20 – Maombi
Haya ni maneno matakatifu ya Mungu Mwenyezi.
Hatupendi maneno ya wanadamu.
Kwa mtu yeyote anayempenda Mungu... hivi ndivyo Mungu anasema kuhusu: Maombi.
Haya ni maneno matakatifu ya Mungu Mwenyezi.
Hatupendi maneno ya wanadamu.
Kwa mtu yeyote anayempenda Mungu... hivi ndivyo Mungu anasema kuhusu: Maombi.
Kwa maana macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, na masikio yake husikiliza maombi yao, bali uso wa Bwana ni dhidi yao watendao maovu.”
”(Kwa Mwimbishaji: Kwa Filimbi. Zaburi Ya Daudi) Ee BWANA, tegea sikio maneno yangu, uangalie kupiga kite kwangu. Sikiliza kilio changu ili unisaidie, Mfalme wangu na Mungu wangu, kwa maana kwako ninaomba. Asubuhi, unasikia sauti yangu, Ee BWANA; asubuhi naleta haja zangu mbele zako, na kusubiri kwa matumaini.
”“Hivi basi, ndivyo iwapasavyo kuomba: “ ‘Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe. Ufalme wako uje. Mapenzi yako yafanyike hapa duniani kama huko mbinguni. Utupatie leo riziki zetu za kila siku. Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tulivyokwisha kuwasamehe wadeni wetu. Usitutie majaribuni, bali utuokoe kutoka kwa yule mwovu [kwa kuwa Ufalme ni wako na nguvu na utukufu, hata milele. Amen].’
”Kisha Abrahamu akasema tena: “Sasa kwa kuwa nimekuwa na ujasiri wa kuzungumza na Bwana, ingawa mimi si kitu bali ni mavumbi na majivu;
”Kisha akaomba, “Ee BWANA, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, nipatie ushindi leo, uonyeshe huruma kwa bwana wangu Abrahamu. Tazama, nimesimama karibu na kisima hiki cha maji, nao binti za watu wa mji huu wanakuja kuteka maji. Basi na iwe hivi, nitakapomwambia binti mmojawapo, ‘Tafadhali tua mtungi wako nipate kunywa maji,’ naye akisema, ‘Kunywa, nitawanywesha na ngamia wako pia.’ Basi na awe ndiye uliyemchagua kwa ajili ya mtumishi wako Isaki. Kwa hili nitajua umemhurumia bwana wangu.” Ikawa kabla hajamaliza kuomba, Rebeka akatokea akiwa na mtungi begani mwake. Alikuwa binti wa Bethueli. Bethueli alikuwa mwana wa Milka aliyekuwa mke wa Nahori ndugu wa Abrahamu.
”Isaki akamwomba BWANA kwa ajili ya mke wake, kwa sababu alikuwa tasa. BWANA akajibu maombi yake na Rebeka mkewe akapata mimba.
”Kwa hiyo Yakobo akaachwa peke yake na mtu mmoja akashikana naye mweleka mpaka mapambazuko. Yule mtu alipoona kuwa hawezi kumshinda, aligusa kiungio cha nyonga ya Yakobo kwa hiyo nyonga yake ikateguka wakati alipokuwa akishikana mweleka na yule mtu. Ndipo yule mtu akasema, “Niache niende, kwa kuwa ni mapambazuko.” Lakini Yakobo akajibu, “Sitakuacha uende usiponibariki.” Yule mtu akamwuliza, “Jina lako nani?” Akajibu, “Yakobo.” Ndipo yule mtu akasema, “Jina lako halitakuwa tena Yakobo, bali Israeli, kwa sababu umeshindana na Mungu na watu pia, nawe umeshinda.” Yakobo akasema, “Tafadhali niambie jina lako.” Lakini akajibu, “Kwa nini kuniuliza Jina langu?” Ndipo akambariki huko. Kwa hiyo Yakobo akapaita mahali pale Penieli, akasema, “Ni kwa sababu nimemwona Mungu uso kwa uso na bado maisha yangu yameokoka.”
”Mose alikuwa huko pamoja na BWANA kwa siku arobaini mchana na usiku bila kula chakula wala kunywa maji. Naye akaandika juu ya vibao maneno ya Agano, yaani zile Amri Kumi.
”Lakini Mose na Aroni wakaanguka kufudifudi na kulia kwa sauti, wakasema, “Ee Mungu, Mungu wa roho za wanadamu wote, utakuwa na hasira na kusanyiko lote wakati ni mtu mmoja tu ametenda dhambi?”
”Lakini kama mtamtafuta BWANA Mungu wenu, mtampata; kama mtamtafuta kwa moyo wenu wote na kwa roho yote. Wakati mnapokuwa katika dhiki, nayo mambo haya yote yamewatokea siku hizo, ndipo mtamrudia BWANA Mungu wenu na kumtii. Kwa maana BWANA Mungu wenu ni Mungu mwenye huruma, hatawaacha au kuwaangamiza wala kusahau Agano alilofanya na baba zenu, alilowathibitishia kwa kiapo.
”Nilipopanda mlimani kupokea mbao za mawe, mbao za Agano lile BWANA alilofanya nanyi, nilikaa mlimani siku arobaini mchana na usiku, sikula mkate wala sikunywa maji.
”Ndipo tena nikasujudu mbele za BWANA kwa siku arobaini mchana na usiku. Sikula mkate wala sikunywa maji, kwa sababu ya dhambi yote mliyoifanya, mkifanya lile lililo ovu mbele za BWANA na kumkasirisha.
”Nilianguka kifudifudi mbele za BWANA kwa zile siku arobaini mchana na usiku kwa sababu BWANA alikuwa amesema angewaangamiza ninyi.
”Basi nilikaa mlimani kwa siku arobaini mchana na usiku, kama nilivyofanya mara ya kwanza, pia BWANA alinisikiliza hata wakati huu. Haikuwa nia yake kuwaangamiza.
”Ndipo Yoshua akararua mavazi yake, akapomoka kifudifudi mbele ya Sanduku la BWANA, akabakia hapo mpaka jioni. Wazee wa Israeli wakafanya vivyo hivyo, wakatia mavumbi vichwani mwao.
”Ndipo Waisraeli, watu wote, wakapanda Betheli, huko wakakaa mbele za BWANA wakilia. Wakafunga siku ile mpaka jioni na kutoa sadaka ya kutekezwa na sadaka ya amani kwa BWANA.
”BWANA akaja akasimama hapo, akiita kama mara zile nyingine, “Samweli! Samweli!” Kisha Samweli akasema, “Nena BWANA, kwa kuwa mtumishi wako anasikiliza.”
”Kwa habari yangu, iwe mbali nami kutenda dhambi dhidi ya BWANA kwa kushindwa kuwaombea. Mimi nitawafundisha njia iliyo njema na ya kunyooka.
”Kisha Solomoni akasimama mbele ya madhabahu ya BWANA machoni pa kusanyiko lote la Israeli, akakunjua mikono yake kuelekea mbinguni na kusema: “Ee BWANA, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe mbinguni juu wala duniani chini, wewe unayetunza Agano lako la upendo pamoja na watumishi wanaodumu katika njia yako kwa moyo wote.
”Wakati Solomoni alipomaliza dua hizi zote na maombi kwa BWANA, akainuka kutoka mbele ya madhabahu ya BWANA, mahali alipokuwa amepiga magoti, mikono yake ikawa imekunjuliwa kuelekea juu mbinguni.
”Wakati wa kutoa dhabihu ya jioni, nabii Eliya akasogea mbele na kuomba, akisema: “Ee BWANA, Mungu wa Abrahamu, na Isaki na Israeli, ijulikane leo kwamba wewe ndiye Mungu katika Israeli na ya kwamba mimi ni mtumishi wako na nimefanya mambo haya yote kwa neno lako. Unijibu mimi, Ee BWANA, nijibu mimi, ili watu hawa wajue kwamba wewe, Ee BWANA, ndiwe Mungu, na kwamba unaigeuza mioyo yao ikurudie tena.” Kisha moto wa BWANA ukashuka na kuiteketeza ile dhabihu, zile kuni, yale mawe, ule udongo, na pia kuramba yale maji yaliyokuwa ndani ya handaki. Wakati watu wote walipoona hili, wakaanguka kifudifudi na kulia, “BWANA: yeye ndiye Mungu! BWANA: yeye ndiye Mungu!”
”Tega sikio, Ee BWANA, usikie; fungua macho yako, Ee BWANA, uone; sikiliza maneno ambayo Senakeribu ametuma kumtukana Mungu aliye hai.
”Sasa basi, Ee BWANA Mungu wetu, tuokoe kutoka mkononi mwake, ili kwamba falme zote duniani zipate kujua kwamba wewe peke yako, Ee BWANA, ndiwe Mungu.”
”Hezekia akaelekeza uso wake ukutani akamwomba BWANA akisema, “Ee BWANA, kumbuka jinsi nilivyoenenda mbele zako kwa uaminifu na kujitoa kwa moyo wangu wote, na kufanya yaliyo mema machoni pako.” Hezekia akalia sana sana.
”Yabesi akamlilia Mungu wa Israeli akisema, “Ee Mungu, laiti ungenibariki kweli kweli na kuipanua mipaka yangu! Mkono wako na uwe pamoja nami, uniepushe na uovu ili nisidhurike!” Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.
”Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake, wajulisheni mataifa yale aliyoyatenda.
”Mtafuteni BWANA na nguvu zake, utafuteni uso wake siku zote.
”Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni Mwema, upendo wake wadumu milele.
”Pia ulikuwa wajibu wao kila asubuhi kumshukuru na kumsifu BWANA. Iliwapasa pia kufanya hivyo jioni
”Kisha Solomoni akasimama mbele ya madhabahu ya BWANA machoni pa kusanyiko lote la Israeli, naye akakunjua mikono yake. Basi alikuwa ametengeneza jukwaa la shaba, urefu wake dhiraa tano, na upana wake dhiraa tano na kimo chake dhiraa tatu, naye akaliweka katikati ya ukumbi wa nje. Akapanda juu ya hilo jukwaa kisha akapiga magoti mbele ya kushanyiko lote la Israeli, akanyosha mikono yake kwelekea mbinguni. Akasema: “Ee BWANA, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe mbinguni juu wala duniani chini, wewe unayetunza Agano lako la upendo na watumishi wanaodumu katika njia yako kwa moyo wote.
”Hata hivyo sikiliza dua ya mtumishi wako na maombi yake kwa huruma, Ee BWANA Mungu wangu. Sikia kilio na dua ambayo mtumishi wako anaomba mbele zako siku hii ya leo. Macho yako na yafumbuke kuelekea Hekalu hili usiku na mchana, mahali hapa ambapo ulisema, ‘Jina langu litakuwako humo,’ ili kwamba upate kusikia maombi ambayo mtumishi wako ataomba kuelekea mahali hapa. Usikie maombi ya mtumishi wako na ya watu wako Israeli wakati wanapoomba kuelekea mahali hapa. Sikia kutoka mbinguni, mahali pa makao yako na usikiapo, samehe.
