikia sauti ya BWANA Mungu alipokuwa akitembea bustanini wakati wa utulivu wa jioni, wakajificha kutoka mbele za BWANA Mungu katikati ya miti ya bustani. Lakini BWANA Mungu akamwita Adamu, “Uko wapi?” Naye akajibu, “Nilikusikia katika bustani nikaogopa kwa sababu nilikuwa uchi, hivyo nikajificha.” Mungu akamwuliza, “Ni nani aliyekuambia yakuwa ulikuwa uchi? Je, umekula matunda ya mti niliokuamuru usile?”
”Adamu akasema, “Huyu mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa sehemu ya tunda kutoka kwenye huo mti, nami nikala.” Ndipo BWANA Mungu akamwuliza mwanamke, “Ni nini hili ambalo umelifanya?” Mwanamke akajibu, “Nyoka alinidanganya, nami nikala.”
”Kisha BWANA Mungu akasema, “Sasa mtu huyu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya. Sharti asiruhusiwe kunyosha mkono wake na kuchuma pia kutoka katika mti wa uzima akala, naye akaishi milele.” Hivyo BWANA Mungu akamfukuzia mbali kutoka Bustani ya Edeni, akalime ardhi ambamo alitolewa. Baada ya kumfukuzia mbali Adamu, Mungu akaweka makerubi mashariki ya Bustani ya Edeni, pamoja na upanga wa moto ukimulika huku na huko kulinda njia ya kuuendea mti wa uzima.
”lakini Mungu hakumkubali Kaini pamoja na sadaka yake. Kwa hiyo Kaini akakasirika sana, uso wake ukawa na huzuni. Kisha BWANA akamwambia Kaini, “Kwa nini umekasirika? Kwa nini uso wako una huzuni? Ukifanya lililo sawa, hutakubalika? Lakini usipofanya lililo sawa, dhambi inakuvizia mlangoni mwako, inakutamani wewe, lakini inakupasa uishinde.” Basi Kaini akamwambia ndugu yake Abeli, “Twende shambani.” Walipokuwa shambani, Kaini akamshambulia Abeli ndugu yake, akamwua.
”BWANA akaona jinsi ambavyo uovu wa mwanadamu umekuwa mkubwa duniani na ya kuwa kila mwelekeo wa mawazo ya moyo wake wakati wote ulikuwa mbaya tu.
”Basi BWANA akasema, “Kilio dhidi ya Sodoma na Gomora ni kikubwa sana na dhambi yao inasikitisha sana,
”Usiwe na miungu mingine ila mimi. Usijifanyie sanamu ya kuchonga katika umbo la kitu cho chote kilicho juu mbinguni, au duniani chini, au ndani ya maji. Usivisujudie au kuviabudu; kwa kuwa Mimi, BWANA Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, ninayewaadhibu watoto kwa ajili ya dhambi ya baba zao hadi kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, lakini ninaonyesha upendo kwa vizazi elfu vya wale wanipendao na kuzishika amri zangu.
”Usilitaje bure jina la BWANA Mungu wako, kwa kuwa BWANA hataacha kumhesabia hatia yeye alitajaye jina lake bure.
”Usiue. Usizini. Usiibe. Usitoe ushuhuda wa uongo dhidi ya jirani yako. Usiitamani nyumba ya jirani yako. Usimtamani mke wa jirani yako, wala mtumishi wake wa kiume au wa kike, wala ng'ombe wake au punda wake, wala cho chote kile alicho nacho jirani yako.”
”Mose akawaambia watu, “Msiogope! Mungu amekuja kuwajaribu, ili kwamba hofu ya Mungu iwakalie, msitende dhambi.”
”“Ye yote amshambuliaye baba yake au mama yake ni lazima auawe. “Ye yote amtekaye nyara mwingine akamuuza au akamweka kwake, akikamatwa ni lazima auawe. “Ye yote atakayemlaani baba yake au mama yake ni lazima auawe.
”“Mtu ye yote aziniye na mnyama lazima auawe.
”“Usieneze habari za uongo. Usimsaidie mtu mwovu kwa kuwa shahidi mwenye nia ya kudhuru wengine.
”“ ‘Wakati mtu ye yote atakapokuwa na hatia katika mojawapo ya haya, lazima akiri kuwa ni kwa njia gani ametenda dhambi,
”“ ‘Usikutane kimwili na mke wa jirani yako na kujitia naye unajisi.
”“ ‘Usimtoe mtoto wako ye yote awe kafara kwa mungu Moleki, kamwe usilinajisi jina la Mungu wako. Mimi ndimi BWANA.
”“ ‘Usikutane kimwili na mwanaume kama mtu akutanaye na mwanamke; hilo ni chukizo.
”“ ‘Usikutane kimwili na mnyama na kujitia unajisi kwake. Mwanamke asijipeleke kwa mnyama ili kukutana naye kimwili; huo ni upotovu.
”“ ‘Kila mtu atakayefanya mojawapo ya machukizo haya, watu hao ni lazima wakatiliwe mbali na watu wao.
”“ ‘Usiibe. “ ‘Usiseme uongo. “ ‘Msidanganyane.
”“ ‘Usijilipizie kisasi wala kuwa na kinyongo dhidi ya mmoja wa jamaa yako, lakini mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe. Mimi ndimi BWANA.
”“ ‘Usitumie vipimo vya udanganyifu unapopima urefu, kupima uzito, wala kupima wingi. Tumia mizani halali, mawe ya kupimia uzito halali, efa halali, na hini halali. Mimi ndimi BWANA Mungu wako, ambaye alikutoa katika nchi ya Misri.
”“ ‘Jitakaseni basi, nanyi iweni watakatifu, kwa sababu mimi ndimi BWANA Mungu wenu.
”Waambie Waisraeli: ‘Ikiwa mtu ye yote atamlaani Mungu wake, atakuwa na hatia kwa uovu wake; ye yote atakayekufuru Jina la BWANA ni lazima auawe. Kusanyiko lote litampiga kwa mawe. Iwapo ni mgeni au mzawa, atakapolikufuru Jina la BWANA, ni lazima auawe.
”Ikiwa mtu ye yote atamjeruhi jirani yake, cho chote alichomtenda naye atatendewa: iwapo amemvunja mfupa atavunjwa mfupa, jicho kwa jicho, jino kwa jino. Kama alivyomjeruhi mwenzake, vivyo hivyo ndivyo atakavyojeruhiwa.
”“ ‘Lakini kama watatubu dhambi zao na dhambi za baba zao, udanganyifu wao dhidi yangu na uadui wao kwangu,
”“Waambie Waisraeli, ‘Wakati mwanaume au mwanamke akimkosea mwenzake kwa njia yo yote, na kwa hivyo akawa si mwaminifu kwa BWANA, mtu huyo ana hatia,
”Watu wakamjia Mose na kusema, “Tumetenda dhambi wakati tuliponena dhidi ya BWANA na dhidi yako. Mwombe BWANA ili atuondolee hawa nyoka.” Hivyo Mose akawaombea hao watu.
”“Lakini mkishindwa kufanya hili, mtakuwa mnatenda dhambi dhidi ya BWANA; nanyi iweni na hakika kuwa dhambi yenu itawapata.
”Usiwe na miungu mingine ila mimi. Usijitengenezee sanamu katika umbo la kitu cho chote kilicho juu mbinguni au duniani chini au ndani ya maji. Usivisujudie wala kuviabudu; kwa maana Mimi, BWANA Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, ninayewaadhibu watoto kwa ajili ya dhambi za baba zao hata kizazi cha tatu na cha nne cha wale wanichukiao, lakini ninaonyesha upendo kwa maelfu ya vizazi vya wale wanipendao na kuzishika amri zangu.
”Usilitaje jina la BWANA Mungu wako bure, kwa kuwa BWANA hataacha kumhesabia hatia yeye alitajaye jina lake bure.
”Usiue. Usizini. Usiibe. Usimshuhudie jirani yako uongo. Usitamani mke wa jirani yako. Usitamani nyumba ya jirani yako au shamba lake, mtumishi wake wa kiume au wa kike, ng'ombe au punda wake, wala kitu cho chote cha jirani yako.”
”Hivyo iweni waangalifu kuyafanya yale BWANA Mungu wenu aliyowaagiza; msigeuke upande wa kuume wala wa kushoto.
”Vinyago vya miungu yao mtavichoma moto. Msitamani fedha wala dhahabu iliyo juu yao, wala msizichukue kwa ajili yenu, la sivyo mtakuwa mmetekwa navyo. Kwa kuwa ni chukizo kwa BWANA Mungu wenu. Msilete vitu vya machukizo katika nyumba zenu kwani ninyi, mtatengwa kama vitu hivyo kwa maangamizo. Ukichukie kabisa kitu hicho kwa kuwa kimetengwa kwa maangamizo.
”Usiwe na mawe ya kupimia ya aina mbili katika mkoba wako, moja zito na jingine jepesi. Usiwe na vipimo viwili tofauti katika nyumba yako, kimoja kikubwa, kingine kidogo. Ni lazima uwe na uzito na vipimo sahihi na vya haki, ili upate kuishi maisha marefu katika nchi anayokupa BWANA Mungu wako. Kwa maana BWANA Mungu wako humchukia ye yote ambaye hufanya mambo kama haya, ye yote anayetenda kwa udanganyifu.
”“Alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga au mwenye kusubu sanamu, kitu ambacho ni chukizo kwa BWANA, kazi ya mikono ya fundi stadi, na kuisimamisha kwa siri.” Kisha watu wote watasema, “Amen!”
”“Alaaniwe mtu apotoshaye haki ya mgeni, yatima au mjane.” Kisha watu wote watasema, “Amen!”
”“Alaaniwe mtu amuuaye jirani yake kwa siri.” Kisha watu wote watasema, “Amen!”
”“Alaaniwe mtu apokeaye rushwa ili kumwua mtu asiye na hatia.” Kisha watu wote watasema, “Amen!”
”“Alaaniwe mtu ambaye hatashika maneno haya ya sheria hii kwa kuyafanya.” Kisha watu wote watasema, “Amen!”
”Hata hivyo, kama hutamtii BWANA Mungu wako na kuzishika kwa bidii amri zake zote na maagizo ninayokupa leo, laana hizi zote zitakuja juu yako na kukupata:
”Wakamfanya Mungu kuwa na wivu kwa miungu yao migeni, na kumkasirisha kwa sanamu zao za machukizo. Wakatoa dhabihu kwa pepo, ambao si Mungu: miungu wasiyoijua, miungu iliyojitokeza siku za karibuni, miungu ambayo baba zenu hawakuiogopa.
”Lakini Waisraeli wakamwambia BWANA, “Tumetenda dhambi. Ututendee lile unaloona kuwa jema kwako, lakini twakusihi utuokoe sasa.”
”Katika siku hizo Israeli hawakuwa na mfalme, kila mmoja akafanya kama alivyoona vyema machoni pake mwenyewe.
”Hii Dhambi ya hawa vijana ilikuwa kubwa sana machoni pa BWANA, kwa kuwa waliitendea dhabihu ya BWANA kwa dharau.
”Kwa maana kuasi ni kama dhambi ya uaguzi, nao ukaidi ni kama uovu wa kuabudu sanamu. Kwa sababu umelikataa neno la BWANA, naye amekukataa wewe kuendelea kuwa mfalme.”
”“Watakapotenda dhambi dhidi yako, kwa kuwa hakuna mtu ye yote ambaye hatendi dhambi, nawe ukachukizwa nao nakuwakabidhi kwa adui, ambaye atawachukua utumwani katika nchi yake mwenyewe, mbali au karibu;
”Wakawatoa kafara wana wao na mabinti zao katika moto. Wakafanya uaguzi na uchawi, nao wakajiuza wenyewe katika kutenda uovu machoni pa BWANA, wakamghadhibisha. Basi BWANA akawakasirikia sana Israeli na kuwaondoa kwenye uwepo wake. Ni kabila la Yuda tu ndilo lililobaki;
”basi kutoka mbinguni, mahali pa makao yako, usikie dua yao na maombi yao na ukatetee haki yao. Uwasamehe watu wako, waliotenda dhambi dhidi yako.
