02 – Mungu
Haya ni maneno matakatifu ya Mungu Mwenyezi.
Hatupendi maneno ya wanadamu.
Kwa mtu yeyote anayempenda Mungu... hivi ndivyo Mungu anasema kuhusu: Mungu.
Haya ni maneno matakatifu ya Mungu Mwenyezi.
Hatupendi maneno ya wanadamu.
Kwa mtu yeyote anayempenda Mungu... hivi ndivyo Mungu anasema kuhusu: Mungu.
“Mimi ni Alfa na Omega,” asema Bwana Mungu, “aliyeko, aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.”
”“Mungu aliyeumba dunia na vyote vilivyomo ndani yake, yeye ndiye Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika mahekalu yaliyojengwa kwa mikono ya wanadamu.
”Wala hakuna kiumbe cho chote kilichofichika machoni pa Mungu. Kila kitu kimefunuliwa na kiko wazi machoni pake yeye ambaye kwake ni lazima tutatoa hesabu.
”Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na dunia.
”Abramu alipokuwa na miaka tisini na tisa, BWANA akamtokea akamwambia, “Mimi ndimi Mungu Mwenyezi; enenda mbele zangu na uishi kwa unyofu.
”Mose akamwambia Mungu, “Ikiwa nitawaendea Waisraeli na kuwaambia, ‘Mungu wa baba zenu amenituma kwenu,’ nao wakiniuliza, ‘Jina lake ni nani?’ Nitawaambia nini?” Mungu akamwambia Mose, “MIMI NIKO AMBAYE NIKO. Hivyo ndivyo utakavyowaambia Waisraeli: ‘MIMI NIKO amenituma kwenu.’ ” Vile vile Mungu akamwambia Mose, “Waambie Waisraeli, ‘BWANA, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaki, na Mungu wa Yakobo amenituma kwenu.’ Hili ndilo Jina langu milele, Jina ambalo mtanikumbuka kwalo kutoka kizazi hadi kizazi.
”BWANA ni nguvu zangu na wimbo wangu; amekuwa wokovu wangu. Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu, Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza. BWANA ni shujaa wa vita; BWANA ndilo jina lake.
”“Mkono wako wa kuume, Ee BWANA ulitukuka kwa uweza. Mkono wako wa kuume, Ee BWANA, ukamponda adui.
”BWANA akapita mbele ya Mose, akitangaza, “BWANA, BWANA, Mungu mwenye huruma na neema, asiye mwepesi wa hasira, mwingi wa upendo na uaminifu, akidumisha upendo kwa maelfu, pia akisamehe uovu, uasi na dhambi. Lakini haachi kuadhibu mwenye hatia; huwaadhibu watoto na watoto wao kwa ajili ya dhambi ya baba zao hata katika kizazi cha tatu na cha nne.”
”Usiabudu mungu mwingine, kwa kuwa BWANA, ambaye jina lake ni Wivu, ni Mungu mwenye wivu.
”Hata hivyo, kwa hakika kama niishivyo, na kwa hakika kama utukufu wa BWANA uijazavyo dunia yote,
”Mungu si mtu, hata aseme uongo, wala yeye si mwanadamu, hata ajute. Je, anasema, kisha asitende? Je, anaahidi, asitimize?
”Kwa kuwa BWANA Mungu wenu ni moto ulao, Mungu mwenye wivu.
”Mlionyeshwa mambo haya ili mpate kujua kuwa BWANA ndiye Mungu; hakuna mwingine ila yeye. Kutoka mbinguni amewasikizisha sauti yake ili kuwaadilisha. Hapa duniani aliwaonyesha moto wake mkubwa, nanyi mlisikia maneno yake kutoka kwenye ule moto.
”Sikia, Ee Israeli: BWANA Mungu wako, ni BWANA mmoja.
”Basi ujue kwamba BWANA Mungu wako ndiye Mungu; ni Mungu mwaminifu, anayetunza Agano la upendo kwa maelfu ya vizazi vya wale wanaompenda na kuzishika amri zake. Lakini kwa wale wanaomchukia atawalipiza kwenye nyuso zao kwa maangamizi; hatachelewa kuwalipiza kwenye nyuso zao wale wamchukiao.
”Kwa kuwa BWANA Mungu wenu ni Mungu wa miungu na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye uweza na wa kutisha, ambaye hana upendeleo na hapokei rushwa.
”Yeye ni Mwamba, kazi zake ni kamilifu, njia zake zote ni haki. Mungu mwaminifu ambaye hakosei, yeye ni mnyofu na mwenye haki.
”Mungu wa milele ni kimbilio lako, na chini kuna mikono ya milele. Atamfukuza adui yako mbele yako, akisema, ‘Mwangamize yeye!’
”“Hakuna ye yote aliye mtakatifu kama BWANA, hakuna mwingine zaidi yako; hakuna Mwamba kama Mungu wetu.
”“Lakini kweli, je, Mungu atafanya makao duniani? Mbingu, hata mbingu zilizo juu sana, haziwezi kukutosha wewe. Sembuse Hekalu hili nililojenga!