”wakati dua au maombi yatakapofanywa na mmojawapo wa watu wako Israeli, kila mmoja akijua juu ya taabu ya moyo wake mwenyewe, akainyosha mikono yake kuelekea Hekalu hili, basi usikie kutoka mbinguni, katika makao yako. Usamehe na utende, umpe kila mtu kulingana na matendo yake, kwa kuwa unaujua moyo wake (kwa kuwa ni wewe peke yako ujuaye mioyo ya watu wote), ili wakuogope kwa wakati wote watakaoishi katika nchi uliyowapa baba zetu.
”“Sasa, Mungu wangu, macho yako na yafumbuke na masikio yako yasikie maombi yaombwayo mahali hapa.
”kama watu wangu, wanaoitwa kwa Jina langu, watajinyenyekesha na kuomba na kuutafuta uso wangu na kuacha njia zao mbaya, basi nitasikia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi yao na nitaiponya nchi yao. Sasa macho yangu yatafumbuka na masikio yangu yatasikiliza kwa makini maombi yaombwayo mahali hapa.
”Rehoboamu akatenda maovu kwa sababu hakuuelekeza moyo wake katika kumtafuta BWANA Mungu.
”Kisha Asa akamlilia BWANA Mungu wake na kusema, “Ee BWANA, hakuna ye yote aliye kama wewe wa kuwasadia wasio na nguvu dhidi ya wenye nguvu. Utusaidie, Ee BWANA, wewe ndiwe Mungu wetu, kwa kuwa tunakutumainia wewe, nasi kwa jina lako tumekuja dhidi ya jeshi hili kubwa. Ee BWANA, wewe ndiwe Mungu wetu, usiwaache wanadamu wakushinde wewe.”
”Wakafanya agano kumtafuta BWANA, Mungu wa baba zao kwa moyo wao wote na kwa roho yao yote.
”Ndipo makuhani na Walawi wakasimama wakawabariki watu, naye Mungu akawasikia, kwa sababu maombi yao yalifika mbinguni, makao yake matakatifu.
”Mfalme Hezekia na nabii Isaya mwana wa Amozi wakalilia mbingu katika maombi kuhusu jambo hili.
”Kando ya Mto Ahava, hapo nilitangaza kufunga, ili tujinyenyekeshe mbele za Mungu wetu na kumwomba kwa ajili ya kutujalia safari ya amani sisi na watoto wetu, pamoja na mali zetu zote. Niliona aibu kumwomba mfalme askari na wapanda farasi wa kutulinda njiani kutokana na adui zetu, kwa sababu tulikwisha kumwambia mfalme, “Mkono wa neema wa Mungu wetu uko juu ya kila mmoja anayemtafuta, lakini hasira yake kubwa ni dhidi ya wote wamwachao.” Kwa hiyo tulifunga na kumwomba Mungu wetu kuhusu jambo hili, naye akajibu maombi yetu.
”Ndipo wakati wa kutoa dhabihu ya jioni nikainuka kutoka katika kujidhili kwangu nikiwa na koti na joho langu lililoraruka, nikapiga magoti mikono yangu ikiwa imeinuliwa kwa BWANA Mungu wangu. Nami nikaomba: “Ee Mungu wangu, natahayari na kuona aibu kukuinulia uso wangu Mungu wangu, kwa sababu dhambi zetu zimejikusanya hata kupita juu ya vichwa vyetu na hatia yetu imefika mbinguni.
”Ndipo Ezra akaondoka hapo mbele ya nyumba ya Mungu akaenda kwenye chumba cha Yehohanani mwana wa Eliashibu. Wakati alipokuwa hapo, hakula chakula wala hakunywa maji, kwa sababu aliendelea kuomboleza kuhusu kukosa uaminifu kwa watu wa uhamishoni.
”Niliposikia mambo haya, niliketi na kulia. Kwa siku kadhaa niliomboleza na kufunga na kuomba mbele za Mungu wa mbinguni. Kisha nikasema: “Ee BWANA, Mungu wa mbinguni, mkuu na mwenye kuogofya, ambaye hulishika Agano lake la upendo na wale wampendao na kutii amri zake, masikio yako na yawe masikivu na macho yako yafunguke ili usikie maombi ya mtumishi wako anayoomba mbele yako mchana na usiku kwa ajili ya watumishi wako, watu wa Israeli. Ninaungama dhambi zetu sisi Waisraeli, pamoja na zangu na za nyumba ya baba yangu, tulizotenda dhidi yako.
”Ezra akamsifu BWANA, Mungu mkuu, nao watu wote wakainua mikono yao na kuitikia, “Amen! Amen!” Kisha wakasujudu na kumwabudu BWANA hali nyuso zao zikigusa ardhi.
”Katika siku ya ishirini na nne ya mwezi ule ule, Waisraeli walikusanyika pamoja, wakifunga na kuvaa nguo za gunia na kujipaka mavumbi vichwani mwao. Wale wa uzao wa Israeli walijitenga na wageni wote. Wakasimama mahali pao na kuungama dhambi zao na uovu wa baba zao.
”Katika kila jimbo ambapo amri na agizo la mfalme lilifika, kulikuwa na maombolezo makuu miongoni mwa Wayahudi pamoja na kufunga, kulia na kuomboleza. Watu wengi wakalala juu ya nguo za magunia na majivu.
”“Nenda, kusanya pamoja Wayahudi wote walioko Shushani, fungeni kwa ajili yangu. Msile wala kunywa kwa siku tatu, usiku na mchana. Mimi na wajakazi wangu tutafunga kama mnavyofanya. Baada ya kufanyika hili, nitakwenda kwa mfalme, hata ingawa ni kinyume cha sheria. Ikiwa ni kuangamia na niangamie.”
”Ndipo Ayubu akasimama, akararua joho lake na kunyoa nywele zake. Kisha akaanguka chini katika kuabudu
”“Lakini ingekuwa ni mimi, ningemlalamikia Mungu, ningeliweka shauri langu mbele zake. Yeye hutenda maajabu yasiyoweza kutambuliwa, miujiza isiyoweza kuhesabika.
”Lakini ukimtafuta Mungu, nawe ukamsihi Mwenyezi,
”“Hata sasa ukiutoa moyo wako kwake na kumwinulia mikono yako,
”Niite kwenye shauri nami nitajibu, au niache niseme, nawe upate kujibu.
”Utamwomba yeye, naye atakusikia, nawe utazitimiza nadhiri zako.
”Yeye hajibu wakati watu waliapo kwa sababu ya kiburi cha watu waovu. Naam, Mungu hasikilizi maombi yao ya ubatili, Mwenyezi hayazingatii.
”Baada ya Ayubu kuwaombea rafiki zake, BWANA akamwondoa kwenye uteka, akamfanikisha tena naye akampa mara mbili ya vile alivyokuwa navyo hapo kabla.
”Ninamlilia BWANA kwa sauti kuu, naye ananijibu kutoka katika mlima wake mtakatifu.
”(Kwa Mwimbishaji: Kwa Ala Za Nyuzi Za Muziki. Zaburi Ya Daudi) Unijibu nikuitapo, Ee Mungu wangu mwenye haki! Unipumzishe katika shida zangu, nirehemu, usikie ombi langu.
”(Kwa Mwimbishaji: Kwa Filimbi. Zaburi Ya Daudi) Ee BWANA, tegea sikio maneno yangu, uangalie kupiga kite kwangu. Sikiliza kilio changu ili unisaidie, Mfalme wangu na Mungu wangu, kwa maana kwako ninaomba. Asubuhi, unasikia sauti yangu, Ee BWANA; asubuhi naleta haja zangu mbele zako, na kusubiri kwa matumaini.
”Wote wanaolijua jina lako watakutumaini wewe, kwa maana wewe BWANA, hujawaacha kamwe wakutafutao.
”Katika kiburi chake mtu mwovu hamtafuti Mungu, katika mawazo yake yote hakuna nafasi ya Mungu.
”(Sala Ya Daudi) Sikia, Ee BWANA, kusihi kwangu kwa haki, sikiliza kilio changu. Tega sikio kwa ombi langu, halitoki kwenye midomo ya udanganyifu.
”Ee Mungu, ninakuita, kwa kuwa utanijibu, unitegee sikio lako na usikie ombi langu.
”Katika shida yangu nalimwita BWANA, nilimlilia Mungu wangu anisaidie. Kutoka hekaluni mwake alisikia sauti yangu, kilio changu kikafika mbele zake, masikioni mwake.
”niongoze katika kweli yako na kunifundisha, kwa maana wewe ni Mungu Mwokozi wangu, nalo tumaini langu liko kwako wakati wote.
”Jambo moja ninamwomba BWANA, hili ndilo ninalolitafuta: niweze kukaa nyumbani mwa BWANA siku zote za maisha yangu, niutazame uzuri wa BWANA na kumtafuta hekaluni mwake.
”Uisikie sauti yangu nikuitapo, Ee BWANA, unihurumie na unijibu. Moyo wangu unasema kuhusu wewe, “Utafute uso wake!” Uso wako, BWANA “Nitautafuta.”
”Umngojee BWANA, uwe hodari na mwenye moyo mkuu, nawe, umngojee BWANA.
”(Zaburi Ya Daudi) Ninakuita wewe, Ee BWANA, Mwamba wangu; usiwe kwangu kama kiziwi. Kwa sababu ukinyamaza nitafanana na hao waliokwisha shuka shimoni. Sikia kilio changu unihurumie ninapokuita kwa ajili ya msaada, niinuapo mikono yangu kuelekea Patakatifu pa Patakatifu pako.
”(Zaburi Ya Daudi) Ee BWANA, ninakukimbilia wewe, usiache nikaaibika kamwe, kwa haki yako uniokoe. Nitegee sikio lako, uje uniokoe haraka, uwe kwangu mwamba wa kimbilio, ngome imara ya kuniokoa.
”Nilimtafuta BWANA naye akanijibu, akaniokoa kwenye hofu zangu zote. Wale wamtazamao hutiwa nuru, nyuso zao hazifunikwi na aibu kamwe. Maskini huyu alimwita BWANA akamsikia, akamwokoa katika taabu zake zote. Malaika wa BWANA hufanya kituo akiwazunguka wale wamchao, naye huwaokoa. Onjeni mwone kwamba BWANA ni mwema, heri mtu yule anayemkimbilia.
”Macho ya BWANA yako kwa wenye haki na masikio yake yako makini kusikia kilio chao; uso wa BWANA uko kinyume na watenda mabaya, kufuta kumbukumbu lao duniani. Wenye haki hulia, naye BWANA huwasikia, huwaokoa katika taabu zao zote. BWANA yu karibu nao waliovunjika moyo na huwaokoa waliopondeka roho.
