26 – Serikali
Haya ni maneno matakatifu ya Mungu Mwenyezi.
Hatupendi maneno ya wanadamu.
Kwa mtu yeyote anayempenda Mungu... hivi ndivyo Mungu anasema kuhusu: Serikali.
Haya ni maneno matakatifu ya Mungu Mwenyezi.
Hatupendi maneno ya wanadamu.
Kwa mtu yeyote anayempenda Mungu... hivi ndivyo Mungu anasema kuhusu: Serikali.
Zaidi ya hayo, Manase pia alimwaga damu nyingi isiyo na hatia kwamba aliijaza Yerusalemu kutoka mwanzo hadi mwisho, mbali na dhambi ambayo alikuwa amesababisha Yuda kufanya, hivyo kwamba wakatenda maovu machoni pa BWANA.
”Kwa nini mataifa wanashauriana kufanya mabaya, na mataifa kula njama bure? Wafalme wa dunia wanajipanga na watawala wanajikusanya pamoja dhidi ya BWANA na dhidi ya Mpakwa Mafuta wake. Wanasema, “Tuvunje minyororo yao na kuvitupilia mbali vifungo vyao.” Yeye atawalaye mbinguni hucheka, Bwana huwadharau.
”Yule malaika wa saba akaipiga tarumbeta yake, pakawa na sauti kubwa mbinguni iliyosema: “Ufalme wa ulimwengu umekuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atatawala milele na milele.” Nao wale wazee ishirini na wanne, waliokuwa wameketi mbele za Mungu, kwenye viti vyao vya enzi wakaanguka kifudifudi wakamwabudu Mungu, wakisema: “Tunakushukuru, BWANA Mungu Mwenyezi, uliyeko na uliyekuwako, kwa kuwa umetwaa uweza wako mkuu na ukaanza kutawala. Mataifa walikasirika kwa kuwa wakati wa ghadhabu Yako umewadia. Wakati umewadia wa kuwahukumu waliokufa na kuwapa thawabu watumishi wako manabii na watakatifu wako pamoja na wale wote wanaoliheshimu Jina Lako, wakubwa kwa wadogo: na kuwaangamiza wale wanaoiangamiza dunia.”
”BWANA Mungu alimuumba mtu kutoka mavumbi ya ardhi, akampulizia pumzi ya uhai puani mwake, mtu akawa kiumbe hai.
”“Ye yote amwagaye damu ya mwanadamu, damu yake itamwagwa na mwanadamu, kwa kuwa katika mfano wa Mungu, Mungu alimuumba mwanadamu.
”Hizi ndizo koo za wana wa Noa, kufuatana na vizazi vyao, katika mataifa yao. Kutokana na hawa mataifa yalienea duniani kote baada ya gharika.
”Wakati huo dunia yote ilikuwa na lugha moja na msemo mmoja. Watu walipoelekea upande wa mashariki, wakafika kwenye tambarare katika nchi ya Shinari nao wakaishi huko. Wakasemezana wao kwa wao, “Njoni, tufyatue matofali na tuyachome vizuri kwa moto.” Walitumia matofali badala ya mawe, na lami kwa ajili ya kushikamanishia hayo matofali. Ndipo wakasema, “Njoni, tujijengee mji wenye mnara ambao utafika hadi mbinguni, ili tujipatie jina tusije tukatawanyika usoni pa dunia yote.” Lakini BWANA akashuka ili auone mji na mnara wanadamu waliokuwa wanaujenga. BWANA akasema, “Kama taifa moja wanaozungumza lugha moja wameanza kufanya hili, basi hakuna lo lote watakalopanga kufanya ambalo halitawezekana kwao. Njoni, tushuke tuvuruge lugha yao ili wasielewane wao kwa wao.” Hivyo BWANA akawatawanya kutoka mahali pale kwenda katika dunia yote, nao wakaacha kuujenga huo mji. Ndiyo maana pakaitwa Babeli, kwa sababu hapo ndipo BWANA alipoivuruga lugha ya dunia nzima. Kutoka hapo BWANA akawatawanya katika uso wa dunia yote.
”“Mimi nitakufanya taifa kubwa na nitakubariki, Nitalikuza jina lako, nawe utakuwa baraka.
”Mungu akamwambia, “Mimi ndimi Mungu Mwenyezi, ukazae na kuongezeka. Taifa na jamii ya mataifa itatoka kwako, nao wafalme watatoka viunoni mwako.
”Wewe utakuwa msimamizi wa jumba langu la kifalme, na watu wangu wote watatii amri zako. Ni kuhusu kiti cha ufalme tu nitakuwa mkuu kuliko wewe.” Kwa hiyo Farao akamwambia Yosefu, “Sasa nakuweka uwe msimamizi wa nchi yote ya Misri.” Ndipo Farao akaivua pete yake ya muhuri kutoka kidoleni mwake na kuivalisha katika kidole cha Yosefu. Akamvika majoho mazuri ya kitani safi na mkufu wa dhahabu shingoni mwake. Akampandisha katika gari lake la farasi kama msaidizi wake, watu wakatangulia wakishangilia, wakisema, “Achieni njia!” Ndivyo Farao alivyomweka Yosefu kuwa msimamizi wa nchi yote ya Misri. Kisha Farao akamwambia Yosefu, “Mimi ni Farao, lakini pasipo neno lako, hakuna mtu mwenye ruhusa kuinua mkono au mguu katika nchi yote ya Misri.”
”Ndipo Mose na Aroni wakaenda kwa Farao wakafanya sawasawa kama vile BWANA alivyoagiza. Aroni akaitupa ile fimbo yake chini mbele ya Farao na maafisa wake, nayo ikawa nyoka. Farao naye akawaita watu wenye maarifa na wachawi na waganga wa Kimisri, nao wakafanya vivyo hivyo kwa siri ya uganga wao. Kila mmoja alitupa fimbo yake chini, nayo ikawa nyoka. Lakini fimbo ya Aroni ikazimeza zile fimbo zao. Hata hivyo moyo wa Farao ukawa mgumu, naye hakuwasikiliza Mose na Aroni, sawasawa kama vile BWANA alivyokuwa amesema.
”Kwa hiyo Mose akasema, “Hili ndilo BWANA asemalo: ‘Panapo usiku wa manane Mimi nitapita katika nchi yote ya Misri. Kila mwanaume kifungua mimba katika Misri atakufa, kuanzia mzaliwa wa kwanza wa kiume wa Farao, aketiye penye kiti cha ufalme, hadi mzaliwa wa kwanza wa kiume wa mtumwa wa kike, anayesaga nafaka kwa jiwe, pamoja na kila mzaliwa wa kwanza wa mifugo. Patakuwepo kilio kikubwa katika nchi yote ya Misri, kilio kibaya ambacho hakijakuwepo wala kamwe hakitakuwepo tena. Lakini miongoni mwa Waisraeli hakuna hata mbwa atakayembwekea mwanadamu wala mnyama ye yote.’ Ndipo mtakapojua kuwa BWANA huweka tofauti kati ya Misri na Israeli. Maafisa hawa wako wote watanijia, wakisujudu mbele yangu, wakisema, ‘Ondoka, wewe pamoja na watu wako wote wanaokufuata!’ Baada ya haya nitaondoka.” Kisha Mose, huku akiwa amewaka hasira, akamwacha Farao.
”Ilipofika usiku wa manane, BWANA akawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika Misri, kuanzia mzaliwa wa kwanza wa Farao, mrithi wa kiti cha ufalme, hadi mzaliwa wa kwanza wa mfungwa, aliyekuwa gerezani, na wazaliwa wa kwanza wa mifugo yote pia. Farao, na maafisa wake wote, na Wamisri wote wakaamka usiku, na kulikuwa na kilio kikubwa katika nchi ya Misri, kwa kuwa haikuwepo nyumba ambayo hakufa mtu.
”BWANA atatawala milele na milele.”
”Sasa nisikilize mimi, nitakupa shauri, naye Mungu na awe pamoja nawe. Yapasa wewe uwe mwakilishi wa watu mbele za Mungu na ulete mashauri yao kwake. Uwafundishe amri na sheria, tena uwaonyeshe namna ya kuishi na kazi zinazowapasa wao kufanya. Lakini uchague watu wenye uwezo miongoni mwa watu wote, watu wanaomwogopa Mungu, watu waaminifu wanaochukia mali ya dhuluma, uwateuwe wawe maafisa juu ya maelfu, mamia, hamsini na makumi. Waweke wawe waamuzi wa watu kwa wakati wote, lakini waambie wakuletee kila shauri lililo gumu; yale yaliyo rahisi wayaamue wao wenyewe. Hii itafanya mzigo wako kuwa mwepesi, kwa sababu watashirikiana nawe.
”Akawachagua watu wenye uwezo kutoka Israeli yote akawafanya kuwa viongozi wa watu, maafisa juu ya maelfu, mamia, hamsini na makumi. Wakatumika kama waamuzi wa watu kwa wakati wote. Mashauri magumu wakayaleta kwa Mose, lakini yale yaliyo rahisi wakayaamua wenyewe.
”ninyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani na taifa takatifu.’ Haya ndiyo maneno utakayosema kwa wana wa Israeli.” Kwa hiyo Mose akarudi, akawaita wazee wa watu na kuwaambia maneno yote ambayo BWANA alikuwa amemwamuru ayaseme.
”“Usimkufuru Mungu au kulaani mtawala wa watu wako.
”“ ‘Msijitie unajisi kwa njia yo yote katika hizi, kwa sababu hivi ndivyo mataifa nitakayoyafukuza mbele yenu yalivyojitia unajisi. Hata nchi ikatiwa unajisi, hivyo nikaiadhibu kwa dhambi zake nayo nchi ikawatapika wakazi wake. Lakini ni lazima uzitunze amri zangu na sheria zangu. Mzaliwa na wageni waishio miongoni mwenu kamwe wasifanye mambo yo yote ya machukizo haya, kwa kuwa mambo haya yote yalifanywa na watu walioishi katika nchi hii kabla yenu na nchi ikawa najisi. Kama mkiinajisi nchi, itawatapika kama ilivyowatapika mataifa yaliyowatangulia.
”“ ‘Shika amri na sheria zangu zote na kuzifuata, ili kwamba katika nchi ninayowaleta kuishi isiwatapike. Kamwe msiishi kwa kufuata desturi za mataifa nitakayoyafukuza mbele yenu. Kwa sababu walifanya mambo haya yote, nami nikachukizwa sana nao. Lakini niliwaambia, “Mtaimiliki nchi yao; nitawapa ninyi kuwa urithi, nchi inayotiririka maziwa na asali.” Mimi ndimi BWANA Mungu wenu, ambaye amewatenga kutoka katika mataifa.
”Hizi ndizo amri, sheria na pia masharti ambazo BWANA alifanya kati yake mwenyewe na Waisraeli katika Mlima Sinai kwa kupitia Mose.
”Wakati utakapoingia katika nchi anayowapa BWANA Mungu wenu kuimiliki na kukaa humo, nanyi mkasema, “Na tumweke mfalme juu yetu kama mataifa yanayotuzunguka,” iweni na uhakika wa kumweka mfalme juu yenu ambaye BWANA Mungu wenu atamchagua. Ni lazima atoke miongoni mwa ndugu zenu wenyewe. Msimweke mgeni juu yenu ambaye si ndugu wa Kiisraeli. Hata hivyo, kamwe mfalme asijipatie hesabu kubwa ya farasi kwa ajili yake mwenyewe, au kuwafanya watu warudi Misri ili kupata farasi zaidi, kwa maana BWANA amekuambia, “Hamtairudia njia ile tena.” Kamwe asioe wake wengi, la sivyo moyo wake utapotoka. Kamwe asijilimbikizie kiasi kikubwa cha fedha na dhahabu.
”Atakapokuwa amekalia kiti cha ufalme wake, ajiandikie kwenye kitabu nakala ya sheria kwa ajili yake mwenyewe kutoka zile sheria za makuhani ambao ni Walawi. Atakuwa na nakala hiyo, naye ataisoma siku zote za maisha yake ili kwamba ajifunze kumheshimu BWANA Mungu wake na kufuata kwa uangalifu maneno yote ya sheria hii na amri hizi, naye asijifikirie kuwa ni bora kuliko ndugu zake na kuipotosha sheria. Ndipo yeye na wazao wake watatawala katika ufalme wake kwa muda mrefu katika Israeli.
”Aliye Juu Sana alipowapa mataifa urithi wao, alipogawanya wanadamu wote, aliweka mipaka kwa ajili ya mataifa sawasawa na hesabu ya wana wa Israeli.
”Waisraeli wakamwambia Gideoni, “Ututawale, wewe, wanao na wana wa wana wako, kwa kuwa umetuokoa kutoka mikononi mwa Wamidiani.” Lakini Gideoni akawaambia, “Mimi sitatawala juu yenu, wala wanangu hawatatawala juu yenu. BWANA ndiye atakayetawala juu yenu ninyi.”
”Katika siku hizo Israeli hawakuwa na mfalme, kila mmoja akafanya kama alivyoona vyema machoni pake mwenyewe.
”Samweli alipokuwa mzee, akaweka wanawe kuwa waamuzi wa Israeli. Mzaliwa wa kwanza alikuwa Yoeli na jina la wa pili alikuwa Abiya, nao wakatumika huko Beer-Sheba. Lakini wanawe hawakuenenda katika njia zake. Waliziacha wakageukia faida za udanganyifu nao wakapokea rushwa na kupotosha haki.
”Lakini wao waliposema, “Tupe mfalme wa kutuongoza,” hili lilimchukiza Samweli, hivyo akamwomba BWANA. Naye BWANA akamwambia: “Sikiliza yale yote watu wanayokuambia, si wewe ambaye wamekukataa, bali wamenikataa mimi kuwa mfalme wao.
”Sasa wasikilize, lakini waonye kwa makini na uwafahamishe yale watakayotendewa na mfalme atakayewatawala.” Samweli akawaambia wale watu ambao walikuwa wakiomba wapewe mfalme maneno yote ya BWANA. Akasema, “Hivi ndivyo atakavyowatendea mfalme atakayewatawala. Atawachukua wana wenu na kuwafanya watumike kwa magari yake ya vita na farasi, nao watakimbia mbele ya magari yake. Baadhi yao atawaweka kuwa majemadari wa jeshi wa maelfu na majemadari wa jeshi wa hamsini, wengine kulima mashamba yake na kuvuna mavuno yake, pia na wengine kutengeneza silaha za vita na vifaa kwa ajili ya magari yake. Atawachukua binti zenu kuwa watengeneza manukato, wapishi na waokaji. Atayachukua mashamba yenu yaliyo mazuri, mashamba ya mizabibu na mashamba yenu ya mizeituni na kuwapa watumishi wake. Ataichukua sehemu ya kumi ya nafaka yenu na ya zabibu zenu na kuwapa maafisa wake na watumishi wake. Atawachukua watumishi wenu wa kiume na wa kike na ng'ombe wenu walio wazuri sana na punda zenu kwa matumizi yake mwenyewe. Atachukua sehemu ya kumi ya makundi yenu ya kondoo na mbuzi, na ninyi wenyewe mtakuwa watumwa wake. Siku ile itakapowadia, mtalia kwa kutaka msaada kutokana na mfalme mliyemchagua, naye BWANA hatawajibu.”
”Lakini watu wakakataa kumsikiliza Samweli wakasema, “Hapana! Tunataka mfalme wa kututawala. Kisha tutakuwa kama mataifa mengine yote, tukiwa na mfalme wa kutuongoza na kwenda mbele yetu na kutupigania vita vyetu.”
”Samweli alipomwona Sauli, BWANA akamwambia, “Huyu ndiye mtu yule niliyekuambia habari zake, kwamba yeye atawatawala watu wangu.”
”Ndipo Samweli akachukua chupa ndogo ya mafuta na kuyamimina juu ya kichwa cha Sauli, akambusu, akisema, “Je, BWANA hakukutia mafuta uwe kiongozi juu ya watu wake Israeli?
”Lakini sasa mmemkataa Mungu wenu, ambaye anawaokoa toka katika maafa yenu yote na taabu zenu zote. Nanyi mmesema, ‘Hapana, tuwekee mfalme atutawale.’ Sasa basi, jihudhurisheni wenyewe mbele za BWANA kwa kabila zenu na kwa koo zenu.”
”Samweli akawaambia watu wote, “Je, mnamwona mtu ambaye BWANA amemchagua? Hayupo aliye kama yeye miongoni mwa watu wote.” Ndipo watu wakapiga kelele, wakasema, “Mfalme na aishi maisha marefu.” Samweli akawaeleza watu madaraka ya ufalme. Akayaandika kwenye kitabu na kuweka mbele za BWANA. Kisha Samweli akawaruhusu watu, kila mmoja aende nyumbani kwake.
