21 – Ibada
Haya ni maneno matakatifu ya Mungu Mwenyezi.
Hatupendi maneno ya wanadamu.
Kwa mtu yeyote anayempenda Mungu... hivi ndivyo Mungu anasema kuhusu: Ibada.
Haya ni maneno matakatifu ya Mungu Mwenyezi.
Hatupendi maneno ya wanadamu.
Kwa mtu yeyote anayempenda Mungu... hivi ndivyo Mungu anasema kuhusu: Ibada.
Kila mmoja wa hawa viumbe wenye uhai wanne, alikuwa na mabawa sita na kujawa na macho pande zote, hadi chini ya mabawa. Usiku na mchana hawakuacha kusema: “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni BWANA Mungu Mwenyezi, aliyekuwako, aliyeko na atakayekuja.” Kila mara viumbe hao wenye uhai wanne walipomtukuza, kumheshimu na kumshukuru yeye aliyeketi kwenye kile kiti cha enzi, tena aishiye milele na milele, wale wazee ishirini na wanne huanguka mbele zake yeye aliyeketi kwenye kile kiti cha enzi na kumwabudu yeye aliye hai milele na milele. Wao huziweka taji zao mbele ya hicho kiti cha enzi, wakisema: “Bwana wetu na Mungu wetu, wewe umestahili kupokea utukufu na heshima na uweza, kwa maana ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa mapenzi yako viliumbwa na vimekuwako.”
”Kwa hiyo, Mungu alimtukuza juu sana na kumpa Jina lililo kuu kuliko kila jina, ili kwa Jina la Yesu, kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, vya duniani na vya chini ya nchi, na kila ulimi ukiri ya kwamba YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.
”(Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Gitithi. Zaburi Ya Wana Wa Kora) Ee BWANA Mwenye Nguvu Zote, makao yako yapendeza kama nini! Nafsi yangu inatamani sana, naam, hata kuona shauku, kwa ajili ya nyua za BWANA; moyo wangu na mwili wangu vinamlilia Mungu Aliye Hai. Hata shomoro amejipatia makao, mbayuwayu amejipatia kiota mahali awezapo kuweka makinda yake: mahali karibu na madhabahu yako, Ee BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mfalme wangu na Mungu wangu. Heri wale wanaokaa nyumbani mwako, wanaokusifu wewe daima.
”Enoki akatembea na Mungu, kisha akatoweka, kwa sababu Mungu alimchukua.
”Ndipo Melkizedeki mfalme wa Salemu alipoleta mkate na divai. Alikuwa kuhani wa Mungu Aliye Juu Sana; akambariki Abramu, akisema, “Abarikiwe Abramu na Mungu Aliye Juu Sana, Muumba wa mbingu na nchi. Abarikiwe Mungu Aliye Juu Sana, ambaye amewaweka adui zako mkononi mwako.” Ndipo Abramu akampa Melkizedeki sehemu ya kumi ya kila kitu.
”Lakini Abramu akamwambia mfalme wa Sodoma, “Nimeinua mkono wangu kwa BWANA, Mungu Aliye Juu Sana, Muumba wa mbingu na dunia, na nimeapa
”Abramu akaanguka kifudifudi, naye Mungu akamwambia,
”Yule mtumishi akasujudu na kumwabudu BWANA,
”nikasujudu na nikamwabudu BWANA. Nikamtukuza BWANA, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, aliyeniongoza katika njia sahihi ili nimtwalie mwana na bwana wangu mke katika jamaa zake.
”Ikawa huyo mtumishi wa Abrahamu aliposikia waliyosema, alisujudu mpaka nchi mbele za BWANA.
”Huko malaika wa BWANA akamtokea Mose katika mwali wa moto kutoka katika kichaka. Mose akaona hilo, ingawa kile kichaka kilikuwa kinawaka moto, kilikuwa hakiteketei.
”Mungu akamwambia, “Usikaribie zaidi. Vua viatu vyako, kwa maana mahali unaposimama ni ardhi takatifu.”
”Mungu akamwambia Mose, “MIMI NIKO AMBAYE NIKO. Hivyo ndivyo utakavyowaambia Waisraeli: ‘MIMI NIKO amenituma kwenu.’ ”
”Lakini nimekuacha wewe uwepo kwa kusudi hili hasa, ili nipate kukuonyesha uwezo wangu na ili Jina langu lipate kutangazwa katika dunia yote.
”Wakati wa mchana BWANA aliwatangulia kwa nguzo ya wingu kuwaongoza katika njia yao, na wakati wa usiku aliwatangulia kwa nguzo ya moto kuwaangazia, ili waweze kusafiri mchana au usiku. Ile nguzo ya wingu wakati wa mchana au ile nguzo ya moto wakati wa usiku haikuondoka mahali pake mbele ya watu.
”Ndipo malaika wa Mungu, aliyekuwa akisafiri mbele ya jeshi la Israeli, akaondoka akakaa nyuma yao. Pia ile nguzo ya wingu ikaondoka hapo mbele yao na kusimama nyuma,
”Ndipo Mose na Waisraeli wakamwimbia BWANA wimbo huu: “Nitamwimbia BWANA, kwa kuwa ametukuzwa sana. Farasi na mpanda farasi amewatosa baharini. BWANA ni nguvu zangu na wimbo wangu; amekuwa wokovu wangu. Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu, Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza.
”“Mkono wako wa kuume, Ee BWANA ulitukuka kwa uweza. Mkono wako wa kuume, Ee BWANA, ukamponda adui. Katika ukuu wa utukufu wako, ukawaangusha chini wale waliokupinga. Uliachia hasira yako kali, ikawateketeza kama kapi.
”“Ni nani miongoni mwa miungu aliye kama wewe, Ee BWANA? Ni nani kama Wewe: uliyetukuka katika utakatifu, utishaye katika utukufu, ukitenda maajabu?
”BWANA atatawala milele na milele.”
”Aroni alipokuwa akizungumza na jumuiya yote ya Waisraeli, wakatazama kuelekea jangwani, na huko wakaona utukufu wa BWANA ukitokeza katika wingu.
”BWANA akamwambia Mose, “Nitakujia katika wingu zito, ili watu wanisikie nikinena nawe na kila mara waweke tumaini lao kwako.” Kisha Mose akamwambia BWANA yale ambayo watu walikuwa wamesema.
”Asubuhi ya siku ya tatu kulikuwa na ngurumo na radi pamoja na wingu nene juu ya mlima na mlio mkubwa sana wa tarumbeta. Kila mmoja aliyekuwa kambini akatetemeka. Kisha Mose akawaongoza watu kutoka kambini kukutana na Mungu, nao wakasimama chini ya mlima. Mlima Sinai ulikuwa umefunikwa na moshi, kwa sababu BWANA alishuka juu yake katika moto. Moshi wa moto huo ulipanda juu kama moshi kutoka kwenye tanuru kubwa na mlima wote ukatetemeka kwa nguvu nyingi,
”Mose alipopanda juu mlimani, wingu liliufunika huo mlima, nao utukufu wa BWANA ukatua juu ya Mlima Sinai. Kwa muda wa siku sita wingu lilifunika mlima, na siku ya saba BWANA akamwita Mose kutoka katikati ya lile wingu. Kwa Waisraeli utukufu wa BWANA ulionekana kama moto uteketezao juu ya mlima. Kisha Mose akaingia ndani ya lile wingu alivyokuwa akipanda mlimani. Naye akakaa huko mlimani kwa muda wa siku arobaini, mchana na usiku.
”Hapo juu ya hicho kifuniko, kati ya hao makerubi wawili walioko juu ya hilo Sanduku la Ushuhuda, hapo ndipo nitakapokutana nawe na kukupa maagizo yangu kwa ajili ya Waisraeli.
”Kila mara Mose alipoingia ndani ya hema, nguzo ya wingu ingeshuka chini na kukaa kwenye ingilio, wakati Mungu akizungumza na Mose. Kila mara watu walipoona hiyo nguzo ya wingu ikiwa imesimama kwenye ingilio la hema, wote walisimama wakaabudu, kila mmoja kwenye ingilio la hema lake. BWANA angezungumza na Mose uso kwa uso, kama vile mtu azungumzavyo na rafiki yake. Kisha Mose angerudi kambini, lakini msaidizi wake kijana Yoshua mwana wa Nuni hakuondoka mle Hemani.
”BWANA akajibu, “Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha.”
”Kisha Mose akasema, “Basi nionyeshe utukufu wako.” Ndipo BWANA akasema, “Nitapitisha wema wangu wote mbele yako, nami nitalitangaza Jina langu, BWANA, mbele ya uso wako. Nitakuwa na rehema kwake yeye nimrehemuye, pia nitakuwa na huruma kwake yeye nimhurumiaye.” Lakini Mungu akasema, “Hutaweza kuuona uso wangu, kwa kuwa hakuna mtu ye yote awezaye kuniona akaishi.” Kisha BWANA akasema, “Kuna mahali karibu nami ambapo unaweza kusimama juu ya mwamba. Utukufu wangu unapopita, nitakuweka gengeni kwenye mwamba na kukufunika kwa mkono wangu mpaka nitakapokwisha kupita. Kisha nitaondoa mkono wangu nawe utaona mgongo wangu; lakini kamwe uso wangu hautaonekana.”
”Kisha BWANA akashuka katika wingu akasimama pamoja naye huko, akalitangaza jina lake, BWANA. BWANA akapita mbele ya Mose, akitangaza, “BWANA, BWANA, Mungu mwenye huruma na neema, asiye mwepesi wa hasira, mwingi wa upendo na uaminifu, akidumisha upendo kwa maelfu, pia akisamehe uovu, uasi na dhambi. Lakini haachi kuadhibu mwenye hatia; huwaadhibu watoto na watoto wao kwa ajili ya dhambi ya baba zao hata katika kizazi cha tatu na cha nne.” Mara Mose akasujudu na kuabudu.
”Usiabudu mungu mwingine, kwa kuwa BWANA, ambaye jina lake ni Wivu, ni Mungu mwenye wivu.
”Ndipo wingu likafunika Hema la Kukutania, na utukufu wa BWANA ukaijaza Maskani ya Mungu. Mose hakuweza kuingia ndani ya Hema la Kukutania kwa sababu wingu lilikuwa limetua juu ya Hema, nao utukufu wa BWANA ukaijaza Maskani ya Mungu.
”Kwa hiyo wingu la BWANA lilikuwa juu ya maskani mchana, na moto ulikuwa katika hilo wingu wakati wa usiku, machoni pa nyumba yote ya Israeli siku zote za safari zao.
”Kisha Mose na Aroni wakaingia kwenye Hema la Kukutania. Walipotoka nje wakawabariki watu; nao utukufu wa BWANA ukawatokea watu wote. Moto ukaja kutoka katika uwepo wa BWANA, ukairamba ile sadaka ya kuteketezwa, pamoja na sehemu ya mafuta yaliyokuwa juu ya madhabahu. Watu wote walipoona jambo hili, wakapiga kelele kwa furaha na kusujudu.
”BWANA akamwambia Mose: “Mwambie ndugu yako Aroni asije wakati wo wote atakavyo yeye ndani ya Patakatifu pa Patakatifu nyuma ya pazia mbele ya kiti cha rehema kile kilichoko juu ya Sanduku la Agano, la sivyo atakufa, kwa sababu huwa ninatokea ndani ya wingu juu ya kile kiti cha rehema.
”Katika siku hiyo ambayo Maskani, Hema la Ushuhuda, liliposimamishwa, wingu liliifunika. Kuanzia jioni mpaka asubuhi wingu lililokuwa juu ya maskani lilionekana kama moto. Hivyo ndivyo lilivyoendelea kuwa; wingu liliifunika wakati wa mchana, na usiku lilionekana kama moto.
”Hata hivyo, kwa hakika kama niishivyo, na kwa hakika kama utukufu wa BWANA uijazavyo dunia yote,
”Kora alipokuwa amekusanya wafuasi wake wote kuwapinga Mose na Aroni kwenye mlango wa Hema la Kukutania, utukufu wa BWANA ukatokea kwa kusanyiko lote.
”Lakini wakati kusanyiko lilipokusanyika kupingana na Mose na Aroni, nalo likageuka kuelekea Hema la Kukutania, ghafula wingu likafunika Hema, nao utukufu wa BWANA ukatokea.
”Mose na Aroni wakaondoka pale kwenye kusanyiko mpaka kwenye mlango wa Hema la Kukutania na kuanguka kifudifudi, nao utukufu wa BWANA ukawatokea.
”Kisha BWANA akafungua macho ya Balaamu, naye akamwona malaika wa BWANA amesimama barabarani akiwa ameufuta upanga wake. Balaamu akainama, akaanguka kifudifudi.
”ujumbe wake yeye ambaye husikia maneno ya Mungu, ambaye ana maarifa kutoka kwa Aliye Juu Sana, huona maono kutoka Mwenyezi, ambaye huanguka kifudifudi na ambaye macho yake yamefunguka:
”Mlionyeshwa mambo haya ili mpate kujua kuwa BWANA ndiye Mungu; hakuna mwingine ila yeye. Kutoka mbinguni amewasikizisha sauti yake ili kuwaadilisha. Hapa duniani aliwaonyesha moto wake mkubwa, nanyi mlisikia maneno yake kutoka kwenye ule moto.
”Kubalini na mweke moyoni leo kuwa BWANA ndiye Mungu mbinguni juu na duniani chini. Hakuna mwingine.
”Nanyi mkasema, “BWANA Mungu wetu ametuonyesha utukufu na enzi yake, nasi tumesikia sauti yake kutoka kwenye moto. Leo tumeona kwamba mwanadamu anaweza kuishi hata kama Mungu akizungumza naye.
”Sikia, Ee Israeli: BWANA Mungu wako, ni BWANA mmoja. Mpende BWANA Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote na kwa nguvu zako zote.
”Kwa kuwa BWANA Mungu wenu ni Mungu wa miungu na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye uweza na wa kutisha, ambaye hana upendeleo na hapokei rushwa.
”Mche BWANA Mungu wako na umtumikie yeye. Shikamana naye kwa uthabiti na kuapa kwa jina lake. Yeye ni sifa yako; yeye ni Mungu wako, ambaye alikutendea yale maajabu makubwa na ya kutisha uliyoyaona kwa macho yako mwenyewe.
”Kama hutafuata kwa bidii maneno yote ya sheria hii, ambayo yameandikwa katika kitabu hiki na kama hutalicha hili jina la fahari na la kutisha, yaani la BWANA Mungu wako,
”Nitalitangaza jina la BWANA. Naam, sifuni ukuu wa Mungu wetu! Yeye ni Mwamba, kazi zake ni kamilifu, njia zake zote ni haki. Mungu mwaminifu ambaye hakosei, yeye ni mnyofu na mwenye haki.
”“Tazama basi, Mimi mwenyewe, Mimi Ndiye! Hakuna mungu mwingine ila Mimi. Mimi ninaua na Mimi ninafufua, Mimi nimejeruhi na Mimi nitaponya, wala hakuna awezaye kuokoa kutoka mkononi mwangu.
”“Hakuna mwingine kama Mungu wa Yeshuruni, ambaye hupanda juu ya mbingu ili akusaidie, na juu ya mawingu katika utukufu wake. Mungu wa milele ni kimbilio lako, na chini kuna mikono ya milele. Atamfukuza adui yako mbele yako, akisema, ‘Mwangamize yeye!’
”Akajibu, “La, siko upande wo wote, lakini mimi nimekujia nikiwa amiri jeshi wa jeshi la BWANA.” Yoshua akaanguka kifudifudi hadi nchi, akasujudu, akamwuliza, “Je, Bwana, una ujumbe gani kwa mtumishi wako?” Amiri jeshi wa jeshi la BWANA akajibu, “Vua viatu vyako, kwa maana mahali hapa unaposimama ni patakatifu.” Naye Yoshua akafanya hivyo.
”Uwe na makuhani saba wakibeba mabaragumu ya pembe za kondoo waume mbele ya Sanduku. Siku ya saba, mzunguke mji mara saba, nao makuhani wakipiga baragumu hizo. Utakaposikia makuhani wamepaliza sauti kubwa ya baragumu, watu wote wapige kelele kwa sauti kuu, kisha ukuta wa mji utaanguka na watu watakwea, kila mtu aingie ndani moja kwa moja kutokea pale alipo.”
”Wakati baragumu zilipopigwa, watu walipiga kelele, kwa sauti ya baragumu, na watu kupaza sauti, ukuta ukaanguka; hivyo kila mtu akasonga mbele moja kwa moja kutokea pale alipokuwa kutokea kila upande na kuuteka mji.
”Ndipo Yoshua akararua mavazi yake, akapomoka kifudifudi mbele ya Sanduku la BWANA, akabakia hapo mpaka jioni. Wazee wa Israeli wakafanya vivyo hivyo, wakatia mavumbi vichwani mwao.
”“Sikieni hili, enyi wafalme! Sikilizeni, enyi watawala! Nitamwimbia BWANA, nitaimba; kwa wimbo nitamhimidi BWANA, Mungu wa Israeli.
”Akamjibu, “Kwa nini unauliza Jina langu? Ni Jina la ajabu.” Ndipo Manoa akamchukua mwana-mbuzi, pamoja na sadaka ya unga, naye akamtolea BWANA dhabihu hapo juu ya mwamba. Naye yule malaika wa BWANA akafanya jambo la ajabu wakati Manoa na mkewe wakiwa wanaangalia: Mwali wa moto kutoka hapo madhabahuni ulipowaka kuelekea mbinguni, malaika wa BWANA akapaa ndani ya huo mwali. Manoa na mkewe, kwa kuona jambo hili, wakaanguka chini kifudifudi.
”“Hakuna ye yote aliye mtakatifu kama BWANA, hakuna mwingine zaidi yako; hakuna Mwamba kama Mungu wetu.
”Daudi na nyumba yote ya Israeli walikuwa wanacheza mbele za BWANA kwa nguvu zao zote, kwa nyimbo, vinubi, zeze, matari, kayamba na matoazi.
”Daudi, akiwa amevaa kisibau cha kitani, alicheza mbele za BWANA kwa nguvu zake zote, wakati yeye na nyumba yote ya Israeli walipopandisha Sanduku la BWANA kwa shangwe na sauti za tarumbeta. Ikawa Sanduku la BWANA lilipokuwa linaingia katika Mji wa Daudi, Mikali binti Sauli akachungulia kutoka dirishani. Naye alipoona Mfalme Daudi akirukaruka na kucheza mbele za BWANA, akamdharau moyoni mwake.
”Namwita BWANA, yeye anayestahili kusifiwa, nami ninaokolewa kutoka kwa adui zangu.
”BWANA alinguruma kutoka mbinguni, sauti ya Aliye Juu Sana ilisikika.
”Kwa hiyo nitakusifu wewe, Ee BWANA, katikati ya mataifa; nitaliimbia sifa jina lako.
”Makuhani walipoondoka katika Mahali Patakatifu, wingu likalijaza Hekalu la BWANA. Nao makuhani hawakuweza kufanya huduma yao kwa sababu ya lile wingu, kwa kuwa utukufu wa BWANA ulilijaza Hekalu lake.
