31 – Uinjilisti

Haya ni maneno matakatifu ya Mungu Mwenyezi.
Hatupendi maneno ya wanadamu.
Kwa mtu yeyote anayempenda Mungu... hivi ndivyo Mungu anasema kuhusu: Uinjilisti.

Mistari 3 Muhimu Zaidi

Lakini watamwitaje yeye ambaye hawajamwamini? Nao watawezaje kumwamini yeye ambaye hawajamsikia? Tena watamsikiaje bila mtu kuwahubiria? Nao watahubirije wasipopelekwa? Kama ilivyaoandikwa, “Ni mizuri mno miguu ya hao wanaohubiri Injili ya amani na kuleta habari ya mema!”

Kwa maana sisi kwa Mungu ni harufu nzuri ya manukato ya Kristo miongoni mwa wale wanaookolewa na kwa wale wanaopotea, sisi kwa wale wanaopotea ni harufu ya mauti iletayo mauti, lakini kwa wale wanaookolewa sisi ni harufu nzuri iletayo uzima. Ni nani awezaye mambo hayo?

Kama mtu ye yote hatawakaribisha ninyi, wala kusikiliza maneno yenu, kung'uteni mavumbi kutoka kwenye miguu yenu mtakapokuwa mnatoka kwenye nyumba hiyo au mji huo. Amin, amin nawaambia, miji ya Sodoma na Gomora itastahimili zaidi katika hukumu kuliko mji huo.

Kila Mstari katika Mpangilio wa Biblia - 307 vifungu

“Kwa muda dunia idumupo, wakati wa kupanda na wa kuvuna, wakati wa baridi na wa joto, wakati wa kiangazi na wa masika, mchana na usiku kamwe havitakoma.”

Mose akamjibu, “Itakuwaje kama hawataniamini au kunisikiliza, waseme, ‘BWANA hakukutokea’?”

Mose akamwambia BWANA, “Ee Bwana, kamwe sijapata kuwa msemaji kwa ufasaha wakati uliopita wala tangu ulipoanza kuzungumza na mtumishi wako. Ulimi wangu ni mzito kuzungumza.” BWANA akamwambia, “Ni nani aliyempa mwanadamu kinywa? Ni nani aliyemfanya mtu kuwa kiziwi au bubu? Ni nani anayempa mtu kuona au upofu? Je, si mimi, BWANA? Sasa nenda, nitakusaidia kusema, nami nitakufundisha jambo la kusema.”

Lakini Mose akasema, “Ee Bwana, tafadhali mtume mtu mwingine kufanya kazi hiyo.” Ndipo hasira ya BWANA ikawaka dhidi ya Mose, akamwambia, “Vipi kuhusu ndugu yako, Aroni Mlawi? Ninajua yeye anaweza kuzungumza vizuri. Naye yuko tayari njiani kukulaki, na moyo wake utafurahi wakati atakapokuona. Utazungumza naye na kuweka maneno kinywani mwake. Nitawasaidia ninyi wawili kusema, nami nitawafundisha jambo la kufanya. Aroni ataongea na watu badala yako na itakuwa kwamba yeye amekuwa kinywa chako nawe utakuwa kama Mungu kwake.

Kila mahali nyayo za miguu yenu zitakapokanyaga nimewapa, kama vile nilivyomwahidi Mose.

Mwimbieni BWANA dunia yote; tangazeni wokovu wake siku baada ya siku. Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa, matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote.

Nimehubiri haki katika kusanyiko kubwa, sikufunga mdomo wangu, Ee BWANA, kama ujuavyo. Sikuficha haki yako moyoni mwangu; ninasema juu ya uaminifu wako na wokovu wako. Sikuficha upendo wako na kweli yako mbele ya kusanyiko kubwa.

Kinywa changu kitasimulia haki yako, wokovu wako mchana kutwa, ingawa sifahamu kipimo chake. Ee BWANA Mwenyezi, nitakuja na kutangaza matendo yako makuu, nitatangaza haki yako, yako peke yako. Ee Mungu, umenifundisha tangu ujana wangu, hadi leo ninatangaza matendo yako ya ajabu. Ee Mungu, usiniache, hata niwapo mzee wa mvi, mpaka nitangaze uwezo wako kwa kizazi kijacho, nguvu zako kwa wote watakaokuja baadaye.

Mwimbieni BWANA, lisifuni jina lake; tangazeni wokovu wake siku baada ya siku. Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa, matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote.

Nitasema sheria zako mbele za wafalme wala sitaaibishwa,

Wapandao kwa machozi watavuna kwa nyimbo za shangwe. Yeye azichukuaye mbegu zake kwenda kupanda, huku akilia, atarudi kwa nyimbo za shangwe, akiwa ameyachukua matita ya mavuno yake.

Ee BWANA, weka mlinzi kinywani mwangu, weka ulinzi mlangoni mwa midomo yangu.

Kizazi kimoja kitasifia kazi zako kwa kizazi kingine, watasimulia matendo yako makuu.

Mtu mwovu hupata ujira wa udanganyifu, bali yeye apandaye haki huvuna tuzo ya uhakika.

Tunda la mwenye haki ni mti wa uzima, naye mwenye hekima huvuta roho za watu.

Mtazamo wa tabasamu huleta furaha moyoni, nazo habari njema huipa mifupa afya. Yeye asikilizaye maonyo yatoayo uzima atakuwa miongoni mwa wenye hekima. Yeye anayedharau maonyo hujidharau mwenyewe, bali ye yote anayekubali maonyo hupata ufahamu. Kumcha BWANA humfundisha mtu hekima, nao unyenyekevu huja kabla ya heshima.

Maneno ya kupendeza ni kama sega la asali, ni matamu kwa nafsi na uponyaji kwenye mifupa.

Mtu mwenye maarifa hutumia maneno kwa kujizuia, naye mtu mwenye ufahamu ana moyo wa utulivu. Hata mtu mpumbavu hudhaniwa kuwa na hekima kama akinyamaza, na mwenye ufahamu kama akiuzuia ulimi wake.

Mpumbavu hafurahii ufahamu, bali hufurahia kutangaza maoni yake mwenyewe.

Midomo ya mpumbavu humletea ugomvi na kinywa chake hualika kipigo. Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake na midomo yake ni mtego kwa nafsi yake.

Yeye ajibuye kabla ya kusikiliza, huo ni upumbavu wake na aibu yake.

Mauti na uzima viko katika uwezo wa ulimi, nao waupendao watakula matunda yake.

Kama vile maji baridi kwa nafsi iliyochoka ndivyo zilivyo habari njema kutoka nchi ya mbali.

wakati wa kurarua na wakati wa kushona, wakati wa kunyamaza na wakati wa kuzungumza,

Ye yote atazamaye upepo hatapanda, ye yote aangaliaye mawingu hatavuna.

Panda mbegu yako asubuhi, nako jioni usiruhusu mikono yako ilegee, kwa maana hujui ni ipi itakayofanikiwa, kwamba ni hii au ni ile, au kwamba zote zitafanikiwa sawasawa.

Mhubiri hakuwa tu na hekima, bali aliwagawia watu maarifa pia. Alitafakari na kutafiti na akaweka katika utaratibu mithali nyingi. Mhubiri alitafiti ili kupata maneno sahihi na kila alichoandika kilikuwa sawa na kweli.

Kisha nikasikia sauti ya Bwana ikisema, “Nimtume nani? Ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu?” Nami nikasema, “Mimi hapa. Nitume mimi!”

Akasema, “Nenda ukawaambie watu hawa: “ ‘Mtaendelea daima kusikia, lakini kamwe hamtafahamu; mtaendelea daima kuona, lakini kamwe hamtatambua.’ Fanya mioyo ya watu hawa kuwa migumu, fanya masikio yao yasisikie na upofushe macho yao. Ama sivyo wanaweza kuona kwa macho yao, wakasikia kwa masikio yao, wakatambua kwa mioyo yao, nao wakageuka na kuponywa.” Ndipo nikasema, “Hadi lini, Ee Bwana?” Naye akanijibu: “Hadi miji iwe imeachwa magofu na bila wakazi, hadi nyumba zitakapobaki bila watu, na mashamba yatakapoharibiwa na kuangamizwa,

Kwa sheria na kwa ushuhuda! Kama hawatasema sawasawa na neno hili, hawana mwanga wa mapambazuko.

Hawatadhuru wala kuharibu juu ya mlima wangu mtakatifu wote, kwa kuwa dunia itajawa na kumjua BWANA kama maji yajazavyo bahari.

Wewe uletaye habari njema Sayuni, panda juu ya mlima mrefu. Wewe uletaye habari njema Yerusalemu, inua sauti yako kwa kupiga kelele, inua sauti, usiogope; iambie miji ya Yuda, “Yuko hapa Mungu wenu!”

Tazama jinsi ilivyo mizuri juu ya milima miguu yao wale waletao habari njema, wale wanaotangaza amani, wanaoleta habari njema, wanaotangaza wokovu, wauambiao Sayuni, “Mungu wako anatawala!”

Roho wa BWANA Mwenyezi yu juu yangu, kwa sababu BWANA amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao, kutangaza mwaka wa BWANA uliokubaliwa na siku ya kisasi ya Mungu wetu, kuwafariji wote waombolezao, na kuwapa mahitaji wale wanaohuzunika katika Sayuni, ili kuwapa taji ya uzuri badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho ya kukata tamaa. Nao wataitwa mialoni ya haki, pando la BWANA kwa ajili ya kuonyesha utukufu wake.

Nami nikasema, “Aa, BWANA Mwenyezi, sijui kusema, kwani mimi ni mtoto mdogo tu.” Lakini BWANA akaniambia, “Usiseme, ‘Mimi ni mtoto mdogo tu.’ Utakwenda po pote nitakapokutuma na kunena lo lote nitakalokuagiza. Usiwaogope, kwa maana niko pamoja nawe nikuokoe,” asema BWANA. Kisha BWANA akaunyosha mkono wake na kugusa kinywa changu, akaniambia, “Sasa nimeyaweka maneno yangu kinywani mwako.

“Lakini sasa nitawaagiza wavuvi wengi,” asema BWANA, “nao watawavua. Baada ya hilo nitawaagizia wawindaji wengi, nao watawawinda kwenye kila mlima na kilima na katika nyufa za miamba.

Naye akaniambia, “Mwanadamu, kula kile kilichoko mbele yako, kula huu ukurasa wa kitabu, kisha uende ukaseme na nyumba ya Israeli.” Ndipo nikafungua kinywa changu, naye akanilisha ule ukurasa wa kitabu. Ndipo akaniambia, “Mwanadamu, kula ukurasa huu wa kitabu ninaokupa ujaze tumbo lako.” Kwa hiyo nikaula, ulikuwa mtamu kama asali kinywani mwangu. Kisha akaniambia, “Mwanadamu, sasa nenda katika nyumba ya Israeli ukaseme nao maneno yangu.

Wale wenye hekima watang'aa kama mwanga wa mbingu, nao wale ambao huwaongoza wengi kutenda haki, watang'aa kama nyota milele na milele.

Ndipo neno la BWANA likamjia Yona mara ya pili: “Ondoka uende katika mji mkubwa wa Ninawi, ukautangazie ujumbe ninaokupa.”

Siku ya kwanza, Yona aliingia mjini. Akatangaza: “Baada ya siku arobaini Ninawi utaangamizwa.” Watu wa Ninawi wakamwamini Mungu, wakatangaza kufunga, watu wote kuanzia mkubwa sana hadi yule mdogo kabisa, wakavaa nguo za gunia. Habari zilipomfikia mfalme wa Ninawi, aliondoka kwenye kiti chake cha enzi, akavua majoho yake ya kifalme, akajifunika nguo ya gunia kisha akaketi chini mavumbini. Ndipo akatoa tangazo katika Ninawi yote: “Kwa amri ya mfalme na wakuu wake: “Msiruhusu mtu ye yote au mnyama, makundi ya ng'ombe au wanyama wengine wafugwao, kuonja kitu cho chote, msiwaruhusu kula wala kunywa. Bali wanadamu na wanyama wafunikwe kwa nguo za gunia. Kila mmoja afanye hima kumwomba Mungu. Waziache njia zao mbaya na udhalimu ulio mikononi mwao. Ni nani ajuaye? Huenda Mungu akaghairi kwa huruma yake akaacha hasira yake kali ili tusiangamie.” Mungu alipoona walivyofanya na jinsi walivyogeuka kutoka katika njia zao mbaya, akawa na huruma wala hakuleta maangamizi juu yao kama alivyokuwa ameonya.

Tazama, huko juu milimani, miguu ya huyo mmoja aletaye habari njema, ambaye anatangaza amani! Ee Yuda, sheherekea sikukuu zako, nawe utimize nadhiri zako. Waovu hawatakuvamia tena; wataangamizwa kabisa.

Siku hizo Yohana Mbatizaji alikuja akihubiri katika Nyika ya Uyahudi, akisema, “Tubuni, kwa maana Ufalme wa Mbinguni u karibu.”

Lakini alipowaona Mafarisayo na Masadukayo wengi wakija ili kubatizwa, aliwaambia, “Ninyi watoto wa nyoka! Ni nani aliyewaonya kuikimbia ghadhabu inayokuja? Basi zaeni matunda yastahiliyo toba.

Lakini Yesu akajibu, “Imeandikwa, ‘Mtu haishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.’ ”

Tangu wakati huo, Yesu alianza kuhubiri akisema: “Tubuni, kwa maana Ufalme wa Mbinguni umekaribia.”

Yesu akawaambia, “Njoni, nifuateni, nami nitawafanya muwe wavuvi wa watu.” Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata. Alipoendelea mbele kutoka pale, akawaona ndugu wengine wawili, Yakobo mwana wa Zebedayo na Yohana nduguye, wakiwa wamekaa kwenye mashua pamoja na baba yao Zebedayo wakiziandaa nyavu zao. Yesu akawaita. Nao mara wakaziacha nyavu zao, pamoja na baba yao, wakamfuata.