”Sauli pia akaenda nyumbani kwake huko Gibea, akisindikizwa na watu hodari ambao Mungu alikuwa amegusa mioyo yao. Lakini baadhi ya watu wakorofi walisema, “Huyu mtu atawezaje kutuokoa?” Wakamdharau na wala hawakumletea zawadi. Lakini Sauli akanyamaza kimya.
”Sauli aliposikia maneno yao, Roho wa Mungu akaja juu yake kwa nguvu, naye akawaka hasira. Akachukua jozi ya maksai na kuwakata vipande vipande, naye kuvituma hivyo vipande kupitia wajumbe katika Israeli yote, wakitangaza, “Hivi ndivyo itakavyofanyika kwa maksai wa kila mmoja ambaye hatamfuata Sauli na Samweli.” Kisha hofu ya BWANA ikawaangukia watu, nao wakatoka kama mtu mmoja.
”Kisha watu wakamwambia Samweli, “Ni nani yule aliyeuliza, ‘Je, Sauli atatawala juu yetu?’ Tuletee hawa watu, nasi tutawaua.”
”Kwa hiyo watu wote wakaenda Gilgali na kumthibitisha Sauli kuwa mfalme mbele za BWANA. Huko wakatoa dhabihu za sadaka za amani mbele za BWANA, naye Sauli na Waisraeli wote wakafanya karamu kubwa.
”“Lakini mlipomwona yule Nahashi mfalme wa Waamoni anakuja dhidi yenu, mliniambia, ‘Hapana, tunataka mfalme atutawale,’ hata ingawa BWANA Mungu wenu alikuwa mfalme wenu. Sasa huyu hapa ndiye mfalme mliyemchagua, yule mliyeomba; tazameni, BWANA amemweka mfalme juu yenu. Kama mkimcha BWANA na kumtumikia na kumtii nanyi msipoasi dhidi ya amri zake, ninyi pamoja na mfalme anayetawala juu yenu mkimfuata BWANA, Mungu wenu, mambo yatakuwa mema kwenu! Lakini kama hamkumtii BWANA, nanyi kama mkiasi dhidi ya amri zake, mkono wake utakuwa dhidi yenu, kama ulivyokuwa dhidi ya baba zenu.
”Watu wote wakamwambia Samweli, “Mwombe BWANA Mungu wako kwa ajili ya watumishi wako, ili tusije tukafa, kwa kuwa tumeongeza uovu juu ya dhambi zetu nyingine kwa kuomba mfalme.” Samweli akajibu, “Msiogope, mmefanya uovu huu wote; hata hivyo msimwache BWANA, bali mtumikieni BWANA kwa moyo wenu wote.
”Hata hivyo mkiendelea kufanya uovu, ninyi na mfalme wenu mtafutiliwa mbali!”
”Akangoja kwa siku saba, muda uliowekwa na Samweli, lakini Samweli hakuja Gilgali, nao watu wa Sauli wakaanza kutawanyika. Basi akasema, “Nileteeni hapa sadaka ya kuteketezwa na sadaka za amani.” Naye Sauli akatoa sadaka ya kuteketezwa. Mara alipomaliza kutoa hiyo sadaka, Samweli akatokea, naye Sauli akaondoka kwenda kumlaki. Samweli akamwuliza, “Umefanya nini?” Sauli akajibu, “Nilipoona kwamba watu wanatawanyika, na kwamba hukuja wakati uliopangwa na kwamba Wafilisti walikuwa wakikusanyika huko Mikmashi, nikawaza, ‘Sasa Wafilisti watatelemka dhidi yangu huko Gilgali nami sijaomba kibali kwa BWANA.’ Hivyo nikalazimika kutoa sadaka ya kuteketezwa.” Samweli akasema, “Umetenda kwa upumbavu. Hukuyashika maagizo ya BWANA Mungu wako aliyokupa, kama ungelitii, angeudumisha ufalme wako juu ya Israeli kwa wakati wote. Lakini sasa ufalme wako hautadumu; BWANA amemtafuta mtu aupendezae moyo wake, na amemchagua awe kiongozi wa watu wake, kwa sababu hukuyatii maagizo ya BWANA.”
”Lakini Samweli akajibu: “Je, BWANA anafurahia sadaka za kuteketezwa na dhabihu kama vile kuitii sauti ya BWANA? Kutii ni bora zaidi kuliko dhabihu, nako kusikia ni bora kuliko mafuta ya kondoo dume. Kwa maana kuasi ni kama dhambi ya uaguzi, nao ukaidi ni kama uovu wa kuabudu sanamu. Kwa sababu umelikataa neno la BWANA, naye amekukataa wewe kuendelea kuwa mfalme.”
”Ndipo Sauli akamwambia Samweli, “Nimetenda dhambi. Nimevunja amri ya BWANA na maagizo yako. Niliwaogopa watu na kwa hiyo nikafanya walivyotaka. Sasa ninakusihi, usamehe dhambi yangu nawe urudi pamoja nami, ili nipate kumwabudu BWANA.” Lakini Samweli akamwambia, “Sitarudi pamoja nawe. Umelikataa neno la BWANA, nawe BWANA amekukataa wewe usiendelee kuwa mfalme juu ya Israeli!”
”Basi Samweli akachukua ile pembe ya mafuta na kumtia mafuta mbele ya ndugu zake, kuanzia siku ile na kuendelea Roho wa BWANA akaja juu ya Daudi kwa nguvu. Kisha Samweli akaenda zake Rama.
”Baada ya hilo, dhamiri ya Daudi ikataabika kwa kukata upindo wa joho la Sauli. Akawaambia watu wake, “BWANA na apishie mbali nisije nikafanya jambo kama hilo kwa bwana wangu, yeye ambaye ni mpakwa mafuta wa BWANA, au kuinua mkono wangu dhidi yake, kwani yeye ni mpakwa mafuta wa BWANA.” Kwa maneno haya Daudi akawaonya watu wake na hakuwaruhusu wamshambulie Sauli. Naye Sauli akaondoka pangoni na kwenda zake. Ndipo Daudi naye akatoka pangoni na kumwita Sauli akisema, “Mfalme, bwana wangu!” Sauli alipotazama nyuma, Daudi akainama na kusujudu uso wake mpaka nchi.
”Ninajua kwamba hakika utakuwa mfalme na ya kwamba ufalme wa Israeli utakuwa imara mikononi mwako. Sasa niapie kwa BWANA kwamba hutakatilia mbali uzao wangu wala kulifuta jina langu kutoka katika jamaa ya baba yangu.” Basi Daudi akamwapia Sauli. Kisha Sauli akarudi zake nyumbani, lakini Daudi na watu wake wakapanda kwenda ngomeni.
”Lakini Daudi akamwambia Abishai, “Usimwangamize! Ni nani awezaye kutia mkono juu ya mpakwa mafuta wa BWANA na asiwe na hatia?” Akasema, “Hakika kama vile BWANA aishivyo, BWANA mwenyewe atampiga, au wakati wake utafika, naye atakufa, au atakwenda vitani na kuangamia. Lakini Mungu na apishie mbali nisije nikainua mkono juu ya mpakwa mafuta wa BWANA. Sasa chukua huo mkuki na hilo gudulia la maji, vilivyo karibu na kichwa chake, tuondoke.” Hivyo Daudi akachukua huo mkuki na hilo gudulia la maji vilivyokuwa karibu na kichwa cha Sauli, nao wakaondoka. Hakuna ye yote aliyeona au kufahamu habari hii, wala hakuna hata mmoja aliyeamka usingizini. Wote walikuwa wamelala, kwa sababu BWANA alikuwa amewatia kwenye usingizi mzito.
”Daudi akamwuliza, “Kwa nini hukuogopa kuinua mkono wako ili kumwangamiza mpakwa mafuta wa BWANA?” Kisha Daudi akamwita mmoja wa watu wake na kumwambia, “Nenda ukamwue!” Kwa hiyo akampiga, naye akafa. Kwa maana Daudi alikuwa amemwambia, “Damu yako iwe juu ya kichwa chako mwenyewe. Kinywa chako mwenyewe kimeshuhudia dhidi yako uliposema, ‘Nilimwua mpakwa mafuta wa BWANA.’ ”
”Ndipo watu wa Yuda wakaja Hebroni, huko wakamtia Daudi mafuta awe mfalme juu ya nyumba ya Yuda. Daudi alipoambiwa kuwa ni watu wa Yabeshi-Gileadi waliomzika Sauli,
”Siku zako zitakapokwisha nawe ulale pamoja na baba zako, nitainua mzao wako aingie mahali pako, ambaye atatoka viunoni mwako, nami nitauimarisha ufalme wake. Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili ya Jina langu, nami nitaimarisha kiti cha enzi cha ufalme wake milele. Nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu. Atakapokosea nitamwadhibu kwa fimbo ya wanadamu, kwa adhabu ya kupigwa na wanadamu. Lakini upendo wangu kamwe hautaondolewa kwake, kama nilivyouondoa kwa Sauli, niliyemwondoa atoke mbele yako. Nyumba yako na ufalme wako utadumu milele mbele zangu, kiti chako cha enzi kitafanywa imara milele.’ ” Nathani akamwarifu Daudi maneno yote ya maono haya.
”Daudi akatawala Israeli yote, akitenda lililo haki na sawa kwa watu wake wote.
”Mungu wa Israeli alinena, mwamba wa Israeli akaniambia: ‘Mtu anatawala watu kwa haki, wakati anapotawala akiwa na hofu ya Mungu,
”Wakamwambia mfalme, “Nabii Nathani yuko hapa.” Kisha akaenda mbele ya mfalme na kumsujudia hadi uso wake ukagusa ardhi.
”Kuhani Sadoki akachukua pembe ya mafuta kutoka kwenye hema takatifu na kumtia Solomoni mafuta. Kisha wakapiga tarumbeta na watu wote wakapaza sauti wakisema, “Mfalme Solomoni aishi maisha marefu!” Na watu wote wakakwea wakimfuata, wakipiga filimbi na kushangilia sana, hata ardhi ikatikisika kwa ile sauti.
”Solomoni akaonyesha upendo wake kwa BWANA kwa kuenenda sawasawa na amri za Daudi baba yake, ila yeye alitoa dhabihu na kufukiza uvumba huko mahali pa juu. Mfalme akaenda Gibeoni kutoa dhabihu, kwa maana ndipo palipokuwa mahali maarufu zaidi, naye Solomoni akatoa sadaka elfu moja za kuteketezwa juu ya hiyo madhabahu.
”BWANA akamtokea Solomoni huko Gibeoni wakati wa usiku katika ndoto, naye Mungu akasema, “Omba lo lote utakalo nikupe.” Solomoni akajibu, “Umemfanyia mtumishi wako baba yangu Daudi fadhili nyingi, kwa kuwa alikuwa mwaminifu kwako na mwenye haki tena mnyofu wa moyo. Nawe umemzidishia fadhili hii kuu na umempa mwana wa kuketi kwenye kiti chake cha ufalme kama ilivyo leo. “Sasa, Ee BWANA Mungu wangu, umemfanya mtumishi wako mfalme baada ya baba yangu Daudi. Lakini mimi ni mtoto mdogo tu wala sijui jinsi ya kutekeleza wajibu wangu. Mtumishi wako yuko hapa miongoni mwa watu uliowachagua. Taifa kubwa, watu wengi wasioweza kuhesabika wala kutoa idadi yao. Hivyo mpe mtumishi wako moyo wa ufahamu kutawala watu wako na kupambanua kati ya mema na mabaya. Kwa maana ni nani awezaye kutawala watu wako hawa walio wengi?” Bwana akapendezwa kwamba Solomoni ameliomba jambo hili. Basi Mungu akamwambia, “Kwa kuwa umeomba neno hili na hukuomba maisha marefu au upate utajiri kwa nafsi yako, wala adui zako wafe, bali umeomba ufahamu katika kutoa haki, nitafanya lile uliloomba. Nitakupa moyo wa hekima na wa ufahamu, kiasi kwamba hajakuwepo mtu mwingine kama wewe wala kamwe hatakuwapo baada yako. Zaidi ya hayo, nitakupa yale ambayo hukuomba, yaani utajiri na heshima, ili kwamba maisha yako yote hapatakuwa na mtu kama wewe miongoni mwa wafalme. Nawe kama ukienenda katika njia zangu na kutii sheria na amri zangu kama baba yako Daudi alivyofanya, nitakupa maisha marefu.”
”Kisha Solomoni akasimama mbele ya madhabahu ya BWANA machoni pa kusanyiko lote la Israeli, akakunjua mikono yake kuelekea mbinguni na kusema: “Ee BWANA, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe mbinguni juu wala duniani chini, wewe unayetunza Agano lako la upendo pamoja na watumishi wanaodumu katika njia yako kwa moyo wote.
”Mfalme Solomoni alikuwa mkuu zaidi kwa utajiri na hekima kuliko wafalme wote wa dunia.
”Hata hivyo, Mfalme Solomoni akawapenda wanawake wengi wa kigeni zaidi, mbali na binti Farao: wanawake wa Wamoabu, Waamoni, Waedomu, Wasidoni na Wahiti. Wakitoka katika mataifa ambayo BWANA aliwaambia Waisraeli, “Msije mkaoana nao, kwa hakika wataigeuza mioyo yenu mgeukie miungu yao.” Hata hivyo, Solomoni akakaza kuwapenda. Alikuwa na wake 700 wa uzao wa kifalme na masuria 300, nao hao wake zake wakampotosha. Kadiri Solomoni alivyozidi kuzeeka, wake zake wakageuza moyo wake kuelekea miungu mingine, na moyo wake haukuwa mkamilifu kwa BWANA Mungu wake, kama ulivyokuwa moyo wa Daudi baba yake. Akafuata Ashtorethi mungu mke wa Wasidoni, na Moleki mungu aliyekuwa chukizo la Waamoni. Kwa hiyo Solomoni akafanya uovu machoni pa BWANA; hakumfuata BWANA kikamilifu kama alivyofanya Daudi baba yake. Kwenye kilima mashariki mwa Yerusalemu, Solomoni akajenga mahali pa juu kwa ajili ya Kemoshi chukizo la Wamoabu, na kwa Moleki mungu chukizo la Waamoni. Akafanya hivyo kwa wake zake wote wa kigeni, ambao walifukiza uvumba na kutoa dhabihu kwa miungu yao.
”BWANA akamkasirikia Solomoni kwa sababu moyo wake uligeuka mbali na BWANA, Mungu wa Israeli, ambaye alikuwa amemtokea mara mbili. Ingawa alikuwa amemkataza Solomoni kufuata miungu mingine, Solomoni hakutii amri ya BWANA. Kwa hiyo BWANA akamwambia Solomoni, “Kwa kuwa hii ndiyo hali yako na hukushika Agano langu na sheria zangu nilizokuamuru, hakika nitaurarua ufalme kutoka kwako na kumpa mmoja wa walio chini yako.
”Siku tatu baadaye, Yeroboamu na watu wote wakamrudia Rehoboamu, kama mfalme alivyokuwa amesema, “Rudini kwangu baada ya siku tatu.” Mfalme akawajibu watu kwa ukatili. Akikataa shauri alilopewa na wazee, akafuata shauri la vijana wa rika lake na kusema, “Baba yangu alifanya nira yenu kuwa nzito, mimi nitaifanya kuwa nzito zaidi. Baba yangu aliwachapa kwa mijeledi, mimi nitawachapa kwa nge.”
”Yeroboamu akajenga madhabahu mahali pa juu pa kuabudia miungu na kuwateua makuhani kutoka watu wa aina zote, ijapokuwa hawakuwa Walawi. Akaweka sikukuu katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa nane, kama sikukuu iliyokuwa ikifanyika huko Yuda na akatoa dhabihu juu ya madhabahu. Akafanya hivyo huko Betheli akitoa dhabihu kwa ndama alizotengeneza. Huko Betheli, akawaweka makuhani pia katika sehemu za juu za kuabudia miungu alizotengeneza.
”Mfalme Yeroboamu aliposikia kile mtu wa Mungu alichosema, alipopiga kelele dhidi ya madhabahu huko Betheli, akanyoosha mkono wake kutoka madhabahuni na kusema, “Mkamate!” Lakini mkono aliokuwa ameunyoosha kumwelekea yule mtu ukasinyaa na kubaki hapo hapo, kiasi kwamba hakuweza kuurudisha. Pia, madhabahu ilipasuka na majivu yakamwagika sawasawa na ishara iliyotolewa na mtu wa Mungu kwa neno la BWANA.
”Hata baada ya haya, Yeroboamu hakubadili njia zake mbaya, lakini mara nyingine tena akaweka makuhani kwa ajili ya mahali pa juu pa kuabudia miungu kutoka watu wa aina zote. Ye yote aliyetaka kuwa kuhani alimweka wakfu kwa ajili ya mahali pa juu pa kuabudia miungu. Hii ilikuwa ndiyo dhambi ya nyumba ya Yeroboamu ambayo iliisababishia kuanguka na kuangamia kwake hadi kutoweka kwenye uso wa dunia.