”Nami nitakushukuru mbele ya kusanyiko kubwa, nitakusifu katikati ya watu wengi.
”Tulia mbele za BWANA na umngojee kwa uvumilivu; usisumbuke watu wanapofanikiwa katika njia zao, wanapotekeleza mipango yao miovu.
”“Ee BWANA, usikie maombi yangu, usikie kilio changu unisaidie, usiwe kiziwi kwa kulia kwangu. Kwani mimi ninaishi na wewe kama mgeni, kama walivyokuwa baba zangu wote,
”(Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Daudi) Nilimngoja BWANA kwa saburi, naye akaniinamia akasikia kilio changu.
”Ee BWANA Mungu wangu, umefanya mambo mengi ya ajabu. Mambo uliyopanga kwa ajili yetu hakuna awezaye kukuhesabia; kama ningesema na kuyaelezea, yangekuwa mengi mno kuyaelezea.
”Bali wote wakutafutao washangilie na kukufurahia, wale wapendao wokovu wako siku zote waseme, “BWANA atukuzwe!” Lakini bado mimi ni maskini na mhitaji; Bwana na anifikirie. Wewe ni msaada wangu na Mwokozi wangu; Ee Mungu wangu, usikawie.
”Mchana BWANA huelekeza upendo wake, usiku wimbo wake uko nami: maombi kwa Mungu wa uzima wangu.
”“Tulieni, mjue ya kwamba mimi ndimi Mungu; nitatukuzwa katikati ya mataifa, nitatukuzwa katika dunia.” BWANA Mwenye Nguvu Zote yu pamoja nasi; Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.
”Toa sadaka za shukrani kwa Mungu, timiza nadhiri zako kwake Yeye Aliye Juu Sana, na uniite siku ya taabu; nami nitakuokoa, nawe utanitukuza.”
”Hakika wewe wapendezwa na kweli itokayo moyoni, ndani sana ya moyo wangu wanifundisha hekima.
”(Kwa Mwimbishaji: Na Ala Za Uimbaji. Utenzi Wa Daudi) Ee Mungu, sikiliza maombi yangu, wala usidharau hoja yangu,
”Lakini ninamwita Mungu, naye BWANA huniokoa. Jioni, asubuhi na adhuhuri ninalia kwa huzuni, naye husikia sauti yangu.
”Mtwike BWANA fadhaa zako, naye atakutegemeza, hatamwacha kamwe mwenye haki wake aanguke.
”Ee nguvu yangu, ninakutazama wewe, wewe, Ee Mungu, ndiwe ngome yangu, Mungu wangu unipendaye. Mungu atanitangulia, naye atanifanya niwatazame kwa furaha wale wanaonisingizia.
”(Kwa Mwimbishaji: Kwa Ala Za Nyuzi Za Uimbaji. Zaburi Ya Daudi) Ee Mungu, sikia kilio changu, usikilize maombi yangu. Kutoka miisho ya dunia ninakuita, ninaita huku moyo wangu unadhoofika; uniongoze kwenye mwamba ule ulio juu kuliko mimi.
”(Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Yeduthuni. Zaburi Ya Daudi) Kwa Mungu peke yake nafsi yangu inapata pumziko; wokovu wangu watoka kwake. Yeye peke yake ndiye mwamba wangu na wokovu wangu; yeye ni ngome yangu, sitatikisika kamwe.
”Ee nafsi yangu, upumzike, kwa Mungu peke yake, tumaini langu latoka kwake. Yeye peke yake ndiye mwamba wangu na wokovu wangu; ndiye ngome yangu, sitatikisika. Wokovu wangu na heshima yangu viko kwa Mungu, ndiye mwamba wangu wenye nguvu na kimbilio langu. Enyi watu, mtumainini yeye, wakati wote, mmiminieni yeye mioyo yenu, kwa kuwa Mungu ni kimbilio letu.
”(Zaburi Ya Daudi Wakati Alipokuwa Katika Jangwa La Yuda) Ee Mungu, wewe ni Mungu wangu, nakutafuta kwa moyo wote; nafsi yangu inakuonea kiu, mwili wangu unakuonea wewe shauku, katika nchi kame na iliyochoka mahali ambapo hapana maji.
”Nilimlilia kwa kinywa changu, sifa zake zilikuwa katika ulimi wangu. Kama ningekuwa nimeyaficha maovu moyoni mwangu, Bwana asingekuwa amenisikiliza; lakini hakika Mungu amenisikiliza na amesikia sauti yangu katika maombi. Sifa apewe Mungu, ambaye hakulikataa ombi langu wala kunizuilia upendo wake!
”Nimechoka kwa kuomba msaada, koo langu limekauka. Macho yangu yanafifia, nikimtafuta Mungu wangu.
”Maskini wataona na kufurahi, ninyi mnaomtafuta Mungu, mioyo yenu na iishi!
”(Kwa Mwimbishaji: Kwa Ala Za Uimbaji Za Nyuzi. Zaburi Ya Asafu. Wimbo) Ee Mungu, tunakushukuru, tunakushukuru wewe, kwa kuwa jina lako li karibu; watu husimulia matendo yako ya ajabu.
”(Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Yeduthuni. Zaburi Ya Asafu) Nilimlilia Mungu ili anisaidie, nilimlilia Mungu ili anisikie. Nilipokuwa katika taabu, nilimtafuta Bwana, usiku nilinyosha mikono bila kuchoka na nafsi yangu ilikataa kufarijiwa.
”Nitasikiliza lile atakalosema Mungu aliye BWANA; anaahidi amani kwa watu wake, watakatifu wake, lakini nao wasirudie upumbavu.
”Ee BWANA, sikia maombi yangu, sikiliza kilio changu unihurumie. Katika siku ya shida yangu nitakuita, kwa maana wewe utanijibu.
”Ee BWANA, Mungu uniokoaye, nimelia mbele zako usiku na mchana. Maombi yangu na yafike mbele zako, utegee kilio changu sikio lako.
”Lakini ninakulilia wewe, Ee BWANA unisaidie, asubuhi maombi yangu huja mbele zako.
”Tufundishe kuzihesabu siku zetu vizuri, ili tujipatie moyo wa hekima.
”Yeye akaaye mahali pa salama pake Yeye Aliye Juu Sana, atadumu katika uvuli wake Mwenyezi.
”Ataniita, nami nitamjibu; nitakuwa pamoja naye katika taabu, nitamwokoa na kumheshimu.
”(Zaburi: Wimbo Wa Sabato) Ni vyema kumshukuru BWANA na kuliimbia jina lako, Ee Uliye Juu Sana, kuutangaza upendo wako asubuhi, uaminifu wako wakati wa usiku,
”Njoni, tusujudu tumwabudu, tupige magoti mbele za BWANA Muumba wetu, kwa maana yeye ndiye Mungu wetu na sisi ni watu wa malisho yake, kondoo chini ya utunzaji wake. Kama mkiisikia sauti yake, leo, msiifanye migumu mioyo yenu kama mlivyofanya kule Meriba, kama mlivyofanya siku ile kule Masa jangwani,
”(Maombi Ya Mtu Aliyechoka, Anayeteseka, Anayemimina Malalamiko Kwa BWANA) Ee BWANA, usikie maombi yangu, kilio changu cha kuomba msaada kikufikie. Usinifiche uso wako ninapokuwa katika shida. Unitegee sikio lako, ninapoita, unijibu kwa upesi.
”Ataitikia maombi ya mtu mkiwa, wala hatadharau hoja yao.
”Utukufu kwa jina lake takatifu, mioyo ya wale wamtafutao BWANA na ifurahi. Mtafuteni BWANA na nguvu zake, utafuteni uso wake siku zote.
”Magoti yangu yamelegea kwa kufunga, mwili wangu umedhoofika na kukonda.
”Sifa Kwa Mungu Ninampenda BWANA kwa maana amesikia sauti yangu; amesikia kilio changu ili anihurumie. Kwa sababu amenitegea sikio lake, nitamwita siku zote za maisha yangu. Kamba za mauti zilinizunguka, maumivu makuu ya kuzimu yalinipata, nikalemewa na taabu na huzuni. Ndipo nikaliitia jina la BWANA: “Ee BWANA, niokoe!”
”Nitakutolea dhabihu ya kukushukuru na kuliita jina la BWANA.
”Wakati wa maumivu yangu makuu nilimlilia BWANA, naye akanijibu kwa kuniweka huru.
”Nitakushukuru, kwa kuwa ulinijibu, umekuwa wakovu wangu.
”Heri wale wanaozishika shuhuda zake, wamtafutao kwa moyo wao wote.
”Ninakutafuta kwa moyo wangu wote, usiniache niende mbali na amri zako.
”Ee BWANA, ninakuita kwa moyo wangu wote, nami nitayatii maagizo yako. Ninakuita; niokoe nami nitazishika sheria zako. Ninaamka asubuhi na mapema na kukuomba msaada; nimeweka tumaini langu katika neno lako. Sikufumba macho yangu usiku kucha, ili niweze kutafakari juu ya ahadi zako. Usikie sauti yangu sawasawa na upendo wako. Ee BWANA, uyahifadhi maisha yangu, sawasawa na sheria zako.
”(Wimbo Wa Kwenda Juu) Kutoka katika vilindi ninakulilia, Ee BWANA, Ee BWANA, sikia sauti yangu. Masikio yako na yawe masikivu kwa kilio changu unihurumie.
”Namngojea BWANA, nafsi yangu inangojea, katika neno lake naweka tumaini langu. Nafsi yangu inamngojea Bwana kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi, naam, kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi.
”Mshukuruni BWANA, kwa kuwa ni mwema. Fadhili zake zadumu milele.
”Mshukuruni Mungu wa miungu. Fadhili zake zadumu milele.
”Mshukuruni Bwana wa mabwana: Fadhili zake zadumu milele.
”(Zaburi Ya Daudi) Ee BWANA, ninakuita wewe, uje kwangu hima. Sikia sauti yangu ninapokuita. Maombi yangu na yafike mbele zako kama uvumba; kuinua mikono yangu juu na kuwe kama dhabihu ya jioni.
”(Utenzi Wa Daudi Alipokuwa Pangoni. Maombi) Namlilia BWANA kwa sauti kubwa, nainua sauti yangu kwa BWANA anihurumie. Namimina malalamiko yangu mbele zake, mbele zake naeleza shida zangu.
”(Zaburi Ya Daudi) Ee BWANA, sikia sala yangu, sikiliza kilio changu unihurumie; katika uaminifu na haki yako njoo unisaidie.
”Macho yao wote yanakutazama wewe, nawe huwapa chakula chao wakati wake. Waufumbua mkono wako, watosheleza haja ya kila kitu kilicho hai. BWANA ni mwenye haki katika njia zake zote na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya. BWANA yu karibu na wote wamwitao, karibu na wote wamwitao kwa uaminifu. Huwatimizia wamchao matakwa yao, husikia kilio chao na kuwaokoa.
