03 – Wanadamu
Haya ni maneno matakatifu ya Mungu Mwenyezi.
Hatupendi maneno ya wanadamu.
Kwa mtu yeyote anayempenda Mungu... hivi ndivyo Mungu anasema kuhusu: Wanadamu.
Haya ni maneno matakatifu ya Mungu Mwenyezi.
Hatupendi maneno ya wanadamu.
Kwa mtu yeyote anayempenda Mungu... hivi ndivyo Mungu anasema kuhusu: Wanadamu.
Kwa maana wewe ndiwe uliyeumba utu wangu wa ndani; uliniunga pamoja tumboni mwa mama yangu. Ninakusifu kwa sababu nimeumbwa kwa namna ya ajabu na ya kutisha; kazi zako ni za ajabu, ninajua hayo kikamilifu.
”Wala hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume wala mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu.
”Wakati huu dunia ilikuwa imejaa uharibifu na jeuri machoni pa Mungu. Mungu akaona jinsi dunia ilivyoharibika, kwa maana watu wote duniani walikuwa wameharibu njia zao.
”Ndipo Mungu akasema, “Tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu, wakatawale juu ya samaki wa baharini na ndege wa angani, juu ya mifugo, juu ya dunia yote, na juu ya viumbe wote watambaao juu ya nchi.” Kwa hiyo Mungu alimuumba mtu kwa mfano wake mwenyewe, kwa mfano wa Mungu alimuumba; mwanaume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabariki na akawaambia, “Zaeni na mkaongezeke, mkaijaze tena dunia na kuitiisha. Mkatawale samaki wa baharini, ndege wa angani na kila kiumbe hai kiendacho juu ya ardhi.” Kisha Mungu akasema, “Nimewapa kila mche utoao mbegu juu ya uso wa dunia yote na kila mti wenye matunda yenye mbegu ndani yake. Vitakuwa kwa ajili ya chakula chenu, cha wanyama wote wa dunia, ndege wote wa angani na viumbe vyote viendavyo juu ya ardhi. Kila kiumbe chenye pumzi ya uhai, ninawapa kila mche wa kijani kuwa chakula.” Ikawa hivyo.
”BWANA Mungu alimuumba mtu kutoka mavumbi ya ardhi, akampulizia pumzi ya uhai puani mwake, mtu akawa kiumbe hai.
”BWANA Mungu akasema, “Si vyema huyu mtu awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kumfaa.”
”Huyo mwanaume akasema, “Huyu sasa ni mfupa wa mifupa yangu na nyama ya nyama yangu, ataitwa ‘mwanamke,’ kwa kuwa alitolewa katika mwanaume.” Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja. Adamu na mkewe wote wawili walikuwa uchi, wala hawakuona aibu.
”Kwa jasho la uso wako utakula chakula chako hadi utakaporudi ardhini, kwa kuwa ulitwaliwa kutoka humo, kwa kuwa wewe u mavumbi na mavumbini wewe utarudi.”
”Hii ni orodha iliyoandikwa ya vizazi vya Adamu. Wakati Mungu alipomuumba Adamu, alimfanya kwa sura ya Mungu. Aliwaumba mwanaume na mwanamke, akawabariki. Walipokwisha kuumbwa akawaita “Mwanadamu.”
”Ndipo BWANA akasema, “Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye ni wa kufa, siku zake zitakuwa miaka 120.”
”BWANA akaona jinsi ambavyo uovu wa mwanadamu umekuwa mkubwa duniani na ya kuwa kila mwelekeo wa mawazo ya moyo wake wakati wote ulikuwa mbaya tu. BWANA akasikitika kwamba alimuumba mwanadamu duniani, moyo wa Mungu ukajaa masikitiko.
”Wakati huu dunia ilikuwa imejaa uharibifu na jeuri machoni pa Mungu. Mungu akaona jinsi dunia ilivyoharibika, kwa maana watu wote duniani walikuwa wameharibu njia zao.
”BWANA akasikia harufu nzuri ya kupendeza, naye akasema moyoni mwake, “Kamwe sitailaani tena ardhi kwa sababu ya mwanadamu, hata ingawaje kila mwelekeo wa moyo wake ni mbaya tangu ujana. Kamwe sitaangamiza tena viumbe hai vyote kama nilivyofanya.”
”Kwa kuwa uhai wa kiumbe uko ndani ya damu, nami nimewapa hiyo damu ili mfanyie upatanisho kwa ajili yenu wenyewe juu ya madhabahu; damu ndiyo ifanyayo upatanisho kwa ajili ya maisha ya mtu.
”“BWANA huua na huleta uhai, hushusha chini mpaka kaburini na kufufua.
”Lakini BWANA akamwambia Samweli, “Usitazame sura yake wala kimo chake, kwa kuwa nimemkataa. BWANA hatazami katika vile vitu mwanadamu avitazamavyo. Mwanadamu hutazama katika sura ya nje, lakini BWANA hutazama moyoni.”