”Umefanya maovu mengi kuliko wote walio kutangulia. Umejitengenezea miungu mingine, sanamu za chuma, umenighadhibisha na kunitupa nyuma yako. “ ‘Kwa sababu ya hili, nitaleta maafa juu ya nyumba ya Yeroboamu. Nitakatilia mbali kutoka kwa Yeroboamu kila mzaliwa wa mwisho wa kiume katika Israeli, mtumwa au mtu huru. Nitachoma nyumba ya Yeroboamu mpaka iteketee yote kama mtu achomaye kinyesi.
”Naye atawaacha Israeli kwa ajili ya makosa ya Yeroboamu aliyoyatenda na kusababisha Israeli kuyatenda.”
”Katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Yeroboamu mwana wa Nebati, Abiya akawa mfalme wa Yuda, naye akatawala katika Yerusalemu miaka mitatu. Mama yake aliitwa Maaka binti Abishalomu. Alitenda dhambi zote baba yake alizotenda kabla yake; moyo wake haukuwa mkamilifu kwa BWANA Mungu wake kama moyo wa Daudi baba yake ulivyokuwa.
”Asa akatenda yaliyo mema machoni mwa BWANA, kama alivyokuwa ametenda Daudi baba yake. Akawafukuza mahanithi wa mahali pa kuabudia miungu kutoka katika nchi na kuondoa sanamu zote ambazo baba zake walikuwa wametengeneza. Hata akamwondoa bibi yake Maaka kwenye nafasi yake kama mama malkia, kwa sababu alikuwa ametengeneza nguzo ya Ashera ya kuchukiza. Asa akakatakata hiyo nguzo na kuiteketeza kwa moto kwenye Bonde la Kidroni. Japokuwa hakuondoa mahali pa juu pa kuabudia miungu, moyo wa Asa ulikuwa umejiweka kwa BWANA kikamilifu maisha yake yote.
”Nadabu mwana wa Yeroboamu akawa mfalme wa Israeli katika mwaka wa pili wa utawala wa Mfalme Asa wa Yuda, naye akatawala Israeli kwa miaka miwili. Akafanya maovu machoni pa BWANA, akienenda katika njia za baba yake na katika dhambi yake, ambayo alisababisha Israeli kuifanya.
”kwa sababu ya dhambi alizokuwa amezitenda Yeroboamu na kusababisha Israeli kuzitenda, tena kwa sababu alimkasirisha BWANA, Mungu wa Israeli.
”Katika mwaka wa tatu wa kutawala kwake Asa mfalme wa Yuda, Baasha mwana wa Ahiya akawa mfalme wa Israeli yote huko Tirza, naye akatawala kwa miaka ishirini na minne. Akatenda maovu machoni pa BWANA, akienenda katika njia za Yeroboamu na dhambi yake, ambayo alikuwa amesababisha Israeli kuitenda.
”Mbwa watawala watu wa Baasha watakaofia mjini na ndege wa angani watajilisha kwa wale watakaofia mashambani.”
”Zaidi ya hayo, neno la BWANA likamjia Baasha pamoja na nyumba yake kupitia kwa Yehu mwana wa Hanani, kwa sababu ya maovu yote aliyokuwa ametenda machoni pa BWANA, akamkasirisha kwa mambo aliyotenda, na kuwa kama nyumba ya Yeroboamu, na pia kwa sababu aliiangamiza.
”Hivyo Zimri akaangamiza jamaa yote ya Baasha, kulingana na neno la BWANA lililonenwa dhidi ya Baasha kupitia nabii Yehu: kwa sababu ya dhambi zote Baasha na mwanawe Ela walizokuwa wametenda na wakasababisha Israeli kuzitenda, basi wakamkasirisha BWANA, Mungu wa Israeli kwa sanamu zao zisizofaa.
”Wakati Zimri alipoona kuwa mji umechukuliwa, alikwenda ndani ya ngome ya jumba la kifalme na kulichoma moto jumba la kifalme na kujiteketeza ndani yake. Kwa hiyo akafa, kwa sababu ya dhambi alizofanya, akitenda maovu machoni pa BWANA na kuenenda katika njia za Yeroboamu na katika dhambi alizofanya na kusababisha Israeli kuzifanya.
”Lakini Omri akatenda maovu machoni pa BWANA na kutenda dhambi kuliko wote waliomtangulia. Akaenenda katika njia zote za Yeroboamu mwana wa Nebati na katika dhambi zake, ambazo alisababisha Israeli kutenda, hivyo basi wakamkasirisha BWANA, Mungu wa Israeli kwa sanamu zao zisizofaa.
”Ahabu mwana wa Omri akafanya maovu zaidi machoni mwa BWANA kuliko ye yote aliyewatangulia. Kama vile haikutosha kuishi kama Yeroboamu mwana wa Nebati, akamwoa Yezebeli binti wa Ethbaali, mfalme wa Wasidoni, naye akaanza kumtumikia Baali na kumwabudu. Akajenga madhabahu kwa ajili ya Baali katika hekalu la Baali lile alilolijenga huko Samaria. Pia Ahabu akatengeneza nguzo ya Ashera na kufanya mengi ili kumkasirisha BWANA, Mungu wa Israeli, kuliko walivyofanya wafalme wote wa Israeli waliomtangulia.
”Wakati Yezebeli alipokuwa akiwaua manabii wa BWANA, Obadia alikuwa amewachukua manabii mia moja na kuwaficha katika mapango mawili, hamsini kwenye kila moja na akawa anawapatia chakula na maji.)
”Alipomwona Eliya akamwambia, “Je, ni wewe, mtaabishaji wa Israeli?” Eliya akamjibu, “Mimi sijaitaabisha Israeli. Lakini wewe na jamaa ya baba yako ndio mnaofanya hivyo. Mmeziacha amri za BWANA na mkafuata Mabaali. Sasa waite watu kutoka Israeli yote tukutane nao juu ya Mlima Karmeli. Nawe uwalete hao manabii wa Baali mia nne na hamsini na hao manabii mia nne wa Ashera, walao chakula mezani mwa Yezebeli.”
”Ahabu akamwambia Yezebeli kila kitu Eliya alichokuwa amefanya na jinsi alivyowaua manabii wote kwa upanga. Hivyo Yezebeli akamtuma mjumbe kwa Eliya, kusema, “Hao miungu initendee hivyo na kuzidi, kama kufikia kesho wakati kama huu sitaifanya roho yako kama mmojawapo wa hao manabii.”
”Kisha neno la BWANA likamjia Eliya, Mtishbi: “Shuka ukakutane na Ahabu mfalme wa Israeli, anayetawala Samaria. Sasa yuko katika shamba la mizabibu la Nabothi, ambapo amekwenda alimiliki. Umwambie, ‘Hivi ndivyo BWANA asemavyo: Je, hujamwua mtu na kuitwaa mali yake?’ Kisha umwambie, ‘Hivi ndivyo asemavyo BWANA: Mahali ambapo mbwa walilamba damu ya Nabothi, mbwa watailamba damu yako, naam, yako wewe!’ ” Ahabu akamwambia Eliya, “Kwa hiyo umenipata, wewe adui yangu!” Akajibu, “Ndiyo, nimekupata. Kwa sababu umejiuza mwenyewe kufanya uovu mbele ya macho ya BWANA. ‘Nitaleta maafa juu yako. Nitaangamiza uzao wako na kukatilia mbali kutoka kwa Ahabu kila mzaliwa wa mwisho wa kiume katika Israeli, wa mtumwa au wa mtu huru. Nitaifanya nyumba yako kama ile ya Yeroboamu mwana wa Nebati na ile ya Baasha mwana wa Ahia, kwa sababu umenighadhibisha kwa kuwa umesababisha Israeli kutenda dhambi.’ “Pia kwa habari ya Yezebeli BWANA anasema, ‘Mbwa watamla Yezebeli karibu na ukuta wa Yezreeli.’ “Mbwa watawala wale wa nyumba ya Ahabu watakaofia mjini, nao wale watakaofia mashambani wataliwa na ndege wa angani.”
”(Hapajapata kamwe kuwa na mtu kama Ahabu, aliyejiuza mwenyewe kutenda uovu machoni mwa BWANA, akiwa anachochewa na Yezebeli mkewe. Alitenda kwa uovu sana katika kuabudu sanamu, kama wale Waamori ambao BWANA aliowafukuza mbele ya Israeli.) Ahabu aliposikia maneno haya, akararua nguo zake, akavaa nguo za gunia na kufunga. Akalala na kujifunika nguo za gunia na kwenda kwa unyenyekevu. Ndipo neno la BWANA lilipomjia Eliya Mtishbi kusema, “Umeona jinsi Ahabu alivyojinyenyekeza mbele zangu? Kwa kuwa amejishusha mwenyewe, sitaleta maafa haya wakati akiwa hai, lakini nitayaleta juu ya nyumba yake katika siku za mwanawe.”
”Wakasafisha lile gari la vita katika bwawa la Samaria (mahali makahaba walipooga), na mbwa wakalamba damu yake, sawasawa na neno la BWANA lilivyokuwa limesema. Kwa matukio mengine ya utawala wa Ahabu, pamoja na yote aliyoyafanya, jumba la kifalme alilojenga na kunakishiwa kwa pembe za ndovu, nayo miji aliyoijengea maboma, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Israeli?
”Katika kila jambo alienenda katika njia za Asa baba yake wala hakwenda kinyume chake, akafanya yaliyo mema machoni pa BWANA. Hata hivyo mahali pa juu pa kuabudia palikuwa hapakuondolewa na watu waliendelea kutoa dhabihu na kufukiza uvumba huko. Yehoshafati pia alikuwa na amani na mfalme wa Israeli.
”Ahazia mwana wa Ahabu akawa mfalme wa Israeli huko Samaria katika mwaka wa kumi na saba wa Yehoshafati mfalme wa Yuda, naye alitawala katika Israeli kwa miaka miwili. Akafanya maovu machoni mwa BWANA kwa sababu alienenda katika njia za baba yake na mama yake na katika njia za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambaye alisababisha Israeli itende dhambi. Alimtumikia na kumwabudu Baali na kumghadhibisha BWANA, Mungu wa Israeli, kama vile baba yake alivyokuwa amefanya.
”Akamwambia mfalme, “Hili ndilo asemalo BWANA: Je, ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israeli wa wewe kumwuliza ndiyo maana ukatuma wajumbe kuuliza Baal-Zebubu, aliye mungu wa Ekroni? Kwa sababu umefanya hili, kamwe hutaondoka kwenye kitanda unachokilalia, Hakika utakufa!” Hivyo akafa, sawasawa na lile neno la BWANA ambalo Eliya alikuwa amesema. Kwa kuwa Ahazia hakuwa na mwana, Yoramu akaingia mahali pake kuwa mfalme katika mwaka wa pili wa Yehoramu mwana wa Yehoshafati mfalme wa Yuda.
”Yehoramu mwana wa Ahabu akawa mfalme wa Israeli katika Samaria mwaka wa kumi na nane wa kutawala kwake Yehoshafati mfalme wa Yuda, naye akatawala kwa miaka kumi na miwili. Akafanya maovu machoni pa BWANA, lakini sio kama baba yake na mama yake walivyokuwa wamefanya. Akaondoa nguzo ya ibada ya Baali ambayo baba yake alikuwa ameitengeneza. Hata hivyo akashikamana na dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambazo alisababisha Israeli kuzitenda, wala hakuziacha.
”Katika mwaka wa tano wa Yoramu mwana wa Ahabu mfalme wa Israeli, wakati huo Yehoshafati akiwa mfalme wa Yuda, Yehoramu mwana wa Yehoshafati akaanza kutawala kama mfalme wa Yuda. Alikuwa na umri wa miaka thelathini na miwili alipoanza kutawala, akatawala huko Yerusalemu kwa miaka minane. Akaziendea njia za wafalme wa Israeli, kama nyumba ya Ahabu ilivyokuwa imefanya, kwa kuwa alimwoa binti wa Ahabu. Akatenda maovu machoni pa BWANA.
”Ahazia alikuwa na umri wa miaka ishirini na miwili wakati alipokuwa mfalme, naye akatawala katika Yerusalemu kwa mwaka mmoja. Jina la mama yake ni Athalia, mjukuu wa Omri mfalme wa Israeli. Akaziendea njia za nyumba ya Ahabu na kutenda maovu machoni pa BWANA, kama nyumba ya Ahabu ilivyokuwa imefanya, kwa kuwa alikuwa ameoa kutoka nyumba ya Ahabu.
”Wakati alipofika, akawakuta maafisa wa jeshi wameketi pamoja, akasema, “Nina ujumbe wako, ee jemadari.” Yehu akauliza, “Kwa yupi mmoja wetu?” Akamjibu, “Kwako wewe jemadari.” Yehu akainuka na kuingia ndani ya nyumba. Ndipo yule nabii akamimina mafuta juu ya kichwa cha Yehu na kutangaza kwamba, “Hivi ndivyo asemavyo BWANA, Mungu wa Israeli: ‘Ninakutia mafuta uwe mfalme juu ya watu wa BWANA, Mungu wa Israeli. Inakupasa uiangamize nyumba ya bwana wako Ahabu, nami nitalipiza kisasi juu ya damu ya watumishi wangu manabii na damu ya watumishi wote wa BWANA iliyomwagwa na Yezebeli. Nyumba yote ya Ahabu itaangamia. Nitamkatilia mbali kila mzaliwa wa kiume wa mwisho wa Ahabu katika Israeli, mtumwa ama aliye huru.
”Kisha Yehu akaenda Yezreeli. Yezebeli aliposikia habari hii, akayapaka macho yake rangi, akatengeneza nywele zake na kutazama nje dirishani. Yehu alipokuwa akiingia langoni, Yezebeli akasema, “Je, umekuja kwa amani, Zimri, wewe mwuaji wa bwana wako?” Yehu akaangalia juu dirishani na kuita, “Je, ni nani aliye upande wangu? Ni nani?” Matowashi wawili au watatu wakamtazama. Yehu akasema, “Mtupeni huyo mwanamke chini!” Kwa hiyo wakamtupa chini, sehemu ya damu yake ikatapanyika ukutani na nyingine juu ya farasi walipokuwa wakimkanyaga kwa miguu yao. Yehu akaingia ndani akala na akanywa. Akasema, “Mshughulikieni huyo mwanamke aliyelaaniwa, mzikeni, kwa sababu alikuwa binti wa mfalme.” Lakini walipotoka kwenda ili kumzika, hawakukuta kitu cho chote isipokuwa fuvu la kichwa, miguu yake na mikono. Wakarudi na kumwambia Yehu, ambaye alisema, “Hili ndilo neno la BWANA alilosema kupitia kinywa cha mtumishi wake Eliya Mtishbi, kusema, Katika kiwanja cha Yezreeli mbwa wataila nyama ya Yezebeli. Maiti ya Yezebeli itakuwa kama mavi shambani katika uwanja wa Yezreeli, kwamba hakutakuwepo mtu atakayeweza kusema, ‘Huyu ndiye Yezebeli.’ ”
”Kisha Yehu akawaleta watu wote pamoja na kuwaambia, “Ahabu alimtumikia Baali kidogo, Yehu atamtumikia zaidi. Sasa waiteni manabii wote wa Baali, watumishi wake wote na makuhani wake wote. Hakikisheni kwamba hakuna hata mmoja atakayekosekana, kwa sababu ninakwenda kutoa kafara kubwa sana kwa Baali. Ye yote atakayeshindwa kuja hataendelea kuishi.” Lakini Yehu alifanya hivyo kwa hila ili apate kuwaangamiza watumishi wote wa Baali. Yehu akasema, “Itisheni kusanyiko kwa heshima ya Baali.” Basi wakatangaza jambo hilo. Kisha akapeleka ujumbe katika Israeli yote na watumishi wote wa Baali wakaja, hakuna hata mmoja ambaye hakufika. Wakasongana ndani ya hekalu la Baali mpaka likajaa tangu mwanzo hadi mwisho wake. Naye Yehu akamwambia yule aliyekuwa mtunza chumba cha mavazi, “Leta majoho kwa ajili ya watumishi wote wa Baali.” Basi akawaletea majoho. Kisha Yehu na Yehonadabu mwana wa Rekabu wakaingia ndani ya hekalu la Baali. Yehu akawaambia watumishi wa Baali, “Tazameni kila mahali mhakikishe kwamba hakuna hata mtumishi mmoja wa BWANA aliye hapa pamoja nanyi, wawe ni watumishi wa Baali tu.” Kwa hiyo wakaingia ndani ili kutoa kafara na sadaka ya kuteketezwa. Wakati huu, Yehu alikuwa amewaweka watu wake themanini akiwa amewapa onyo kwamba, “Ikiwa mmoja wenu atamwachia mtu ye yote ninayemweka mikononi mwake atoroke, itakuwa uhai wako kwa uhai wake.”