Yesu akapita katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, akihubiri habari njema za Ufalme wa Mungu, akiponya kila ugonjwa na kila aina ya maradhi miongoni mwa watu.

“Heri ninyi watu watakapowashutumu na kuwatesa na kunena dhidi yenu mabaya ya aina zote kwa uongo kwa ajili yangu. Furahini na kushangilia kwa maana thawabu yenu ni kuu. “Ninyi ni chumvi ya ulimwengu. Lakini chumvi ikipoteza ladha yake, yawezaje kurudishiwa ladha yake tena? Haifai tena kwa kitu cho chote, ila kutupwa nje ikanyagwe na watu.

“Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji uliojengwa kilimani hauwezi kufichika. Wala watu hawawashi taa na kuifunika kwa bakuli. Badala yake, huiweka kwenye kinara chake, nayo hutoa mwanga kwa kila mtu aliyemo ndani ya ile nyumba. Vivyo hivyo, nuru yenu iangaze mbele ya watu, ili wapate kuona matendo yenu mema wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.

“Msijiwekee hazina duniani, mahali ambapo nondo na kutu huharibu, nao wevi huvunja na kuiba. Lakini jiwekeeni hazina mbinguni, mahali ambapo nondo na kutu haviharibu, wala wevi hawavunji na kuiba. Kwa sababu mahali hazina yako ilipo, hapo ndipo pia moyo wako utakapokuwa.

Mwanafunzi mwingine akamwambia, “Bwana, niruhusu kwanza nikamzike baba yangu.” Lakini Yesu akamwambia, “Nifuate, nawe waache wafu wazike wafu wao.”

Yesu alipokuwa akienda kutoka huko, alimwona mtu mmoja jina lake Mathayo akiwa ameketi forodhani mahali pa kutoza ushuru. Yesu akamwambia, “Nifuate.” Mathayo akaondoka, akamfuata.

Yesu akazunguka katika miji yote na vijiji vyote, akifundisha katika masinagogi yao, akihubiri habari njema za Ufalme na kuponya kila ugonjwa na kila aina ya maradhi miongoni mwa watu.

Ndipo akawaambia wanafunzi wake, “Mavuno ni mengi lakini watenda kazi ni wachache, Kwa hiyo mwombeni Bwana wa mavuno, ili apeleke watenda kazi katika shamba lake la mavuno.”

Wakati mnapokwenda, hubirini mkisema, ‘Ufalme wa Mbinguni umekaribia.’ Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo wachafu. Mmepata bure, toeni bure.

Msichukue dhahabu, wala fedha, wala shaba kwenye vifuko vyenu. Msichukue mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala jozi ya pili ya viatu, wala fimbo, kwa maana mtenda kazi anastahili posho yake. “Mji wo wote au kijiji cho chote mtakapoingia, tafuteni humo mtu anayestahili, nanyi kaeni kwake mpaka mtakapoondoka. Mkiingia kwenye nyumba, itakieni amani. Kama nyumba hiyo inastahili, amani yenu na iwe juu yake, la sivyo, amani yenu na iwarudie ninyi.

Kama mtu ye yote hatawakaribisha ninyi, wala kusikiliza maneno yenu, kung'uteni mavumbi kutoka kwenye miguu yenu mtakapokuwa mnatoka kwenye nyumba hiyo au mji huo. Amin, amin nawaambia, miji ya Sodoma na Gomora itastahimili zaidi katika hukumu kuliko mji huo.

“Tazama, ninawatuma kama kondoo katikati ya mbwa mwitu. Kwa hiyo mwe werevu kama nyoka na wapole kama hua. “Jihadharini na wanadamu, kwa maana watawapeleka katika mabaraza yao na kuwapiga kwenye masinagogi yao, nanyi mtaburutwa mbele ya watawala na wafalme kwa ajili yangu, ili kuwa ushuhuda kwao na mbele ya watu Mataifa.

Lakini watakapowapeleka humo, msisumbuke kufikirifikiri mtakalosema, kwa maana mtapewa la kusema wakati huo. Kwa sababu si ninyi mtakaokuwa mkinena, bali ni Roho wa Baba yenu atakayekuwa akinena kupitia kwenu.

“Ndugu atamsaliti ndugu yake ili auawe na baba atamsaliti mtoto wake, watoto wataasi dhidi ya wazazi wao na kuwafanya wauawe. Nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya Jina langu. Lakini yeye atakayevumilia hadi mwisho ataokoka. Wakiwatesa katika mji mmoja, kimbilieni mji mwingine. Amin, amin nawaambia, hamtamaliza miji yote ya Israeli kabla Mwana wa Adamu kuja.

“Kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, mimi nami nitamkiri yeye mbele za Baba yangu aliye mbinguni. Lakini ye yote atakayenikana mimi mbele ya watu, mimi nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni.”

“Msidhani kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani bali upanga. Kwa maana nimekuja kumfitini “ ‘mtu na babaye, binti na mamaye, mkwe na mama mkwe wake; nao adui za mtu watakuwa ni wale watu wa nyumbani kwake.’ “Ye yote ampendaye baba yake au mama yake kuliko anavyonipenda mimi, hastahili kuwa wangu. Ye yote ampendaye mwanawe au binti yake kuliko anavyonipenda Mimi, hastahili kuwa wangu. Tena ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kunifuata, hastahili kuwa wangu. Ayang'ang'aniaye maisha yake atayapoteza, lakini yeye atakayeyatoa maisha yake kwa ajili yangu atayapata. “Mtu ye yote atakayewapokea ninyi atakuwa amenipokea mimi na ye yote atakayenipokea mimi atakuwa amempokea yeye aliyenituma.

Baada ya Yesu kumaliza kutoa maagizo kwa wale wanafunzi wake kumi na wawili, aliondoka hapo akaenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao.

Vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa na maskini wanahubiriwa habari njema. Ana heri mtu yule asiyechukizwa na mimi.”

Tangu siku za Yohana Mbatizaji hadi sasa, Ufalme wa Mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.

Siku ya hukumu watu wa Ninawi watasimama pamoja na kizazi hiki na kukihukumu, kwa maana wao walitubu katika kuhubiri kwa Yona na tazama hapa yupo yeye aliye mkuu kuliko Yona.

Ndipo akawaambia mambo mengi kwa mifano, akisema: “Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake. Alipokuwa akipanda, baadhi zikaanguka kando ya njia, ndege wakaja na kuzila. Nyingine zikaanguka sehemu yenye mawe, ambapo hapana udongo mwingi. Zikaota haraka kwa sababu udongo ulikuwa hauna kina. Lakini jua lilipozidi, mimea hiyo ilinyauka na kukauka kwa sababu mizizi yake haikuwa na kina. Mbegu nyingine zilianguka katikati ya miiba, miiba hiyo ikakua ikazisonga. Mbegu nyingine zilianguka kwenye udongo mzuri ambapo zilitoa mazao, nyingine mara mia moja, nyingine mara sitini na nyingine mara thelathini.

“Sikilizeni basi maana ya ule mfano wa mpanzi: Mtu ye yote anaposikia neno la Ufalme, naye asilielewe, yule mwovu huja na kunyakua kile kilichopandwa moyoni mwake, hii ndiyo ile mbegu iliyopandwa kando ya njia. Ile mbegu iliyopandwa kwenye sehemu yenye mawe ni mtu yule ambaye hulisikia neno na mara hulipokea kwa furaha. Lakini kwa kuwa hana mizizi yenye kina ndani yake, lile neno hukaa kwa muda mfupi. Inapotokea dhiki au mateso kwa ajili ya hilo neno, yeye mara huchukizwa. Ile mbegu iliyopandwa katika miiba ni yule mtu alisikiaye neno, lakini masumbufu ya dunia na ushawishi wa mali hulisonga lile neno na kulifanya lisizae matunda. Lakini ile mbegu iliyopandwa kwenye udongo mzuri ni yule mtu ambaye hulisikia neno na kulielewa. Naye hakika hutoa matunda, akizaa mara mia, au mara sitini, au mara thelathini ya mbegu iliyopandwa.”

Akawaambia mfano mwingine, akasema, “Ufalme wa Mbinguni ni kama punje ya haradali, ambayo mtu aliichukua akaipanda shambani mwake. Ingawa mbegu hiyo ni ndogo kuliko mbegu zote, lakini inapokua ni mmea mkubwa kuliko yote ya bustanini, nao huwa mti mkubwa, hata ndege wa angani huja na kutengeneza viota katika matawi yake.”

Akawajibu, “Kila pando ambalo Baba yangu wa mbinguni hakulipanda, litang'olewa.

Ndipo Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Mtu ye yote akitaka kunifuata, ni lazima ajikane mwenyewe na auchukue msalaba wake, anifuate. Kwa maana ye yote anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini ye yote atakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu atayapata. Kwa maana itamfaidia nini mtu kuupata ulimwengu wote, lakini akayapoteza maisha yake? Au mtu atatoa nini badala ya maisha yake? Kwa maana Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake, naye ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.

Kila mmoja aliyeacha nyumba au ndugu zake wa kiume au wa kike au baba au mama au watoto au mashamba kwa ajili yangu, atapokea mara mia zaidi ya hayo na ataurithi uzima wa milele.

“Kwa maana Ufalme wa Mbinguni unafanana na mtu mwenye shamba aliyetoka alfajiri ili kwenda kuajiri vibarua kufanya kazi katika shamba lake la mizabibu. Baada ya kukubaliana na hao vibarua kuwalipa ujira wa dinari moja kwa siku, akawapeleka kwenye shamba lake la mizabibu. “Mnamo saa tatu akatoka tena, akawakuta wengine wamesimama sokoni bila kazi. Akawaambia, ‘Ninyi nanyi nendeni mkafanye kazi katika shamba langu la mizabibu, nami nitawalipa cho chote kilicho haki yenu.’ Kwa hiyo wakaenda. “Akatoka tena mnamo saa sita na pia saa tisa akafanya vivyo hivyo. Mnamo saa kumi na moja akatoka tena akawakuta wengine bado wamesimama bila kazi. Akawauliza, ‘Kwa nini mmesimama hapa kutwa nzima pasipo kufanya kazi?’ “Wakamjibu, ‘Ni kwa sababu hakuna ye yote aliyetuajiri.’ “Akawaambia, ‘Ninyi nanyi nendeni mkafanye kazi katika shamba langu la mizabibu.’ “Ilipofika jioni, yule mwenye shamba la mizabibu akamwambia msimamizi, ‘Waite hao vibarua na uwalipe ujira wao, ukianzia na wale walioajiriwa mwisho na kuishia na wale walioajiriwa kwanza.’ “Wale vibarua walioajiriwa mnamo saa kumi na moja, wakaja na kila mmoja wao akapokea dinari moja. Hivyo wale walioajiriwa kwanza walipofika, walidhani watalipwa zaidi. Lakini kila mmoja wao pia alipokea dinari moja. Walipoipokea, wakaanza kulalamika dhidi ya yule mwenye shamba, wakisema, ‘Hawa watu walioajiriwa mwisho wamefanya kazi kwa muda wa saa moja tu, nawe umewafanya sawa na sisi ambao tumestahimili taabu na joto lote la mchana kutwa?’ “Yule mwenye shamba akamjibu mmoja wao, ‘Rafiki, sijakudhulumu. Je, hukukubaliana nami kwa ujira wa kawaida wa dinari moja? Chukua ujira wako na uende. Mimi nimeamua kumlipa huyu mtu aliyeajiriwa mwisho kama nilivyokupa wewe. Je, sina haki yangu kufanya kile nitakacho na mali yangu mwenyewe? Au unaona wivu kwa kuwa nimekuwa mkarimu?’

“Ufalme wa Mbinguni unaweza kufananishwa na mfalme mmoja aliyemwandalia mwanawe karamu ya arusi. Akawatuma watumishi wake kuwaita wale waliokuwa wamealikwa karamuni, lakini wakakataa kuja. “Kisha akawatuma watumishi wengine akisema, ‘Waambieni wale walioalikwa kwamba karamu iko tayari kwa ajili yenu, nimekwisha kuchinja mafahali wangu na vinono. Karibuni.’ “Lakini hawakuzingatia, wakaenda zao, huyu shambani mwake na mwingine kwenye biashara zake. Wengine wao wakawakamata wale watumishi wake wakawatenda vibaya na kuwaua. Yule mfalme akakasirika sana, akapeleka jeshi lake likawaangamiza wale wauaji na kuuteketeza mji wao kwa moto.

“Kisha akawaambia watumishi wake, ‘Karamu ya arusi imeshakuwa tayari, lakini wale niliowaalika hawakustahili kuja. Kwa hiyo nendeni katika njia panda mkamwalike karamuni ye yote mtakayemwona’ Wale watumishi wakaenda barabarani wakawakusanya watu wote waliowaona, wema na wabaya. Ukumbi wa arusi ukajaa wageni.

“Ndipo mtasalitiwa, ili mteswe na kuuawa, nanyi mtachukiwa na mataifa yote kwa ajili yangu. Wakati huo, wengi wataacha imani yao, nao watasalitiana kila mmoja na mwenzake na kuchukiana. Watatokea manabii wengi wa uongo, nao watawadanganya watu wengi.

Injili ya Ufalme itahubiriwa ulimwenguni pote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote. Ndipo ule mwisho utakapokuja.

Yesu akawajia na kusema, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Kwa sababu hii, enendeni ulimwenguni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, nanyi wafundisheni kuyashika mambo yote niliyowaamuru ninyi. Hakika mimi niko pamoja nanyi siku zote, hadi mwisho wa nyakati.” Amen.