”na kusema: “Nilitoka tumboni mwa mama yangu uchi, nami nitaondoka uchi, BWANA alinipa, naye BWANA ameviondoa, jina la BWANA litukuzwe.”
”Kama Mungu hawaamini watumishi wake, kama yeye huwalaumu malaika zake kwa kukosea, ni mara ngapi zaidi wale waishio katika nyumba za udongo wa mfinyanzi, ambazo misingi yake ipo mavumbini, ambao wamepondwa kama nondo!
”kwa kuwa sisi tumezaliwa jana tu na hatujui lo lote, nazo siku zetu duniani ni kama kivuli tu.
”“Mikono yako ndiyo iliyoniumba na kunifanya. Je, sasa utageuka na kuniangamiza? Kumbuka kuwa ulinifinyanga kama udongo wa mfinyanzi. Je, sasa utanifanya kuwa mavumbi tena? Je, wewe hukunimimina mimi kama maziwa na kunigandisha kama jibini, ukanivika ngozi na nyama na kuniunga pamoja kwa mifupa na mishipa? Umenipa uhai na kunitendea wema, katika uangalizi wako umeilinda roho yangu.
”Mkononi mwake uko uhai wa kila kiumbe na pumzi ya wanadamu wote.
”“Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake ni chache nazo zimejaa taabu. Huchanua kama ua kisha hunyauka, huwa kama kivuli kipitacho upesi, wala hadumu.
”Siku za mwanadamu zimewekewa mpaka, umekwisha kutangaza idadi ya miezi yake na kuweka mpaka ambao hawezi kuuvuka.
”sembuse mwanadamu ambaye ni mwovu na mpotovu, ambaye hunywa uovu kama anywavyo maji!
”“Ni miaka michache tu itapita kabla sijaenda safari ambayo sitarudi.
”sembuse mtu ambaye ni funza, mwanadamu ambaye ni buu tu!”
”kwa muda wote nitakaokuwa na uhai ndani yangu, nayo pumzi ya Mungu ikiwa puani mwangu, midomo yangu haitanena uovu, wala ulimi wangu hautatamka udanganyifu.
”Roho wa Mungu ameniumba, pumzi ya Mwenyezi hunipa uhai.
”mwanadamu ni kitu gani hata umkumbuke, binadamu hata umwangalie?
”Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu, umemvika taji ya utukufu na heshima. Umemfanya mtawala juu ya kazi za mikono yako; umevitia vitu vyote chini ya miguu yake. Kondoo, mbuzi na ng'ombe wote pia, naam, na wanyama wa kondeni, ndege wa angani na samaki wa baharini, naam, kila kiogeleacho katika njia za bahari.
”(Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Mahalathi. Zaburi Ya Daudi) Mpumbavu anasema moyoni mwake, “Hakuna Mungu.” Wameharibika, matendo yao ni maovu kabisa; hakuna atendaye mema. Toka mbinguni BWANA anawachungulia wanadamu chini aone kama wako wenye akili, wo wote wanaomtafuta Mungu. Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja; hakuna atendaye mema, naam! Hata mmoja.
”(Zaburi Ya Daudi) Dunia ni mali ya BWANA, pamoja na vyote vilivyomo ndani yake, ulimwengu na wote waishio ndani yake, maana aliiwekea misingi yake baharini na kuifanya imara juu ya maji.
”Kutoka mbinguni BWANA hutazama chini na kuwaona wanadamu wote; kutoka maskani mwake huwaangalia wote wakaao duniani, yeye ambaye huumba mioyo yao wote, ambaye huangalia kila kitu wanachokitenda.
”“Ee BWANA, nijulishe mwisho wa maisha yangu na hesabu ya siku zangu; nijalie kujua jinsi maisha yangu yanavyopita upesi. Umefanya maisha yangu mafupi kama pumzi; muda wangu wa kuishi ni kama hauna thamani kwako. Maisha ya kila mwanadamu ni kama pumzi.
”Unakemea na kuadhibu wanadamu kwa ajili ya dhambi zao; unaharibu utajiri wao kama nondo aharibuvyo: kila mwanadamu ni kama pumzi tu.
”Hakika mimi nilizaliwa mwenye dhambi, mwenye dhambi tangu nilipotungwa mimba kwa mama yangu.
”Bali dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika, moyo uliovunjika wenye toba, Ee Mungu, hutaudharau.
”(Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Mahalathi. Utenzi Wa Daudi) Mpumbavu anasema moyoni mwake, “Hakuna Mungu.” Wameharibika, na njia zao ni za uovu kabisa, hakuna hata mmoja atendaye mema. Mungu huwachungulia wanadamu chini kutoka mbinguni aone kama wako wenye akili, wo wote wanaomtafuta Mungu. Kila mmoja amegeukia mbali, wameharibika wote pamoja, hakuna hata mmoja atendaye mema, naam! Hata mmoja.