”“Ndipo watakaponiita lakini sitawajibu, watanitafuta lakini hawatanipata. Kwa kuwa walichukia maarifa, wala hawakuchagua kumcha BWANA, kwa kuwa hawakukubali mashauri yangu, na kukataa maonyo yangu,
”Nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.
”Kama mtu ye yote akikataa kusikia sheria, hata maombi yake ni chukizo.
”Usiwe mwepesi kuzungumza, usiwe na haraka katika moyo wako kuzungumza lo lote mbele za Mungu. Mungu yuko mbinguni nawe uko duniani, kwa hiyo maneno yako na yawe machache.
”Sikukuu zenu za Miandamo ya Mwezi na sikukuu zenu zilizoamriwa moyo wangu unazichukia. Zimekuwa mzigo kwangu, nimechoka kuzivumilia. Mnaponyosha mikono yenu katika kuomba, nitaficha macho yangu nisiwaone; hata mkiomba maombi mengi sitasikiliza. Mikono yenu imejaa damu; jiosheni na mkajitakase. Yaondoeni matendo yenu maovu mbele zangu! Acheni kutenda mabaya,
”Nitamngojea BWANA, ambaye ameificha nyumba ya Yakobo uso wake. Nitaliweka tumaini langu kwake.
”Nafsi yangu yakutamani wakati wa usiku, wakati wa asubuhi roho yangu yakuonea shauku. Wakati hukumu zako zinapokuja juu ya dunia, watu wa ulimwengu hujifunza haki.
”Enyi watu wa Sayuni, mnaoishi Yerusalemu, hamtalia tena. Tazama jinsi atakavyokuwa na huruma mtakapolia kwa kumwomba msaada! Mara asikiapo, atawajibu.
”bali wale wamtumainio BWANA atafanya upya nguvu zao. Watapaa juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio wala hawatachoka, watatembea kwa miguu wala hawatazimia.
”Mtafuteni BWANA maadamu anapatikana; mwiteni maadamu yu karibu.
”hawa nitawaleta kwenye mlima wangu mtakatifu na kuwapa furaha ndani ya nyumba yangu ya sala. Sadaka zao za kuteketeza na dhabihu zao zitakubalika juu ya madhabahu yangu, kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote.”
”Je, hii ndiyo aina ya mfungo niliouchagua, siku moja tu kwa ajili ya mtu kujinyenyekeza? Je, ni kwa kuinamisha kichwa chini kama unyasi Na kwa kujilaza juu ya nguo ya gunia na majivu? Je, huo ndio mnaouita mfungo, siku iliyokubalika kwa BWANA? “Je, hii si ndiyo aina ya mfungo niliyoichagua: kufungua minyororo ya udhalimu na kufungua kamba za nira, kuwaweka huru walioonewa na kuvunja kila nira?
”Lakini maovu yenu yamewatenga ninyi na Mungu wenu, dhambi zenu zimewaficha ninyi uso wake, ili asisikie.
”“Nilijifunua kwa watu wale ambao hawakuniulizia, nimeonekana kwa watu wale ambao hawakunitafuta. Kwa taifa lile ambalo halikuliita Jina langu, nilisema, ‘Niko hapa, niko hapa.’
”Kabla hawajaita nitajibu, nao wakiwa katika kunena nitasikia.
”Kwa hivyo, hili ndilo asemalo BWANA: ‘Nitaleta juu yao maafa ambayo hawawezi kuyakimbia. Hata kama wakinililia mimi sitawasikiliza. Miji ya Yuda na watu wa Yerusalemu watakwenda kuililia miungu ambayo wameifukizia uvumba, lakini haitawasaidia kamwe wakati maafa yatakapowapiga.
”Kwa maana ninajua mipango niliyo nayo kwa ajili yenu,” asema BWANA, “ni mipango ya kuwafanikisha na wala si ya kuwadhuru, ni mipango ya kuwapa tumaini katika siku zijazo. Kisha mtaniita na mtakuja na kuniomba, nami nitawasikiliza. Mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote. Nitaonekana kwenu,” asema BWANA, “nami nitawarudisha watu wenu waliotekwa. Nitawakusanya kutoka katika mataifa yote na mahali pote nilipokuwa nimewafukuzia, nami nitawarudisha mahali ambapo nilikuwa nimewatoa ili wachukuliwe uhamishoni,” asema BWANA.
”‘Niite nami nitakuitika na kukuambia mambo makuu na yasiyochunguzika usiyoyajua.’
”Basi wewe nenda katika nyumba ya BWANA siku ya kufunga na uwasomee watu maneno ya BWANA kutoka katika kitabu hiki yale uliyoyaandika kutoka kinywani mwangu. Wasomee watu wote wa Yuda waliofika kutoka kwenye miji yao. Labda wataomba na kusihi mbele za BWANA na kila mmoja atageuka kutoka katika njia zake mbaya, kwa sababu hasira na ghadhabu zilizotamkwa dhidi ya watu hawa na BWANA ni kubwa.”
”“Katika siku hizo, wakati huo,” asema BWANA, “watu wa Israeli pamoja na watu wa Yuda wataenda wakilia ili kumtafuta BWANA Mungu wao. Wataiuliza njia iendayo Sayuni na kuelekeza nyuso zao huko. Watakuja na kuambatana na BWANA katika Agano la milele ambalo halitasahaulika.
”BWANA ni mwema kwa wale ambao tumaini lao ni kwake, kwa yule ambaye humtafuta; ni vyema kungojea kwa utulivu kwa ajili ya wokovu wa BWANA.
”Na tuinue mioyo yetu pamoja na mikono yetu kwa Mungu mbinguni, na tuseme:
”Akaniambia, “Unaliona hili, mwanadamu? Utaona vitu ambavyo ni machukizo kuliko hili.” Ndipo akanileta mpaka kwenye ukumbi wa ndani wa nyumba ya BWANA, nako huko katika ingilio la Hekalu, kati ya baraza na madhabahu, walikuwapo wanaume wapatao ishirini na watano. Wakiwa wamelipa kisogo Hekalu la BWANA na kuelekeza nyuso zao upande wa mashariki, wakilisujudia jua huko mashariki. Akaniambia, “Je, umeona hili mwanadamu? Je, ni jambo dogo sana kwa nyumba ya Yuda kufanya machukizo wanayoyafanya hapa? Je, ni lazima pia waijaze nchi dhuluma na kuendelea siku zote kunikasirisha? Watazame wanavyonibania pua kana kwamba ninanuka! Kwa hiyo nitashughulika nao kwa hasira, sitawaonea huruma wala kuwaachilia. Wajapopiga makelele masikioni mwangu, sitawasikiliza.”
”Yeye hubadili nyakati na majira, huwaweka wafalme na kuwaondoa. Huwapa hekima wenye hekima na maarifa wenye ufahamu. Hufunua siri na mambo yaliyofichika, anajua yale yaliyo gizani, nuru hukaa kwake. Ninakushukuru na kukuhimidi, Ee Mungu wa baba zangu: Umenipa hekima na uwezo, umenijulisha kile tulichokuomba, umetujulisha kujua ndoto ya mfalme.”
”Wasimamizi wa kifalme, wasaidizi, wakuu, washauri na watawala wote wamekubaliana kwamba mfalme atoe sheria na kukazia amri kuwa ye yote atakayemwomba Mungu ye yote au mwanadamu katika muda huu wa siku thelathini zijazo, isipokuwa kwako wewe, Ee mfalme, atatupwa ndani ya tundu la simba. Sasa, Ee mfalme, toa amri na uiandike ili kwamba isiweze kubadilishwa, kwa kulingana na sheria za Wamedi na Waajemi, ambazo haziwezi kubatilishwa.” Hivyo Mfalme Dario akaiweka amri hiyo katika maandishi.
”Ikawa Danieli alipofahamu kuwa amri ile imetangazwa, alikwenda nyumbani kwenye chumba chake cha ghorofani ambako madirisha yalifunguka kuelekea Yerusalemu. Mara tatu kwa siku akapiga magoti na kuomba, akimshukuru Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya mwanzoni. Ndipo watu hawa wakamwendea kama kikundi na kumkuta Danieli anaomba na kumsihi Mungu kwa ajili ya msaada. Basi wakaenda kwa mfalme na kusema naye kuhusu amri ya kifalme: “Je, hukutangaza amri kwamba kwa muda huu wa siku thelathini zijazo mtu ye yote ambaye atamwomba mungu au mwanadamu ye yote isipokuwa wewe, Ee mfalme, angetupwa ndani ya tundu la simba?” Mfalme akajibu, “Amri ndivyo ilivyo, kulingana na sheria za Wamedi na Waajemi, ambazo haziwezi kutanguka.” Ndipo wakamwambia mfalme, “Danieli, ambaye ni mmoja wa watu wa uhamisho kutoka Yuda hakuheshimu, Ee mfalme, wala hajali amri uliyoiweka kwa maandishi. Angalia anaomba mara tatu kwa siku.”
”Kwa hiyo nikamgeukia BWANA Mungu na kumsihi katika maombi na dua, katika kufunga, kuvaa nguo ya gunia na kujipaka majivu. Nikamwomba BWANA Mungu wangu na kutubu: “Ee Bwana, Mungu mkuu na unayetisha, anayeshika Agano lake la upendo kwao wanaompenda na kutii maagizo yake, tumetenda dhambi na kufanya mabaya. Tumekuwa waovu na tumeasi, tumegeuka mbali na maagizo yako na sheria zako.
”“Basi Mungu wetu, sasa sikia maombi na dua ya mtumishi wako. Ee Bwana, kwa ajili yako tuangalie kwa huruma kuhusu ukiwa wa mahali pako patakatifu. Ee Mungu, tega sikio na ukasikie, fumbua macho yako ukaone ukiwa wa mji ule wenye Jina lako. Hatukutolei maombi yetu kwa sababu sisi tuna haki, bali kwa sababu ya rehema zako nyingi. Ee Bwana, sikiliza! Ee Bwana, samehe! Ee Bwana, sikia na ukatende! Kwa ajili yako, Ee Mungu wangu, usikawie, kwa sababu mji wako na watu wako wanaitwa kwa Jina lako.”
”Basi, nilipokuwa bado nikinena na kuomba, nikiungama dhambi yangu na dhambi ya watu wangu Israeli na nikifanya maombi yangu kwa BWANA Mungu wangu kwa ajili ya mlima wake mtakatifu, wakati nilipokuwa bado katika maombi, Gabrieli, yule mtu niliyekuwa nimemwona katika maono hapo awali, alinijia kwa kasi karibia na wakati wa kutoa dhabihu ya jioni. Akanielimisha na kuniambia, “Danieli, sasa nimekuja kukupa akili na ufahamu. Mara ulipoanza kuomba, jibu lilitolewa, ambalo nimekuja kukupasha habari, kwa maana wewe unapendwa sana. Kwa hiyo, tafakari ujumbe huu na uelewe maono haya:
”Wakati huo, mimi Danieli, nikaomboleza kwa majuma matatu. Sikula chakula kizuri, nyama wala divai havikugusa midomo yangu, nami sikujipaka mafuta kamwe mpaka majuma matatu yalipotimia.