”Lakini BWANA akawarehemu na akawahurumia, akaonyesha kujishughulisha nao kwa sababu ya Agano lake na Abrahamu, Isaki na Yakobo. Hadi leo, hajawaangamiza wala kuwafukuza mbele zake.
”Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni Mwema, upendo wake wadumu milele.
”“Nawe Solomoni mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa kujitoa kwa moyo wote na kwa nia ya kumkubali, kwa maana BWANA huuchunguza kila moyo na kujua kila kusudi la kila fikira. Ukimtafuta, ataonekana kwako, bali kama ukimwacha, yeye atakukataa wewe milele.
”Ukuu na uweza, ni vyako, Ee BWANA, na utukufu na enzi na uzuri, kwa kuwa kila kilichoko mbinguni na duniani ni chako wewe. Ee BWANA, ufalme ni wako, umetukuzwa kuwa mkuu juu ya yote. Utajiri na heshima vyatoka kwako, wewe ndiwe utawalaye vitu vyote. Mikononi mwako kuna nguvu na uweza kuinua na kuwapa wote nguvu,
”akasema: “Ee BWANA, Mungu wa baba zetu, si wewe ndiwe uliye Mungu mbinguni? Si wewe ndiwe utawalaye juu ya falme zote za mataifa? Uweza na nguvu viko mkononi mwako, wala hakuna ye yote awezaye kushindana nawe.
”Ee BWANA, Mungu wa Israeli, wewe ni mwenye haki! Leo hii tumeachwa kama mabaki. Tupo hapa mbele zako na hatia yetu, ingawa katika hali hii hakuna hata mmoja wetu anayeweza kusimama mbele zako.”
”Wewe peke yako ndiwe BWANA. Uliumba mbingu, hata mbingu za mbingu, nalo jeshi lote la angani, dunia na vyote vilivyo ndani yake, bahari na vyote vilivyomo ndani yake. Huvipa vitu vyote uhai, nalo jeshi la mbinguni linakuabudu wewe.
”“Je, waweza kujua siri za Mungu? Je, waweza kuyachunguza mambo yote kumhusu Mwenyezi?
”“Ninajua ya kuwa unaweza kufanya mambo yote, wala hakuna mpango wako unaoweza kuzuilika.
”Yeye atawalaye mbinguni hucheka, Bwana huwadharau.
”Mungu ni mwamuzi mwenye haki, Mungu aghadhibikaye kila siku.
”(Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Mahalathi. Zaburi Ya Daudi) Mpumbavu anasema moyoni mwake, “Hakuna Mungu.” Wameharibika, matendo yao ni maovu kabisa; hakuna atendaye mema. Toka mbinguni BWANA anawachungulia wanadamu chini aone kama wako wenye akili, wo wote wanaomtafuta Mungu. Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja; hakuna atendaye mema, naam! Hata mmoja.
”Uonyeshe ajabu ya upendo wako mkuu, wewe uokoaye kwa mkono wako wa kuume wale wanaokukimbilia kutokana na adui zao.
”(Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Daudi) Mbingu zinatangaza utukufu wa Mungu, anga zahubiri kazi ya mikono yake.
”(Zaburi Ya Daudi) BWANA ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu.
”Sauti ya BWANA ina nguvu; sauti ya BWANA ni tukufu.
”Kutoka mbinguni BWANA hutazama chini na kuwaona wanadamu wote; kutoka maskani mwake huwaangalia wote wakaao duniani,
”Waovu hula njama dhidi ya wenye haki na kuwasagia meno, bali Bwana huwacheka waovu, kwa sababu anajua siku yao inakuja.
”Kwa kuwa Mungu ni mfalme wa dunia yote, mwimbieni zaburi za sifa. Mungu anatawala juu ya mataifa, Mungu ameketi juu ya kiti chake cha enzi kitakatifu.
”Usinitupe kutoka mbele zako wala kuniondolea Roho wako Mtakatifu.
”Ee BWANA, unijibu, kwa wema wa upendo wako; kwa huruma zako nyingi unigeukie.
”Jina lake tukufu lisifiwe milele, ulimwengu wote ujae utukufu wake. Amen na Amen.
”Ee BWANA, wewe ni mwema na mwenye kusamehe, umejaa upendo kwa wote wakuitao.
”Ee BWANA, katikati ya miungu hakuna kama wewe, hakuna matendo ya kulinganishwa na yako. Ee BWANA, mataifa yote uliyoyafanya yatakuja na kuabudu mbele zako; wataliletea utukufu jina lako. Kwa maana wewe ni mkuu na unafanya mambo ya ajabu; wewe peke yako ndiwe Mungu.
”Lakini wewe, Ee BWANA, ni Mungu wa huruma na neema, si mwepesi wa hasira, bali ni mwingi wa upendo na uaminifu.
”Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chako cha enzi; upendo na uaminifu vinakutangulia.
”Kabla ya kuzaliwa milima au hujaumba dunia na ulimwengu, wewe ni Mungu tangu milele hata milele.