”Alikumbuka kwamba wao walikuwa nyama tu, upepo upitao ambao haurudi.
”Kumbuka jinsi maisha yangu yanavyopita haraka. Ni ubatili kiasi gani umemuumba mwanadamu! Ni mtu gani awezaye kuishi na asione kifo, au kujiokoa mwenyewe kutoka nguvu za kaburi?
”Siku zetu za kuishi ni miaka sabini, ikiwa tuna nguvu ni miaka themanini, lakini yote ni ya shida na taabu, nazo zapita haraka, nasi twatoweka.
”Tufundishe kuzihesabu siku zetu vizuri, ili tujipatie moyo wa hekima.
”Siku zangu ni kama kivuli cha jioni, ninanyauka kama jani. Lakini wewe, Ee BWANA, umeketi katika kiti chako cha enzi milele, sifa zako za ukuu zaendelea vizazi vyote.
”kwa kuwa anajua tulivyoumbwa, anakumbuka kwamba sisi tu mavumbi. Kuhusu mwanadamu, siku zake ni kama majani, anachanua kama ua la shambani; upepo huvuma juu yake nalo hutoweka, mahali pake hapalikumbuki tena.
”Unapoficha uso wako, wanapata hofu, unapoondoa pumzi yao, wanakufa na kurudi mavumbini.
”Mbingu zilizo juu sana ni mali ya BWANA, lakini dunia amempa mwanadamu. Sio wafu wanaomsifu BWANA, wale washukao mahali pa kimya,
”(Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Daudi) Ee BWANA, umenichunguza na kunijua. Unajua ninapoketi na ninapoinuka; unatambua mawazo yangu tokea mbali. Unafahamu kutoka kwangu na kulala kwangu; unaelewa njia zangu zote. Kabla neno halijafika katika ulimi wangu, wewe walijua kikamilifu, Ee BWANA.
”Kwa maana wewe ndiwe uliyeumba utu wangu wa ndani; uliniunga pamoja tumboni mwa mama yangu. Ninakusifu kwa sababu nimeumbwa kwa namna ya ajabu na ya kutisha; kazi zako ni za ajabu, ninajua hayo kikamilifu. Umbile langu halikufichika kwako, nilipoumbwa mahali pa siri. Nilipoungwa pamoja kwa ustadi katika vilindi vya nchi, macho yako yaliniona kabla mwili wangu haujakamilika. Siku zangu zote ulizonipangia ziliandikwa katika kitabu chako kabla haijakuwapo hata moja. Tazama jinsi gani yalivyo ya thamani mawazo yako kwangu, Ee Mungu! Jinsi gani jumla yake ilivyo kubwa! Kama ningezihesabu, zingekuwa nyingi kuliko mchanga. Niamkapo, bado niko pamoja nawe.
”Mwanadamu ni kama pumzi, siku zake ni kama kivuli kinachopita.
”Usiweke tumaini lako kwa wakuu, kwa wanadamu ambao hufa, ambao hawawezi kuokoa. Roho yao itokapo hurudi mavumbini, siku hiyo hiyo mipango yao yote hukoma.
”BWANA huwachukia sana watu wenye moyo wa upotovu, bali hupendezwa na wale ambao njia zao hazina lawama.
”Moyo wa mfalme uko katika mkono wa BWANA; huuongoza kama mkondo wa maji, po pote apendapo. Njia zote za mwanadamu huonekana sawa kwake, bali BWANA huupima moyo.
”Tajiri na maskini wanafanana kwa hili: BWANA ni Muumba wao wote.
”Mtu hutoka tumboni mwa mama yake uchi, naye jinsi alivyokuja vivyo hivyo huondoka. Hachukui cho chote kutokana na kazi yake ambacho anaweza kukibeba mkononi mwake.
”Afadhali sifa nzuri kuliko manukato safi, nayo siku ya kufa kuliko ya kuzaliwa.
”Hakuna mtu mwenye haki duniani ambaye hufanya mambo ya haki na kamwe asitende dhambi.
”Hakuna mwanadamu awezaye kushikilia roho yake asife, wala hakuna mwenye uwezo juu ya siku ya kufa kwake. Kama vile hakuna ye yote arudishwaye nyuma wakati wa vita, kadhalika uovu hautawaweka huru wale wautendao.
”Huu ni ubaya ulio katika kila kitu kinachotendeka chini ya jua: Mwisho unaofanana huwapata wote. Zaidi ya hayo, mioyo ya watu, imejaa ubaya na kuna wazimu mioyoni mwao wangali hai, hatimaye huungana na waliokufa.
”Kama vile usivyofahamu njia ya upepo, au jinsi mwili uumbwavyo ndani ya tumbo la mama, vivyo hivyo huwezi kufahamu kazi ya Mungu, Muumba wa vitu vyote.
