17 – Dini za uwongo
Haya ni maneno matakatifu ya Mungu Mwenyezi.
Hatupendi maneno ya wanadamu.
Kwa mtu yeyote anayempenda Mungu... hivi ndivyo Mungu anasema kuhusu: Dini za uwongo.
Haya ni maneno matakatifu ya Mungu Mwenyezi.
Hatupendi maneno ya wanadamu.
Kwa mtu yeyote anayempenda Mungu... hivi ndivyo Mungu anasema kuhusu: Dini za uwongo.
Lakini sanamu zao ni za fedha na dhahabu, zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu. Zina vinywa, lakini haziwezi kusema, zina macho, lakini haziwezi kuona; zina masikio, lakini haziwezi kusikia, zina pua, lakini haziwezi kunusa; zina mikono, lakini haziwezi kupapasa, zina miguu, lakini haziwezi kutembea; wala koo zao haziwezi kutoa sauti. Wale wanaozitengeneza watafanana nazo, vivyo hivyo wale wote wanaozitumainia.
”Usiwe na miungu mingine ila mimi. Usijifanyie sanamu ya kuchonga katika umbo la kitu cho chote kilicho juu mbinguni, au duniani chini, au ndani ya maji. Usivisujudie au kuviabudu; kwa kuwa Mimi, BWANA Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, ninayewaadhibu watoto kwa ajili ya dhambi ya baba zao hadi kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
”“ ‘Mwanaume au mwanamke ambaye ni mchawi, mwaguzi au mwenye kupunga pepo miongoni mwenu lazima auawe. Mtawapiga kwa mawe; nayo damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao wenyewe.’ ”
”Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa porini ambao BWANA Mungu aliwafanya. Nyoka akamwambia mwanamke, “Ati kweli Mungu alisema, ‘Kamwe msile matunda ya mti wo wote wa bustanini’?”
”Ndipo wakasema, “Njoni, tujijengee mji wenye mnara ambao utafika hadi mbinguni, ili tujipatie jina tusije tukatawanyika usoni pa dunia yote.” Lakini BWANA akashuka ili auone mji na mnara wanadamu waliokuwa wanaujenga. BWANA akasema, “Kama taifa moja wanaozungumza lugha moja wameanza kufanya hili, basi hakuna lo lote watakalopanga kufanya ambalo halitawezekana kwao. Njoni, tushuke tuvuruge lugha yao ili wasielewane wao kwa wao.” Hivyo BWANA akawatawanya kutoka mahali pale kwenda katika dunia yote, nao wakaacha kuujenga huo mji. Ndiyo maana pakaitwa Babeli, kwa sababu hapo ndipo BWANA alipoivuruga lugha ya dunia nzima. Kutoka hapo BWANA akawatawanya katika uso wa dunia yote.
”Pia malaika wa BWANA akamwambia: “Wewe sasa una mimba nawe utamzaa mwana. Utamwita jina lake Ishmaeli, kwa sababu BWANA amesikia juu ya huzuni yako. Atakuwa punda-mwitu katikati ya wanadamu, mkono wake utakuwa dhidi ya kila mtu na mkono wa kila mtu dhidi yake, naye ataishi kwa uhasama na ndugu zake wote.”
”Abrahamu akamwambia Mungu, “Laiti Ishmaeli naye angeshiriki baraka yako!” Ndipo Mungu akasema, “Ndiyo, lakini mkeo Sara atakuzalia wewe mwana, nawe utamwita jina lake Isaki. Nitalithibitisha Agano langu naye kama Agano la milele kwa ajili yake na wazao wake baada yake. Kwa upande wa Ishmaeli, nimekusikia: hakika nitambariki, nitamfanya awe na uzao mwingi na nitaongeza sana idadi yake. Atakuwa baba wa watawala kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kubwa. Lakini Agano langu nitalithibitisha kwa Isaki, ambaye Sara atakuzalia mwaka ujao majira kama haya.”
”Siku ile ile, Abrahamu akamchukua Ishmaeli mwanawe na wote waliozaliwa nyumbani mwake pamoja na walionunuliwa kwa fedha zake, kila mwanaume wa nyumbani mwake, akawatahiri, kama Mungu alivyomwagiza.
”Ndipo Mose na Aroni wakaenda kwa Farao wakafanya sawasawa kama vile BWANA alivyoagiza. Aroni akaitupa ile fimbo yake chini mbele ya Farao na maafisa wake, nayo ikawa nyoka. Farao naye akawaita watu wenye maarifa na wachawi na waganga wa Kimisri, nao wakafanya vivyo hivyo kwa siri ya uganga wao. Kila mmoja alitupa fimbo yake chini, nayo ikawa nyoka. Lakini fimbo ya Aroni ikazimeza zile fimbo zao. Hata hivyo moyo wa Farao ukawa mgumu, naye hakuwasikiliza Mose na Aroni, sawasawa kama vile BWANA alivyokuwa amesema.
”Lakini waganga wa Misri kwa kutumia siri ya uganga wao wakafanya vivyo hivyo, nao moyo wa Farao ukawa mgumu, hakuwasikiliza Mose na Aroni, kama vile BWANA alivyokuwa amesema.
”Ndipo Aroni akaunyosha mkono wake juu ya maji ya Misri, nao vyura wakatokea na kuifunika nchi. Lakini waganga wakafanya vivyo hivyo kwa siri ya uganga wao, nao pia wakafanya vyura kuja juu ya nchi ya Misri.
”Wakafanya hivyo, Aroni aliponyosha mkono wake wenye fimbo na kuyapiga mavumbi ya nchi, viroboto wakawajia watu na wanyama. Mavumbi yote katika nchi ya Misri yakawa viroboto. Lakini waganga walipojaribu kutengeneza viroboto kwa siri ya uganga wao, hawakuweza. Nao viroboto walikuwa juu ya watu na wanyama. Waganga wale wakamwambia Farao, “Hiki ni kidole cha Mungu.” Lakini moyo wa Farao ukawa mgumu naye hakuwasikiliza, kama vile BWANA alivyosema.
”Waganga hawakuweza kusimama mbele ya Mose kwa sababu ya majipu yale yaliyokuwa miilini mwao na juu ya miili ya Wamisri wote.
”Usiwe na miungu mingine ila mimi. Usijifanyie sanamu ya kuchonga katika umbo la kitu cho chote kilicho juu mbinguni, au duniani chini, au ndani ya maji. Usivisujudie au kuviabudu; kwa kuwa Mimi, BWANA Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, ninayewaadhibu watoto kwa ajili ya dhambi ya baba zao hadi kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
”Msijifanyizie miungu yo yote na kuilinganisha nami, msijitengenezee miungu ya fedha wala miungu ya dhahabu.
”“Usiruhusu mwanamke mchawi aishi.
”“Mtu awaye yote anayemtolea mungu mwingine dhabihu isipokuwa BWANA, lazima aangamizwe.
”“Uzingatie kutenda kila kitu nilichokuambia. Usiombe kwa majina ya miungu mingine, wala usiyaruhusu kusikika kinywani mwako.
”Watu walipoona kuwa Mose amekawia sana kushuka kutoka mlimani, walimkusanyikia Aroni na kumwambia, “Njoo, tutengenezee miungu itakayotutangulia. Kwa maana huyu jamaa yetu Mose aliyetupandisha kutoka Misri, hatujui jambo lililompata.” Aroni akawajibu, “Vueni vipuli vya dhahabu ambavyo wake zenu, wana wenu na binti zenu wamevaa, mkaniletee.” Kwa hiyo watu wote wakavua vipuli vyao, wakavileta kwa Aroni. Akavichukua vile vitu walivyomkabidhi, akavifanyiza kwa kusubu sanamu yenye umbo la ndama, akaichonga kwa kutumia chombo. Kisha wakasema, “Hii ndiyo miungu yenu, Ee Israeli, iliyowapandisha kutoka Misri.”
”Wamekuwa wepesi kugeuka na kuacha niliyowaamuru, na wamejitengenezea sanamu ya kuyeyusha yenye umbo la ndama. Wameisujudia na kuitolea dhabihu, nao wamesema, ‘Hii ndiyo miungu yenu, Ee Israeli iliyokupandisha kutoka Misri.’ ” BWANA akamwambia Mose, “Nimeona watu hawa, nao ni watu wenye shingo ngumu. Sasa niache ili hasira yangu ipate kuwaka dhidi yao, nami nipate kuwaangamiza. Kisha nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa.”
”Hivyo Mose akarudi kwa BWANA na kumwambia, “Lo! Hawa watu wamefanya dhambi kubwa namna gani! Wamejitengenezea miungu ya dhahabu.
”Bomoa madhabahu zao, vunja mawe yao ya kuabudia na ukatekate nguzo zao za Ashera. Usiabudu mungu mwingine, kwa kuwa BWANA, ambaye jina lake ni Wivu, ni Mungu mwenye wivu. “Uwe mwangalifu usifanye agano na wale watu wanaoishi katika nchi, kwa maana wakati wanapojifanyia ukahaba kwa miungu yao na kuwatolea kafara, watakualika wewe nawe utakula sadaka za matambiko yao. Unapowachagua baadhi ya binti zao kuwa wake wa wana wenu na binti hao wakajifanyia ukahaba kwa miungu yao, watawaongoza wana wenu kufanya vivyo hivyo. “Usijifanyie sanamu za kusubu.