”Kisha Solomoni akasimama mbele ya madhabahu ya BWANA machoni pa kusanyiko lote la Israeli, akakunjua mikono yake kuelekea mbinguni na kusema: “Ee BWANA, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe mbinguni juu wala duniani chini, wewe unayetunza Agano lako la upendo pamoja na watumishi wanaodumu katika njia yako kwa moyo wote.
”“Lakini kweli, je, Mungu atafanya makao duniani? Mbingu, hata mbingu zilizo juu sana, haziwezi kukutosha wewe. Sembuse Hekalu hili nililojenga!
”Wakati watu wote walipoona hili, wakaanguka kifudifudi na kulia, “BWANA: yeye ndiye Mungu! BWANA: yeye ndiye Mungu!”
”Mikaya akaendelea, “Kwa hiyo lisikie neno la BWANA: Nilimwona BWANA ameketi juu ya kiti chake cha enzi pamoja na jeshi lote la mbinguni wamesimama kumzunguka kulia kwake na kushoto kwake.
”Naye Hezekia akamwomba BWANA akisema: “Ee BWANA, Mungu wa Israeli, uliyeketi kwenye kiti chako cha enzi kati ya makerubi, wewe peke yako, ndiwe Mungu juu ya falme zote za dunia. Wewe ndiye uliyeumba mbingu na dunia.
”Daudi pamoja na Waisraeli wote walikuwa wanasifu kwa nguvu zao zote mbele za Mungu, kwa nyimbo na kwa vinubi, zeze, matari, matoazi na tarumbeta.
”Daudi akawaambia viongozi wa Walawi kuwaweka ndugu zao waimbaji ili waimbe nyimbo za shangwe, wakiwa na vyombo vya uimbaji: zeze, vinubi na matoazi.
”Basi Daudi alikuwa amevaa joho la kitani safi, kama walivyokuwa wamevaa Walawi wote waliokuwa wanalichukua lile Sanduku, waimbaji nao walivaa vivyo hivyo, pamoja na Kenania aliyekuwa anaongoza nyimbo za waimbaji. Daudi alivaa pia kisibau cha kitani safi. Hivyo Israeli wote wakalipandisha Sanduku la Agano la BWANA kwa shangwe, wakipiga pembe za kondoo waume, tarumbeta, matoazi, wakipiga zeze na vinubi. Wakati Sanduku la Agano la BWANA lilipokuwa linaingia katika Mji wa Daudi, Mikali binti Sauli akachungulia dirishani. Alipomwona Mfalme Daudi akicheza na kusifu, akamdharau moyoni mwake.
”Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake, wajulisheni mataifa yale aliyoyatenda. Mwimbieni yeye, mwimbieni yeye sifa, waambieni matendo yake yote ya ajabu. Utukufu kwa jina lake takatifu, mioyo ya wale wamtafutao BWANA na ifurahi. Mtafuteni BWANA na nguvu zake, utafuteni uso wake siku zote.
”Mwimbieni BWANA dunia yote; tangazeni wokovu wake siku baada ya siku. Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa, matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote. Kwa kuwa BWANA ni mkuu, mwenye kustahili kusifiwa kuliko wote, yeye ni wa kuogopwa kuliko miungu yote. Kwa maana miungu yote ya mataifa ni sanamu, lakini BWANA aliziumba mbingu. Fahari na enzi viko mbele yake, nguvu na utukufu vimo patakatifu pake. Mpeni BWANA, enyi jamaa za mataifa, mpeni BWANA utukufu na nguvu, mpeni BWANA utukufu unaostahili jina lake. Leteni sadaka na mje katika nyua zake; mwabuduni BWANA katika uzuri wa utakatifu wake, Dunia yote na itetemeke mbele zake. Ulimwengu ameuweka imara; hauwezi kusogezwa. Mbingu na zishangilie, nchi na ifurahi; katikati ya mataifa semeni, “BWANA anatawala.” Bahari na ivume na vyote vilivyomo ndani yake; mashamba na yashangilie, na vyote vilivyomo ndani yake. Kisha miti yote ya msituni itaimba kwa furaha, itaimba mbele za BWANA kwa maana anakuja kuihukumu dunia. Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni Mwema, upendo wake wadumu milele. Mlilieni, “Ee Mungu Mwokozi wetu, tuokoe; utukusanye tena kutoka katika mataifa, ili tuweze kulishukuru jina lako takatifu, na kujisifu katika sifa zako.” Atukuzwe BWANA, Mungu wa Israeli, tangu milele na hata milele. Nao watu wote wakasema, “Amen,” na, “Msifuni BWANA.”
”Pia ulikuwa wajibu wao kila asubuhi kumshukuru na kumsifu BWANA. Iliwapasa pia kufanya hivyo jioni
”Daudi akamhimidi BWANA mbele ya kusanyiko lote, akisema: “Uhimidiwe wewe, Ee BWANA, Mungu wa Israeli baba yetu, tangu milele hata milele. Ukuu na uweza, ni vyako, Ee BWANA, na utukufu na enzi na uzuri, kwa kuwa kila kilichoko mbinguni na duniani ni chako wewe. Ee BWANA, ufalme ni wako, umetukuzwa kuwa mkuu juu ya yote. Utajiri na heshima vyatoka kwako, wewe ndiwe utawalaye vitu vyote. Mikononi mwako kuna nguvu na uweza kuinua na kuwapa wote nguvu, Sasa, Mungu wetu, tunakushukuru na kulisifu Jina lako tukufu.
”Basi makuhani wakaondoka hapo mahali patakatifu. Makuhani wote waliokuwa huko walikuwa wamejiweka wakfu, bila kujali migawanyo yao. Walawi wote waliokuwa waimbaji, yaani, Asafu, Hemani, Yeduthuni, wana wa ndugu zao, walisimama upande wa mashariki wa madhabahu, wakiwa wamevaa kitani safi huku wakipiga matoazi, vinubi na zeze. Walikuwa pamoja na makuhani 120 wakipiga tarumbeta. Wapiga tarumbeta na waimbaji wakaungana katika sauti linganifu, ikawa kama vile ni sauti moja, wakimsifu na kumshukuru BWANA, nao alipoinua sauti zao pamoja na tarumbeta na matoazi na vyombo vingine vya uimbaji, wakamsifu BWANA wakisema: “Yeye ni mwema; upendo wake unadumu milele.” Ndipo Hekalu la BWANA likajazwa na wingu, nao makuhani hawakuweza kusimama kufanya huduma yao kwa sababu ya wingu, kwa maana utukufu wa BWANA ulilijaza Hekalu la Mungu.
”Kisha Solomoni akasimama mbele ya madhabahu ya BWANA machoni pa kusanyiko lote la Israeli, naye akakunjua mikono yake. Basi alikuwa ametengeneza jukwaa la shaba, urefu wake dhiraa tano, na upana wake dhiraa tano na kimo chake dhiraa tatu, naye akaliweka katikati ya ukumbi wa nje. Akapanda juu ya hilo jukwaa kisha akapiga magoti mbele ya kushanyiko lote la Israeli, akanyosha mikono yake kwelekea mbinguni. Akasema: “Ee BWANA, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe mbinguni juu wala duniani chini, wewe unayetunza Agano lako la upendo na watumishi wanaodumu katika njia yako kwa moyo wote.
”“Lakini kweli, je, Mungu atafanya makao duniani? Mbingu, hata mbingu zilizo juu sana, haziwezi kukutosha wewe. Sembuse Hekalu hili nililojenga!
”Baada ya Solomoni kumaliza kuomba, moto ukashuka kutoka mbinguni na kuteketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu, nao utukufu wa BWANA ukalijaza Hekalu. Makuhani hawakuweza kuingia ndani ya Hekalu la BWANA kwa sababu utukufu wa BWANA ulilijaza. Waisraeli wote walipoona moto ukishuka na utukufu wa BWANA ukiwa juu ya Hekalu, wakapiga magoti sakafuni wakasujudu nyuso zao mpaka chini, nao wakamwabudu na kumshukuru BWANA wakisema, “Yeye ni mwema; upendo wake unadumu milele.”
”Makuhani wakasimama kwenye nafasi zao, vivyo hivyo Walawi wakiwa na vyombo vya uimbaji vya BWANA ambavyo Mfalme Daudi alikuwa ametengeneza kwa ajili ya kumsifu BWANA, navyo vilitumika wakati aliposhukuru, akisema, “Upendo wake wadumu milele.” Mkabala na Walawi, makuhani walipiga tarumbeta zao, nao Waisraeli wote walikuwa wamesimama.
”Mikaya akaendelea, “Kwa hiyo lisikie neno la BWANA: Nilimwona BWANA ameketi juu ya kiti chake cha enzi pamoja na jeshi lote la mbinguni likiwa limesimama kumzunguka kulia kwake na kushoto kwake.
”Alipomaliza kushauriana na watu, Yehoshafati akawaweka watu wa kumwimbia BWANA na kumsifu katika uzuri wa utakatifu wake walipokuwa wametangulia mbele ya jeshi, wakisema: “Mshukuruni BWANA kwa kuwa upendo wake wadumu milele.”
”Mfalme Hezekia na maafisa wake wakawaamuru Walawi kumsifu BWANA kwa maneno ya Daudi na ya Asafu mwonaji. Hivyo wakaimba sifa kwa furaha nao wakainamisha vichwa vyao na kuabudu.
”Waisraeli waliokuwa Yerusalemu wakaadhimisha Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu kwa muda wa siku saba wakiwa na ala za uimbaji za kumsifu BWANA.
”Wajenzi walipoweka msingi wa Hekalu la BWANA, makuhani wakiwa wamevalia mavazi yao wakiwa na tarumbeta na Walawi (wana wa Asafu) wakiwa na matoazi, walishika nafasi zao za kumtukuza BWANA, kama ilivyoagizwa na Daudi mfalme wa Israeli. Waliimba nyimbo za sifa na za shukrani kwa BWANA hivi: “Yeye ni mwema; upendo wake kwa Israeli wadumu milele.” Watu wote wakapaza sauti kubwa za sifa kwa BWANA, kwa sababu msingi wa nyumba ya BWANA ulikuwa umewekwa.
”Ndipo wakati wa kutoa dhabihu ya jioni nikainuka kutoka katika kujidhili kwangu nikiwa na koti na joho langu lililoraruka, nikapiga magoti mikono yangu ikiwa imeinuliwa kwa BWANA Mungu wangu.
”Ezra akamsifu BWANA, Mungu mkuu, nao watu wote wakainua mikono yao na kuitikia, “Amen! Amen!” Kisha wakasujudu na kumwabudu BWANA hali nyuso zao zikigusa ardhi.
”Walawi wafuatao walikuwa wamesimama kwenye ngazi: Yeshua, Bani, Kadmieli, Shebania, Buni, Sherebia, Bani na Kenani. Hawa walimlilia BWANA Mungu wao kwa sauti kubwa. Nao Walawi Yeshua, Kadmieli, Bani, Hashabnea, Sherebia, Hodia, Shebania na Pethahia wakasema: “Simameni mumsifu BWANA Mungu wenu, yeye ambaye ni Mungu tangu milele hata milele.” “Libarikiwe jina lake tukufu, litukuzwe juu ya baraka zote na sifa. Wewe peke yako ndiwe BWANA. Uliumba mbingu, hata mbingu za mbingu, nalo jeshi lote la angani, dunia na vyote vilivyo ndani yake, bahari na vyote vilivyomo ndani yake. Huvipa vitu vyote uhai, nalo jeshi la mbinguni linakuabudu wewe.
”“Kwa sababu ya huruma zako kuu hukuwaacha jangwani. Wakati wa mchana ile nguzo ya wingu haikukoma kuwaongoza katika njia yao, wala nguzo ya moto haikuacha kuwamulikia usiku njia iliyowapasa kuiendea.
”Wakati wa kuwekwa wakfu ukuta wa Yerusalemu, Walawi walitafutwa huko walikokuwa wakiishi, nao wakaletwa Yerusalemu kuadhimisha kwa shangwe huko kuweka wakfu kwa nyimbo za shukrani na kwa uimbaji kwa kutumia matoazi, vinubi na zeze.
”Kwa muda mrefu uliopita, katika siku za Daudi na Asafu, walikuwepo viongozi wa waimbaji na wa nyimbo za sifa na za kumshukuru Mungu.
”Ndipo Ayubu akasimama, akararua joho lake na kunyoa nywele zake. Kisha akaanguka chini katika kuabudu na kusema: “Nilitoka tumboni mwa mama yangu uchi, nami nitaondoka uchi, BWANA alinipa, naye BWANA ameviondoa, jina la BWANA litukuzwe.”
”“Lakini ingekuwa ni mimi, ningemlalamikia Mungu, ningeliweka shauri langu mbele zake. Yeye hutenda maajabu yasiyoweza kutambuliwa, miujiza isiyoweza kuhesabika.
”“Je, waweza kujua siri za Mungu? Je, waweza kuyachunguza mambo yote kumhusu Mwenyezi?
”“Hata sasa ukiutoa moyo wako kwake na kumwinulia mikono yako,
”Ninajua kwamba Mkombozi wangu yu hai, naye kwamba mwishoni atasimama juu ya nchi. Nami baada ya ngozi yangu kuharibiwa, bado nikiwa na mwili huu nitamwona Mungu; mimi nitamwona kwa macho yangu mwenyewe: mimi, wala si mwingine. Tazama jinsi moyo wangu unavyomtamani sana!
”ndipo Mwenyezi atakuwa dhahabu yako naye atakuwa fedha yako iliyo bora. Hakika ndipo utakapojifurahisha kwa Mwenyezi, nawe utamwinulia Mungu uso wako.
”“Mungu ametukuzwa katika nguvu zake. Ni nani aliye mwalimu kama yeye? Ni nani aliyemwelekeza katika njia zake, au kumwambia, ‘Wewe umetenda yasiyo sawa’? Kumbuka kuzitukuza kazi zake, ambazo watu wamezisifu katika wimbo.
”“Kwa hili moyo wangu unatetemeka, nao unaruka kutoka mahali pake. Sikiliza! Sikiliza ngurumo ya sauti yake, sauti ya ngurumo itokayo kinywani mwake. Huuachilia umeme wake wa radi chini ya mbingu yote na kuupeleka hata miisho ya dunia. Baada ya hayo huja sauti ya ngurumo yake, Mungu hunguruma kwa sauti yake ya fahari. Wakati sauti yake ingurumapo tena, huuachilia umeme wake wa radi. Sauti ya Mungu hunguruma kwa jinsi ya ajabu, hutenda mambo makuu kupita ufahamu wetu.
”Je, wajua jinsi mawingu yanavyokaa yakiwa yametulia, hayo maajabu yake yeye aliyemkamilifu katika maarifa?
”Kutoka kaskazini yeye huja na fahari kuu, Mungu huja katika utukufu wa kutisha. Yeye Mwenyezi hatuwezi kumfikia, naye ametukuzwa katika uweza; katika hukumu zake na haki yake kuu, hataonea.
”Yeye atawalaye mbinguni hucheka, Bwana huwadharau.
”“Nimemtawaza mfalme wangu juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.”
”Nitamshukuru BWANA kwa ajili ya haki yake, na nitaliimbia sifa jina la BWANA Aliye Juu Sana.
”(Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Gitithi. Zaburi Ya Daudi) Ee BWANA, Bwana wetu, tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote! Umeuweka utukufu wako juu ya mbingu.
”Ee BWANA, Bwana wetu, tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!
”(Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Muth-Labeni. Zaburi Ya Daudi) Ee BWANA, nitakutukuza kwa moyo wangu wote, nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu. Nitafurahi na kushangilia katika wewe, nitaliimbia sifa jina lako, Ewe Uliye Juu Sana.
”Mwimbieni BWANA sifa, amefanywa mtawala Sayuni, tangazeni miongoni mwa mataifa, yale aliyoyatenda.
”ili niweze kutangaza sifa zako katika malango ya Binti Sayuni na huko niushangilie wokovu wako.
”BWANA ni Mfalme milele na milele, mataifa wataangamia watoke nchini mwake.
”BWANA yuko ndani ya Hekalu lake takatifu; BWANA yuko kwenye kiti chake cha enzi mbinguni. Huwaangalia wana wa watu, macho yake yanawajaribu.
”Nitamwimbia BWANA, kwa kuwa amekuwa mwema kwangu.
”Nilinde kama mboni ya jicho lako, unifiche chini ya kivuli cha mbawa zako
”(Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Daudi Mtumishi Wa Mungu Aliyomwimbia Mungu Wakati Mungu Alipomwokoa Mkononi Mwa Sauli Na Adui Wengine) Nakupenda wewe, Ee BWANA, nguvu yangu. BWANA ni mwamba wangu, ngome yangu na mwokozi wangu, Mungu wangu ni mwamba, ambaye kwake ninakimbilia. Yeye ni ngao yangu na pembe ya wokovu wangu, ngome yangu. Ninamwita BWANA anayestahili kusifiwa, nami nimeokoka kutoka kwa adui zangu.
”BWANA alinguruma kutoka mbinguni, sauti ya Aliye Juu Sana ilisikika.
”Kuhusu Mungu, njia yake ni kamilifu, neno la BWANA ni kamili. Yeye ni ngao kwa wote wanaokimbilia kwake. Kwa maana ni nani aliye Mungu zaidi ya BWANA? Ni nani aliye Mwamba isipokuwa Mungu wetu?
”BWANA yu hai! Sifa ni kwa Mwamba wangu! Atukuzwe Mungu Mwokozi wangu!
”(Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Daudi) Mbingu zinatangaza utukufu wa Mungu, anga zahubiri kazi ya mikono yake.
”Ee BWANA, utukuzwe katika nguvu zako, tutaimba na kusifu nguvu zako.
”Hata hivyo umesimikwa katika kiti cha enzi kama Mtakatifu; wewe ni sifa ya Israeli.
”Nitalitangaza jina lako kwa ndugu zangu, katika kusanyiko nitakusifu wewe. Ninyi ambao mnamcha BWANA msifuni! Ninyi nyote wazao wote wa Yakobo, mheshimuni yeye! Mcheni yeye, ninyi wazao wote wa Israeli! Kwa maana hakupuuza wala kudharau mateso ya aliyeonewa; hakumficha uso wake bali alisikiliza kilio chake ili amsaidie. Kwako wewe hutoka kiini cha sifa zangu katika kusanyiko kubwa, nitatimiza nadhiri zangu mbele ya wale wakuchao wewe. Maskini watakula na kushiba, wale wamtafutao BWANA watamsifu, mioyo yenu na iishi milele! Miisho yote ya dunia itakumbuka na kumgeukia BWANA, nazo jamaa zote za mataifa watasujudu mbele zake, kwa maana ufalme ni wa BWANA naye hutawala juu ya mataifa. Matajiri wote wa dunia watasherehekea na kuabudu; wote waendao mavumbini watapiga magoti mbele yake, wote ambao hawawezi kudumisha uhai wao.
”Inueni vichwa vyenu, enyi malango, inukeni enyi milango ya kale, ili mfalme wa utukufu apate kuingia. Ni nani huyu Mfalme wa utukufu? Ni BWANA aliye na nguvu na uweza, ni BWANA aliye hodari katika vita. Inueni vichwa vyenu, enyi malango, viinueni juu enyi milango ya kale, ili mfalme wa utukufu apate kuingia. Ni nani huyu, huyu mfalme wa utukufu? Ni BWANA Mwenye Nguvu Zote; yeye ndiye Mfalme wa utukufu.