”Sauti husema, “Piga kelele.” Nami nikasema, “Nipige kelele gani?” “Wanadamu wote ni kama majani, nao utukufu wao wote ni kama maua ya kondeni. Majani hunyauka na maua huanguka, kwa sababu pumzi ya BWANA huyapuliza. Hakika wanadamu ni majani.
”Hili ndilo asemalo Mungu, BWANA, yeye aliyeziumba mbingu na kuzitanda, aliyeitandaza dunia na vyote vitokavyo humo, awapaye watu wake pumzi na uzima kwa wale waendao humo:
”“Hili ndilo asemalo BWANA, Mkombozi wako, aliyekuumba tumboni: “Mimi ni BWANA, yeye aliyeumba vitu vyote, yeye peke yake aliyezitanda mbingu, yeye aliyeitandaza nchi mwenyewe,
”“Mimi, naam mimi, ndimi niwafarijie ninyi. Ninyi ni nani hata kuwaogopa wanadamu wanaokufa, wana wa wanadamu ambao ni majani tu,
”Sisi sote, kama kondoo, tumepotea, kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe, naye BWANA aliweka juu yake maovu yetu sisi sote.
”“Kwa kuwa mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu,” asema BWANA. “Kama vile mbingu zilivyo juu kuliko dunia, ndivyo njia zangu zilivyo juu kuliko njia zenu na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.
”Sisi sote tumekuwa kama mtu aliye najisi, nayo matendo yetu yote ya uadilifu ni kama matambaa machafu; sisi sote tunasinyaa kama jani na kama upepo maovu yetu hutupeperusha. Hakuna ye yote anayeliitia jina lako wala anayejitahidi kukushika, kwa kuwa umetuficha uso wako na kutuacha tudhoofike kwa sababu ya dhambi zetu. Lakini, Ee BWANA, wewe ndiwe Baba yetu. Sisi ni udongo wa mfinyanzi wewe ndiye mfinyanzi; sisi sote tu kazi ya mkono wako.
”“Kabla sijakuumba ndani ya tumbo la mama yako, nilikujua; kabla hujazaliwa nilikutenga kwa kazi maalum; nilikuweka uwe nabii kwa mataifa.”
”‘Lakini ninyi mmetenda kwa uovu zaidi kuliko baba zenu. Tazama jinsi ambavyo kila mmoja wenu anafuata ukaidi wa moyo wake mbaya badala ya kunitii mimi.
”Hili ndilo asemalo BWANA: “Amelaaniwa yeye amtegemeaye mwanadamu, ategemeaye mwenye mwili kwa ajili ya nguvu zake, ambaye moyo wake umemwacha BWANA.
”Moyo ni mdanganyifu kuliko vitu vyote, ni mwovu kupita kiasi. Ni nani awezaye kuujua? “Mimi BWANA huchunguza moyo na kuzijaribu nia, kumlipa mtu kwa kadiri ya mwenendo wake, kwa kadiri ya matendo yake yanavyostahili.”
”Kwa kuwa kila roho ni mali yangu, kama vile ilivyo roho ya baba, vivyo hivyo roho ya mtoto ni mali yangu. Roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa.
”Nitawapa moyo mpya na kuweka roho mpya ndani yenu, nitaondoa ndani yenu moyo wenu wa jiwe na kuwapa moyo wa nyama.
”Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo kwa hii mifupa: Nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi. Nitawawekea mishipa, nami nitaifanya nyama ije juu yenu na kuwafunika kwa ngozi. Nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtakuwa hai. Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimi BWANA.’ ”
”Alipoona makutano aliwahurumia kwa sababu walikuwa wanasumbuka bila msaada, kama kondoo wasio na mchungaji.
”Hata nywele za vichwa vyenu zote zimehesabiwa. Hivyo msiogope, kwa maana ninyi ni wa thamani kubwa zaidi kuliko shomoro wengi.
”Mtu mwema hutoa yaliyo mema kutoka katika hazina ya mambo mema yaliyohifadhiwa ndani yake, naye mtu mwovu hutoa yaliyo maovu kutoka katika hazina ya mambo maovu yaliyohifadhiwa ndani yake.
”Lakini kitokacho kinywani hutoka moyoni, na hiki ndicho kimtiacho mtu unajisi. Kwa maana ndani ya moyo hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushahidi wa uongo na masingizio.
”Yesu akasema, “Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mbinguni ni wa wale walio kama hawa.”
”Kesheni na muombe, msije mkaanguka majaribuni. Hakika roho iko radhi lakini mwili ni dhaifu.”
”Kwa maana kutoka ndani ya moyo wa mtu hutoka: Mawazo mabaya, uasherati, wizi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, uovu, udanganyifu, ufisadi, wivu, matukano, kiburi na upumbavu. Maovu haya yote hutoka ndani ya mtu nayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi.”
”Lakini tangu mwanzo wa uumbaji, ‘Mungu aliwaumba mume na mke. Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe na hao wawili, watakuwa mwili mmoja.’ Kwa hiyo hawatakuwa wawili tena bali mwili mmoja. Basi, alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.”