”Mkono ulinigusa, ukaninyanyua, nikapiga magoti na vitanga vyangu vikiwa vimeshika chini, huku nikiwa ningali bado ninatetemeka. Akasema, “Danieli, wewe mtu upendwaye sana, fikiri kwa makini maneno ninayokwenda kunena nawe sasa, simama wima, kwa maana sasa nimetumwa kwako.” Naye aliposema nami haya, nikasimama nikitetemeka. Ndipo akaendelea kusema, “Danieli usiogope. Tangu siku ya kwanza ulipotia moyo wako ili kupata ufahamu na kujinyenyekeza mbele ya Mungu wako, maneno yako yalisikiwa, nami nimekuja kwa ajili ya kuitikia maneno yako. Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinizuia kwa siku ishirini na moja. Ndipo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu, alikuja kunisaidia, kwa sababu nilikuwa nimezuiliwa huko na mfalme wa Uajemi. Sasa nimekuja kukueleza mambo yatakayowatokea watu wako wakati ujao, kwa maana maono hayo yanahusu wakati ambao haujaja bado.” Wakati alipokuwa akinieleza haya, nilisujudu uso wangu ukiwa umeelekea chini nikawa bubu.
”Kisha nitarudi mahali pangu mpaka watakapokubali kosa lao. Nao watautafuta uso wangu; katika taabu yao watanitafuta kwa bidii.”
”Tangazeni saumu takatifu; liiteni kusanyiko takatifu. Iteni wazee na wote waishio katika nchi waende katika nyumba ya BWANA Mungu wenu, wakamlilie BWANA.
”“Hata sasa,” asema BWANA, “nirudieni kwa mioyo yenu yote, kwa kufunga, kwa kulia na kuomboleza.” Rarueni mioyo yenu na siyo mavazi yenu. Mrudieni BWANA, Mungu wenu, kwa maana yeye ndiye mwenye neema na mwingi wa huruma, si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa upendo, huona huruma, hujizuia kuleta maafa.
”Akiwa ndani ya tumbo la nyangumi, Yona alimwomba BWANA Mungu wake. Akasema: “Katika shida yangu nalimwita BWANA, naye akanijibu. Kutoka kina cha kaburi niliomba msaada, nawe ukasikiliza kilio changu.
”“Wakati uhai wangu ulipokuwa unatoka, nilikukumbuka wewe, BWANA, nayo maombi yangu yalikufikia wewe, katika Hekalu lako takatifu.
”Watu wa Ninawi wakamwamini Mungu, wakatangaza kufunga, watu wote kuanzia mkubwa sana hadi yule mdogo kabisa, wakavaa nguo za gunia. Habari zilipomfikia mfalme wa Ninawi, aliondoka kwenye kiti chake cha enzi, akavua majoho yake ya kifalme, akajifunika nguo ya gunia kisha akaketi chini mavumbini. Ndipo akatoa tangazo katika Ninawi yote: “Kwa amri ya mfalme na wakuu wake: “Msiruhusu mtu ye yote au mnyama, makundi ya ng'ombe au wanyama wengine wafugwao, kuonja kitu cho chote, msiwaruhusu kula wala kunywa. Bali wanadamu na wanyama wafunikwe kwa nguo za gunia. Kila mmoja afanye hima kumwomba Mungu. Waziache njia zao mbaya na udhalimu ulio mikononi mwao. Ni nani ajuaye? Huenda Mungu akaghairi kwa huruma yake akaacha hasira yake kali ili tusiangamie.” Mungu alipoona walivyofanya na jinsi walivyogeuka kutoka katika njia zao mbaya, akawa na huruma wala hakuleta maangamizi juu yao kama alivyokuwa ameonya.
”Kisha watamlilia BWANA, lakini hatawajibu. Wakati huo atawaficha uso wake kwa sababu ya uovu waliotenda.
”Lakini mimi, namtazama BWANA kwa matumaini, namngoja Mungu Mwokozi wangu; Mungu wangu atanisikia mimi.
”Mtafuteni BWANA, enyi nyote wanyenyekevu wa nchi, ninyi ambao hufanya lile analoamuru. Tafuteni haki, tafuteni unyenyekevu; labda mtahifadhiwa siku ya hasira ya BWANA.
”“Waulize watu wote wa nchi na makuhani, ‘Je, mlipofunga na kuomboleza katika mwezi wa tano na wa saba kwa miaka sabini iliyopita, mlifunga kweli kwa ajili yangu?
”na wenyeji wa mji mmoja watakwenda kwenye mji mwingine na kusema, ‘Twende mara moja na tukamsihi BWANA, na kumtafuta BWANA Mwenye Nguvu Zote. Mimi mwenyewe ninakwenda.’ Pia watu wa kabila nyingi na mataifa yenye nguvu yatakuja Yerusalemu kumtafuta BWANA Mwenye Nguvu Zote na kumsihi.”
”Hii theluthi moja nitaileta katika moto; nitawasafisha kama fedha isafishwavyo na kuwajaribu kama dhahabu. Wataliitia Jina langu nami nitawajibu; nitasema, ‘Hawa ni watu wangu,’ nao watasema, ‘BWANA ni Mungu wetu.’ ”
”Baada ya kufunga siku arobaini mchana na usiku, hatimaye akaona njaa.
”Lakini mimi ninawaambia: Wapendeni adui zenu na waombeeni wanaowatesa ninyi,
”“Nanyi msalipo, msiwe kama wanafiki, maana wao hupenda kusali wakiwa wamesimama katika masinagogi na kando ya barabara ili waonekane na watu. Amin, amin nawaambieni, wao wamekwisha kupata thawabu yao. Lakini wewe unaposali, ingia chumbani mwako, funga mlango na umwombe Baba yako aliye sirini. Naye Baba yako aonaye sirini atakupa thawabu yako. Nanyi mnaposali msiseme maneno kama wafanyavyo watu wasiomjua Mungu. Kwa maana wao hudhani kwamba watasikiwa kwa sababu ya wingi wa maneno yao. Msiwe kama wao, kwa sababu Baba yenu anajua kile mnachohitaji kabla hamjamwomba.
”“Hivi basi, ndivyo iwapasavyo kuomba: “ ‘Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe. Ufalme wako uje. Mapenzi yako yafanyike hapa duniani kama huko mbinguni. Utupatie leo riziki zetu za kila siku. Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tulivyokwisha kuwasamehe wadeni wetu. Usitutie majaribuni, bali utuokoe kutoka kwa yule mwovu [kwa kuwa Ufalme ni wako na nguvu na utukufu, hata milele. Amen].’
”“Mnapofunga, msiwe wenye huzuni kama wafanyavyo wanafiki. Maana wao hukunja nyuso zao ili kuwaonyesha wengine kwamba wamefunga. Amin, amin nawaambia wao wamekwisha kupata thawabu yao kamilifu. Lakini mnapofunga, jipakeni mafuta kichwani na kunawa nyuso zenu ili kufunga kwenu kusionekane na watu wengine ila Baba yenu aketiye mahali pa siri, naye Baba yenu aonaye sirini atawapa thawabu yenu kwa wazi.
”Kwa hiyo msiwe na wasiwasi, mkisema, ‘Tutakula nini?’ Au ‘Tutakunywa nini?’ Au ‘Tutavaa nini?’ Kwa maana watu wasiomjua Mungu ndio wanaoshindania hayo, lakini Baba yenu wa mbinguni anafahamu kwamba mnahitaji hayo yote. Lakini utafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake na haya yote mtaongezewa.
”“Ombeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtapata, bisheni nanyi mtafunguliwa mlango. Kwa maana kila aombaye hupewa, naye atafutaye huona, naye abishaye hufunguliwa mlango. “Au ni nani miongoni mwenu ambaye mwanawe akimwomba mkate atampa jiwe? Au mwanawe akimwomba samaki atampa nyoka? Ikiwa ninyi basi mlio waovu mnajua jinsi ya kuwapa watoto wenu vitu vizuri, si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa vitu vizuri wale wamwombao?
”Wanafunzi wa Yohana Mbatizaji wakaja na kumwuliza Yesu, “Imekuwaje kwamba sisi na Mafarisayo tunafunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?” Yesu akawajibu, “Je, wageni wa bwana arusi waweza kuomboleza wakati angali pamoja nao? Wakati utafika ambapo bwana arusi ataondolewa kwao, hapo ndipo watakapofunga.
”Wakati huo Yesu alisema, “Ninakuhimidi Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa umewaficha mambo haya wenye hekima na wenye elimu, nawe ukawafunulia watoto wachanga.
”Baada ya kuwaaga, akaenda zake mlimani peke yake kuomba. Jioni ilipofika, Yesu alikuwa huko peke yake.
”“Tena nawaambia, ikiwa wawili wenu watakubaliana duniani kuhusu jambo lo lote watakaloomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. Kwa kuwa wanapokusanyika pamoja watu wawili au watatu kwa Jina langu, mimi niko papo hapo pamoja nao.”
”Yesu akawajibu, “Amin, amin nawaambia, kama mkiwa na imani wala msiwe na shaka, si kwamba mtaweza kufanya tu yale yaliyofanyika kwa huu mtini, bali hata mkiuambia huu mlima, ‘Ng'oka, ukatupwe baharini,’ nalo litafanyika. Lo lote mtakaloomba katika kusali, mkiamini, mtapokea.”
”Kisha akachukua kikombe, akashukuru, akawapa akisema, “Nyweni nyote katika kikombe hiki.
”Kisha Yesu akaenda pamoja na wanafunzi wake mpaka kwenye bustani iitwayo Gethsemane, akawaambia, “Kaeni hapa wakati ninakwenda kule kuomba.” Akamchukua Petro pamoja na wale wana wawili wa Zebedayo, naye akaanza kuhuzunika na kufadhaika. Kisha Yesu akawaambia, “Moyo wangu umejawa na huzuni kiasi cha kufa. Kaeni hapa na mkeshe pamoja nami.” Akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi akaomba, akisema, “Baba yangu, kama inawezekana, kikombe hiki na kiniepuke, lakini si kama nitakavyo mimi bali kama utakavyo wewe.” Kisha akarudi kwa wanafunzi wake na kuwakuta wamelala. Akamwuliza Petro, “Je, ninyi wanaume, hamkuweza kukesha pamoja nami kwa saa moja? Kesheni na muombe, msije mkaanguka majaribuni. Hakika roho iko radhi lakini mwili ni dhaifu.” Akaenda tena mara ya pili na kuomba, “Baba yangu, kama haiwezekani kikombe hiki kiniepuke nisikinywe, basi mapenzi yako yafanyike.”
”Wakati huo huo pazia la Hekalu likachanika vipande viwili, kuanzia juu hadi chini. Dunia ikatetemeka na miamba ikapasuka.