”Hawatatoa kamwe dhabihu zao kwa sanamu za mbuzi ambazo wamekuwa wakijifanyia nazo ukahaba. Hili litakuwa agizo la kudumu kwao na kwa ajili ya vizazi vijavyo.’
”“ ‘Msiabudu sanamu, wala msijitengenezee miungu ya shaba. Mimi ndimi BWANA Mungu wenu.
”“ ‘Msile nyama yo yote yenye damu ndani yake. “ ‘Msifanye uaguzi wala uchawi.
”“ ‘Msichanje chale miili yenu kwa ajili ya mfu, wala msijichore alama juu ya miili yenu. Mimi ndimi BWANA.
”“ ‘Msiwaendee waaguzi, wala msitafute wapunga pepo, kwa maana watawanajisi. Mimi ndimi BWANA Mungu wako.
”“Sema na wana wa Israeli: ‘Mwisraeli ye yote au mgeni anayeishi katika Israeli ambaye atamtoa ye yote miongoni mwa watoto wake kuwa sadaka kwa mungu Moleki, mtu huyo lazima auawe. Watu wa jumuiya hiyo watampiga kwa mawe. Mimi nitauelekeza uso wangu dhidi ya mtu huyo, nami nitamkatilia mbali na watu wake. Kwa maana kwa kumtoa mmoja wa watoto wake kwa mungu Moleki, amenajisi madhabahu yangu na kulinajisi Jina langu takatifu.
”“ ‘Mimi nitauelekeza uso wangu dhidi ya mtu anayewaendea waaguzi na wenye pepo kwa kujifanyia ukahaba kwa kuwafuata, nami nitamkatilia mbali na watu wake.
”“ ‘Mwanaume au mwanamke ambaye ni mchawi, mwaguzi au mwenye kupunga pepo miongoni mwenu lazima auawe. Mtawapiga kwa mawe; nayo damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao wenyewe.’ ”
”“ ‘Msijitengenezee sanamu au kusimamisha kinyago cha kuchonga, mnara, wala jiwe la kuabudia, pia msijiwekee jiwe lililochongwa katika nchi yenu na kusujudu mbele yake. Mimi ndimi BWANA Mungu wenu.
”Nitapaharibu mahali penu pa juu pa kuabudia miungu, nitabomoa madhabahu zenu za kufukizia uvumba na kuzilundika maiti zenu juu ya sanamu zenu zisizo na uhai, nami nitawachukia ninyi sana.
”wafukuzeni wakazi wote wa nchi iliyo mbele yenu. Haribuni sanamu zao zote za kuchongwa, na sanamu zilizotengenezwa kwa kuyeyusha chuma, na kupabomoa mahali pao pa ibada.
”Hamkuona umbo la aina yo yote siku ambayo BWANA alizungumza na ninyi kule Horebu kutoka kwenye moto. Kwa hiyo mjihadhari kwa uangalifu sana, ili msije mkajichafua na kujitengenezea sanamu au kinyago chenye umbo lo lote kama la mwanaume au mwanamke, au kama mnyama aliye juu ya nchi au ndege ye yote arukaye angani, au kama kiumbe kitambaacho juu ya ardhi au samaki ye yote aliye ndani ya maji. Na utazamapo juu angani na ukaliona jua, mwezi na nyota na vyote vinavyoipamba mbingu, usije ukashawishiwa kuviinamia na kuviabudu vile ambavyo BWANA Mungu wenu alivyogawia mataifa yote chini ya mbingu.
”Kwa kuwa BWANA Mungu wenu ni moto ulao, Mungu mwenye wivu.
”Usiwe na miungu mingine ila mimi. Usijitengenezee sanamu katika umbo la kitu cho chote kilicho juu mbinguni au duniani chini au ndani ya maji. Usivisujudie wala kuviabudu; kwa maana Mimi, BWANA Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, ninayewaadhibu watoto kwa ajili ya dhambi za baba zao hata kizazi cha tatu na cha nne cha wale wanichukiao,
”Usifuate miungu mingine, miungu ya mataifa yanayokuzunguka; kwa kuwa BWANA Mungu wako, ambaye yuko katikati yako, ni Mungu mwenye wivu na hasira yake itawaka dhidi yako, naye atakuangamiza kutoka katika uso wa nchi.
”Usioane nao. Usimtoe binti yako kuolewa na mwanawe, au kumchukua binti yake aolewe na mwanao. Kwa maana watamgeuza mwanao aache kunifuata, ili aitumikia miungu mingine, nayo hasira ya BWANA itawaka dhidi yako, naye atakuangamiza ghafula. Hili ndilo utakalowafanyia: Vunja madhabahu zao, yabomoe mawe yao yaliyowekwa wakfu, katakata nguzo zao za Ashera na kuchoma sanamu zao kwa moto.
”Haribuni kabisa kila mahali pao pa kuabudia kwenye milima mirefu, vilima na chini ya kila mti mkubwa ambamo mataifa haya mnayokwenda kuchukua ardhi yao huabudia miungu yao. Bomoeni madhabahu zao, vunjeni yale mawe wanayoabudu, chomeni moto nguzo zao za Ashera; katilieni mbali sanamu za miungu yao na mfute majina yao mahali hapo. Kamwe msimwabudu BWANA Mungu wenu kama wanavyoabudu wao.
”na baada ya kuangamizwa mbele yenu, mwe waangalifu msijiingize katika tanzi kwa kuuliza habari za miungu yao, mkisema, “Je, mataifa haya hutumikiaje miungu yao? Nasi tutafanya vivyo hivyo.” Kamwe msimwabudu BWANA Mungu wenu kwa njia wanayoabudu miungu yao, kwa sababu katika kuabudu miungu yao, wanafanya aina zote za machukizo anayoyachukia BWANA. Hata huwateketeza wana wao na binti zao kwa moto kama kafara kwa miungu yao.
”Kama nabii, au yule anayetabiri kwa njia ya ndoto, akijitokeza miongoni mwenu na akawatangazia ishara ya miujiza na ajabu, ikiwa ishara au ajabu ya aliyozungumza ikatokea, naye akasema, “Na tufuate miungu mingine” (miungu ambayo hamjaifahamu) “na tuiabudu,” kamwe msiyasikilize maneno ya nabii wala mwota ndoto huyo. BWANA Mungu wenu anawajaribu kuangalia kama mnampenda kwa moyo wenu wote na kwa roho yenu yote.
”Kama ndugu yako hasa, au mwanao au binti yako, au mke umpendaye, au rafiki yako wa karibu sana akikushawishi kwa siri, akisema, “Na twende tukaabudu miungu mingine” (miungu ambayo ninyi wala baba zenu hamkuifahamu, miungu ya watu wanaowazunguka, ikiwa karibu au mbali, kutoka mwisho mmoja wa nchi mpaka mwingine), usikubali wala usimsikilize. Usimhurumie! Usimwache wala usimkinge.
”naye amekwenda kinyume na agizo langu kuabudu miungu mingine na kuisujudia, kama vile jua, mwezi au nyota za angani, hili likiwa limeletwa mbele yenu, ni lazima kulichunguza kikamilifu. Ikiwa ni kweli na kuwa limehakikishwa kwamba hili ni chukizo lililofanyika katika Israeli, mchukueni huyo mwanaume au mwanamke ambaye amelifanya tendo hili ovu kwenye lango la mji wenu na kumpiga mawe mtu huyo mpaka afe.
”Asionekane mtu ye yote miongoni mwenu ampitishaye mwanawe au binti yake katika moto, atakayefanya uaguzi, ulozi, anayetabiri nyakati, anayejishughulisha na uchawi, wala alogaye kwa kupiga mafundo, wala apandishaye pepo, anayeabudu mizimu, wala awaombaye wafu. Mtu ye yote afanyaye mambo haya ni chukizo kwa BWANA, tena ni kwa sababu ya matendo haya ya kuchukiza wayafanyayo ndiyo maana BWANA Mungu wenu atayafukuza mataifa hayo mbele yenu.
”Lakini nabii ambaye atathubutu kusema kwa Jina langu kitu cho chote ambacho sikumwamuru akiseme, au nabii ambaye husema kwa jina la miungu mingine ni lazima auawe.”
”“Alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga au mwenye kusubu sanamu, kitu ambacho ni chukizo kwa BWANA, kazi ya mikono ya fundi stadi, na kuisimamisha kwa siri.” Kisha watu wote watasema, “Amen!”
”Wakamfanya Mungu kuwa na wivu kwa miungu yao migeni, na kumkasirisha kwa sanamu zao za machukizo. Wakatoa dhabihu kwa pepo, ambao si Mungu: miungu wasiyoijua, miungu iliyojitokeza siku za karibuni, miungu ambayo baba zenu hawakuiogopa.
”Wamenifanya niwe na wivu kwa kile ambacho si mungu, na kunikasirisha kwa sanamu zao zisizokuwa na thamani. Nitawafanya wawaonee wivu wale ambao si taifa, nitawafanya wakasirishwe na taifa lile lisilo na ufahamu.