”Jambo moja ninamwomba BWANA, hili ndilo ninalolitafuta: niweze kukaa nyumbani mwa BWANA siku zote za maisha yangu, niutazame uzuri wa BWANA na kumtafuta hekaluni mwake.
”Kisha kichwa changu kitainuliwa juu ya adui zangu wanaonizunguka; katika maskani yake nitatoa dhabihu kwa kelele za shangwe; nitamwimbia BWANA na kumsifu. Uisikie sauti yangu nikuitapo, Ee BWANA, unihurumie na unijibu. Moyo wangu unasema kuhusu wewe, “Utafute uso wake!” Uso wako, BWANA “Nitautafuta.”
”BWANA ni nguvu zangu na ngao yangu, moyo wangu umemtumaini yeye, nami nimesaidiwa. Moyo wangu unarukaruka kwa furaha nami nitamshukuru kwa wimbo.
”(Zaburi Ya Daudi) Mpeni BWANA Enyi mashujaa, mpeni BWANA utukufu na nguvu. Mpeni BWANA utukufu unaostahili jina lake; mwabuduni BWANA katika uzuri wa utakatifu wake. Sauti ya BWANA iko juu ya maji; Mungu wa utukufu hupiga radi, BWANA hupiga radi juu ya maji makuu. Sauti ya BWANA ina nguvu; sauti ya BWANA ni tukufu.
”Sauti ya BWANA huzalisha ayala, na huuacha msitu wazi. Hekaluni mwake wote wasema, “Utukufu!” BWANA huketi akiwa ametawazwa juu ya gharika; BWANA ametawazwa kuwa Mfalme milele.
”Mwimbieni BWANA, enyi watakatifu wake; lisifuni jina lake takatifu, kwa kumbukumbu la utakatifu wake.
”Uligeuza maombolezo yangu kuwa kucheza, ulinivua nguo za gunia ukanivika shangwe, ili moyo wangu uweze kukusifu na usikae kimya. Ee BWANA Mungu wangu, nitakushukuru milele.
”Mwimbieni BWANA kwa furaha, enyi wenye haki; kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo. Msifuni BWANA kwa kinubi, mwimbieni sifa kwa zeze la nyuzi kumi. Mwimbieni wimbo mpya; pigeni kwa ustadi, pigeni kelele za furaha.
”(Zaburi Ya Daudi, Alipojifanya Mwendawazimu Mbele Ya Abimeleki, Ambaye Alimfukuza, Naye Akaondoka) Nitamtukuza BWANA nyakati zote, sifa zake zitakuwa midomoni mwangu siku zote. Nafsi yangu itajisifu katika BWANA walioonewa wasikie na wafurahi. Mtukuzeni BWANA pamoja nami, naam, na tulitukuze jina lake pamoja.
”Nami nitakushukuru mbele ya kusanyiko kubwa, nitakusifu katikati ya watu wengi.
”Wale wanaofurahia hukumu yangu ya haki na wapige kelele za shangwe na furaha; hebu waseme siku zote, “BWANA atukuzwe, ambaye amefurahia mafanikio ya mtumishi wake.” Ulimi wangu utanena haki yako na sifa zako mchana kutwa.
”Akaweka wimbo mpya kinywani mwangu, wimbo wa sifa kwa Mungu wetu. Wengi wataona na kuogopa na kuweka tumaini lao kwa BWANA.
”Bali wote wakutafutao washangilie na kukufurahia, wale wapendao wokovu wako siku zote waseme, “BWANA atukuzwe!”
”Katika uadilifu wangu unanitegemeza na kuniweka kwenye uwepo wako milele. Msifuni BWANA, Mungu wa Israeli, tangu milele na hata milele. Amen na Amen.
”(Kwa Mwimbishaji: Utenzi Wa Wana Wa Kora) Kama vile paa aoneavyo shauku vijito vya maji, ndivyo nafsi yangu ikuoneavyo shauku, Ee Mungu. Nafsi yangu inamwonea Mungu kiu, Mungu aliye hai. Ni lini nitaweza kwenda kukutana na Mungu?
”Mchana BWANA huelekeza upendo wake, usiku wimbo wake uko nami: maombi kwa Mungu wa uzima wangu.
”Ndipo nitakwenda madhabahuni pa Mungu, kwa Mungu, furaha yangu na shangwe yangu. Nitakusifu kwa kinubi, Ee Mungu, Mungu wangu.
”Jifunge upanga wako pajani mwako, Ee mwenye nguvu, jivike fahari na utukufu. Katika fahari yako songa mbele kwa ushindi, kwa ajili ya kweli, unyenyekevu na haki, mkono wako wa kuume na uonyeshe matendo ya kutisha.
”Ee Mungu, kiti chako cha enzi kitadumu milele na milele, fimbo ya utawala wa haki itakuwa fimbo ya utawala wa ufalme wako.
”Nitadumisha kumbukumbu lako katika vizazi vyote, kwa hiyo mataifa watakusifu milele na milele.
”“Tulieni, mjue ya kwamba mimi ndimi Mungu; nitatukuzwa katikati ya mataifa, nitatukuzwa katika dunia.”
”(Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Wana Wa Kora) Pigeni makofi, enyi mataifa yote, mpigieni Mungu kelele za shangwe! Jinsi gani alivyo wa kutisha, BWANA Aliye Juu Sana, Mfalme mkuu juu ya dunia yote.
”Mungu amepaa katikati ya kelele za shangwe, BWANA katikati ya sauti za tarumbeta. Mwimbieni Mungu sifa, imbeni sifa, mwimbieni sifa Mfalme wetu, imbeni sifa. Kwa kuwa Mungu ni mfalme wa dunia yote, mwimbieni zaburi za sifa. Mungu anatawala juu ya mataifa, Mungu ameketi juu ya kiti chake cha enzi kitakatifu. Wakuu wa mataifa wanakusanyika kama watu wa Mungu wa Abrahamu, kwa kuwa wafalme wa dunia ni mali ya Mungu; yeye ametukuka sana.
”(Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Wana Wa Kora) BWANA ni mkuu na anayestahili kusifiwa sana, katika mji wa Mungu wetu, mlima wake mtakatifu.
”Kwa kuwa huyu Mungu ni Mungu wetu milele na milele; atakuwa kiongozi wetu hata mwisho.
”Toa sadaka za shukrani kwa Mungu, timiza nadhiri zako kwake Yeye Aliye Juu Sana, na uniite siku ya taabu; nami nitakuokoa, nawe utanitukuza.”
”Atoaye dhabihu za shukrani ananiheshimu mimi, naye aiandaa njia yake jinsi ipasavyo nitamwonyesha wokovu wa Mungu.”
”Ee Mungu, Mungu uniokoaye, niokoe na hatia ya kumwaga damu, ulimi wangu utaimba juu ya haki yako. Ee BWANA, fungua midomo yangu, na kinywa changu kitatangaza sifa zako.
”Ee Mungu, utukuzwe, juu mbinguni, utukufu wako na uenee duniani kote.
”Ee Mungu, moyo wangu uko imara, naam moyo wangu uko imara, nitaimba na kupiga vinanda.
”Lakini mimi nitaimba juu ya nguvu zako, wakati wa asubuhi nitaimba juu ya upendo wako; kwa maana wewe ndiwe ngome yangu na kimbilio langu wakati wa shida. Ee uliye Nguvu zangu, ninakuimbia sifa, wewe, Ee Mungu ndiwe ngome yangu, Mungu unipendaye.
”Ndipo daima nitaliimbia sifa jina lako na kuzitimiza nadhiri zangu siku baada ya siku.
”(Zaburi Ya Daudi Wakati Alipokuwa Katika Jangwa La Yuda) Ee Mungu, wewe ni Mungu wangu, nakutafuta kwa moyo wote; nafsi yangu inakuonea kiu, mwili wangu unakuonea wewe shauku, katika nchi kame na iliyochoka mahali ambapo hapana maji. Nimekuona katika mahali patakatifu na kuuona uwezo wako na utukufu wako. Kwa sababu upendo wako ni bora kuliko uhai, midomo yangu itakuadhimisha. Nitakusifu siku zote za maisha yangu, na kwa jina lako nitainua mikono yangu. Nafsi yangu itatoshelezwa kama kwa wingi wa vyakula; kwa midomo iimbayo kinywa changu kitakusifu wewe. Kitandani mwangu ninakukumbuka wewe, ninawaza juu yako makesha yote ya usiku.
”Bali mfalme atafurahi katika Mungu, wale wote waapao kwa jina la Mungu watamsifu, bali vinywa vya waongo vitanyamazishwa.
”(Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Daudi. Wimbo) Ee Mungu, sifa zakungojea katika Sayuni; kwako wewe nadhiri zetu zitatimizwa.
”(Kwa Mwimbishaji: Wimbo. Zaburi) Mpigieni Mungu kelele za shangwe, dunia yote! Imbeni utukufu wa jina lake; mpeni sifa zake kwa utukufu! Mwambieni Mungu, “Jinsi gani yalivyo ya kutisha matendo yako! Uwezo wako ni mkuu mno kiasi kwamba adui wananyenyekea mbele zako. Dunia yote yakusujudia, wanakuimbia wewe sifa, wanaliimbia sifa jina lako.”
”Yeye hutawala kwa uwezo wake milele, macho yake huangalia mataifa yote, waasi na wasithubutu kujiinua dhidi yake. Enyi mataifa, msifuni Mungu wetu, sauti ya sifa yake na isikike,
”Mwimbieni Mungu, liimbieni sifa jina lake, mwinueni juu yeye aendeshwaye juu ya mawingu, jina lake ni BWANA, furahini mbele zake.
”dunia ilitikisika, mbingu zikanyesha mvua, mbele za Mungu, Mungu wa Mlima Sinai, mbele za Mungu, Mungu wa Israeli.
”Mwimbieni Mungu, enyi falme za dunia, mwimbieni Bwana sifa, mwimbieni sifa yeye apandaye mbingu za kale zilizo juu, yeye angurumaye kwa sauti kuu. Tangazeni uwezo wa Mungu, ambaye fahari yake iko juu ya Israeli, ambaye uwezo wake uko katika anga. Ee Mungu, wewe unatisha katika mahali patakatifu pako, Mungu wa Israeli huwapa watu wake uwezo na nguvu. Mungu Asifiwe!
”Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo, nami nitamtukuza kwa kumtolea shukrani.
”Mbingu na dunia na vimsifu, bahari na vyote viendavyo ndani yake,
”Lakini wote wakutafutao na washangilie na kukufurahia, wale wapendao wokovu wako daima na waseme, “Mungu na atukuzwe!”
”Tangu kuzaliwa nimekutegemea wewe, ulinitoa tumboni mwa mama yangu. Nitakusifu wewe daima. Nimekuwa kama kioja kwa wengi, lakini wewe ni kimbilio langu imara. Kinywa changu kimejazwa sifa zako, nikitangaza utukufu wako mchana kutwa.
”Lakini mimi, nitatumaini siku zote, nitakusifu zaidi na zaidi.
”Ee Mungu wangu, nitakusifu kwa kinubi kwa ajili ya uaminifu wako; Ee Mtakatifu Pekee wa Israeli, nitakuimbia sifa kwa zeze. Midomo yangu itapaza sauti kwa furaha ninapokuimbia sifa, mimi, ambaye umenikomboa.
”Makabila ya jangwani watamsujudia, na adui zake wataramba mavumbi.
”Wafalme wote watamsujudia na mataifa yote yatamtumikia.
”Jina lake na lidumu milele, na lidumu kama jua. Mataifa yote yatabarikiwa kupitia yeye, nao watamwita mbarikiwa. BWANA Mungu, Mungu wa Israeli, apewe sifa, yeye ambaye peke yake hutenda mambo ya ajabu. Jina lake tukufu lisifiwe milele, ulimwengu wote ujae utukufu wake. Amen na Amen.
”Nitayakumbuka matendo ya BWANA; naam, nitaikumbuka miujiza yako ya zamani. Nitazitafakari kazi zako zote na kuyawaza matendo yako makuu. Ee Mungu, njia zako ni takatifu. Ni mungu yupi aliye mkuu kama Mungu wetu? Wewe ndiwe Mungu utendaye miujiza, umeonyesha uwezo wako katikati ya mataifa.
”Aliwaongoza kwa wingu mchana na kwa nuru kutoka kwenye moto usiku kucha.
”Walikumbuka kwamba Mungu alikuwa Mwamba wao, kwamba Mungu Aliye Juu Sana alikuwa Mkombozi wao.
”(Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Gitithi. Zaburi Ya Asafu) Mwimbieni kwa furaha Mungu aliye nguvu yetu; mpigieni kelele za shangwe Mungu wa Yakobo! Anzeni wimbo, pigeni matari, pigeni kinubi na zeze kwa sauti nzuri.
”Na wajue kwamba wewe, ambaye jina lako ni BWANA, kwamba wewe peke yako ndiwe Uliye Juu Sana ya dunia yote.
”(Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Gitithi. Zaburi Ya Wana Wa Kora) Ee BWANA Mwenye Nguvu Zote, makao yako yapendeza kama nini! Nafsi yangu inatamani sana, naam, hata kuona shauku, kwa ajili ya nyua za BWANA; moyo wangu na mwili wangu vinamlilia Mungu Aliye Hai. Hata shomoro amejipatia makao, mbayuwayu amejipatia kiota mahali awezapo kuweka makinda yake: mahali karibu na madhabahu yako, Ee BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mfalme wangu na Mungu wangu. Heri wale wanaokaa nyumbani mwako, wanaokusifu wewe daima.
”Ee BWANA, mataifa yote uliyoyafanya yatakuja na kuabudu mbele zako; wataliletea utukufu jina lako. Kwa maana wewe ni mkuu na unafanya mambo ya ajabu; wewe peke yako ndiwe Mungu. Ee BWANA, nifundishe njia yako, nami nitakwenda katika kweli yako; nipe moyo usiositasita, ili niweze kulicha jina lako. Ee BWANA, wangu, nitakusifu kwa moyo wote; nitaliadhimisha jina lako milele.
”Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba, “Chemchemi zangu zote ziko kwako.”
”nuru ya macho yangu imefifia kwa ajili ya huzuni. Ee BWANA, ninakuita kila siku, ninakunyoshea wewe mikono yangu.
”(Utenzi Wa Ethani Wa Jamii Ya Ezra) Nitaimba juu ya upendo mkuu wa BWANA milele; kwa kinywa changu nitajulisha uaminifu wako ujulikane kwa vizazi vyote.
”Ee BWANA, mbingu zinayasifu maajabu yako, uaminifu wako pia, katika kusanyiko la watakatifu. Kwa kuwa ni nani katika mbingu juu anayeweza kulinganishwa na BWANA? Ni nani miongoni mwa viumbe vya mbinguni aliye kama BWANA? Katika kusanyiko la watakatifu Mungu huogopwa sana, anahofiwa kuliko wote wanaomzunguka.
”Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chako cha enzi; upendo na uaminifu vinakutangulia.
”Kwa kuwa wewe ni utukufu na nguvu yao, kwa wema wako unatukuza pembe yetu. Naam, ngao yetu ni mali ya BWANA, aliye Mtakatifu Pekee wa Israeli ni mfalme wetu.
”(Maombi Ya Mose, Mtu Wa Mungu) BWANA, wewe umekuwa makao yetu katika vizazi vyote. Kabla ya kuzaliwa milima au hujaumba dunia na ulimwengu, wewe ni Mungu tangu milele hata milele.
”Yeye akaaye mahali pa salama pake Yeye Aliye Juu Sana, atadumu katika uvuli wake Mwenyezi.
”(Zaburi: Wimbo Wa Sabato) Ni vyema kumshukuru BWANA na kuliimbia jina lako, Ee Uliye Juu Sana,
”BWANA anatawala, amejivika utukufu; BWANA amejivika utukufu tena amejivika nguvu. Dunia imewekwa imara, haitaondoshwa. Kiti chako cha enzi kimekuwa thabiti tangu zamani; wewe umekuwako tangu milele. Bahari zimeinua, Ee BWANA, bahari zimeinua sauti zake; bahari zimeinua sauti za mawimbi yake. Yeye ni mkuu kuliko ngurumo ya maji makuu, ni mkuu kuliko mawimbi ya bahari: BWANA aishiye juu sana ni mkuu. Ee BWANA, sheria zako ni imara; utakatifu umepamba nyumba yako pasipo mwisho.
”Njoni, tumwimbie BWANA kwa furaha; tumfanyie kelele za shangwe Mwamba wa wokovu wetu. Tuje mbele zake kwa shukrani, tumtukuze kwa vinanda na nyimbo. Kwa kuwa BWANA ni Mungu mkuu, mfalme mkuu juu ya miungu yote.
”Njoni, tusujudu tumwabudu, tupige magoti mbele za BWANA Muumba wetu,
”Mwimbieni BWANA wimbo mpya; mwimbieni BWANA dunia yote. Mwimbieni BWANA, lisifuni jina lake; tangazeni wokovu wake siku baada ya siku. Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa, matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote. Kwa kuwa BWANA ni mkuu mwenye kustahili kusifiwa kuliko wote; yeye ni wa kuogopwa kuliko miungu yote. Kwa maana miungu yote ya mataifa ni sanamu, lakini BWANA aliziumba mbingu. Fahari na enzi viko mbele yake; nguvu na utukufu vimo patakatifu pake. Mpeni BWANA, enyi jamaa za mataifa, mpeni BWANA utukufu na nguvu. Mpeni BWANA utukufu unaostahili jina lake; leteni sadaka na mje katika nyua zake. Mwabuduni BWANA katika uzuri wa utakatifu wake; dunia yote na itetemeke mbele zake. Katikati ya mataifa semeni, “BWANA anatawala.” Ulimwengu ameuweka imara hauwezi kusogezwa, atawahukumu mataifa kwa uadilifu. Mbingu na zishangilie, nchi na ifurahi; bahari na ivume, na vyote vilivyomo ndani yake; mashamba na yashangilie, pamoja na vyote vilivyomo ndani yake. Kisha miti yote ya msituni itaimba kwa furaha, vitaimba mbele za BWANA kwa maana anakuja, anakuja kuhukumu dunia. Ataihukumu dunia kwa haki na mataifa katika kweli yake.
”BWANA anatawala, nchi na ifurahi, visiwa vyote vishangilie. Mawingu na giza nene vinamzunguka, haki na hukumu ndio msingi wa kiti chake cha enzi.
”Milima huyeyuka kama nta mbele za BWANA, mbele za Bwana wa dunia yote. Mbingu zinatangaza haki yake, na mataifa yote huona utukufu wake.
”Kwa kuwa wewe, Ee BWANA, ndiwe Uliye Juu Sana kuliko dunia yote; umetukuka sana juu ya miungu yote.
”Mwimbieni BWANA wimbo mpya, kwa maana ametenda mambo ya ajabu; kitanga chake cha kuume na mkono wake mtakatifu umemfanyia wokovu.