”Akawatoa wanawe kuwa kafara kwa kuwapitisha katika moto katika Bonde la Hinomu, akafanya ulozi, uaguzi na uchawi, akataka ushauri kwa wenye pepo wa utambuzi na wenye kuwasiliana na mizimu. Akafanya maovu mengi machoni pa BWANA, akaichochea hasira yake.
”Huu ndio mwisho wa watu wote wanaomsahau Mungu, vivyo hivyo matumaini ya wasiomjali Mungu huangamia.
”Kama nilifanya dhambi, ungekuwa umeniona, wala usingeacha kosa langu lipite bila kuadhibiwa.
”Ninyi, hata hivyo, hunipakaza uongo, ninyi ni matabibu wasiofaa kitu, ninyi nyote!
”Ni makosa na dhambi ngapi nilizotenda? Nionyeshe kosa langu na dhambi yangu.
”“Mwanadamu ni kitu gani, hata aweze kuwa safi, au yeye aliyezaliwa na mwanamke, hata aweze kuwa mwadilifu?
”Ndipo huja mbele za watu na kusema, ‘Nilitenda dhambi na kupotosha kilichokuwa haki, lakini sikuadhibiwa kama nilivyostahili. Alinikomboa nafsi yangu nisitumbukie shimoni, nami nitaishi ili kuufurahia mwanga.’
”Heri mtu yule ambaye haendi katika shauri la watu waovu, wala hakusimama katika njia ya wenye dhambi au kuketi katika baraza la wenye mizaha.
”Sivyo walivyo waovu! Wao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo. Kwa hiyo waovu hawatastahimili hukumu, wala wenye dhambi katika kusanyiko la wenye haki. Kwa maana BWANA huziangalia njia za mwenye haki, bali njia ya waovu itaangamia.
”Enyi watu, mtabadilisha utukufu wangu kuwa aibu mpaka lini? Mtapenda udanganyifu na kufuata miungu ya uongo mpaka lini?
”Wenye kiburi hawawezi kusimama mbele yako, unawachukia wote watendao mabaya. Unawaangamiza wasemao uongo, wamwagao damu na wadanganyifu BWANA huwachukia.
”Katika kiburi chake mtu mwovu humtesa mtu aliye maskini, waovu na wanaswe katika hila wanazozitunga. Hujivunia tamaa za moyo wake; humbariki mlafi na kumtukana BWANA. Katika kiburi chake mtu mwovu hamtafuti Mungu, katika mawazo yake yote hakuna nafasi ya Mungu.
”Kinywa chake kimejaa laana, uongo na vitisho, shida na ubaya viko chini ya ulimi wake.
”(Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Mahalathi. Zaburi Ya Daudi) Mpumbavu anasema moyoni mwake, “Hakuna Mungu.” Wameharibika, matendo yao ni maovu kabisa; hakuna atendaye mema.
”Uangalie mateso na shida zangu na uniondolee dhambi zangu zote.
”(Utenzi: Zaburi Ya Daudi. Funzo) Heri mtu yule ambaye amesamehewa makosa yake, ambaye dhambi zake zimefunikwa.
”Kisha nilikujulisha dhambi yangu wala sikuficha uovu wangu. Nikasema, “Nitaungama makosa yangu kwa BWANA,” ndipo uliponisamehe hatia ya dhambi yangu.
”Maneno ya kinywa chake ni maovu na ya udanganyifu, ameacha kuwa mwenye hekima na kutenda mema.
”Epuka hasira na uache ghadhabu, usihangaike, itakuongoza tu kwenye ubaya.
”Naungama uovu wangu, ninataabishwa na dhambi yangu.
”Nilisema, “Ee BWANA nihurumie, niponye, maana nimekutenda dhambi wewe.”
”(Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Daudi Baada Ya Kukemewa Na Nabii Nathani Kwa Kuzini Na Bathsheba) Ee Mungu, unihurumie, kwa kadiri ya upendo wako usiokoma, kwa kadiri ya huruma yako kuu uyafute makosa yangu. Unioshe na uovu wangu wote na unitakase dhambi yangu. Kwa maana ninajua makosa yangu, na dhambi yangu iko mbele yangu daima. Dhidi yako, wewe peke yako, nimetenda dhambi na kufanya yaliyo mabaya machoni pako, ili uthibitike kuwa mkweli unenapo na kuwa na haki utoapo hukumu.
”Hakika mimi nilizaliwa mwenye dhambi, mwenye dhambi tangu nilipotungwa mimba kwa mama yangu.
”Uufiche uso wako usiitazame dhambi yangu na uufute uovu wangu wote. Ee Mungu, uniumbie moyo safi, uifanye upya roho ya uthabiti ndani yangu. Usinitupe kutoka mbele zako wala kuniondolea Roho wako Mtakatifu.
”Ulimi wako hupanga mashauri mabaya ya maangamizi, ni kama wembe mkali, ninyi mfanyao hila.
”(Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Mahalathi. Utenzi Wa Daudi) Mpumbavu anasema moyoni mwake, “Hakuna Mungu.” Wameharibika, na njia zao ni za uovu kabisa, hakuna hata mmoja atendaye mema. Mungu huwachungulia wanadamu chini kutoka mbinguni aone kama wako wenye akili, wo wote wanaomtafuta Mungu. Kila mmoja amegeukia mbali, wameharibika wote pamoja, hakuna hata mmoja atendaye mema, naam! Hata mmoja.
”Kwa ajili ya dhambi za vinywa vyao, kwa ajili ya maneno ya midomo yao, waache wanaswe katika kiburi chao. Kwa ajili ya laana na uongo wanaotamka,
”Ee Mungu, wewe unajua upumbavu wangu, wala maovu yangu hayakufichika kwako.
”Hawakulishika Agano la Mungu na walikataa kuishi kwa sheria yake.
”Lakini waliendelea kutenda dhambi dhidi yake, wakiasi jangwani dhidi ya Aliye Juu Sana.
”Usituhesabie dhambi za baba zetu, huruma yako na itujie hima, kwa maana tu wahitaji mno. Ee Mungu Mwokozi wetu, utusaidie, kwa ajili ya utukufu wa jina lako; tuokoe na kutusamehe dhambi zetu kwa ajili ya jina lako.
”Umeyaweka maovu yetu mbele yako, dhambi zetu za sirini katika nuru ya uwepo wako.
”Wale wanaompenda BWANA na wauchukie uovu, kwa maana yeye hulinda maisha ya waaminifu wake na kuwaokoa kutoka mkononi mwa mwovu.
”Mdanganyifu hatakaa nyumbani mwangu, yeye asemaye kwa uongo hatasimama mbele yangu.
”yeye hatutendei kulingana na dhambi zetu wala hatupatilizi kwa kadiri ya maovu yetu. Kama vile mbingu zilivyo juu sana juu ya dunia, ndivyo wema wake ulivyo mwingi kwa wanaomcha; kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, ndivyo Mungu alivyoziweka dhambi zetu mbali nasi.
”Tumetenda dhambi, kama vile baba zetu walivyotenda, tumekosa na tumetenda kwa uovu.
”bali walijichanganya na mataifa na wakazikubali desturi zao. Waliabudu sanamu zao, zikawa mtego kwao. Wakawatoa wana wao na binti zao dhabihu kwa mashetani. Walimwaga damu isiyo na hatia, damu za wana wao na binti zao, ambao waliwatoa dhabihu kwa sanamu za Kanaani, nayo nchi ikanajisika kwa damu zao. Wakajinajisi wenyewe kwa yale waliyotenda; kwa matendo yao wenyewe wakajifanyia ukahaba.
”Heri wale walio waadilifu katika njia zao, wanaoenenda katika sheria ya BWANA.
”Nimelificha neno lako moyoni mwangu ili nisikutende dhambi.
”Unawakataa wote wanaoyaasi maagizo yako, kwa maana udanganyifu wao ni bure.
”Chemchemi za machozi zinatiririka kutoka machoni pangu, kwa kuwa sheria yako haifuatwi.
”Ee Mungu, nichunguze, uujue moyo wangu, nijaribu na ujue mawazo yangu. Uone kama kuna njia iletayo machukizo ndani yangu, uniongoze katika njia ya milele.
”Mwanangu, kama wenye dhambi wakikushawishi, usikubaliane nao.
”Mtu mbaya sana na mlaghai, ambaye huzungukazunguka na maneno ya upotovu, ambaye anakonyeza kwa jicho lake, anayetoa ishara kwa miguu yake na kuashiria kwa vidole vyake, ambaye hupanga ubaya kwa udanganyifu moyoni mwake: daima huchochea fitina.
”Kuna vitu sita anavyovichukia BWANA, naam, viko saba vilivyo chukizo kwake: macho ya kiburi, ulimi udanganyao, mikono imwagayo damu isiyo na hatia, moyo ule uwazao mipango miovu, miguu ile iliyo myepesi kukimbilia uovu, shahidi wa uongo ambaye humwaga uongo na mtu ambaye huchochea fitina kati ya ndugu.
”Kumcha BWANA ni kuchukia uovu, ninachukia kiburi na majivuno, tabia mbaya na mazungumzo potovu.
”BWANA huwachukia sana watu wenye moyo wa upotovu, bali hupendezwa na wale ambao njia zao hazina lawama. Uwe na hakika na hili: Waovu hawataepuka kuadhibiwa, bali wale wenye haki watakuwa huru.
”Iko njia ionekanayo sawa kwa mtu, bali mwishoni huelekea mautini.
”BWANA huchukia sana mawazo ya mwovu, bali mawazo ya wale walio safi humfurahisha yeye. Mtu mwenye tamaa huletea jamaa yake taabu, bali yeye achukiaye rushwa ataishi.
”BWANA huwachukia sana wote wenye kiburi cha moyo. Uwe na hakika kwa hili: Hawataepuka kuadhibiwa.
”Mtu mpotovu huchochea ugomvi, nayo maongezi ya upuzi hutenganisha marafiki wa karibu.
”Ikiwa mtu atalipa baya kwa jema, kamwe ubaya hautaondoka katika nyumba yake.
”Yeye asemaye asiye na haki ana haki, naye asemaye mwenye haki hana haki, BWANA huwachukia sana wote wawili.
”Shahidi wa uongo hataacha kuadhibiwa, naye amwagaye uongo hataachwa huru.
”Mipango ya mpumbavu ni dhambi, watu humchukia mwenye dhihaka.
”Ulimi wa uongo, huwachukia wale unaowaumiza, nacho kinywa cha kujipendekeza hutenda uharibifu.
”Kama mtu ye yote akikataa kusikia sheria, hata maombi yake ni chukizo.
”Yeye afichaye dhambi zake hatafanikiwa, bali ye yote aziungamaye na kuziacha hupata rehema. Amebarikiwa mtu ambaye siku zote humcha BWANA, bali yeye afanyaye moyo wake kuwa mgumu huangukia kwenye taabu.
”Kama mtawala akisikiliza uongo, maafisa wake wote huwa waovu.
”wale ambao ni safi machoni pao wenyewe kumbe hawakuoshwa uchafu wao;
”Usiwe mwepesi kukasirika rohoni mwako, kwa kuwa hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu.
”Hakuna mtu mwenye haki duniani ambaye hufanya mambo ya haki na kamwe asitende dhambi.
”Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa: Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu. Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au baya.
”jiosheni na mkajitakase. Yaondoeni matendo yenu maovu mbele zangu! Acheni kutenda mabaya,
”“Njoni basi na tuhojiane,” asema BWANA. “Ingawa dhambi zenu ni kama rangi nyekundu, zitakuwa nyeupe kama theluji; ingawa ni nyekundu sana kama damu, zitakuwa nyeupe kama sufu.
”Lakini waasi na wenye dhambi wote wataangamizwa, nao wanaomwacha BWANA wataangamia.
”Nyuso zao zinavyoonekana zinashuhudia dhidi yao, hujivunia dhambi yao kama Sodoma, wala hawaifichi. Ole wao! Wamejiletea maafa juu yao wenyewe.
”Ole wao wanaoita ubaya ni wema na wema ni ubaya, wawekao giza badala ya nuru na nuru badala ya giza, wawekao uchungu badala ya utamu na utamu badala ya uchungu. Ole wao walio na hekima machoni pao wenyewe na kujiona wenye akili machoni pao wenyewe.