”Lakini hawakuwasikiliza hata waamuzi wao, bali walifanya uasherati kwa kuifuata miungu mingine na kuiabudu. Waligeuka mara na kuiacha njia ambayo baba zao waliiendea, yaani, njia ya kutii amri za BWANA.
”Lakini kila mara mwamuzi alipokufa, watu walirudia katika hali mbaya ya uovu zaidi kuliko baba zao, wakiifuata miungu mingine kuitumikia na kuiabudu. Walikataa kuacha matendo yao maovu na njia zao za ukaidi.
”Wana wa Israeli wakatenda tena maovu machoni pa BWANA. Wakaabudu Mabaali na Maashtorethi, miungu ya Aramu, miungu ya Sidoni, miungu ya Moabu, miungu ya Waamoni na miungu ya Wafilisti. Kwa kuwa Waisraeli walimwacha BWANA wala hawakuendelea kumtumikia, hivyo hasira ya BWANA ikawaka dhidi ya Israeli, naye akawatia mikononi mwa Wafilisti na Waamoni,
”Ndipo Waisraeli wakamlilia BWANA wakasema, “Tumetenda dhambi dhidi yako, kumwacha Mungu wetu na kutumikia Mabaali.”
”Lakini ninyi mmeniacha mimi na kutumikia miungu mingine, kwa hiyo sitawaokoa tena. Nendeni mkaililie ile miungu mlioichagua. Hiyo miungu na iwaokoe mnapokuwa katika taabu!.” Lakini Waisraeli wakamwambia BWANA, “Tumetenda dhambi. Ututendee lile unaloona kuwa jema kwako, lakini twakusihi utuokoe sasa.” Nao wakaiondoa hiyo miungu migeni katikati yao nao wakamtumikia BWANA. Naye akahuzunika kwa sababu ya taabu ya Israeli.
”Kisha wakaliingiza lile Sanduku ndani ya hekalu la Dagoni na kuliweka kando ya huyo Dagoni. Watu wa Ashdodi walipoamka asubuhi na mapema kesho yake kumbe, wakamkuta Dagoni ameanguka chini kifudifudi mbele ya Sanduku la BWANA! Wakamwinua Dagoni na kumrudisha mahali pake. Lakini asubuhi iliyofuata, walipoamka kumbe, walimkuta huyo Dagoni ameanguka chini kifudifudi mbele ya Sanduku la BWANA! Kichwa chake na mikono vilikuwa vimevunjwa navyo vimelala kizingitini, ni kiwiliwili chake tu kilichokuwa kimebaki. Ndiyo sababu mpaka leo makuhani wa Dagoni wala wengine waingiao katika hekalu la Dagoni huko Ashdodi hawakanyagi kizingiti. Mkono wa BWANA ulikuwa mzito juu ya watu wa Ashdodi na vijiji vya jirani akaleta uharibifu juu yao na kuwatesa kwa majipu. Watu wa Ashdodi walipoona kile kilichokuwa kikitokea, wakasema, “Sanduku la Mungu wa Israeli kamwe lisikae hapa pamoja na sisi, kwa sababu mkono wake ni mzito juu yetu na juu ya Dagoni mungu wetu.”
”Kwa maana kuasi ni kama dhambi ya uaguzi, nao ukaidi ni kama uovu wa kuabudu sanamu. Kwa sababu umelikataa neno la BWANA, naye amekukataa wewe kuendelea kuwa mfalme.”
”Wakati huo Samweli alikuwa amekufa, nao Israeli wote walikuwa wamemwombolezea na kumzika kwenye mji wake mwenyewe huko Rama. Sauli alikuwa amewafukuza wenye pepo wa utambuzi na wachawi.
”Basi Sauli akawaambia watumishi wake, “Nitafutieni mwanamke mwenye pepo wa utambuzi ili nimwendee, nipate kuuliza kwake.” Watumishi wake wakamwambia, “Yuko mwanamke mmoja huko Endori.” Hivyo Sauli akajigeuza kwa kuvaa mavazi mengine, naye usiku akiwa amefuatana na watu wawili wakaenda kwa huyo mwanamke. Akamwambia, “Nibashirie na unipandishie huyo nitakayekutajia.” Huyo mwanamke akamwambia, “Wewe unajua lile alilofanya Mfalme Sauli. Amewakatilia mbali wapunga pepo, wapiga ramli wote na wachawi katika nchi. Mbona umenitegea maisha yangu ili wapate kuniua?”
”Kadiri Solomoni alivyozidi kuzeeka, wake zake wakageuza moyo wake kuelekea miungu mingine, na moyo wake haukuwa mkamilifu kwa BWANA Mungu wake, kama ulivyokuwa moyo wa Daudi baba yake. Akafuata Ashtorethi mungu mke wa Wasidoni, na Moleki mungu aliyekuwa chukizo la Waamoni. Kwa hiyo Solomoni akafanya uovu machoni pa BWANA; hakumfuata BWANA kikamilifu kama alivyofanya Daudi baba yake. Kwenye kilima mashariki mwa Yerusalemu, Solomoni akajenga mahali pa juu kwa ajili ya Kemoshi chukizo la Wamoabu, na kwa Moleki mungu chukizo la Waamoni. Akafanya hivyo kwa wake zake wote wa kigeni, ambao walifukiza uvumba na kutoa dhabihu kwa miungu yao.
”Nitafanya hivi kwa sababu wameniacha mimi na kuabudu Ashtorethi mungu mke wa Wasidoni, Kemoshi mungu wa Wamoabu, na Moleki mungu wa Waamoni, nao hawakwenda katika njia zangu ili kufanya yaliyo sawa machoni pangu, wala kushika amri na sheria zangu kama Daudi, babaye Solomoni, alivyofanya.
”Baada ya kutafuta shauri, mfalme akatengeneza ndama wawili wa dhahabu. Akawaambia watu, “Ni gharama kubwa kwenu kukwea kwenda Yerusalemu. Hii hapa miungu yenu, Ee Israeli, iliyowapandisha kutoka Misri.”
”Pia wakajijengea mahali pa juu pa kuabudia miungu, mawe ya kuabudiwa na nguzo za Ashera juu ya kila kilima kilichoinuka na kila mti uliotanda. Walikuwepo hata wanaume mahanithi wa mahali pa ibada za sanamu katika nchi; watu wakajiingiza katika kutenda machukizo ya mataifa ambayo BWANA aliyafukuza mbele ya Waisraeli.
”Eliya akasimama mbele ya watu na kusema, “Mtasitasita katika mawazo mawili hadi lini? Ikiwa BWANA ndiye Mungu, mfuateni yeye; lakini ikiwa Baali ni Mungu, basi mfuateni yeye.” Lakini watu hawakusema kitu. Kisha Eliya akawaambia, “Ni mimi peke yangu nabii wa BWANA aliyebaki, lakini Baali ana manabii mia nne na hamsini. Leteni mafahali wawili. Wao na wajichagulie mmoja, wamkate vipande vipande na waweke juu ya kuni lakini wasiiwashie moto. Nitamwandaa huyo fahali mwingine na kumweka juu ya kuni lakini sitawasha moto. Kisha mliitie jina la mungu wenu, nami nitaliitia jina la BWANA Mungu yule ambaye atajibu kwa moto, huyo ndiye Mungu.” Kisha watu wote wakasema, “Hilo unalosema ni jema.”
”Eliya akawaambia manabii wa Baali, “Chagueni mmoja kati ya hawa mafahali na muwe wa kwanza kumwandaa, kwa kuwa ninyi mko wengi sana. Liitieni jina la mungu wenu, lakini msiwashe moto.” Kwa hiyo wakamchukua yule fahali waliyepewa, nao wakamwandaa. Kisha wakaliitia jina la Baali kutoka asubuhi hadi adhuhuri, wakapiga kelele, “Ee Baali, utujibu!” Lakini hapakuwa na jibu; hakuna aliyejibu. Nao wakacheza kuizunguka madhabahu waliyoijenga. Wakati wa adhuhuri, Eliya akaanza kuwadhihaki, akisema, “Pigeni kelele zaidi! Hakika yeye ni mungu! Labda amezama katika mawazo mazito, au ana shughuli nyingi, au amesafiri. Labda amelala usingizi mzito, naye ni lazima aamshwe.” Kwa hiyo wakapiga kelele zaidi na kama ilivyokuwa desturi yao wakajichanja wenyewe kwa visu na vyembe, mpaka damu ikachuruzika. Adhuhuri ikapita, nao wakaendelea na utabiri wao wa kiwazimu mpaka wakati wa dhabihu ya jioni. Lakini hapakuwa na jibu, hakuna aliyejibu, hakuna aliyeangalia.
”Kisha Eliya akawaambia watu wote, “Sogeeni karibu nami.” Watu wote wakamkaribia, naye akakarabati madhabahu ya BWANA, ambayo ilikuwa imevunjwa. Eliya akachukua mawe kumi na mawili, moja kwa ajili ya kila kabila la wana wa Yakobo, ambaye neno la BWANA lilimjia, likisema, “Jina lako litakuwa Israeli.” Kwa mawe hayo, akajenga madhabahu katika jina la BWANA, na akachimba handaki kuizunguka, ukubwa wa kutosha vipimo viwili vya mbegu. Akapanga kuni, akamkata yule fahali vipande vipande na kuvipanga juu ya kuni. Kisha akawaambia, “Jazeni mapipa manne maji na kuyamwaga juu ya sadaka ya kuteketezwa na juu ya kuni.” Akawaambia, “Fanyeni hivyo tena.” Nao wakafanya hivyo tena. Akaagiza, “Fanyeni kwa mara ya tatu.” Nao wakafanya hivyo kwa mara ya tatu. Maji yakatiririka kuizunguka madhabahu na hata kujaza lile handaki.