”Mpigieni kelele za shangwe, dunia yote, ipaze sauti kwa nyimbo za shangwe na vinanda; mwimbieni BWANA kwa kinubi, kwa kinubi na sauti za kuimba, kwa tarumbeta na mvumo wa baragumu za pembe za kondoo dume: shangilieni kwa furaha mbele za BWANA, aliye Mfalme. Bahari na ivume na kila kiliomo ndani yake, dunia na wote wakaao ndani yake. Mito na ipige makofi, milima na iimbe pamoja kwa furaha,
”BWANA anatawala, mataifa na yatetemeke; anaketi kwenye kiti cha enzi katikati ya makerubi, dunia na itikisike. BWANA ni mkuu katika Sayuni; ametukuzwa juu ya mataifa yote. Wanalisifu jina lako ambalo ni kuu na la kuogopwa: yeye ni mtakatifu! Mfalme mwenye nguvu hupenda haki, wewe umethibitisha adili; katika Yakobo umefanya yaliyo haki na sawa. Mtukuzeni BWANA Mungu wetu, na mkaabudu katika mahali pa kuwekea miguu yake; yeye ni mtakatifu.
”Mtukuzeni BWANA Mungu wetu na mwabudu kwenye mlima wake mtakatifu, kwa maana BWANA Mungu wetu ni mtakatifu.
”(Zaburi Ya Shukrani) Mpigieni BWANA kelele za shangwe, dunia yote. Mwabuduni BWANA kwa furaha; njoni mbele zake kwa nyimbo za shangwe. Jueni kwamba BWANA ndiye Mungu. Yeye ndiye aliyetuumba, sisi tu mali yake; sisi tu watu wake, kondoo wa malisho yake. Ingieni malangoni mwake kwa shukrani na katika nyua zake kwa kusifu, mshukuruni yeye na kulisifu jina lake. Kwa maana BWANA ni mwema na upendo wake wadumu milele; uaminifu wake unadumu kwa vizazi vyote.
”(Zaburi Ya Daudi) Nitaimba juu ya upendo wako na haki yako; kwako wewe, Ee BWANA, nitaimba sifa.
”Mataifa wataogopa jina la BWANA, wafalme wote wa dunia watauheshimu utukufu wako. Kwa maana BWANA ataijenga tena Sayuni na kutokea katika utukufu wake.
”Hapo mwanzo uliweka misingi ya dunia, na mbingu ni kazi ya mikono yako. Hivi vitatoweka, lakini wewe utadumu, vyote vitachakaa kama vazi. Utavibadilisha kama nguo navyo vitaondoshwa. Lakini wewe, U yeye yule, nayo miaka yako haikomi kamwe.
”(Zaburi Ya Daudi) Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA, vyote vilivyomo ndani yangu vilihimidi jina lake takatifu. Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA, wala usisahau wema wake wote,
”BWANA ameweka imara kiti chake cha enzi mbinguni, ufalme wake unatawala juu ya vyote.
”Mhimidini BWANA, enyi malaika zake, ninyi mlio mashujaa mnaozitii amri zake, ninyi mnaotii neno lake. Mhimidini BWANA, ninyi jeshi lake lote la mbinguni, ninyi watumishi wake mnaofanya mapenzi yake. Mhimidini BWANA, kazi zake zote kila mahali katika milki yake. Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA.
”Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA. Ee BWANA Mungu wangu, wewe ni mkuu sana, umejivika utukufu na enzi. Amejifunika katika nuru kama vile kwa vazi, amezitandaza mbingu kama hema
”Ee BWANA, jinsi gani zilivyo nyingi kazi zako! Kwa hekima ulizifanya zote, dunia imejaa viumbe vyako. Pale iko bahari, kubwa na yenye nafasi tele, imejaa viumbe visivyo na idadi, vitu vyenye uhai vikubwa na vidogo.
”Utukufu wa BWANA na udumu milele, BWANA na azifurahie kazi zake, yeye aitazamaye dunia, nayo ikatetemeka, aigusaye milima nayo ikatoa moshi. Nitamwimbia BWANA maisha yangu yote; nitaimba sifa kwa Mungu wangu muda wote ninaoishi. Kutafakari kwangu na kumpendeze yeye, ninapofurahi katika BWANA. Lakini wenye dhambi na watoweke katika dunia na waovu wasiwepo tena. Ee nafsi yangu, Msifu BWANA. Mhimidini BWANA.
”Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake, wajulisheni mataifa yale aliyoyatenda. Mwimbieni yeye, mwimbieni yeye sifa, waambieni matendo yake yote ya ajabu. Utukufu kwa jina lake takatifu, mioyo ya wale wamtafutao BWANA na ifurahi. Mtafuteni BWANA na nguvu zake, utafuteni uso wake siku zote. Kumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya, miujiza yake na hukumu alizozitamka.
”Msifuni BWANA. Mshukuruni BWANA, kwa kuwa ni mwema; upendo wake wadumu milele. Ni nani awezaye kusimulia matendo makuu ya BWANA au kutangaza kikamilifu sifa zake?
”Ee BWANA Mungu wetu, utuokoe, utukusanye tena kutoka kwa mataifa, ili tuweze kulishukuru jina lako takatifu na kujisifu katika sifa zako. Atukuzwe BWANA, Mungu wa Israeli, tangu milele na hata milele. Watu wote na waseme, “Amen!” Msifuni BWANA.
”Mshukuruni BWANA, kwa kuwa yeye ni mwema, upendo wake wadumu milele.
”Na wamtukuze yeye katika kusanyiko la watu, na wamsifu katika baraza la wazee.
”(Zaburi Ya Daudi. Wimbo) Ee Mungu, moyo wangu ni thabiti, nitaimba na kusifu kwa moyo wangu wote. Amka, kinubi na zeze! Nitayaamsha mapambazuko. Ee BWANA, nitakusifu katikati ya mataifa, nitaimba sifa zako katikati ya mataifa. Kwa maana upendo wako ni mkuu, juu kuliko mbingu, uaminifu wako hufika mpaka angani. Ee Mungu, utukuzwe, juu ya mbingu, utukufu wako na uwe duniani pote.
”Kwa kinywa changu nitamtukuza sana BWANA katika umati mkubwa nitamsifu.
”Msifuni BWANA. Nitamtukuza BWANA kwa moyo wangu wote, katika baraza la wanyofu na katika kusanyiko. Kazi za BWANA ni kuu, wote wanaopendezwa nazo huzitafakari. Kazi zake zimejaa fahari na utukufu, haki yake hudumu daima.
”Aliwapa watu wake ukombozi, aliamuru Agano lake milele, jina lake ni takatifu na la kuogopwa. Kumcha BWANA ndicho chanzo cha hekima, wote wanaozifuata amri zake wana busara. Sifa zake zadumu milele.
”Msifuni BWANA. Enyi watumishi wa BWANA msifuni, lisifuni jina la BWANA. Jina la BWANA na lisifiwe, sasa na hata milele. Kuanzia maawio ya jua hadi machweo yake, jina la BWANA linapaswa kusifiwa.
”BWANA ametukuka juu ya mataifa yote, utukufu wake juu ya mbingu. Ni nani aliye kama BWANA Mungu wetu, Yeye ambaye ameketi juu kwenye kiti cha enzi, ambaye huinama atazame chini aone mbingu na nchi?
”Sio kwetu sisi, Ee BWANA, sio kwetu sisi bali utukufu ni kwa jina lako, kwa sababu ya upendo na uaminifu wako.
”bali ni sisi tunaomtukuza BWANA, sasa na hata milele. Msifuni BWANA.
”Nitakutolea dhabihu ya kukushukuru na kuliita jina la BWANA. Nitazitimiza nadhiri zangu kwa BWANA mbele za watu wake wote, katika nyua za nyumba ya BWANA, katikati yako, Ee Yerusalemu. Msifuni BWANA.
”Msifuni BWANA, enyi mataifa yote; mtukuzeni yeye, enyi watu wote. Kwa kuwa upendo wake kwetu ni mkuu, uaminifu wa BWANA unadumu milele. Msifuni BWANA.
”Wote wamchao BWANA na waseme sasa: “Upendo wake wadumu milele.”
”Mkono wa kuume wa BWANA umeinuliwa juu, mkono wa kuume wa BWANA umetenda mambo makuu!”
”Nitakushukuru, kwa kuwa ulinijibu, umekuwa wakovu wangu. Jiwe walilolikataa waashi, limekuwa jiwe kuu la pembeni. BWANA ametenda hili, nalo ni la kushangaza machoni petu. Hii ndiyo siku BWANA aliyoifanya, tushangilie na kufurahi ndani yake.
”Wewe ni Mungu wangu, nitakushukuru, wewe ni Mungu wangu, nitakutukuza. Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema; upendo wake wadumu milele.
”Nitakusifu kwa moyo mnyofu ninapojifunza sheria zako za haki.
”Usiku wa manane ninaamka kukushukuru kwa sababu ya sheria zako za haki.
”Ninakusifu mara saba kwa siku, kwa ajili ya sheria zako za haki.
”Midomo yangu na ibubujike sifa, kwa kuwa unanifundisha maagizo yako.
”“Twendeni kwenye makao yake, na tuabudu kwenye kiti cha kuwekea miguu yake;
”Inueni mikono yenu katika mahali patakatifu na mumsifu BWANA.
”Msifuni BWANA. Lisifuni jina la BWANA, msifuni, enyi watumishi wa BWANA, ninyi ambao mnatumika ndani ya nyumba ya BWANA, katika nyua za nyumba ya Mungu wetu. Msifuni BWANA, kwa kuwa BWANA ni mwema, liimbieni sifa jina lake, kwa maana hilo lapendeza.
”Msifuni BWANA kutoka Sayuni, msifuni yeye aishiye Yerusalemu. Msifuni BWANA.
”Mshukuruni Mungu wa miungu. Fadhili zake zadumu milele. Mshukuruni Bwana wa mabwana: Fadhili zake zadumu milele.
”Mshukuruni Mungu wa mbinguni, Fadhili zake zadumu milele.
”(Zaburi Ya Daudi) Nitakusifu wewe, Ee BWANA, kwa moyo wangu wote, mbele ya “miungu” nitaimba sifa zako. Nitasujudu nikielekea Hekalu lako takatifu, nami nitalisifu jina lako kwa ajili ya upendo wako na uaminifu, kwa kuwa umelikuza jina lako na neno lako juu ya vitu vyote. Nilipoita, ulinijibu; ulinifanya jasiri na mwenye moyo hodari. Wafalme wote wa dunia, na wakusifu wewe Ee BWANA, wakati wanaposikia maneno ya kinywa chako. Wao na waimbe kuhusu njia za BWANA, kwa maana utukufu wa BWANA ni mkuu.
”Ninakusifu kwa sababu nimeumbwa kwa namna ya ajabu na ya kutisha; kazi zako ni za ajabu, ninajua hayo kikamilifu.
”Nanyosha mikono yangu kwako, nafsi yangu inakuonea kiu kama ardhi kame.
”Ee Mungu, nitakuimbia wimbo mpya, kwa zeze yenye nyuzi kumi nitakuimbia,
”(Wimbo Wa Sifa. Wa Daudi) Nitakutukuza wewe, Mungu wangu Mfalme, nitalisifu jina lako milele na milele. Kila siku nitakusifu na kulitukuza jina lako milele na milele. BWANA ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana, ukuu wake haupimiki. Kizazi kimoja kitasifia kazi zako kwa kizazi kingine, watasimulia matendo yako makuu. Watasema juu ya utukufu wa fahari ya ukuu wako, nami nitatafakari juu ya kazi zako za ajabu. Watasimulia uwezo wa kazi zako za kutisha, nami nitatangaza matendo yako makuu. Wataadhimisha wema wako mwingi na wataimba kwa shangwe juu ya haki yako.
”Ee BWANA, vyote ulivyovifanya vitakusifu, watakatifu wako watakutukuza. Watasimulia utukufu wa ufalme wako na kusema juu ya ukuu wako, ili watu wote wajue matendo yako makuu na utukufu wa fahari ya ufalme wako. Ufalme wako ni ufalme wa milele, mamlaka yako hudumu vizazi vyote. BWANA ni mwaminifu kwa ahadi zake zote na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya.
”Kinywa changu kitazinena sifa za BWANA. Kila kiumbe na kilisifu jina lake takatifu milele na milele.
”Msifuni BWANA! Ee nafsi yangu, umsifu BWANA, Nitamsifu BWANA maisha yangu yote; nitamwimbia Mungu wangu sifa wakati wote niishipo.
”BWANA atamiliki milele, Mungu wako, Ee Sayuni, kwa vizazi vyote. Msifuni BWANA.
”Msifuni BWANA. Tazama jinsi ilivyo vyema kumwimbia Mungu wetu sifa, jinsi inavyopendeza na kustahili kumsifu yeye!
”Huzihesabu nyota na huipa kila moja jina lake. Bwana wetu ni mkuu na mwenye uwezo mwingi, ufahamu wake hauna kikomo. BWANA huwahifadhi wanyenyekevu lakini huwashusha waovu mpaka mavumbini. Mwimbieni BWANA kwa shukrani, mpigieni Mungu wetu kinubi.
”Msifuni BWANA. Msifuni BWANA kutoka mbinguni, msifuni juu vileleni. Msifuni, enyi malaika wake wote, msifuni yeye, enyi jeshi lake lote la mbinguni. Msifuni yeye, enyi jua na mwezi, msifuni yeye, enyi nyota zote zing'aazo. Msifuni yeye, enyi mbingu zilizo juu sana na ninyi maji juu ya anga. Vilisifu jina la BWANA kwa maana aliamuru navyo vikaumbwa. Aliviweka mahali pake milele na milele, alitoa amri ambayo haibadiliki milele.
”Mtukuzeni BWANA kutoka duniani, ninyi viumbe vikubwa vya baharini na vilindi vyote vya bahari, umeme wa radi na mvua ya mawe, theluji na mawingu, pepo za dhoruba zinazofanya amri zake, ninyi milima na vilima vyote, miti ya matunda na mierezi yote, wanyama wa mwituni na mifugo yote, viumbe vidogo na ndege warukao, wafalme wa dunia na mataifa yote, ninyi wakuu na watawala wote wa dunia, wanaume vijana na wanawali, wazee na watoto. Wote na walisifu jina la BWANA, kwa maana jina lake pekee limetukuka, utukufu U juu ya nchi na mbingu.
”Msifuni BWANA. Mwimbieni BWANA wimbo mpya, sifa zake katika kusanyiko la watakatifu. Israeli na washangilie katika Muumba wao, watu wa Sayuni na wafurahi katika mfalme wao. Na walisifu jina lake kwa kucheza na wampigie muziki kwa matari na kinubi. Kwa maana BWANA anapendezwa na watu wake, anawavika wanyenyekevu taji ya wokovu. Watakatifu na washangilie katika heshima hii na waimbe kwa shangwe vitandani mwao. Sifa za Mungu na ziwe vinywani mwao na upanga ukatao kuwili mikononi mwao,
”Msifuni BWANA. Msifuni Mungu katika patakatifu pake, msifuni katika mbingu zake kuu. Msifuni kwa matendo yake makuu, msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake. Msifuni kwa mvumo wa tarumbeta, msifuni kwa kinubi na zeze, Msifuni kwa matari na kucheza, msifuni kwa kinanda cha nyuzi na filimbi, Msifuni kwa matoazi yaliayo, msifuni kwa matoazi yavumayo sana. Kila chenye pumzi na kimsifu BWANA. Msifuni BWANA. Haleluya!
”“Kumcha BWANA ni mwanzo wa hekima na kumjua Mtakatifu ni ufahamu.
”Ni nani ameshapanda mbinguni na kushuka? Ni nani ameshakusanya upepo kwenye vitanga vya mikono yake? Ni nani ameshafungia maji kwenye nguo yake? Ni nani ameimarisha miisho yote ya dunia? Jina lake ni nani na mwanawe anaitwa nani? Niambie kama unajua!
”Unibusu kwa busu la kinywa chako, kwa maana upendo wako unafurahisha kuliko divai. Manukato yako yananukia vizuri, jina lako ni kama manukato yaliyomiminwa. Ndiyo sababu wanawali wanakupenda! Nichukue twende nawe, na tufanye haraka! Mfalme na anilete ndani ya vyumba vyake. Tunakushangilia na kukufurahia, tutasifu upendo wako zaidi kuliko divai. Tazama ni jinsi gani ilivyo haki wakupende!
”Ni nani huyu anayekuja kutoka jangwani kama nguzo ya moshi, anayenukia manemane na uvumba iliyotengenezwa kwa vikolezo vyote vya mfanyabiashara?
”Amka, upepo wa kaskazini, na uje, upepo wa kusini! Vuma juu ya bustani yangu, ili harufu yake nzuri iweze kuenea mpaka ng'ambo. Mpendwa wangu na aje bustanini mwake na kuonja matunda mazuri sana.
”Ingieni kwenye miamba, jificheni ardhini kutokana na utisho wa BWANA na utukufu wa enzi yake!
”Watu watakimbilia kwenye mapango ndani ya miamba na kwenye mahandaki ardhini kutokana na utisho wa BWANA na utukufu wa enzi yake, ainukapo kuitikisa dunia.
”Watakimbilia kwenye mapango miambani na kwenye nyufa za miamba kutokana na utisho wa BWANA na utukufu wa enzi yake, ainukapo kuitikisa dunia.
”Kisha BWANA ataumba juu ya Mlima wote wa Sayuni na juu ya wale wote wanaokusanyika hapo, wingu la moshi wakati wa mchana na kung'aa kwa miali ya moto wakati wa usiku, juu ya huo utukufu wote kutatanda kifuniko cha ulinzi.
”Lakini BWANA Mwenye Nguvu Zote atatukuzwa kwa ajili ya haki yake, naye Mungu Mtakatifu atajionyesha mwenyewe kuwa mtakatifu kwa haki yake.
”Katika mwaka ule Mfalme Uzia alipokufa, nilimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu na kilichotukuzwa sana, nalo pindo la joho lake likajaza Hekalu. Juu yake walikuwepo maserafi, kila mmoja alikuwa na mabawa sita: Kwa mabawa mawili walifunika nyuso zao, kwa mengine mawili walifunika miguu yao na kwa mawili walikuwa wakiruka. Nao walikuwa wakiitana kila mmoja na mwenzake: “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu ni BWANA Mwenye Nguvu Zote; dunia yote imejaa utukufu wake.” Kwa kutoa kwao sauti miimo ya milango na vizingiti vilitikisika, nalo Hekalu likajaa moshi. Ndipo nikalia, “Ole wangu mimi! Nimeangamia! Kwa kuwa mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninaishi katikati ya watu wenye midomo michafu, nayo macho yangu yamemwona Mfalme, BWANA Mwenye Nguvu Zote.”
”Kwa maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume, nao utawala utakuwa mabegani mwake. Naye ataitwa Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani. Kuongezeka kwa utawala wake na amani hakutakuwa na mwisho. Atatawala katika kiti cha enzi cha Daudi na juu ya ufalme wake, akiuthibitisha na kuutegemeza kwa haki na kwa adili, tangu wakati huo na hata milele. Wivu wa BWANA Mwenye Nguvu Zote utatimiza haya.