”Kwa kuwa wewe, Ee BWANA, ndiwe Uliye Juu Sana kuliko dunia yote; umetukuka sana juu ya miungu yote.
”BWANA anatawala, mataifa na yatetemeke; anaketi kwenye kiti cha enzi katikati ya makerubi, dunia na itikisike.
”Mtukuzeni BWANA Mungu wetu na mwabudu kwenye mlima wake mtakatifu, kwa maana BWANA Mungu wetu ni mtakatifu.
”Kwa maana BWANA ni mwema na upendo wake wadumu milele; uaminifu wake unadumu kwa vizazi vyote.
”Hapo mwanzo uliweka misingi ya dunia, na mbingu ni kazi ya mikono yako. Hivi vitatoweka, lakini wewe utadumu, vyote vitachakaa kama vazi. Utavibadilisha kama nguo navyo vitaondoshwa. Lakini wewe, U yeye yule, nayo miaka yako haikomi kamwe.
”BWANA ni mwenye huruma na rehema, si mwepesi wa hasira, amejaa upendo.
”Kama vile mbingu zilivyo juu sana juu ya dunia, ndivyo wema wake ulivyo mwingi kwa wanaomcha; kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, ndivyo Mungu alivyoziweka dhambi zetu mbali nasi.
”Lakini kutoka milele hata milele upendo wa BWANA uko kwa wale wamchao, nayo haki yake kwa watoto wa watoto wao: kwa wale walishikao Agano lake na kukumbuka kuyatii mausia yake. BWANA ameweka imara kiti chake cha enzi mbinguni, ufalme wake unatawala juu ya vyote.
”Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA. Ee BWANA Mungu wangu, wewe ni mkuu sana, umejivika utukufu na enzi. Amejifunika katika nuru kama vile kwa vazi, amezitandaza mbingu kama hema
”Mshukuruni BWANA, kwa kuwa yeye ni mwema, upendo wake wadumu milele.
”BWANA ametukuka juu ya mataifa yote, utukufu wake juu ya mbingu.
”Mungu wetu yuko mbinguni, naye hufanya lo lote limpendezalo.
”BWANA hufanya lo lote apendalo, mbinguni na duniani, katika bahari na vilindi vyake vyote.
”Mshukuruni BWANA, kwa kuwa ni mwema. Fadhili zake zadumu milele.
”Mshukuruni Bwana wa mabwana: Fadhili zake zadumu milele.
”Ambaye kwa ufahamu wake aliziumba mbingu, Fadhili zake zadumu milele.
”Mshukuruni Mungu wa mbinguni, Fadhili zake zadumu milele.
”Niende wapi nijiepushe na Roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako? Kama nikienda juu mbinguni, wewe uko huko; nikifanya vilindi kuwa kitanda changu, wewe uko huko.
”BWANA ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana, ukuu wake haupimiki.
”Watasema juu ya utukufu wa fahari ya ukuu wako, nami nitatafakari juu ya kazi zako za ajabu.
”BWANA ni mwenye neema na mwingi wa huruma, si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa upendo.
”BWANA ni mwenye haki katika njia zake zote na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya. BWANA yu karibu na wote wamwitao, karibu na wote wamwitao kwa uaminifu.
”Muumba wa mbingu na dunia, bahari na vyote vilivyomo ndani yake: BWANA anayedumu kuwa mwaminifu milele na milele. Naye huwapatia haki walioonewa na kuwapa wenye njaa chakula. BWANA huwaweka wafungwa huru,
”Huzihesabu nyota na huipa kila moja jina lake. Bwana wetu ni mkuu na mwenye uwezo mwingi, ufahamu wake hauna kikomo.
”Nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.
”Macho ya BWANA yako kila mahali, yakiwaangalia waovu na wema.
”Ni nani ameshapanda mbinguni na kushuka? Ni nani ameshakusanya upepo kwenye vitanga vya mikono yake? Ni nani ameshafungia maji kwenye nguo yake? Ni nani ameimarisha miisho yote ya dunia? Jina lake ni nani na mwanawe anaitwa nani? Niambie kama unajua!
”Ingieni kwenye miamba, jificheni ardhini kutokana na utisho wa BWANA na utukufu wa enzi yake!
”Nao walikuwa wakiitana kila mmoja na mwenzake: “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu ni BWANA Mwenye Nguvu Zote; dunia yote imejaa utukufu wake.”
”BWANA Mwenye Nguvu Zote ndiye peke yake ikupasaye kumheshimu kuwa mtakatifu, ndiye peke yake utakayemwogopa, ndiye peke yake utakayemhofu,
”Kwa maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume, nao utawala utakuwa mabegani mwake. Naye ataitwa Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani.
”Roho wa BWANA atakaa juu yake, Roho wa hekima na wa ufahamu, Roho wa shauri na uweza, Roho wa maarifa na wa kumcha BWANA
”Hata hivyo BWANA anatamani kutupatia neema, anainuka ili kuwaonyesha huruma. Kwa kuwa BWANA ni Mungu wa haki. Wamebarikiwa wote wanaomngojea yeye!