”Kwa hiyo, kama ndimi za moto zirambavyo nyasi na kama vile majani makavu yazamavyo katika miali ya moto, ndivyo mizizi yao itakavyooza na maua yao yatakavyopeperushwa kama mavumbi; kwa kuwa wameikataa sheria ya BWANA Mwenye Nguvu Zote na kulisukumia mbali neno la Aliye Mtakatifu wa Israeli.
”Nitauadhibu ulimwengu kwa ajili ya uovu wake, waovu kwa ajili ya dhambi zao. Nitakomesha majivuno ya wenye kiburi Na nitakishusha kiburi cha watu wakatili.
”Hawa ni watu waasi, watoto wadanganyifu, watoto ambao hawataki kusikiliza mafundisho ya BWANA.
”Kwa kuwa mpumbavu hunena upumbavu, moyo wake hushughulika na uovu: Hutenda mambo yasiyo ya uchaji Mungu, na hueneza habari za makosa kuhusu BWANA; yeye huwaacha wenye njaa bila kitu na wenye kiu huwanyima maji. Taratibu za mtu mbaya kabisa ni ovu, hufanya mipango miovu ili kumwangamiza maskini kwa uongo, hata wakati ambapo hoja za mhitaji ni za haki.
”“Mimi, naam mimi, ndimi nizifutaye dhambi zako, kwa ajili yangu mwenyewe, wala sizikumbuki dhambi zako tena. Tafakari mambo yaliyopita, njoo na tuhojiane, leta shauri lako, uweze kupewa haki yako.
”Lakini alitobolewa kwa ajili ya makosa yetu, alichubuliwa kwa ajili ya maovu yetu; adhabu iliyotuletea sisi amani ilikuwa juu yake, na kwa majeraha yake sisi tumepona. Sisi sote, kama kondoo, tumepotea, kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe, naye BWANA aliweka juu yake maovu yetu sisi sote.
”Ni mbwa wenye tamaa kubwa, kamwe hawatosheki. Wao ni wachungaji waliopungukiwa na ufahamu; wote wamegeukia njia yao wenyewe, kila mmoja hutafuta faida yake mwenyewe.
”Mnamdhihaki nani? Ni nani mnayemcheka kwa dharau na kumtolea ndimi zenu? Je, ninyi si watoto wa waasi, Uzao wa waongo?
”Lakini maovu yenu yamewatenga ninyi na Mungu wenu, dhambi zenu zimewaficha ninyi uso wake, ili asisikie. Kwa maana mikono yenu imetiwa mawaa kwa damu na vidole vyenu kwa hatia. Midomo yenu imenena uongo, nazo ndimi zenu zimenong'ona mambo maovu. Hakuna hata mmoja anayedai kwa haki; hakuna hata mmoja anayetetea shauri lake kwa haki. Wanategemea mabishano matupu na kusema uongo, huchukua mimba ya magomvi na kuzaa uovu.
”Sisi sote tumekuwa kama mtu aliye najisi, nayo matendo yetu yote ya uadilifu ni kama matambaa machafu; sisi sote tunasinyaa kama jani na kama upepo maovu yetu hutupeperusha.
”Hata ujisafishe kwa magadi na kutumia sabuni nyingi, bado doa la hatia yako liko mbele zangu,” asema BWANA Mwenyezi.
”Ungama dhambi zako tu: kwamba umemwasi BWANA Mungu wako, umetapanya wema wako kwa miungu ya kigeni chini ya kila mti unaotanda, nawe hukunitii mimi,’ ” asema BWANA.
”Sisi na tulale chini katika aibu yetu, fedheha yetu na itufunike. Tumetenda dhambi dhidi ya BWANA Mungu wetu, sisi na mababa zetu; tangu ujana wetu hadi leo hatukumtii BWANA Mungu wetu.”
”Ee Yerusalemu, uusafishe uovu kutoka moyoni mwako na uokolewe. Utaendelea kuficha mawazo mapotovu mpaka lini?
”Je, wanaona aibu kwa ajili ya tabia yao inayochukiza mno? Hapana, hawana aibu hata kidogo; hawajui hata kuona haya. Kwa hiyo wataanguka miongoni mwa hao walioanguka, watashushwa nitakapowaadhibu,” asema BWANA.
”Sikia Ee nchi: Ninaleta maafa juu ya watu hawa, matunda ya mipango yao, kwa sababu hawakusikiliza maneno yangu na wameikataa sheria yangu.
”Lakini tazama, mnatumainia maneno ya udanganyifu yasiyo na maana. “ ‘Je, mtaiba na kuua, mtazini na kuapa kwa uongo na kufukiza uvumba kwa Baali na kufuata miungu mingine ambayo hamkuijua, kisha mje na kusimama mbele yangu katika nyumba hii, inayoitwa kwa Jina langu, mkisema, “Tuko salama.” Salama kwa kufanya mambo haya yote ya kuchukiza?
”Kwa nini basi watu hawa walipotea? Kwa nini Yerusalemu inapotea kila mara? Wanang'ang'ania udanganyifu na wanakataa kurudi.
”Nimewasikiliza kwa makini, lakini hawataki kusema lililo sawa. Hakuna anayetubia makosa yake akisema, “Nimefanya nini?” Kila mmoja hufuata njia yake mwenyewe kama farasi anayekwenda vitani.
”“Huweka tayari ndimi zao kama upinde, ili kurusha uongo; wamekuwa na nguvu katika nchi kwa ajili ya uongo, wala si katika kweli. Wanatoka dhambi moja hadi nyingine, hawanitambui mimi,” asema BWANA. “Jihadhari na rafiki zako; usiwaamini ndugu zako. Kwa kuwa kila ndugu ni mdanganyifu, na kila rafiki ni msingiziaji. Rafiki humdanganya rafiki, hakuna ye yote asemaye kweli. Wamefundisha ndimi zao kudanganya, wanajichosha wenyewe katika kutenda dhambi.
”Ndimi zao ni mshale wenye sumu, hunena kwa udanganyifu. Kwa kinywa chake kila mmoja huzungumza maneno mazuri na jirani yake, lakini moyoni mwake humtegea mtego.
”BWANA akasema, “Ni kwa sababu wameiacha sheria yangu, niliyoiweka mbele yao: hawajaniheshimu mimi wala kufuata sheria yangu. Badala yake wamefuata ukaidi wa mioyo yao, wamefuata mabaali, kama vile baba zao walivyowafundisha.”
”Ingawa dhambi zetu zinashuhudia juu yetu, Ee BWANA, tenda jambo kwa ajili ya jina lako. Kwa kuwa kukengeuka kwetu ni kukubwa, nasi tumetenda dhambi dhidi yako.
”Ee BWANA, tunatambua uovu wetu na kosa la baba zetu; kweli tumetenda dhambi dhidi yako.
”Moyo ni mdanganyifu kuliko vitu vyote, ni mwovu kupita kiasi. Ni nani awezaye kuujua?
”Nako miongoni mwa manabii wa Yerusalemu nimeona jambo baya sana: Wanafanya uzinzi na kuenenda katika uongo. Wanatia nguvu mikono ya watenda mabaya, kwa ajili hiyo hakuna ye yote anayeachana na uovu wake. Wote wako kama Sodoma kwangu; watu na Yerusalemu wako kama Gomora.”
”Tena na tena, niliwatuma watumishi wangu manabii ambao walisema, ‘Msifanye jambo hili la kuchukiza ambalo nalichukia!’
”BWANA alipokuwa hawezi kuendelea kuvumilia matendo yenu maovu na mambo ya machukizo mliyoyafanya, nchi yenu ilikuwa kitu cha kulaania na kuachwa ukiwa pasipo wakazi, kama ilivyo leo.
”Lakini nyumba ya Israeli haitakusikiliza kwa kuwa hawako radhi kunisikiliza mimi, kwa kuwa nyumba yote ya Israeli ni wenye vipaji vya nyuso vigumu na mioyo ya ukaidi.
”Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Kwa kuwa umemwaga tamaa zako na kuonyesha uchi wako katika uzinzi wako kwa wapenzi wako na kwa sababu ya sanamu zako zote za machukizo na kwa sababu uliwapa damu ya watoto wako,
”“ ‘Sasa hii ilikuwa ndiyo dhambi ya dada yako Sodoma: yeye na binti zake walikuwa na majivuno, walafi na wazembe, hawakuwasaidia maskini na wahitaji.
”Kwa kuwa kila roho ni mali yangu, kama vile ilivyo roho ya baba, vivyo hivyo roho ya mtoto ni mali yangu. Roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa.
”Roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa. Mwana hataadhibiwa kwa ajili ya makosa ya baba yake, wala baba hataadhibiwa kwa ajili ya makosa ya mwanawe. Haki ya mtu mwenye haki itahesabiwa juu yake na uovu wa mtu mwovu utalipizwa juu yake.
”“Lakini mtu mwovu akiacha dhambi zake zote alizozitenda na kushika amri zangu zote na kufanya lililo haki na sawa, hakika ataishi, hatakufa. Hakuna kosa lo lote alilotenda litakalokumbukwa juu yake. Kwa ajili ya mambo ya haki aliyoyatenda, ataishi. Je, mimi ninafurahia kifo cha mtu mwovu? Asema BWANA Mwenyezi. Je, si mimi ninafurahi wanapogeuka kutoka katika njia zao mbaya na kuishi?
”“Lakini kama mtu mwenye haki akiacha haki yake na kutenda dhambi na kufanya mambo ya machukizo ambayo mtu mwovu hufanya, Je, ataishi? Hakuna hata mojawapo ya matendo ya haki aliyotenda litakalokumbukwa. Kwa sababu ya kukosa uaminifu kwake anayo hatia na kwa sababu ya dhambi alizozitenda, atakufa.
”Kama mtu mwenye haki akiacha haki yake na kutenda dhambi, atakufa kwa ajili ya dhambi yake, kwa sababu ya dhambi alizotenda, atakufa.
”Lakini mtu mwovu akigeuka kutoka katika maovu aliyoyatenda na kufanya yaliyo haki na sawa, ataokoa maisha yake. Kwa kuwa anayafikiria na kugeuka kutoka makosa yake yote aliyoyatenda na kuyaacha, hakika ataishi, hatakufa.
”“Kwa hiyo, Ee nyumba ya Israeli, nitawahukumu, kila mmoja sawasawa na njia zake, asema BWANA Mwenyezi. Tubuni! Geukeni kutoka katika makosa yenu yote, ndipo dhambi haitakuwa anguko lenu. Tupilieni mbali makosa yenu yote mliyoyatenda, nanyi mpate moyo mpya na roho mpya. Kwa nini mfe, Ee nyumba ya Israeli? Kwa maana sifurahii kifo cha mtu awaye yote afaye katika uovu, asema BWANA Mwenyezi. Tubuni basi, mkaishi!
”Hapo ndipo nitakapokumbuka mwenendo wenu na matendo yenu yote ambayo kwayo mlijitia unajisi, nanyi mtajichukia wenyewe kwa ajili ya maovu yote mliyokuwa mmetenda.
”Kama mtu mwenye haki akigeuka kutoka katika uadilifu wake na kufanya uovu, atakufa kwa ajili ya huo uovu. Naye mtu mwovu kama akigeuka kutoka katika uovu wake na kufanya lile lililo haki na sawa, kwa kufanya hivyo ataishi.
”Mnategemea panga zenu, mnafanya mambo ya machukizo na kila mmoja wenu humtia unajisi mke wa jirani yake. Je, mtaimiliki nchi?’
”Kuna kulaani tu, uongo na uuaji, wizi na uzinzi, bila kuwa na mipaka, nao umwagaji damu mmoja baada ya mwingine.
”Hili ndilo asemalo BWANA: “Kwa dhambi tatu za Yuda, hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. Kwa sababu wameikataa sheria ya BWANA na hawakuzishika amri zake, kwa sababu wamepotoshwa na miungu ya uongo, miungu ambayo babu zao waliifuata.
”Je, naweza kuhukumu kuwa mtu mwenye mizani ya udanganyifu hana hatia, aliye na mfuko wa mawe ya kupimia ya uongo? Matajiri wake ni wajeuri; watu wake ni waongo na ndimi zao zinazungumza kwa udanganyifu.