”Roho wa BWANA atakaa juu yake, Roho wa hekima na wa ufahamu, Roho wa shauri na uweza, Roho wa maarifa na wa kumcha BWANA
”Katika siku hiyo mtasema: “Mshukuruni BWANA, mliitie jina lake; julisheni miongoni mwa mataifa yale aliyoyafanya, tangazeni kuwa jina lake limetukuka. Mwimbieni BWANA, kwa kuwa ametenda mambo makuu, hili na lijulikane duniani kote. Paza sauti uimbe kwa furaha, watu wa Sayuni, kwa maana mkuu ni yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli miongoni mwenu.”
”Katika siku ile watu watamwangalia Muumba wao na kuelekeza macho yao kwa huyo Aliye Mtakatifu wa Israeli.
”Wanainua sauti zao, wanapiga kelele kwa furaha, kutoka magharibi wanasifu kwa ukelele utukufu wa BWANA. Kwa hiyo upande wa mashariki mpeni BWANA utukufu, liadhimisheni jina la BWANA, Mungu wa Israeli, katika visiwa vya bahari.
”Ee BWANA, wewe ni Mungu wangu, nitakutukuza na kulisifu jina lako, kwa maana katika ukamilifu wa uaminifu umetenda mambo ya ajabu, mambo yaliyokusudiwa tangu zamani. Umeufanya mji kuwa lundo la kifusi, mji wenye ngome kuwa magofu, ngome imara ya wageni kuwa si mji tena, wala hautajengwa tena kamwe. Kwa hiyo mataifa yenye nguvu yatakuheshimu, miji ya mataifa katili itakuheshimu wewe.
”Mtumaini BWANA milele, kwa kuwa BWANA, BWANA, ni Mwamba wa milele.
”Katika siku ile, BWANA Mwenye Nguvu Zote atakuwa taji la utukufu, taji zuri la maua kwa mabaki ya watu wake.
”Nanyi mtaimba kama usiku mnaoadhimisha sikukuu takatifu, mioyo yenu itashangilia kama vile watu wanapokwea na filimbi kwenye mlima wa BWANA, kwa Mwamba wa Israeli. BWANA atawasababisha watu waisikie sauti yake ya utukufu, naye atawafanya wauone mkono wake ukishuka pamoja na hasira yake kali na moto ulao, kukiwa na tufani ya mvua, ngurumo za radi na mvua ya mawe.
”Macho yenu yatamwona mfalme katika uzuri wake na kuiona nchi inayoenea mbali.
”Kwa kuwa BWANA ni mwamuzi wetu, BWANA ndiye mtoa sheria wetu, BWANA ni mfalme wetu, yeye ndiye atakayetuokoa.
”waliokombolewa na BWANA watarudi. Wataingia Sayuni wakiimba; furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao. Watapata furaha na shangwe; huzuni na majonzi vitakimbia.
”BWANA ataniokoa, nasi tutaimba kwa vyombo vya nyuzi siku zote za maisha yetu katika Hekalu la BWANA.
”Utukufu wa BWANA utafunuliwa, nao wanadamu wote kwa pamoja watauona. Kwa maana kinywa cha BWANA kimenena.”
”Ni nani aliyepima maji ya bahari kwenye konzi ya mkono wake, au kuzipima mbingu kwa shibiri yake? Ni nani aliyeyashika mavumbi ya dunia katika kikapu, au kupima milima kwenye kipimio na vilima kwenye mizani?
”Je, hujui? Je, hujasikia? Je, hujaambiwa tangu mwanzo? Je, hujafahamu tangu kuumbwa kwa dunia? Anakaa kwenye kiti cha enzi juu ya duara ya dunia, nao watu wakaao ndani yake ni kama panzi. Huzitandaza mbingu kama chandarua na kuzitandaza kama hema la kuishi. Huwafanya wakuu kuwa si kitu na kuwashusha watawala wa dunia hii kuwa kitu bure.
”Inueni macho yenu mtazame mbinguni: Ni nani aliyeumba hivi vyote? Yeye aletaye nje jeshi la nyota moja baada ya nyingine na kuziita kila moja kwa jina lake? Kwa sababu ya uweza wake mkuu na nguvu zake kuu, hakuna hata mojawapo inayokosekana.
”Je wewe, hufahamu? Je wewe, hujasikia? BWANA ni Mungu wa milele, Muumba wa miisho ya dunia. Hatachoka wala kulegea, wala hakuna hata mmoja awezaye kuupima ufahamu wake.
”Utaipepeta, nao upepo utaichukua, dhoruba itaipeperushia mbali. Bali wewe utajifurahisha katika BWANA na katika utukufu wa yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.
”“Mimi ndimi BWANA; hilo ndilo Jina langu! Sitampa mwingine utukufu wangu wala sanamu sifa zangu. Tazama, mambo ya kwanza yametokea, nami natangaza mambo mapya; kabla hayajatokea nawatangazia habari zake.” Mwimbieni BWANA wimbo mpya, sifa zake toka miisho ya dunia, ninyi mshukao chini baharini, na vyote vilivyomo ndani yake, enyi visiwa na wote wakaao ndani yake. Jangwa na miji yake na vipaze sauti zao; makao anamoishi Kedari na yashangilie. Watu wa Sela waimbe kwa furaha na wapige kelele kutoka vilele vya milima. Wampe BWANA utukufu na kutangaza sifa zake katika visiwa.
”kila mmoja ambaye ameitwa kwa Jina langu, niliyemwumba kwa utukufu wangu, niliyemhuluku na kumfanya.”
”“Ninyi ni mashahidi wangu,” asema BWANA, “na mtumishi wangu niliyemchagua, ili mpate kunijua na kuniamini na kutambua kwamba Mimi ndiye. Kabla yangu hakuna mungu aliyefanyizwa, wala hatakuwepo mwingine baada yangu. Mimi, naam mimi, ndimi BWANA, zaidi yangu hakuna mwokozi.
”Mimi ndimi BWANA, yeye Aliye Mtakatifu wako, Muumba wa Israeli, Mfalme wako.”
”Watu wale niliowaumba kwa ajili yangu, ili wapate kutangaza sifa zangu.
”“Hili ndilo asemalo BWANA, Mfalme wa Israeli na Mkombozi, BWANA Mwenye Nguvu Zote: Mimi ni wa kwanza na Mimi ni wa mwisho; zaidi yangu hakuna Mungu.
”Enyi mbingu, imbeni kwa furaha, kwa maana BWANA amefanya jambo hili, Ee vilindi vya dunia, piga kelele. Enyi milima, pazeni sauti kwa nyimbo, enyi misitu na miti yenu yote, kwa maana BWANA amemkomboa Yakobo, ameuonyesha utukufu wake katika Israeli.
”Mimi ndimi BWANA, wala hakuna mwingine, zaidi yangu hakuna Mungu. Nitakutia nguvu, ingawa wewe hukunitambua, ili kwamba kutoka maawio ya jua mpaka machweo yake, watu wapate kujua kwamba hakuna Mungu mwingine ila Mimi. Mimi ndimi BWANA wala hakuna mwingine. Mimi ninaumba nuru na kuhuluku giza, ninaleta mafanikio na kusababisha maafa, Mimi, BWANA, hufanya vitu hivi vyote.
”Kwa kuwa hili ndilo asemalo BWANA, yeye aliyeumba mbingu, ndiye Mungu; yeye aliyeifanya dunia na kuiumba, yeye ndiye aliyeiwekea misingi imara, hakuiumba ili iwe tupu, bali aliiumba ikaliwe na viumbe vyake, anasema: “Mimi ndimi BWANA, wala hakuna mwingine.
”“Nigeukieni mimi nanyi mkaokolewe, enyi miisho yote ya dunia; kwa maana mimi ndimi Mungu, wala hapana mwingine. Nimeapa kwa nafsi yangu, kinywa changu kimenena katika uadilifu wote neno ambalo halitatanguka: Kila goti litapigwa mbele zangu, kwangu mimi kila ulimi utaapa.
”Kumbukeni mambo yaliyopita, yale ya zamani za kale; mimi ndimi Mungu, wala hakuna mwingine; mimi ndimi Mungu, wala hakuna mwingine aliye kama mimi. Ni mimi tangazaye mwisho tangu mwanzo, naam, tangu zamani za kale, mambo ambayo hayajatendeka. Ninasema: Kusudi langu ndilo litakalosimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote.
”Mkombozi wetu: BWANA Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake; ndiye yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.
”“Ee Yakobo, nisikilize mimi, Israeli, ambaye nimekuita: Mimi ndiye; mimi ndimi mwanzo na mwisho. Mkono wangu mwenyewe uliweka misingi ya dunia, nao mkono wangu wa kuume umezitanda mbingu; niziitapo, zote husimama pamoja.
”Hili ndilo asemalo BWANA, yeye Mkombozi na Aliye Mtakatifu wa Israeli, kwake yeye ambaye alidharauliwa na kuchukiwa na taifa, kwa mtumishi wa watawala: “Wafalme watakuona na kusimama, wakuu wataona na kuanguka kifudifudi, kwa sababu ya BWANA, aliye mwaminifu, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, ambaye amekuchagua wewe.”
”Pigeni kelele kwa furaha, Enyi mbingu; furahi, Ee dunia; pazeni sauti kwa kuimba, Enyi milima! Kwa maana BWANA anawafariji watu wake, naye atakuwa na huruma kwa watu wake walioumizwa.
”Sikiliza! Walinzi wako wanapaza sauti zao, kwa pamoja wanapaza sauti zao kwa furaha. Wakati BWANA atakaporejea Sayuni, wataliona kwa macho yao wenyewe. Pazeni sauti ya nyimbo za furaha kwa pamoja, enyi magofu ya Yerusalemu, kwa maana BWANA amewafariji watu wake, ameikomboa Yerusalemu.
”Kwa maana Muumba wako ndiye mume wako, BWANA Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli ni Mkombozi wako, yeye anaitwa Mungu wa dunia yote.
”Mtatoka nje kwa furaha na kuongozwa kwa amani; milima na vilima vitapaza sauti kwa nyimbo mbele yenu, nayo miti yote ya shambani itapiga makofi.
”Kwa maana hili ndilo asemalo Aliye juu, yeye aliyeinuliwa sana, yeye aishiye milele, ambaye jina lake ni Mtakatifu: “Ninaishi mimi mahali palipoinuka tena palipo patakatifu, tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na mwenye roho ya unyenyekevu, ili kuzihuisha roho za wanyenyekevu na kuihuisha mioyo yao waliotubu.
”Jua halitakuwa tena nuru yako mchana, wala mwangaza wa mwezi hautakuangazia, kwa maana BWANA atakuwa nuru yako ya milele, naye Mungu wako atakuwa utukufu wako. Jua lako halitazama tena, nao mwezi wako hautafifia tena; BWANA atakuwa nuru yako milele, nazo siku zako za huzuni zitakoma. Ndipo watu wako wote watakuwa waadilifu nao wataimiliki nchi milele. Wao ni chipukizi nililolipanda, kazi ya mikono yangu, kwa ajili ya kuonyesha utukufu wangu.
”na kuwapa mahitaji wale wanaohuzunika katika Sayuni, ili kuwapa taji ya uzuri badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho ya kukata tamaa. Nao wataitwa mialoni ya haki, pando la BWANA kwa ajili ya kuonyesha utukufu wake.
”aliyetuma mkono wake uliotukuka wenye nguvu kuwa katika mkono wa kuume wa Mose, aliyegawa maji ya bahari mbele yao, ili kujipatia jina milele,
”Lakini wewe ni Baba yetu, ingawa Abrahamu hatufahamu sisi wala Israeli hatutambui; wewe, Ee BWANA, ni Baba yetu, Mkombozi wetu tangu zamani za kale ndilo jina lako.
”Lakini, Ee BWANA, wewe ndiwe Baba yetu. Sisi ni udongo wa mfinyanzi wewe ndiye mfinyanzi; sisi sote tu kazi ya mkono wako.
”Hili ndilo asemalo BWANA, “Mbingu ni kiti changu cha enzi, nayo dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu. Iko wapi nyumba mtakayojenga kwa ajili yangu? Mahali pangu pa kupumzika patakuwa wapi?
”“Kama vile mbingu mpya na nchi mpya ninazozifanya zitakavyodumu mbele zangu,” asema BWANA, “ndivyo jina lenu na wazao wenu watakavyodumu. Kutoka Mwezi Mpya hata Mwezi Mpya mwingine na kutoka Sabato hadi Sabato nyingine, wanadamu wote watakuja na kusujudu mbele zangu,” asema BWANA.
”Je, haiwapasi kuniogopa mimi?” asema BWANA. “Je, haiwapasi kutetemeka mbele zangu? Niliufanya mchanga kuwa mpaka wa bahari, kizuizi cha milele ambacho haiwezi kupita. Mawimbi yanaweza kuumuka, lakini hayawezi kuupita; yanaweza kunguruma, lakini hayawezi kuuvuka.
”Lakini BWANA ni Mungu wa kweli, yeye ndiye Mungu aliye hai, Mfalme wa milele. Akiwa amekasirika, dunia hutetemeka, mataifa hayawezi kustahimili hasira yake.
”Mwimbieni BWANA! Mpeni BWANA sifa! Huokoa uhai wa mhitaji kutoka mikononi mwa waovu.
”Je, mtu ye yote aweza kujificha mahali pa siri ili nisiweze kumwona?” BWANA asema. “Je, mimi sikuijaza mbingu na nchi?” BWANA asema.
”“Je, neno langu si kama moto,” asema BWANA, “na kama nyundo ivunjayo mwamba vipande vipande?
”Mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.
”“Ee BWANA Mwenyezi, umeumba mbingu na nchi kwa uwezo wako mkuu na kwa mkono ulionyooshwa. Hakuna jambo lililo gumu usiloliweza. Huonyesha upendo kwa maelfu lakini huleta adhabu kwa ajili ya dhambi za baba mapajani mwa watoto wao baada yao. Ee Mungu mkuu na mwenye uweza, ambaye jina lako ni BWANA Mwenye Nguvu Zote,
”“Mimi ndimi BWANA, Mungu wa wote wenye mwili, Je, kuna jambo lo lote lililo gumu nisiloliweza?
”sauti za shangwe na furaha, sauti za bibi na bwana arusi na sauti za wale waletao sadaka za shukrani katika nyumba ya BWANA, wakisema, “ ‘ “Mshukuruni BWANA Mwenye Nguvu Zote, kwa maana BWANA ni mwema; upendo wake wadumu milele.” Kwa kuwa nitairudishia nchi baraka kama zilivyokuwa hapo awali,’ asema BWANA.
”Inuka, lia usiku, zamu za usiku zianzapo; mimina moyo wako kama maji mbele za Bwana. Mwinulie yeye mikono yako kwa ajili ya maisha ya watoto wako, ambao wanazimia kwa njaa kwenye kila mwanzo wa barabara.
”Na tuinue mioyo yetu pamoja na mikono yetu kwa Mungu mbinguni, na tuseme:
”Wewe, Ee BWANA tawala milele, kiti chako cha enzi chadumu kutoka kizazi mpaka kizazi.
”Viumbe wale waliposogea nilisikia sauti ya mabawa yao, kama ngurumo ya maji yaendayo kasi, kama sauti ya Mwenyezi, kama makelele ya jeshi. Waliposimama kimya walishusha mabawa yao. Ndipo ikaja sauti toka juu ya ile nafasi ya wazi iliyokuwa juu ya vichwa vyao, wakati waliposimama mabawa yao yakiwa yameshushwa. Juu ya ile nafasi ya wazi iliyokuwa juu ya vichwa vyao kulikuwa na kitu mfano wa kiti cha enzi kuonekana kwake chenye rangi ya yakuti samawi, na juu ya kile kiti cha enzi kulikuwa na umbo mfano wa mwanadamu. Nikaona kwamba kutokana na kile nilichoona kama kiuno chake kuelekea juu alionekana kama chuma inayowaka kana kwamba imejaa moto na kuanzia kiuno kwenda chini alionekana kama moto na mwanga mkali ulimzunguka. Kama vile kuonekana kwa upinde wa mvua mawinguni siku ya mvua, ndivyo ulivyokuwa ule mng'ao uliomzunguka. Hivi ndivyo ilivyokuwa kuonekana kwa utukufu wa BWANA. Nilipouona, nikaanguka kifudifudi, nikasikia sauti ya mtu anaongea.
”Ndipo Roho akaniinua, nikasikia sauti kubwa nyuma yangu ya ngurumo. (Utukufu wa BWANA na utukuzwe katika mahali pa makao yake!)
”Kwa hiyo niliinuka nikaenda mpaka mahali pa tambarare. Utukufu wa BWANA ulikuwa umesimama huko, kama utukufu ule niliouona kando ya Mto Kebari, nami nikaanguka kifudifudi.
”Hapo mbele yangu palikuwa na utukufu wa Mungu wa Israeli, kama utukufu ule niliouona katika maono kule ua wa ndani.
”Kisha utukufu wa BWANA ukainuka kutoka juu ya wale makerubi ukaenda kwenye kizingiti cha Hekalu. Wingu likajaza Hekalu, nao ukumbi ukajawa na mng'ao wa utukufu wa BWANA. Sauti ya mabawa ya wale makerubi ingeweza kusikika mpaka kwenye ukumbi wa nje, kama sauti ya Mungu Mwenyezi wakati anapoongea.
”Kisha utukufu wa Mungu ukaondoka pale kwenye kizingiti cha Hekalu na kusimama juu ya wale makerubi. Nilipokuwa nikitazama, makerubi yakatanda mabawa yao na kuinuka kutoka ardhini, nao walipokuwa wakienda yale magurudumu yakaenda pamoja nao. Wakasimama kwenye ingilio la lango la mashariki la nyumba ya BWANA, nao utukufu wa Mungu wa Israeli ukawa juu yao.
”Ndipo wale makerubi, wenye magurudumu pembeni mwao, wakakunjua mabawa yao, nao utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwa juu yao. Basi utukufu wa BWANA ukapaa juu kutoka katika mji, ukatua juu ya mlima ulio upande wa mashariki ya mji.
”Nami hivyo ndivyo nitakavyoonyesha ukuu wangu na utakatifu wangu, nami nitajijulisha mbele ya macho ya mataifa mengi. Ndipo watakapojua kuwa Mimi ndimi BWANA.’
”nami nikaona utukufu wa Mungu wa Israeli ukija kutoka upande wa mashariki. Sauti yake ilikuwa kama ya ngurumo ya maji yaendayo kasi, nayo nchi ikang'aa kwa utukufu wake. Maono niliyoyaona yalikuwa kama maono yale niliyokuwa nimeyaona wakati Mungu alipokuja kuangamiza mji na kama maono niliyokuwa nimeyaona kando ya Mto wa Kebari, nami nikaanguka kifudifudi. Utukufu wa BWANA ukaingia hekaluni kwa kupitia lango linaloelekea upande wa mashariki. Kisha Roho akanichukua na kunileta katika ule ua wa ndani, nao utukufu wa BWANA ulilijaza Hekalu. Wakati yule mtu akiwa amesimama kando yangu, nilisikia mtu mmoja akisema nami kutoka ndani ya Hekalu. Akasema, “Mwanadamu, hapa ni mahali pa kiti changu cha enzi na mahali pa kuweka nyayo za miguu yangu. Hapa ndipo nitakapoishi miongoni mwa Waisraeli milele. Kamwe nyumba ya Israeli hawatalinajisi tena Jina langu takatifu, yaani, wao wala wafalme wao, kwa ukahaba wao na kwa sanamu zao zisizokuwa na uhai za wafalme wao katika mahali pao pa juu pa kuabudia miungu.