”Wakabomoa ile nguzo ya kuabudiwa ya Baali pamoja na hekalu la Baali, nao watu wakapafanya kuwa choo hadi leo.
”Lakini Yehu hakuwa mwangalifu kushika sheria za BWANA, Mungu wa Israeli, kwa moyo wake wote. Hakuziacha dhambi za Yeroboamu, ambazo alikuwa amesababisha Israeli kuzitenda.
”Akaangalia na tazama alikuwako mfalme, akiwa amesimama karibu na nguzo, kama ilivyokuwa desturi. Maafisa na wapiga tarumbeta walikuwa pembeni mwa mfalme, nao watu wote wa nchi walikuwa wakifurahi na kupiga tarumbeta. Kisha Athalia akararua majoho yake na kupiga kelele, “Uhaini! Uhaini!”
”Yoashi akafanya yaliyo mema machoni pa Mungu miaka yote ambayo Yehoyada kuhani alikuwa akimwelekeza. Hata hivyo mahali pa juu pa kuabudia hapakuondolewa, watu waliendelea kutoa kafara na kufukiza uvumba huko.
”Katika mwaka wa ishirini na tatu wa kutawala kwake Yoashi mwana wa Ahazia mfalme wa Yuda, Yehoahazi mwana wa Yehu alianza kutawala Israeli katika Samaria, naye akatawala miaka kumi na saba. Akafanya maovu machoni pa BWANA kwa kufuata dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambazo alikuwa amesababisha Israeli kuzitenda na wala hakuziacha.
”Katika mwaka wa thelathini na saba wa kutawala kwake Yoashi mfalme wa Yuda, Yehoashi mwana wa Yehoahazi alianza kutawala Israeli huko Samaria, naye akatawala miaka kumi na sita. Alifanya maovu machoni pa BWANA na hakuacha dhambi yo yote kati ya zile za Yeroboamu mwana wa Nebati ambazo alikuwa amesababisha Israeli kuzitenda, aliendelea kuzitenda.
”Katika mwaka wa pili wa kutawala kwake Yehoashi mwana wa Yehoahazi mfalme wa Israeli, Amazia mwana wa Yoashi mfalme wa Yuda alianza kutawala. Alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipokuwa mfalme, naye akatawala katika Yerusalemu miaka ishirini na tisa. Jina la mama yake aliitwa Yehoadani, kutoka Yerusalemu. Akatenda yaliyo mema machoni pa BWANA, lakini sio kama Daudi baba yake alivyokuwa amefanya. Katika kila kitu alifuata mfano wa Yoashi baba yake. Hata hivyo mahali pa juu pa kuabudia miungu hapakuondolewa; watu waliendelea kutoa kafara na kufukiza uvumba huko.
”Katika mwaka wa kumi na tano wa kutawala kwake Amazia mwana wa Yoashi mfalme wa Yuda, Yeroboamu mwana wa Yehoashi mfalme wa Israeli alianza kutawala huko Samaria, naye akatawala kwa miaka arobaini na mmoja. Akafanya maovu machoni pa BWANA na hakuacha dhambi hata moja ya Yeroboamu mwana wa Nebati, ambazo alikuwa amesababisha Israeli kuzitenda.
”Katika mwaka wa ishirini na saba wa kutawala kwake Yeroboamu mfalme wa Israeli Azaria mwana wa Amazia mfalme wa Yuda alianza kutawala. Alikuwa na umri wa miaka kumi na sita alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka hamsini na miwili. Jina la mama yake aliitwa Yekolia kutoka Yerusalemu. Akatenda yaliyo mema machoni pa BWANA, kama Amazia baba yake alivyofanya. Hata hivyo, mahali pa juu pa kuabudia miungu hapakuondolewa; watu waliendelea kutoa kafara na kufukiza uvumba huko. BWANA akampiga mfalme kwa ukoma mpaka siku aliyokufa, naye aliishi katika nyumba iliyotengwa peke yake. Yothamu mwana wa mfalme akawa msimamizi wa jumba la kifalme na akawatawala watu wa nchi.
”Katika mwaka wa thelathini na nane wa kutawala kwake Azaria mfalme wa Yuda, Zekaria mwana wa Yeroboamu akawa mfalme wa Israeli katika Samaria, naye akatawala miezi sita. Akafanya maovu machoni pa BWANA, kama baba zake walivyofanya. Hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati ambazo alisababisha Israeli kuzitenda.
”Shalumu mwana wa Yabeshi akawa mfalme katika mwaka wa thelathini na tisa wa Uzia mfalme wa Yuda, naye akatawala katika Samaria kwa mwezi mmoja. Kisha Menahemu mwana wa Gadi akaenda kutoka Tirza mpaka Samaria. Akamshambulia Shalumu mwana Yabeshi huko Samaria, akamwua na kuingia mahali pake kuwa mfalme.
”Katika mwaka wa thelathini na tisa wa kutawala kwake Azaria mfalme wa Yuda, Menahemu mwana wa Gadi akawa mfalme wa Israeli na alitawala huko Samaria kwa miaka kumi. Akatenda maovu machoni pa BWANA. Katika wakati wa utawala wake wote hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati ambazo alisababisha Israeli kuzitenda.
”Katika mwaka wa hamsini wa kutawala kwake Azaria mfalme wa Yuda, Pekahia mwana wa Menahemu akawa mfalme wa Israeli huko Samaria, akatawala miaka miwili. Pekahia akafanya uovu machoni pa BWANA. Hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambazo alisababisha Israeli kuzitenda.
”Katika mwaka wa hamsini na mbili wa kutawala kwake Azaria mfalme wa Yuda, Peka mwana wa Remalia akawa mfalme wa Israeli huko Samaria, naye alitawala miaka ishirini. Akafanya maovu machoni pa BWANA. Hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambazo alisababisha Israeli kuzitenda.
”Katika mwaka wa pili wa kutawala kwake Peka mwana wa Remalia mfalme wa Israeli, Yothamu mwana wa Uzia mfalme wa Yuda alianza kutawala. Alikuwa na miaka ishirini na mitano wakati alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na sita. Jina la mama yake aliitwa Yerusha binti Zadoki. Akafanya yaliyo mema machoni pa BWANA, kama Uzia baba yake alivyokuwa amefanya. Hata hivyo, mahali pa juu hapakuondolewa; watu waliendelea kutoa kafara na kufukiza uvumba huko. Yothamu akajenga upya Lango la Juu la Hekalu la BWANA.
”Katika mwaka wa kumi na saba wa kutawala kwake Peka mwana wa Remalia, Ahazi mwana wa Yothamu mfalme wa Yuda alianza kutawala. Ahazi alikuwa na miaka ishirini alipoanza kutawala kama mfalme, naye akatawala katika Yerusalemu kwa miaka kumi na sita. Tofauti na Daudi baba yake, hakufanya yaliyo sawa mbele ya macho ya BWANA, Mungu wake. Akaenenda katika njia za wafalme wa Israeli na hata kumtoa mwanawe kafara katika moto, akafuata njia za machukizo za mataifa ambayo BWANA alikuwa ameyafukuza mbele ya Waisraeli. Akatoa kafara na kufukiza uvumba katika mahali pa juu pa kuabudia miungu, juu ya vilele vya vilima, na chini ya kila mti uliotanda.
”Katika mwaka wa kumi na mbili wa kutawala kwake Ahazi mfalme wa Yuda, Hoshea mwana wa Ela akawa mfalme wa Israeli katika Samaria, akatawala kwa miaka tisa. Akafanya maovu machoni pa BWANA, lakini si kama wafalme wengine wa Israeli waliomtangulia.
”Katika mwaka wa tatu wa kutawala kwake Hoshea mwana wa Ela mfalme wa Israeli, Hezekia mwana wa Ahazi mfalme wa Yuda alianza kutawala. Alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, naye akatawala katika Yerusalemu kwa miaka ishirini na tisa. Jina la mama yake aliitwa Abiya binti Zekaria. Akafanya yaliyo mema machoni pa BWANA, kama Daudi baba yake alivyofanya. Akapaondoa mahali pa juu pa kuabudia miungu, akazivunja sanamu, akakatakata nguzo za Ashera. Akavunja vipande vipande ile nyoka ya shaba Mose aliyotengeneza, kwa kuwa hadi siku hizo wana wa Israeli walikuwa wanaifukizia uvumba (nayo ilikuwa ikiitwa Nehushtani). Hezekia aliweka tumaini lake kwa BWANA, Mungu wa Israeli. Hapakuwepo na mfalme mwingine wa kufanana naye miongoni mwa wafalme wa Yuda, kabla yake au baada yake. Alishikamana na BWANA kwa bidii wala hakuacha kumfuata; alishika amri ambazo BWANA alikuwa amempa Mose.
”Basi Hezekia mfalme wa Yuda akamtumia ujumbe mfalme wa Ashuru huko Lakishi akisema: “Nimefanya makosa. Ondoka katika nchi yangu, nami nitakulipa cho chote unachokitaka kwangu.” Mfalme wa Ashuru akamtoza Hezekia mfalme wa Yuda talanta 300 za fedha na talanta thelathini za dhahabu. Basi Hezekia akampa fedha yote iliyopatikana ndani ya Hekalu la BWANA na katika hazina ya jumba la kifalme. Wakati huu Hezekia mfalme wa Yuda akabandua dhahabu yote iliyokuwa imefunika milango na miimo ya Hekalu la BWANA, akampa mfalme wa Ashuru.
”Hezekia akawapokea wale wajumbe na kuwaonyesha vitu vyote vile vilivyokuwa katika ghala zake, yaani fedha, dhahabu, vikolezo na mafuta safi, ghala la silaha na kila kitu kilichokuwa katika hazina zake. Hapakuwa na kitu cho chote katika jumba lake la kifalme au katika ufalme wake wote ambacho Hezekia hakuwaonyesha. Kisha nabii Isaya akaenda kwa Mfalme Hezekia na kumwuliza, “Hao watu wamesema nini na wametoka wapi?” Hezekia akajibu, “Wametoka nchi ya mbali. Wametoka Babeli.” Nabii akauliza, “Wameona nini katika jumba lako la kifalme?” Hezekia akasema, “Wameona kila kitu katika jumba langu la kifalme. Hakuna kitu katika hazina yangu ambacho sikuwaonyesha.” Kisha Isaya akamwambia Hezekia, “Sikia neno la BWANA: Hakika wakati utakuja ambao kila kitu katika jumba lako la kifalme na vyote vile ambavyo baba zako waliweka akiba mpaka siku hii ya leo, vitachukuliwa kwenda Babeli. Hakuna cho chote kitakachobaki, asema BWANA.
”Manase alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili alipoanza kutawala, akatawala katika Yerusalemu kwa miaka hamsini na mitano. Jina la mama yake aliitwa Hefsiba. Akafanya maovu machoni pa BWANA, akafuata desturi za machukizo za mataifa ambayo BWANA aliyafukuza mbele ya Waisraeli. Akajenga tena mahali pa juu pa kuabudia miungu ambapo baba yake Hezekia alikuwa amepabomoa. Pia akasimamisha madhabahu za Baali na kutengeneza nguzo ya Ashera, kama Ahabu mfalme wa Israeli alivyofanya. Akasujudia na kuabudu jeshi lote la angani. Akajenga madhabahu ndani ya Hekalu la BWANA, ambalo BWANA alikuwa amesema, “Katika Yerusalemu nitaliweka Jina langu.” Katika nyua zote mbili za Hekalu la BWANA, akajenga madhabahu kwa ajili ya jeshi lote la angani. Akamtoa kafara mwanawe mwenyewe katika moto, akafanya uchawi na uaguzi, na akataka shauri kwa wapiga ramli na kwa mizimu. Akafanya maovu mengi sana machoni mwa BWANA na kumghadhibisha. Akachukua nguzo ya Ashera aliyoitengeneza na kuiweka ndani ya Hekalu, ambalo BWANA alikuwa amemwambia Daudi na Solomoni mwanawe hivi, “Katika Hekalu hili na katika Yerusalemu, ambavyo nimevichagua kutoka katika makabila yote ya Israeli, nitaliweka Jina langu milele.
”Zaidi ya hayo, Manase pia alimwaga damu nyingi isiyo na hatia kwamba aliijaza Yerusalemu kutoka mwanzo hadi mwisho, mbali na dhambi ambayo alikuwa amesababisha Yuda kufanya, hivyo kwamba wakatenda maovu machoni pa BWANA.
”Amoni alikuwa na miaka ishirini na miwili alipoanza kutawala, akatawala katika Yerusalemu kwa miaka miwili. Jina la mama yake aliitwa Meshulemethi binti Haruzi, alitoka Yotba. Akatenda maovu machoni mwa BWANA, kama baba yake Manase alivyofanya. Akaenenda katika njia zote za baba yake, akaabudu sanamu ambazo baba yake aliziabudu na kuzisujudia. Akamwacha BWANA, Mungu wa baba zake, wala hakuenenda katika njia za BWANA.
”Yosia alikuwa na miaka minane alipoanza kutawala, naye akatawala katika Yerusalemu miaka thelathini na mmoja. Jina la mama yake aliitwa Yedida binti Adaya, kutoka Boskathi. Akafanya yaliyo mema machoni pa BWANA na kuenenda katika njia zote za Daudi baba yake, bila kugeuka upande wa kuume wala wa kushoto.
”Hilkia kuhani mkuu akamwambia Shafani mwandishi, “Nimekipata Kitabu cha Torati ndani ya Hekalu la BWANA.” Akampa Shafani, ambaye alikisoma. Kisha Shafani mwandishi akamwendea mfalme na kumpa taarifa akisema: “Maafisa wako wametoa ile fedha ambayo ilikuwa ndani ya Hekalu la BWANA na imekabidhiwa mikononi mwa wasimamizi wa marekebisho ya Hekalu.” Ndipo Shafani mwandishi akampasha mfalme habari kwamba: “Hilkia kuhani amenipa kitabu hiki.” Naye Shafani akakisoma kile kitabu mbele ya mfalme. Mfalme aliposikia maneno ya kile kitabu cha Torati, akararua majoho yake. Akatoa amri hizi kwa Hilkia kuhani, Ahikamu mwana wa Shafani, Akbori mwana wa Mikaya, Shafani mwandishi na Asaia mhudumu wa mfalme: “Nendeni na mkaulize kwa BWANA kwa ajili yangu, na kwa ajili ya watu na Yuda wote kuhusu kile kilichoandikwa ndani ya kitabu hiki ambacho kimepatikana. Hasira ya BWANA ni kubwa inayowaka dhidi yetu kwa sababu baba zetu hawakuyatii maneno ya kitabu hiki, hawajatenda kulingana na yale yote yaliyoandikwa humo kutuhusu sisi.”
”Alizivunja madhabahu ambazo wafalme wa Yuda walikuwa wamezijenga kwenye paa la ghorofa ya Ahazi, pia madhabahu alizokuwa amezijenga Manase katika nyua mbili za Hekalu la BWANA. Akaziondoa huko, akazivunja vipande vipande na kutupa hicho kifusi katika Bonde la Kidroni. Mfalme pia akapaharibu mahali pa juu pa kuabudia miungu palipokuwa mashariki ya Yerusalemu upande wa kusini wa Kilima cha Uharibifu, pale ambapo Solomoni mfalme wa Israeli alikuwa amejenga kwa ajili ya Ashtorethi mungu mke aliye chukizo la Wasidoni, kwa ajili ya Kemoshi yule mungu chukizo la Wamoabu, na kwa ajili ya Moleki mungu aliye chukizo la watu wa Amoni, pasifae tena kufanyia hizo ibada. Yosia akapasua yale mawe ya kuabudiwa na kuzikatakata nguzo za Ashera. Kisha akafunika hayo maeneo kwa mifupa ya wanadamu.
”Zaidi ya hayo, Yosia akawaondoa wapunga pepo, wanaoabudu mizimu, sanamu za kuagulia, sanamu za kuabudiwa na vitu vingine vyote vya machukizo vilivyoonekana katika Yuda na Yerusalemu. Haya aliyafanya ili kutimiza itakiwavyo kulingana na sheria iliyoandikwa ndani ya kile kitabu ambacho Hilkia kuhani alikikuta ndani ya Hekalu la BWANA. Kabla wala baada ya Mfalme Yosia hapakuwepo na mfalme mwingine ye yote ambaye alimpenda BWANA kwa moyo wake wote, kwa roho yake yote na kwa nguvu zake zote, sawasawa na Sheria yote ya Mose. Hata hivyo, BWANA hakuacha ghadhabu yake iliyowaka dhidi ya Yuda kwa sababu ya yale yote ambayo Manase alikuwa amefanya ili kumghadhibisha.
”Yehoahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitatu alipoanza kutawala, akatawala katika Yerusalemu kwa miezi mitatu. Jina la mama yake aliitwa Hamutali binti Yeremia kutoka Libna. Akafanya maovu machoni mwa BWANA, kama baba zake walivyofanya.
”Yehoiakimu alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, naye akatawala katika Yerusalemu miaka kumi na mmoja. Jina la mama yake aliitwa Zebida binti Pedaya kutoka Ruma. Naye akafanya maovu machoni mwa BWANA, kama baba zake walivyokuwa wamefanya.
”Yehoyakini alikuwa na umri wa miaka kumi na minane alipoanza kutawala, naye akatawala katika Yerusalemu kwa miezi mitatu. Jina la mama yake aliitwa Nehushta binti Elnathani kutoka Yerusalemu. Akafanya maovu machoni pa BWANA, kama vile baba yake alivyokuwa amefanya.
”Kama vile BWANA alivyokuwa amesema, Nebukadneza akaondoa hazina yote kutoka Hekalu la BWANA na kutoka jumba la mfalme, akavichukua vyombo vyote vya dhahabu ambavyo Solomoni mfalme wa Israeli alikuwa amevitengeneza kwa ajili ya Hekalu la BWANA. Akawachukua Yerusalemu wote kwenda uhamishoni: yaani, maafisa wote na mashujaa, watu wenye ustadi na ufundi, jumla yao watu elfu kumi. Watu maskini sana ndio tu waliobaki katika nchi. Nebukadneza akamchukua mateka Yehoyakini kwenda Babeli. Pia akawachukua utumwani kutoka Yerusalemu kwenda Babeli mama yake mfalme, wake zake, maafisa wake na viongozi wote wa nchi. Mfalme wa Babeli pia akawahamishia Babeli mashujaa elfu saba, wenye nguvu na wanaofaa kupigana vita, watu wenye ustadi na mafundi elfu moja.
”Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mmoja alipoanza kutawala, naye akatawala katika Yerusalemu miaka kumi na mmoja. Jina la mama yake aliitwa Hamuthi binti Yeremia, kutoka Libna. Akafanya maovu machoni mwa BWANA, kama alivyofanya Yehoiakimu. Ilikuwa ni kwa sababu ya hasira ya BWANA haya yote yakatokea katika Yerusalemu na katika Yuda, na mwishoni akawasukumia mbali na uso wake. Basi, Sedekia akaasi dhidi ya mfalme wa Babeli.
”naye akakamatwa. Akapelekwa kwa mfalme wa Babeli huko Ribla, mahali ambapo hukumu yake ilitangazwa. Wakawaua wanawe Sedekia mbele ya macho yake. Kisha wakayang'oa macho yake, wakamfunga kwa pingu za shaba na kumpeleka Babeli.
”Sauli alikufa kwa sababu hakuwa mwaminifu kwa BWANA. Hakulishika neno la BWANA, hata akataka shauri kwa mwaguzi kwa ajili ya uongozi, hakumwuliza BWANA. Kwa hiyo BWANA alimwua, na ufalme akampa Daudi mwana wa Yese.
”Israeli yote walimjia Daudi kwa pamoja huko Hebroni wakamwambia, “Sisi ni nyama yako na damu yako. Wakati wote uliopita, hata wakati Sauli alipokuwa mfalme, wewe ndiwe uliyeiongoza Israeli vitani, naye BWANA Mungu wako alikuambia, ‘Wewe utawachunga watu wangu Israeli, na utakuwa mtawala wao.’ ”
”“Hata hivyo BWANA, Mungu wa Israeli, alinichagua mimi kutoka jamaa yangu yote niwe mfalme juu ya Israeli milele. Alimchagua Yuda kuwa kiongozi na kutoka katika nyumba ya Yuda akaichagua jamaa yangu na kutoka katika wana wa baba yangu ikampendeza kunifanya niwe mfalme juu ya Israeli yote. Miongoni mwa wanangu wote, naye BWANA amenipa wengi, amemchagua Solomoni mwanangu ili kukikalia kiti cha enzi cha ufalme wa BWANA juu ya Israeli.
”Aliniambia, ‘Solomoni mwanao ndiye atakayejenga nyumba yangu na nyua zangu, kwa maana nimemchagua yeye kuwa mwanangu, nami nitakuwa baba yake. Nitaufanya imara ufalme wake milele kama akiendelea kuzishika amri zangu na sheria zangu, kama afanyavyo hivi leo.’ “Hivyo basi ninawaagiza mbele za Israeli yote na kusanyiko hili la BWANA naye Mungu wetu akiwa anasikia: Iweni na bidii kuzifuata amri za BWANA Mungu wenu, ili mpate kumiliki nchi hii nzuri na kuwaachia wana wenu kuwa urithi milele.
”Daudi mwana wa Yese alikuwa mfalme wa Israeli yote. Alitawala Israeli kwa miaka arobaini, kwa miaka saba alitawala huko Hebroni na kwa miaka thelathini na mitatu alitawala huko Yerusalemu. Daudi akafa akiwa mzee mwenye umri mwema, akiwa ameshiba siku, utajiri na heshima. Naye Solomoni mwanawe akaingia mahali pake kuwa mfalme.
”Solomoni mwana wa Daudi alijiimarisha kwenye milango yote! Katika ufalme wake, kwa kuwa BWANA Mungu wake alikuwa pamoja naye, naye akamfanya mkuu mno. Ndipo Solomoni akasema na Israeli wote, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, waamuzi na viongozi wote katika Israeli, pamoja na wakuu wa jamaa. Naye Solomoni na kusanyiko lote wakakwea mpaka mahali pa juu pa kuabudia huko Gibeoni, kwa kuwa huko ndiko hema la Mungu la Mkutano lilipokuwa, ambalo Mose mtumishi wa BWANA alikuwa amelitengeneza huko jangwani. Basi Daudi alikuwa amelipandisha Sanduku la Mungu kutoka Kiriath-Yearimu mpaka mahali alipokuwa amepatengeneza kwa ajili yake, kwa sababu alikuwa amesimamisha hema kwa ajili ya hilo Sanduku huko Yerusalemu.
”Kisha Solomoni akasimama mbele ya madhabahu ya BWANA machoni pa kusanyiko lote la Israeli, naye akakunjua mikono yake. Basi alikuwa ametengeneza jukwaa la shaba, urefu wake dhiraa tano, na upana wake dhiraa tano na kimo chake dhiraa tatu, naye akaliweka katikati ya ukumbi wa nje. Akapanda juu ya hilo jukwaa kisha akapiga magoti mbele ya kushanyiko lote la Israeli, akanyosha mikono yake kwelekea mbinguni. Akasema: “Ee BWANA, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe mbinguni juu wala duniani chini, wewe unayetunza Agano lako la upendo na watumishi wanaodumu katika njia yako kwa moyo wote.
”Baada ya Solomoni kumaliza kuomba, moto ukashuka kutoka mbinguni na kuteketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu, nao utukufu wa BWANA ukalijaza Hekalu. Makuhani hawakuweza kuingia ndani ya Hekalu la BWANA kwa sababu utukufu wa BWANA ulilijaza. Waisraeli wote walipoona moto ukishuka na utukufu wa BWANA ukiwa juu ya Hekalu, wakapiga magoti sakafuni wakasujudu nyuso zao mpaka chini, nao wakamwabudu na kumshukuru BWANA wakisema, “Yeye ni mwema; upendo wake unadumu milele.” Ndipo mfalme na watu wote wakatoa dhabihu mbele za BWANA Mungu. Naye Mfalme Solomoni akatoa dhabihu ya ng'ombe 22,000 pamoja na kondoo na mbuzi 120,000. Hivyo ndivyo mfalme na watu wote walivyoweka wakfu Hekalu la Mungu.
”BWANA Mungu akamtokea Solomoni usiku na kumwambia: “Nimesikia maombi yako nami nimechagua mahali hapa kwa ajili yangu mwenyewe kuwa Hekalu kwa ajili ya dhabihu. “Wakati nitakapofunga mbingu ili isiwepo mvua, au nikiamuru nzige kula mazao ya nchi au nikituma tauni miongoni mwa watu wangu, kama watu wangu, wanaoitwa kwa Jina langu, watajinyenyekesha na kuomba na kuutafuta uso wangu na kuacha njia zao mbaya, basi nitasikia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi yao na nitaiponya nchi yao.
”Mfalme Rehoboamu akajiweka imara katika Yerusalemu na akaendelea kuwa mfalme. Alikuwa na umri wa miaka arobaini na mmoja alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na saba, mji ambao BWANA alikuwa ameuchagua miongoni mwa makabila yote ya Israeli ili aliweke Jina lake humo. Mama yake aliitwa Naama, alikuwa Mwaamoni. Rehoboamu akatenda maovu kwa sababu hakuuelekeza moyo wake katika kumtafuta BWANA Mungu.
”Abiya na watu wake wakawachinja kwa machinjo makuu, hata wakawepo majeruhi 500,000 miongoni mwa watu wenye uwezo wa Israeli.
”Yeroboamu hakupata nguvu tena wakati wa utawala wa Abiya. Naye BWANA akampiga Yeroboamu akafa.
”Asa akatenda yaliyo mema na haki machoni pa BWANA Mungu wake. Akaziondoa madhabahu za kigeni na mahali pa juu pa kuabudia miungu, akayavunja yale mawe ya kuabudiwa na kuzikatakata nguzo za Maashera. Akawaamuru Yuda kumtafuta BWANA, Mungu wa baba zao na kutii sheria zake na amri zake. Akaondoa mahali pa juu pa kuabudia miungu na madhabahu za kufukizia uvumba kwenye kila mji katika Yuda, nao ufalme ulikuwa na amani katika utawala wake.
”Ingawa hakuondoa mahali pa juu pa kuabudia miungu katika Israeli, Asa akauweka moyo wake wote kwa BWANA kikamilifu siku zote za maisha yake.
”Asa akamkasirikia mwonaji kwa sababu ya jambo hili. Alikuwa ameghadhibika sana hata akamweka gerezani. Wakati huo huo Asa akaanza kuwatesa na kuwaonea baadhi ya watu kwa ukatili.
”Katika mwaka wa thelathini na tisa wa utawala wake, Asa alipatwa na ugonjwa kwenye miguu yake. Ingawa ugonjwa wake ulimzidia sana, hata katika kuugua kwake hakutafuta msaada kutoka kwa BWANA bali kwa matabibu tu.
”BWANA Mungu alikuwa na Yehoshafati kwa sababu katika miaka yake ya mwanzoni alienenda katika njia za Daudi baba yake. Hakutafuta Mabaali bali alimtafuta Mungu wa baba yake na kuzifuata amri zake badala ya kufuata desturi za watu wa Israeli. Kwa hiyo BWANA akauimarisha ufalme chini ya uongozi wake, nao Yuda wote wakamletea Yehoshafati zawadi, hivyo akawa na utajiri mwingi na heshima. Moyo wake ukawa hodari katika njia za BWANA na zaidi ya yote, akaondoa mahali pa juu pa kuabudia miungu na nguzo za Maashera katika Yuda.
”Mikaya akaendelea, “Kwa hiyo lisikie neno la BWANA: Nilimwona BWANA ameketi juu ya kiti chake cha enzi pamoja na jeshi lote la mbinguni likiwa limesimama kumzunguka kulia kwake na kushoto kwake. Naye BWANA akasema, ‘Ni nani atakayemshawishi Ahabu ili aishambulie Ramoth-Gileadi na kukiendea kifo chake huko?’ “Mmoja akapendekeza hili na mwingine lile. Mwishoni, roho akajitokeza, akasimama mbele za BWANA na kusema, ‘Nitamshawishi.’ “BWANA akauliza, ‘Kwa njia gani?’ “Akasema, ‘Nitakwenda na kuwa roho ya uongo katika vinywa vya manabii wake wote.’ “BWANA akasema, ‘Utafanikiwa katika kumshawishi. Nenda ukafanye hivyo.’ “Kwa hiyo sasa BWANA ameweka roho ya kudanganya ndani ya vinywa vya hawa manabii wako wote. BWANA ameamuru maafa kwa ajili yako.”
”Kisha Zedekia mwana wa Kenaana akatoka na kumpiga Mikaya kofi usoni. Akauliza, “Huyo Roho kutoka kwa BWANA alipita njia gani, alipotoka kwangu ili kusema nawe?” Mikaya akajibu, “Utagundua siku hiyo utakapokwenda kujificha kwenye chumba cha ndani.” Kisha mfalme wa Israeli akaagiza, “Mchukueni na mkamrudishe kwa Amoni mtawala wa mji na kwa Yoashi mwana wa mfalme. Mkaseme, ‘Hivi ndivyo asemavyo mfalme: Mwekeni mtu huyu gerezani na asipewe cho chote ila mkate na maji mpaka nitakaporudi salama.’ ” Mikaya akasema, “Kama utarudi salama, basi BWANA hajanena kupitia kwangu.” Kisha akaongeza kusema, “Zingatieni maneno yangu, enyi watu wote!”
”Lakini mtu fulani akavuta upinde pasipo lengo na kumpiga mfalme wa Israeli katikati ya kiungio cha mavazi yake ya chuma, mfalme akamwambia mwendesha gari lake, “Geuza gari na uniondoe mimi katika mapigano, nimejeruhiwa.” Vita vikaendelea mchana kutwa naye Mfalme Ahabu akategemezwa ndani ya gari kuelekea Waaramu. Damu kutoka kwenye jeraha lake ikachuruzika ndani ya gari na jioni yake akafa.
”Hatimaye Yehoshafati mfalme wa Yuda akafanya urafiki na Ahazia mfalme wa Israeli ambaye alifanya maovu sana. Akaungana naye kutengeneza meli nyingi za kwenda Tarshishi, nazo zilitengenezwa huko Esion-Geberi. Ndipo Eliezeri mwana wa Dodavahu wa Maresha akatoa unabii dhidi ya Yehoshafati, akasema, “Kwa kuwa umeungana na Ahazia, BWANA ataangamiza vile mlivyotengeneza.” Zile meli zikavunjika na hazikuweza kung'oa nanga ili kwenda Tarshishi.
”Yehoramu alikuwa na umri wa miaka thelathini na miwili alipokuwa mfalme, akatawala huko Yerusalemu kwa miaka minane. Akaiendea njia ya wafalme wa Israeli, kama ilivyokuwa imefanya nyumba ya Ahabu, kwa sababu alioa binti wa Ahabu. Akatenda maovu machoni pa BWANA.
”BWANA akaamsha chuki ya Wafilisti na ya Waarabu walioishi karibu na Wakushi dhidi ya Yehoramu. Wakaishambulia Yuda, wakaivamia na kuchukua mali zote zilizopatikana katika jumba la mfalme pamoja na wanawe na wake zake. Hakubakiziwa mwana ye yote isipokuwa Ahazia aliyekuwa mdogo wa wote. Baada ya mambo haya yote, BWANA akampiga Yehoramu kwa ugonjwa usioponyeka wa matumbo. Ikawa baada ya muda, mwisho wa mwaka wa pili, matumbo yake yakatoka nje kwa sababu ya ugonjwa, naye akafa katika maumivu makali sana. Watu wake hawakuwasha moto kwa heshima yake, kama walivyokuwa wamewafanyia baba zake.
”Ahazia alikuwa na umri wa miaka ishirini na miwili alipokuwa mfalme, naye akatawala huko Yerusalemu kwa mwaka mmoja. Mama yake aliitwa Athalia mjukuu wa kike wa Omri. Ahazia naye akaziendea njia za nyumba ya Ahabu kwa sababu mama yake alikuwa mshauri wake katika kutenda maovu. Akafanya yaliyo maovu machoni pa BWANA kama walivyokuwa wamefanya nyumba ya Ahabu, kwa kuwa baada ya kufa kwa baba yake nyumba ya Ahabu ndio waliokuwa washauri wake, kwa uangamivu wake.
”Ndipo akaenda kumsaka Ahazia, nao watu wake wakamkamata alipokuwa amejificha huko Samaria. Akaletwa kwa Yehu, naye Yehu akamwua. Wakamzika kwani walisema, “Alikuwa mwana wa Yehoshafati, ambaye alimtafuta BWANA kwa moyo wake wote.” Hivyo hapakuwa na mtu mwenye uwezo katika nyumba ya Ahazia aliyeweza kushika ufalme.
”Athalia aliposikia kelele za watu wakikimbia na kumsifu mfalme, akawaendea watu katika Hekalu la BWANA. Athalia akaangalia, tazama alikuwepo mfalme akiwa amesimama karibu na nguzo yake kwenye ingilio. Maafisa na wapiga tarumbeta walikuwa kando ya mfalme, nao watu wote wa nchi walikuwa wanashangilia na kupiga tarumbeta na waimbaji wakiwa na vyombo vya uimbaji, walikuwa wakiongoza nyimbo za sifa. Ndipo Athalia akararua mavazi yake na kupiga kelele, akisema, “Uhaini! Uhaini!”