”Yesu akamwambia, “Mbona unaniita mwema? Hakuna aliye mwema isipokuwa Mungu peke yake.
”Vivyo hivyo mtu mwema hutoa mambo mema kutoka kwenye hazina ya moyo wake, naye mtu mwovu hutoa mambo mabaya kutoka kwenye hazina ya moyo wake. Kwa kuwa mtu hunena kwa kinywa chake yale yaliyoujaza moyo wake.
”Naam, hata idadi ya nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa. Kwa hiyo msiogope, ninyi ni wa thamani kuliko mashomoro wengi.
”Bali wote waliompokea, aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake. Hawa ndio waliozaliwa si kwa damu wala kwa mapenzi ya mwili au kwa mapenzi ya mtu, bali kwa mapenzi ya Mungu.
”Lakini Yesu hakujiaminisha kwao kwa sababu aliwajua wanadamu wote. Hakuhitaji ushuhuda wa mtu ye yote kuhusu mtu, kwa kuwa alijua yote yaliyokuwa moyoni mwa mtu.
”Yesu akamjibu, “Amin, amin nakuambia, mtu hawezi kuuona Ufalme wa Mungu asipozaliwa mara ya pili.” Nikodemo akauliza, “Awezaje mtu kuzaliwa wakati akiwa mzee? Hakika hawezi kuingia mara ya pili kwenye tumbo la mama yake ili azaliwe!” Yesu akamwambia, “Amin, amin nakuambia, hakuna mtu ye yote anayeweza kuingia katika Ufalme wa Mungu isipokuwa amezaliwa kwa maji na kwa Roho. Mwili huzaa mwili, lakini Roho huzaa roho. Kwa hiyo usishangae ninapokuambia huna budi ‘kuzaliwa mara ya pili.’
”“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
”Hii ndiyo hukumu kwamba: Nuru imekuja ulimwenguni, nao watu wakapenda giza kuliko nuru kwa sababu matendo yao ni maovu.
”Akawaambia, “Ninyi mmetoka chini, mimi nimetoka juu. Ninyi ni wa ulimwengu huu, mimi si wa ulimwengu huu. Niliwaambia kuwa mtakufa katika dhambi zenu, kwa maana msipoamini ya kwamba ‘Mimi Ndiye,’ mtakufa katika dhambi zenu.”
”Wala hatumikiwi na mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji cho chote, kwa sababu yeye mwenyewe ndiye awapaye watu wote uhai na pumzi na vitu vyote. Kutoka kwa mtu mmoja, yeye aliumba mataifa yote ya wanadamu ili waikalie dunia yote, naye akaweka nyakati za kuishi. Mungu alifanya hivyo ili wanadamu wamtafute na huenda wakamfikia ingawa kwa kupapasapapasa ijapokuwa kwa kweli hakai mbali na kila mmoja wetu. ‘Kwa kuwa katika yeye tunaishi, tunatembea na kuwa na uzima wetu.’ Kama baadhi ya watunga mashairi wenu walivyosema, ‘Sisi ni watoto wake.’
”Ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni dhidi ya uasi wote na uovu wa wanadamu ambao huipinga kweli kwa uovu wao,
”Ingawa wakijidai kuwa wenye hekima, wakawa wajinga na kubadili utukufu wa Mungu aishiye milele kwa sanamu zilizofanywa zifanane na mwanadamu ambaye hufa, na mfano wa ndege, wanyama na viumbe vitambaavyo. Kwa hiyo, Mungu akawaacha wazifuate tamaa mbaya za mioyo yao katika uasherati, hata wakavunjiana heshima miili yao wao kwa wao.
”La hasha! Mungu na aonekane mwenye haki na kila mwanadamu kuwa mwongo, kama ilivyoandikwa: “Ili uweze kujulikana kuwa na haki katika maneno yako, nawe ukashinde katika hukumu.”
”Kama ilivyoandikwa: “Hakuna mwenye haki, hakuna hata mmoja. Hakuna hata mmoja mwenye ufahamu, hakuna hata mmoja amtafutaye Mungu. Wote wamegeukia mbali, wote kwa pamoja hawafai; hakuna atendaye mema, naam, hata mmoja.”
”kwa kuwa wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu,
”Kwa hiyo kama vile dhambi ilivyoingia ulimwenguni kupitia kwa mtu mmoja na kupitia dhambi hii, mauti ikawafikia watu wote, kwa sababu wote wamefanya dhambi.