”Kwa kuwa BWANA ni mwamuzi wetu, BWANA ndiye mtoa sheria wetu, BWANA ni mfalme wetu, yeye ndiye atakayetuokoa.
”Mbele yake mataifa yote ni kama si kitu, yanaonekana yasio na thamani na zaidi ya bure kabisa. Basi, utamlinganisha Mungu na nani? Utamlinganisha na kitu gani?
”Anakaa kwenye kiti cha enzi juu ya duara ya dunia, nao watu wakaao ndani yake ni kama panzi. Huzitandaza mbingu kama chandarua na kuzitandaza kama hema la kuishi.
”Je wewe, hufahamu? Je wewe, hujasikia? BWANA ni Mungu wa milele, Muumba wa miisho ya dunia. Hatachoka wala kulegea, wala hakuna hata mmoja awezaye kuupima ufahamu wake.
”“Mimi ndimi BWANA; hilo ndilo Jina langu! Sitampa mwingine utukufu wangu wala sanamu sifa zangu.
”“Ninyi ni mashahidi wangu,” asema BWANA, “na mtumishi wangu niliyemchagua, ili mpate kunijua na kuniamini na kutambua kwamba Mimi ndiye. Kabla yangu hakuna mungu aliyefanyizwa, wala hatakuwepo mwingine baada yangu. Mimi, naam mimi, ndimi BWANA, zaidi yangu hakuna mwokozi.
”“Hili ndilo asemalo BWANA, Mfalme wa Israeli na Mkombozi, BWANA Mwenye Nguvu Zote: Mimi ni wa kwanza na Mimi ni wa mwisho; zaidi yangu hakuna Mungu.
”“Hili ndilo asemalo BWANA, Mkombozi wako, aliyekuumba tumboni: “Mimi ni BWANA, yeye aliyeumba vitu vyote, yeye peke yake aliyezitanda mbingu, yeye aliyeitandaza nchi mwenyewe,
”ili kwamba kutoka maawio ya jua mpaka machweo yake, watu wapate kujua kwamba hakuna Mungu mwingine ila Mimi. Mimi ndimi BWANA wala hakuna mwingine. Mimi ninaumba nuru na kuhuluku giza, ninaleta mafanikio na kusababisha maafa, Mimi, BWANA, hufanya vitu hivi vyote.
”Kwa kuwa hili ndilo asemalo BWANA, yeye aliyeumba mbingu, ndiye Mungu; yeye aliyeifanya dunia na kuiumba, yeye ndiye aliyeiwekea misingi imara, hakuiumba ili iwe tupu, bali aliiumba ikaliwe na viumbe vyake, anasema: “Mimi ndimi BWANA, wala hakuna mwingine.
”Tangazeni lile litakalokuwapo, lisemeni hilo, wao na wafanye shauri pamoja. Ni nani aliyetangulia kusema hili tangu zamani, aliyetangaza tangu zamani za kale? Je, haikuwa Mimi, BWANA? Wala hapana Mungu mwingine zaidi yangu mimi, Mungu mwenye haki na Mwokozi; hapana mwingine ila mimi. “Nigeukieni mimi nanyi mkaokolewe, enyi miisho yote ya dunia; kwa maana mimi ndimi Mungu, wala hapana mwingine.
”Kumbukeni mambo yaliyopita, yale ya zamani za kale; mimi ndimi Mungu, wala hakuna mwingine; mimi ndimi Mungu, wala hakuna mwingine aliye kama mimi. Ni mimi tangazaye mwisho tangu mwanzo, naam, tangu zamani za kale, mambo ambayo hayajatendeka. Ninasema: Kusudi langu ndilo litakalosimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote.
”Kwa maana Muumba wako ndiye mume wako, BWANA Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli ni Mkombozi wako, yeye anaitwa Mungu wa dunia yote.
”“Kwa kuwa mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu,” asema BWANA. “Kama vile mbingu zilivyo juu kuliko dunia, ndivyo njia zangu zilivyo juu kuliko njia zenu na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.
”Kwa maana hili ndilo asemalo Aliye juu, yeye aliyeinuliwa sana, yeye aishiye milele, ambaye jina lake ni Mtakatifu: “Ninaishi mimi mahali palipoinuka tena palipo patakatifu, tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na mwenye roho ya unyenyekevu, ili kuzihuisha roho za wanyenyekevu na kuihuisha mioyo yao waliotubu.
”Hili ndilo asemalo BWANA, “Mbingu ni kiti changu cha enzi, nayo dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu. Iko wapi nyumba mtakayojenga kwa ajili yangu? Mahali pangu pa kupumzika patakuwa wapi?
”Lakini BWANA ni Mungu wa kweli, yeye ndiye Mungu aliye hai, Mfalme wa milele. Akiwa amekasirika, dunia hutetemeka, mataifa hayawezi kustahimili hasira yake.
”Lakini Mungu aliiumba dunia kwa uweza wake, akaufanya ulimwengu kwa hekima yake na kwa ufahamu wake akazitandaza mbingu.