”“Basi nitakuja karibu nanyi ili kuhukumu. Nami nitakuwa mwepesi kushuhudia dhidi ya wachawi, wazinzi, waapao kwa uongo, wanaopunja vibarua malipo yao, wanaowaonea wajane na yatima, nao wanaowanyima wageni haki, lakini hawaniogopi mimi,” asema BWANA Mwenye Nguvu Zote.
”Naye atamzaa mwana, nawe utamwita Jina lake Yesu, kwa maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka katika dhambi zao.”
”Watu walimwendea kutoka Yerusalemu, Uyahudi yote na nchi zote za kandokando ya Mto Yordani. Nao wakaziungama dhambi zao, akawabatiza katika Mto Yordani.
”“Mmesikia walivyoambiwa watu wa zamani kwamba, ‘Usiue, ye yote atakayeua atapaswa hukumu.’ Lakini mimi nawaambia kwamba, ye yote atakayemkasirikia ndugu yake wa kiume au wa kike, atapaswa hukumu. Tena, ye yote atakayemwambia ndugu yake wa kiume au wa kike, ‘Raca’, yaani kumdharau na kumdhihaki, atapaswa kufanyiwa baraza. Lakini ye yote atakayesema ‘Wewe mpumbavu ulaaniwe!’ Atapaswa hukumu ya moto wa jehanamu.
”“Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Usizini’. Lakini mimi nawaambia kwamba, ye yote amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake. Jicho lako la kuume likikufanya utende dhambi, ling'oe ulitupe mbali. Ni afadhali kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako kuliko mwili wako mzima utupwe jehanamu. Kama mkono wako wa kuume ukikufanya utende dhambi, ukate uutupe mbali. Ni afadhali kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako kuliko mwili wako mzima utupwe jehanamu.
”“Pia ilinenwa kwamba, ‘Mtu ye yote amwachaye mkewe na ampe hati ya talaka.’ Lakini mimi nawaambia, ye yote amwachaye mkewe isipokuwa kwa kosa la uasherati, amfanya mkewe kuwa mzinzi. Na ye yote amwoaye yule mwanamke aliyeachwa azini.
”Kwa hiyo iweni wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.
”Usitutie majaribuni, bali utuokoe kutoka kwa yule mwovu [kwa kuwa Ufalme ni wako na nguvu na utukufu, hata milele. Amen].’
”Kwa kuwa kama mkiwasamehe watu wengine wanapowakosea, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe na ninyi pia. Lakini msipowasamehe watu wengine makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.
”Vivyo hivyo, mti mwema huzaa matunda mazuri na mti mbaya huzaa matunda mabaya. Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya wala mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mazuri. Kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni. Hivyo kwa matunda yao mtawatambua.
”“Si kila mtu aniambiaye, ‘Bwana, Bwana,’ atakayeingia katika Ufalme wa Mbinguni bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, ‘Bwana, Bwana, hatukutoa unabii kwa jina lako na kwa jina lako kutoa pepo wachafu na kufanya miujiza mingi?’ Ndipo nitakapowaambia wazi, ‘Sikuwajua kamwe. Ondokeni kwangu, ninyi watenda maovu!’
”Kwa hiyo nawaambia, kila dhambi na kufuru watu watasamehewa, lakini mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa. Mtu ye yote atakayesema neno dhidi ya Mwana wa Adamu atasamehewa, lakini ye yote anenaye neno dhidi ya Roho Mtakatifu hatasamehewa, iwe katika ulimwengu huu au katika ulimwengu ujao.
”Lakini nawaambia, katika siku ya hukumu watu watatoa hesabu kuhusu kila neno lisilo maana walilonena. Kwa maana kwa maneno yako utahesabiwa haki na kwa maneno yako utahukumiwa.”
”Kwa maana ndani ya moyo hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushahidi wa uongo na masingizio.
”Kwa maana itamfaidia nini mtu kuupata ulimwengu wote, lakini akayapoteza maisha yake? Au mtu atatoa nini badala ya maisha yake?
”Lakini kama mtu ye yote anamsababisha mmojawapo wa hawa wadogo wanaoniamini atende dhambi, ingekuwa bora kwake afungiwe jiwe kubwa la kusagia shingoni mwake na kutoswa katika kilindi cha bahari.
”Ikiwa mkono wako au mguu wako unakusababisha utende dhambi, ukate na uutupe mbali. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa huna mkono mmoja au mguu mmoja, kuliko kuwa na mikono miwili au miguu miwili na kutupwa katika moto wa milele. Nalo jicho lako kama linakusababisha utende dhambi ling'oe, ulitupe mbali. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa na jicho moja, kuliko kuwa na macho mawili ukatupwa katika moto wa jehanamu.
”“Kama ndugu yako akikukosea, nenda ukamwonyeshe kosa lake, kati yenu ninyi wawili peke yenu. Kama akikusikiliza, utakuwa umempata tena ndugu yako. Lakini kama hatakusikiliza, nenda na mtu mwingine mmoja au wawili ili kila neno lithibitishwe na ushahidi wa mashahidi wawili au watatu. Kama akikataa kuwasikiliza hao, liambie kanisa, naye kama akikataa hata kulisikiliza kanisa, basi mtendeeni mtu huyo kama vile ambavyo mngemtendea asiyeamini.
”Ndipo Petro akamjia Yesu na kumwuliza, “Bwana, ndugu yangu anikosee mara ngapi nami nimsamehe? Je, hata mara saba?” Yesu akamjibu, “Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.
”“Hivi ndivyo Baba yangu wa mbinguni atakavyomfanyia kila mmoja wenu ikiwa hatamsamehe kutoka moyoni kila mmoja ndugu yake aliyemkosea.”
”Mimi nawaambia, ye yote amwachaye mkewe isipokuwa kwa sababu ya uasherati naye akaoa mke mwingine, anazini. Naye amwoaye yule mwanamke aliyeachwa pia anazini.”
”Mtu mmoja akamjia Yesu na kumwuliza, “Mwalimu mwema, nifanye jambo gani jema ili nipate uzima wa milele?” Yesu akamjibu, “Mbona unaniita mimi mwema? Hakuna aliye mwema ila Mmoja tu, ndiye Mungu: Lakini ukitaka kuingia uzimani, zitii amri.” Yule mtu akamwuliza, “Amri zipi?” Yesu akamjibu, “Usiue, usizini, usiibe, usishuhudie uongo, waheshimu baba yako na mama yako na umpende jirani yako kama nafsi yako.”
”“Ole wenu, walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wanafiki! Kwa maana mnasafisha nje ya kikombe na kisahani, lakini ndani mmejaa unyang'anyi na kutokuwa na kiasi.
”Kwa sababu ya kuongezeka kwa uovu upendo wa watu wengi utapoa,
”Hii ndiyo damu yangu ya Agano, ile imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.
”Kesheni na muombe, msije mkaanguka majaribuni. Hakika roho iko radhi lakini mwili ni dhaifu.”
”Yohana alikuja, akibatiza huko nyikani, akihubiri ubatizo wa toba kwa ajili ya ondoleo la dhambi. Watu kutoka Uyahudi wote na sehemu zote za Yerusalemu walikuwa wakimwendea, naye akawabatiza katika Mto Yordani, wakitubu dhambi zao.
”akisema, “Wakati umewadia, Ufalme wa Mungu umekaribia. Tubuni na kuiamini Habari Njema.”
”Akaendelea kusema, “Kile kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. Kwa maana kutoka ndani ya moyo wa mtu hutoka: Mawazo mabaya, uasherati, wizi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, uovu, udanganyifu, ufisadi, wivu, matukano, kiburi na upumbavu. Maovu haya yote hutoka ndani ya mtu nayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi.”
”Kama mkono wako ukikusababisha kutenda dhambi, ukate. Ni afadhali kuingia katika uzima ukiwa na mkono mmoja kuliko kuwa na mikono miwili ukaingia jehanamu mahali ambako moto hauzimiki. [Mahali ambako funza wake hawafi wala moto wake hauzimiki].
”Kama mguu wako ukikusababisha kutenda dhambi, ukate. Ni afadhali kuingia katika uzima ukiwa kilema kuliko kuwa na miguu miwili ukaingia jehanamu mahali ambako moto hauzimiki. [Mahali ambako funza wake hawafi wala moto hauzimiki.]
”Nalo jicho lako likikusababisha kutenda dhambi, ling'oe. Ni afadhali kuwa chongo ukaingia katika Ufalme wa Mungu kuliko kuwa na macho mawili na ukatupwa jehanamu, mahali ambako “ ‘funza wake hawafi, wala moto wake hauzimiki.’
”Yesu alipokuwa anaondoka, mtu mmoja akamkimbilia, akapiga magoti mbele yake, akamwuliza, “Mwalimu mwema, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?” Yesu akamwambia, “Mbona unaniita mwema? Hakuna aliye mwema isipokuwa Mungu peke yake. Unazijua amri: ‘Usiue, usizini, usiibe, usishuhudie uongo, usidanganye, waheshimu baba yako na mama yako.’ ”
”Nanyi kila msimamapo kusali, sameheni, mkiwa na neno na mtu ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.
”Lakini kama ninyi msiposamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.”
”Kesheni na kuomba msije mkaingia majaribuni. Roho iko radhi lakini mwili ni dhaifu.”
”kuwajulisha watu wake juu ya wokovu utakaopatikana kwa kusamehewa dhambi zao,
”Akaenda katika nchi yote kandokando ya Mto Yordani, akihubiri ubatizo wa toba kwa ajili ya msamaha wa dhambi.
”Yesu akawajibu, “Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio wagonjwa. Sikuja kuwaita wenye haki bali wenye dhambi wapate kutubu.”
”Kwa hiyo, nakuambia, dhambi zake zilizokuwa nyingi zimesamehewa, kwani ameonyesha upendo mwingi. Lakini yule aliyesamehewa kidogo, hupenda kidogo.” Kisha akamwambia yule mwanamke, “Dhambi zako simesamehewa.” Lakini wale waliokuwa wameketi pamoja naye chakulani wakaanza kusemezana wao kwa wao, “Huyu ni nani ambaye hata anasamehe dhambi?”
”Zile za kwenye mwamba ni wale ambao hulipokea neno kwa furaha wanapolisikia, lakini hawana mizizi. Wanaamini kwa kitambo kidogo, lakini wakati wa kujaribiwa huiacha imani.
”Utusamehe dhambi zetu, kwa kuwa na sisi huwasamehe wote wanaotukosea. Wala usitutie majaribuni, bali utuokoe kutoka kwa yule mwovu.’ ”
”Nawaambieni, vivyo hivyo kutakuwa na furaha zaidi mbinguni kwa sababu ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa wenye haki tisini na tisa ambao hawana haja ya kutubu.”
”Vivyo hivyo, nawaambia, kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu juu ya mwenye dhambi mmoja atubuye.”
”“Yule tajiri akasema, ‘Hapana, baba Abrahamu, lakini mtu kutoka kwa wafu akiwaendea, watatubu.’ “Abrahamu akamwambia, ‘Kama wasipowasikiliza Mose na manabii, hawataweza kushawishiwa hata kama atafufuka mtu kutoka kwa wafu.’ ”
”Kwa hiyo, jilindeni. “Kama ndugu yako akikukosea mwonye, naye akitubu, msamehe. Kama akikukosea mara saba kwa siku moja na mara saba kwa siku moja akaja kwako akisema, ‘Ninatubu’, msamehe.”
”“Lakini yule mtoza ushuru akasimama mbali, hakuthubutu hata kuinua uso wake kutazama mbinguni, bali alijipiga piga kifuani na kusema: ‘Mungu, nihurumie, mimi mwenye dhambi.’
”Mtawala mmoja akamwuliza Yesu, “Mwalimu mwema, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?” Yesu akamjibu, “Mbona unaniita mwema? Hakuna mtu ye yote aliye mwema ila Mungu peke yake. Unazifahamu amri: ‘Usizini, usiue, usiibe, usishuhudie uongo, waheshimu baba yako na mama yako.’ ”
”Toba na msamaha wa dhambi utatangazwa kupitia jina lake, kuanzia Yerusalemu.
”Siku iliyofuata, Yohana alimwona Yesu akimjia akasema, “Tazama, Mwana-Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu!