”Au hamjui ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Kwa hiyo tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti, ili kama vile Kristo alivyofufuka kutoka kwa wafu kwa utukufu wa Baba, vivyo hivyo sisi nasi pia tupate kuenenda katika upya wa uzima. Kwa maana ikiwa tumeungana naye katika mauti yake, bila shaka tutaungana naye katika ufufuo wake. Kwa maana twajua kwamba utu wetu wa kale ulisulibiwa pamoja naye ili ule mwili wa dhambi upate kuangamizwa, nasi tusiendelee kuwa tena watumwa wa dhambi. Kwa maana mtu ye yote aliyekufa amewekwa huru mbali na dhambi. Basi ikiwa tulikufa pamoja na Kristo, tunaamini kwamba pia tutaishi pamoja naye. Kwa maana tunajua kwamba Kristo, akiisha kufufuka kutoka kwa wafu, hatakufa tena, mauti haina tena mamlaka juu yake. Kifo alichokufa, aliifia dhambi mara moja tu, lakini uzima alio nao anamwishia Mungu. Vivyo hivyo, jihesabuni wafu katika dhambi lakini mlio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu. Kwa hiyo, msiruhusu dhambi itawale ndani ya miili yenu, ipatikanayo na kufa, ili kuwafanya mzitii tamaa mbaya. Wala msivitoe viungo vya miili yenu vitumike kama vyombo vya uovu vya kutenda dhambi, bali jitoeni kwa Mungu, kama watu waliotolewa kutoka mautini kuingia uzimani. Nanyi vitoeni viungo vya miili yenu kwake kama vyombo vya haki.
”Ninasema kwa namna ya kibinadamu kwa sababu ya udhaifu wenu wa hali ya asili. Kama vile kwanza mlivyokuwa mmevitoa viungo vya miili yenu kama watumwa wa mambo machafu na uovu uliokuwa ukiongezeka zaidi na zaidi, hivyo sasa vitoeni viungo vya miili yenu vitumike kwa ajili ya haki ambayo matokeo yake ni utakatifu.
”Kwa maana tulipokuwa tunatawaliwa na asili ya dhambi, tamaa za dhambi zilizochochewa na sheria zilikuwa zikitenda kazi katika miili yetu, hivyo tulizaa matunda ya mauti.
”Kwa maana ninafahamu kwamba hakuna jema lo lote likaalo ndani yangu, yaani, katika asili yangu ya dhambi. Kwa kuwa nina shauku ya kutenda lililo jema, lakini siwezi kulitenda.
”Ole wangu mimi maskini! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?
”Kwa maana kile ambacho sheria haikuwa na uwezo wa kufanya, kwa vile ilivyokuwa dhaifu katika mwili, Mungu kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe kwa mfano wa mwanadamu mwenye mwili ulio wa dhambi na kwa ajili ya dhambi, yeye aliihukumu dhambi katika mwili, ili kwamba haki ipatikanayo kwa sheria itimizwe ndani yetu sisi, ambao hatuenendi kwa kuufuata mwili bali kwa kufuata Roho. Kwa maana wale wanaoishi kwa kuufuata mwili huziweka nia zao katika vitu vya mwili, lakini wale wanaoishi kwa kufuata Roho, huziweka nia zao katika mambo ya Roho. Kwa maana kuwa na nia ya mwili ni mauti, bali kuwa na nia inayoongozwa na Roho ni uzima na amani. Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui na Mungu, kwa maana haiitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii. Wale wanaotawaliwa na mwili, hawawezi kumpendeza Mungu. Lakini ninyi, hamtawaliwi na mwili, bali na Roho, ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu. Mtu ye yote ambaye hana Roho wa Kristo, yeye si wa Kristo.
”kwa maana mkiishi kwa kuufuata mwili, mtakufa, lakini kama mkiyaua matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi.
”Hii ina maana kwamba, si watoto waliozaliwa kimwili walio watoto wa Mungu, bali ni watoto wa ahadi wanaohesabiwa kuwa uzao wa Abrahamu.
”Bali jivikeni Bwana Yesu Kristo, wala msifikiri jinsi mtakavyotimiza tamaa za miili yenu yenye asili ya dhambi.
”Mtu ambaye hana Roho wa Mungu hawezi kupokea mambo yatokayo kwa Roho wa Mungu, kwa kuwa ni upuzi kwake, naye hawezi kuyaelewa kwa sababu hayo yanaeleweka tu kwa jinsi ya rohoni.
”Je, hamjui ya kwamba ninyi ni Hekalu la Mungu na kwamba Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu ye yote akiliharibu Hekalu la Mungu, Mungu atamwangamiza mtu huyo, Kwa maana Hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.
”Je, hamjui ya kwamba miili yenu ni Hekalu la Roho Mtakatifu akaaye ndani yenu, ambaye mmepewa na Mungu? Ninyi si mali yenu wenyewe, kwa maana mmenunuliwa kwa gharama. Kwa hiyo mtukuzeni Mungu katika miili yenu na katika roho zenu ambazo ni mali ya Mungu.
”Kwa maana kama vile mauti ilivyokuja kwa njia ya mtu mmoja, vivyo hivyo, ufufuo wa wafu umekuja kwa njia ya mtu mmoja. Kwa maana kama vile katika Adamu watu wote wanakufa, vivyo hivyo katika Kristo wote watafanywa hai.