”Wakati wa kutoa dhabihu ya jioni, nabii Eliya akasogea mbele na kuomba, akisema: “Ee BWANA, Mungu wa Abrahamu, na Isaki na Israeli, ijulikane leo kwamba wewe ndiye Mungu katika Israeli na ya kwamba mimi ni mtumishi wako na nimefanya mambo haya yote kwa neno lako. Unijibu mimi, Ee BWANA, nijibu mimi, ili watu hawa wajue kwamba wewe, Ee BWANA, ndiwe Mungu, na kwamba unaigeuza mioyo yao ikurudie tena.” Kisha moto wa BWANA ukashuka na kuiteketeza ile dhabihu, zile kuni, yale mawe, ule udongo, na pia kuramba yale maji yaliyokuwa ndani ya handaki. Wakati watu wote walipoona hili, wakaanguka kifudifudi na kulia, “BWANA: yeye ndiye Mungu! BWANA: yeye ndiye Mungu!” Kisha Eliya akawaamuru, “Wakamateni hao manabii wa Baali. Msimwache hata mmoja atoroke!” Wakawakamata, naye Eliya akawaleta mpaka Bonde la Kishoni na kuwachinja huko.
”Alitenda kwa uovu sana katika kuabudu sanamu, kama wale Waamori ambao BWANA aliowafukuza mbele ya Israeli.)
”Yoramu alipomwona Yehu akauliza, “Je, Yehu, umekuja kwa amani?” Yehu akajibu, “Kunawezaje kuwa na amani wakati ibada za sanamu na uchawi wa mama yako Yezebeli ungaliko?”
”Wakaileta ile nguzo ya kuabudiwa nje ya hekalu la Baali na wakaichoma moto. Wakabomoa ile nguzo ya kuabudiwa ya Baali pamoja na hekalu la Baali, nao watu wakapafanya kuwa choo hadi leo.
”Wakafukiza uvumba kila mahali palipoinuka, kama walivyofanya yale mataifa ambayo BWANA alikuwa ameyafukuza mbele yao. Wakafanya mambo maovu ambayo yalimghadhibisha BWANA. Wakaabudu sanamu, ingawa BWANA alikuwa amesema, “Msifanye mambo haya.”
”Lakini hawakusikiliza, walikuwa na shingo ngumu kama baba zao, ambao hawakumtegemea BWANA Mungu wao. Walizikataa amri zake na Agano alilokuwa amelifanya na baba zao na maonyo aliyokuwa amewapa. Wakafuata sanamu zisizofaa, nao wenyewe wakawa hawafai. Wakayaigiza mataifa yaliyowazunguka, ingawa BWANA alikuwa amewaonya akiwaambia, “Msifanye kama wanavyofanya,” nao wakafanya mambo ambayo BWANA alikuwa amewakataza wasifanye. Wakayaacha maagizo yote ya BWANA Mungu wao na kujitengenezea sanamu mbili walizozisubu katika sura ya ndama na nguzo ya Ashera. Wakasujudia mianga yote ya angani, wakamtumikia Baali. Wakawatoa kafara wana wao na mabinti zao katika moto. Wakafanya uaguzi na uchawi, nao wakajiuza wenyewe katika kutenda uovu machoni pa BWANA, wakamghadhibisha. Basi BWANA akawakasirikia sana Israeli na kuwaondoa kwenye uwepo wake. Ni kabila la Yuda tu ndilo lililobaki;
”Hata hivyo, kila kikundi cha taifa lililoletwa Samaria kilitengeneza miungu yao wenyewe katika miji kadhaa mahali walipoishi, nao wakaiweka mahali pa ibada za miungu ambapo watu wa Samaria walikuwa wametengeneza katika mahali pa juu.
”Walimwabudu BWANA, lakini pia waliitumikia miungu yao kulingana na desturi za mataifa walikotoka. Mpaka leo wanashikilia desturi zao za zamani. Hawamwabudu BWANA wala kuzishika hukumu na maagizo, sheria na amri ambazo BWANA aliwapa uzao wa Yakobo, ambaye alimwita Israeli. Wakati BWANA alipofanya Agano na Waisraeli aliwaamuru akisema: “Msiiabudu miungu mingine yo yote wala kuisujudia, wala kuitumikia wala kuitolea dhabihu.
”Akapaondoa mahali pa juu pa kuabudia miungu, akazivunja sanamu, akakatakata nguzo za Ashera. Akavunja vipande vipande ile nyoka ya shaba Mose aliyotengeneza, kwa kuwa hadi siku hizo wana wa Israeli walikuwa wanaifukizia uvumba (nayo ilikuwa ikiitwa Nehushtani).
”“Ni kweli, Ee BWANA, kwamba wafalme wa Ashuru wameyaangamiza mataifa haya na nchi zao. Wameitupa miungu yao kwenye moto na kuiangamiza, kwa kuwa haikuwa miungu bali ni miti na mawe tu, iliyotengenezwa kwa mikono ya wanadamu.
”Akamtoa kafara mwanawe mwenyewe katika moto, akafanya uchawi na uaguzi, na akataka shauri kwa wapiga ramli na kwa mizimu. Akafanya maovu mengi sana machoni mwa BWANA na kumghadhibisha.
”“Manase mfalme wa Yuda ametenda dhambi hizi za kuchukiza. Amefanya maovu mengi kuliko Waamori waliokuwepo kabla yake na ameiongoza Yuda katika dhambi kwa sanamu zake. Kwa hiyo hili ndilo asemalo BWANA, Mungu wa Israeli: Nitaleta maafa makubwa juu ya Yerusalemu na Yuda kiasi kwamba masikio ya kila mmoja atakayesikia habari zake yatawasha.
”Akaenenda katika njia zote za baba yake, akaabudu sanamu ambazo baba yake aliziabudu na kuzisujudia.
”Akawafukuza makuhani wa kipagani waliokuwa wameteuliwa na wafalme wa Yuda kufukiza uvumba katika mahali pa juu pa kuabudia miungu katika miji ya Yuda na ile inayozunguka Yerusalemu, yaani wale waliofukiza uvumba kwa Baali, kwa jua na mwezi, kwa makundi ya nyota, na jeshi lote la angani. Akaiondoa nguzo ya Ashera kutoka kwenye Hekalu la BWANA na kuipeleka kwenye Bonde la Kidroni nje ya Yerusalemu na kuiteketeza huko. Akaisaga hadi ikawa unga na kusambaza hilo vumbi juu ya makaburi ya watu wabaya ambao waliitolea kafara. Akabomoa pia nyumba za mahanithi wa mahali pa ibada za miungu, zilizokuwa ndani ya Hekalu la BWANA na mahali wanawake walipofuma kwa ajili ya Ashera. Yosia akawaleta makuhani wote wa BWANA kutoka miji yote ya Yuda na kupafanya mahali pa juu pa kuabudia miungu pasifae tena kufanyia hizo ibada, kuanzia Geba hadi Beer-Sheba, mahali pote ambapo hao makuhani wa miungu walifukiza uvumba. Akabomoa mahali pa kuwekea vitu vya ibada za miungu palipokuwa katika malango, kwenye ingilio la lango la Yoshua, mtawala wa mji, lililoko upande wa kushoto wa lango la mji.
”Zaidi ya hayo, Yosia akawaondoa wapunga pepo, wanaoabudu mizimu, sanamu za kuagulia, sanamu za kuabudiwa na vitu vingine vyote vya machukizo vilivyoonekana katika Yuda na Yerusalemu. Haya aliyafanya ili kutimiza itakiwavyo kulingana na sheria iliyoandikwa ndani ya kile kitabu ambacho Hilkia kuhani alikikuta ndani ya Hekalu la BWANA.
”Sauli alikufa kwa sababu hakuwa mwaminifu kwa BWANA. Hakulishika neno la BWANA, hata akataka shauri kwa mwaguzi kwa ajili ya uongozi,
”Kwa maana miungu yote ya mataifa ni sanamu, lakini BWANA aliziumba mbingu.
”Naye akawa amechagua makuhani wake mwenyewe kwa ajili ya mahali pa juu pa kuabudia sanamu za mbuzi na za ndama ambazo alikuwa ametengeneza.
”Akaziondoa madhabahu za kigeni na mahali pa juu pa kuabudia miungu, akayavunja yale mawe ya kuabudiwa na kuzikatakata nguzo za Maashera.
”Wakaacha Hekalu la BWANA, Mungu wa baba zao, wakaabudu nguzo za maashera na sanamu. Kwa sababu ya kosa lao, hasira ya Mungu ikaja juu ya Yuda na Yerusalemu.