Yohana alikuja, akibatiza huko nyikani, akihubiri ubatizo wa toba kwa ajili ya ondoleo la dhambi.

Baada ya Yohana kukamatwa na kutiwa gerezani, Yesu aliingia Galilaya akaanza kuhubiri habari njema ya Mungu, akisema, “Wakati umewadia, Ufalme wa Mungu umekaribia. Tubuni na kuiamini Habari Njema.”

Yesu alipokuwa akitembea kandokando ya Bahari ya Galilaya alimwona Simoni na Andrea nduguye wakizitupa nyavu zao baharini, kwa kuwa hawa wawili walikuwa wavuvi. Yesu akawaambia, “Njoni nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu.” Mara wakaacha nyavu zao, wakamfuata Yesu.

Yesu akawajibu, “Twendeni mahali pengine kwenye vijiji vya jirani, ili niweze kuhubiri huko nako, kwa sababu hicho ndicho nilichokuja kukifanya.”

Alipokuwa akitembea, akamwona Lawi mwana wa Alfayo ameketi forodhani mahali pa kukusanya kodi, akamwambia, “Nifuate.” Lawi akaondoka, akamfuata Yesu.

Akawachagua kumi na wawili ambao pia aliwaita mitume, ili wapate kuwa pamoja naye na kuwatuma kwenda kuhubiri na kuwa na mamlaka ya kutoa pepo wachafu.

“Sikilizeni! Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake. Alipokuwa akipanda, mbegu nyingine zilianguka kando ya njia, ndege wakaja na wakazila. Nyingine zilianguka kwenye ardhi yenye mwamba isiyo na udongo wa kutosha. Zikaota haraka, kwa kuwa udongo ulikuwa haba, jua lilipozidi, mimea ikanyauka na kukauka kwa kuwa mizizi yake ilikuwa haina kina. Mbegu nyingine zilianguka kwenye miiba, miiba hiyo ikakua ikaisonga hiyo mimea hivyo haikutoa mazao. Mbegu nyingine zilianguka kwenye udongo mzuri, zikaota vizuri na kukua, zikatoa mazao, moja thelathini, nyingine sitini na nyingine mia moja.” Kisha Yesu akasema, “Mwenye masikio ya kusikia na asikie.” Alipokuwa peke yake, wale waliokuwepo pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili, wakamwuliza kuhusu mifano yake. Naye akawaambia, “Ninyi mmepewa kujua siri ya Ufalme wa Mungu, lakini kwa wale walioko nje, kila kitu husemwa kwao kwa mifano ili, “ ‘daima waone lakini wasitambue, daima wasikie lakini wasielewe; wasije wakageuka, wakatubu na kusamehewa!’ ”

Kisha Yesu akawauliza, “Hamwelewi maana ya mfano huu? Basi mtaelewaje mifano mingine? Yule mpanzi hupanda neno. Hawa ndio wale walio kando ya njia, ambako neno lilipandwa. Walisikiapo neno, Shetani huja mara na kulichukua lile neno lililopandwa ndani yao. Nazo hizi ni zile mbegu zilizoanguka kwenye udongo wenye miamba, wanapolisikia neno, mara hulipokea kwa furaha. Basi kwa kuwa hawana mizizi, hudumu kwa muda mfupi tu, kisha dhiki au mateso yanapoinuka kwa ajili ya lile neno, wao mara huiacha imani. Lakini wengine, kama mbegu iliyopandwa kwenye miiba, hulisikia lile neno, lakini masumbufu ya maisha haya, udanganyifu wa mali na tamaa ya mambo mengine huja na kulisonga lile neno na kulifanya lisizae. Wengine, kama mbegu iliyopandwa kwenye udongo mzuri, hulisikia lile neno, wakalipokea na kutoa mazao: Wengine thelathini, wengine sitini na wengine mara mia moja ya ile iliyopandwa.”

Pia akawaambia, “Ufalme wa Mungu unafanana na mtu apandaye mbegu shambani. Akiisha kuzipanda, usiku na mchana, akiwa amelala au ameamka, mbegu huota na kukua pasipo yeye kujua ikuavyo. Udongo huifanya iote kuwa mche, halafu suke, kisha nafaka kamili kwenye suke. Lakini nafaka inapokuwa imekomaa, mara mkulima huingia shambani na mundu wa kuvunia maana mavuno yamekuwa tayari.”

Akawaambia tena, “Tuufananishe Ufalme wa Mungu na nini? Au tutumie mfano gani ili kuueleza? Uko kama punje ya haradali, ambayo ni mbegu ndogo sana kuliko mbegu zote zinazopandwa ardhini. Lakini ikishaota, hukua ikawa mmea mkubwa kuliko yote katika bustani, ikawa na matawi makubwa hata ndege wa angani kujenga viota kwenye matawi yake.”

Yesu hakumruhusu, bali alimwambia, “Nenda nyumbani kwa jamaa yako ukawaeleze mambo makuu aliyokutendea Bwana na jinsi alivyokuhurumia.” Yule mtu akaenda zake akaanza kutangaza katika Dekapoli jinsi Yesu alivyomtendea, nao watu wote wakastaajabu.

Akawaita wale kumi na wawili, akawatuma wawili wawili na kuwapa mamlaka kutoa pepo wachafu. Akawaagiza akisema, “Msichukue cho chote kwa ajili ya safari isipokuwa fimbo tu. Msichukue mkate, wala mkoba, wala fedha kwenye mikanda yenu, bali mvae viatu, lakini msivae nguo ya ziada.” Akawaambia, “Mkiingia kwenye nyumba yo yote, kaeni humo hadi mtakapoondoka katika mji huo.

Kama mahali po pote hawatawakaribisha wala kuwasikiliza, mtakapoondoka huko, kung'uteni mavumbi yaliyoko miguuni mwenu, ili kuwa ushuhuda dhidi yao.” Kwa hiyo wakatoka na kuhubiri kwamba inawapasa watu kutubu na kuacha dhambi.

Naye akawaambia, “Ninyi mnayo njia nzuri ya kukataa amri za Mungu ili mpate kuzishika desturi zenu!

Walikuwa pia na visamaki vichache, Yesu akavibariki, akawaamuru wanafunzi wake wawagawie watu. Wale watu walikula na kutosheka, baadaye wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia wakajaza vikapu saba. Watu waliokula walikuwa wapata 4,000. Akiisha kuwaaga,

Ndipo akauita ule umati wa watu pamoja na wanafunzi wake, akasema, “Mtu ye yote akitaka kunifuata, ni lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake, anifuate. Kwa maana mtu ye yote anayetaka kuiokoa nafsi ataipoteza, lakini yeye ayapotezaye maisha yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili atayaokoa. Mtu atafaidiwa nini kama akiupata ulimwengu wote lakini akaipoteza nafsi yake? Au mtu atatoa nini apate tena maisha yake?

Mtu ye yote anayenionea aibu mimi na maneno yangu katika kizazi hiki cha uzinzi na cha dhambi, Mwana wa Adamu, atamwonea aibu wakati atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu.”

Yesu akasema, “Amin, nawaambia, hakuna mtu ye yote aliyeacha nyumba, ndugu wa kiume, au ndugu wa kike, mama, baba, watoto au mashamba kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, ambaye hatalipwa mara mia katika ulimwengu huu, nyumba, ndugu wa kiume, ndugu wa kike, mama, baba, watoto, mashamba pamoja na mateso, kisha uzima wa milele katika ulimwengu ujao.

“Lakini ninyi jihadharini. Kwa maana watawapeleka mahakamani na kuwapiga mijeledi katika masinagogi. Mtashtakiwa mbele ya watawala na wafalme kwa ajili yangu, ili kuwa ushuhuda kwao. Nayo habari njema lazima ihubiriwe kwanza kwa mataifa yote kabla ule mwisho haujawadia.

Mtakapokamatwa na kushtakiwa, msisumbuke kuhusu mtakalosema. Semeni tu lo lote mtakalopewa wakati huo, kwa kuwa si ninyi msemao bali ni Roho Mtakatifu.

“Ndugu atamsaliti ndugu yake ili auawe, baba atamsaliti mwanawe. Watoto watawaasi wazazi wao na kusababisha wauawe. Watu wote watawachukia kwa ajili ya Jina langu, lakini atakayevumilia hata mwisho ataokoka.

Akawaambia, “Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Ye yote aaminiye na kubatizwa ataokoka. Lakini ye yote asiyeamini atahukumiwa.

Kisha wanafunzi wake wakatoka, wakahubiri kila mahali, naye Bwana akatenda kazi pamoja nao na kulithibitisha neno lake kwa ishara zilizofuatana nalo.

kama vile yalivyokabidhiwa kwetu na wale ambao walikuwa mashahidi walioona na watumishi wa Bwana,

kuwajulisha watu wake juu ya wokovu utakaopatikana kwa kusamehewa dhambi zao,

Lakini malaika akawaambia: “Msiogope. Kwa maana tazama nawaletea habari njema za furaha itakayokuwa kwa watu wote.

Akaenda katika nchi yote kandokando ya Mto Yordani, akihubiri ubatizo wa toba kwa ajili ya msamaha wa dhambi. Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: “Sauti ya mtu aliaye nyikani, ‘Itengenezeni njia ya Bwana, yanyosheni mapito yake, kila bonde litajazwa, kila mlima na kilima kitasawazishwa. Njia zilizopinda zitanyooshwa, zilizoparuza zitasawazishwa. Nao watu wote watauona wokovu wa Mungu.’ ”

Basi, kwa maonyo mengine mengi Yohana aliwahubiri watu Habari Njema.

“Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa sababu amenitia mafuta kuwaletea maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao na vipofu kupata kuona tena, kuwaweka huru wanaoonewa

Lakini yeye akawaambia, “Imenipasa kuhubiri habari njema za Ufalme wa Mungu katika miji mingine pia, kwa maana kwa kusudi hili nilitumwa.”

Alipomaliza kunena, akamwambia Simoni, “Sasa peleka mashua hadi kilindini kisha mshushe nyavu zenu mkavue samaki.” Simoni akamjibu, “Bwana, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha na hatukuvua cho chote. Lakini, kwa neno lako nitazishusha nyavu.” Nao walipozishusha nyavu zao, wakavua samaki wengi sana, nyavu zao zikajaa zikaanza kukatika. Wakawaashiria wavuvi wenzao kwenye ile mashua nyingine ili waje kuwasaidia. Wakaja, wakajaza mashua zote mbili samaki hata zikaanza kuzama. Simoni Petro alipoona haya yaliyotukia alianguka miguuni mwa Yesu na kumwambia, “Bwana, ondoka kwangu, mimi ni mtu mwenye dhambi!” Kwa kuwa yeye na wavuvi wenzake walikuwa wameshangazwa sana na wingi wa samaki waliokuwa wamepata, vivyo hivyo wenzake Simoni, yaani, Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo walishangazwa pia. Ndipo Yesu akamwambia Simoni, “Usiogope, tangu sasa utakuwa mvuvi wa watu.” Hivyo wakasogeza mashua zao mpaka ufuoni mwa bahari, wakaacha kila kitu na kumfuata Yesu.

Baada ya haya Yesu alitoka na kumwona mtoza ushuru mmoja jina lake Lawi akiwa amekaa forodhani, mahali pake pa kukusanyia kodi, akamwambia, “Nifuate.” Naye Lawi akaacha kila kitu, akaondoka, akamfuata.

“Furahini na kurukaruka kwa shangwe kwa sababu thawabu yenu ni kubwa mbinguni, kwa kuwa hivyo ndivyo baba zao walivyowatenda manabii.

Hivyo akawajibu wale wajumbe, “Rudini mkamwambie Yohana yote mliyoyaona na kuyasikia. Vipofu wanaona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa na maskini wahubiriwa Habari Njema. Amebarikiwa mtu yule asiyechukizwa nami.”

Baada ya haya Yesu alikwenda akawa anazunguka katika miji na vijiji akihubiri habari njema za Ufalme wa Mungu. Wale wanafunzi wake kumi na wawili walikuwa pamoja naye,

“Mpanzi alitoka kwenda kusia mbegu zake. Alipokuwa akitawanya mbegu, nyingine zilianguka kando ya njia, zikakanyagwakanyagwa na ndege wa angani wakazila. Mbegu nyingine zilianguka penye miamba, nazo zilipoota, hiyo mimea ikakauka kwa kukosa unyevu. Nazo mbegu nyingine zilianguka kwenye miiba, ile miiba ikakua pamoja nazo na kusonga hiyo mimea ikafa. Mbegu nyingine zilianguka penye udongo mzuri. Zikaota na kuzaa mara mia zaidi ya mbegu alizopanda.” Baada ya kusema haya, Yesu akapaza sauti akasema, “Mwenye masikio ya kusikia na asikie.” Wanafunzi wake wakamwuliza maana ya mfano huu. Naye akasema, “Ninyi mmejaliwa kufahamu siri za Ufalme wa Mungu, lakini kwa wengine nazungumza kwa mifano, ili, “ ‘ingawa wanaona, wasione; ingawa wanasikia, wasielewe.’

“Maana ya mfano huu ni hii: Mbegu ni neno la Mungu. Zile zilizoanguka kando ya njia, ni wale ambao husikia neno na ibilisi huja na kuliondoa kutoka mioyoni mwao, ili wasije wakaamini na kuokoka. Zile za kwenye mwamba ni wale ambao hulipokea neno kwa furaha wanapolisikia, lakini hawana mizizi. Wanaamini kwa kitambo kidogo, lakini wakati wa kujaribiwa huiacha imani. Zile mbegu zilizoanguka kwenye miiba ni mfano wa wale wanaosikia, lakini wanapoendelea husongwa na masumbufu ya maisha haya, utajiri na anasa, nao hawakui. Lakini zile mbegu kwenye udongo mzuri ni mfano wa wale ambao hulisikia neno la Mungu na kulishika kwa moyo mnyofu na wa utii, nao kwa kuvumilia kwingi huzaa matunda.