”“Kwa hiyo nitawafundisha: wakati huu nitawafundisha nguvu zangu na uwezo wangu. Ndipo watakapojua kuwa Jina langu ndimi BWANA.
”Je, mtu ye yote aweza kujificha mahali pa siri ili nisiweze kumwona?” BWANA asema. “Je, mimi sikuijaza mbingu na nchi?” BWANA asema.
”BWANA alitutokea wakati uliopita akisema: “Nimekupenda kwa upendo wa milele, nimekuvuta kwa wema.
”Mtu hatamfundisha tena jirani yake, au mtu kumfundisha ndugu yake akisema, ‘Umjue BWANA Mungu,’ kwa sababu wote watanijua mimi, kuanzia aliye mdogo kabisa kwao hata aliye mkuu sana,” asema BWANA. “Kwa sababu nitausamehe uovu wao na sitazikumbuka dhambi zao tena.”
”“Ee BWANA Mwenyezi, umeumba mbingu na nchi kwa uwezo wako mkuu na kwa mkono ulionyooshwa. Hakuna jambo lililo gumu usiloliweza. Huonyesha upendo kwa maelfu lakini huleta adhabu kwa ajili ya dhambi za baba mapajani mwa watoto wao baada yao. Ee Mungu mkuu na mwenye uweza, ambaye jina lako ni BWANA Mwenye Nguvu Zote,
”“Mimi ndimi BWANA, Mungu wa wote wenye mwili, Je, kuna jambo lo lote lililo gumu nisiloliweza?
”na akasema: “Lihimidiwe jina la Mungu milele na milele, hekima na uweza ni vyake. Yeye hubadili nyakati na majira, huwaweka wafalme na kuwaondoa. Huwapa hekima wenye hekima na maarifa wenye ufahamu. Hufunua siri na mambo yaliyofichika, anajua yale yaliyo gizani, nuru hukaa kwake.
”Nitakuposa uwe wangu milele; nitakuposa kwa uadilifu na haki, kwa upendo na huruma.
”BWANA Mungu Mwenye Nguvu Zote, BWANA ndilo jina lake!
”Yeye ambaye hufanya milima, anaumba upepo, na kufunua mawazo yake kwa mwanadamu, yeye ageuzaye asubuhi kuwa giza, na kukanyaga mahali pa juu pa nchi: BWANA Mungu Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake.
”BWANA ni mwenye wivu na Mungu mlipiza kisasi; BWANA hulipiza kisasi na amejaa ghadhabu. BWANA hulipiza kisasi juu ya watesi wake, naye anadumisha ghadhabu yake dhidi ya adui zake. BWANA si mwepesi wa hasira naye ni mwenye nguvu, BWANA hataacha kuadhibu wenye hatia. Njia yake ipo katika kisulisuli na tufani, na mawingu ni vumbi la miguu yake.
”Kwa kuwa dunia itajazwa na maarifa ya utukufu wa BWANA, kama maji yaifunikavyo bahari.
”BWANA Mungu wako yu pamoja nawe, yeye ni mwenye nguvu kuokoa. Atakufurahia kwa furaha kubwa, atakutuliza kwa pendo lake, atakufurahia kwa kuimba.”
”Lakini mimi nawaambia, Msiape kabisa, ama kwa mbingu, kwa kuwa ni kiti cha enzi cha Mungu, au kwa nchi, kwa kuwa ndipo mahali pake pa kuwekea miguu, au kwa Yerusalemu, kwa kuwa ndio mji wa Mfalme Mkuu.
”Kwa hiyo iweni wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.
”“Hivi basi, ndivyo iwapasavyo kuomba: “ ‘Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe.
”Usitutie majaribuni, bali utuokoe kutoka kwa yule mwovu [kwa kuwa Ufalme ni wako na nguvu na utukufu, hata milele. Amen].’
”Wakati huo Yesu alisema, “Ninakuhimidi Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa umewaficha mambo haya wenye hekima na wenye elimu, nawe ukawafunulia watoto wachanga.
”Lakini Yesu akawatazama, akawaambia, “Kwa mwanadamu jambo hili haliwezekani, lakini kwa Mungu mambo yote yanawezekana.”
”‘Mimi ni Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaki, na Mungu wa Yakobo?’ Yeye si Mungu wa wafu bali ni Mungu wa walio hai.”
”“Mwana wa Adamu atakapokuja katika utukufu wake na malaika wote watakatifu pamoja naye, ndipo atakapoketi juu ya kiti cha enzi cha utukufu wake. Mataifa yote watakusanyika mbele zake, naye atawatenga kama mchungaji anavyotenga kondoo na mbuzi.
”Yesu akawajia na kusema, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Kwa sababu hii, enendeni ulimwenguni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu,
”Yesu akawatazama, akawaambia, “Kwa mwanadamu hili haliwezekani, lakini kwa Mungu sivyo. Yote kwa Mungu yanawezekana.”
”Yesu akajibu, “Amri iliyo kuu ndiyo hii, ‘Sikia Ee Israeli, Bwana Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja.
”Yesu akajibu, “Mimi ndimi, nanyi mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa Mwenye Nguvu, akija na mawingu ya mbinguni.”