”Kisha yule mtu akanileta kwa njia ya lango la kaskazini mpaka mbele ya Hekalu. Nikatazama nami nikauona utukufu wa BWANA ukilijaza Hekalu la BWANA, nami nikaanguka kifudifudi.
”Wakati wa usiku lile fumbo lilifunuliwa kwa Danieli katika maono. Ndipo Danieli akamhimidi Mungu wa mbinguni, na akasema: “Lihimidiwe jina la Mungu milele na milele, hekima na uweza ni vyake. Yeye hubadili nyakati na majira, huwaweka wafalme na kuwaondoa. Huwapa hekima wenye hekima na maarifa wenye ufahamu. Hufunua siri na mambo yaliyofichika, anajua yale yaliyo gizani, nuru hukaa kwake. Ninakushukuru na kukuhimidi, Ee Mungu wa baba zangu: Umenipa hekima na uwezo, umenijulisha kile tulichokuomba, umetujulisha kujua ndoto ya mfalme.”
”“Katika siku za wafalme hao, Mungu wa mbinguni atauweka ufalme ambao kamwe hautaangamizwa, wala hautaachiwa taifa jingine. Utaziponda zile falme zote na kuzikomesha, bali wenyewe utadumu milele.
”Mwisho wa huo wakati, mimi Nebukadneza, niliinua macho yangu kuelekea mbinguni, nazo fahamu zangu zikanirudia. Ndipo nikamsifu Yeye Aliye Juu Sana, nikamheshimu na kumhimidi yeye aishiye milele. Utawala wake ni utawala wa milele; ufalme wake hudumu kutoka kizazi na kizazi.
”Basi mimi, Nebukadneza, humhimidi, humtukuza na kumsifu Mfalme wa mbinguni, kwa sababu kila kitu afanyacho ni haki na njia zake zote ni adili. Nao waendao kwa kiburi anaweza kuwashusha.
”“Nilipokuwa ninaendelea kutazama, “viti vya enzi vikawekwa, naye Mzee wa Siku akaketi. Mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, nywele za kichwa chake zilikuwa nyeupe kama sufu. Kiti chake cha enzi kilikuwa kinawaka kwa miali ya moto, nayo magurudumu yake yote yalikuwa yanawaka moto. Mto wa moto ulikuwa unatiririka, ukipita mbele yake. Maelfu elfu wakamhudumia, kumi elfu mara kumi elfu wakasimama mbele zake. Mahakama ikakaa ili kuhukumu na vitabu vikafunguliwa.
”“Katika maono yangu ya usiku nilitazama, mbele yangu nikamwona anayefanana na mwanadamu, akija pamoja na mawingu ya mbinguni. Akamkaribia huyo Mzee wa Siku na akaongozwa mbele zake. Akapewa mamlaka, utukufu na ufalme wenye nguvu, watu, kabila zote za mataifa na watu wa kila lugha wakamwabudu. Utawala wake ni utawala wa milele ambao hautapita, nao ufalme wake ni ule ambao kamwe hautaangamizwa.
”Lakini watakatifu wa Yeye Aliye Juu Sana watapokea ufalme na kuumiliki milele, naam, milele na milele.’
”Ndipo ufalme, mamlaka na ukuu wa falme chini ya mbingu yote utakabidhiwa kwa watakatifu, watu wa Yeye Aliye Juu Sana. Ufalme wake utakuwa ufalme wa milele, nao watawala wote watamwabudu na kumtii yeye.’
”Atasimama na kulichunga kundi lake katika nguvu ya BWANA, katika utukufu wa jina la BWANA Mungu wake. Nao wataishi kwa usalama, kwa kuwa wakati huo ukuu wake utaenea hadi miisho ya dunia.
”Milima hutikisika mbele yake na vilima huyeyuka. Nchi hutetemeka mbele yake, dunia na wote waishio ndani yake.
”Kwa kuwa dunia itajazwa na maarifa ya utukufu wa BWANA, kama maji yaifunikavyo bahari.
”Mungu alitoka Temani, yeye aliye Mtakatifu kutoka Mlima Parani. Utukufu wake ulifunika mbingu na sifa zake zikaifunika dunia. Mng'ao wake ulikuwa kama jua lichomozalo, mionzi ilimulika kutoka mkononi mwake, ambako nguvu zake zilifichwa.
”milima ilikuona ikatetemeka. Mafuriko ya maji yakapita huko; vilindi vilinguruma na kuinua mawimbi yake juu.
”Nitatikisa mataifa yote, nacho kile kinachotamaniwa na mataifa yote kitakuja, nami nitaujaza utukufu katika nyumba hii,’ asema BWANA Mwenye Nguvu Zote.
”Mimi mwenyewe nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka,’ asema BWANA, ‘nami nitakuwa utukufu wake ndani yake.’
”Kisha akaniambia, “Hili ni neno la BWANA kwa Zerubabeli: ‘Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa Roho yangu,’ asema BWANA Mwenye Nguvu Zote.
”Ni yeye atakayejenga Hekalu la BWANA, naye atavikwa utukufu na ataketi kumiliki katika kiti cha enzi naye atakuwa kuhani katika kiti chake cha enzi. Hapo patakuwa amani kati ya hao wawili.’
”Shangilia sana, Ee Binti Sayuni! Piga kelele, Binti Yerusalemu! Tazama, Mfalme wako anakuja kwako, ni mwenye haki naye ana wokovu, mpole naye amepanda punda, mwana punda, mtoto wa punda.
”Siku hiyo miguu yake itasimama juu ya Mlima wa Mizeituni, mashariki mwa Yerusalemu, nao Mlima wa Mizeituni utagawanyika mara mbili kuanzia mashariki hadi magharibi, ukifanya bonde kubwa, nusu ya mlima ukisogea kuelekea kaskazini na nusu kuelekea kusini.
”BWANA atakuwa mfalme juu ya dunia yote. Katika siku hiyo atakuwepo BWANA mmoja na jina lake litakuwa jina pekee.
”Ndipo wale waliomcha BWANA wakasemezana wao kwa wao, naye BWANA akasikiliza naye akasikia. Kitabu cha kumbukumbu kikaandikwa mbele yake kuhusu wale ambao walimcha BWANA na kuliheshimu jina lake.
”“Tazama, bikira atachukua mimba, naye atamzaa mwana, nao watamwita Jina lake Imanueli,” maana yake, “Mungu pamoja nasi.”
”wakiuliza, “Yuko wapi huyo aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tumeona nyota yake ikitokea mashariki, nasi tumekuja kumwabudu.”
”Walipoingia ndani ya ile nyumba, wakamwona mtoto pamoja na Maria mama yake, wakamsujudu na kumwabudu yule mtoto Yesu. Ndipo wakafungua hazina zao, wakamtolea zawadi za dhahabu, uvumba na manemane.
”Naye Yesu alipokwisha kubatizwa, mara alipotoka ndani ya maji, ghafula mbingu zikamfungukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua na kutulia juu yake. Nayo sauti kutoka mbinguni ikasema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa, ambaye ninapendezwa sana naye.”
”Vivyo hivyo, nuru yenu iangaze mbele ya watu, ili wapate kuona matendo yenu mema wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.
”“Hivi basi, ndivyo iwapasavyo kuomba: “ ‘Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe. Ufalme wako uje. Mapenzi yako yafanyike hapa duniani kama huko mbinguni.
”Usitutie majaribuni, bali utuokoe kutoka kwa yule mwovu [kwa kuwa Ufalme ni wako na nguvu na utukufu, hata milele. Amen].’
”Wale watu wakashangaa, wakisema, “Ni mtu wa namna gani huyu? Hata upepo na mawimbi vinamtii!”
”Nawaambia wazi kwamba, yeye aliye mkuu kuliko Hekalu yupo hapa.
”Ndipo wote waliokuwamo ndani ya kile chombo wakamwabudu Yesu wakisema, “Hakika, wewe ndiwe Mwana wa Mungu.”
”Hao watu wakashangaa walipoona bubu wakisema, vilema wakipona, viwete wakitembea na vipofu wakiona, wakamtukuza Mungu wa Israeli.
”Kwa maana Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake, naye ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
”Wakiwa huko, Yesu alibadilika sura mbele yao. Uso wake ukang'aa kama jua na nguo zake zikawa na weupe wa kuumiza macho.
”Petro alipokuwa angali ananena, ghafula, wingu linalong'aa likawafunika na sauti ikatoka kwenye hilo wingu ikisema, “Huyu ni mwanangu mpendwa, ninayependezwa naye sana, msikilizeni yeye.” Wale wanafunzi, waliposikia haya, wakaanguka chini kifudifudi, wakajawa na hofu.
”Lakini Yesu akawatazama, akawaambia, “Kwa mwanadamu jambo hili haliwezekani, lakini kwa Mungu mambo yote yanawezekana.”
”Yesu akawaambia, “Amin, amin nawaambia, wakati wa kufanywa upya vitu vyote, wakati Mwana wa Adamu atakapoketi kwenye kiti chake cha utukufu cha enzi, ninyi mliomfuata pia mtaketi katika viti vya enzi kumi na viwili, mkiyahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli.
”“Mwambieni Binti Sayuni, ‘Tazama, mfalme wako anakuja kwako, ni mnyenyekevu, naye amepanda punda, juu ya mwana-punda, mtoto wa punda.’ ”
”Ule umati wa watu uliomtangulia na ule uliomfuata ukapiga kelele ukisema, “Hosana Mwana wa Daudi!” “Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana!” “Hosana juu mbinguni!”
”Lakini viongozi wa makuhani na walimu wa sheria walipoona mambo ya ajabu aliyofanya na kuwasikia watoto wakishangilia katika eneo la Hekalu wakisema, “Hosana Mwana wa Daudi”, walikasirika. Wakamwuliza Yesu, “Je, unasikia hayo hawa wanayosema?” Akawajibu, “Naam; kwani hamkusoma, “ ‘Kutoka katika vinywa vya watoto wachanga na wale wanaonyonya umeamuru sifa kamili?’ ”
”Yesu akamjibu, “ ‘Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote.’ Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.
”“Ndipo itakapotokea ishara ya Mwana wa Adamu angani na makabila yote ya dunia yataomboleza. Nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya angani, katika uwezo na utukufu mkuu. Naye atawatuma malaika zake kwa sauti kuu ya tarumbeta, nao watawakusanya wateule wake kutoka pande zote nne za dunia, kutoka mwisho mmoja wa mbingu hadi mwisho mwingine.
”“Mwana wa Adamu atakapokuja katika utukufu wake na malaika wote watakatifu pamoja naye, ndipo atakapoketi juu ya kiti cha enzi cha utukufu wake. Mataifa yote watakusanyika mbele zake, naye atawatenga kama mchungaji anavyotenga kondoo na mbuzi.
”Walipokwisha kuimba wimbo, wakatoka kwenda mlima wa Mizeituni.
”Yesu akajibu, “Wewe umenena. Lakini ninawaambia nyote, tangu sasa mtamwona Mwana wa Adamu akiwa ameketi mkono wa kuume wa Mwenye Nguvu, na akija juu ya mawingu ya mbinguni.”
”Wakati Yesu akiwa amesimama mbele ya mtawala, mtawala akamwuliza, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?” Yesu akasema, “Wewe wasema hivyo.”
”Juu ya kichwa chake, kwenye msalaba, wakaandika shtaka lake: HUYU NI YESU, MFALME WA WAYAHUDI.
”Ghafula Yesu akakutana nao, akasema, “salamu!” Wale wanawake wakamkaribia wakaishika miguu yake, wakamwabudu.
”Walipomwona, wakamwabudu, lakini baadhi yao wakaona shaka. Yesu akawajia na kusema, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
”Nao wakawa wameogopa sana, wakaulizana, “Ni nani huyu ambaye hata upepo na mawimbi vinamtii?”
”Mtu ye yote anayenionea aibu mimi na maneno yangu katika kizazi hiki cha uzinzi na cha dhambi, Mwana wa Adamu, atamwonea aibu wakati atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu.”
”Ndipo pakatokea wingu, likawafunika, nayo sauti kutoka katika lile wingu ikasema, “Huyu ni Mwanangu, nimpendaye, msikilizeni yeye.”
”Yesu akawatazama, akawaambia, “Kwa mwanadamu hili haliwezekani, lakini kwa Mungu sivyo. Yote kwa Mungu yanawezekana.”
”Kisha wale waliokuwa wametangulia mbele na wale waliokuwa wakifuata nyuma wakapaza sauti, wakisema, “Hosana!” “Amebarikiwa yeye ajaye kwa jina la Bwana! “Umebarikiwa Ufalme unaokuja wa baba yetu Daudi!” “Hosana kwake yeye aliye juu!”
”Yesu akajibu, “Amri iliyo kuu ndiyo hii, ‘Sikia Ee Israeli, Bwana Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja. Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa akili zako zote na kwa nguvu zako zote.’
”“Ndipo watu wote watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni kwa nguvu nyingi na utukufu.
”Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
”Walipokwisha kuimba wimbo, wakatoka wakaenda kwenye Mlima wa Mizeituni.
”Yesu akajibu, “Mimi ndimi, nanyi mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa Mwenye Nguvu, akija na mawingu ya mbinguni.”
”Pilato akamwuliza, “Je, wewe ndiye Mfalme wa Wayahudi?” Yesu akajibu, “Wewe umesema.”
”Tangazo likaandikwa la mashtaka dhidi yake lenye maneno haya: “MFALME WA WAYAHUDI.”
”Baada ya Bwana Yesu kusema nao, alichukuliwa juu mbinguni na kuketi mkono wa kuume wa Mungu.
”Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume na utamwita jina lake Yesu. Yeye atakuwa mkuu, naye ataitwa Mwana wa Aliye Juu Sana. BWANA Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake. Ataimiliki nyumba ya Yakobo milele na ufalme wake hautakuwa na mwisho.” Maria akamwuliza huyo malaika, “Maadamu mimi ni bikira, jambo hili litawezekanaje?” Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, nazo nguvu zake Yeye Aliye Juu Sana zitakufunika kama kivuli, kwa hiyo mtoto atakayezaliwa atakuwa mtakatifu, naye ataitwa Mwana wa Mungu.
”Kwa maana kwa Mungu hakuna lisilowezekana.”
”Naye Maria akasema: “Moyo wangu wamwadhimisha Bwana, nayo roho yangu inamfurahia Mungu Mwokozi wangu,
”kwa maana yeye Mwenye Nguvu amenitendea mambo ya ajabu, jina lake ni takatifu.
”katika utakatifu na haki mbele zake, siku zetu zote.
”Ghafula pakawa na jeshi kubwa la mbinguni pamoja na huyo malaika wakimsifu Mungu wakisema, “Atukuzwe Mungu juu mbinguni na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia.”
”Wale wachungaji wakarudi, huku wakimtukuza Mungu na kumsifu kwa ajili ya mambo yote waliyokuwa wameambiwa na kuyaona.
”Yesu akamjibu, “Imeandikwa: ‘Mwabudu Bwana Mungu wako na umtumikie yeye peke yake.’ ”
”Simoni Petro alipoona haya yaliyotukia alianguka miguuni mwa Yesu na kumwambia, “Bwana, ondoka kwangu, mimi ni mtu mwenye dhambi!”
”Akawauliza wanafunzi wake, “Imani yenu iko wapi?” Kwa woga na mshangao wakaulizana, “Huyu ni mtu wa namna gani ambaye anaamuru hata upepo na maji navyo vikamtii?”
”Kama mtu ye yote akinionea aibu mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu atamwonea aibu mtu huyo atakapokuja katika utukufu wake na katika utukufu wa Baba na wa malaika watakatifu.
”Watu wote wakastaajabia uweza mkuu wa Mungu. Wakati bado watu wanastaajabia hayo yote aliyokuwa akiyafanya Yesu, yeye akawaambia wanafunzi wake:
”Saa ile ile, Yesu akashangilia katika Roho Mtakatifu akasema, “Nakushukuru Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa sababu mambo haya umewaficha wenye hekima na wenye akili, nawe umewafunulia watoto wadogo. Naam, Baba, kwa kuwa hayo ndiyo yaliyokuwa mapenzi yako.
”Akajibu, “ ‘Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote na kwa akili zako zote, tena mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.’ ”
”Akawaambia, “Mnapoomba, semeni hivi: “ ‘Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje.
”Mmoja wao alipoona kwamba amepona, akarudi kwa Yesu, akimsifu Mungu kwa sauti kuu. Akajitupa miguuni mwa Yesu akamshukuru. Yeye alikuwa Msamaria.
”Yesu akajibu, “Yasiyowezekana kwa wanadamu kwa Mungu yawezekana.”
”Akapata kuona saa ile ile, akamfuata Yesu, huku akimsifu Mungu. Watu wote walipoona mambo hayo, nao wakamsifu Mungu.
”Alipokaribia mahali yanapoanzia matelemko ya Mlima wa Mizeituni, umati wote wa wafuasi wake wakaanza kumsifu Mungu kwa furaha kwa sauti kuu kwa ajili ya matendo yote ya miujiza waliyoyaona. Wakasema: “Amebarikiwa Mfalme ajaye kwa jina la Bwana!” “Amani mbinguni na Utukufu huko juu sana.” Baadhi ya Mafarisayo waliokuwemo miongoni mwa ule umati wa watu wakamwambia, “Mwalimu, waamuru wanafunzi wako wanyamaze.” Yesu akawajibu, “Nawaambia ninyi, kama hawa wakinyamaza, mawe yatapiga kelele.”
”Wakati huo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni pamoja na uweza na utukufu mkuu.
”Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.”
”Lakini kuanzia sasa, Mwana wa Adamu ataketi mkono wa kuume wa Mungu Mwenye Nguvu.” Wote wakauliza, “Wewe basi ndiwe Mwana wa Mungu?” Yeye akawajibu, “Ninyi mmesema kwamba Mimi ndiye.”
”Basi Pilato akamwuliza Yesu, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?” Yesu akajibu, “Wewe wasema.”
”Kwenye msalaba juu ya kichwa chake, kulikuwa na maandishi haya: HUYU NDIYE MFALME WA WAYAHUDI. Maandishi haya yalikuwa yameandikwa kwa lugha ya Kiyunani, Kilatini na Kiebrania.
”Kisha akasema, “Bwana Yesu, unikumbuke utakapokuja katika Ufalme wako.”
”Kisha wakamwabudu na kurudi Yerusalemu wakiwa wamejawa na furaha kuu. Nao wakadumu ndani ya Hekalu wakimtukuza Mungu. Amen.
”Vitu vyote viliumbwa kwa yeye, wala pasipo yeye hakuna cho chote kilichoumbwa ambacho kimeumbwa.
”Neno alifanyika mwili, akakaa miongoni mwetu, nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli.
”Nathanaeli akamwambia, “Mwalimu, wewe ni Mwana wa Mungu! Wewe ni Mfalme wa Israeli!”
”Yeye hana budi kuwa mkuu zaidi na mimi nizidi kuwa mdogo.” “Yeye ajaye kutoka juu yu juu ya yote, yeye aliye wa duniani ni wa dunia, naye huzungumza mambo ya duniani. Yeye aliyekuja kutoka mbinguni, yu juu ya yote.