”Kwa maana nyama zote si za aina moja. Binadamu wana nyama ya aina moja, wanyama wana aina nyingine, kadhalika ndege na samaki wana nyama tofauti.
”Hivyo ndivyo itakavyokuwa wakati wa ufufuo wa wafu. Ule mwili wa kuharibika uliopandwa, utafufuliwa usioharibika, unapandwa katika aibu, unafufuliwa katika utukufu, unapandwa katika udhaifu, unafufuliwa katika nguvu, unapandwa mwili wa asili, unafufuliwa mwili wa kiroho. Kama kuna mwili wa asili, basi kuna mwili wa kiroho pia. Kwa hiyo imeandikwa, “Mtu wa kwanza Adamu alifanyika kiumbe hai”; Adamu wa mwisho, yeye ni roho iletayo uzima. Lakini si ule wa kiroho uliotangulia, bali ni ule wa asili, kisha ule wa kiroho. Mtu wa kwanza aliumbwa kwa mavumbi ya ardhini, mtu wa pili alitoka mbinguni. Kama vile alivyokuwa yule wa ardhini, ndivyo walivyo wale walio wa ardhini; na kwa vile alivyo mtu yule aliyetoka mbinguni, ndivyo walivyo wale walio wa mbinguni. Kama vile tulivyochukua mfano wa yule mtu wa ardhini, ndivyo tutakavyochukua mfano wa yule mtu aliyetoka mbinguni. Ndugu zangu nisemalo ni hili: nyama na damu haviwezi kuurithi Ufalme wa Mungu, wala kuharibika kurithi kutokuharibika.
”Kwa hiyo, hatukati tamaa. Ingawa utu wetu wa nje unachakaa, utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku.
”Kwa maana twajua kwamba kama hema yetu ya dunia tunayoishi ikiharibiwa, tunalo jengo kutoka kwa Mungu, nyumba isiyojengwa kwa mikono ya wanadamu. Kwa maana katika hema hii twalia kwa uchungu, tukitamani kuvikwa makao yetu ya mbinguni, kwa kuwa tukiisha kuvikwa hatutaonekana tena kuwa uchi. Kwa kuwa tukiwa bado katika hema hii twalia kwa uchungu na kulemewa, kwa sababu hatutaki kuvuliwa bali kuvikwa makao yetu ya mbinguni ili kwamba kile kipatikanacho na mauti kimezwe na uzima.
”Wapenzi, kwa kuwa tunazo ahadi hizi, basi na tujitakase nafsi zetu kutokana na kila kitu kitiacho mwili na roho unajisi, tukitimiza utakatifu kwa kumcha Mungu.
”Wala hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume wala mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu.
”Kwa hiyo nasema, enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa maana mwili hutamani yale yaliyo kinyume na Roho, nayo Roho hutamani yale yaliyo kinyume na mwili. Roho na mwili hupingana na kwa sababu hiyo hamwezi kufanya mnayotaka.
”Wote walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili na shauku zake pamoja na tamaa zake.
”Apandaye kwa mwili, katika mwili wake, atavuna uharibifu, lakini yeye apandaye katika Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele.
”Sisi sote pia tuliishi katikati yao hapo zamani, tukitimiza tamaa za asili yetu ya dhambi na kufuata tamaa zake na mawazo yake. Nasi kwa asili tulikuwa wana wa ghadhabu, kama mtu mwingine ye yote.
”Watu hao akili zao zimetiwa giza na wametengwa mbali na uzima wa Mungu kwa sababu ya ujinga wao kutokana na ugumu wa mioyo yao.
”Kwa maana kwangu mimi, kuishi ni Kristo na kufa ni faida.
”Kwa maana sisi ndio tulio tohara, sisi tumwabuduo Mungu katika Roho, tunaona fahari katika Kristo Yesu, ambao hatuweki tumaini letu katika mwili,
”Kwa maana, kama nilivyokwisha kuwaambia mara nyingi kabla, nami sasa nasema tena hata kwa machozi, watu wengi wanaishi kama adui wa msalaba wa Kristo. Mwisho wa watu hao ni uangamivu, Mungu wao ni tumbo na utukufu wao ni aibu na mawazo yao yamo katika mambo ya dunia. Lakini uenyeji wetu uko mbinguni. Nasi tunamngoja kwa shauku Mwokozi kutoka huko, yaani, Bwana Yesu Kristo, atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, ili upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote chini yake.
”Angalieni mtu ye yote asiwafanye ninyi mateka kwa elimu batili na madanganyo matupu yanayotegemea mapokeo ya wanadamu na mafundisho ya ulimwengu ambayo siyo ya Kristo.
”Hapa hakuna Myunani wala Myahudi, aliyetahiriwa wala asiyetahiriwa, asiyestaarabika wala aliyestaarabika, mtumwa wala mtu huru, bali Kristo ni yote na ndani ya wote.