”Yesu, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, akarudi kutoka Yordani akaongozwa na Roho Mtakatifu hadi jangwani,
”Iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma.
”Saa ile ile, Yesu akashangilia katika Roho Mtakatifu akasema, “Nakushukuru Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa sababu mambo haya umewaficha wenye hekima na wenye akili, nawe umewafunulia watoto wadogo. Naam, Baba, kwa kuwa hayo ndiyo yaliyokuwa mapenzi yako.
”Akawaambia, “Mnapoomba, semeni hivi: “ ‘Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje.
”Hapo mwanzo alikuwako Neno, huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Tangu mwanzo huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu. Vitu vyote viliumbwa kwa yeye, wala pasipo yeye hakuna cho chote kilichoumbwa ambacho kimeumbwa.
”“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
”Baba anampenda Mwana, naye ametia vitu vyote mikononi mwake.
”Mungu ni Roho na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.”
”Yesu akawaambia, “Mimi ndimi mkate wa uzima. Yeye ajaye kwangu, hataona njaa kamwe na yeye aniaminiye, hataona kiu kamwe.
”Mimi ni mkate wa uzima.
”Mimi ni mkate wa uzima ule uliotoka mbinguni. Mtu ye yote akiula mkate huu, ataishi milele. Mkate huu ni mwili wangu, ambao nitautoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.”
”Kisha Yesu akasema nao tena akawaambia, “Mimi ni nuru ya ulimwengu. Mtu ye yote akinifuata hatatembea gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.”
”Mimi najishuhudia mwenyewe, naye Baba aliyenituma hunishuhudia.”
”Akawaambia, “Ninyi mmetoka chini, mimi nimetoka juu. Ninyi ni wa ulimwengu huu, mimi si wa ulimwengu huu.
”Yesu akawaambia, “Amin, amin nawaambia, kabla Abrahamu hajakuwako, ‘Mimi niko.’ ”
”“Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo.
”Yesu akamwambia, “Mimi ndiye huo ufufuo na uzima. Yeye aniaminiye mimi, hata akifa atakuwa anaishi
”Yesu akawaambia, “Mimi ndimi njia na kweli na uzima. Mtu hawezi kuja kwa Baba isipokuwa kwa kupitia kwangu. Kama mngenijua mimi, mngemjua na Baba pia. Tangu sasa, mnamjua Baba yangu, tena mmemwona.”
”Lakini huyo Msaidizi, yaani, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwenu kwa Jina langu, atawafundisha mambo yote na kuwakumbusha yote niliyowaambia.
”Hakuna mtu mwenye upendo mkuu kuliko huu, mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.
”Yesu alipowaambia, “Mimi ndiye,” walirudi nyuma na kuanguka chini!
”Kisha wakaomba, wakasema, “Bwana, wewe waujua moyo wa kila mtu. Tuonyeshe ni yupi kati ya hawa wawili uliyemchagua
”“Hata hivyo, Yeye Aliye Juu Sana hakai kwenye nyumba zilizojengwa kwa mikono ya wanadamu. Kama nabii alivyosema: “ ‘Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu. Mtanijengea nyumba ya namna gani? asema Bwana. Au mahali pangu pa kupumzikia patakuwa wapi?
”“Mungu aliyeumba dunia na vyote vilivyomo ndani yake, yeye ndiye Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika mahekalu yaliyojengwa kwa mikono ya wanadamu.
”Ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni dhidi ya uasi wote na uovu wa wanadamu ambao huipinga kweli kwa uovu wao, kwa maana yote yanayoweza kujulikana kumhusu Mungu ni dhahiri kwao, kwa sababu Mungu mwenyewe ameliweka wazi kwao. Kwa maana tangu kuumbwa kwa ulimwengu, asili ya Mungu asiyeonekana kwa macho, yaani, uweza wake wa milele na asili yake ya Uungu, umeonekana waziwazi ukitambuliwa kutokana na yale aliyoyafanya ili wanadamu wasiwe na udhuru.
”Lakini Mungu anaudhihirisha upendo wake kwetu kwamba: Tulipokuwa tungali wenye dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yetu.
”Kwa maana nimekwisha kujua kwa hakika ya kuwa wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuja, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kingine cho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.
”Tazama jinsi kilivyo kina cha utajiri wa hekima na maarifa ya Mungu! Tazama jinsi ambavyo hukumu zake hazichunguziki, na ambavyo njia zake zisivyotafutikana! “Ni nani aliyeijua nia ya Bwana? Au ni nani ambaye amekuwa mshauri wake?” “Au ni nani aliyempa cho chote ili arudishiwe?” Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake, viko kwake na kwa ajili yake. Utukufu ni wake milele! Amen.
”ili imani yenu isiwe imejengwa katika hekima ya wanadamu bali katika nguvu za Mungu.
”Kwa kuwa Ufalme wa Mungu si maneno matupu tu bali ni nguvu.