”Kama vile Mose alivyomwinua yule nyoka kule jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa juu. Ili kila mtu amwaminiye awe na uzima wa milele. “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Kwa maana Mungu hakumtuma Mwanawe kuuhukumu ulimwengu, bali kwa yeye ulimwengu upate kuokolewa. Ye yote amwaminiye hahukumiwi, lakini asiyeamini amekwisha kuhukumiwa, kwa sababu hakumwamini Mwana pekee wa Mungu. Hii ndiyo hukumu kwamba: Nuru imekuja ulimwenguni, nao watu wakapenda giza kuliko nuru kwa sababu matendo yao ni maovu. Kwa kuwa kila atendaye maovu huchukia nuru, wala haji kwenye nuru ili matendo yake maovu yasifichuliwe. Lakini wale watendao yaliyo mema huja kwenye nuru, kusudi ionekane wazi kwamba matendo yao yametendeka katika Mungu.”
”Baadaye Yesu akamkuta yule mtu aliyemponya ndani ya Hekalu na kumwambia, “Tazama umeponywa, usitende dhambi tena. La sivyo, lisije likakupata jambo baya zaidi.”
”Wakamwambia Yesu, “Mwalimu, huyu mwanamke amekutwa akizini. Katika sheria, Mose alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake wa namna hii, mpaka wafe. Sasa wewe wasemaje?” Walimwuliza swali hili kama mtego ili wapate sababu ya kumshtaki. Lakini Yesu akainama akaanza kuandika ardhini kwa kidole chake. Walipoendelea kumwulizauliza akainuka, akawaambia, “Kama kuna mtu ye yote miongoni mwenu ambaye hana dhambi na awe wa kwanza kumtupia jiwe.” Akainama tena na kuandika ardhini. Waliposikia haya, wakaanza kuondoka mmoja mmoja, wakianzia wazee, hadi Yesu akabaki peke yake na yule mwanamke akiwa amesimama mbele yake. Yesu akainuka na kumwambia, “Wako wapi wale waliokuwa wanakuhukumu kuwa mwenye hatia?” Yule mwanamke akajibu, “Hakuna hata mmoja Bwana.” Yesu akamwambia, “Hata mimi sikuhukumu. Nenda zako, kuanzia sasa usitende dhambi tena.”]
”Niliwaambia kuwa mtakufa katika dhambi zenu, kwa maana msipoamini ya kwamba ‘Mimi Ndiye,’ mtakufa katika dhambi zenu.”
”Yesu akajibu, “Amin, amin nawaambia, kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.
”Tunajua ya kuwa Mungu hawasikilizi wenye dhambi, lakini huwasikiliza wote wanaomcha na kumtii.
”Yuko amhukumuye yeye anikataaye mimi na kutokuyapokea maneno yangu, yaani, yale maneno niliyosema yenyewe yatamhukumu siku ya mwisho.
”“Kama mnanipenda, mtazishika amri zangu.
”Naye atakapokuja, atauthibitishia ulimwengu kuhusu dhambi, haki na hukumu. Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi, kwa habari ya haki, kwa sababu ninakwenda kwa Baba, nanyi hamtaniona tena, kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa.
”Petro akawajibu, “Tubuni, mkabatizwe kila mmoja wenu kwa jina la Yesu Kristo, ili mpate kusamehewa dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
”Tubuni basi mkamgeukie Mungu, ili dhambi zenu zifutwe, ili zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwepo kwake Bwana.
”“Ninyi watu wenye shingo ngumu, msiotahiriwa mioyo wala masikio, daima hamwachi kumpinga Roho Mtakatifu, kama walivyofanya baba zetu.
”Kwa hiyo tubia huu uovu wako na umwombe Mungu, ili yamkini, aweze kusamehe mawazo uliyo nayo moyoni mwako.
”Sasa basi, mbona unakawia? Inuka, ukabatizwe na dhambi zako zikasafishwe, ukiliita Jina lake.’
”Ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni dhidi ya uasi wote na uovu wa wanadamu ambao huipinga kweli kwa uovu wao,
”Kwa hiyo, Mungu akawaacha wazifuate tamaa mbaya za mioyo yao katika uasherati, hata wakavunjiana heshima miili yao wao kwa wao. Kwa sababu waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakaabudu na kutumikia kiumbe badala ya Muumba, ahimidiwaye milele! Amen. Kwa sababu hii, Mungu aliwaacha wavunjiane heshima kwa kufuata tamaa zao za aibu. Hata wanawake wao wakabadili matumizi ya asili ya miili yao wakaitumia isivyokusudiwa. Vivyo hivyo wanaume pia wakiacha matumizi ya asili ya wanawake wakawakiana tamaa wao kwa wao. Wanaume wakafanyiana matendo ya aibu na wanaume wengine nao wakapata katika maisha yao adhabu iliyowastahili kwa ajili ya upotovu wao.
”Nao kwa kuwa walikataa kumkubali Mungu, yeye akawaacha wafuate akili zao za upotovu, watende mambo yale yasiyostahili kutendwa. Wakiwa wamejawa na udhalimu wa kila namna, uasherati, uovu, tamaa mbaya na hila. Wamejawa na husuda, uuaji, ugomvi, udanganyifu, hadaa na nia mbaya. Wao pia ni wasengenyaji, wasingiziaji, wanaomchukia Mungu, wajeuri, wenye kiburi na majivuno, wenye hila, wasiotii wazazi wao, wajinga, wasioamini, wasio na huruma na wakatili. Ingawa wanafahamu sheria ya haki ya Mungu kwamba watu wanaofanya mambo kama hayo wanastahili mauti, si kwamba wanaendelea kutenda hayo tu, bali pia wanakubaliana na wale wanaoyatenda.
”Kwa hiyo huna udhuru wo wote, wewe mtu uwaye yote, utoaye hukumu kwa mwingine, kwa maana katika jambo lo lote unalowahukumu wengine, unajihukumu wewe mwenyewe kwa sababu wewe unayehukumu unafanya mambo yayo hayo.
”Lakini kwa wale watafutao mambo yao wenyewe na wale wanaokataa kweli na kuzifuata njia mbaya, kutakuwa na ghadhabu na hasira ya Mungu. Kutakuwa na taabu na dhiki kwa kila mmoja atendaye maovu, Myahudi kwanza na mtu Mataifa pia,
”Hili litatukia siku hiyo Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu kwa njia ya Yesu Kristo, kama isemavyo Injili yangu.
”Tusemeje basi? Je, sisi ni bora kuliko wao? La hasha! Kwa maana tumekwisha kuhakikisha kwa vyo vyote kwamba Wayahudi na watu Mataifa wote wako chini ya nguvu ya dhambi. Kama ilivyoandikwa: “Hakuna mwenye haki, hakuna hata mmoja. Hakuna hata mmoja mwenye ufahamu, hakuna hata mmoja amtafutaye Mungu. Wote wamegeukia mbali, wote kwa pamoja hawafai; hakuna atendaye mema, naam, hata mmoja.”
”“Hakuna hofu ya Mungu machoni pao.” Basi tunajua ya kwamba cho chote sheria inachosema, inawaambia wale walio chini ya sheria ili kila kinywa kinyamazishwe na ulimwengu wote uwajibike kwa Mungu.
”Kwa hiyo hakuna binadamu hata mmoja atakayehesabiwa haki mbele za Mungu kwa matendo ya sheria, kwa maana sheria hutufanya tuitambue dhambi.
”kwa kuwa wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu, wanahesabiwa haki bure kwa neema yake kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu. Yeye ambaye Mungu alimtoa awe dhabihu ya upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake. Alifanya hivi ili kuonyesha haki yake, kwa sababu kwa ustahimili wake aliziachilia zile dhambi zilizotangulia kufanywa.
”“Wamebarikiwa wale ambao uovu wao umesamehewa ambao dhambi zao zimefutwa.
”Lakini Mungu anaudhihirisha upendo wake kwetu kwamba: Tulipokuwa tungali wenye dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yetu. Basi, kwa kuwa sasa tumehesabiwa haki kwa damu yake, si zaidi sana tutaokolewa kutoka katika ghadhabu ya Mungu kwa yeye!
”Kwa hiyo kama vile dhambi ilivyoingia ulimwenguni kupitia kwa mtu mmoja na kupitia dhambi hii, mauti ikawafikia watu wote, kwa sababu wote wamefanya dhambi. Kwa maana kabla sheria haijatolewa, dhambi ilikuwepo ulimwenguni. Lakini dhambi haihesabiwi wakati hakuna sheria.
”Zaidi ya hayo, sheria ilikuja, ili uvunjaji wa sheria uongezeke. Lakini dhambi ilipoongezeka, neema iliongezeka zaidi. Ili kwamba kama vile dhambi ilivyotawala kwa njia ya mauti, vivyo hivyo neema iweze kutawala kwa njia ya kuhesabiwa haki hata uzima wa milele katika Yesu Kristo Bwana wetu.
”Tuseme nini basi? Je, tuendelee kutenda dhambi ili neema ipate kuongezeka? La hasha! Sisi tulioifia dhambi, tutawezaje kuendelea kuishi tena katika dhambi? Au hamjui ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?
”Kwa hiyo tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti, ili kama vile Kristo alivyofufuka kutoka kwa wafu kwa utukufu wa Baba, vivyo hivyo sisi nasi pia tupate kuenenda katika upya wa uzima. Kwa maana ikiwa tumeungana naye katika mauti yake, bila shaka tutaungana naye katika ufufuo wake. Kwa maana twajua kwamba utu wetu wa kale ulisulibiwa pamoja naye ili ule mwili wa dhambi upate kuangamizwa, nasi tusiendelee kuwa tena watumwa wa dhambi. Kwa maana mtu ye yote aliyekufa amewekwa huru mbali na dhambi.
”Kwa maana mtu ye yote aliyekufa amewekwa huru mbali na dhambi. Basi ikiwa tulikufa pamoja na Kristo, tunaamini kwamba pia tutaishi pamoja naye. Kwa maana tunajua kwamba Kristo, akiisha kufufuka kutoka kwa wafu, hatakufa tena, mauti haina tena mamlaka juu yake. Kifo alichokufa, aliifia dhambi mara moja tu, lakini uzima alio nao anamwishia Mungu. Vivyo hivyo, jihesabuni wafu katika dhambi lakini mlio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu.
”Kwa hiyo, msiruhusu dhambi itawale ndani ya miili yenu, ipatikanayo na kufa, ili kuwafanya mzitii tamaa mbaya. Wala msivitoe viungo vya miili yenu vitumike kama vyombo vya uovu vya kutenda dhambi, bali jitoeni kwa Mungu, kama watu waliotolewa kutoka mautini kuingia uzimani. Nanyi vitoeni viungo vya miili yenu kwake kama vyombo vya haki. Kwa maana dhambi haitakuwa na mamlaka juu yenu, kwa sababu hampo chini ya sheria, bali chini ya neema.
”Ni nini basi? Je, tutende dhambi kwa kuwa hatuko chini ya sheria bali chini ya neema? La, hasha! Je, hamjui kwamba mnapojitoa kwa mtu ye yote kama watumwa watiifu, ninyi ni watumwa wa yule mnayemtii, aidha watumwa wa dhambi, ambayo matokeo yake ni mauti, au watumwa wa utii ambao matokeo yake ni haki?
”Lakini Mungu ashukuriwe kwa kuwa ninyi ambao kwanza mlikuwa watumwa wa dhambi, mmekuwa watii kutoka moyoni kwa mafundisho mliyopewa, Nanyi, mkiisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mmekuwa watumwa wa haki. Ninasema kwa namna ya kibinadamu kwa sababu ya udhaifu wenu wa hali ya asili. Kama vile kwanza mlivyokuwa mmevitoa viungo vya miili yenu kama watumwa wa mambo machafu na uovu uliokuwa ukiongezeka zaidi na zaidi, hivyo sasa vitoeni viungo vya miili yenu vitumike kwa ajili ya haki ambayo matokeo yake ni utakatifu.
”Mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa hamtawaliwi na haki. Lakini mlipata faida gani kwa mambo hayo ambayo sasa mnayaonea aibu? Mwisho wa mambo hayo ni mauti.