”Kisha Yehoyada akafanya agano kwamba yeye na watu wote pamoja na mfalme watakuwa watu wa BWANA. Kisha watu wote wakaenda kwenye hekalu la Baali na kulibomoa. Wakavunjavunja madhabahu pamoja na sanamu na kumwua Matani kuhani wa Baali mbele ya hizo madhabahu. Kisha Kuhani Yehoyada akaweka uangalizi wa Hekalu la BWANA mikononi mwa makuhani, waliokuwa Walawi, ambao Mfalme Daudi alikuwa amewagawa ili wahudumu hekaluni kwa ajili ya kutoa sadaka za kuteketezwa za BWANA kama ilivyoandikwa katika Sheria ya Mose, kwa kushangilia na kuimba kama Daudi alivyokuwa ameagiza.
”Yoashi alikuwa na umri wa miaka saba alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka arobaini. Mama yake aliitwa Sibia aliyekuwa ametoka Beer-Sheba. Yoashi akafanya yaliyo mema machoni pa BWANA miaka yote ya Yehoyada kuhani.
”Ndipo Roho wa BWANA akaja juu ya Zekaria mwana wa Yehoyada kuhani. Akasimama mbele ya watu akasema, “Hili ndilo asemalo Mungu, ‘Kwa nini mnakataa kuzitii amri za BWANA? Hamtafanikiwa kwa kuwa mmemwacha BWANA, yeye naye amewaacha ninyi.’ ” Lakini wakafanya shauri baya juu yake na kwa amri ya mfalme wakampiga kwa mawe mpaka akafa katika ukumbi wa Hekalu la BWANA. Mfalme Yoashi hakukumbuka wema aliotendewa na Yehoyada baba yake Zekaria ila alimwua mwanawe, ambaye alisema wakati akiwa amelala akingojea kufa, “BWANA na alione hili na alipize kisasi.”
”Amazia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka ishirini na tisa. Mama yake aliitwa Yehoadani kutoka Yerusalemu. Akatenda yaliyo mema machoni pa BWANA, lakini si kwa moyo wake wote.
”Kuanzia wakati ule Amazia alipogeuka na kuacha kumfuata BWANA walifanya shauri baya dhidi yake huko Yerusalemu naye akakimbilia Lakishi, lakini wakatuma watu wamfuatilie huko Lakishi nao wakamwulia huko.
”Uzia alikuwa na umri wa miaka kumi na sita alipokuwa mfalme, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka hamsini na miwili. Mama yake aliitwa Yekolia wa Yerusalemu. Akafanya yaliyo mema machoni pa BWANA sawasawa na Amazia baba yake alivyokuwa amefanya. Akamtafuta Mungu katika siku za Zekaria, aliyemwelekeza kumcha Mungu. Wakati wote alipomtafuta BWANA, Mungu alimfanikisha.
”Lakini baada ya Uzia kuwa na nguvu sana, majivuno yake yakamsababishia kuanguka. Alikosa uaminifu kwa BWANA Mungu wake, naye akaingia hekaluni mwa BWANA ili afukize uvumba kwenye madhabahu ya kufukizia uvumba. Azaria kuhani akiwa pamoja na makuhani wengine themanini wa BWANA wenye ujasiri wakamfuata huko ndani. Wakamkabili na kumwambia, “Siyo sawa kwako, Uzia, kumfukizia BWANA uvumba. Hiyo ni kazi ya makuhani, wazao wa Aroni, ambao wamewekwa wakfu ili kufukiza uvumba. Ondoka mahali patakatifu, kwa kuwa umekosa uaminifu nawe hutaheshimiwa na BWANA.” Uzia, ambaye alikuwa na chetezo mkononi mwake tayari kufukiza uvumba, akakasirika. Alipokuwa anawaghadhibikia makuhani mbele ya madhabahu ya kufukizia uvumba katika Hekalu la BWANA, ukoma ukamtokea penye kipaji chake cha uso. Azaria Kuhani Mkuu pamoja na makuhani wengine wote walipomtazama wakaona kwamba alikuwa na ukoma penye kipaji chake cha uso wakaharakisha kumtoa nje. Naam, hata yeye mwenyewe alikuwa anatamani kuondoka kwa sababu BWANA alikuwa amempiga. Mfalme Uzia alikuwa na ukoma mpaka siku ya kufa kwake. Akatengwa katika nyumba ya pekee akiwa mwenye ukoma, naye akawa ametengwa kutoka Hekalu la BWANA. Yothamu mwanawe akawa msimamizi wa jumba la kifalme, pia akawaongoza watu wa nchi.
”Yothamu alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na sita. Mama yake aliitwa Yerusha binti Sadoki. Akafanya yaliyo mema machoni pa BWANA kama vile Uzia baba yake alivyokuwa amefanya, lakini tofauti na yeye, hakuingilia huduma za hekaluni mwa BWANA. Lakini hata hivyo, watu wakaendelea na desturi zao mbaya.
”Ahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala. Akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na sita. Tofauti na Daudi baba yake, hakufanya yaliyo mema machoni pa BWANA. Akaziendea njia za wafalme wa Israeli na pia akasubu sanamu kwa ajili ya kuabudu Mabaali. Akatoa sadaka za kuteketezwa katika Bonde la Hinomu na kuwatoa wanawe kafara kwa kuwateketeza kwa moto, akifuata njia za machukizo za yale mataifa BWANA aliyoyafukuza humo mbele ya Waisraeli.
”Katika wakati wake wa mateso Mfalme Ahazi akazidi kukosa uaminifu kwa BWANA. Akatoa kafara kwa miungu ya Dameski, ambao walikuwa wamemshinda, kwa kuwa aliwaza, “Kwa kuwa miungu ya mfalme wa Aramu imewasaidia wao, nitaitolea dhabihu ili inisaidie na mimi.” Lakini haya ndiyo yaliyokuwa maangamizi yake na Israeli wote. Ahazi akakusanya pamoja vyombo vya nyumba ya Mungu na kuvivunja vipande vipande. Akafunga milango ya Hekalu la BWANA na kusimamisha madhabahu katika kila njia panda ya barabara za Yerusalemu. Katika kila mji wa Yuda akajenga mahali pa juu pa kuabudia miungu ili kutolea miungu mingine kafara za kuteketezwa na kuchochea hasira ya BWANA, Mungu wa baba zake.
”Hezekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala. Akatawala huko Yerusalemu kwa miaka ishirini na tisa. Mama yake aliitwa Abiya binti Zekaria. Akafanya yaliyo mema machoni pa BWANA sawasawa na alivyokuwa amefanya Daudi baba yake. Katika mwezi wa kwanza wa mwaka wa kwanza wa kutawala kwake alifungua milango ya Hekalu la BWANA, na kuikarabati.
”Mfalme Hezekia na nabii Isaya mwana wa Amozi wakalilia mbingu katika maombi kuhusu jambo hili. Naye BWANA akamtuma malaika ambaye aliangamiza wanaume wote wenye kupigana na viongozi na maafisa katika kambi ya mfalme wa Ashuru. Kwa hiyo, Mfalme wa Ashuru akarudi kwenye nchi yake mwenyewe kwa aibu. Naye alipokwenda katika hekalu la mungu wake, baadhi ya watoto wake walimkata na kumwua kwa upanga. Hivyo BWANA akamwokoa Hezekia na watu wa Yerusalemu kutoka mkononi mwa Senakeribu mfalme wa Ashuru na kutoka mikononi mwa wengine wote. BWANA akawastarehesha kila upande. Watu wengi wakaleta sadaka Yerusalemu kwa ajili ya BWANA na zawadi za thamani kwa ajili ya Hezekia mfalme wa Yuda. Tangu hapo na kuendelea, Hezekia aliheshimiwa sana na mataifa yote.
”Lakini wakati wajumbe walipotumwa na watawala wa Babeli kumwuliza juu ya ishara ambayo ilitokea katika nchi, Mungu alimwacha ili kumjaribu na kujua kila kitu kilichokuwa moyoni mwake.
”Manase alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa muda wa miaka hamsini na mitano. Akafanya yaliyo maovu machoni pa BWANA, akafanya machukizo kama walivyofanya mataifa BWANA aliyoyafukuza mbele ya Waisraeli. Akajenga upya mahali pa juu pa kuabudia miungu ambapo Hezekia baba yake, alikuwa amepabomoa, pia akasimamisha madhabahu za Mabaali na nguzo za Maashera. Akalisujudia jeshi lote la vitu vya angani na kuliabudu. Akajenga madhabahu za Baali katika Hekalu la BWANA ambamo BWANA alikuwa amesema, “Jina langu litakaa Yerusalemu milele.” Katika nyua zote za Hekalu la BWANA akajengea madhabahu kwa ajili ya jeshi lote la vitu vya angani. Akawatoa wanawe kuwa kafara kwa kuwapitisha katika moto katika Bonde la Hinomu, akafanya ulozi, uaguzi na uchawi, akataka ushauri kwa wenye pepo wa utambuzi na wenye kuwasiliana na mizimu. Akafanya maovu mengi machoni pa BWANA, akaichochea hasira yake. Akachukua ile sanamu aliyoichonga akaiweka katika Hekalu la BWANA ambalo Mungu alikuwa amemwambia Daudi na mwanawe Solomoni, “Katika Hekalu hili na katika Yerusalemu niliouchagua kutoka kabila zote za Israeli, nitaliweka Jina langu milele. Sitaifanya miguu ya Waisraeli iondoke tena katika nchi niliyowapa baba zenu, kama watakuwa waangalifu kufanya kila kitu nilichowaamuru kuhusu sheria zote, maagizo na amri zilizotolewa kwa mkono wa Mose.” Lakini Manase akawaongoza Yuda na watu wa Yerusalemu katika upotovu, kiasi kwamba walifanya maovu mengi kupita mataifa ambayo BWANA aliwaangamiza mbele ya Waisraeli.
”BWANA akasema na Manase pamoja na watu wake, lakini hawakumjali. Hivyo BWANA akaleta juu yao majemadari wa jeshi la mfalme wa Ashuru, ambao walimchukua Manase kwenda kifungoni, wakaweka ndoana katika pua yake, wakamfunga kwa pingu za shaba na kumpeleka Babeli. Katika dhiki yake akamsihi BWANA Mungu wake na kujinyenyekeza sana mbele za Mungu wa baba zake. Naye alipomwomba, BWANA akaguswa na kule kusihi kwake na akasikiliza kilio chake, kwa hiyo akamrudisha Yerusalemu na kwenye ufalme wake. Ndipo Manase akatambua kwamba BWANA ndiye Mungu.
”Akaondolea mbali miungu ya kigeni na kuondoa sanamu kutoka katika Hekalu la BWANA pamoja na madhabahu zote alizozijenga katika kile kilima kilichojengwa Hekalu na katika Yerusalemu, akazitupa nje ya mji. Kisha akarudisha madhabahu ya BWANA na kutolea juu yake dhabihu za sadaka za amani pamoja na sadaka za shukrani, naye akawaamuru Yuda wamtumikie BWANA, Mungu wa Israeli. Lakini hata hivyo watu wakaendelea kutoa dhabihu mahali pa juu pa kuabudia miungu, lakini wakimtolea BWANA Mungu wao peke yake.
”Amoni alikuwa na umri wa miaka ishirini na miwili, alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka miwili. Akafanya maovu machoni pa BWANA kama alivyokuwa amefanya Manase baba yake. Amoni akaabudu na kutoa dhabihu kwa sanamu zote alizokuwa ametengeneza Manase. Lakini tofauti na Manase baba yake, hakujinyenyekeza mbele za BWANA, badala yake Amoni aliongeza makosa zaidi na zaidi.
”Yosia alikuwa na umri wa miaka minane alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka thelathini na mmoja. Akafanya yaliyo mema machoni pa BWANA na kuenenda katika njia za Daudi baba yake, pasipo kugeuka upande wa kuume wala wa kushoto. Katika mwaka wa nane wa utawala wake, alipokuwa angali bado mdogo, alianza kumtafuta Mungu wa Daudi baba yake. Katika mwaka wake wa kumi na mbili alianza kusafisha mahali pa juu pa kuabudia miungu pa Yuda na Yerusalemu, akiondoa nguzo za Ashera, sanamu za kuchonga na vinyago vya kusubu. Mbele ya macho yake, wakazibomoa madhabahu za Mabaali, wakazivunja madhabahu za kufukizia uvumba zilizokuwa zimesimama juu yake, wakazivunja nguzo za Ashera, sanamu na vinyago. Hivi alivivunja vipande vipande na kuvisambaza juu ya makaburi ya waliokuwa wamevitolea kafara.
”Hilkia akamwambia Shafani mwandishi, “nimekiona Kitabu cha Sheria ndani ya Hekalu la BWANA.” Akampatia Shafani kile Kitabu. Ndipo Shafani akakipeleka kile Kitabu kwa mfalme na kumwambia, “Maafisa wako wanafanya kila kitu kama walivyokabidhiwa kufanya. Wamelipa fedha zilizokuwa katika Hekalu la BWANA na wamewakabidhi wasimamizi na wafanyakazi.” Kisha Shafani mwandishi akamwarifu mfalme kuwa, “Kuhani Hilkia amenipatia Kitabu.” Naye Shafani akakisoma mbele ya mfalme. Mfalme aliposikia yale maneno ya Sheria, akayararua mavazi yake. Akatoa maagizo haya kwa Hilkia, Ahikamu mwana wa Shafani, Abdoni mwana wa Mika, Shafani mwandishi na Asaya mtumishi wa mfalme, “Nendeni mkamwulize BWANA kwa ajili yangu na kwa ajili ya mabaki walioko Israeli na Yuda kuhusu haya yaliyoandikwa katika kitabu hiki ambacho kimeonekana hekaluni. Hasira ya BWANA ni kubwa mno ambayo imemwagwa juu yetu kwa sababu baba zetu hawakulishika neno la BWANA wala hawakutenda sawasawa na yale yote yaliyoandikwa katika Kitabu hiki.”
”‘Hili ndilo BWANA asemalo: Nitaleta maafa juu ya mahali hapa na watu wake, laana zote zilizoandikwa ndani ya hicho kitabu ambazo zimesomwa mbele ya mfalme wa Yuda. Kwa sababu wameniacha mimi na kufukiza uvumba kwa miungu mingine ili waichochee hasira yangu kwa kazi yote ya mikono yao, hivyo hasira yangu itamwagwa juu ya mahali hapa, wala haitatulizwa. Mwambieni mfalme wa Yuda, aliyewatuma kumwuliza BWANA, Hili ndilo BWANA, Mungu wa Israeli, asemalo kuhusu maneno uliyoyasikia: Kwa sababu moyo wako ulikuwa mwepesi kusikia, nawe ukajinyenyekeza mbele za Mungu wakati uliposikia kile alichokisema dhidi ya mahali hapa na watu wake na kwa sababu ulijinyenyekeza mbele zangu ukararua mavazi yako na kulia mbele zangu, nimekusikia, asema BWANA.
”Mfalme akasimama karibu na nguzo yake na kufanya upya Agano mbele za BWANA ili kumfuata BWANA na kuzishika amri zake, maagizo na sheria kwa moyo wake wote na kwa roho yake yote na ili kuyatii maneno ya Agano yaliyoandikwa katika kitabu hiki. Ndipo akamtaka kila mmoja katika Yerusalemu na Benyamini kuweka ahadi zao wenyewe kwa hilo Agano, watu wa Yerusalemu wakafanya hivyo kwa kufuata Agano la BWANA, Mungu wa baba zao. Yosia akaondoa machukizo yote ya sanamu kutoka katika nchi yote iliyokuwa mali ya Waisraeli na akawataka wale wote waliokuweko katika Israeli wamtumikie BWANA Mungu wao. Kwa muda wote alioishi, hawakushindwa kumfuata BWANA, Mungu wa baba zao.
”Yehoahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitatu alipoanza kutawala, naye akatawala katika Yerusalemu kwa miezi mitatu.
”Yehoyakimu alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka kumi na mmoja. Akafanya maovu machoni pa BWANA Mungu wake.
”Yehoyakimu alikuwa na miaka kumi na minane alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miezi mitatu na siku kumi. Akafanya yaliyo maovu machoni pa BWANA.
”Mnamo majira ya vuli, Mfalme Nebukadneza akatuma watu wakamleta Babeli, pamoja na vyombo vya thamani kutoka katika Hekalu la BWANA naye akamfanya Sedekia, ndugu yake Yehoyakimu kuwa mfalme wa Yuda na Yerusalemu.
”Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mmoja alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa muda wa miaka kumi na mmoja. Akafanya yaliyo maovu machoni pa BWANA Mungu wake wala hakujinyenyekeza mbele ya nabii Yeremia, ambaye alinena neno la BWANA. Pia alimwasi Mfalme Nebukadneza, ambaye alikuwa amemwapisha kwa jina la Mungu. Akashupaza shingo na akafanya moyo wake kuwa mgumu wala hakutaka kumgeukia BWANA, Mungu wa Israeli. Zaidi ya hayo viongozi wote wa makuhani pamoja na watu wakazidi kukosa uaminifu zaidi na zaidi, wakafanya machukizo yote kama walivyofanya mataifa wakinajisi Hekalu la BWANA alilokuwa amelitakasa huko Yerusalemu.
”Lakini waliwadhihaki wajumbe wa BWANA wakayadharau maneno yake na kuwacheka manabii wake mpaka ghadhabu ya BWANA ikawa kubwa dhidi ya watu wake na hakukuwa na namna ya kuituliza. Mungu akamwinua dhidi yao mfalme wa Wakaldayo, aliyewaua vijana wao wa kiume kwa upanga ndani ya mahali patakatifu, ambaye hakumbakiza kijana mwanaume wala kijana mwanamke, wazee wala vikongwe. Mungu akawatia wote mikononi mwa Nebukadneza. Akavichukua kwenda Babeli vyombo vyote kutoka katika Hekalu la Mungu, vikubwa na vidogo, hazina za Hekalu la BWANA pamoja na hazina za mfalme na za maafisa wake. Wakalitia moto Hekalu la Mungu na kuzibomoa kuta za Yerusalemu, wakachoma moto majumba yote ya kifalme na kuharibu kila kitu chake cha thamani. Wale watu walionusurika kuuawa kwa upanga wakachukuliwa kwenda uhamishoni Babeli, nao wakawa watumishi wake na wa wanawe mpaka wakati wa utawala wa ufalme wa Uajemi. Nchi ikaendelea kufurahia pumziko lake la Sabato, wakati wote wa kufanywa kwake ukiwa ilipumzika mpaka ile miaka sabini ilipotimia katika kutimiza neno la BWANA lililonenwa na Yeremia.
”Katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Koreshi mfalme wa Uajemi, ili litimie lile neno la BWANA lililosemwa na nabii Yeremia, BWANA akausukuma moyo wa Koreshi mfalme wa Uajemi kutoa tangazo kwa maandishi katika utawala wake wote: “Hili ndilo asemalo Koreshi mfalme wa Uajemi: “ ‘BWANA, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote za duniani na ameniagiza kumjengea Hekalu huko Yerusalemu katika Yuda. Ye yote wa watu wake miongoni mwenu, Mungu wake na awe pamoja naye, huyo mtu na apande.’ ”
”Katika mwaka wa kwanza wa Koreshi mfalme wa Uajemi, ili kutimiza neno la BWANA lililosemwa na Yeremia, BWANA aliusukuma moyo wa Koreshi mfalme wa Uajemi kutangaza katika himaya yake yote na kuliweka katika maandishi: “Hili ndilo asemalo Koreshi mfalme wa Uajemi: “ ‘BWANA, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote za duniani na ameniagiza kumjengea Hekalu huko Yerusalemu katika Yuda. Ye yote wa watu wake miongoni mwenu, Mungu wake na awe pamoja naye, wacha apande kwenda Yerusalemu katika Yuda na kujenga Hekalu la BWANA, Mungu wa Israeli, Mungu aliyeko huko Yerusalemu.
”Maafisa wetu na wafanye kwa niaba ya kusanyiko lote. Kisha kila mmoja katika miji yetu ambaye ameoa mwanamke wa kigeni aje kwa wakati uliopangwa, akiwa pamoja na wazee na waamuzi wa kila mji, hadi hasira kali ya Mungu wetu katika shauri hili itakapoondolewa kwetu.”
”Baada ya matukio haya, Mfalme Ahusuero alimheshimu Hamani mwana wa Hamedatha, Mwagagi, akampandisha na kumpa kiti chake cha heshima cha juu sana kuliko wakuu wengine wote. Maafisa wote wa kifalme waliokaa langoni mwa mfalme walipiga magoti na kumpa Hamani heshima, kwa kuwa mfalme alikuwa ameamuru hili kuhusu Hamani. Lakini Mordekai hakumpigia magoti wala kumheshimu. Kisha maafisa wa kifalme waliokuwa langoni mwa mfalme walimuuliza Mordekai, “Kwa nini hutii agizo la mfalme?” Siku baada ya siku walizungumza naye lakini hakukubali. Kwa hiyo walimweleza Hamani kuona kama tabia ya Mordekai itaweza kuvumiliwa, kwa maana alikuwa amewaambia kuwa yeye ni Myahudi.
”Kisha siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kwanza waandishi wa mfalme waliitwa. Wakaandika barua kwa kila jimbo na katika kila lugha ya watu kama agizo la Hamani lilivyotoka kwa mfalme, kwa watawala wa majimbo mbalimbali, na wakuu wa watu mbalimbali. Hizi ziliandikwa kwa jina la Mfalme Ahusuero mwenyewe na kutiwa muhuri wa pete yake mwenyewe. Barua zilipelekwa na tarishi katika majimbo yote ya mfalme zikiwa na amri ya kuharibu, kuua na kuangamiza Wayahudi wote wadogo kwa wakubwa, wanawake na watoto wadogo kwa siku moja. Katika siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili, ndio mwezi wa Adari, walipaswa pia kuteka nyara vitu vyao. Nakala ya andiko la amri ilipaswa kutolewa kama sheria katika kila jimbo na kufahamishwa kwa watu wa kila taifa ili waweze kuwa tayari kwa siku ile. Kwa kuharakishwa na amri ya mfalme, matarishi walikwenda na andiko lilitolewa katika mji wa ngome ya Shushani. Mfalme na Hamani waliketi na kunywa, lakini mji wa Shushani ulifadhaika.
”Siku ya tatu Esta alivaa mavazi yake ya kimalkia, naye akasimama katika ua wa ndani wa jumba la mfalme, mbele ya ukumbi wa mfalme. Naye mfalme alikuwa akiketi katika kiti chake cha kifalme katika ukumbi, akielekea langoni. Alipomwona Malkia Esta amesimama uani alipendezwa naye, akamnyoshea fimbo ya utawala ya dhahabu ile iliyokuwa mkononi mwake. Kwa hiyo Esta alikaribia na kuigusa ncha ya fimbo ya mfalme. Kisha mfalme aliuliza, “Malkia Esta, ni nini? Ombi lako ni nini? Hata kama ni nusu ya ufalme, utapewa.”
”Wakati nchi inapoangukia mikononi mwa waovu, yeye huwafunga macho mahakimu wake. Kama si yeye, basi ni nani?
”Je, yeye aichukiaye haki aweza kutawala? Je, utamhukumu mwenye haki, Aliye na Nguvu Zote?
”Je, si ni yeye awaambiaye wafalme, ‘Ninyi hamfai kitu,’ nao watu mashuhuri, ‘Ninyi ni waovu!’
”Kwa nini mataifa wanashauriana kufanya mabaya, na mataifa kula njama bure? Wafalme wa dunia wanajipanga na watawala wanajikusanya pamoja dhidi ya BWANA na dhidi ya Mpakwa Mafuta wake. Wanasema, “Tuvunje minyororo yao na kuvitupilia mbali vifungo vyao.” Yeye atawalaye mbinguni hucheka, Bwana huwadharau.
”“Nimemtawaza mfalme wangu juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.” Nitatangaza amri ya BWANA: Yeye aliniambia, “Wewe ni Mwanangu, leo mimi nimekuzaa. Niombe, nami nitayafanya mataifa kuwa urithi wako, miisho ya dunia kuwa milki yako. Utawatawala kwa fimbo ya kifalme ya chuma na kuwavunjavunja kama chombo cha mfinyanzi.” Kwa hiyo, ninyi wafalme, iweni na hekima; mwonyeke, enyi watawala wa dunia. Mtumikieni BWANA kwa hofu na mshangilieni kwa kutetemeka.
”Waovu wataishia kuzimu, naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu. Lakini mhitaji hatasahaulika siku zote, wala matumaini ya walioonewa hayatapotea. Ee BWANA, inuka, usimwache binadamu ashinde, mataifa na yahukumiwe mbele zako. Ee BWANA, wapige kwa hofu, mataifa na yajue kuwa wao ni watu tu.
”BWANA ni Mfalme milele na milele, mataifa wataangamia watoke nchini mwake.
”BWANA huwajaribu wenye haki, lakini waovu na wale wanaopenda jeuri nafsi yake huwachukia.
”Miisho yote ya dunia itakumbuka na kumgeukia BWANA, nazo jamaa zote za mataifa watasujudu mbele zake, kwa maana ufalme ni wa BWANA naye hutawala juu ya mataifa.
”Ni nani huyu, huyu mfalme wa utukufu? Ni BWANA Mwenye Nguvu Zote; yeye ndiye Mfalme wa utukufu.
”BWANA huzuia mipango ya mataifa, hupinga makusudi ya mataifa. Lakini mipango ya BWANA inasimama imara milele, makusudi ya moyo wake kwa vizazi vyote. Heri taifa ambalo BWANA ni Mungu wao, watu ambao aliwachagua kuwa urithi wake.
”Jinsi gani alivyo wa kutisha, BWANA Aliye Juu Sana, Mfalme mkuu juu ya dunia yote. Ametiisha mataifa chini yetu na mataifa chini ya miguu yetu. Alituchagulia urithi wetu kwa ajili yetu fahari ya Yakobo, aliyempenda. Mungu amepaa katikati ya kelele za shangwe, BWANA katikati ya sauti za tarumbeta. Mwimbieni Mungu sifa, imbeni sifa, mwimbieni sifa Mfalme wetu, imbeni sifa. Kwa kuwa Mungu ni mfalme wa dunia yote, mwimbieni zaburi za sifa. Mungu anatawala juu ya mataifa, Mungu ameketi juu ya kiti chake cha enzi kitakatifu.
”Kwa kuwa BWANA ni Mungu mkuu, mfalme mkuu juu ya miungu yote.
”kwa tarumbeta na mvumo wa baragumu za pembe za kondoo dume: shangilieni kwa furaha mbele za BWANA, aliye Mfalme.
”Mataifa wataogopa jina la BWANA, wafalme wote wa dunia watauheshimu utukufu wako.
”Kwa msaada wangu wafalme hutawala na watawala hutunga sheria zilizo za haki, kwa msaada wangu wakuu hutawala, na wenye vyeo wote watawalao dunia.
”Haki huinua taifa, bali dhambi ni aibu kwa watu wote. Mfalme hupendezwa na mtumishi mwenye hekima, bali ghadhabu yake humwangukia mtumishi mwenye kuaibisha.
”Midomo ya mfalme huzungumza kwa hekima ya kiungu, wala kinywa chake hakipotoshi haki. Vipimo na mizani za halali hutoka kwa BWANA, mawe yote ya kupimia yaliyo katika mfuko ameyafanya yeye. Wafalme huchukia sana kutenda maovu, kwa maana kiti cha kifalme hufanywa imara kwa njia ya haki. Wafalme hufurahia midomo ya uaminifu, humthamini mtu asemaye kweli. Ghadhabu ya mfalme ni mjumbe wa mauti, bali mtu mwenye hekima ataituliza. Uso wa mfalme ung'aapo, ina inamaanisha uhai, upendeleo wake ni kama wingu la mvua wakati wa vuli.
”Haistahili mpumbavu kuishi katika anasa, itakuwa vibaya kiasi gani kwa mtumwa kuwatawala wakuu. Hekima ya mtu humpa uvumilivu, ni kwa utukufu wake kusamehe makosa. Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba, bali wema wake ni kama umande juu ya majani.
”Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba; yeye amkasirishaye hupoteza uhai wake.
”Wakati mfalme aketipo katika kiti chake cha enzi kuhukumu, hupepeta ubaya wote kwa macho yake.
”Moyo wa mfalme uko katika mkono wa BWANA; huuongoza kama mkondo wa maji, po pote apendapo.
”Mwanangu, mche BWANA na mfalme, wala usijiunge na waasi, kwa maana hao wawili watatuma maangamizi ya ghafula juu yao, naye ni nani ajuaye maafa wawezayo kuleta?
”Ni Utukufu wa Mungu kuficha jambo, bali ni utukufu wa wafalme kuchunguza jambo. Kama mbingu zilivyo juu na nchi ilivyo chini, ndivyo ambavyo mioyo ya wafalme haichunguziki. Ondoa takataka kwenye madini ya fedha, nako ndani yake kutatokea kitu halisi kwa ajili ya mfua fedha. Ondoa waovu mbele ya mfalme, nacho kiti chake cha enzi kitaimarishwa kwa njia ya haki. Usijikweze mwenyewe mbele ya mfalme, wala usidai nafasi miongoni mwa watu wakuu. Ni afadhali yeye akuambie, “Njoo huku juu,” kuliko yeye kukuaibisha mbele ya mkuu. Kile ulichokiona kwa macho yako
”Kama simba angurumaye au dubu ashambuliaye, divyo alivyo mtu mwovu atawalaye wanyonge. Mtawala dhalimu hana akili, bali yeye achukiaye mapato ya udhalimu atafurahia maisha marefu.
”Wenye haki wanapostawi, watu hufurahi; waovu watawalapo, watu hulia kwa huzuni. Mtu apendaye hekima huleta furaha kwa baba yake, bali aambatanaye na kahaba hutapanya mali yake. Kwa haki mfalme huipa nchi uthabiti, bali mfalme aliye na tamaa ya rushwa huiangamiza.
”Kama mtawala akisikiliza uongo, maafisa wake wote huwa waovu. Mtu maskini na mtu anayeonea wanafanana kwa jambo hili: BWANA hutia nuru macho yao wote wawili. Kama mfalme akiwaamua maskini kwa haki, kiti chake cha enzi kitakuwa thabiti siku zote.
”“Ee Lemueli, haifai wafalme, haifai wafalme kunywa mvinyo, haifai watawala kutamani sana kileo, wasije wakanywa na kusahau ile sheria inayoamuru na kuwanyima haki zao wote walioonewa.
”Nawaambia, Tii amri ya mfalme, kwa sababu uliapa mbele za Mungu. Usiharakishe kuondoka mbele ya mfalme. Usiendelee kutenda lililo baya, kwa maana mfalme atafanya lo lote apendalo. Kwa kuwa neno la mfalme ndilo lenye mamlaka ya mwisho, nani awezaye kumwambia, “Je, wewe unafanya nini?”
”Usimshutumu mfalme hata ikiwa ni katika mawazo yako, au kumlaani tajiri katika chumba chako cha kulala, kwa sababu ndege wa angani wanaweza kuchukua maneno yako, naye ndege anayeruka anaweza kutoa taarifa ya yale uliyosema.
”Nchi yenu imekuwa ukiwa, miji yenu imeteketezwa kwa moto; nchi yenu imeachwa tupu na wageni mbele ya macho yenu, imeharibiwa kama vile imepinduliwa na wageni. Binti Sayuni ameachwa kama kipenu katika shamba la mizabibu, kama kibanda katika shamba la matikitimaji, kama mji uliohusuriwa. Kama BWANA Mungu Mwenye Nguvu Zote asingelituachia walionusurika, tungelikuwa kama Sodoma, tungelifanana na Gomora. Sikieni neno la BWANA, ninyi watawala wa Sodoma; sikilizeni sheria ya Mungu wetu, enyi watu wa Gomora!
”Acheni kuniletea sadaka zisizokuwa na maana! Uvumba wenu ni chukizo kwangu. Miandamo ya Mwezi, Sabato na makusanyiko ya ibada: siwezi kuvumilia makusanyiko yenu maovu. Sikukuu zenu za Miandamo ya Mwezi na sikukuu zenu zilizoamriwa moyo wangu unazichukia. Zimekuwa mzigo kwangu, nimechoka kuzivumilia.
”Atahukumu kati ya mataifa na ataamua magomvi ya mataifa mengi. Watafua panga zao kuwa majembe na mikuki yao kuwa miundu ya kukata matawi. Taifa halitainua upanga dhidi ya taifa jingine, wala hayatafanya mazoezi ya vita tena.
”“Usiite fitina kila kitu ambacho watu hawa hukiita fitina, usiogope kile wanachokiogopa, wala usikihofu.
”Kwa maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume, nao utawala utakuwa mabegani mwake. Naye ataitwa Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani. Kuongezeka kwa utawala wake na amani hakutakuwa na mwisho. Atatawala katika kiti cha enzi cha Daudi na juu ya ufalme wake, akiuthibitisha na kuutegemeza kwa haki na kwa adili, tangu wakati huo na hata milele. Wivu wa BWANA Mwenye Nguvu Zote utatimiza haya.