”Lakini kwetu sisi yuko Mungu mmoja, aliye Baba, ambaye vitu vyote vyatoka kwake na kwa ajili yake sisi twaishi na kuna Bwana mmoja tu, Yesu Kristo, ambaye kwa yeye vitu vyote vimekuwepo na kwa yeye sisi tunaishi.
”ambayo aliitumia alipomfufua Kristo kutoka kwa wafu, akamketisha mkono wake wa kuume katika mbingu, juu sana kuliko falme zote na mamlaka, enzi na milki na juu ya kila jina litajwalo, si katika ulimwengu huu tu, bali na katika ule ujao pia. Naye Mungu ameweka vitu vyote viwe chini ya miguu yake na amemfanya yeye awe kichwa cha vitu vyote kwa ajili ya Kanisa, ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake yeye aliye yote katika yote.
”Lakini Mungu kwa upendo wake mwingi kwetu sisi, ambaye ni mwingi wa rehema,
”Kwa maana kwa kupitia kwake, sisi sote tunaweza kumkaribia Baba katika Roho mmoja.
”Mungu mmoja ambaye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote, katika yote na ndani ya yote.
”Wala msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu, ambaye kwa huyo mlitiwa muhuri kwa ajili ya siku ya ukombozi.
”Kwa hiyo, Mungu alimtukuza juu sana na kumpa Jina lililo kuu kuliko kila jina, ili kwa Jina la Yesu, kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, vya duniani na vya chini ya nchi, na kila ulimi ukiri ya kwamba YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.
”Yeye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. Kwa yeye vitu vyote vilivyoko mbinguni na juu ya nchi viliumbwa, vile vitu vinavyoonekana na vile visivyoonekana, kama ni viti vya enzi au falme, au wenye mamlaka au watawala, vitu vyote viliumbwa na yeye na kwa ajili yake. Yeye alikuwapo kabla ya vitu vyote na katika yeye vitu vyote vinashikamana pamoja. Yeye ndiye kichwa cha mwili, yaani, Kanisa, naye ni wa mwanzo na mzaliwa wa kwanza kutoka kwa wafu, ili yeye awe mkuu katika vitu vyote. Kwa kuwa ilimpendeza Mungu kwamba ukamilifu wake wote wa Kiungu uwe ndani yake
”Maana ukamilifu wote wa Uungu umo ndani ya Kristo katika umbile la mwili wa kibinadamu, nanyi mmepewa ukamilifu ndani ya Kristo, ambaye yeye ndiye mkuu juu ya kila enzi na kila mamlaka.
”Basi, Mfalme wa milele, asiye na mwisho, asiyeonekana, aliye Mungu pekee, apewe heshima na utukufu milele na milele. Amen.
”Yeye peke yake hapatikani na mauti, ambaye anakaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa, ambaye hakuna mwanadamu aliyemwona wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye milele. Amen.
”Zamani Mungu alisema na baba zetu kwa njia ya manabii mara nyingi na kwa njia mbalimbali, lakini katika siku hizi za mwisho anasema nasi kwa njia ya Mwanawe, ambaye amemweka kuwa mrithi wa vitu vyote, na ambaye kwa yeye aliuumba ulimwengu. Mwana ni mng'ao wa utukufu wa Mungu na mfano halisi wa nafsi yake, akivihifadhi vitu vyote kwa neno lake lenye uweza. Akiisha kufanya utakaso kwa ajili ya dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko mbinguni.
”Lakini kwa habari za Mwana asema, “Kiti chako cha enzi, Ee Mungu, kitadumu milele na milele, nayo haki itakuwa fimbo ya utawala ya ufalme wako.
”Wala hakuna kiumbe cho chote kilichofichika machoni pa Mungu. Kila kitu kimefunuliwa na kiko wazi machoni pake yeye ambaye kwake ni lazima tutatoa hesabu.
”kwa kuwa “Mungu wetu ni moto ulao.”
”Yesu Kristo ni yeye yule jana, leo na hata milele.
”Kila kitolewacho kilicho chema na kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kutoka kwa Baba wa mianga, ambaye kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.
”Unaamini kwamba kuna Mungu mmoja. Vyema! Hata mashetani yanaamini hivyo na kutetemeka.
”ambaye ameingia mbinguni na amekaa mkono wa kuume wa Mungu: pamoja na malaika, mamlaka na nguvu zote vikiwa vimetiishwa chini yake.
”Maana alipewa heshima na utukufu kutoka kwa Mungu Baba, sauti ilipomjia katika Utukufu Mkuu ikisema, “Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.”
”Huu ndio ujumbe tuliosikia kutoka kwake na kuwatangazia ninyi: kwamba Mungu ni nuru na ndani yake hamna giza lo lote.
”Yeye asiyependa hamjui Mungu, kwa sababu Mungu ni pendo.
”Hivyo nasi twajua na kulitumainia pendo la Mungu alilo nalo kwa ajili yetu. Mungu ni Upendo. Kila akaaye katika upendo hukaa ndani ya Mungu na Mungu hukaa ndani yake.
”Kwa maana wako watatu washuhudiao [mbinguni: hao ni Baba, Neno na Roho Mtakatifu. Hawa watatu ni wamoja. Pia wako mashahidi watatu duniani], yaani Roho, Maji na Damu; wote hawa watatu wanakubaliana katika umoja.