“Rudi nyumbani ukawaeleze mambo makuu Mungu aliyokutendea.” Kwa hiyo yule mtu akaenda, akatangaza katika mji wote mambo makuu Yesu aliyomtendea.

Yesu akiisha kuwaita wale kumi na wawili pamoja, aliwapa mamlaka na uwezo wa kutoa pepo wachafu wote na kuponya magonjwa yote, kisha akawatuma waende wakahubiri Ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa. Akawaagiza akisema, “Msichukue cho chote safarini, wala fimbo, wala mkoba, wala chakula, wala fedha, wala msichukue kanzu ya ziada. Katika nyumba yo yote mwingiayo, kaeni humo hadi mtakapoondoka katika mji huo.

Kama watu wasipowakaribisha, mnapoondoka katika mji wao, kung'uteni mavumbi miguuni mwenu kuwa ushuhuda dhidi yao.” Hivyo wale wanafunzi wakaondoka wakaenda kutoka kijiji hadi kijiji, wakihubiri habari njema na kuponya wagonjwa kila mahali.

Kisha akawaambia wote, “Ye yote anayetaka kunifuata ni lazima ajikane mwenyewe, achukue msalaba wake kila siku na anifuate. Kwa maana ye yote atakayekuyaponya maisha yake atayapoteza, lakini ye yote atakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu atayaokoa. Je, itamfaidia nini mtu kuupata ulimwengu wote, lakini akayapoteza maisha yake?

Kama mtu ye yote akinionea aibu mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu atamwonea aibu mtu huyo atakapokuja katika utukufu wake na katika utukufu wa Baba na wa malaika watakatifu.

Yesu akamwambia mtu mwingine, “Nifuate.” Mtu huyo akamjibu, “Bwana, niache kwanza nikamzike baba yangu.” Yesu akamwambia, “Waache wafu wawazike wafu wao, bali wewe nenda ukautangaze Ufalme wa Mungu.”

Mtu mwingine akamwambia, “Bwana, nitakufuata lakini naomba kwanza nikaage jamaa yangu.” Yesu akamwambia, “Mtu ye yote atiaye mkono wake kulima, kisha akatazama nyuma, hafai kwa Ufalme wa Mungu.”

Baada ya hayo, Yesu akawachagua wengine sabini na wawili, akawatuma wawili wawili katika kila mji na kila sehemu aliyokusudia kwenda yeye mwenyewe.

Akawaambia, “Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache. Kwa hiyo mwombeni Bwana wa mavuno, awapeleke watenda kazi katika shamba lake.

Haya! nendeni. Ninawatuma kama kondoo katikati ya mbwa mwitu. Msichukue mkoba wala mfuko, wala viatu na msimsalimu mtu ye yote njiani.

Lakini mkiingia katika mji, nao hawakuwakaribisha, tokeni mwende katika barabara zake mkaseme: ‘Hata mavumbi ya mji wenu yaliyoshikamana na miguu yetu, tunayakung'uta dhidi yenu. Lakini mjue kwamba Ufalme wa Mungu umekaribia.’ Ninawaambia, hukumu ya Mungu katika Sodoma itavumilika zaidi kuliko ya mji ule.

“Yeye awasikilizaye ninyi, anisikiliza mimi, naye awakataaye ninyi, amenikataa mimi. Lakini yeye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma.”

Siku ile ya hukumu, watu wa Ninawi watasimama pamoja na kizazi hiki na kukihukumu kwa sababu wao walitubu walipomsikia Yona akihubiri. Lakini sasa, yeye aliye mkuu kuliko Yona yuko hapa.

“Ninawaambia kwamba, ye yote atakayenikiri mbele ya watu, Mwana wa Adamu naye atamkiri mbele za malaika wa Mungu. Lakini yeye atakayenikana mbele ya watu, Mwana wa Adamu naye atamkana mbele ya malaika wa Mungu.

“Watakapowapeleka katika masinagogi mbele ya watawala na wenye mamlaka, msiwe na wasiwasi kuhusu namna mtakavyojitetea au mtakavyosema: Kwa maana Roho Mtakatifu atawafundisha wakati huo huo mnachopaswa kusema.”

Uzeni mali zenu mkawape maskini. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, mkajiwekee hazina mbinguni isiyokwisha, mahali ambapo mwivi hakaribii wala nondo haharibu. Kwa maana hazina yako ilipo, ndipo na moyo wako utakapokuwa pia.

Mnadhani nimekuja kuleta amani duniani? La, nawaambia sivyo, nimekuja kuleta mafarakano. Kuanzia sasa, kutakuwa na watu watano katika nyumba moja, watatu dhidi ya wawili na wawili dhidi ya watatu. Watafarakana baba dhidi ya mwanawe na mwana dhidi ya babaye, mama dhidi ya bintiye na binti dhidi ya mamaye, mama mkwe dhidi ya mkwewe. Naye mkwe dhidi ya mama mkwe wake.”

Nawaambia, la hasha! Ninyi nanyi msipotubu, wote mtaangamia vivyo hivyo.”

Yesu akamjibu, “Mtu mmoja alikuwa anaandaa karamu kubwa, akaalika watu wengi. Wakati wa karamu ulipofika akamtuma mtumishi wake akawaambie wale walioalikwa, ‘Karibuni, kila kitu ni tayari sasa.’ “Lakini wote, kila mmoja, wakaanza kutoa udhuru: Wa kwanza akasema, ‘Nimenunua shamba, lazima niende kuliona. Tafadhali niwie radhi.’ “Mwingine akasema, ‘Ndipo tu nimenunua jozi tano za ng'ombe wa kulimia, nami ninakwenda kuwajaribu, tafadhali niwie radhi.’ Naye mwingine akasema, ‘Nimeoa mke, kwa hiyo siwezi kuja.’ “Yule mtumishi akarudi, akampa bwana wake taarifa. Ndipo yule mwenye nyumba akakasirika, akamwagiza yule mtumishi wake akisema, ‘Nenda upesi kwenye mitaa na vichochoro vya mjini uwalete maskini, vilema, vipofu na viwete.’ “Yule mtumishi akamwambia, ‘Bwana, yale uliyoniagiza nimefanya, lakini bado ipo nafasi.’ “Ndipo yule bwana akamwambia mtumishi wake, ‘Nenda kwenye barabara na vijia vilivyoko nje ya mji na uwalazimishe watu waingie ili nyumba yangu ipate kujaa. Kwa maana nawaambia, hakuna hata mmoja wa wale walioalikwa atakayeionja karamu yangu.’ ”

“Mtu ye yote anayekuja kwangu hawezi kuwa mwanafunzi wangu kama hatanipenda mimi zaidi ya baba yake na mama yake, mke wake na watoto, ndugu zake na dada zake, naam, hata maisha yake mwenyewe. Ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kunifuata hawezi kuwa mwanafunzi wangu.

Vivyo hivyo, ye yote miongoni mwenu ambaye hawezi kuacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. “Chumvi ni kitu kizuri, lakini chumvi ikiwa imepoteza ladha yake, inawezaje kurudishiwa tena ladha yake?

Nawaambieni, vivyo hivyo kutakuwa na furaha zaidi mbinguni kwa sababu ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa wenye haki tisini na tisa ambao hawana haja ya kutubu.”

Vivyo hivyo, nawaambia, kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu juu ya mwenye dhambi mmoja atubuye.”

Kwa maana Mwana wa Adamu amekuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.”

Siku moja, Yesu alipokuwa akifundisha watu Hekaluni na kuhubiri habari njema, viongozi wa makuhani, walimu wa sheria, pamoja na wazee wakamjia.

“Lakini kabla yote hayajatokea, watawakamata ninyi na kuwatesa. Watawatia mikononi mwa wakuu wa masinagogi na kufungwa magerezani, nanyi mtapelekwa mbele ya wafalme na watawala kwa ajili ya Jina langu. Hii itawapa nafasi ya kushuhudia.

Lakini msiwe na wasiwasi kwamba mtasema nini kabla ya mashtaka. Kwa maana nitawapa maneno na hekima ambayo hakuna hata adui yenu mmoja atakayeweza kushindana nayo wala kuipinga.

Mtasalitiwa hata na wazazi, ndugu, jamaa na marafiki na baadhi yenu watawaua. Mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya Jina langu.

Kisha Yesu akawauliza, “Nilipowatuma bila mfuko, wala mkoba, wala viatu, mlipungukiwa na kitu cho chote?” Wakajibu, “La, hatukupungukiwa na kitu cho chote.” Akawaambia, “Lakini sasa, aliye na mfuko na auchukue na aliye na mkoba vivyo hivyo. Naye asiye na upanga, auze joho lake anunue mmoja.

Toba na msamaha wa dhambi utatangazwa kupitia jina lake, kuanzia Yerusalemu. Ninyi ni mashahidi wa mambo haya.

Bali wote waliompokea, aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake. Hawa ndio waliozaliwa si kwa damu wala kwa mapenzi ya mwili au kwa mapenzi ya mtu, bali kwa mapenzi ya Mungu.

Siku iliyofuata Yesu aliamua kwenda Galilaya. Akamkuta Filipo, akamwambia, “Nifuate.”

Yesu akamjibu, “Amin, amin nakuambia, mtu hawezi kuuona Ufalme wa Mungu asipozaliwa mara ya pili.” Nikodemo akauliza, “Awezaje mtu kuzaliwa wakati akiwa mzee? Hakika hawezi kuingia mara ya pili kwenye tumbo la mama yake ili azaliwe!” Yesu akamwambia, “Amin, amin nakuambia, hakuna mtu ye yote anayeweza kuingia katika Ufalme wa Mungu isipokuwa amezaliwa kwa maji na kwa Roho. Mwili huzaa mwili, lakini Roho huzaa roho. Kwa hiyo usishangae ninapokuambia huna budi ‘kuzaliwa mara ya pili.’ Upepo huvuma po pote upendapo. Mvumo wake unausikia lakini huwezi ukafahamu utokako wala uendako. Ndivyo ilivyo kwa kila mtu aliyezaliwa na Roho.”

Amin, amin ninakuambia, sisi tunazungumza lile tunalolijua na tunashuhudia lile tuliloliona. Lakini ninyi watu hamkubali ushuhuda wetu. Nimewaambia mambo ya duniani, nanyi hamkuniamini, mtaniaminije basi nitakapowaambia mambo ya mbinguni?

“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Kwa maana Mungu hakumtuma Mwanawe kuuhukumu ulimwengu, bali kwa yeye ulimwengu upate kuokolewa. Ye yote amwaminiye hahukumiwi, lakini asiyeamini amekwisha kuhukumiwa, kwa sababu hakumwamini Mwana pekee wa Mungu. Hii ndiyo hukumu kwamba: Nuru imekuja ulimwenguni, nao watu wakapenda giza kuliko nuru kwa sababu matendo yao ni maovu. Kwa kuwa kila atendaye maovu huchukia nuru, wala haji kwenye nuru ili matendo yake maovu yasifichuliwe. Lakini wale watendao yaliyo mema huja kwenye nuru, kusudi ionekane wazi kwamba matendo yao yametendeka katika Mungu.”

Ye yote anayemwamini Mwana ana uzima wa milele, lakini yeye asiyemwamini Mwana hatauona uzima, bali ghadhabu ya Mungu itakuwa juu yake.”

Je, ninyi hamsemi, ‘Bado miezi minne tuvune?’ Inueni macho yenu myaangalie mashamba jinsi mazao yalivyo tayari kuvunwa! Mvunaji tayari anapokea mshahara wake, naye anakusanya mazao kwa ajili ya uzima wa milele. Ili yeye apandaye na yeye avunae wafurahi pamoja. Hivyo kule kusema, ‘Mmoja hupanda na mwingine huvuna,’ ni kweli kabisa. Niliwatuma mkavune mazao ambayo hamkupanda, wengine walifanya kazi ngumu, nanyi mmevuna faida ya taabu yao.”

“Amin, amin ninawaambia, ye yote anayesikia maneno yangu na kumwamini yeye aliyenituma, anao uzima wa milele, naye hatahukumiwa, bali amepita kutoka mautini, na kuingia uzimani.

Niliwaambia kuwa mtakufa katika dhambi zenu, kwa maana msipoamini ya kwamba ‘Mimi Ndiye,’ mtakufa katika dhambi zenu.”

Kisha Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, “Kama mkidumu katika maneno yangu, mtakuwa wanafunzi wangu kweli kweli. Ndipo mtaijua kweli nayo kweli itawaweka huru.”

Yanipasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenituma wakati bado ni mchana, kwa kuwa usiku waja ambapo hakuna mtu awezaye kufanya kazi.

“Amin, amin nawaambia, yeye asiyeingia katika zizi la kondoo kwa kupitia kwenye lango, lakini akwea kuingia ndani kwa njia nyingine, ni mwivi na mnyang'anyi.

Yuko amhukumuye yeye anikataaye mimi na kutokuyapokea maneno yangu, yaani, yale maneno niliyosema yenyewe yatamhukumu siku ya mwisho. Kwa maana sisemi kwa ajili yangu mwenyewe, bali Baba aliyenituma aliniamuru ni nini cha kusema na jinsi ya kukisema.

Yesu akawaambia, “Mimi ndimi njia na kweli na uzima. Mtu hawezi kuja kwa Baba isipokuwa kwa kupitia kwangu.

Lakini haya yameandikwa ili mweze kuamini ya kuwa Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu na kwa kumwamini mpate uzima katika jina lake.