”Mapema sana alfajiri kulipokuwa bado kungali giza, Yesu akaamka, akaondoka, akaenda mahali pa faragha, ili kuomba.
”Basi wanafunzi wa Yohana pamoja na Mafarisayo walikuwa wakifunga. Baadhi ya watu wakamjia Yesu na kumwuliza, “Mbona wanafunzi wa Yohana na wa Mafarisayo hufunga lakini wanafunzi wako hawafungi?” Yesu akawajibu, “Wageni wa bwana arusi wawezaje kufunga wakati bwana arusi akiwa pamoja nao? Maadamu bwana arusi yuko pamoja nao, hawawezi kufunga. Lakini wakati utakuja ambapo bwana arusi ataondolewa kwao, siku hiyo ndipo watakapofunga.
”Baada ya kuwaaga wale watu, akaenda mlimani kuomba.
”Yesu akamwambia, “Kama ukiweza kuamini, yote yawezekana kwake yeye aaminiye.” Mara baba yake yule mvulana akapiga kelele akisema, “Ninaamini. Nisaidie kutokuamini kwangu!”
”Yesu akawajibu, “Hali hii haiwezi kutoka isipokuwa kwa kuomba na kufunga.”
”Amin, amin nawaambia, mtu ye yote atakayeuambia mlima huu, ‘Ng'oka ukatupwe baharini,’ wala asione shaka moyoni mwake, bali aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake. Kwa sababu hiyo nawaambia, yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mmeyapokea nayo yatakuwa yenu.
”Nanyi kila msimamapo kusali, sameheni, mkiwa na neno na mtu ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. Lakini kama ninyi msiposamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.”
”Wakaenda mahali paitwapo Gethsemane, Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kaeni hapa wakati ninakwenda kule kuomba.” Kisha akawachukua pamoja naye Petro, Yakobo na Yohana. Naye akaanza kuhuzunika sana na kutaabika. Akawaambia, “Moyo wangu umejawa na huzuni kiasi cha kufa. Kaeni hapa na mkeshe.” Akaenda mbele kidogo, akajitupa chini kifudifudi akaomba akisema, kama ikiwezekana saa hiyo ya mateso imwepuke. Akasema, “Abba, Baba, mambo yote yawezekana kwako. Niondolee kikombe hiki, lakini si kama nitakavyo mimi, bali mapenzi yako yatimizwe.” Akarudi kwa wanafunzi wake akawakuta wamelala, naye akamwambia Petro, “Simoni, umelala? Je, hukuweza kukesha hata kwa saa moja? Kesheni na kuomba msije mkaingia majaribuni. Roho iko radhi lakini mwili ni dhaifu.”
”Pazia la Hekalu likachanika vipande viwili kuanzia juu hadi chini.
”Kwa maana kwa Mungu hakuna lisilowezekana.”
”Hivyo alikuwa mjane na umri wake ulikuwa miaka themanini na minne. Yeye hakuondoka humo Hekaluni usiku wala mchana bali alikuwa akimwabudu Mungu, akifunga na kuomba. Wakati uo huo, Ana alikuja akaanza kusifu akimshukuru Mungu na kusema habari za huyo mtoto kwa watu wote waliokuwa wakitarajia ukombozi wa Yerusalemu.
”Baada ya watu wote kubatizwa, Yesu naye akabatizwa. Naye alipokuwa akiomba, mbingu zilifunguka.
”mahali ambako kwa siku arobaini alikuwa akijaribiwa na ibilisi. Kwa siku zote hizo hakula cho chote, hivyo baada ya muda huo akaona njaa.
”Lakini mara kwa mara Yesu alijitenga nao ili kwenda mahali pa faragha kuomba.
”Wakamwambia Yesu, “Wanafunzi wa Yohana na wa Mafarisayo mara kwa mara hufunga na kuomba, lakini wanafunzi wako wanaendelea kula na kunywa.” Yesu akawajibu, “Je, mnaweza kuwafanya wageni wa bwana arusi kufunga wakati akiwa pamoja nao? Lakini wakati utafika ambapo bwana arusi ataondolewa kwao, ndipo watakapofunga.”
”Ikawa katika siku hizo Yesu alikwenda mlimani kuomba, akakesha usiku kucha akimwomba Mungu.
”“Lakini nawaambia wale wanaonisikia, wapendeni adui zenu. Watendeeni mema wanaowachukia. Wabarikini wale wanaowalaani, waombeeni wale wanaowatendea mabaya.
”Yapata siku nane baada ya Yesu kusema hayo, aliwachukua Petro, Yakobo na Yohana akaenda nao mlimani kuomba. Alipokuwa akiomba, mwonekano wa sura yake ukabadilika, mavazi yake yakametameta kama mwanga wa umeme wa radi.
”Siku moja, Yesu alikuwa mahali fulani akiomba. Alipomaliza kuomba, mmoja wa wanafunzi wake akamwambia, “Bwana, tufundishe kuomba, kama vile Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake.” Akawaambia, “Mnapoomba, semeni hivi: “ ‘Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje. Utupatie kila siku riziki zetu. Utusamehe dhambi zetu, kwa kuwa na sisi huwasamehe wote wanaotukosea. Wala usitutie majaribuni, bali utuokoe kutoka kwa yule mwovu.’ ”
”Kisha akawaambia, “Ni nani miongoni mwenu mwenye rafiki yake, naye akamwendea usiku wa manane na kumwambia, ‘Rafiki, nikopeshe mikate mitatu. Kwa sababu rafiki yangu amekuja kutoka safarini, nami sina kitu cha kumpa.’ “Kisha yule aliyeko ndani amjibu, ‘Usinisumbue. Mlango umefungwa, nami na watoto wangu tumelala. Siwezi kuamka nikupe cho chote.’ Nawaambia, ingawa huyo mtu hataamka na kumpa hiyo mikate kwa sababu ni rafiki yake, lakini kwa sababu ya kuendelea kwake kuomba, ataamka na kumpa kiasi anachohitaji.
”“Kwa hiyo nawaambia: Ombeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtapata, bisheni, nanyi mtafunguliwa mlango. Kwa kuwa kila aombaye hupewa, naye kila atafutaye hupata na kila abishaye hufunguliwa mlango. “Je, kuna ye yote miongoni mwenu, ambaye mtoto wake akimwomba samaki, atampa nyoka badala ya samaki? Au mtoto akimwomba yai atampa nge? Basi ikiwa ninyi mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, si zaidi sana Baba yenu wa mbinguni atawapa Roho Mtakatifu wale wamwombao!”
”kama watumishi wanaomngojea bwana wao arudi kutoka kwenye karamu ya arusi, ili ajapo na kugonga mlango waweze kumfungulia mara. Heri wale watumishi ambao bwana wao atakapokuja atawakuta wakiwa wanakesha. Amin, nawaambia, atajifunga mkanda wake na kuwaketisha ili wale, naye atakuja na kuwahudumia.
”Kisha Yesu akawapa wanafunzi wake mfano ili kuwaonyesha kuwa yawapasa kuomba pasipo kukata tamaa. Akawaambia, “Katika mji mmoja alikuwapo hakimu ambaye hakumwogopa Mungu wala kumjali mtu. Katika mji huo alikuwako mjane mmoja ambaye alikuwa akija kwake mara kwa mara akimwomba, ‘Tafadhali nipatie haki kati yangu na adui yangu.’ “Kwa muda mrefu yule hakimu alikataa. Lakini hatimaye akasema moyoni mwake, ‘Japokuwa simwogopi Mungu wala simjali mwanadamu, lakini kwa kuwa huyu mjane ananisumbuasumbua, nitahakikisha amepata haki yake ili asiendelee kunichosha kwa kunijia mara kwa mara!’ ” Bwana akasema, “Sikilizeni asemavyo huyu hakimu dhalimu. Je, Mungu hatawatendea haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku? Je, atakawia kuwasaidia? Ninawaambia, atawapatia haki upesi. Lakini je, Mwana wa Adamu atakapokuja ataikuta imani duniani?”
”“Watu wawili walikwenda Hekaluni kusali, mmoja wao alikuwa Farisayo na mwingine alikuwa mtoza ushuru. Yule Farisayo, akiwa amesimama peke yake, akasali hivi: ‘Mungu, ninakushukuru kwa sababu mimi si kama watu wengine: Wanyang'anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru. Mimi nafunga mara mbili kwa juma, natoa sehemu ya kumi ya mapato yangu.’ “Lakini yule mtoza ushuru akasimama mbali, hakuthubutu hata kuinua uso wake kutazama mbinguni, bali alijipiga piga kifuani na kusema: ‘Mungu, nihurumie, mimi mwenye dhambi.’ “Nawaambia, huyu mtoza ushuru alirudi nyumbani akiwa amehesabiwa haki mbele za Mungu zaidi ya yule Farisayo. Kwa maana ye yote ajikwezaye atashushwa na ye yote ajishushaye atakwezwa.”
”Kesheni daima na mwombe ili mweze kuokoka na yale yote yatakayotokea na kusimama mbele ya Mwana wa Adamu.”
”Lakini nimekuombea wewe Simoni ili imani yako isishindwe, nawe ukiisha kunirudia, uwaimarishe ndugu zako.”
”Walipofika huko, akawaambia wanafunzi wake, “Ombeni msije mkaangukia majaribuni.” Akajitenga nao, kama umbali wa kutupa jiwe, akapiga magoti, akaomba, akisema, “Baba, kama ni mapenzi yako, niondolee kikombe hiki, lakini si kama mimi nipendavyo, bali mapenzi yako yatendeke.” Malaika kutoka mbinguni akamtokea, akamtia nguvu. Naye akiwa katika maumivu makuu, akaomba kwa bidii, nalo jasho lake likawa kama matone ya damu yakidondoka ardhini. Baada ya kuomba, akawarudia wanafunzi wake akawakuta wamelala, wakiwa wamechoka kutokana na huzuni. Naye akawauliza, “Mbona mmelala? Amkeni mwombe ili msiangukie majaribuni.”
”Yesu akasema, “Baba, wasamehe, kwa maana hawajui walitendalo!” Wakagawana nguo zake kwa kupiga kura.
”kwa sababu jua liliacha kutoa nuru. Pazia la Hekalu likachanika vipande viwili.
”Ndipo Yesu akachukua ile mikate, akamshukuru Mungu na kuwagawia wale watu waliokuwa wamekaa kwa kiasi walichohitaji. Akafanya vivyo hivyo na wale samaki. Kila mtu akapata kadiri alivyotaka.
”Yeye atokaye kwa Mungu husikia kile Mungu asemacho. Sababu ya ninyi kutosikia ni kwa kuwa hamtokani na Mungu.”
”Tunajua ya kuwa Mungu hawasikilizi wenye dhambi, lakini huwasikiliza wote wanaomcha na kumtii.