”Nasi pia twajua ya kwamba Mwana wa Mungu amekuja, naye ametupa sisi ufahamu ili tupate kumjua yeye aliye Kweli. Nasi tumo ndani yake yeye aliye Kweli, yaani, ndani ya Yesu Kristo Mwanawe. Yeye ndiye Mungu wa kweli na uzima wa milele.
”kwake yeye Mungu pekee Mwokozi wetu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu, utukufu, ukuu, uweza na mamlaka vina yeye tangu milele, sasa na hata milele! Amen.
”“Mimi ni Alfa na Omega,” asema Bwana Mungu, “aliyeko, aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.”
”“Kwa malaika wa Kanisa lililoko Sardi andika: “Haya ndiyo maneno yake yeye aliye na zile Roho saba za Mungu na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, kwamba una sifa ya kuwa hai, lakini umekufa.
”Ghafula nilikuwa katika Roho, hapo mbele yangu kilikuwapo kiti cha enzi mbinguni, kikiwa kimekaliwa na mtu mmoja. Yeye aliyekuwa amekikalia alikuwa anaonekana kama yaspi na akiki. Kukizunguka kile kiti cha enzi palikuwa na upinde wa mvua ulioonekana kama zumaridi. Pia kukizunguka hicho kiti cha enzi palikuwa na viti ishirini na vinne na juu ya hivyo viti walikuwa wameketi wazee ishirini na wanne, waliovaa majoho meupe, wakiwa na taji za dhahabu vichwani mwao. Kwenye kile kiti cha enzi palikuwa panatoka miali ya umeme wa radi, ngurumo na sauti za radi. Mbele ya hicho kiti cha enzi, palikuwa na taa saba zilizokuwa zinawaka. Hizi ndizo Roho saba za Mungu. Pia mbele ya hicho kiti cha enzi palikuwa na kile kilichoonekana kama bahari ya kioo, iliyokuwa angavu kama jiwe lisilo na rangi yo yote ling'aalo sana. Katikati, kukizunguka kile kiti cha enzi, kulikuwa na viumbe wanne wenye uhai, wakiwa wamejawa na macho mbele na nyuma. Huyo kiumbe wa kwanza mwenye uhai alikuwa kama simba, wa pili alikuwa kama ng'ombe dume, wa tatu alikuwa na uso kama wa mwanadamu na wa nne alikuwa kama tai anayeruka. Kila mmoja wa hawa viumbe wenye uhai wanne, alikuwa na mabawa sita na kujawa na macho pande zote, hadi chini ya mabawa. Usiku na mchana hawakuacha kusema: “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni BWANA Mungu Mwenyezi, aliyekuwako, aliyeko na atakayekuja.” Kila mara viumbe hao wenye uhai wanne walipomtukuza, kumheshimu na kumshukuru yeye aliyeketi kwenye kile kiti cha enzi, tena aishiye milele na milele, wale wazee ishirini na wanne huanguka mbele zake yeye aliyeketi kwenye kile kiti cha enzi na kumwabudu yeye aliye hai milele na milele. Wao huziweka taji zao mbele ya hicho kiti cha enzi, wakisema: “Bwana wetu na Mungu wetu, wewe umestahili kupokea utukufu na heshima na uweza, kwa maana ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa mapenzi yako viliumbwa na vimekuwako.”
”Ndipo nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale viumbe wenye uhai wanne na miongoni mwa wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, akiwa kama amechinjwa. Alikuwa na pembe saba na macho saba, ambazo ndizo zile Roho saba za Mungu zilizotumwa duniani pote.
”Kisha nikasikia kila kiumbe mbinguni na duniani, chini ya nchi na baharini na vyote vilivyomo ndani yake vikiimba: “Sifa na heshima na utukufu na uweza ni vyake yeye aketiye juu ya hicho kiti cha enzi na kwa Mwana-Kondoo, milele na milele!”
”Akasema kwa sauti kubwa, “Mcheni Mungu na kumpa utukufu, kwa maana saa ya hukumu yake imewadia. Mwabuduni yeye aliyeziumba mbingu, dunia, bahari na chemchemi za maji.”
”Kisha nikasikia sauti kama ya umati mkubwa, kama sauti ya maji mengi yaendayo kasi na kama ngurumo kubwa ya radi wakipiga kelele wakisema: “Haleluya! Kwa maana BWANA Mungu wetu Mwenyezi anatawala.
”Kwenye joho lake na paja lake liliandikwa jina hili: MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA.
”Sikuona Hekalu ndani ya huo mji kwa sababu BWANA Mungu Mwenyezi na Mwana-Kondoo ndio Hekalu lake. Ule mji hauhitaji jua wala mwezi kuuangazia, kwa sababu utukufu wa Mungu ndio nuru yake na Mwana-Kondoo ndiye taa yake.
”Mimi ni Alfa na Omega, wa Kwanza na wa Mwisho, Mwanzo na Mwisho.
”