Akawaambia, “Shusheni nyavu upande wa kuume wa mashua yenu nanyi mtapata samaki.” Wakashusha nyavu na tazama wakapata samaki wengi mno hata wakashindwa kuvutia zile nyavu zilizojaa samaki ndani ya mashua. Yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu akamwambia Petro, “Huyu ni Bwana!” Simoni Petro aliposikia haya, akajifunga nguo yake kwa kuwa alikuwa uchi, naye akajitosa baharini. Wale wanafunzi wengine wakaja kwa ile mashua huku wakikokota ule wavu uliyojaa samaki, maana hawakuwa mbali na nchi kavu, ilikuwa yapata dhiraa 200. Walipofika pwani, wakaona moto wa makaa na samaki wakiokwa juu yake na mikate. Yesu akawaambia, “Leteni baadhi ya hao samaki mliovua sasa hivi.” Simoni Petro akapanda kwenye mashua na kuukokota ule wavu pwani. Ulikuwa umejaa samaki wakubwa 153. Ingawa samaki walikuwa wengi kiasi hicho, ule wavu haukuchanika.

Lakini mtapokea nguvu akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, Uyahudi kote na Samaria, hadi miisho ya dunia.”

Lakini ye yote atakayeliita jina la Bwana, ataokolewa.’

Petro akawajibu, “Tubuni, mkabatizwe kila mmoja wenu kwa jina la Yesu Kristo, ili mpate kusamehewa dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu na watoto wenu na kwa wale wote walio mbali na kila mtu ambaye Bwana Mungu wetu atamwita amjie.” Petro akawaonya kwa maneno mengine mengi na kuwasihi akisema, “Jiepusheni na kizazi hiki kilichopotoka.”

Wale wote waliopokea ujumbe wa Petro kwa furaha wakabatizwa na siku ile waliongezeka watu wapatao 3,000.

wakimsifu Mungu na kuwapendeza watu wote. Kila siku Bwana akaliongeza kanisa kwa wale watu waliokuwa wakiokolewa.

Tubuni basi mkamgeukie Mungu, ili dhambi zenu zifutwe, ili zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwepo kwake Bwana. Kwamba apate kumtuma Kristo, ambaye amewekwa kwa ajili yenu, yaani Yesu, ambaye ilimpasa mbingu zimpokee mpaka wakati wa kufanywa upya kila kitu, kama Mungu alivyosema kwa vinywa vya manabii wake wote watakatifu kabla ya mwanzo wa ulimwengu.

Lakini wengi wale waliosikia lile neno waliamini, idadi yao ilikuwa yapata wanaume 5,000.

Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hakuna Jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.”

Wale viongozi na wazee walipoona ujasiri wa Petro na Yohana na kujua ya kuwa walikuwa watu wa kawaida, wasio na elimu, walishangaa sana, wakatambua kwamba hawa watu walikuwa na Yesu.

Kisha wakawaita tena ndani na kuwaamuru wasiseme wala kufundisha kamwe kwa hili jina la Yesu. Lakini Petro na Yohana wakajibu, “Amueni ninyi wenyewe iwapo ni haki mbele za Mungu kuwatii ninyi kuliko Mungu. Lakini sisi hatuwezi kuacha kusema yale tuliyoyaona na kuyasikia.”

Sasa, Bwana angalia vitisho vyao na utuwezeshe sisi watumishi wako kulinena neno lako kwa ujasiri mkuu. Nyosha mkono wako ili kuponya wagonjwa na kutenda ishara na miujiza kwa jina la Mwanao mtakatifu Yesu.” Walipokwisha kuomba, mahali pale walipokuwa wamekutanika pakatikiswa, nao wote wakajazwa na Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri.

Mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwa Bwana Yesu kwa nguvu nyingi na neema ya Mungu ilikuwa juu yao wote.

Wakiisha kuwaleta hao mitume wakawaamuru kusimama mbele ya baraza. Kuhani Mkuu akawahoji. “Tuliwaonya kwa nguvu msifundishe kwa jina hili, lakini ninyi mmeijaza Yerusalemu yote mafundisho yenu na tena mmekusudia kuleta damu ya mtu huyu juu yetu.” Petro na wale mitume wengine wakajibu, “Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu.

Wakapokea ushauri wa Gamalieli. Wakawaita mitume ndani, wakaamuru wachapwe mijeledi, kisha wakawaagiza wasinene tena kwa jina la Yesu, nao wakawaachia waende zao. Wale mitume walitoka nje ya baraza, wakiwa wamejaa furaha kwa sababu wamehesabiwa kustahili kupata aibu kwa ajili ya jina la Yesu. Kila siku, Hekaluni na nyumba kwa nyumba, hawakuacha kufundisha na kuhubiri habari njema kwamba Yesu ndiye Kristo.

Kwa hiyo wale waliotawanyika wakalihubiri neno la Mungu kila mahali walipokwenda. Filipo akatelemkia mji mmoja wa Samaria akawahubiria habari za Kristo.

Lakini watu walipomwamini Filipo akihubiri habari njema za Ufalme wa Mungu na jina la Yesu Kristo, wakabatizwa wanaume na wanawake.

Nao walipokwisha kutoa ushuhuda na kuhubiri neno la Bwana, wakarudi Yerusalemu wakihubiri injili katika vijiji vingi vya Samaria.

Ndipo Filipo akaanza kutumia fungu lile la maandiko akamweleza habari njema za Yesu. Walipokuwa wakiendelea na safari wakafika mahali palipokuwa na maji, yule towashi akamwambia Filipo, “Tazama, hapa kuna maji. Kitu gani kitanizuia nisibatizwe?” ( Filipo akamwambia, “Kama ukiamini kwa moyo wako wote unaweza kubatizwa.” Akajibu, “Naamini kuwa Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu).” Naye akaamuru lile gari lisimamishwe. Wakatelemka kwenye maji wote wawili, yule towashi na Filipo, naye Filipo akambatiza.

Filipo akajikuta yuko Azoto, akasafiri akihubiri injili katika miji yote mpaka alipofika Kaisaria.

Lakini Barnaba akamchukua, akampeleka kwa wale mitume. Akawaeleza jinsi Sauli akiwa njiani alivyomwona Bwana, jinsi Bwana alivyosema naye na jinsi alivyohubiri kwa ujasiri kwa jina la Yesu huko Dameski. Kwa hiyo Sauli akakaa nao akishirikiana nao na akihubiri waziwazi kwa jina la Yesu kila mahali huko Yerusalemu. Alinena na kuhojiana na Wayahudi wenye asili ya Kiyunani lakini wao walijaribu kumwua.

Ninyi mnajua ule ujumbe uliotumwa kwa Israeli, ukitangaza habari njema za amani kwa Yesu Kristo. Yeye ni Bwana wa wote. Mnajua yale yaliyotukia katika Uyahudi wote kuanzia Galilaya baada ya mahubiri ya Yohana Mbatizaji:

Naye alituamuru kuhubiri kwa watu wote na kushuhudia kwamba yeye ndiye aliyetiwa mafuta na Mungu kuwa hakimu wa walio hai na wafu. Manabii wote walishuhudia juu yake kwamba kila mtu amwaminiye hupokea msamaha wa dhambi katika Jina lake.” Wakati Petro akiwa anasema maneno hayo, Roho Mtakatifu aliwashukia wote waliokuwa wakisikiliza ule ujumbe.

Mitume na ndugu walioamini waliokuwa huko Uyahudi wakasikia kuwa watu Mataifa nao wamepokea neno la Mungu.

Akatuambia jinsi alivyoona malaika aliyekuwa amesimama katika nyumba yake na kusema, ‘Tuma watu waende Yafa wakamlete Simoni aitwaye Petro. Yeye atakupa ujumbe ambao kwa huo wewe na wa nyumbani mwako wote mtaokoka.’

Waliposikia haya hawakuwa na la kupinga zaidi. Nao wakamwadhimisha Mungu wakisema, “Basi, Mungu amewapa hata watu Mataifa toba iletayo uzima wa milele.”

Lakini baadhi yao walikuwapo watu wa Kipro na Kirene, ambao walipokuja Antiokia walinena na Wayunani pia wakimhubiri Bwana Yesu. Mkono wa Bwana ulikuwa pamoja nao, nayo idadi kubwa ya watu wakaamini na kumgeukia Bwana.

Kabla ya kuja kwa Yesu, Yohana alihubiri toba na ubatizo kwa watu wote wa Israeli.

“Nasi tunawaletea habari njema kwamba yale Mungu aliyowaahidi baba zetu

Sabato iliyofuata karibu watu wote wa mji ule walikuja kusikiliza neno la Mungu.

Ndipo Paulo na Barnaba wakawajibu kwa ujasiri, wakisema, “Ilitupasa kunena nanyi neno la Mungu kwanza. Lakini kwa kuwa mmelikataa, mkajihukumu wenyewe kuwa hamstahili uzima wa milele, sasa tunawageukia watu Mataifa. Kwa maana hili ndilo Bwana alilotuamuru: “ ‘Nimewafanya ninyi kuwa nuru kwa watu Mataifa, ili mpate kuuleta wokovu hadi miisho ya dunia.’ ”

Watu Mataifa waliposikia haya wakafurahi na kulitukuza neno la Bwana; nao wote waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini. Neno la Bwana likaenea katika eneo lile lote.

Lakini Wayahudi wakawachochea wanawake wenye kumcha Mungu, wenye vyeo pamoja na watu maarufu katika mji, wakachochea mateso dhidi ya Paulo na Barnaba na kuwafukuza kutoka kwenye eneo lao. Hivyo Paulo na Barnaba wakakung'uta mavumbi kutoka kwenye miguu yao ili kuwapinga, nao wakaenda Ikonio.

Huko Ikonio Paulo na Barnaba waliingia pamoja katika sinagogi la Wayahudi kama kawaida yao. Huko wakahubiri kwa uwezo mkubwa kiasi kwamba Wayahudi pamoja na watu Mataifa wakaamini. Lakini wale Wayahudi waliokataa kuamini, wakawachochea watu Mataifa, wakatia chuki ndani ya mioyo yao dhidi ya wale walioamini.

Hivyo Paulo na Barnaba wakakaa huko kwa muda wa kutosha wakihubiri kwa ujasiri juu ya Bwana, ambaye alithibitisha ujumbe wa neema yake kwa kuwawezesha kufanya ishara na miujiza.

“Enyi watu, kwa nini mnafanya mambo haya? Sisi ni wanadamu tu kama ninyi! Tunawaletea habari njema, tukiwaambia kwamba mgeuke mtoke katika mambo haya yasiyofaa mmwelekee Mungu aliye hai, aliyeziumba mbingu na nchi na bahari na kila kitu kilicho ndani yake.

Baada ya kuhubiri habari njema katika mji huo wa Derbe na kupata wanafunzi wengi, walirudi Listra, kisha wakaenda Ikonio na Antiokia, wakiwaimarisha wanafunzi na kuwatia moyo waendelee kudumu katika imani. Wakawaonya wakisema, “Imetupasa kuingia katika Ufalme wa Mungu kwa kupitia katika taabu nyingi.”

Baada ya majadiliano mengi, Petro akasimama na kusema, “Ndugu zangu, mnajua kwamba siku za kwanza Mungu alinichagua ili kwa midomo yangu watu Mataifa wapate kusikia ujumbe wa injili na kuamini.

Paulo pamoja na wenzake wakasafiri sehemu za Frigia na Galatia, wakiwa wamekatazwa na Roho Mtakatifu wasihubiri neno huko Asia. Walipofika kwenye mpaka wa Misia, wakajaribu kuingia Bithinia lakini Roho wa Yesu hakuwaruhusu. Kwa hiyo wakapita Misia, wakafika Troa. Wakati wa usiku Paulo akaona maono, mtu wa Makedonia amesimama akimsihi, “Vuka uje huku Makedonia ukatusaidie.” Baada ya Paulo kuona maono haya, mara tulijiandaa kuondoka kwenda Makedonia tukiwa tumesadiki kwa hakika kwamba Mungu ametuita kuhubiri habari njema huko.

Yule askari wa gereza akaagiza taa ziletwe, akaingia ndani ya kile chumba cha gereza, akapiga magoti akitetemeka mbele ya Paulo na Sila. Kisha akawaleta nje akisema, “Bwana zangu, nifanye nini ili nipate kuokoka?” Wakamjibu, “Mwamini Bwana Yesu Kristo, nawe utaokoka, pamoja na wa nyumbani mwako.”

Kama desturi yake Paulo aliingia ndani ya sinagogi na kwa muda wa majuma matatu akawa anahojiana nao kutoka kwenye Maandiko akidhihirisha wazi na kuthibitisha kwamba ilikuwa lazima Kristo ateswe na afufuke kutoka kwa wafu, akasema, “Huyu Yesu ninayewaambia habari zake, ndiye Kristo.” Baadhi ya Wayahudi wakasadiki, wakaungana na Paulo na Sila, wakiwepo idadi kubwa ya Wayunani waliomcha Mungu na wengi wa wanawake mashuhuri.

Hawa Wayahudi wa Beroya walikuwa waungwana zaidi kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa waliupokea ule ujumbe kwa shauku kubwa na kuyachunguza Maandiko kila siku ili kuona kama yale Paulo aliyosema yalikuwa kweli.