”Mungu mwenyewe, Mungu wa amani, awatakase ninyi kabisa. Nanyi mhifadhiwe roho zenu, nafsi zenu na miili yenu, bila kuwa na lawama katika Bwana wetu Yesu Kristo.
”Kwa kuwa hatukuja humu duniani na kitu cho chote, wala hatuwezi kutoka humu na kitu.
”Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali roho ya nguvu, ya upendo na ya moyo wa kiasi.
”Kwa maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kumkufuru Mungu, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio watakatifu, wasio na upendo, wasiopenda kupatanishwa, wasingiziaji, wasiozuia tamaa zao, wakatili, wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi, waliojaa majivuno, wapendao anasa zaidi kuliko kumpenda Mungu. Wakiwa na mfano wa utauwa kwa nje lakini wakizikana nguvu za Mungu. Jiepushe na watu wa namna hiyo.
”Kwa wale walio safi, kila kitu ni safi kwao. Lakini kwa wale waliopotoka na wasioamini, hakuna cho chote kilicho safi. Kwa kweli nia zao na dhamiri zao zimepotoka. Wanadai kumjua Mungu, lakini kwa matendo yao wanamkana. Hao watu ni chukizo, wasiotii, wasiofaa kwa jambo lo lote jema.
”Lakini kuna mahali mtu fulani ameshuhudia akisema: “Mwanadamu ni kitu gani hata umfikirie, mwana wa mwanadamu ni nani hata umjali? Umemfanya kuwa chini kidogo kuliko malaika; umemvika taji ya utukufu na heshima, nawe umeweka vitu vyote chini ya miguu yake.” Kwa kuweka vitu vyote chini yake, Mungu hakuacha kitu cho chote ambacho hakukiweka chini ya mwanadamu. Lakini kwa sasa, hatuoni kwamba kila kitu kiko chini yake.
”Basi kwa kuwa watoto wana nyama na damu, yeye pia alishiriki katika ubinadamu wao, ili kwa kifo chake, apate kumwangamiza huyo mwenye nguvu za mauti, yaani, Shetani, na kuwaweka huru wale waliokuwa utumwani maisha yao yote kwa sababu ya kuogopa mauti.
”Kwa maana Neno la Mungu li hai tena lina nguvu tena lina makali kuliko upanga uwao wote wenye makali kuwili, tena linachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, viungo na mafuta yaliyo ndani yake, tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. Wala hakuna kiumbe cho chote kilichofichika machoni pa Mungu. Kila kitu kimefunuliwa na kiko wazi machoni pake yeye ambaye kwake ni lazima tutatoa hesabu.
”Kama vile mwanadamu alivyowekewa kufa mara moja tu na baada ya kufa akabili hukumu,
”Lakini kila mtu hujaribiwa wakati anapovutwa na kudanganywa na tamaa zake mwenyewe zilizo mbaya. Basi ile tamaa mbaya ikishachukua mimba, huzaa dhambi, ile dhambi ikikomaa, huzaa mauti. Ndugu zangu, msidanganyike.
”Kama vile ambavyo mwili pasipo roho umekufa, kadhalika nayo imani pasipo matendo imekufa.
”Basi sikilizeni ninyi msemao, “Leo au kesho tutakwenda katika mji huu ama ule tukae humo mwaka mmoja, tufanye biashara na kupata faida.” Lakini hamjui hata litakalotukia kesho. Maisha yenu ni nini? Ninyi ni ukungu ambao huonekana kwa kitambo kidogo kisha hutoweka.
”Maana, “Watu wote ni kama majani, na utukufu wao ni kama ua la shambani; majani hunyauka na ua lake hupukutika,
”Wapenzi, ninawasihi, mkiwa kama wageni na wapitaji hapa ulimwenguni, epukeni tamaa mbaya za mwili ambazo hupigana vita na roho zenu.
”Msiupende ulimwengu wala mambo yaliyoko ulimwenguni. Kama mtu ye yote akiupenda ulimwengu, upendo wa Baba haumo ndani yake. Kwa maana kila kitu kilichomo ulimwenguni, yaani tamaa ya mwili, tamaa ya macho na kiburi cha uzima: havitokani na Baba bali hutokana na ulimwengu. Nao ulimwengu unapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu milele.
”Oneni ni pendo kuu namna gani alilotupa Baba, kwamba sisi tuitwe watoto wa Mungu! Nasi ndivyo tulivyo. Sababu kwa nini ulimwengu haututambui, ni kwa kuwa haukumtambua yeye.
”wengine waokoeni kwa kuwanyakua kutoka kwenye moto; nao wengine wahurumieni mkiwa na hofu, mkichukia hata vazi lenye mawaa na kutiwa unajisi na mwili.
”Tazama! Anakuja na mawingu na kila jicho litamwona, hata wale waliomchoma mkuki; na mataifa yote ulimwenguni yataomboleza kwa sababu yake. Naam, ndivyo itakavyokuwa! Amen.
”