”Akatoa kafara kwa miungu ya Dameski, ambao walikuwa wamemshinda, kwa kuwa aliwaza, “Kwa kuwa miungu ya mfalme wa Aramu imewasaidia wao, nitaitolea dhabihu ili inisaidie na mimi.” Lakini haya ndiyo yaliyokuwa maangamizi yake na Israeli wote. Ahazi akakusanya pamoja vyombo vya nyumba ya Mungu na kuvivunja vipande vipande. Akafunga milango ya Hekalu la BWANA na kusimamisha madhabahu katika kila njia panda ya barabara za Yerusalemu. Katika kila mji wa Yuda akajenga mahali pa juu pa kuabudia miungu ili kutolea miungu mingine kafara za kuteketezwa na kuchochea hasira ya BWANA, Mungu wa baba zake.
”Akafanya yaliyo maovu machoni pa BWANA, akafanya machukizo kama walivyofanya mataifa BWANA aliyoyafukuza mbele ya Waisraeli. Akajenga upya mahali pa juu pa kuabudia miungu ambapo Hezekia baba yake, alikuwa amepabomoa, pia akasimamisha madhabahu za Mabaali na nguzo za Maashera. Akalisujudia jeshi lote la vitu vya angani na kuliabudu.
”Akawatoa wanawe kuwa kafara kwa kuwapitisha katika moto katika Bonde la Hinomu, akafanya ulozi, uaguzi na uchawi, akataka ushauri kwa wenye pepo wa utambuzi na wenye kuwasiliana na mizimu. Akafanya maovu mengi machoni pa BWANA, akaichochea hasira yake. Akachukua ile sanamu aliyoichonga akaiweka katika Hekalu la BWANA ambalo Mungu alikuwa amemwambia Daudi na mwanawe Solomoni, “Katika Hekalu hili na katika Yerusalemu niliouchagua kutoka kabila zote za Israeli, nitaliweka Jina langu milele.
”Huzuni itaongezeka kwa wale wanaokimbilia miungu mingine. Sitazimimina sadaka zao za damu au kutaja majina yao midomoni mwangu.
”Wakamkasirisha Mungu kwa mahali pao pa juu pa kuabudia miungu, walichochea wivu wake kwa sanamu zao. Wakati Mungu alipowasikia, alikasirika sana, akamkataa Israeli kabisa.
”Kwa maana miungu yote ya mataifa ni sanamu, lakini BWANA aliziumba mbingu.
”Wote waabuduo sanamu waaibishwe, wale wajisifiao sanamu: mwabuduni yeye, enyi miungu yote!
”Waliabudu sanamu zao, zikawa mtego kwao. Wakawatoa wana wao na binti zao dhabihu kwa mashetani. Walimwaga damu isiyo na hatia, damu za wana wao na binti zao, ambao waliwatoa dhabihu kwa sanamu za Kanaani, nayo nchi ikanajisika kwa damu zao.
”Lakini sanamu zao ni za fedha na dhahabu, zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu. Zina vinywa, lakini haziwezi kusema, zina macho, lakini haziwezi kuona; zina masikio, lakini haziwezi kusikia, zina pua, lakini haziwezi kunusa; zina mikono, lakini haziwezi kupapasa, zina miguu, lakini haziwezi kutembea; wala koo zao haziwezi kutoa sauti. Wale wanaozitengeneza watafanana nazo, vivyo hivyo wale wote wanaozitumainia.
”Sanamu za mataifa ni fedha na dhahabu, zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu. Zina vinywa, lakini haziwezi kusema, zina macho, lakini haziwezi kuona, zina masikio, lakini haziwezi kusikia, wala hakuna pumzi katika vinywa vyao. Wale wanaozitengeneza watafanana nazo, vivyo hivyo wote wanaozitumainia.
”Umewatelekeza watu wako, nyumba ya Yakobo. Wamejaa ushirikina utokao Mashariki, wanapiga ramli kama Wafilisti na wanashikana mikono na wapagani.
”Nchi yao imejaa sanamu, wanasujudia kazi za mikono yao, vitu vile ambavyo vidole vyao vimevitengeneza.
”Katika siku ile watu watawatupia panya na popo vinyago vyao vya fedha na vya dhahabu, walivyovitengeneza ili waviabudu.
”Wakati watu wanapowaambia ninyi kutafuta ushauri kwa waaguzi na wenye kuongea na mizimu, ambao hunong'ona na kunung'unika, je, watu wasingeuliza kwa Mungu wao? Kwa nini watake shauri kwa wafu kwa ajili ya walio hai? Kwa sheria na kwa ushuhuda! Kama hawatasema sawasawa na neno hili, hawana mwanga wa mapambazuko.
”Tazama jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya asubuhi, mwana wa mapambazuko! Umetupwa chini duniani, wewe uliyepata kuangusha mataifa! Ulisema moyoni mwako, “Nitapanda juu hadi mbinguni, nitakiinua kiti changu cha enzi juu ya nyota za Mungu, nitaketi nimetawazwa juu ya mlima wa kusanyiko, kwenye vimo vya juu sana vya Mlima Mtakatifu. Nitapaa juu kupita mawingu, nitajifanya kama Yeye Aliye Juu Sana.” Lakini umeshushwa chini hadi kuzimu, hadi kwenye vina vya shimo.
”Wamisri watakufa moyo, na nitaifanya mipango yao kuwa batili, watatafuta ushauri kwa sanamu na kwa roho za waliokufa, kwa wapiga ramli na kwa wale waongeao na mizimu.
”Kisha mtanajisi sanamu zenu zilizofunikwa kwa fedha na vinyago vyenu vilivyofunikwa kwa dhahabu, mtazitupilia mbali kama vitambaa vya wakati wa hedhi na kuziambia, “Haya, tokeni hapa!”
”Kwa kuwa katika siku ile kila mmoja wenu atazikataa sanamu za fedha na za dhahabu zilizotengenezwa kwa mikono yenu yenye dhambi.
”“Mimi ndimi BWANA; hilo ndilo Jina langu! Sitampa mwingine utukufu wangu wala sanamu sifa zangu.
”Lakini wale wanaotumaini sanamu, wanaoviambia vinyago, ‘Ninyi ndio miungu yetu,’ watarudishwa nyuma kwa aibu kubwa.
”“Ninyi ni mashahidi wangu,” asema BWANA, “na mtumishi wangu niliyemchagua, ili mpate kunijua na kuniamini na kutambua kwamba Mimi ndiye. Kabla yangu hakuna mungu aliyefanyizwa, wala hatakuwepo mwingine baada yangu.
”“Hili ndilo asemalo BWANA, Mfalme wa Israeli na Mkombozi, BWANA Mwenye Nguvu Zote: Mimi ni wa kwanza na Mimi ni wa mwisho; zaidi yangu hakuna Mungu.
”Wote wachongao sanamu ni ubatili, navyo vitu wanavyovithamini havifai kitu. Wale ambao wangesema juu yao ni vipofu, ni wajinga, ili wao waaibike. Ni nani atengenezaye mungu na kusubu sanamu, ambayo haiwezi kumfaidia kitu cho chote? Yeye pamoja na wenziwe wa aina yake wataaibishwa, mafundi wao si kitu ila ni wanadamu tu. Wote na wakusanyike pamoja na kuwa na msimamo wao, watashushwa chini kwa hofu na kwa fedheha. Muhunzi huchukua kifaa na kukifanyia kazi kwenye makaa ya moto, hutengeneza sanamu kwa nyundo, huifanyiza kwa nguvu za mkono wake. Huona njaa na kupoteza nguvu zake, asipokunywa maji huzimia. Seremala hupima kwa kutumia kamba na huuchora mstari kwa kalamu; huchonga kwa patasi na kutia alama kwa bikari. Huifanyiza katika umbo la binadamu, la mwanadamu katika utukufu wake wote, ili iweze kukaa katika sehemu yake ya ibada ya miungu. Hukata miti ya mierezi, huchukua mteashuri au mwaloni. Huuacha ukue miongoni mwa miti ya msituni, au hupanda msunobari, mvua huufanya ukue. Ni kuni kwa ajili ya binadamu, huchukua baadhi yake na kuota moto, huwasha moto na kuoka mkate. Lakini pia huutumia kumtengeneza mungu na akamwabudu, huitengeneza sanamu na kuisujudia.
”Mabaki yake hutengeneza mungu, sanamu yake; yeye huisujudia na kuiabudu. Huiomba na kusema, “Niokoe; wewe ni mungu wangu.” Hawajui cho chote, hawaelewi cho chote, macho yao yamefungwa hivyo hawawezi kuona, akili zao zimefungwa hivyo hawawezi kufahamu.
”Mimi ndimi BWANA, wala hakuna mwingine, zaidi yangu hakuna Mungu. Nitakutia nguvu, ingawa wewe hukunitambua,
”“Kusanyikeni pamoja mje, enyi wakimbizi kutoka katika mataifa. Wale wabebao sanamu za mti ni watu wasio na akili, Wale waombao miungu ile isiyoweza kuokoa.
”Wengine humwaga dhahabu kutoka kwenye mifuko yao na kupima fedha kwenye mizani; huajiri mfua dhahabu kutengeneza mungu, kisha huisujudia na kuiabudu. Huiinua kuiweka mabegani na kuichukua; huiweka mahali pake, papo hapo ndipo isimamapo, wala haiwezi kusogea kutoka mahali pale. Ingawa mtu huililia, haijibu; haiwezi kumwokoa kwenye taabu zake.