Ndipo Paulo akasimama katikati ya Areopago akasema, “Enyi watu wa Athene! Ninaona kwamba katika kila jambo ninyi ni watu wa dini sana. Kwa kuwa nilipokuwa nikitembea mjini na kuangalia kwa bidii vitu vyenu vya kuabudiwa, niliona huko madhabahu moja iliyoandikwa: KWA MUNGU ASIYEJULIKANA. Basi sasa kile ambacho mmekuwa mkikiabudu kama kisichojulikana, ndicho ninachowahubiria. “Mungu aliyeumba dunia na vyote vilivyomo ndani yake, yeye ndiye Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika mahekalu yaliyojengwa kwa mikono ya wanadamu. Wala hatumikiwi na mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji cho chote, kwa sababu yeye mwenyewe ndiye awapaye watu wote uhai na pumzi na vitu vyote. Kutoka kwa mtu mmoja, yeye aliumba mataifa yote ya wanadamu ili waikalie dunia yote, naye akaweka nyakati za kuishi. Mungu alifanya hivyo ili wanadamu wamtafute na huenda wakamfikia ingawa kwa kupapasapapasa ijapokuwa kwa kweli hakai mbali na kila mmoja wetu. ‘Kwa kuwa katika yeye tunaishi, tunatembea na kuwa na uzima wetu.’ Kama baadhi ya watunga mashairi wenu walivyosema, ‘Sisi ni watoto wake.’ “Kwa kuwa sisi ni watoto wa Mungu, haitupasi kudhani kuwa Uungu ni kama sanamu ya dhahabu au ya fedha au ya jiwe iliyotengenezwa kwa ubunifu na ustadi wa mwanadamu. Zamani wakati wa ujinga, Mungu alijifanya kama haoni, lakini sasa anawaamuru watu wote kila mahali watubu. Kwa kuwa ameweka siku ambayo atauhukumu ulimwengu kwa haki akimtumia mtu aliyemchagua, kwake huyo amewahakikishia watu wote kwa kumfufua Kristo kutoka kwa wafu.”

Basi akaja Efeso Myahudi mmoja, jina lake Apolo, mwenyeji wa Aleksandria. Yeye alikuwa mtu mwenye uwezo mkubwa wa kunena, pia alikuwa hodari katika maandiko. Alikuwa amefundishwa katika njia ya Bwana, naye alikuwa na bidii katika roho, akafundisha kwa usahihi juu ya Yesu, ingawa alijua tu ubatizo wa Yohana. Apolo alianza kunena kwa ujasiri mkubwa katika sinagogi, Lakini Prisila na Akila walipomsikia walimchukua kando na kumweleza njia ya Mungu kwa ufasaha zaidi.

Paulo akaingia katika sinagogi na kunena humo kwa ujasiri kwa muda wa miezi mitatu, akawa na majadiliano ya kuwafanya watu waamini mambo yanayohusu Ufalme wa Mungu. Lakini baadhi yao kwa ukaidi walipokataa kuamini na kukashifu ujumbe wake mbele ya umati wa watu, Paulo aliachana nao, akawachukua wanafunzi na kuhojiana nao kila siku katika darasa la mtu mmoja aitwaye Tirano. Jambo hili likaendelea kwa muda wa miaka miwili, kiasi kwamba Wayahudi na Wayunani wote walioishi huko Asia wakawa wamesikia neno la Bwana.

Mnajua kwamba sikusita kuhubiri jambo lo lote ambalo lingekuwa la kuwafaa ninyi, lakini nilifundisha hadharani na nyumba kwa nyumba. Nimewashuhudia Wayahudi na Wayunani kwamba inawapasa kumgeukia Mungu kwa kutubu dhambi na kumwamini Bwana wetu Yesu Kristo. “Nami sasa nimesukumwa na Roho, ninakwenda Yerusalemu wala sijui ni nini kitakachonipata huko. Ila ninachojua tu ni kwamba Roho Mtakatifu amenionya kuwa vifungo na mateso vinaningoja. Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa ya thamani kwangu, kama kuyamaliza mashindano na kukamilisha ile kazi Bwana Yesu aliyonipa, yaani, kazi ya kuishuhudia injili ya neema ya Mungu.

Kwa kuwa utakuwa shahidi wake kwa watu kuhusu kile ulichokiona na kukisikia.

Usiku uliofuata, Bwana akasimama karibu naye akamwambia, “Jipe moyo! Kama vile ulivyonishuhudia hapa Yerusalemu, hivyo imekupasa kunishuhudia huko Rumi pia.”

Lakini sasa inuka usimame kwa miguu yako, kwa sababu nimekutokea kwa kusudi hili, ili kukuweka utumike na kushuhudia juu ya mambo ambayo umeyaona na yale nitakayokutokea kwayo.

uyafumbue macho yao ili wageuke kutoka gizani waingie nuruni na kutoka kwenye nguvu za Shetani, wamgeukie Mungu ili wapate msamaha wa dhambi na sehemu miongoni mwa wale waliotakaswa kwa kuniamini mimi.’

Hadi leo nimepata msaada kutoka kwa Mungu na hivyo nasimama hapa nikishuhudia wakubwa na wadogo, bila kusema cho chote zaidi ya yale ambayo manabii na Mose walisema yatatukia: kwamba Kristo atateswa na kwamba yeye atakuwa wa kwanza kufufuka kutoka kwa wafu, atatangaza nuru kwa watu wake na kwa watu Mataifa.”

Kwa miaka miwili mizima Paulo alikaa huko kwenye nyumba yake mwenyewe aliyokuwa amepanga. Akawakaribisha wote waliokwenda kumwona. Akahubiri Ufalme wa Mungu na kufundisha mambo yale yaliyomhusu Bwana Yesu Kristo, kwa ujasiri wote na bila kizuizi cho chote.

Kwanza kabisa, namshukuru Mungu wangu kwa njia ya Yesu Kristo kwa ajili yenu nyote, kwa sababu imani yenu inatangazwa duniani kote.

Mimi ni mdeni kwa Wayunani na kwa wasio Wayunani, kwa wenye hekima na kwa wasio na hekima. Ndiyo sababu ninatamani sana kuihubiri Injili kwenu pia ninyi mlioko Rumi. Mimi siionei haya Injili ya Kristo kwa maana ni uweza wa Mungu uletao wokovu kwa kila aaminiye, kwanza kwa Myahudi na kwa Myunani pia.

Lakini Mungu anaudhihirisha upendo wake kwetu kwamba: Tulipokuwa tungali wenye dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yetu.

Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Kwa sababu kama ukikiri kwa kinywa chako kwamba “Yesu ni Bwana,” na kuamini moyoni mwako kwamba Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini na hivyo kuhesabiwa haki, tena kwa kinywa mtu hukiri na hivyo kupata wokovu. Kama yasemavyo Maandiko, “Ye yote amwaminiye hatatahayarika.” Kwa maana hakuna tofauti kati ya Myahudi na Myunani, yeye ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao. Kwa maana, “Kila mtu atakayeliitia Jina la Bwana, ataokoka.”

Lakini watamwitaje yeye ambaye hawajamwamini? Nao watawezaje kumwamini yeye ambaye hawajamsikia? Tena watamsikiaje bila mtu kuwahubiria? Nao watahubirije wasipopelekwa? Kama ilivyaoandikwa, “Ni mizuri mno miguu ya hao wanaohubiri Injili ya amani na kuleta habari ya mema!”

Lakini si wote waliotii Habari Njema. Kwa maana Isaya asema, “Bwana, ni nani aliyeamini ujumbe wetu?”

Basi, imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la Kristo. Lakini nauliza, Je, wao hawakusikia? Naam, wamesikia, kwa maana: “Sauti yao imeenea duniani kote, nayo maneno yao yamefika hadi miisho ya ulimwengu.”

kwa nguvu za ishara na miujiza, kwa uweza wa Roho wa Mungu, hivyo kuanzia Yerusalemu hadi maeneo yote ya kandokando yake mpaka Iliriko, nimekwisha kuihubiri Injili ya Kristo kwa ukamilifu.

Sasa atukuzwe yeye awezaye kuwafanya ninyi imara kwa Injili yangu na kuhubiriwa kwa Yesu Kristo, kutokana na kufunuliwa siri zilizofichika tangu zamani za kale. Lakini sasa siri hiyo imefunuliwa na kujulikana kupitia maandiko ya kinabii kutokana na amri ya Mungu wa milele, ili mataifa yote yaweze kumwamini na kumtii

Kwa maana Kristo hakunituma ili kubatiza bali kuhubiri Injili na nifanye hivyo si kwa kutumia maneno ya hekima ya kibinadamu ya kushawishi, ili msalaba wa Kristo usije ukakosa nguvu yake. Kwa maana ujumbe wa msalaba kwa wale wanaopotea ni upuzi, lakini kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu. Kwa maana imeandikwa: “Nitaiharibu hekima ya wenye hekima, na kuzibatilisha akili za wenye akili.”

Kwa kuwa katika hekima ya Mungu, ulimwengu kwa hekima yake haukumjua yeye, ilimpendeza Mungu kuwaokoa wale waaminio kwa upuzi wa lile neno lililohubiriwa. Wayahudi wanataka miujiza na Wayunani wanatafuta hekima, lakini sisi tunamhubiri Kristo aliyesulibiwa, ambaye kwa Wayahudi ni kitu cha kukwaza na kwa Wayunani ni upuzi. Lakini kwa wale ambao Mungu amewaita, Wayahudi pia Wayunani, Kristo ni nguvu na hekima ya Mungu. Kwa maana upumbavu wa Mungu una hekima zaidi kuliko hekima ya wanadamu, nao udhaifu wa Mungu una nguvu kuliko nguvu ya wanadamu.

Ndugu zangu nilipokuja kwenu, sikuja na maneno ya ushawishi wala hekima ya hali ya juu nilipowahubiria siri ya Mungu. Kwa kuwa niliamua kutokujua kitu cho chote wakati nikiwa nanyi isipokuwa Yesu Kristo, naye amesulibiwa msalabani. Mimi nilikuja kwenu nikiwa dhaifu na mwenye hofu na kwa kutetemeka sana. Kuhubiri kwangu na ujumbe wangu haukuwa kwa hekima na maneno ya kuwashawishi watu, bali kwa madhihirisho ya nguvu za Roho Mtakatifu ili imani yenu isiwe imejengwa katika hekima ya wanadamu bali katika nguvu za Mungu.

Lakini miongoni mwa watu waliokomaa twanena hekima, wala si hekima ya ulimwengu huu au ya watawala wa dunia hii wanaobatilika. Sisi tunanena hekima ya Mungu ambayo ni siri, tena iliyofichika kwa wanadamu, ambayo Mungu aliikusudia kabla ya ulimwengu kuwepo, kwa ajili ya utukufu wetu. Hakuna hata mtawala mmoja wa nyakati zetu aliyeelewa jambo hili. Kwa maana kama wangelielewa, wasingemsulibisha Bwana wa utukufu. Lakini ni kama ilivyoandikwa: “Lile jambo ambalo jicho halijapata kuona, sikio halijapata kusikia, wala halikuingia moyoni, lile ambalo Mungu aliwaandalia wale wampendao”:

Lakini mambo haya Mungu ametufunulia kwa njia ya Roho wake. Roho huchunguza kila kitu, hata mambo ya ndani sana ya Mungu. Kwa maana ni nani anayejua mawazo ya mtu isipokuwa roho iliyo ndani ya huyo mtu? Vivyo hivyo hakuna mtu ajuaye mawazo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu. Basi hatukupokea roho ya dunia bali Roho yule atokaye kwa Mungu, ili tuweze kuelewa kile kipawa ambacho Mungu ametupatia bure. Haya ndiyo tusemayo, si kwa maneno tuliyofundishwa kwa hekima ya wanadamu bali kwa maneno tuliyofundishwa na Roho, tukifafanua kweli za kiroho kwa wale watu wa kiroho.

Mtu ambaye hana Roho wa Mungu hawezi kupokea mambo yatokayo kwa Roho wa Mungu, kwa kuwa ni upuzi kwake, naye hawezi kuyaelewa kwa sababu hayo yanaeleweka tu kwa jinsi ya rohoni. Mtu wa kiroho hutambua mambo yote, lakini yeye mwenyewe hatambuliwi na mtu ye yote. “Kwa maana ni nani aliyejua nia ya Bwana ili apate kumfundisha?” Lakini sisi tunayo nia ya Kristo.

Ndugu zangu, mimi sikuweza kusema nanyi kama watu wa kiroho, bali kama watu wa mwilini, kama watoto wachanga katika Kristo. Naliwanywesha maziwa, wala si chakula kigumu, kwa kuwa hamkuwa tayari kwa hicho chakula kigumu. Naam, hata sasa hamkiwezi.

Mimi nilipanda mbegu, Apolo akatia maji, lakini Mungu ndiye aliyekuza. Hivyo mwenye kupanda mbegu na mwenye kutia maji si kitu, bali Mungu peke yake ndiye akuzaye. Apandaye mbegu ni sawa na yule atiaye maji. Kila mmoja atalipwa kulingana na kazi yake. Sisi ni watenda kazi pamoja na Mungu, ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu.

Kwa neema Mungu aliyonipa, niliweka msingi kama mjenzi stadi na mtu mwingine anajenga juu ya huo msingi. Lakini kila mmoja inampasa awe mwangalifu jinsi anavyojenga juu yake. Kwa maana hakuna mtu ye yote awezaye kuweka msingi mwingine wo wote isipokuwa ule uliokwisha kuwekwa, ambao ni Yesu Kristo. Kama mtu ye yote akijenga juu ya msingi huu kwa kutumia dhahabu, fedha, mawe ya thamani, miti, majani au nyasi, kazi yake itaonekana kuwa ikoje, kwa kuwa siku ile itaidhihirisha kazi yake. Itadhihirishwa kwa moto, nao moto utapima ubora wa kazi ya kila mtu. Kama kile alichojenga kitabaki, atapokea thawabu. Kama kazi ya mtu itateketea, atapata hasara, ila yeye mwenyewe ataokolewa, lakini kama mtu aliyenusurika kwenye moto.

Lakini ninapohubiri injili siwezi kujisifu maana ninalazimika kuhubiri. Ole wangu nisipoihubiri Injili!

Nikihubiri kwa hiari ninayo thawabu, lakini kama si kwa hiari, ni kwamba nalazimika kufanya hivyo, basi ninachofanya ni kutekeleza tu uwakili niliowekewa. Basi je, thawabu yangu ni nini? Thawabu yangu ni hii: Ni kwamba katika kuhubiri Injili niitoe bila gharama, nisije nikatumia vibaya ule uwezo wangu nilio nao katika Injili.