”Lakini sasa kwa kuwa mmewekwa huru mbali na dhambi na mmekuwa watumwa wa Mungu, faida mnayopata ni utakatifu, ambao mwisho wake ni uzima wa milele. Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
”Kwa maana tulipokuwa tunatawaliwa na asili ya dhambi, tamaa za dhambi zilizochochewa na sheria zilikuwa zikitenda kazi katika miili yetu, hivyo tulizaa matunda ya mauti. Lakini sasa, kwa kufia kile kilichokuwa kimetufunga kwanza, tumewekwa huru kutoka katika sheria ili tutumike katika njia mpya ya Roho, wala si katika njia ya zamani ya sheria iliyoandikwa.
”Tuseme nini basi? Kwamba sheria ni dhambi? La, hasha! Lakini, isingekuwa kwa sababu ya sheria, nisingalijua dhambi. Nisingalijua kutamani ni nini kama sheria haikusema, “Usitamani.” Lakini dhambi kwa kupata nafasi katika amri, hii ikazaa ndani yangu kila aina ya tamaa. Kwa maana pasipo sheria, dhambi imekufa. Wakati fulani nilikuwa hai pasipo sheria, lakini amri ilipokuja, dhambi ikawa hai, nami nikafa. Nikaona kwamba ile amri iliyokusudiwa kuleta uzima, ilileta mauti. Kwa maana dhambi kwa kupata nafasi katika amri, ilinidanganya na kwa kupitia hiyo amri, ikaniua.
”Lakini dhambi kwa kupata nafasi katika amri, hii ikazaa ndani yangu kila aina ya tamaa. Kwa maana pasipo sheria, dhambi imekufa.
”Je, kile kilicho chema basi kilikuwa mauti kwangu? La, hasha! Lakini ili dhambi itambuliwe kuwa ni dhambi, ilileta mauti ndani yangu kupitia kile kilichokuwa chema, ili kwa njia ya amri dhambi izidi kuwa mbaya kupita kiasi.
”Kwa maana tunajua kwamba sheria ni ya kiroho, lakini mimi ni wa kimwili nikiwa nimeuzwa kwenye utumwa wa dhambi. Sielewi nitendalo, kwa maana lile ninalotaka kulitenda, silitendi, lakini ninatenda lile ninalolichukia. Basi kama ninatenda lile nisilotaka kutenda, ni kwamba ninakubali kuwa sheria ni njema. Lakini, kwa kweli si mimi tena nitendaye lile nisilotaka bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. Kwa maana ninafahamu kwamba hakuna jema lo lote likaalo ndani yangu, yaani, katika asili yangu ya dhambi. Kwa kuwa nina shauku ya kutenda lililo jema, lakini siwezi kulitenda. Sitendi lile jema nitakalo kutenda bali lile baya nisilolitaka, ndilo nitendalo. Basi kama ninatenda lile nisilotaka kutenda, si mimi tena nifanyaye hivyo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.
”Hivyo naiona sheria ikitenda kazi. Ninapotaka kutenda jema, jambo baya liko papo hapo. Kwa maana katika utu wangu wa ndani naifurahia sheria ya Mungu. Lakini ninaona kuna sheria nyingine inayotenda kazi katika viungo vya mwili wangu inayopigana vita dhidi ya ile sheria ya akili yangu. Sheria hii inanifanya mateka wa ile sheria ya dhambi inayofanya kazi katika viungo vya mwili wangu. Ole wangu mimi maskini! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti? Ashukuriwe Mungu kwa njia ya Yesu Kristo Bwana wetu! Hivyo basi, mimi mwenyewe kwa akili zangu ni mtumwa wa sheria ya Mungu, lakini katika asili ya dhambi ni mtumwa wa sheria ya dhambi.
”Kwa hiyo, sasa hakuna hukumu ya adhabu kwa wale walio ndani ya Kristo Yesu, wale ambao hawaenendi kwa kuufuata mwili bali kwa kufuata Roho. Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima katika Kristo Yesu imeniweka huru mbali na sheria ya dhambi na mauti. Kwa maana kile ambacho sheria haikuwa na uwezo wa kufanya, kwa vile ilivyokuwa dhaifu katika mwili, Mungu kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe kwa mfano wa mwanadamu mwenye mwili ulio wa dhambi na kwa ajili ya dhambi, yeye aliihukumu dhambi katika mwili, ili kwamba haki ipatikanayo kwa sheria itimizwe ndani yetu sisi, ambao hatuenendi kwa kuufuata mwili bali kwa kufuata Roho. Kwa maana wale wanaoishi kwa kuufuata mwili huziweka nia zao katika vitu vya mwili, lakini wale wanaoishi kwa kufuata Roho, huziweka nia zao katika mambo ya Roho. Kwa maana kuwa na nia ya mwili ni mauti, bali kuwa na nia inayoongozwa na Roho ni uzima na amani. Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui na Mungu, kwa maana haiitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii. Wale wanaotawaliwa na mwili, hawawezi kumpendeza Mungu.
”Kwa hiyo ndugu zangu, sisi tu wadeni, si wa mwili, ili tuishi kwa kuufuata mwili, kwa maana mkiishi kwa kuufuata mwili, mtakufa, lakini kama mkiyaua matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi.
”Hili ndilo Agano langu nao nitakapoziondoa dhambi zao.”
”Upendo lazima usiwe wa unafiki. Chukieni lililo ovu, shikamaneni na lililo jema.
”Kwa kuwa amri hizi zisemazo, “Usizini,” “Usiue,” “Usiibe,” “Usitamani,” na amri nyingine zote, zinajumlishwa katika amri hii moja: “Mpende jirani yako kama nafsi yako.”
”Basi na tuenende kwa adabu kama inavyopasa wakati wa mchana, si kwa kufanya karamu za ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu. Bali jivikeni Bwana Yesu Kristo, wala msifikiri jinsi mtakavyotimiza tamaa za miili yenu yenye asili ya dhambi.
”Basi kwa nini wewe wamhukumu ndugu yako? Au kwa nini wewe unamdharau ndugu yako? Kwa kuwa sote tutasimama mbele ya kiti cha Mungu cha hukumu.
”Lakini kama mtu ana shaka kuhusu kile anachokula, asile hicho kitu, kwa sababu hakula kwa imani. Kwa kuwa cho chote kinachofanywa pasipo imani ni dhambi.
”Ndugu zangu, nawasihi mjihadhari na kujiepusha na wale watu waletao matengano na kuweka vikwazo mbele yenu dhidi ya mafundisho mliyojifunza. Kwa maana watu kama hao hawamtumikii Bwana Kristo, bali wanatumikia tamaa zao wenyewe. Kwa kutumia maneno laini na ya kubembeleza, hupotosha mioyo ya watu wajinga.
”Je, hamjui ya kwamba ninyi ni Hekalu la Mungu na kwamba Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu ye yote akiliharibu Hekalu la Mungu, Mungu atamwangamiza mtu huyo, Kwa maana Hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.
”Niliwaandikia katika waraka wangu kuwa msishirikiane na wazinzi. Sina maana kwamba msishirikiane na wazinzi wa ulimwengu huu, au wenye tamaa mbaya, wanyang'anyi au waabudu sanamu. Kwa kufanya hivyo ingewalazimu mtoke humu ulimwenguni. Lakini sasa nawaandikia kwamba msishirikiane na mtu ye yote anayejiita ndugu, hali akiwa ni mzinzi, au mwenye tamaa mbaya, mwabudu sanamu au msingiziaji, mlevi au mdhalimu. Mtu kama huyo hata msile naye. Yanihusu nini kuwahukumu wale watu walio nje ya kanisa? Je, si mnapaswa kuwahukumu hao walio ndani ya kanisa? Mungu atawahukumu hao walio nje ya kanisa. “Ninyi mwondoeni huyo mtu mwovu miongoni mwenu.”
”Je, hamjui kwamba wasio haki hawataurithi Ufalme wa Mungu? Msidanganyike: Waasherati hawaurithi Ufalme wa Mungu, wala waombao sanamu, wala wahanithi, wala walawiti, wala wezi, wala wenye tamaa mbaya, wala walafi, wala wanaodhihaki, wala wanyang'anyi. Baadhi yenu mlikuwa kama hao. Lakini mlioshwa, mlitakaswa, mlihesabiwa haki kwa jina la Bwana Yesu Kristo na katika Roho wa Mungu wetu.
”Ikimbieni zinaa. Dhambi nyingine zote atendazo mtu ziko nje ya mwili wake, lakini yeye aziniye hutenda dhambi ndani ya mwili wake mwenyewe. Je, hamjui ya kwamba miili yenu ni Hekalu la Roho Mtakatifu akaaye ndani yenu, ambaye mmepewa na Mungu? Ninyi si mali yenu wenyewe, kwa maana mmenunuliwa kwa gharama. Kwa hiyo mtukuzeni Mungu katika miili yenu na katika roho zenu ambazo ni mali ya Mungu.
”Wala tusifanye uzinzi kama baadhi yao walivyofanya, wakafa watu 23,000 kwa siku moja. Wala tusimjaribu Bwana, kama baadhi yao walivyofanya, wakafa kwa kuumwa na nyoka. Msinung'unike kama baadhi yao walivyofanya, wakaangamizwa na mharabu. Mambo haya yote yaliwapata wao ili yawe mifano kwa wengine, nayo yaliandikwa ili yatuonye sisi ambao mwisho wa nyakati umetufikia. Hivyo, yeye ajidhaniaye amesimama, aangalie asianguke.
”Hakuna jaribu lo lote lililowapata ambalo si la kawaida kwa wanadamu. Naye Mungu ni mwaminifu ambaye hataruhusu mjaribiwe kupita mnavyoweza. Lakini mnapojaribiwa atawapa njia ya kutokea ili mweze kustahimili.
”Kwa maana yale niliyopokea ndiyo niliyowapa ninyi, kama yenye umuhimu wa kwanza: Kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yasemayo Maandiko, ya kuwa alizikwa na alifufuka siku ya tatu,
”Msidanganyike: “Ushirika na watu wabaya huharibu tabia njema.” Zindukeni mwe na akili kama iwapasavyo, msitende dhambi tena; kwa maana watu wengine hawamjui Mungu. Nasema mambo haya ili mwone aibu.
”Uchungu wa mauti ni dhambi na nguvu ya dhambi ni sheria.
”Kwa kuwa sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mmoja apate kulipwa kwa ajili ya yale ambayo yametendwa katika mwili wake, yakiwa mema au mabaya.
”Kwa maana Mungu alimfanya yeye asiyekuwa na dhambi kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kufanywa haki ya Mungu katika yeye.
”Wapenzi, kwa kuwa tunazo ahadi hizi, basi na tujitakase nafsi zetu kutokana na kila kitu kitiacho mwili na roho unajisi, tukitimiza utakatifu kwa kumcha Mungu.
”Kwa kuwa nina hofu ya kwamba nitakapokuja naweza kuwakuta nisivyotaka, nanyi mkanikuta msivyotaka. Nina hofu kwamba panaweza kuwa na ugomvi, wivu, ghadhabu, fitina, masingizio, masengenyo, majivuno na machafuko. Nina hofu kwamba nitakapokuja tena kwenu, Mungu wangu atanidhili mbele yenu, nami nitasikitishwa na wengi waliotenda dhambi huko nyuma na wala hawajatubia uchafu wao, yaani, uasherati na ufisadi walioufanya.
”Lakini Maandiko yamefanya vitu vyote vifungwe chini ya nguvu ya dhambi, ili yale yaliyoahidiwa kwa njia ya imani katika Yesu Kristo yapate kupewa wale wanaoamini.
”Kwa hiyo nasema, enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa maana mwili hutamani yale yaliyo kinyume na Roho, nayo Roho hutamani yale yaliyo kinyume na mwili. Roho na mwili hupingana na kwa sababu hiyo hamwezi kufanya mnayotaka. Lakini kama mkiongozwa na Roho, hamko chini ya sheria.
”Basi matendo ya mwili ni dhahiri nayo ni haya: Uasherati, uchafu, ufisadi, kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine yanayofanana na hayo. Nawaonya, kama nilivyokwisha kuwaonya kabla, kwamba watu watendao mambo kama hayo, hawataurithi Ufalme wa Mungu.
”Wote walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili na shauku zake pamoja na tamaa zake. Kwa kuwa tunaishi kwa Roho, basi, tuenende kwa Roho.