”“Endelea basi na uaguzi wako na wingi wa uchawi wako, ambao umeutumikia tangu utoto wako. Labda utafanikiwa, labda unaweza ukasababisha hofu kuu. Ushauri wote uliopokea umekuchosha bure! Wanajimu wako na waje mbele, wale watazamao nyota na watabirio mwezi baada ya mwezi, wao na wawaokoe na lile linalokuja juu yenu. Hakika wako kama mabua makavu, moto utawateketeza. Hawawezi hata kujiokoa wao wenyewe kutokana na nguvu za mwali wa moto. Hapa hakuna makaa ya kumtia mtu ye yote joto; hapa hakuna moto wa kuota. Hayo ndiyo yote wanayoweza kuwatendea ninyi, hawa ambao umetaabika nao na kufanya nao biashara tangu utoto. Kila mmoja atatoroka; hakuna ye yote awezaye kukuokoa.
”“ ‘Je, mtaiba na kuua, mtazini na kuapa kwa uongo na kufukiza uvumba kwa Baali na kufuata miungu mingine ambayo hamkuijua, kisha mje na kusimama mbele yangu katika nyumba hii, inayoitwa kwa Jina langu, mkisema, “Tuko salama.” Salama kwa kufanya mambo haya yote ya kuchukiza? Je, nyumba hii, iitwayo kwa Jina langu, imekuwa pango la wanyang'anyi kwenu? Lakini nimekuwa nikiona yanayotendeka! Asema BWANA.
”Watoto wanakusanya kuni, baba zao wanawasha moto na wanawake wanakanda unga na kuoka mikate kwa ajili ya Malkia wa Mbinguni. Wanamimina sadaka za vinywaji kwa miungu mingine ili kunikasirisha.
”Itawekwa wazi juani na kwenye mwezi na nyota zote za mbingu, ambazo walizipenda na kuzitumikia na ambazo wamezifuata kutafuta ushauri na kuziabudu. Hawatakusanywa pamoja au kuzikwa, lakini watakuwa kama mavi yaliyotapakaa juu ya ardhi.
”Kwa maana desturi za mataifa hazina maana, wanakata mti kutoka msituni na fundi anauchonga kwa patasi. Wanaparemba kwa fedha na dhahabu, wanakikaza kwa nyundo na misumari ili kisitikisike. Sanamu zao ni kama sanamu iliyowekwa shambani kutishia ndege kwenye shamba la matango, nazo haziwezi kuongea; sharti zibebwe kwa sababu haziwezi kutembea. Usiziogope; haziwezi kudhuru wala kutenda lo lote jema.”
”“Waambie hivi: ‘Miungu hii, ambayo haikuumba mbingu na dunia, itaangamia kutoka duniani na kutoka chini ya mbingu.’ ”
”Kila mmoja ni mjinga na hana maarifa, kila sonara ameaibishwa na sanamu zake. Vinyago vyake ni madanganyo, wala havina pumzi ndani yake. Havina maana, ni vitu vya mzaha tu, hukumu yao itakapokuja, wataangamia.
”Watu hawa waovu, wanaokataa kusikiliza maneno yangu, wafuatao ukaidi wa mioyo yao na kufuata miungu mingine kuitumikia na kuiabudu, watakuwa kama mkanda huu ambao haufai kabisa!
”Je, watu hujitengenezea miungu yao wenyewe? Naam, lakini hao si miungu!”
”Kwa kuwa wameniacha na kupafanya mahali hapa kuwa pa miungu ya kigeni, wameiteketezea sadaka miungu ambayo wao wala baba zao wala wafalme wa Yuda kamwe hawakuijua, nao wamelijaza eneo hili kwa damu isiyo na hatia. Wamejenga mahali pa juu pa kuabudia miungu pa Baali ili kuteketeza wana wao katika moto kama sadaka kwa Baali, kitu ambacho sikukiamuru wala kukitaja, wala hakikuingia akilini mwangu. Hivyo jihadharini, siku zinakuja, asema BWANA, wakati watu hawatapaita tena mahali hapa Tofethi ama Bonde la Ben-Hinomu, bali Bonde la Machinjo.
”Nyumba zilizoko Yerusalemu na zile za wafalme wa Yuda zitatiwa unajisi kama mahali hapa, yaani, Tofethi. Nyumba zote ambazo walifukiza uvumba juu ya mapaa yake kwa jeshi lote la angani na kumimina dhabihu ya kinywaji kwa miungu mingine.’ ”
”Msiifuate miungu mingine ili kuitumikia na kuiabudu, msinikasirishe kwa vitu ambavyo mmevitengeneza kwa mikono yenu.”
”Kwa hiyo msiwasikilize manabii wenu, waaguzi wenu, waota ndoto wenu, watabiri na wachawi wanaowaambia ninyi, ‘Hamtamtumikia mfalme wa Babeli.’ Wanawatabiria ninyi uongo ambako kutawafanya ninyi mhamishwe mbali kutoka kwenye nchi yenu, nitawafukuzia mbali nanyi mtaangamia.
”Waliweka miungu yao ya kuchukiza sana katika nyumba iitwayo kwa Jina langu na kuinajisi. Wakajenga mahali pa juu pa kuabudia miungu kwa ajili ya Baali katika Bonde la Ben-Hinomu ambapo walitoa wana wao na binti zao kafara kwa Moleki, ingawa kamwe sikuamuru, wala halikuingia akilini mwangu, kwamba watafanya chukizo kama hilo na kumfanya Yuda atende dhambi.
”“Kila mtu hana ufahamu na hana maarifa; kila sonara ameaibika kwa sanamu zake. Vinyago vyake ni vya udanganyifu, havina pumzi ndani yake. Hazifai kitu, ni vitu vya kufanyia mzaha, hukumu yao itawadia, zitaangamia.
”na useme, ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Ole wao wanawake washonao hirizi za uchawi juu ya viwiko vyao vyote na kutengeneza shela za urefu wa aina mbalimbali kwa ajili ya kufunika vichwa vyao kwa makusudi ya kuwanasa watu. Je, mtatega uhai wa watu wangu lakini ninyi mponye wa kwenu?
”“ ‘Kwa hiyo hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Mimi niko kinyume na hizo hirizi zenu za uchawi ambazo kwa hizo mnawatega watu kama ndege, nami nitazirarua kutoka mikononi mwenu, nitawaweka huru watu wale mliowatega kama ndege.
”“Mwanadamu, watu hawa wameweka sanamu katika mioyo yao na kuweka vitu viovu vya kukwaza mbele ya macho yao. Je, kweli niwaruhusu waniulize jambo lo lote? Kwa hiyo sema nao uwaambie, ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Wakati Mwisraeli ye yote anapoweka sanamu moyoni mwake na kuweka kitu kiovu cha kukwaza mbele ya macho yake na kisha akaenda kwa nabii, Mimi BWANA nitamjibu peke yangu sawasawa na ukubwa wa ibada yake ya sanamu. Nitafanya jambo hili ili kukamata tena mioyo ya watu wa Israeli, ambao wote wameniacha kwa ajili ya sanamu zao.
”“Kwa hiyo iambie nyumba ya Israeli, ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Tubuni! Geukeni kutoka kwenye sanamu zenu na mkatae matendo yenu yote ya machukizo! “ ‘Mwisraeli ye yote au mgeni ye yote anayeishi katika Israeli anapojitenga nami na kujiwekea sanamu katika moyo wake na kwa hivyo kuweka kitu kiovu cha kukwaza mbele ya macho yake na kisha akamwendea nabii kuuliza shauri kwangu, mimi BWANA nitamjibu mwenyewe.
”Kwa kuwa mfalme wa Babeli sasa amesimama katika njia panda, katika makutano ya njia mbili, akipiga ramli: anapiga kura kwa kutumia mishale, anataka shauri kwa sanamu zake, anachunguza maini ya wanyama.
”Danieli akajibu, “Hakuna mwenye hekima, msihiri, mganga au mwaguzi anayeweza kumweleza mfalme siri aliyouliza, lakini yuko Mungu mbinguni afunuaye siri. Amemwonyesha Mfalme Nebukadneza kitakachotokea siku zijazo. Ndoto yako na maono yaliyopita akilini mwako ulipokuwa umelala kitandani mwako ni haya:
”Walipokuja waganga, wasihiri, wanajimu na waaguzi, niliwaambia ndoto yangu, lakini hawakuweza kunifasiria.
”Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinizuia kwa siku ishirini na moja. Ndipo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu, alikuja kunisaidia, kwa sababu nilikuwa nimezuiliwa huko na mfalme wa Uajemi.
”“Wale watu wanaong'ang'ana na sanamu zisizofaa hupoteza neema ile ambayo ingekuwa yao.
”Nitaangamiza uchawi wenu na hamtapiga tena ramli. Nitaangamiza vinyago vyenu vya kuchonga na mawe yenu ya ibada yatoke katikati yenu; hamtasujudia tena kazi ya mikono yenu. Nitang'oa nguzo za Ashera katikati yenu na kubomoa miji yenu.