Ingawa mimi ni huru, wala si mtumwa wa mtu ye yote, nimejifanya kuwa mtumwa wa kila mtu, ili niweze kuwavuta wengi zaidi. Kwa Wayahudi, nilikuwa kama Myahudi, ili niwapate Wayahudi. Kwa watu wale walio chini ya sheria, nilikuwa kama aliye chini ya sheria (ingawa mimi siko chini ya sheria), ili niweze kuwapata wale walio chini ya sheria. Kwa watu wasio na Sheria nilikuwa kama asiye na Sheria (ingawa siko huru mbali na Sheria ya Mungu, bali niko chini ya Sheria ya Kristo), ili niweze kuwapata wale wasio na Sheria. Kwa walio dhaifu nilikuwa dhaifu, ili niweze kuwapata walio dhaifu. Nimekuwa mtu wa hali zote kwa watu wote ili kwa njia yo yote niweze kuwaokoa baadhi yao.

Ningekuwa na karama ya unabii na kujua siri zote na maarifa yote, hata kama nina imani kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, mimi si kitu. Kama nikitoa mali yote niliyo nayo na kama nikijitolea mwili wangu uchomwe moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.

Basi ndugu zangu nataka niwakumbushe kuhusu Injili niliyowahubiria, mkaipokea na ambayo katika hiyo mmesimama. Kwa Injili hii mnaokolewa mkishikilia kwa uthabiti neno nililowahubiria ninyi. La sivyo, mmeamini katika ubatili.

Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo na neema yake kwangu haikuwa kitu bure. Bali nilizidi sana kufanya kazi kuliko mitume wote, lakini haikuwa mimi, bali ni ile neema ya Mungu iliyokuwa pamoja nami. Hivyo basi, kama ilikuwa ni mimi au ni wao hili ndilo tulihubirilo na hili ndilo mliaminilo.

Ninyi wapumbavu! Mpandacho hakiwi hai kama hakikufa. Mpandapo, hampandi mwili ule unaotegemewa kuwako, bali mwapanda mbegu tupu, pengine ya ngano au ya kitu kingine.

Lakini Mungu ashukuriwe, yeye ambaye siku zote hutufanya tuandamane kwa ushindi tukiwa ndani ya Kristo. Naye kwa kupitia sisi hueneza kila mahali harufu nzuri ya kumjua yeye. Kwa maana sisi kwa Mungu ni harufu nzuri ya manukato ya Kristo miongoni mwa wale wanaookolewa na kwa wale wanaopotea, sisi kwa wale wanaopotea ni harufu ya mauti iletayo mauti, lakini kwa wale wanaookolewa sisi ni harufu nzuri iletayo uzima. Ni nani awezaye mambo hayo?

Tofauti na watu wengine wengi, sisi hatufanyi biashara na Neno la Mungu kwa ajili ya kupata faida. Kinyume chake, katika Kristo tunalisema Neno la Mungu kwa unyofu, kama watu tuliotumwa kutoka kwa Mungu.

Basi ikiwa ile huduma iliyoleta mauti, ile iliyoandikwa kwa herufi juu ya jiwe ilikuja kwa utukufu hata Waisraeli wakawa hawawezi kuutazama uso wa Mose kwa sababu ya ule utukufu wake, ingawa ulikuwa ni wa kufifia, je, huduma ya Roho haitakuwa na utukufu zaidi? Ikiwa huduma ile iwahukumuyo wanadamu ina utukufu, je, haitakuwa ya utukufu zaidi ile huduma iletayo haki? Kwa maana kile kilichokuwa na utukufu sasa hakina utukufu ukilinganisha na huu utukufu uzidio sana wa Agano Jipya. Ikiwa kile kilichokuwa kinafifia kilikuja kwa utukufu, si zaidi sana utukufu wa kile kinachodumu?

Kwa hiyo, kwa kuwa tunalo tumaini hili, tuna ujasiri sana.

Haya yote yanatokana na Mungu, ambaye ametupatanisha sisi na nafsi yake kwa njia ya Yesu Kristo na kutupatia sisi huduma ya upatanisho: Kwamba Mungu alikuwa ndani ya Kristo akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake mwenyewe, akiwa hawahesabii watu dhambi zao. Naye ametukabidhi sisi ujumbe huu wa upatanisho.

Kwa hiyo sisi ni mabalozi wa Kristo, kana kwamba Mungu anawasihi kwa kupitia vinywa vyetu, nasi twawaomba sana ninyi kwa niaba ya Kristo, mpatanishwe na Mungu.

Kwa maana asema: “Wakati wangu uliokubalika nilikusikia, siku ya wokovu nilikusaidia.” Tazama, wakati uliokubalika ndio huu, siku ya wokovu ndiyo sasa.

Hatuweki kitu cha kukwaza katika njia ya mtu ye yote, ili huduma yetu isionekane kuwa na lawama,

Kwa maana huzuni ya kimungu huleta toba iletayo wokovu na wala haina majuto. Lakini huzuni ya kidunia husababisha mauti.

Kumbukeni kwamba: Ye yote apandaye kwa uchache pia atavuna kwa uchache, naye apandaye kwa ukarimu pia atavuna kwa ukarimu.

Yeye ampaye mpanzi mbegu kwa ajili ya kupanda na mkate kuwa chakula, atawapa na kuzizidisha mbegu zenu za kupanda na kuongeza mavuno ya haki yenu.

ili tuweze kuhubiri Injili sehemu zilizo mbali na maeneo yenu. Kwa maana hatutaki kujisifu kwa ajili ya kazi ambayo imekwisha kufanyika tayari katika eneo la mtu mwingine.

Je, nilitenda dhambi kwa kujishusha ili kuwainua ninyi kwa kuwahubiria Injili ya Mungu pasipo malipo?

Lakini hata ikiwa sisi au malaika atokaye mbinguni akihubiri injili nyingine tofauti na ile tuliyowahubiria sisi, basi mtu huyo alaaniwe milele! Kama vile tulivyokwisha kusema kabla, sasa nasema tena, ikiwa mtu ye yote atawahubiria injili kinyume na ile mliyoipokea na alaaniwe milele!

Je, sasa mimi ninatafuta kukubaliwa na wanadamu au kukubaliwa na Mungu? Au nataka kuwapendeza wanadamu? Kama ningekuwa bado najaribu kuwapendeza wanadamu, nisingekuwa mtumishi wa Kristo. Ndugu zangu, nataka mjue kwamba Injili niliyowahubiria haikutokana na wanadamu.

Nimesulibiwa pamoja na Kristo, wala si mimi tena ninayeishi bali Kristo ndiye aishiye ndani yangu. Uhai nilio nao sasa katika mwili, ninaishi kwa imani ya Mwana wa Mungu, aliyenipenda na kujitoa kwa ajili yangu.

Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi. Kwa kuwa kile apandacho mtu ndicho atakachovuna. Apandaye kwa mwili, katika mwili wake, atavuna uharibifu, lakini yeye apandaye katika Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele.

Alikuja na kuhubiri amani kwenu ninyi mliokuwa mbali na pia akahubiri amani kwao waliokuwa karibu.

Yeye ndiye aliyeweka wengine kuwa mitume, wengine kuwa manabii, wengine kuwa wainjilisti, wengine kuwa wachungaji na walimu, kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu kwa ajili ya kazi za huduma, ili kwamba mwili wa Kristo upate kujengwa mpaka sote tutakapoufikia umoja katika imani na katika kumjua sana Mwana wa Mungu na kuwa watu wazima kwa kufikia kimo cha ukamilifu wa Kristo. Ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwatupwa huku na huku na kuchukuliwa na kila upepo wa mafundisho kwa hila za watu, kwa ujanja, kwa kufuata njia zao za udanganyifu.

Mkiishi maisha ya upendo, kama vile Kristo alivyotupenda sisi akajitoa kwa ajili yetu kuwa sadaka yenye harufu nzuri na dhabihu kwa Mungu.

Niombeeni na mimi pia, ili kila nifunguapo kinywa changu, nipewe maneno ya kusema, niweze kutangaza siri ya Injili kwa ujasiri, ambayo mimi ni balozi wake katika vifungo. Ombeni ili nipate kuhubiri kwa ujasiri kama inipasavyo.

Kwa sababu ya vifungo vyangu, ndugu wengi katika Bwana wametiwa moyo kuhubiri neno la Mungu kwa ujasiri zaidi na bila woga. Ni kweli kwamba wengine wanamhubiri Kristo kutokana na wivu na kwa kutaka kushindana, lakini wengine wanamhubiri Kristo kwa nia njema. Hawa wa mwisho wanamhubiri Kristo kwa moyo wa upendo, wakifahamu kwamba nimo humu gerezani kwa ajili ya kuitetea Injili. Hao wa kwanza wanamtangaza Kristo kutokana na tamaa zao wenyewe wala si kwa moyo mweupe bali wanakusudia kuongeza mateso yangu katika huku kufungwa kwangu. Lakini inadhuru nini? Jambo la muhimu ni kwamba kwa kila njia, ikiwa ni kwa nia mbaya au njema Kristo anahubiriwa. Nami kwa ajili ya jambo hilo ninafurahi. Naam, nami nitaendelea kufurahi,

mradi tu kwamba mnaendelea kuwa waaminifu, mkiwa mmefanywa imara na thabiti katika imani, pasipo kuliacha tumaini lililoahidiwa na Injili. Hii ndiyo ile Injili mliyoisikia ambayo imehubiriwa kwa kila kiumbe chini ya mbingu na ambayo mimi Paulo, nimekuwa mtumwa wake. Sasa nafurahia kule kuteseka kwangu kwa ajili yenu na katika mwili wangu ninatimiliza yale yaliyopungua katika mateso ya Kristo kwa ajili ya mwili wake, ambao ni Kanisa. Mimi nimekuwa mtumishi wa Kanisa kwa wajibu alionipa Mungu ili kuwaletea ninyi Neno la Mungu kwa ukamilifu. Siri hii ilikuwa imefichika kwa karne nyingi na vizazi vingi, lakini sasa imefunuliwa kwa watakatifu. Kwao, Mungu amechagua kujulisha miongoni mwa watu Mataifa utukufu wa utajiri wa siri hii, ambayo ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu. Yeye Kristo ndiye tunayemtangaza, tukimwonya kila mtu na kumfundisha kila mtu kwa hekima yote ili tuweze kumleta kila mmoja akiwa amekamilika katika Kristo.

Kwa kuwa mnajua kwamba mtapokea urithi wenu kutoka kwa Bwana kuwa thawabu yenu. Ni Bwana Yesu Kristo mnayemtumikia.

Pia tuombeeni na sisi ili Mungu atufungulie mlango wa kunena, ili tupate kuitangaza siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake pia mimi nimefungwa. Ombeni ili nipate kuitangaza Injili kwa udhahiri kama ipasavyo kunena. Iweni na hekima jinsi mnavyoenenda mbele yao wale walio nje, mkiutumia vizuri wakati wenu. Maneno yenu yawe yamejaa neema siku zote, yanayofaa, ili mjue jinsi iwapasavyo na inavyofaa kumjibu kila mtu.

kwa sababu ujumbe wetu wa Injili haukuja kwenu kwa maneno matupu bali pia ulidhihirishwa katika nguvu na katika Roho Mtakatifu, tena ukiwa na uthibitisho kamili, kama vile ninyi wenyewe mnavyojua jinsi tulivyoenenda katikati yenu kwa ajili yenu. Nanyi mkawa wafuasi wetu na wa Bwana, ingawa mlipata mateso mengi, mlilipokea lile Neno kwa furaha katika Roho Mtakatifu.

kama vile mjuavyo, tulikuwa tumeteswa na kutukanwa huko Filipi, lakini hata hivyo, kwa msaada wa Mungu wetu, tulikuwa na ujasiri wa kuwaambia Injili ya Mungu ingawa kulikuwa na upinzani mkubwa. Kwa maana himizo letu halikutokana na hila wala nia mbaya au udanganyifu. Kinyume chake, tulinena kama watu tuliokubaliwa na Mungu tukakabidhiwa Injili. Sisi hatujaribu kuwapendeza wanadamu bali kumpendeza Mungu, yeye ayachunguzaye mawazo ya ndani sana ya mioyo yetu. Kama mjuavyo na Mungu akiwa shahidi yetu hatukuja kwenu kwa maneno ya kujipendekeza au maneno yasiyo ya kweli kwa ajili ya kuficha tamaa mbaya. Wala hatukuwa tunatafuta sifa kutoka kwa wanadamu, wala kutoka kwenu au kwa mtu mwingine awaye yote. Kama mitume wa Kristo tungaliweza kuwa mzigo kwenu, lakini tulikuwa wapole katikati yenu kama mama anayewatunza watoto wake wadogo. Tuliwapenda sana kiasi kwamba tulifurahia kushirikiana nanyi, si Injili ya Mungu tu, bali hata maisha yetu, kwa sababu mlikuwa wa thamani mno kwetu. Ndugu zetu, mnakumbuka juhudi yetu na taabu yetu. Tulifanya kazi usiku na mchana, ili tusimlemee mtu ye yote wa kwenu wakati tulipokuwa tunawahubiria Injili ya Mungu.

siku hiyo atakapokuja kutukuzwa katika watakatifu wake na kustaajabiwa miongoni mwa wote walioamini. Ninyi pia mtakuwa miongoni mwa hawa kwa sababu mliamini ushuhuda wetu kwenu.