”Mlinzi humfungulia lango na kondoo huisikia sauti yake. Huwaita kondoo wake kwa majina yao na kuwatoa nje ya zizi. Akiisha kuwatoa wote nje, hutangulia mbele yao na kondoo humfuata kwa kuwa wanaijua sauti yake.
”Ninao kondoo wengine ambao si wa zizi hili, inanipasa kuwaleta, nao wataisikia sauti yangu, hivyo patakuwa na kundi moja na mchungaji mmoja.
”Kondoo wangu huisikia sauti yangu nami nawajua, nao hunifuata,
”Kwa hiyo wakaliondoa lile jiwe kutoka penye kaburi. Yesu akainua macho yake juu akasema, “Baba, ninakushukuru kwa kuwa wanisikia. Ninajua ya kuwa wewe hunisikia siku zote, lakini nimesema haya kwa ajili ya umati huu uliosimama hapa, ili wapate kuamini ya kuwa wewe umenituma.” Baada ya kusema haya, Yesu akapaza sauti yake akaita, “Lazaro, njoo huku!”
”Nanyi mkiomba lo lote kwa Jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba apate kutukuzwa katika Mwana. Kama mkiniomba lo lote kwa Jina langu nitalifanya. “Kama mnanipenda, mtazishika amri zangu. Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine akae nanyi milele. Huyo ndiye Roho wa kweli ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa sababu haumwoni wala haumjui. Ninyi mnamjua kwa kuwa yuko pamoja nanyi naye anakaa ndani yenu.
”Lakini huyo Msaidizi, yaani, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwenu kwa Jina langu, atawafundisha mambo yote na kuwakumbusha yote niliyowaambia.
”Ninyi mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni lo lote mtakalo, nanyi mtatendewa.
”Si ninyi mlionichagua, bali mimi ndiye niliyewachagua ninyi na kuwaweka mwende mkazae matunda na matunda yenu yapate kudumu, ili lo lote mtakalomwomba Baba katika Jina langu, awape.
”Atakapokuja huyo Roho wa kweli atawaongoza awatie katika kweli yote. Yeye hatanena kwa ajili yake mwenyewe, bali atanena yale yote atakayosikia, naye atawaonyesha mambo yajayo.
”Katika siku hiyo hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin nawaambia, kama mkimwomba Baba jambo lo lote kwa Jina langu, yeye atawapa. Mpaka sasa hamjaomba jambo lo lote kwa Jina langu. Ombeni nanyi mtapewa, ili furaha yenu ipate kuwa kamili.
”Baada ya Yesu kusema haya, alitazama kuelekea mbinguni akawaombea na kusema: “Baba, saa imewadia. Umtukuze Mwanao, ili Mwanao apate kukutukuza wewe. Kwa kuwa umempa mamlaka juu ya wote wenye mwili ili awape uzima wa milele wale uliompa. Nao uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe uliye Mungu wa pekee, wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma. Nimekutukuza wewe duniani kwa kuitimiza ile kazi uliyonipa niifanye. Hivyo sasa, Baba, unitukuze mbele zako kwa ule utukufu niliokuwa nao pamoja na wewe kabla ulimwengu haujakuwako. “Nimewajulisha jina lako wale ulionipa kutoka katika ulimwengu. Walikuwa wako, ukanipa mimi, nao wamelitii neno lako. Sasa wamejua ya kuwa vyote ulivyonipa vimetoka kwako, kwa kuwa maneno yale ulionipa nimewapa wao, nao wameyapokea na kujua kwamba kweli nimetoka kwako, nao wameamini kuwa wewe ulinituma. Ninawaombea wao. Mimi siuombei ulimwengu, bali nawaombea wale ulionipa kwa sababu wao ni wako. Wote walio wangu ni wako na walio wako ni wangu, nami nimetukuzwa ndani yao. Mimi sasa simo tena ulimwenguni, lakini wao bado wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba Mtakatifu, uwalinde kwa uweza wa jina lako ulilonipa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo wamoja. Nilipokuwa pamoja nao, niliwalinda, wakawa salama kwa lile jina ulilonipa. Hakuna hata mmoja aliyepotea, isipokuwa yule aliyekusudiwa, ili Maandiko yapate kutimia. “Lakini sasa naja kwako, nami ninasema mambo haya wakati bado nikiwa ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu kamili ndani yao. Nimewapa neno lako, nao ulimwengu umewachukia kwa kuwa wao si wa ulimwengu kama mimi nisivyo wa ulimwengu huu. Siombi kwamba uwaondoe ulimwenguni, bali uwalinde dhidi ya yule mwovu. Wao si wa ulimwengu huu, kama vile mimi nisivyo wa ulimwengu. Uwatakase kwa ile kweli, neno lako ndilo kweli. Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami nawatuma vivyo hivyo. Kwa ajili yao najiweka wakfu ili wao nao wapate kutakaswa katika ile kweli. “Siwaombei hawa peke yao, bali nawaombea na wale wote watakaoniamini kupitia neno lao ili wawe na umoja kama vile wewe Baba ulivyo ndani yangu na mimi nilivyo ndani yako, wao nao wawe ndani yetu, ili ulimwengu upate kuamini ya kuwa wewe ndiye uliyenituma mimi. Utukufu ule ulionipa nimewapa wao, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo wamoja. Mimi ndani yako na wewe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja na ulimwengu upate kujua ya kuwa umenituma, nami nimewapenda wao kama unavyonipenda mimi. “Baba, shauku yangu ni kwamba, wale ulionipa wawe pamoja nami pale nilipo, ili waweze kuuona utukufu wangu, yaani, utukufu ule ulionipa kwa kuwa ulinipenda hata kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. “Baba Mwenye Haki, ingawa ulimwengu haukujui, mimi ninakujua, nao wanajua ya kuwa umenituma. Nimefanya jina lako lijulikane kwao nami nitaendelea kufanya lijulikane, ili kwamba upendo ule unaonipenda mimi uwe ndani yao na mimi mwenyewe nipate kuwa ndani yao.”
”Hawa wote waliungana pamoja katika maombi. Pamoja nao walikuwapo wanawake kadha wa kadha na Maria mama yake Yesu pamoja na ndugu zake Yesu.
”Ilipowadia siku ya Pentekoste, walikuwa wote mahali pamoja. Ghafula sauti kama mvumo mkubwa wa upepo uliotoka mbinguni, ukaijaza nyumba yote walimokuwa wameketi. Zikatokea ndimi kama za moto zilizogawanyika na kukaa juu ya kila mmoja wao. Wote wakajazwa na Roho Mtakatifu, wakaanza kunena kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia.
”Watu hao waliposikia hayo, wakainua sauti zao wakamwomba Mungu kwa pamoja, wakisema, “Bwana Mwenyezi, uliyeumba mbingu na nchi na bahari, na vitu vyote vilivyomo.
”Walipokwisha kuomba, mahali pale walipokuwa wamekutanika pakatikiswa, nao wote wakajazwa na Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri.
”Nao walipofika wakawaombea ili wampokee Roho Mtakatifu,
”Kornelio akajibu, “Siku nne zilizopita, nilikuwa nyumbani nikisali saa kama hii, saa tisa alasiri. Ghafula mtu mwenye nguo za kumetameta akasimama mbele yangu, akasema, ‘Kornelio, maombi yako yamesikiwa na sadaka zako zimekumbukwa mbele za Mungu.
”Kwa hiyo Petro akawekwa gerezani, lakini kanisa lilikuwa likimwombea kwa Mungu kwa bidii. Usiku ule kabla ya siku ambayo Herode Agripa alikuwa amekusudia kumtoa na kumfanyia mashtaka, Petro alikuwa amelala kati ya askari wawili, akiwa amefungwa kwa minyororo miwili. Nao walinzi wa zamu walikuwa wakilinda penye lango la gereza. Ghafula malaika wa Bwana akatokea na nuru ikamulika mle ndani ya gereza. Yule malaika akampiga Petro ubavuni na kumwamsha, akisema, “Ondoka upesi!” Mara ile minyororo ikaanguka kutoka mikononi mwa Petro.
”Ndipo baada ya kufunga na kuomba, wakawawekea mikono yao.
”Nao baada ya kuwateua wazee katika kila kanisa, kwa kufunga na kuomba wakawakabidhi kwa Bwana waliyemwamini.
”Ilipokaribia usiku wa manane, Paulo na Sila walikuwa wakiomba na kuimba nyimbo za kumsifu Mungu, nao wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. Ghafula pakatokea tetemeko kubwa la ardhi, hata msingi wa gereza ukatikisika. Mara milango ya gereza ikafunguka na ile minyororo iliyowafunga kila mmoja ikafunguka.
”Paulo alipoweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akawashukia, nao wakanena kwa lugha mpya na kutabiri.
”Paulo alipomaliza kusema haya akapiga magoti pamoja nao wote akaomba.
”Sasa basi, mbona unakawia? Inuka, ukabatizwe na dhambi zako zikasafishwe, ukiliita Jina lake.’
”Baada ya kusema maneno haya, Paulo akachukua mkate, akamshukuru Mungu mbele yao wote, akaumega akaanza kula.
”Vivyo hivyo, Roho hutusaidia katika udhaifu wetu, kwa sababu hatujui kuomba ipasavyo. Lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa uchungu kusikoweza kutamkwa. Naye Mungu aichunguzaye mioyo, anaijua nia ya Roho, kwa sababu Roho huwaombea watakatifu sawasawa na mapenzi ya Mungu.
”Ndugu zangu, shauku ya moyo wangu na maombi yangu kwa Mungu ni kwa ajili ya Waisraeli, kwamba waokolewe.
”Iweni na furaha katika tumaini, katika dhiki iweni na saburi, dumuni katika maombi.
”Yeye anayehesabu siku moja kuwa takatifu kuliko nyingine, hufanya hivyo kwa kumheshimu Bwana. Naye alaye nyama hula kwa Bwana, kwa maana humshukuru Mungu, naye akataaye kula nyama hufanya hivyo kwa Bwana na humshukuru Mungu.
”Basi, ndugu zangu, nawasihi kwa Jina la Bwana wetu Yesu Kristo na kwa upendo wa Roho Mtakatifu, kujiunga nami katika taabu zangu mkiniombea kwa Mungu.
”Kwa maana mtu ye yote anayesema kwa lugha, hasemi na wanadamu bali anasema na Mungu. Kwa kuwa hakuna mtu ye yote anayemwelewa, kwani anasema mambo ya siri kwa Roho.
”Anenaye kwa lugha hujijenga mwenyewe, bali atoaye unabii hulijenga kanisa.