”Yesu akamjibu, “Mwanamke, niamini, wakati unakuja ambapo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala huko Yerusalemu. Ninyi Wasamaria mnaabudu msichokijua. Sisi Wayahudi tunamwabudu Mungu tunayemjua kwa sababu wokovu unatoka kwa Wayahudi. Lakini saa yaja, tena ipo, ambapo wale waabuduo halisi, watamwabudu Baba katika roho na kweli. Watu wanaoabudu namna hii, ndio Baba anawatafuta. Mungu ni Roho na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.”
”ili wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba. Ye yote asiyemheshimu Mwana, hamheshimu Baba aliyemtuma.
”Kisha Yesu akasema nao tena akawaambia, “Mimi ni nuru ya ulimwengu. Mtu ye yote akinifuata hatatembea gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.”
”Yesu akawaambia, “Amin, amin nawaambia, kabla Abrahamu hajakuwako, ‘Mimi niko.’ ”
”Yule mtu akasema, “Bwana, naamini.” Naye akamwabudu.
”Mimi na Baba yangu tu umoja.”
”Yesu akamwambia, “Sikukuambia kwamba kama ukiamini utauona utukufu wa Mungu?”
”Siku iliyofuata umati mkubwa uliokuwa umekuja kwenye Sikukuu walisikia kwamba Yesu angekuja Yerusalemu. Basi wakachukua matawi ya mitende wakatoka kwenda kumlaki, huku wakipaza sauti wakisema, “Hosana!” “Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana!” “Amebarikiwa Mfalme wa Israeli!” Yesu akamkuta mwana-punda akampanda, kama ilivyoandikwa, “Usiogope, Ewe binti Sayuni; tazama, Mfalme wako anakuja, amepanda mwana-punda!”
”Yesu akawajibu, “Saa imewadia ya Mwana wa Adamu kutukuzwa.
”Baba, litukuze jina lako.” Ndipo ikaja sauti kutoka mbinguni, “Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena.”
”Baada ya Yuda kutoka nje, Yesu akasema, “Sasa Mwana wa Adamu ametukuzwa, naye Mungu ametukuzwa ndani yake. Ikiwa Mungu ametukuzwa ndani ya Mwana, Mungu atamtukuza Mwana ndani yake mwenyewe naye atamtukuza mara.
”Nanyi mkiomba lo lote kwa Jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba apate kutukuzwa katika Mwana.
”Kwa hiyo Baba yangu hutukuzwa, kwa vile mzaavyo matunda mengi, nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.
”Baada ya Yesu kusema haya, alitazama kuelekea mbinguni akawaombea na kusema: “Baba, saa imewadia. Umtukuze Mwanao, ili Mwanao apate kukutukuza wewe. Kwa kuwa umempa mamlaka juu ya wote wenye mwili ili awape uzima wa milele wale uliompa. Nao uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe uliye Mungu wa pekee, wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma. Nimekutukuza wewe duniani kwa kuitimiza ile kazi uliyonipa niifanye. Hivyo sasa, Baba, unitukuze mbele zako kwa ule utukufu niliokuwa nao pamoja na wewe kabla ulimwengu haujakuwako.
”Wao wakamjibu, “Yesu wa Nazareti.” Yesu akawajibu, “Mimi ndiye.” Yuda, yule aliyemsaliti alikuwa amesimama pamoja nao. Yesu alipowaambia, “Mimi ndiye,” walirudi nyuma na kuanguka chini!
”Kwa hiyo Pilato akaingia ndani akamwita Yesu, akamwuliza, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?”
”Yesu akajibu, “Ufalme wangu si wa ulimwengu huu. Ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu wafuasi wangu wangenipigania ili nisitiwe mikononi mwa Wayahudi. Lakini kama ilivyo ufalme wangu hautoki hapa ulimwenguni.” Pilato akamwuliza, “Kwa hiyo wewe ni mfalme?” Yesu akajibu, “Wewe wasema kwamba mimi ni mfalme. Kwa kusudi hili nilizaliwa na kwa ajili ya hili nilikuja ulimwenguni ili niishuhudie kweli. Mtu ye yote aliye wa kweli husikia sauti yangu.”
”Lakini ninyi mna desturi yenu kwamba wakati wa Pasaka nimwachie huru mfungwa mmoja mnayemtaka. Je, mnataka niwafungulie huyu ‘Mfalme wa Wayahudi?’ ”
”Pilato akaamuru tangazo liandikwe na liwekwe juu kwenye msalaba wa Yesu: “YESU WA NAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI.” Kwa kuwa mahali hapo aliposulibiwa palikuwa karibu na mjini, Wayahudi wengi walisoma maandishi haya yaliyokuwa yameandikwa kwa lugha za Kiebrania, Kiyunani na Kilatini. Viongozi wa makuhani wa Wayahudi wakapinga, wakamwambia Pilato, “Usiandike, ‘Mfalme wa Wayahudi,’ bali andika kwamba, mtu huyu alisema, ‘Mimi ni mfalme wa Wayahudi.’ ” Pilato akawajibu, “Nilichokwisha kuandika, nimeandika!”
”Tomasi akamwambia, “Bwana wangu na Mungu wangu!”
”Basi ikiwa yeye ametukuzwa kwa mkono wa kuume wa Mungu, amepokea kutoka kwa Baba ahadi ya Roho Mtakatifu, naye amemimina kile mnachoona sasa na kusikia.
”“Kwa hiyo Israeli wote na wajue jambo hili kwa uhakika kwamba: Mungu amemfanya huyu Yesu, ambaye ninyi mlimsulibisha, kuwa Bwana na Kristo.”
”Akaruka juu na kusimama, akaanza kutembea. Kisha akaingia Hekaluni pamoja na Petro na Yohana, huku akitembea na kurukaruka na kumsifu Mungu.
”Mungu alimtukuza akamweka mkono wake wa kuume kuwa Kiongozi na Mwokozi ili awape Israeli toba na msamaha wa dhambi.
”“Ndipo Bwana akamwambia, ‘Vua viatu vyako kwa maana hapo unaposimama ni mahali patakatifu.
”Lakini yeye Stefano akiwa amejaa Roho Mtakatifu, alikaza macho mbinguni, akaona utukufu wa Mungu, naye Yesu akiwa amesimama mkono wa kuume wa Mungu. Akasema, “Tazameni! Naona mbingu zimefunguka na Mwana wa Adamu amesimama upande wa kuume wa Mungu.”
”Ninyi mnajua ule ujumbe uliotumwa kwa Israeli, ukitangaza habari njema za amani kwa Yesu Kristo. Yeye ni Bwana wa wote.
”Ilipokaribia usiku wa manane, Paulo na Sila walikuwa wakiomba na kuimba nyimbo za kumsifu Mungu, nao wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. Ghafula pakatokea tetemeko kubwa la ardhi, hata msingi wa gereza ukatikisika. Mara milango ya gereza ikafunguka na ile minyororo iliyowafunga kila mmoja ikafunguka.
”“Mungu aliyeumba dunia na vyote vilivyomo ndani yake, yeye ndiye Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika mahekalu yaliyojengwa kwa mikono ya wanadamu.
”na ambaye kwa uwezo wa Roho wa utakatifu alidhihirishwa kuwa Mwana wa Mungu kwa ufufuo wake kutoka kwa wafu, yaani, Yesu Kristo Bwana wetu.
”Kwa maana tangu kuumbwa kwa ulimwengu, asili ya Mungu asiyeonekana kwa macho, yaani, uweza wake wa milele na asili yake ya Uungu, umeonekana waziwazi ukitambuliwa kutokana na yale aliyoyafanya ili wanadamu wasiwe na udhuru.
”Wao ni wa uzao wa mababa wakuu wa kwanza, ambao kutoka kwao Kristo alikuja kwa jinsi ya mwili kama mwanadamu, yeye ambaye ni Mungu aliye juu ya vyote, mwenye kuhimidiwa milele! Amen.
”Tazama jinsi kilivyo kina cha utajiri wa hekima na maarifa ya Mungu! Tazama jinsi ambavyo hukumu zake hazichunguziki, na ambavyo njia zake zisivyotafutikana! “Ni nani aliyeijua nia ya Bwana? Au ni nani ambaye amekuwa mshauri wake?”
”Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake, viko kwake na kwa ajili yake. Utukufu ni wake milele! Amen.
”Kwa hiyo, ndugu zangu, nawasihi kwa rehema zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu na inayompendeza Mungu, hii ndiyo ibada yenu yenye maana.
”Kwa kuwa imeandikwa: “ ‘Kama niishivyo,’ asema Bwana, ‘kila goti litapigwa mbele zangu, na kila ulimi utamkiri Mungu.’ ”
”ili kwa moyo mmoja mpate kumtukuza Mungu aliye Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo. Karibishaneni ninyi kwa ninyi kama Kristo alivyowakaribisha ninyi ili kumletea Mungu utukufu. Kwa maana nawaambia kwamba, Kristo amekuwa mtumishi kwa wale waliotahiriwa ili kuonyesha kweli ya Mungu na kuthibitisha zile ahadi walizopewa baba zetu wa zamani, pia ili watu Mataifa wamtukuze Mungu kwa rehema zake. Kama ilivyoandikwa: “Kwa hiyo nitakutukuza katikati ya watu Mataifa; nitaliimbia sifa jina lako.” Tena yasema, “Enyi watu Mataifa, furahini pamoja na watu wa Mungu.” Tena, “Mhimidini Bwana, ninyi watu wote Mataifa, na kumwimbia sifa, enyi mataifa yote.”
”Sasa atukuzwe yeye awezaye kuwafanya ninyi imara kwa Injili yangu na kuhubiriwa kwa Yesu Kristo, kutokana na kufunuliwa siri zilizofichika tangu zamani za kale. Lakini sasa siri hiyo imefunuliwa na kujulikana kupitia maandiko ya kinabii kutokana na amri ya Mungu wa milele, ili mataifa yote yaweze kumwamini na kumtii Mungu aliye pekee, mwenye hekima, ambaye kwa njia ya Yesu Kristo utukufu una yeye milele na milele! Amen.
”kwa maana mmenunuliwa kwa gharama. Kwa hiyo mtukuzeni Mungu katika miili yenu na katika roho zenu ambazo ni mali ya Mungu.
”Lakini kwetu sisi yuko Mungu mmoja, aliye Baba, ambaye vitu vyote vyatoka kwake na kwa ajili yake sisi twaishi na kuna Bwana mmoja tu, Yesu Kristo, ambaye kwa yeye vitu vyote vimekuwepo na kwa yeye sisi tunaishi.
”Basi, lo lote mfanyalo, kama ni kula au kunywa, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.
”nazo siri za moyo wake zitawekwa wazi. Kwa hiyo ataanguka chini na kumwabudu Mungu akikiri, “Kweli Mungu yuko katikati yenu!”
”Kwa kuwa Mungu, yeye aliyesema, “Nuru na ing'ae gizani,” ameifanya nuru yake ing'ae mioyoni mwetu ili kutupatia nuru ya maarifa ya utukufu wa Mungu katika uso wa Kristo.
”aliyejitoa kwa ajili ya dhambi zetu ili apate kutuokoa kutoka katika ulimwengu huu wa sasa ulio mbaya, sawasawa na mapenzi yake yeye aliye Mungu na Baba yetu. Utukufu una yeye milele na milele. Amen.
”Ahimidiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki sisi kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho ndani ya Kristo.
”Kwa hiyo tunamsifu Mungu kwa huruma zake kuu alizotumiminia sisi katika Mwanawe Mpendwa.
”ili kwamba, sisi tuliokuwa wa kwanza kuweka tumaini katika Kristo, tupate kuishi kwa sifa ya utukufu wake. Ninyi pia mliingia ndani ya Kristo mliposikia Neno la kweli, Injili ya wokovu wenu. Mkiisha kuamini, ndani yake mlitiwa muhuri, yaani, Roho Mtakatifu mliyeahidiwa, yeye ambaye ni amana yetu akituhakikishia urithi wetu hadi ukombozi wa wale walio milki ya Mungu kwa sifa ya utukufu wake.
”Nazidi kumwomba Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awajalieni ninyi roho ya hekima na ya ufunuo, ili mpate kumjua zaidi. Ninaomba pia kwamba macho ya mioyo yenu yatiwe nuru ili mpate kujua tumaini mliloitiwa, utajiri wa urithi wa utukufu wake kwa watakatifu na uweza wake mkuu usiolinganishwa kwa ajili yetu sisi tuaminio. Uweza huo unaofanya kazi ndani yetu, ni sawa na ile nguvu kuu mno ambayo aliitumia alipomfufua Kristo kutoka kwa wafu, akamketisha mkono wake wa kuume katika mbingu, juu sana kuliko falme zote na mamlaka, enzi na milki na juu ya kila jina litajwalo, si katika ulimwengu huu tu, bali na katika ule ujao pia. Naye Mungu ameweka vitu vyote viwe chini ya miguu yake na amemfanya yeye awe kichwa cha vitu vyote kwa ajili ya Kanisa, ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake yeye aliye yote katika yote.
”Kwa sababu hii nampigia Baba magoti, ambaye ubaba wote wa kila jamaa za mbinguni na za duniani unatokana naye. Namwomba Mungu awaimarishe kwa kuwatia nguvu mioyo yenu kwa njia ya Roho wake kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, ili kwamba, Kristo apate kukaa mioyoni mwenu kwa njia ya imani. Nami ninaomba kwamba ninyi mkiwa wenye mizizi tena imara katika msingi wa upendo, mwe na uwezo wa kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, urefu, kimo na kina upendo wa Kristo na kujua upendo huu kwamba unapita fahamu, ili mpate kujazwa na kufikia kipimo cha ukamilifu wote wa Mungu. Basi kwa yeye awezaye kutenda mambo ya ajabu yasiyopimika kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya uweza wake ule utendao kazi ndani yetu, yeye atukuzwe katika kanisa na katika Kristo Yesu kwa vizazi vyote, milele na milele. Amen.
”Mungu mmoja ambaye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote, katika yote na ndani ya yote.
”Yeye aliyeshuka ndiye aliyepaa juu zaidi kupita mbingu zote, ili apate kuujaza ulimwengu wote.)
”Msemezane ninyi kwa ninyi kwa zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, mkimwimbia na kumsifu Bwana mioyoni mwenu, siku zote mkimshukuru Mungu Baba kwa kila jambo katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo.
”mkiwa mmejawa na matunda ya haki yapatikanayo kwa njia ya Yesu Kristo, kwa utukufu na sifa za Mungu.
”Kwa hiyo, Mungu alimtukuza juu sana na kumpa Jina lililo kuu kuliko kila jina, ili kwa Jina la Yesu, kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, vya duniani na vya chini ya nchi, na kila ulimi ukiri ya kwamba YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.
”Kwa maana sisi ndio tulio tohara, sisi tumwabuduo Mungu katika Roho, tunaona fahari katika Kristo Yesu, ambao hatuweki tumaini letu katika mwili,
”Mungu wetu aliye Baba yetu apewe utukufu milele na milele. Amen.
”Yeye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. Kwa yeye vitu vyote vilivyoko mbinguni na juu ya nchi viliumbwa, vile vitu vinavyoonekana na vile visivyoonekana, kama ni viti vya enzi au falme, au wenye mamlaka au watawala, vitu vyote viliumbwa na yeye na kwa ajili yake. Yeye alikuwapo kabla ya vitu vyote na katika yeye vitu vyote vinashikamana pamoja. Yeye ndiye kichwa cha mwili, yaani, Kanisa, naye ni wa mwanzo na mzaliwa wa kwanza kutoka kwa wafu, ili yeye awe mkuu katika vitu vyote. Kwa kuwa ilimpendeza Mungu kwamba ukamilifu wake wote wa Kiungu uwe ndani yake na kwa njia ya Mwanawe aweze kuvipatanisha vitu vyote na yeye mwenyewe, ikiwa ni vitu vilivyoko duniani au vilivyoko mbinguni, kwa kufanya amani kwa damu yake iliyomwagika msalabani.
”Kwao, Mungu amechagua kujulisha miongoni mwa watu Mataifa utukufu wa utajiri wa siri hii, ambayo ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu.
”Maana ukamilifu wote wa Uungu umo ndani ya Kristo katika umbile la mwili wa kibinadamu, nanyi mmepewa ukamilifu ndani ya Kristo, ambaye yeye ndiye mkuu juu ya kila enzi na kila mamlaka.
”Basi, kwa kuwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu, Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Yafikirini mambo yaliyo juu, wala si ya duniani. Kwa maana ninyi mlikufa, nao uhai wenu sasa umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. Wakati Kristo atakapotokea yeye aliye uzima wenu ndipo nanyi mtakapotokea pamoja naye katika utukufu.
”Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu, mkifundishana na kuonyana katika hekima yote, mkimwimbia Mungu zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni huku mkiwa na shukrani mioyoni mwenu. Lo lote mfanyalo, ikiwa ni kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika Jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba katika yeye.
”Kwa kusudi hili Mungu aliwaita kwa njia ya kuhubiri kwetu Injili, ili kwamba mpate kushiriki katika utukufu wa Bwana Yesu Kristo.
”Basi, Mfalme wa milele, asiye na mwisho, asiyeonekana, aliye Mungu pekee, apewe heshima na utukufu milele na milele. Amen.
”ambaye Mungu atamleta kwa wakati wake mwenyewe, yeye ahimidiwaye, aliye peke yake Mtawala, Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana. Yeye peke yake hapatikani na mauti, ambaye anakaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa, ambaye hakuna mwanadamu aliyemwona wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye milele. Amen.
”Bwana ataniokoa katika kila shambulio baya na kunileta salama katika Ufalme wake wa mbinguni. Atukuzwe yeye milele na milele. Amen.
”tukilitazamia tumaini lenye baraka na ufunuo wa utukufu wa Mungu wetu Mkuu na Mwokozi wetu Yesu Kristo,
”lakini katika siku hizi za mwisho anasema nasi kwa njia ya Mwanawe, ambaye amemweka kuwa mrithi wa vitu vyote, na ambaye kwa yeye aliuumba ulimwengu. Mwana ni mng'ao wa utukufu wa Mungu na mfano halisi wa nafsi yake, akivihifadhi vitu vyote kwa neno lake lenye uweza. Akiisha kufanya utakaso kwa ajili ya dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko mbinguni.
”Tena, Mungu amletapo mzaliwa wake wa kwanza ulimwenguni, husema, “Malaika wote wa Mungu na wamsujudu.” Anenapo kuhusu malaika husema, “Huwafanya malaika zake kuwa upepo, watumishi wake kuwa miali ya moto.” Lakini kwa habari za Mwana asema, “Kiti chako cha enzi, Ee Mungu, kitadumu milele na milele, nayo haki itakuwa fimbo ya utawala ya ufalme wako.
”Lakini twamwona Yesu, aliyefanywa chini kidogo kuliko malaika, sasa akiwa amevikwa taji ya utukufu na heshima kwa sababu alistahimili mauti, ili kwamba kwa neema ya Mungu apate kuonja mauti kwa ajili ya kila mtu.
”Yeye husema, “Nitalitangaza jina lako kwa ndugu zangu; mbele ya kusanyiko nitaimba sifa zako.”