Kwa kusudi hili Mungu aliwaita kwa njia ya kuhubiri kwetu Injili, ili kwamba mpate kushiriki katika utukufu wa Bwana Yesu Kristo. Hivyo basi, ndugu wapendwa, simameni imara na myashike sana yale mafundisho tuliyowapa ikiwa ni kwa maneno ya kinywa au kwa barua.

Pigana vile vita vizuri vya imani. Shika uzima wa milele ambao ndio ulioitiwa ulipokiri ule ukiri mzuri mbele ya mashahidi wengi.

Kwa hiyo usione haya kushuhudia kuhusu Bwana wetu, wala usinionee haya mimi niliye mfungwa kwa ajili yake. Bali uishiriki pamoja nami taabu ya Injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu, ambaye alituokoa na kutuita katika mwito mtakatifu: si kwa kadiri ya matendo yetu mema bali kwa sababu ya kusudi lake mwenyewe na neema yake. Neema hii tulipewa katika Kristo Yesu kabla ya kuwako kwa ulimwengu. Lakini sasa imefunuliwa kwa kudhihirishwa kwake Mwokozi wetu, Kristo Yesu, ambaye amebatilisha mauti na kuleta uzima na kutokufa kwa njia ya Injili. Nami nimewekwa kuwa mhubiri, mtume na mwalimu wa Injili hii. Hii ndiyo sababu ninateseka namna hii, lakini sioni haya kwa maana ninamjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kuwa anaweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hadi siku ile.

Nayo mambo yale uliyonisikia nikiyasema mbele ya mashahidi wengi, uwakabidhi watu waaminifu watakaoweza kuwafundisha watu wengine vile vile.

Kwa hiyo ninavumilia mambo yote kwa ajili ya wateule wa Mungu, kusudi wao nao wapate wokovu ulio katika Kristo Yesu, pamoja na utukufu wa milele. Hili ni neno la kuaminiwa: Kwa maana kama tumekufa pamoja naye, tutaishi pia pamoja naye. Kama tukistahimili, pia tutatawala pamoja naye. Kama tukimkana yeye, naye atatukana sisi.

Endelea kuwakumbusha mambo haya ukiwaonya mbele za Bwana waache kushindana kwa maneno ambayo hayana faida yo yote bali huwaangamiza tu wale wanaoyasikia. Jitahidi kujionyesha kwa Mungu kuwa umekubaliwa naye, mtenda kazi asiye na sababu ya kuona aibu, ukilitumia kwa usahihi neno la kweli. Jiepushe na maneno mabaya, yasiyo na maana, yasiyo ya utauwa, kwa maana hayo huzidi kuwatosa watu katika kukosa heshima kwa Mungu.

Uhubiri Neno, uwe tayari wakati ufaao na wakati usiofaa, karipia, kemea na kuonya kwa uvumilivu wote na kwa mafundisho mazuri. Maana wakati utakuja watu watakapokataa kuyakubali mafundisho yenye uzima, badala yake, ili kutimiza tamaa zao wenyewe, watajikusanyia idadi kubwa ya walimu wapate kuwaambia yale ambayo masikio yao yanayowasha yanatamani kuyasikia. Watakataa kusikiliza kweli na kuzigeukia hadithi za uongo. Kwa habari yako wewe, vumilia mateso, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiza wajibu wote wa huduma yako.

Lakini Bwana alisimama upande wangu akanitia nguvu, ili kwa kupitia mimi lile Neno lihubiriwe kwa ukamilifu, watu wote Mataifa wapate kulisikia. Mimi niliokolewa kutoka katika kinywa cha simba.

Kwa maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa.

Naomba utiwe nguvu katika kuishuhudia imani yako, ili upate kuwa na ufahamu mkamilifu juu ya kila kitu chema tulicho nacho ndani ya Kristo. Upendo wako umenifurahisha mno na kunitia moyo, kwa sababu wewe ndugu, umeiburudisha mioyo ya watakatifu. Hata hivyo, ingawa katika Kristo ningeweza kuwa na ujasiri na kukuagiza yale yakupasayo kutenda,

Kwa hiyo, kwa kuwa bado ahadi ya kuingia rahani iko wazi, tujihadhari ili hata mmoja wenu asije akaikosa. Kwa maana sisi pia tumesikia Injili iliyohubiriwa kwetu, kama nao walivyosikia, lakini ujumbe ule waliousikia haukuwa na maana kwao, kwa sababu wale waliousikia hawakuuchanganya na imani. Sasa sisi ambao tumeamini tunaingia katika ile raha, kama vile Mungu alivyosema, “Hivyo natangaza kwa kiapo katika hasira yangu, ‘Kamwe hawataingia rahani mwangu.’ ” Lakini kazi yake ilikamilika tangu kuumbwa kwa ulimwengu.

Kwa maana Neno la Mungu li hai tena lina nguvu tena lina makali kuliko upanga uwao wote wenye makali kuwili, tena linachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, viungo na mafuta yaliyo ndani yake, tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. Wala hakuna kiumbe cho chote kilichofichika machoni pa Mungu. Kila kitu kimefunuliwa na kiko wazi machoni pake yeye ambaye kwake ni lazima tutatoa hesabu.

Kwa hiyo msiutupe ujasiri wenu, kwa maana una thawabu kubwa mno.

Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, kwa maana ye yote anayemjia Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko na ya kuwa huwapa thawabu wale wamtafutao kwa bidii.

Kama mtu ye yote miongoni mwenu amepungukiwa na hekima na amwombe Mungu, yeye awapaye watu wote kwa ukarimu wala hana kinyongo, naye atapewa.

Kama mtu akidhani ya kuwa anayo dini lakini hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hujidanganya moyoni mwake, wala dini yake mtu huyo haifai kitu.

Ndugu zangu, ye yote miongoni mwenu akipotoka na kuicha kweli, naye akarejezwa na mtu mwingine, hamna budi kujua kwamba ye yote amrejezaye mwenye dhambi kutoka katika upotovu wake, ataiokoa roho ya huyo mwenye dhambi kutoka katika mauti na kusitiri wingi wa dhambi.

Mitume walidhihirishiwa kwamba walikuwa hawajihudumii wao wenyewe, bali walihudumu kwa ajili yenu katika mambo hayo ambayo sasa yamehubiriwa kwenu na wale waliowahubiri ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Mambo ambayo hata malaika wanatamani kuyafahamu.

Kwa maana mmezaliwa upya, si kwa mbegu ile iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika, kwa neno la Mungu lililo hai na linalodumu hata milele. Maana, “Watu wote ni kama majani, na utukufu wao ni kama ua la shambani; majani hunyauka na ua lake hupukutika, lakini neno la Mungu ladumu milele.” Hili ndilo neno lililohubiriwa kwenu.

Kama watoto wachanga, waliozaliwa sasa, yatamanini maziwa ya kiroho yasiyochanganywa na kitu kingine cho chote, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu, ikiwa kweli mmeonja ya kwamba Bwana ni mwema.

Kwenu ninyi mnaoamini, yeye ni wa thamani. Lakini kwao wasioamini, “Jiwe lile walilolikataa waashi limekuwa Jiwe Kuu la pembeni,” tena, “Jiwe lenye kuwafanya watu wajikwae, mwamba wa kuwafanya waanguke.” Wanajikwaa kwa sababu hawakulitii lile neno: kama walivyowekewa tangu zamani.

Lakini ninyi ni taifa teule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu la Mungu, mlioitwa ili kutangaza sifa zake yeye aliyewaita kutoka gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu.

Bali mtakaseni Kristo kuwa Bwana mioyoni mwenu. Siku zote mwe tayari kumjibu mtu ye yote atakayewauliza kuhusu tumaini lililomo ndani yenu. Lakini fanyeni hivyo kwa upole na kwa heshima, mkizitunza dhamiri zenu ziwe safi, ili wale wasemao mabaya dhidi ya mwenendo wenu mzuri katika Kristo, waaibike kwa ajili ya masingizio yao.

Tulipowafahamisha juu ya uweza na kuja kwa Bwana wetu Yesu Kristo, hatukufuata hadithi zilizotungwa kwa werevu, bali tulishuhudia kwa macho yetu ukuu wake.

Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake kama watu wengine wanavyodhani kukawia. Yeye anawavumilia, maana hataki mtu ye yote aangamie, bali kila mmoja afikilie toba.

Kama tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki, atatusamehe dhambi zetu na kutusafisha toka kwenye udhalimu wote.

Ye yote aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wa Mungu wakaa ndani yake, wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa na Mungu. Kwa jinsi hii tunaweza kujua dhahiri watoto wa Mungu na pia watoto wa ibilisi. Ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.

Sisi twatokana na Mungu na ye yote anayemjua Mungu hutusikiliza, lakini asiyetokana na Mungu hatusikilizi. Hivi ndivyo tunavyoweza kutambua Roho wa Kweli na roho ya upotovu.

Kama tunaukubali ushuhuda wa wanadamu, basi ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi, kwa kuwa huu ndio ushuhuda wa Mungu kwamba amemshuhudia Mwanawe. Kila mtu amwaminiye Mwana wa Mungu anao huu ushuhuda moyoni mwake. Kila mtu asiyemwamini Mungu amemfanya yeye kuwa mwongo, kwa sababu hakuamini ushuhuda Mungu alioutoa kuhusu Mwanawe. Huu ndio ushuhuda: kwamba Mungu ametupa uzima wa milele, nao huo uzima umo katika Mwanawe.

ambaye anashuhudia kuhusu kila kitu alichoona, yaani, Neno la Mungu na ushuhuda wa Yesu Kristo.

Tazama! Nasimama mlangoni nabisha. Kama mtu ye yote akisikia sauti yangu na kufungua mlango, nitaingia ndani na kula pamoja naye, naye pamoja nami.

Nao walikuwa wakipiga kelele kwa sauti kubwa wakisema: “Wokovu una Mungu wetu, yeye aketiye kwenye kiti cha enzi na Mwana-Kondoo!”

Nami nitawapa mashahidi wangu wawili uwezo, nao watoe unabii kwa muda wa siku 1,260, wakiwa wamevaa nguo za gunia.” Hawa ndio ile mizeituni miwili na vile vinara viwili vya taa visimamavyo mbele za Bwana Mungu wa dunia yote. Kama mtu ye yote akitaka kuwadhuru, moto hutoka vinywani mwao na kuwateketeza adui zao. Hivi ndivyo impasavyo kufa mtu ye yote atakayetaka kuwadhuru. Watu hawa wanao uwezo wa kufunga anga ili mvua isinyeshe wakati wote watakapokuwa wanatoa unabii wao. Nao watakuwa na uwezo wa kuyabadili maji kuwa damu na kuipiga dunia kwa kila aina ya mapigo mara kwa mara kama watakavyo.

Basi watakapokuwa wamemaliza ushuhuda wao, yule mnyama atokaye katika lile Shimo lisilo na mwisho atapigana nao vita, atawashinda na kuwaua. Maiti zao zitabaki katika barabara ya mji mkubwa, ambao kwa fumbo unaitwa Sodoma na Misri, ambapo pia Bwana wao alisulibiwa. Kwa muda wa siku tatu na nusu, watu wa kila kabila, jamaa, lugha na taifa wataziangalia hizo maiti zao na hawataruhusu wazikwe. Watu waishio duniani watazitazama kwa furaha maiti za hao manabii wawili na kushangilia kwa kupeana zawadi kwa sababu hao manabii waliwatesa watu waishio duniani. Lakini baada ya zile siku tatu na nusu, pumzi ya uhai kutoka kwa Mungu ikawaingia, nao wakasimama kwa miguu yao na wote waliowaona wakaingiwa na hofu kuu.

Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo na kwa neno la ushuhuda wao. Wala wao hawakuyapenda maisha yao hata kufa.

Kisha lile joka likapatwa na hasira kali kwa ajili ya huyo mwanamke, likaondoka ili kupigana vita na watoto waliosalia wa huyo mwanamke, yaani, wale wanaozitii amri za Mungu na kuushika ushuhuda wa Yesu Kristo. Lile joka likasimama kwenye mchanga wa bahari.

Vinywani mwao hapakuonekana uongo, wala hawakuwa na hatia yo yote.

Baada ya haya nikasikia sauti kama ya umati mkubwa mbinguni wakipiga kelele wakisema: “Haleluya! Wokovu na utukufu na uweza ni vya Mungu wetu,

Ndipo malaika akaniambia, “Andika: ‘Wamebarikiwa wale walioalikwa kwenye karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo!’ ” Naye akaongeza kusema, “Haya ndiyo maneno ya kweli ya Mungu.” Ndipo nikaanguka kifudifudi miguuni pake ili kumwabudu, lakini yeye akaniambia, “Usifanye hivyo! Mimi pia ni mtumishi mwenzako pamoja na ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Mwabudu Mungu! Maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii.”

Kisha nikaona viti vya enzi vilivyokuwa vimekaliwa na hao waliopewa mamlaka ya kuhukumu. Nami nikaona roho za wale waliokatwa vichwa kwa sababu ya ushuhuda wa Yesu na kwa sababu ya neno la Mungu. Hawakuwa wamemsujudia huyo mnyama wala sanamu yake wala hawakupokea ile chapa yake kwenye vipaji vya nyuso zao au kwenye mikono yao. Wakawa hai na kutawala pamoja na Kristo miaka 1,000.

“Tazama, naja upesi! Thawabu yangu i mkononi mwangu, nami nitampa kila mtu sawasawa na alivyotenda.

Swahili - Kiswahili - SW

NEN'2014 - Neno Bibilia Takatifu Kiswahili Contemporary Version - 2014

This Bible text is from Biblica Open Kiswahili Contemporary Version Neno 2015
https://open.bible/bibles/swahili-biblica-text-bible/
provided by: Biblica Inc, available by Creative Commons CC-BY-SA-4.0,
and this new compilation is shared as www.creativecommons.org/licenses/by-sa/4.0.
Languages are made available to you by www.ipedge.net