”“Sanamu ina thamani gani, kwani mwanadamu ndiye aliyechonga? Ama kinyago kinachofundisha uongo? Kwa kuwa yeye aliyekitengeneza hutegemea kazi ya mikono yake mwenyewe; hutengeneza sanamu zisizoweza kuzungumza. Ole wake yeye auambiaye mti, ‘Uwe hai!’ Ama asemaye na jiwe lisilo na uhai, ‘Amka!’ Je, linaweza kuongoza? Limefunikwa kwa dhahabu na fedha, hakuna pumzi ndani yake.
”“Nitaiadhibu Yuda na wote wakaao Yerusalemu. Kutoka mahali hapa nitakatilia mbali kila mabaki ya Baali, majina ya wapagani na makuhani waabuduo sanamu: wale ambao husujudu juu ya mapaa kuabudu jeshi la vitu vya angani, wale ambao husujudu na kuapa kwa BWANA na ambao pia huapa kwa Malkamu,
”Sanamu huzungumza udanganyifu, waaguzi huona maono ya uongo; husimulia ndoto ambazo si za kweli, wanatoa faraja batili. Kwa hiyo watu wanatangatanga kama kondoo walioonewa kwa kukosa mchungaji.
”Yuda amevunja uaminifu. Jambo la kuchukiza limetendeka katika Israeli na katika Yerusalemu: Yuda amepanajisi mahali patakatifu apendapo BWANA, kwa kuoa binti wa mungu mgeni. Kwa maana kwa mtu awaye yote atendaye jambo hili, BWANA na amkatilie mbali kutoka hema za Yakobo, hata kama huwa anamletea BWANA Mwenye Nguvu Zote sadaka.
”Nanyi msimwite mtu ye yote ‘Baba,’ hapa duniani kwa maana mnaye Baba mmoja, naye yuko mbinguni.
”Yesu akamjibu, “Amin, amin nakuambia, mtu hawezi kuuona Ufalme wa Mungu asipozaliwa mara ya pili.” Nikodemo akauliza, “Awezaje mtu kuzaliwa wakati akiwa mzee? Hakika hawezi kuingia mara ya pili kwenye tumbo la mama yake ili azaliwe!” Yesu akamwambia, “Amin, amin nakuambia, hakuna mtu ye yote anayeweza kuingia katika Ufalme wa Mungu isipokuwa amezaliwa kwa maji na kwa Roho. Mwili huzaa mwili, lakini Roho huzaa roho. Kwa hiyo usishangae ninapokuambia huna budi ‘kuzaliwa mara ya pili.’ Upepo huvuma po pote upendapo. Mvumo wake unausikia lakini huwezi ukafahamu utokako wala uendako. Ndivyo ilivyo kwa kila mtu aliyezaliwa na Roho.”
”“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Kwa maana Mungu hakumtuma Mwanawe kuuhukumu ulimwengu, bali kwa yeye ulimwengu upate kuokolewa. Ye yote amwaminiye hahukumiwi, lakini asiyeamini amekwisha kuhukumiwa, kwa sababu hakumwamini Mwana pekee wa Mungu.
”“Amin, amin nawaambia, yeye asiyeingia katika zizi la kondoo kwa kupitia kwenye lango, lakini akwea kuingia ndani kwa njia nyingine, ni mwivi na mnyang'anyi.
”Yesu akawaambia, “Mimi ndimi njia na kweli na uzima. Mtu hawezi kuja kwa Baba isipokuwa kwa kupitia kwangu.
”Atakapokuja huyo Roho wa kweli atawaongoza awatie katika kweli yote. Yeye hatanena kwa ajili yake mwenyewe, bali atanena yale yote atakayosikia, naye atawaonyesha mambo yajayo.
”Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hakuna Jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.”
”Basi mtu mmoja jina lake Simoni alikuwa amefanya uchawi kwa muda mrefu katika mji huo akiwashangaza watu wote wa Samaria. Alijitapa kwamba yeye ni mtu mkuu, watu wote wakubwa kwa wadogo wakamsikiliza na kumaka wakisema “Mtu huyu ndiye uweza wa Mungu ujulikanao kama ‘Uweza Mkuu.’ ” Wakamfuata kwa sababu kwa muda mrefu alikuwa amewashangaza kwa uchawi wake. Lakini watu walipomwamini Filipo akihubiri habari njema za Ufalme wa Mungu na jina la Yesu Kristo, wakabatizwa wanaume na wanawake. Simoni naye akaamini na akabatizwa. Akamfuata Filipo kila mahali, akistaajabishwa na ishara kuu na miujiza aliyoiona.
”Walipokwisha kupita katika nchi zote hizo wakafika Pafo, ambapo walikutana na Myahudi mmoja mchawi aliyekuwa nabii wa uongo, jina lake Bar Yesu. Mtu huyu alikuwa pamoja na Sergio Paulo, mtu mwenye hekima aliyekuwa msaidizi wa mwakilishi wa mtawala wa kile kisiwa, Sergio Paulo akawaita Sauli na Barnaba akitaka kusikia neno la Mungu. Lakini Elima yule mchawi (hii ndiyo maana ya jina lake), aliwapinga Barnaba na Sauli na kujaribu kumpotosha yule mkuu wa kile kisiwa aiache imani. Ndipo Sauli, ambaye pia aliitwa Paulo, akiwa amejawa na Roho Mtakatifu, akamkazia macho yule Elima mchawi, kamwambia, “Ewe mwana wa ibilisi, wewe ni adui wa kila kilicho haki! Umejaa kila aina ya udanganyifu na ulaghai. Je, hutaacha kuzipotosha njia za Bwana zilizonyooka? Nawe sasa sikiliza, mkono wa Bwana u dhidi yako. Utakuwa kipofu, wala hutaona jua kwa muda.” Mara ukungu na giza vikamfunika, naye akaenda huko na huko akitafuta mtu wa kumshika mkono ili amwonyeshe njia. Yule mkuu wa kile kisiwa alipoona yaliyotukia, akaamini kwa sababu alistaajabishwa na mafundisho kuhusu Bwana.
”Wakamwita Barnaba Zeu na Paulo wakamwita Herme kwa kuwa ndiye aliyekuwa msemaji mkuu. Kuhani wa Zeu, ambaye hekalu lake lilikuwa nje kidogo tu ya mji, akaleta mafahali na mashada ya maua penye lango la mji kwa sababu yeye pamoja na ule umati wa watu walitaka kuwatolea dhabihu. Lakini mitume Paulo na Barnaba waliposikia na kuona mambo haya waliyotaka kufanya, wakararua nguo zao, wakawaendea wale watu kwa haraka, wakawapigia kelele, wakisema, “Enyi watu, kwa nini mnafanya mambo haya? Sisi ni wanadamu tu kama ninyi! Tunawaletea habari njema, tukiwaambia kwamba mgeuke mtoke katika mambo haya yasiyofaa mmwelekee Mungu aliye hai, aliyeziumba mbingu na nchi na bahari na kila kitu kilicho ndani yake.
”Siku moja, tulipokuwa tukienda mahali pa kusalia, tulikutana na mtumwa mmoja wa kike ambaye alikuwa na pepo wa uaguzi. Naye alikuwa amewapatia mabwana zake mapato makubwa ya fedha kwa ubashiri. Huyu mtumwa wa kike alikuwa akimfuata Paulo na sisi akipiga kelele, “Watu hawa ni watumishi wa Mungu Aliye Juu Sana, wao wanawatangazieni njia ya wokovu.” Akaendelea kufanya hivi kwa siku nyingi, lakini Paulo akiwa ameudhika sana, akageuka na kumwambia yule pepo mchafu, “Ninakuamuru katika jina la Yesu Kristo, umtoke!” Yule pepo mchafu akamtoka saa ile ile.
”Ndipo Paulo akasimama katikati ya Areopago akasema, “Enyi watu wa Athene! Ninaona kwamba katika kila jambo ninyi ni watu wa dini sana. Kwa kuwa nilipokuwa nikitembea mjini na kuangalia kwa bidii vitu vyenu vya kuabudiwa, niliona huko madhabahu moja iliyoandikwa: KWA MUNGU ASIYEJULIKANA. Basi sasa kile ambacho mmekuwa mkikiabudu kama kisichojulikana, ndicho ninachowahubiria. “Mungu aliyeumba dunia na vyote vilivyomo ndani yake, yeye ndiye Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika mahekalu yaliyojengwa kwa mikono ya wanadamu. Wala hatumikiwi na mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji cho chote, kwa sababu yeye mwenyewe ndiye awapaye watu wote uhai na pumzi na vitu vyote. Kutoka kwa mtu mmoja, yeye aliumba mataifa yote ya wanadamu ili waikalie dunia yote, naye akaweka nyakati za kuishi. Mungu alifanya hivyo ili wanadamu wamtafute na huenda wakamfikia ingawa kwa kupapasapapasa ijapokuwa kwa kweli hakai mbali na kila mmoja wetu. ‘Kwa kuwa katika yeye tunaishi, tunatembea na kuwa na uzima wetu.’ Kama baadhi ya watunga mashairi wenu walivyosema, ‘Sisi ni watoto wake.’ “Kwa kuwa sisi ni watoto wa Mungu, haitupasi kudhani kuwa Uungu ni kama sanamu ya dhahabu au ya fedha au ya jiwe iliyotengenezwa kwa ubunifu na ustadi wa mwanadamu. Zamani wakati wa ujinga, Mungu alijifanya kama haoni, lakini sasa anawaamuru watu wote kila mahali watubu.