”Ndugu zangu, ikiwa mtu ameghafilika akatenda dhambi, basi ninyi mlio wa rohoni, mrejezeni upya mtu huyo kwa roho ya upole. Lakini jihadharini, ili ninyi wenyewe msije mkajaribiwa.
”Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi. Kwa kuwa kile apandacho mtu ndicho atakachovuna. Apandaye kwa mwili, katika mwili wake, atavuna uharibifu, lakini yeye apandaye katika Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele.
”Katika yeye tunao ukombozi kwa njia ya damu yake, yaani, msamaha wa dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake
”Kwa habari zenu, mlikuwa wafu katika makosa na dhambi zenu, ambazo mlizitenda mlipofuatisha namna ya ulimwengu huu na za yule mtawala wa ufalme wa anga, yule roho atendaye kazi sasa ndani ya wale wasiotii. Sisi sote pia tuliishi katikati yao hapo zamani, tukitimiza tamaa za asili yetu ya dhambi na kufuata tamaa zake na mawazo yake. Nasi kwa asili tulikuwa wana wa ghadhabu, kama mtu mwingine ye yote.
”Hivyo nawaambia hivi, nami nasisitiza katika Bwana kwamba, msiishi tena kama watu Mataifa waishivyo, katika ubatili wa mawazo yao. Watu hao akili zao zimetiwa giza na wametengwa mbali na uzima wa Mungu kwa sababu ya ujinga wao kutokana na ugumu wa mioyo yao. Wakiisha kufa ganzi, wamejitia katika mambo ya ufisadi na kupendelea kila aina ya uchafu, wakiendelea kutamani zaidi.
”Mlifundishwa kuuvua mwenendo wenu wa zamani, utu wenu wa kale, ulioharibiwa na tamaa zake za udanganyifu, ili mfanywe upya roho na nia zenu, mkajivike utu mpya, ulioumbwa sawasawa na mfano wa Mungu katika haki yote na utakatifu.
”Ondoeni kabisa uchungu, ghadhabu, hasira, makelele na masingizio pamoja na kila aina ya uovu.
”Lakini uasherati, usitajwe miongoni mwenu, wala uchafu wa aina yo yote, wala tamaa, kwa sababu mambo haya hayastahili miongoni mwa watakatifu. Wala pasiwepo mazungumzo machafu ya aibu, au maneno ya upuzi au mzaha, ambayo hayafai, badala yake mshukuruni Mungu. Kwa habari ya mambo haya mjue hakika kwamba: Mwasherati, wala mtu mwovu, wala mwenye tamaa mbaya, mtu kama huyo ni mwabudu sanamu, kamwe hataurithi Ufalme wa Kristo na wa Mungu. Mtu ye yote na asiwadanganye kwa maneno matupu, kwa kuwa hasira ya Mungu huwaka kwa sababu ya mambo kama haya juu ya wale wasiomtii.
”Msishiriki matendo ya giza yasiyofaa, bali yafichueni. Kwa maana ni aibu hata kutaja mambo yale ambayo wasiotii wanayafanya sirini.
”Pia msilewe kwa mvinyo, ambamo ndani yake mna upotovu, bali mjazwe Roho.
”Hapo kwanza ninyi mlikuwa mmetengana na Mungu na mlikuwa adui zake katika nia zenu kwa sababu ya mwenendo wenu mbaya. Lakini sasa Mungu amewapatanisha ninyi kwa njia ya mwili wa Kristo kwa kupitia mauti, ili awalete mbele zake mkiwa watakatifu, bila dosari wala lawama,
”Kwa hiyo, ueni kabisa cho chote kilicho ndani yenu cha asili ya kidunia: Yaani, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya na kutamani, ambayo ndiyo ibada ya sanamu. Kwa sababu ya mambo haya, ghadhabu ya Mungu inakuja. Ninyi pia zamani mlienenda katika mambo haya mlipoishi maisha hayo. Lakini sasa yawekeni mbali nanyi mambo kama haya yote, yaani: Hasira, ghadhabu, uovu, masingizio na lugha chafu kutoka midomoni mwenu. Msiambiane uongo kwa maana mmevua kabisa utu wenu wa kale pamoja na matendo yake,
”Ye yote atendaye mabaya atalipwa kwa ajili ya mabaya yake, wala hakuna upendeleo.
”Kwa maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu ninyi mwe watakatifu, ili kwamba mjiepushe na uasherati, ili kwamba kila mmoja wenu ajifunze kuutawala mwili wake mwenyewe katika utakatifu na heshima,
”Kwa maana Mungu hakutuitia uchafu, bali utakatifu. Kwa hiyo, mtu ye yote anayekataa mafundisho haya hamkatai mwanadamu, bali anamkataa Mungu anayewapa ninyi Roho wake Mtakatifu.
”Jaribuni kila kitu. Yashikeni yaliyo mema. Jiepusheni na uovu wa kila namna. Mungu mwenyewe, Mungu wa amani, awatakase ninyi kabisa. Nanyi mhifadhiwe roho zenu, nafsi zenu na miili yenu, bila kuwa na lawama katika Bwana wetu Yesu Kristo.
”Atawaadhibu wale wasiomjua Mungu na ambao hawakuitii Injili ya Bwana wetu Yesu.
”Lakini tunajua ya kuwa sheria si kwa ajili ya wenye haki, bali kwa ajili ya wavunja sheria na waasi, kwa ajili ya wasiomcha Mungu na wenye dhambi, wasio watakatifu na wanaokufuru, kwa wale wawauao baba zao au mama zao, kwa wauaji, kwa wazinzi na wahanithi, wauza watu na kwa waongo na waapao kwa uongo, na kwa cho chote kingine kilicho kinyume na mafundisho ya kweli,
”Msemo huu ni wa kweli na unaostahili kukubalika, usemao kwamba: Kristo Yesu alikuja ulimwenguni kuokoa wenye dhambi, ambao mimi ndiye niliye mbaya kuliko wote. Lakini kwa sababu hiyo nilipata rehema, ili kwamba katika mimi niliyekuwa mwenye dhambi kuliko wote, Kristo Yesu apate kuonyesha uvumilivu wake usio na kikomo, niwe kielelezo kwa wale watakaomwamini wapate uzima wa milele.
”Wale wanaodumu katika dhambi uwakemee hadharani, ili wengine wapate kuogopa.
”Dhambi za watu wengine ni dhahiri nazo zinawatangulia kwenda hukumuni na dhambi za watu wengine zinawafuata nyuma yao.
”Lakini wale watu wanaotamani kuwa na mali kwa haraka haraka huanguka kwenye majaribu na wamenaswa na tamaa nyingi za kipumbavu, zenye kudhuru, zinazowazamisha watu katika uharibifu na maangamizi. Kwa maana kupenda fedha ndiyo shina moja la maovu ya kila namna. Baadhi ya watu wakitamani fedha, wameiacha imani na kujichoma wenyewe kwa maumivu mengi.
”Kwa maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kumkufuru Mungu, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio watakatifu, wasio na upendo, wasiopenda kupatanishwa, wasingiziaji, wasiozuia tamaa zao, wakatili, wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi, waliojaa majivuno, wapendao anasa zaidi kuliko kumpenda Mungu. Wakiwa na mfano wa utauwa kwa nje lakini wakizikana nguvu za Mungu. Jiepushe na watu wa namna hiyo. Miongoni mwao wamo wale wajiingizao katika nyumba za watu na kuwachukua mateka wanawake wajinga, waliolemewa na dhambi zao na kuyumbishwa na aina zote za tamaa mbaya. Wakijifunza siku zote lakini kamwe wasiweze kufikia ujuzi wa kweli.
”Lakini watu waovu na wadanganyaji watazidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika.
”Wanadai kumjua Mungu, lakini kwa matendo yao wanamkana. Hao watu ni chukizo, wasiotii, wasiofaa kwa jambo lo lote jema.
”Maana sisi wenyewe wakati fulani tulikuwa wajinga, wasiotii, tukiwa watumwa wa tamaa mbaya na anasa za kila aina. Tuliishi katika uovu na wivu, tukichukiwa na kuchukiana sisi kwa sisi.
”Kwa kuwa yeye mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wale wanaojaribiwa.
”Lakini mtiane moyo mtu na mwenzake kila siku, maadamu iitwapo Leo, ili asiwepo hata mmoja wenu mwenye kufanywa mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.
”Kama ilivyonenwa: “Leo, kama mtaisikia sauti yake, msifanye mioyo yenu migumu kama mlivyofanya wakati wa kuasi.”
”Kwa kuwa hatuna Kuhani Mkuu asiyeweza kuchukuliana na sisi katika udhaifu wetu, lakini tunaye mmoja ambaye alijaribiwa kwa kila namna, kama vile sisi tujaribiwavyo, lakini yeye hakutenda dhambi.
”kwa sababu kwa dhabihu moja amewafanya kuwa wakamilifu milele wale wote wanaotakaswa. Pia Roho Mtakatifu anatushuhudia kuhusu jambo hili. Kwanza anasema: “Hili ndilo Agano nitakalofanya nao baada ya siku hizo, asema Bwana. Nitaziweka sheria zangu mioyoni mwao, na kuziandika katika nia zao.” Kisha aongeza kusema: “Dhambi zao na kutokutii kwao sitakumbuka tena.” Basi haya yakiisha kusamehewa, hakuna tena dhabihu yo yote inayotolewa kwa ajili ya dhambi.
”Kama tukiendelea kutenda dhambi kwa makusudi baada ya kupokea ufahamu wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi. Lakini kinachobaki ni kungoja kwa hofu hukumu ya moto uwakao utakaowaangamiza adui za Mungu. Ye yote aliyeikataa sheria ya Mose alikufa pasipo huruma kwa ushahidi wa watu wawili au watatu. Je, mnadhani ni adhabu kali kiasi gani anayostahili kupewa mtu aliyemkanyaga Mwana wa Mungu chini ya nyayo zake, yeye aliyeifanya damu ya Agano iliyomtakasa kuwa kitu najisi na kumtendea maovu Roho wa neema? Kwa kuwa tunamjua yeye aliyesema, “Kulipiza kisasi ni juu yangu; mimi nitalipiza.” Tena asema, “Bwana atawahukumu watu wake.” Ni jambo la kutisha kuanguka mikononi mwa Mungu aliye hai.
”Kwa sababu hii, kwa kuwa tumezungukwa na wingu kubwa namna hii la mashahidi, basi na tuweke kando kila kitu kinachotuzuia na ile dhambi inayotuzinga kwa urahisi, nasi tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa kwa ajili yetu.
”Katika kushindana kwenu dhidi ya dhambi, bado hamjapigana kiasi cha kumwaga damu yenu.
”Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote na huo utakatifu, ambao bila kuwa nao, hakuna mtu atakayemwona Bwana.
”Ndoa na iheshimiwe na watu wote, nayo malazi yawe safi, kwa kuwa Mungu atawahukumu wazinzi na waasherati wote.
”Heri mtu anayevumilia wakati wa majaribu, kwa sababu akiisha kushinda hilo jaribio atapewa taji ya uzima Mungu aliyowaahidia wale wampendao. Mtu anapojaribiwa asiseme, “Ninajaribiwa na Mungu.” Kwa maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu wala yeye hamjaribu mtu ye yote. Lakini kila mtu hujaribiwa wakati anapovutwa na kudanganywa na tamaa zake mwenyewe zilizo mbaya. Basi ile tamaa mbaya ikishachukua mimba, huzaa dhambi, ile dhambi ikikomaa, huzaa mauti. Ndugu zangu, msidanganyike.
”Kwa hiyo, ondoleeni mbali uchafu wote na uovu ambao umezidi kuwa mwingi, mkalipokee kwa unyenyekevu lile Neno lililopandwa ndani yenu ambalo laweza kuokoa nafsi zenu. Basi iweni watendaji wa Neno wala msiwe wasikiaji tu, huku mkijidanganya nafsi zenu.
”Kwa maana mtu ye yote anayeishika sheria yote lakini akajikwaa katika kipengele kimoja tu, ana hatia ya kuivunja sheria yote.