”Kwa kuwa tunaye Kuhani Mkuu kuliko wote ambaye ameingia mbinguni, Yesu Mwana wa Mungu, basi na tushikamane sana kwa uthabiti na ule ukiri wa imani yetu. Kwa kuwa hatuna Kuhani Mkuu asiyeweza kuchukuliana na sisi katika udhaifu wetu, lakini tunaye mmoja ambaye alijaribiwa kwa kila namna, kama vile sisi tujaribiwavyo, lakini yeye hakutenda dhambi. Basi na tukikaribie kiti cha rehema kwa ujasiri, ili tupewe rehema na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.
”Kwa kuwa ilitupasa tuwe na Kuhani Mkuu wa namna hii, yaani, aliye mtakatifu, asiye na lawama, asiye na dosari, aliyetengwa na wenye dhambi na kuinuliwa juu ya mbingu.
”Basi jambo tunalotaka kulisema ni hili: Tunaye Kuhani Mkuu ambaye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni,
”Hakuingia kwa njia ya damu ya mbuzi na ya ndama, lakini aliingia Patakatifu pa Patakatifu mara moja tu kwa damu yake mwenyewe, akiisha kupata ukombozi wa milele.
”Lakini huyu kuhani akiisha kutoa dhabihu moja kwa ajili ya dhambi kwa wakati wote, aliketi mkono wa kuume wa Mungu.
”Kwa hiyo, ndugu zangu, kwa kuwa tunao ujasiri wa kupaingia Patakatifu pa Patakatifu kwa damu ya Yesu,
”Basi na tumtazame sana Yesu mwanzilishi na mkamilishaji wa imani yetu, yeye ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake alistahimili msalaba, bila kujali aibu ya huo msalaba, naye ameketi mkono wa kuume wa Mungu.
”Kwa hiyo, kwa kuwa tunapokea ufalme ule ambao hauwezi kutetemeshwa, basi na tuwe na shukrani na hivyo tumwabudu Mungu kwa namna inavyompendeza, kwa unyenyekevu na uchaji, kwa kuwa “Mungu wetu ni moto ulao.”
”Yesu Kristo ni yeye yule jana, leo na hata milele.
”Basi kwa njia ya Yesu, tuzidi kumtolea Mungu dhabihu ya sifa, yaani, matunda ya midomo inayolikiri Jina lake.
”Basi Mungu wa amani, ambaye kwa damu ya Agano la milele alimleta tena kutoka kwa wafu Bwana wetu Yesu, yule Mchungaji Mkuu wa kondoo, awafanye ninyi wakamilifu mkiwa mmekamilishwa katika kila jambo jema ili mpate kutenda mapenzi yake, ili atende ndani yetu kile kinachompendeza machoni Pake, kwa njia ya Yesu Kristo, ambaye utukufu una yeye milele na milele. Amen.
”Je, mtu ye yote miongoni mwenu amepatwa na taabu? Basi inampasa aombe. Je, kuna ye yote mwenye furaha? Basi na aimbe nyimbo za kusifu.
”ambaye ameingia mbinguni na amekaa mkono wa kuume wa Mungu: pamoja na malaika, mamlaka na nguvu zote vikiwa vimetiishwa chini yake.
”Ye yote asemaye hana budi kusema kama mtu asemaye maneno ya Mungu mwenyewe. Ye yote ahudumuye hana budi kuhudumu kwa nguvu zile apewazo na Mungu, ili Mungu apate kutukuzwa katika mambo yote kwa njia ya Yesu Kristo. Utukufu na uweza una yeye milele na milele. Amen.
”Lakini kama mtu ye yote akiteseka kwa kuwa ni mkristo, asihesabu jambo hilo kuwa ni aibu, bali amtukuze Mungu kwa sababu ameitwa kwa jina hilo.
”Nanyi mkiisha kuteswa kwa kitambo kidogo, Mungu wa neema yote aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele ndani ya Kristo, yeye mwenyewe atawatengeneza upya, atawasaidia, atawatia nguvu na kuwathibitisha. Uweza una yeye milele na milele. Amen.
”Tulipowafahamisha juu ya uweza na kuja kwa Bwana wetu Yesu Kristo, hatukufuata hadithi zilizotungwa kwa werevu, bali tulishuhudia kwa macho yetu ukuu wake. Maana alipewa heshima na utukufu kutoka kwa Mungu Baba, sauti ilipomjia katika Utukufu Mkuu ikisema, “Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.”
”Bali kueni katika neema na katika kumjua Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na milele! Amen.
”kwake yeye Mungu pekee Mwokozi wetu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu, utukufu, ukuu, uweza na mamlaka vina yeye tangu milele, sasa na hata milele! Amen.
”na kutoka kwa Yesu Kristo ambaye ni shahidi mwaminifu, aliye mzaliwa wa kwanza kutoka kwa wafu, ambaye yeye ndiye mtawala wa wafalme wa dunia. Kwake yeye anayetupenda na ambaye ametuweka huru kutoka katika dhambi zetu kwa damu yake, akatufanya sisi kuwa ufalme na makuhani, tumtumikie Mungu wake ambaye ni Baba yake. Utukufu na uwezo vina yeye milele na milele! Amen. Tazama! Anakuja na mawingu na kila jicho litamwona, hata wale waliomchoma mkuki; na mataifa yote ulimwenguni yataomboleza kwa sababu yake. Naam, ndivyo itakavyokuwa! Amen.
”“Mimi ni Alfa na Omega,” asema Bwana Mungu, “aliyeko, aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.”
”Ndipo nikageuka ili nione ni sauti ya nani iliyokuwa ikisema nami. Nami nilipogeuka, nikaona vinara saba vya taa vya dhahabu, katikati ya vile vinara vya taa, nikaona mtu kama Mwana wa Adamu, amevaa joho refu na mkanda wa dhahabu umefungwa kifuani mwake. Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu, nyeupe kama theluji, nayo macho yake yalikuwa kama mwali wa moto. Nyayo zake zilikuwa kama shaba iliyosuguliwa sana, kama vile imesafishwa katika tanuru ya moto, nayo sauti yake ilikuwa kama sauti ya maji mengi. Katika mkono wake wa kuume alishikilia nyota saba na kinywani mwake ulitoka upanga wenye makali kuwili. Uso wake kama jua kali linalong'aa kwa nguvu zake zote. Nilipomwona, nilianguka miguuni pake kama aliyekufa. Ndipo akaweka mkono wake wa kuume juu yangu na kusema: “Usiogope, Mimi ni wa Kwanza na wa Mwisho. Mimi ni yeye aliye hai, niliyekuwa nimekufa na tazama, ni hai milele na milele! Nami ninazo funguo za mauti na kuzimu.
”Ghafula nilikuwa katika Roho, hapo mbele yangu kilikuwapo kiti cha enzi mbinguni, kikiwa kimekaliwa na mtu mmoja. Yeye aliyekuwa amekikalia alikuwa anaonekana kama yaspi na akiki. Kukizunguka kile kiti cha enzi palikuwa na upinde wa mvua ulioonekana kama zumaridi. Pia kukizunguka hicho kiti cha enzi palikuwa na viti ishirini na vinne na juu ya hivyo viti walikuwa wameketi wazee ishirini na wanne, waliovaa majoho meupe, wakiwa na taji za dhahabu vichwani mwao.
”Kwenye kile kiti cha enzi palikuwa panatoka miali ya umeme wa radi, ngurumo na sauti za radi. Mbele ya hicho kiti cha enzi, palikuwa na taa saba zilizokuwa zinawaka. Hizi ndizo Roho saba za Mungu. Pia mbele ya hicho kiti cha enzi palikuwa na kile kilichoonekana kama bahari ya kioo, iliyokuwa angavu kama jiwe lisilo na rangi yo yote ling'aalo sana. Katikati, kukizunguka kile kiti cha enzi, kulikuwa na viumbe wanne wenye uhai, wakiwa wamejawa na macho mbele na nyuma.
”Kila mmoja wa hawa viumbe wenye uhai wanne, alikuwa na mabawa sita na kujawa na macho pande zote, hadi chini ya mabawa. Usiku na mchana hawakuacha kusema: “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni BWANA Mungu Mwenyezi, aliyekuwako, aliyeko na atakayekuja.” Kila mara viumbe hao wenye uhai wanne walipomtukuza, kumheshimu na kumshukuru yeye aliyeketi kwenye kile kiti cha enzi, tena aishiye milele na milele, wale wazee ishirini na wanne huanguka mbele zake yeye aliyeketi kwenye kile kiti cha enzi na kumwabudu yeye aliye hai milele na milele. Wao huziweka taji zao mbele ya hicho kiti cha enzi, wakisema: “Bwana wetu na Mungu wetu, wewe umestahili kupokea utukufu na heshima na uweza, kwa maana ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa mapenzi yako viliumbwa na vimekuwako.”
”Kisha, mmoja wa wale wazee akaniambia, “Usilie! Tazama, Simba wa kabila la Yuda, wa Uzao wa Daudi, ameshinda. Yeye ndiye anayeweza kukifungua hicho kitabu na kuvunja hizo lakiri zake saba.” Ndipo nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale viumbe wenye uhai wanne na miongoni mwa wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, akiwa kama amechinjwa. Alikuwa na pembe saba na macho saba, ambazo ndizo zile Roho saba za Mungu zilizotumwa duniani pote. Huyo Mwana-Kondoo akaja na kukitwaa kile kitabu kutoka kwenye mkono wa kuume wa yule aliyeketi kwenye kile kiti cha enzi. Alipokwisha kukitwaa kile kitabu, wale viumbe wenye uhai wanne pamoja na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele ya yule Mwana-Kondoo. Kila mmoja wao alikuwa na kinubi, nao walikuwa wameshika mabakuli ya dhahabu yaliyojaa uvumba, ambayo ni maombi ya watakatifu. Nao wakaimba wimbo mpya, wakisema: “Wewe unastahili kukitwaa kitabu na kuzivunja lakiri zake, kwa sababu ulichinjwa na kwa damu yako ukamnunulia Mungu watu kutoka katika kila kabila, kila lugha, kila jamaa na kila taifa. Wewe umewafanya hawa wawe ufalme na makuhani wa kumtumikia Mungu wetu, nao watatawala duniani.”
”Kisha nikatazama, nikasikia sauti za malaika wengi wakiwa wamekizunguka kile kiti cha enzi, pamoja na wale viumbe wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne, idadi yao ilikuwa kumi elfu mara kumi elfu na maelfu ya maelfu. Nao wakiimba kwa sauti kuu, wakisema: “Anastahili Mwana-Kondoo, yeye aliyechinjwa, kupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na sifa!” Kisha nikasikia kila kiumbe mbinguni na duniani, chini ya nchi na baharini na vyote vilivyomo ndani yake vikiimba: “Sifa na heshima na utukufu na uweza ni vyake yeye aketiye juu ya hicho kiti cha enzi na kwa Mwana-Kondoo, milele na milele!” Wale viumbe wenye uhai wanne wakasema, “Amen!” Nao wale wazee ishirini na wanne wakaanguka kifudifudi wakaabudu.
”Baada ya hili nikatazama na hapo mbele yangu palikuwa na umati mkubwa wa watu ambao hakuna ye yote awezaye kuuhesabu, kutoka kila taifa, kila kabila, kila jamaa na kila lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi na mbele ya Mwana-Kondoo. Walikuwa wamevaa mavazi meupe na wakiwa wameshika matawi ya mitende mikononi mwao. Nao walikuwa wakipiga kelele kwa sauti kubwa wakisema: “Wokovu una Mungu wetu, yeye aketiye kwenye kiti cha enzi na Mwana-Kondoo!” Malaika wote walikuwa wamesimama kukizunguka kile kiti cha enzi na wale wazee ishirini na wanne na wale viumbe wanne wenye uhai. Wakaanguka kifudifudi mbele ya hicho kiti cha enzi na kumwabudu Mungu, wakisema: “Amen! Sifa na utukufu na hekima na shukrani na heshima na uweza na nguvu viwe kwa Mungu wetu milele na milele. Amen!”
”Kwa hiyo, “Wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu na kumtumikia usiku na mchana katika Hekalu lake; naye aketiye katika kile kiti cha enzi atakaa pamoja nao na kuwalinda.
”Yule malaika wa saba akaipiga tarumbeta yake, pakawa na sauti kubwa mbinguni iliyosema: “Ufalme wa ulimwengu umekuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atatawala milele na milele.” Nao wale wazee ishirini na wanne, waliokuwa wameketi mbele za Mungu, kwenye viti vyao vya enzi wakaanguka kifudifudi wakamwabudu Mungu, wakisema: “Tunakushukuru, BWANA Mungu Mwenyezi, uliyeko na uliyekuwako, kwa kuwa umetwaa uweza wako mkuu na ukaanza kutawala.
”Kisha nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema: “Sasa Wokovu na uweza na Ufalme wa Mungu wetu umekuja na mamlaka ya Kristo wake. Kwa kuwa ametupwa chini mshtaki wa ndugu zetu, anayewashtaki mbele za Mungu usiku na mchana.
”Nami nikasikia sauti kutoka mbinguni kama sauti ya maji mengi yaendayo kasi na sauti kama ngurumo ya radi. Sauti hiyo niliyoisikia ilikuwa kama sauti ya wapiga vinubi wakipiga vinubi vyao. Nao wakaimba wimbo mpya mbele ya hicho kiti cha enzi na mbele ya wale viumbe wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne. Hakuna mtu ye yote aliyeweza kujifunza wimbo huo isipokuwa hao 144,000 waliokuwa wamekombolewa kutoka duniani. Hawa ndio wale ambao hawakujitia unajisi kwa wanawake, kwa kuwa wao ni mabikira. Wao humfuata Mwana-Kondoo kila aendako. Hawa wamekombolewa kutoka miongoni mwa wanadamu wakawa malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo. Vinywani mwao hapakuonekana uongo, wala hawakuwa na hatia yo yote.
”Akasema kwa sauti kubwa, “Mcheni Mungu na kumpa utukufu, kwa maana saa ya hukumu yake imewadia. Mwabuduni yeye aliyeziumba mbingu, dunia, bahari na chemchemi za maji.”
”Nikatazama, hapo mbele yangu palikuwa na wingu jeupe, na aliyekuwa ameketi juu ya hilo wingu alikuwa “kama Mwana wa Adamu” mwenye taji ya dhahabu kichwani mwake na mundu mkali mkononi mwake.
”Nao wakaimba wimbo wa Mose, mtumishi wa Mungu na wimbo wa Mwana-Kondoo wakisema: “BWANA Mungu Mwenyezi, matendo yako ni makuu na ya ajabu. Njia zako wewe ni za haki na za kweli Mfalme wa nyakati zote! Ni nani ambaye hatakuogopa wewe Bwana na kulitukuza jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako ndiwe mtakatifu. Mataifa yote yatakuja na kuabudu mbele zako, kwa kuwa matendo yako ya haki yamedhihirishwa.”
”Nalo lile Hekalu lilijawa na moshi uliotokana na utukufu wa Mungu na uweza wake, wala hakuna ye yote aliyeweza kuingia mle Hekaluni mpaka yale mapigo saba ya wale malaika saba yalipomalizika.
”Watafanya vita na Mwana-Kondoo, lakini Mwana-Kondoo atawashinda kwa sababu yeye ni Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme. Yeye atakuwa pamoja na watu wake walioitwa ambao ni wateule wake na wafuasi wake waaminifu.”
”Baada ya haya nikasikia sauti kama ya umati mkubwa mbinguni wakipiga kelele wakisema: “Haleluya! Wokovu na utukufu na uweza ni vya Mungu wetu,
”Wale wazee ishirini na wanne pamoja na wale viumbe wenye uhai wanne wakaanguka kifudifudi, wakamwabudu Mungu, aliyekuwa ameketi kwenye kile kiti cha enzi. Wakasema kwa sauti kuu: “Amen, Haleluya!” Kisha sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi, ikisema: “Msifuni Mungu wetu, ninyi watumishi wake wote, ninyi nyote mnaomcha, wadogo kwa wakubwa!” Kisha nikasikia sauti kama ya umati mkubwa, kama sauti ya maji mengi yaendayo kasi na kama ngurumo kubwa ya radi wakipiga kelele wakisema: “Haleluya! Kwa maana BWANA Mungu wetu Mwenyezi anatawala. Tufurahi, tushangilie na kumpa utukufu! Kwa maana arusi ya Mwana-Kondoo imewadia na bibi arusi wake amejiweka tayari.
”Macho yake ni kama miali ya moto na juu ya kichwa chake kuna taji nyingi. Alikuwa na jina lililoandikwa ambalo hakuna mtu ye yote anayelijua isipokuwa yeye mwenyewe. Alikuwa amevaa joho lililochovywa kwenye damu na Jina lake ni “Neno la Mungu.” Majeshi ya mbinguni walikuwa wakimfuata, wakiwa wamepanda farasi weupe, hali wamevaa mavazi ya kitani nzuri, nyeupe safi. Kinywani mwake hutoka upanga mkali ambao kwa huo atayaangusha mataifa. “Atayatawala kwa fimbo yake ya utawala ya chuma.” Atalikanyaga shinikizo la mvinyo wa ghadhabu ya Mungu Mwenyezi.
”Kwenye joho lake na paja lake liliandikwa jina hili: MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA.
”Kisha nikaona kiti kikubwa cheupe cha enzi pamoja na yeye aliyeketi juu yake. Dunia na mbingu zikaukimbia uso wake wala mahali pao hapakuonekana. Nami nikawaona wafu wakubwa na wadogo, wakiwa wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi na vitabu vikafunguliwa. Pia kitabu kingine kikafunguliwa ambacho ni cha uzima. Hao wafu wakahukumiwa sawasawa na matendo yao kama yalivyoandikwa ndani ya hivyo vitabu.
”Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya, kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza vimekwisha kupita, wala hapakuwepo na bahari tena. Nikaona Mji Mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, ukiwa umeandaliwa kama bibi arusi aliyepambwa kwa ajili ya mumewe. Nami nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, “Sasa makao ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atakaa pamoja nao. Yeye atakuwa Mungu wao nao watakuwa watu wake, naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.
”Sikuona Hekalu ndani ya huo mji kwa sababu BWANA Mungu Mwenyezi na Mwana-Kondoo ndio Hekalu lake. Ule mji hauhitaji jua wala mwezi kuuangazia, kwa sababu utukufu wa Mungu ndio nuru yake na Mwana-Kondoo ndiye taa yake.
”Kisha yule malaika akanionyesha mto wa maji ya uzima, maangavu kama kioo yakitiririka kutoka kwenye kile kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo, kupitia katikati ya barabara kuu ya huo mji. Kwenye kila upande wa huo mto kulikuwa na mti wa uzima utoao matunda ya aina kumi na mbili, ukizaa matunda yake kila mwezi. Nayo majani ya mti huo ni kwa ajili ya uponyaji wa mataifa. Katika mji huo hakutakuwa tena na kitu cho chote kilicholaaniwa, bali kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo kitakuwamo humo na watumishi wake watamtumikia, nao watamwona uso wake na Jina lake litakuwa kwenye vipaji vya nyuso zao.
”Mimi ni Alfa na Omega, wa Kwanza na wa Mwisho, Mwanzo na Mwisho.
”