”Idadi kubwa ya wale waliofanya mambo ya uganga wakaleta vitabu vyao na kuviteketeza kwa moto hadharani. Walipofanya hesabu ya thamani ya vitabu vilivyoteketezwa ilikuwa drakam 50,000 za fedha.
”Ingawa wakijidai kuwa wenye hekima, wakawa wajinga na kubadili utukufu wa Mungu aishiye milele kwa sanamu zilizofanywa zifanane na mwanadamu ambaye hufa, na mfano wa ndege, wanyama na viumbe vitambaavyo.
”Kwa sababu waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakaabudu na kutumikia kiumbe badala ya Muumba, ahimidiwaye milele! Amen.
”Hivyo basi, kuhusu kula chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu, tunajua kwamba “sanamu si kitu cho chote kabisa duniani na kwamba kuna Mungu mmoja tu.” Kwa maana hata kama wapo hao wanaoitwa “miungu” kama ni mbinguni au duniani (kama ilivyo kweli wapo “miungu” wengi na “mabwana” wengi).
”Kwa hiyo wapenzi wangu, zikimbieni ibada za sanamu.
”Je, nina maana kwamba kafara iliyotolewa kwa sanamu ni kitu chenye maana yo yote? Au kwamba sanamu ni kitu chenye maana yo yote? La hasha! Lakini kafara za watu wasiomjua Mungu hutolewa kwa mashetani, wala si kwa Mungu. Nami sitaki ninyi mwe na ushirika na mashetani. Hamwezi kunywa katika kikombe cha Bwana na cha mashetani pia. Hamwezi kuwa na sehemu katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani. Je, tunataka kuamsha wivu wa Bwana? Je, sisi tuna nguvu kuliko yeye?
”Mnajua kwamba mlipokuwa hamumjui Mungu, mlishawishika na kupotoshwa na sanamu zisizonena. Kwa hiyo nataka mfahamu ya kuwa hakuna mtu anayeongozwa na Roho wa Mungu anayeweza kusema, “Yesu na alaaniwe.” Pia hakuna mtu awezaye kusema, “Yesu ni Bwana,” isipokuwa ameongozwa na Roho Mtakatifu.
”Kuna mapatano gani kati ya Kristo na Beliari? Yeye aaminiye ana sehemu gani na yeye asiyeamini? Kuna mapatano gani kati ya Hekalu la Mungu na sanamu? Kwa kuwa sisi tu Hekalu la Mungu aliye hai. Kama Mungu alivyosema: “Nitakaa pamoja nao na kutembea katikati yao, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.”
”Watu kama hao ni mitume wa uongo, ni wafanyakazi wadanganyifu, wanaojigeuza waonekane kama mitume wa Kristo. Wala hii si ajabu, kwa kuwa hata Shetani mwenyewe hujigeuza aonekane kama malaika wa nuru.
”Nashangaa kwamba mnamwacha upesi hivyo yeye aliyewaita kwa neema ya Kristo na kuifuata injili nyingine, ambayo kwa kweli si injili kamwe, ila kwa dhahiri kuna watu wanaowachanganya na wanaotaka kuipotosha Injili ya Kristo. Lakini hata ikiwa sisi au malaika atokaye mbinguni akihubiri injili nyingine tofauti na ile tuliyowahubiria sisi, basi mtu huyo alaaniwe milele! Kama vile tulivyokwisha kusema kabla, sasa nasema tena, ikiwa mtu ye yote atawahubiria injili kinyume na ile mliyoipokea na alaaniwe milele!
”Kwa maana kuna Mungu mmoja na mpatanishi mmoja kati ya Mungu na wanadamu, yaani, mwanadamu Kristo Yesu,
”Roho asema waziwazi kwamba katika siku za mwisho baadhi ya watu wataiacha imani na kufuata roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani.
”Kama vile mwanadamu alivyowekewa kufa mara moja tu na baada ya kufa akabili hukumu,
”Unaamini kwamba kuna Mungu mmoja. Vyema! Hata mashetani yanaamini hivyo na kutetemeka.
”Je, mwongo ni nani? Mwongo ni mtu yule asemaye kwamba Yesu si Kristo. Mtu wa namna hiyo ndiye mpinga Kristo, yaani, yeye humkana Baba na Mwana. Hakuna ye yote amkanaye Mwana aliye na Baba. Ye yote anayemkubali Mwana anaye na Baba pia.
”Wapenzi, msiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho mwone kama zimetoka kwa Mungu, kwa sababu manabii wengi wa uongo wametokea ulimwenguni. Hivi ndivyo mnavyoweza kutambua Roho wa Mungu: Kila roho inayokubali kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatoka kwa Mungu. Lakini kila roho ambayo haimkubali Yesu haitoki kwa Mungu. Hii ndiyo roho ya mpinga Kristo, ambayo mmesikia kwamba inakuja na sasa tayari iko ulimwenguni.
”Sisi twatokana na Mungu na ye yote anayemjua Mungu hutusikiliza, lakini asiyetokana na Mungu hatusikilizi. Hivi ndivyo tunavyoweza kutambua Roho wa Kweli na roho ya upotovu.
”Watoto wadogo, jilindeni nafsi zenu na sanamu. Amen.
”Mtu ye yote asiyedumu katika mafundisho ya Kristo, bali akayaacha, yeye hana Mungu. Ye yote anayedumu katika mafundisho ana Baba na Mwana pia. Msimpokee mtu ye yote anayewajia ambaye hawaletei mafundisho haya, wala msimkaribishe nyumbani mwenu. Ye yote amkaribishaye mtu wa namna hiyo anashiriki katika matendo maovu ya mtu huyo.
”Wanadamu waliosalia, ambao hawakuuawa katika mapigo hayo, bado walikataa kutubia kazi za mikono yao na hawakuacha kuabudu mashetani na sanamu za dhahabu, za fedha, za shaba, za mawe na za miti, ambazo haziwezi kuona, kusikia wala kutembea. Wala hawakutubu na kuacha matendo yao ya uuaji, uchawi, uasherati wala wizi wao.
”Lile joka kuu likatupwa chini, yule nyoka wa zamani aitwaye ibilisi au Shetani, aupotoshaye ulimwenguni wote. Akatupwa chini duniani, yeye pamoja na malaika zake.
”Watu wakaliabudu lile joka kwa sababu lilikuwa limempa huyo mnyama mamlaka yake, pia wakamwabudu huyo mnyama na kuuliza, “Ni nani aliye kama huyu mnyama? Ni nani awezaye kupigana vita naye?”
”Akapewa uwezo wa kuipa pumzi ile sanamu ya yule mnyama wa kwanza, ili iweze kusema na kuwasababisha wale wote waliokataa kuiabudu hiyo sanamu kuuawa. Pia alimlazimisha kila mmoja, mdogo na mkubwa, tajiri na maskini, mtu huru na mtumwa, atiwe chapa kwenye mkono wake wa kuume au kwenye kipaji chake cha uso, ili kwamba mtu ye yote asiweze kununua wala kuuza isipokuwa amekuwa na hiyo chapa, ambayo ni jina la huyo mnyama au tarakimu za jina lake. Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na ufahamu na ahesabu tarakimu za huyo mnyama, kwa maana ni tarakimu za kibinadamu. Tarakimu zake ni 666.
”Malaika wa tatu akawafuata hao wawili akisema kwa sauti kubwa, “Kama mtu ye yote anamwabudu huyo mnyama na sanamu yake na kutiwa chapa yake kwenye kipaji chake cha uso au kwenye mkono wake, yeye naye, atakunywa mvinyo wa hasira kali ya Mungu ambayo imemiminwa katika kikombe cha ghadhabu yake pasipo kuchanganywa na maji. Naye atateswa kwa moto uwakao na kiberiti mbele ya malaika watakatifu na mbele za Mwana-Kondoo. Nao moshi wa mateso yao hupanda juu milele na milele. Hakuna mapumziko, mchana wala usiku, kwa wale wamwabuduo huyo mnyama na sanamu yake, au kwa ye yote anayepokea chapa ya jina lake.”
”Huyo mwanamke alikuwa amevaa mavazi ya rangi ya zambarau na nyekundu, akimetameta kwa dhahabu, vito vya thamani na lulu. Mkononi mwake alikuwa ameshika kikombe cha dhahabu kilichojaa mambo ya machukizo na uchafu wa uzinzi wake. Kwenye kipaji chake cha uso palikuwa pameandikwa jina: “SIRI, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA DUNIA.” Nikaona kuwa huyo mwanamke alikuwa amelewa kwa damu ya watakatifu, yaani, damu ya wale watu waliouawa kwa ushuhuda wa Yesu. Nilipomwona huyo mwanamke, nilistaajabu sana.
”Mwanga wa taa hautaangaza ndani yako tena. Sauti ya bwana arusi na bibi arusi kamwe haitasikiwa ndani yako tena. Wafanyabiashara wako walikuwa watu maarufu wa dunia. Mataifa yote yalipotoshwa kwa uchawi wako.
”Lakini waoga, wasioamini, wachafu, wauaji, wazinzi, wachawi, waabudu sanamu, pamoja na waongo wote, mahali pao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.”
”