”Ni kitu gani kinachosababisha mapigano na ugomvi miongoni mwenu? Je, haya hayatokani na tamaa zenu zinazoshindana ndani yenu? Mnatamani lakini hampati, kwa hiyo mwaua. Mwatamani kupata lakini hampati vile mnavyotaka, kwa hiyo mnajitia katika magomvi na mapigano. Mmepungukiwa kwa sababu hamumwombi Mungu.
”Ninyi wanaume na wanawake wazinzi, hamjui ya kwamba urafiki na dunia ni uadui na Mungu? Kwa hiyo mtu ye yote anayetaka kuwa rafiki wa dunia hufanyika adui wa Mungu. Au mwadhani kwamba Andiko lasema bure kuwa, huyo Roho ambaye Mungu amemweka ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu? Lakini yeye hutupatia neema zaidi. Hii ndiyo sababu Andiko husema: “Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.” Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, ninyi wenye dhambi na kuisafisha mioyo yenu, ninyi wenye nia mbili. Huzunikeni, ombolezeni na kulia. Kicheko chenu na kigeuzwe kuwa kuomboleza na furaha yenu kuwa huzuni. Jinyenyekezeni mbele za Bwana, naye atawainua.
”Ndugu, msineneane mabaya ninyi kwa ninyi. Mtu ye yote anayesema mabaya dhidi ya ndugu yake au kumhukumu anasema dhidi ya sheria na kuihukumu. Unapoihukumu sheria, basi huishiki sheria bali umekuwa hakimu wa kuihukumu hiyo sheria. Yuko Mtoa-Sheria mmoja tu na yeye peke yake ndiye Hakimu, ndiye awezaye kuokoa au kuangamiza. Lakini wewe ni nani hata umhukumu jirani yako?
”Basi mtu ye yote anayejua jema limpasalo kutenda, lakini asilitende, mtu huyo anatenda dhambi.
”hamna budi kujua kwamba ye yote amrejezaye mwenye dhambi kutoka katika upotovu wake, ataiokoa roho ya huyo mwenye dhambi kutoka katika mauti na kusitiri wingi wa dhambi.
”Kama watoto watiifu, msifuate tamaa zenu mbaya za kwanza za wakati wa ujinga. Bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote, kwa maana imeandikwa: “Mtakuwa watakatifu, kwa kuwa Mimi ni mtakatifu.”
”Kwa hiyo, wekeni mbali nanyi uovu wote na udanganyifu wote, unafiki, wivu na masingizio ya kila namna.
”Wapenzi, ninawasihi, mkiwa kama wageni na wapitaji hapa ulimwenguni, epukeni tamaa mbaya za mwili ambazo hupigana vita na roho zenu.
”Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, ili kwamba tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tupate kuishi katika haki. Kwa kupigwa kwake, ninyi mmeponywa. Kwa maana mlikuwa mmepotea kama kondoo, lakini sasa mmerudi kwa Mchungaji na Mwangalizi wa roho zenu.
”Kwa kuwa Kristo naye aliteswa mara moja tu, mwenye haki kwa ajili ya wasio na haki, ili awalete ninyi kwa Mungu. Mwili wake ukauawa, lakini akafanywa hai katika Roho,
”Kwa hiyo, kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni nia iyo hiyo kwa maana mtu aliyekwisha kuteswa katika mwili ameachana na dhambi. Matokeo yake, maisha yake yaliyobaki ya kuishi hapa duniani, haishi tena kwa kufuata tamaa mbaya za wanadamu, bali anaishi kwa kufuata mapenzi ya Mungu. Maana wakati uliopita mmekwisha kutumia muda wa kutosha katika maisha yenu mkifanya yale ambayo watu wasiomjua Mungu hupenda kutenda, wakiishi katika uasherati, tamaa mbaya, ulevi, karamu za ulafi, vileo, ngoma mbaya na ibada za sanamu ambazo ni chukizo.
”Nao katika tamaa zao mbaya, watajipatia faida kwenu kwa maneno ya madanganyo waliyotunga wenyewe. Lakini hukumu imekwisha kutangazwa dhidi yao tangu zamani, ambayo haikawii wala uangamivu wao haujalala usingizi. Kwa maana kama Mungu hakuwasamehe malaika walipotenda dhambi, bali aliwatupa kuzimu, katika vifungo vya giza wakae humo mpaka ije hukumu;
”ikiwa hivyo ndivyo, basi Bwana anajua jinsi ya kuwaokoa wacha Mungu kutoka katika majaribu na kuwaweka waasi katika adhabu hadi siku ya hukumu. Hii ni hakika hasa kwa wale wanaofuata tamaa mbaya za mwili na kudharau mamlaka. Kwa ushupavu na kwa kiburi watu hawa hawaogopi kunena mabaya dhidi ya viumbe vya mbinguni,
”Wakiwa na macho yaliyojaa uzinzi, kamwe hawaachi kutenda dhambi. Huwashawishi wale wasio imara, wao ni hodari kwa kutamani, wana wa laana!
”Imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli isemayo: “Mbwa ameyarudia matapishi yake mwenyewe,” tena nyingine yasema, “Nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaagaa matopeni.”
”Kwanza kabisa, ni lazima mfahamu ya kwamba siku za mwisho watakuja watu wenye dhihaka wakidhihaki na kuzifuata tamaa zao mbaya,
”Kama tukisema kwamba twashirikiana naye huku tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatutendi lililo kweli. Lakini tukienenda nuruni, kama yeye alivyo nuruni, twashirikiana sisi kwa sisi na damu yake Yesu, Mwana wake yatusafisha dhambi yote. Kama tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe wala kweli haimo ndani yetu. Kama tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki, atatusamehe dhambi zetu na kutusafisha toka kwenye udhalimu wote. Kama tukisema hatukutenda dhambi, twamfanya yeye kuwa mwongo na neno lake halimo ndani yetu.
”Watoto wangu wapendwa, nawaandikieni haya ili msitende dhambi. Lakini kama mtu ye yote akitenda dhambi, tunaye mwombezi kwa Baba: ndiye Yesu Kristo mwenye haki. Yeye ndiye dhabihu ya upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu, wala si kwa ajili ya dhambi zetu tu, bali pia kwa ajili ya dhambi za ulimwengu wote. Basi katika hili twajua ya kuwa tumemjua kama tunazishika amri zake. Mtu ye yote asemaye kuwa, “Ninamjua” lakini hazishiki amri zake, ni mwongo, wala ndani ya mtu huyo hamna kweli. Lakini kama mtu ye yote analitii neno lake, upendo wa Mungu umekamilika ndani yake kweli kweli. Katika hili twajua kuwa tumo ndani yake. Ye yote anayesema anakaa ndani yake hana budi kuenenda kama Yesu alivyoenenda.
”Lakini ye yote amchukiaye ndugu yake, yuko gizani na anaenenda gizani, wala hajui anakokwenda, kwa sababu giza limempofusha macho.
”Nawaandikia ninyi, watoto wadogo, kwa sababu dhambi zenu zimesamehewa kwa ajili ya Jina lake.
”Msiupende ulimwengu wala mambo yaliyoko ulimwenguni. Kama mtu ye yote akiupenda ulimwengu, upendo wa Baba haumo ndani yake. Kwa maana kila kitu kilichomo ulimwenguni, yaani tamaa ya mwili, tamaa ya macho na kiburi cha uzima: havitokani na Baba bali hutokana na ulimwengu. Nao ulimwengu unapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu milele.
”Kila mtu atendaye dhambi afanya uasi, kwa kuwa dhambi ni uasi. Lakini mwajua ya kuwa yeye alidhihirishwa ili aziondoe dhambi, wala ndani yake hamna dhambi. Kila mtu akaaye ndani yake hatendi dhambi. Kila mtu atendaye dhambi hakumwona yeye wala hakumtambua. Watoto wadogo, mtu ye yote asiwadanganye. Kila mtu atendaye haki ana haki, kama yeye alivyo na haki. Yeye atendaye dhambi ni wa ibilisi, kwa sababu ibilisi amekuwa akitenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa ili aziangamize kazi za ibilisi. Ye yote aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wa Mungu wakaa ndani yake, wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa na Mungu. Kwa jinsi hii tunaweza kujua dhahiri watoto wa Mungu na pia watoto wa ibilisi. Ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.
”Ye yote amchukiaye ndugu yake ni mwuaji, nanyi mwajua ya kwamba mwuaji hana uzima wa milele ndani yake.
”Ikiwa mtu anavyo vitu vya ulimwengu huu na akamwona ndugu yake ni mhitaji lakini asimhurumie, upendo wa Mungu wakaaje ndani ya mtu huyo?
”Hili ndilo pendo, si kwamba tulimpenda Mungu, bali yeye alitupenda, akamtuma Mwanawe, ili yeye awe dhabihu ya kipatanisho kwa ajili ya dhambi zetu.
”Kama mtu akimwona ndugu yake anatenda dhambi isiyo ya mauti, inampasa aombe, naye Mungu atampa uzima mtu huyo, ninamaanisha, wale ambao dhambi yao si ya mauti. Iko dhambi ya mauti, sisemi kwamba utaomba kwa ajili ya hiyo. Jambo lo lote lisilo la haki ni dhambi, lakini iko dhambi isiyo ya mauti. Tunajua ya kuwa yeye aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, bali aliyezaliwa na Mungu hujilinda wala yule mwovu hawezi kumdhuru.
”Mtu ye yote asiyedumu katika mafundisho ya Kristo, bali akayaacha, yeye hana Mungu. Ye yote anayedumu katika mafundisho ana Baba na Mwana pia. Msimpokee mtu ye yote anayewajia ambaye hawaletei mafundisho haya, wala msimkaribishe nyumbani mwenu. Ye yote amkaribishaye mtu wa namna hiyo anashiriki katika matendo maovu ya mtu huyo.
”ili kumhukumu kila mmoja na kuwapatiliza wote wasiomcha Mungu kwa matendo yao yote ya uasi waliyoyatenda, pamoja na maneno yote ya kuchukiza ambayo wenye dhambi wamesema dhidi yake.”
”Watu hawa ni wenye kunung'unika na wenye kutafuta makosa; wao hufuata tamaa zao mbaya, hujisifu kwa maneno makuu kuhusu wao wenyewe na kuwasifu mno watu wenye vyeo kwa ajili ya kujipatia faida.
”Basi tubuni! Ama sivyo, nitakuja kwako upesi na kupigana na watu hao kwa upanga wa kinywa changu.
”Nimempa muda ili atubie uasherati wake, lakini hataki.
”Nayajua matendo yako, ya kwamba wewe si baridi wala si moto. Afadhali ungelikuwa baridi au moto. Hivyo kwa kuwa u uvuguvugu, kwamba wewe si baridi wala si moto, nitakutapika utoke kinywani mwangu.
”Wala hawakutubu na kuacha matendo yao ya uuaji, uchawi, uasherati wala wizi wao.
”Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni ikisema: “Tokeni katikati yake, enyi watu wangu, ili msije mkashiriki dhambi zake, ili msije mkapatwa na pigo lake lo lote; kwa kuwa dhambi zake zimerundikana hadi mbinguni, naye Mungu ameukumbuka uhalifu wake.
”Kisha nikaona kiti kikubwa cheupe cha enzi pamoja na yeye aliyeketi juu yake. Dunia na mbingu zikaukimbia uso wake wala mahali pao hapakuonekana. Nami nikawaona wafu wakubwa na wadogo, wakiwa wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi na vitabu vikafunguliwa. Pia kitabu kingine kikafunguliwa ambacho ni cha uzima. Hao wafu wakahukumiwa sawasawa na matendo yao kama yalivyoandikwa ndani ya hivyo vitabu.
”Lakini waoga, wasioamini, wachafu, wauaji, wazinzi, wachawi, waabudu sanamu, pamoja na waongo wote, mahali pao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.”
”Lakini kitu kichafu hakitaingia humo kamwe, wala mtu ye yote atendaye mambo ya aibu au ya udanganyifu. Bali watakaoingia humo ni wale tu ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.
”Atendaye mabaya na aendelee kutenda mabaya, aliye mchafu na aendelee kuwa mchafu, yeye atendaye haki na aendelee kutenda haki na yeye aliye mtakatifu na aendelee kuwa mtakatifu.”
”Huko nje wako mbwa, wachawi, wazinzi, wauaji, waabuduo sanamu na kila mtu apendaye udanganyifu na kuufanya.
”