”Kwa sababu hii, yeye anenaye kwa lugha na aombe kwamba apate kutafsiri kile anachonena. Kwa maana nikiomba kwa lugha, roho yangu inaomba, lakini akili yangu haina matunda. Nifanyeje basi? Nitaomba kwa roho, lakini nitaomba kwa akili yangu pia. Nitaimba kwa roho na nitaimba kwa akili yangu pia. Ikiwa unabariki kwa roho, mtu mwingine atakayejikuta miongoni mwa hao wasiojua, atawezaje kusema “Amen” katika kushukuru kwako, wakati haelewi unachosema? Mnaweza kuwa mnatoa shukrani kweli, sawa, lakini huyo mtu mwingine hajengeki. Namshukuru Mungu kwamba mimi nanena kwa lugha kuliko ninyi nyote. Lakini ndani ya kanisa ni afadhali niseme maneno matano ya kueleweka kwa akili ili niwafundishe wengine kuliko kusema maneno 10,000 kwa lugha.
”Basi kunena kwa lugha mpya ni ishara, si kwa watu waaminio, bali kwa ajili ya wasioamini, wakati unabii si kwa ajili ya wasioamini, bali kwa ajili ya waaminio. Kwa hiyo kama kanisa lote likikutana na kila mmoja akanena kwa lugha, kisha wakaingia wageni wasioamini, je, hawatasema kwamba wote mna wazimu? Lakini kama mtu asiyeamini au asiyeelewa akiingia wakati kila mtu anatoa unabii, ataaminishwa na watu wote kuwa yeye ni mwenye dhambi na kuhukumiwa na wote, nazo siri za moyo wake zitawekwa wazi. Kwa hiyo ataanguka chini na kumwabudu Mungu akikiri, “Kweli Mungu yuko katikati yenu!”
”Kama mtu ye yote akinena kwa lugha, basi waseme watu wawili au watatu si zaidi, mmoja baada ya mwingine na lazima awepo mtu wa kutafsiri. Lakini kama hakuna mtu ye yote wa kutafsiri, hao watu na wanyamaze kimya kanisani na wanene na nafsi zao wenyewe na Mungu.
”Kwa hiyo ndugu zangu, takeni sana kutoa unabii na msikataze watu kusema kwa lugha.
”sijaacha kumshukuru Mungu kwa ajili yenu, nikiwakumbuka katika maombi yangu. Nazidi kumwomba Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awajalieni ninyi roho ya hekima na ya ufunuo, ili mpate kumjua zaidi.
”Kwa maana kwa kupitia kwake, sisi sote tunaweza kumkaribia Baba katika Roho mmoja.
”Basi kwa yeye awezaye kutenda mambo ya ajabu yasiyopimika kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya uweza wake ule utendao kazi ndani yetu, yeye atukuzwe katika kanisa na katika Kristo Yesu kwa vizazi vyote, milele na milele. Amen.
”Msemezane ninyi kwa ninyi kwa zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, mkimwimbia na kumsifu Bwana mioyoni mwenu, siku zote mkimshukuru Mungu Baba kwa kila jambo katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo.
”Mkiomba kwa Roho siku zote katika sala zote na maombi, mkikesha kila wakati mkiwaombea watakatifu wote.
”Ninamshukuru Mungu wangu kila niwakumbukapo ninyi. Katika maombi yangu yote daima nimekuwa nikiwaombea ninyi nyote kwa furaha,
”Haya ndiyo maombi yangu kwamba upendo wenu uongezeke zaidi na zaidi katika maarifa na ufahamu wote, ili mpate kutambua yale yaliyo mema, mkawe safi, wasio na hatia hadi siku ya Kristo, mkiwa mmejawa na matunda ya haki yapatikanayo kwa njia ya Yesu Kristo, kwa utukufu na sifa za Mungu.
”Msijisumbue kwa jambo lo lote, bali katika kila jambo kwa kuomba na kusihi pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Nayo amani ya Mungu, inayopita fahamu zote, itawalinda mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.
”Naweza kuyafanya mambo yote katika yeye anitiaye nguvu. Lakini, mlifanya vyema kushiriki nami katika taabu zangu.
”Naye Mungu wangu atawajaza ninyi kila mnachohitaji kwa kadiri ya utajiri wake katika utukufu ndani ya Kristo Yesu.
”Siku zote tunamshukuru Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, tunapowaombea ninyi,
”Kwa sababu hii, tangu siku ile tuliposikia habari zenu, hatukukoma kuomba kwa ajili yenu na kumsihi Mungu awajaze ninyi maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote ya kiroho na ufahamu.
”Dumuni sana katika maombi, mkikesha katika hayo pamoja na kushukuru. Pia tuombeeni na sisi ili Mungu atufungulie mlango wa kunena, ili tupate kuitangaza siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake pia mimi nimefungwa.
”Epafra, ambaye ni mmoja wenu na mtumishi wa Kristo Yesu, anawasalimu. Yeye siku zote anawaombea kwa bidii kwamba msimame imara katika mapenzi yote ya Mungu mkiwa wakamilifu na thabiti.
”Siku zote tunamshukuru Mungu kwa ajili yenu ninyi nyote, tukiwataja kwenye maombi yetu daima.
”Furahini siku zote; ombeni pasipo kukoma; shukuruni kwa kila jambo, kwa maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu kwa ajili yenu katika Kristo Yesu.
”Ndugu, tuombeeni.
”Hatimaye, ndugu, tuombeeni ili kwamba Neno la Bwana lipate kuenea kwa haraka na kuheshimiwa kila mahali, kama vile ilivyokuwa kwa upande wenu.
”Awali ya yote, nasihi, kwanza kabisa, naagiza kwamba dua, sala, maombezi na shukrani zifanyike kwa ajili ya watu wote: kwa ajili ya wafalme na wale wote wenye mamlaka, ili tupate kuishi kwa amani na utulivu, katika uchaji wote wa Mungu na utakatifu.
”Nataka kila mahali wanaume wasali wakiinua mikono mitakatifu pasipo hasira wala kugombana.
”Kwa maana kila kitu alichokiumba Mungu ni chema, wala hakuna kitu cho chote cha kukataliwa kama kikipokewa kwa shukrani, kwa sababu kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.
”Mwanamke ambaye ni mjane kweli kweli, yaani, yeye aliyebaki peke yake huweka tumaini lake kwa Mungu naye hudumu katika maombi usiku na mchana akimwomba Mungu ili amsaidie.
”Ninamshukuru Mungu, ninayemtumikia kwa dhamiri safi, kama walivyofanya baba zangu, ninapokukumbuka usiku na mchana katika maombi yangu.
”Siku zote ninamshukuru Mungu ninapokukumbuka katika maombi yangu,
”Zamani Mungu alisema na baba zetu kwa njia ya manabii mara nyingi na kwa njia mbalimbali, lakini katika siku hizi za mwisho anasema nasi kwa njia ya Mwanawe, ambaye amemweka kuwa mrithi wa vitu vyote, na ambaye kwa yeye aliuumba ulimwengu.
”Kama ilivyonenwa: “Leo, kama mtaisikia sauti yake, msifanye mioyo yenu migumu kama mlivyofanya wakati wa kuasi.”
”kwa hiyo Mungu ameweka siku nyingine, akaiita Leo, akisema kwa kinywa cha Daudi baadaye sana, kwa maneno yaliyotangulia kunenwa: “Leo, kama mkiisikia sauti yake, msifanye migumu mioyo yenu.”
”Basi na tukikaribie kiti cha rehema kwa ujasiri, ili tupewe rehema na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.
”Katika siku za maisha ya Yesu hapa duniani, alimtolea maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, yeye awezaye kumwokoa na mauti, naye Mungu akamsikia kwa sababu ya kutii kwake kwa unyenyekevu. Ingawa alikuwa Mwana, alijifunza utii kutokana na mateso aliyoyapata,
”Kwa hiyo, ndugu zangu, kwa kuwa tunao ujasiri wa kupaingia Patakatifu pa Patakatifu kwa damu ya Yesu,
”Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, kwa maana ye yote anayemjia Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko na ya kuwa huwapa thawabu wale wamtafutao kwa bidii.
”Basi kwa njia ya Yesu, tuzidi kumtolea Mungu dhabihu ya sifa, yaani, matunda ya midomo inayolikiri Jina lake.
”Kama mtu ye yote miongoni mwenu amepungukiwa na hekima na amwombe Mungu, yeye awapaye watu wote kwa ukarimu wala hana kinyongo, naye atapewa. Lakini anapoomba, lazima aamini wala asiwe na shaka, kwa sababu mtu aliye na shaka ni kama wimbi la bahari, lililochukuliwa na upepo na kutupwa huku na huku.
”Mnapoomba hampati kwa sababu mnaomba kwa nia mbaya, ili mpate kuvitumia hivyo mtakavyopata kwa tamaa zenu.
”Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, ninyi wenye dhambi na kuisafisha mioyo yenu, ninyi wenye nia mbili. Huzunikeni, ombolezeni na kulia. Kicheko chenu na kigeuzwe kuwa kuomboleza na furaha yenu kuwa huzuni. Jinyenyekezeni mbele za Bwana, naye atawainua.
”Je, mtu ye yote miongoni mwenu amepatwa na taabu? Basi inampasa aombe. Je, kuna ye yote mwenye furaha? Basi na aimbe nyimbo za kusifu. Je, kuna ye yote miongoni mwenu aliye mgonjwa? Basi inampasa awaite wazee wa kanisa wamwombee na kumpaka mafuta kwa Jina la Bwana. Kule kuomba kwa imani kutamwokoa huyo mgonjwa, naye Bwana atamwinua na kama ametenda dhambi, atasamehewa. Kwa hiyo ungamianeni makosa yenu ninyi kwa ninyi na kuombeana ili mpate kuponywa. Maombi ya mwenye haki yana nguvu tena yanafaa sana. Eliya alikuwa mwanadamu kama sisi. Akaomba kwa bidii kwamba mvua isinyeshe nayo haikunyesha juu ya nchi kwa muda wa miaka mitatu na miezi sita. Kisha akaomba tena, mbingu zikatoa mvua nayo ardhi ikatoa mazao yake.
”Kwa maana macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, na masikio yake husikiliza maombi yao, bali uso wa Bwana ni dhidi yao watendao maovu.”
”Mwisho wa mambo yote umekaribia. Kwa hiyo iweni na akili pia mwe na kiasi mkikesha katika kuomba.
”Mtwikeni yeye fadhaa zenu zote kwa maana hujishughulisha sana na mambo yenu.
”Kama tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki, atatusamehe dhambi zetu na kutusafisha toka kwenye udhalimu wote.
”lo lote tuombalo, twalipokea kutoka kwake, kwa sababu tumezitii amri zake na kutenda yale yanayompendeza.
”Huu ndio ujasiri tulionao tunapomkaribia Mungu, kwamba kama tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Nasi kama tunajua ya kuwa atusikia, lo lote tuombalo, tunajua ya kwamba tumekwisha kupata zile haja tulizomwomba.
”Mpenzi, naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako kama vile roho yako ifanikiwavyo.
”Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho anayaambia makanisa.
”Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho anayaambia makanisa.
”Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho anayaambia makanisa.
”Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho anayaambia makanisa.”
”