”Babeli, johari ya falme, utukufu wa kiburi cha Wababeli, itaangushwa na Mungu kama Sodoma na Gomora. Hautakaliwa na watu kamwe wala watu hawataishi humo kwa vizazi vyote, hakuna Mwarabu atakayepiga hema lake huko, hakuna mchungaji atakayepumzisha makundi yake ya kondoo na mbuzi huko.
”utaichukua dhihaka hii dhidi ya mfalme wa Babeli: Tazama jinsi mtesi alivyofikia mwisho! Tazama jinsi ghadhabu yake kali ilivyokoma! BWANA amevunja fimbo ya mwovu, fimbo ya utawala ya watawala,
”Dunia imetiwa unajisi na watu wake, wameacha kutii sheria, wamevunja amri na kuvunja Agano la milele. Kwa hiyo laana inaiteketeza dunia, watu wake lazima waichukue hatia yao. Kwa hiyo wakazi wa dunia wameteketezwa, nao waliosalia ni wachache sana.
”Tazama, mfalme atatawala kwa uadilifu na watawala watatawala kwa haki.
”Kwa kuwa BWANA ni mwamuzi wetu, BWANA ndiye mtoa sheria wetu, BWANA ni mfalme wetu, yeye ndiye atakayetuokoa.
”amwambiaye Koreshi, ‘Yeye ni mchungaji wangu, naye atatimiza yote yanipendezayo; atauambia Yerusalemu, “Ukajengwe tena,” na kuhusu Hekalu, “Misingi yake na iwekwe.” ’
”“Hili ndilo asemalo BWANA kwa mpakwa mafuta wake, Koreshi, ambaye nimemshika mkono wake wa kuume kutiisha mataifa mbele yake na kuwavua wafalme silaha zao, kufungua milango mbele yake ili kwamba malango yasije yakafungwa:
”Kwa maana taifa au ufalme ule ambao hautakutumikia utaangamia; utaharibiwa kabisa.
”Tazama, leo nimekuweka juu ya mataifa na falme ili kung'oa na kubomoa, ili kuharibu na kuangamiza, ili kujenga na kupanda.”
”Nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda wamekuwa si waaminifu kwangu kamwe,” asema BWANA.
”Ee nyumba ya Israeli,” asema BWANA, “Ninaleta taifa toka mbali dhidi yako, taifa la kale na linaloendelea kudumu, taifa ambalo lugha yao huijui, wala msemo wao huwezi kuuelewa.
”“Kuanzia aliye mdogo kabisa hadi mkubwa kabisa, wote wanatamani kupata faida isiyo halali; makuhani na manabii wanafanana, wote wanafanya udanganyifu.
”Lakini BWANA ni Mungu wa kweli, yeye ndiye Mungu aliye hai, Mfalme wa milele. Akiwa amekasirika, dunia hutetemeka, mataifa hayawezi kustahimili hasira yake.
”Lakini kama taifa lo lote halitasikiliza na kutii, nitaling'oa kabisa na kuliangamiza,” asema BWANA.
”Kisha neno la BWANA likanijia kusema: “Ee nyumba ya Israeli, je, siwezi kuwafanyia kama huyu mfinyanzi afanyavyo?” Asema BWANA. “Kama vile udongo ulivyo katika mikono ya mfinyanzi, ndivyo mlivyo katika mkono wangu, Ee nyumba ya Israeli. Ikiwa wakati wo wote nikitangaza kuwa taifa au ufalme utang'olewa, utaangushwa na kuangamizwa, ikiwa lile taifa nililolionya litatubia uovu wake, ndipo nitakapokuwa na huruma wala sitawapiga kwa maafa niliyokuwa nimekusudia kwa ajili yao. Ikiwa wakati mwingine nitatangaza kuwa taifa ama utawala ujengwe na kusimikwa, ikiwa utafanya maovu mbele zangu na hukunitii, ndipo nitakapoghairi makusudio yangu mema niliyokuwa nimeyakusudia kwa ajili yake.
”wafalme wote wa pande za kaskazini, wa karibu na wa mbali mmoja baada ya mwingine, yaani, falme zote juu ya uso wa dunia. Baada ya hao wote, mfalme wa Sheshaki atakunywa pia. “Kisha uwaambie, ‘Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli asemalo: Kunyweni, mlewe na mtapike, angukeni wala msiinuke tena kwa sababu ya upanga nitakaotuma miongoni mwenu.’
”Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote asemalo: “Tazama! Maafa yanaenea kutoka taifa moja hadi jingine; tufani kubwa inainuka kutoka miisho ya dunia.” Wakati huo, hao waliouawa na BWANA watatapakaa kila mahali, kuanzia mwisho mmoja wa dunia hadi mwisho mwingine. Hawataombolezewa wala kukusanywa au kuzikwa lakini watakuwa kama mavi yaliyoenea juu ya ardhi. Lieni na kuomboleza, enyi wachungaji, mgaegae mavumbini, ninyi viongozi wa kundi. Kwa maana wakati wenu wa kuchinjwa umewadia; mtaanguka na kuvunjwavunjwa kama vyombo vizuri vya udongo. Wachungaji hawatakuwa na mahali pa kukimbilia, viongozi wa kundi hawatapata mahali pa kutorokea. Sikia kilio cha wachungaji, maombolezo ya viongozi wa kundi, kwa maana BWANA anayaharibu malisho yao.
”Pia tafuteni amani na mafanikio ya mji ambamo nimewapeleka uhamishoni. Mwombeni BWANA kwa ajili ya mji kwa sababu ukistawi, ninyi pia mtastawi.”
”Tazama jinsi nyundo ya dunia yote ilivyovunjika na kuharibika! Tazama jinsi Babeli ilivyokuwa ukiwa miongoni mwa mataifa!
”“Kimbieni kutoka Babeli! Okoeni maisha yenu! Msiangamizwe kwa sababu ya dhambi zake. Ni wakati wa kisasi cha BWANA, atamlipa kile anachostahili. Babeli alikuwa kikombe cha dhahabu katika mkono wa BWANA; aliufanya ulimwengu wote ulewe. Mataifa walikunywa mvinyo wake; kwa hiyo sasa wameingiwa na wazimu.
”Hata kama Babeli ikifika angani na kuziimarisha ngome zake ndefu, nitatuma waharabu dhidi yake,” asema BWANA.
”Nitawafanya maafisa wake na wenye busara walewe, watawala wao, maafisa, pamoja na wapiganaji wao; watalala milele na hawataamka,” asema Mfalme, ambaye jina lake ni BWANA Mwenye Nguvu Zote. Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote asemalo: “Ukuta mnene wa Babeli utasawazishwa, na malango yaliyoinuka yatateketezwa kwa moto; mataifa yanajichosha bure, taabu ya mataifa ni nishati tu kwa ajili ya miali ya moto.”
”Yeye hubadili nyakati na majira, huwaweka wafalme na kuwaondoa. Huwapa hekima wenye hekima na maarifa wenye ufahamu.
”“Hii ndiyo iliyokuwa ndoto, nasi sasa tutamfasiria mfalme. Ee mfalme, wewe ni mfalme wa wafalme. Mungu wa mbinguni amekupa wewe utawala, uweza, nguvu na utukufu, mikononi mwako amewaweka wanadamu, wanyama wa kondeni na ndege wa angani. Po pote waishipo amekufanya wewe kuwa mtawala juu yao wote. Wewe ndiye kile kichwa cha dhahabu. “Baada yako, ufalme mwingine utainuka, ulio dhaifu kuliko wako. Baadaye, utafuata ufalme wa tatu, ule wa shaba, utatawala juu ya dunia yote. Hatimaye, kutakuweko na ufalme wa nne, wenye nguvu kama chuma, kwa maana chuma huvunja na kupondaponda kila kitu, kama vile chuma ivunjavyo vitu vipande vipande, ndivyo ufalme huo utakavyopondaponda na kuvunjavunja nyingine zote. Kama vile ulivyoona kuwa kwa sehemu nyayo na vidole vilikuwa vya udongo wa mfinyanzi uliochomwa na kwa sehemu nyingine chuma, hivyo huu utakuwa ufalme uliogawanyikagawanyika, hata hivyo kutakuwa na baadhi zenye nguvu za chuma ndani yake, kama vile ulivyoona chuma imechanganywa na udongo wa mfinyanzi. Kama vile vidole vyake vya miguu vilikuwa kwa sehemu chuma na sehemu udongo wa mfinyanzi, hivyo ufalme huo kwa sehemu utakuwa na nguvu na kwa sehemu udhaifu. Kama vile ulivyoona chuma kikiwa kimechanganyikana na udongo wa mfinyanzi uliochomwa, ndivyo watu watakavyokuwa mchanganyiko wala hawatabaki kuwa wameungana tena kama vile chuma kisivyoweza kuchanganyikana na udongo wa mfinyanzi. “Katika siku za wafalme hao, Mungu wa mbinguni atauweka ufalme ambao kamwe hautaangamizwa, wala hautaachiwa taifa jingine. Utaziponda zile falme zote na kuzikomesha, bali wenyewe utadumu milele. Hii ndiyo maana ya maono ya jiwe lililochongwa kutoka mlimani, lakini si kwa mikono ya mwanadamu, lile jiwe ambalo lilivunja chuma, shaba, udongo wa mfinyanzi, fedha na dhahabu vipande vipande. “Mungu Mkuu amemwonyesha mfalme kile kitakachotokea wakati ujao. Ndoto hii ni ya kweli na tafsiri yake ni ya kuaminika.”
”Ndipo Mfalme Nebukadneza akaanguka kifudifudi mbele ya Danieli kumpa heshima na kuagiza kwamba wamtolee Danieli sadaka na uvumba. Mfalme akamwambia Danieli, “Hakika Mungu wako ni Mungu wa miungu na Bwana wa wafalme na mfunuaji wa siri zote, kwa maana umeweza kufunua siri hii.” Ndipo mfalme akamweka Danieli kwenye nafasi ya juu na kumpa zawadi nyingi tele. Akamfanya kuwa mtawala wa jimbo lote la Babeli na kumweka kuwa mkuu wa wote wenye hekima. Zaidi ya hayo, kwa ombi la Danieli mfalme akawateua Shadraki, Meshaki na Abednego kuwa wasimamizi wa jimbo la Babeli, huku Danieli akibaki katika ukumbi wa kifalme.
”Mfalme Nebukadneza alitengeneza sanamu ya dhahabu, yenye kimo cha dhiraa sitini na upana wake dhiraa sita, akaisimamisha kwenye tambarare ya Dura katika jimbo la nchi ya Babeli. Kisha mfalme akaita wakuu, wasimamizi, watawala, washauri, watunza hazina, waamuzi, mahakimu na maafisa wengine wote wa jimbo kuja kuizindua sanamu ambayo Mfalme Nebukadneza alikuwa ameisimamisha. Basi wakuu, wasimamizi, watawala, washauri, watunza hazina, waamuzi, mahakimu na maafisa wengine wa jimbo walikusanyika kwa ajili ya kuizindua sanamu ile ambayo mfalme alikuwa ameisimamisha, nao wakasimama mbele ya hiyo sanamu. Ndipo mpiga mbiu akatangaza kwa sauti kubwa, kusema, “Enyi watu wa kabila zote, mataifa na watu wa kila lugha, hili ndilo mnaloamriwa kulifanya: Mara mtakaposikia sauti ya baragumu, filimbi, marimba, zeze, kinubi, zumari na aina zote za sauti za ala za uimbaji, lazima mwanguke chini na kuabudu sanamu ya dhahabu ambayo Mfalme Nebukadneza ameisimamisha. Mtu ye yote ambaye hataanguka chini na kuiabudu sanamu hiyo, atatupwa saa iyo hiyo ndani ya tanuru iwakayo moto.” Kwa hiyo, mara waliposikia sauti ya baragumu, filimbi, kinubi, zeze, kinanda na aina zote za ala za uimbaji, watu wa kabila zote, mataifa na watu wa kila lugha wakaanguka chini na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu ambayo Mfalme Nebukadneza alikuwa ameisimamisha.
”Wakati huo baadhi ya Wakaldayo walijitokeza na kuwashtaki Wayahudi. Wakamwambia Mfalme Nebukadneza, “Ee mfalme, uishi milele! Ee mfalme, umetoa amri kwamba kila mmoja atakayesikia sauti ya baragumu, filimbi, kinubi, zeze, kinanda, zumari na aina zote za ala za uimbaji lazima aanguke chini na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu, na kwamba ye yote ambaye hataanguka chini na kuiabudu atatupwa saa iyo hiyo ndani ya tanuru iwakayo moto. Lakini wako baadhi ya Wayahudi ambao umewaweka juu ya mambo ya jimbo la Babeli: yaani, Shadraki, Meshaki na Abednego, ambao hawakujali wewe, Ee mfalme. Hawaitumikii miungu yako wala kuiabudu ile sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.” Mfalme Nebukadneza akiwa amekasirika na mwenye ghadhabu kali, akawaita Shadraki, Meshaki na Abednego. Hivyo watu hawa wakaletwa mbele ya mfalme, naye Nebukadneza akawauliza, “Je, ni kweli kwamba wewe Shadraki, Meshaki na Abednego hamuitumikii miungu yangu wala kuiabudu sanamu ya dhahabu niliyoisimamisha? Basi wakati mtakaposikia sauti ya baragumu, filimbi, marimba, zeze, kinubi, zumari na aina zote za ala za uimbaji, kama mtakuwa tayari kusujudu na kuiabudu hiyo sanamu niliyoitengeneza, vyema sana. Lakini kama hamtaiabudu, mtatupwa saa iyo hiyo ndani ya tanuru iwakayo moto. Naye ni mungu yupi atakayeweza kuwaokoa ninyi, kutoka katika mkono wangu?”
”Shadraki, Meshaki na Abednego wakamjibu mfalme, “Ee Nebukadneza, hatuhitaji kujitetea wenyewe mbele zako kuhusu jambo hili, ikiwa tutatupwa ndani ya tanuru iwakayo moto, Mungu tunayemtumikia anaweza kutuokoa na moto, naye atatuokoa kutoka mkononi mwako, Ee mfalme. Lakini hata ikiwa hatatuokoa, Ee mfalme, tunataka ufahamu kwamba, hatutaitumikia miungu yako wala kuiabudu sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.” Ndipo Nebukadneza akawa na ghadhabu kali sana kwa Shadraki, Meshaki na Abednego, nayo nia yake ikabadilika juu yao. Akaagiza tanuru ichochewe moto mara saba kuliko kawaida yake na kuwaamuru baadhi ya askari wake wenye nguvu kuliko wengine wote katika jeshi lake kuwafunga Shadraki, Meshaki na Abednego na kuwatupa ndani ya tanuru iwakayo moto. Hivyo watu hawa, walifungwa na kutupwa ndani ya tanuru iwakayo moto wakiwa wamevaa majoho yao, suruali, vilemba na nguo zao nyingine. Amri ya mfalme ilikuwa ya haraka sana na tanuru ilikuwa na moto mkali kiasi kwamba miali ya moto iliwaua wale askari waliowachukuwa Shadraki, Meshaki na Abednego. Watu hawa watatu, wakiwa wamefungwa kwa uthabiti sana, walianguka ndani ya tanuru iwakayo moto.
”Ndipo Mfalme Nebukadneza akashangaa akainuka kwa haraka na kuwauliza washauri wake, “Je, hawakuwa watu watatu ambao tuliwafunga na kuwatupa ndani ya moto?” Washauri wakajibu, “Hakika, Ee mfalme.” Mfalme akasema, “Tazama! Naona watu wanne wakitembea-tembea ndani ya moto, hawakufungwa na hawakudhurika, naye mtu yule wanne anaonekana kama mwana wa miungu.” Ndipo Nebukadneza akaukaribia mdomo wa ile tanuru iwakayo moto na kupaza sauti, “Shadraki, Meshaki na Abednego, watumishi wa Mungu Aliye Juu Sana, tokeni! Njoni huku!” Ndipo Shadraki, Meshaki na Abednego wakatoka ndani ya moto. Nao maliwali, wasimamizi, watawala na washauri wa kifalme wakakusanyika kuwazunguka. Waliona kwamba moto haukudhuru miili yao, wala unywele wa vichwa vyao haukuungua, majoho yao hayakuungua, wala hapakuwepo na harufu ya moto kwenye miili yao.
”Ndipo Nebukadneza akasema, “Ahimidiwe Mungu wa Shadraki, Meshaki na Abednego, ambaye amemtuma malaika wake na kuwaokoa watumishi wake. Waliomtumaini na kutoogopa amri ya mfalme nao wakawa tayari kufa kuliko kutumikia au kuabudu mungu mwingine ye yote isipokuwa Mungu wao. Kwa hiyo ninaamuru kwamba watu wa taifa lo lote au lugha yo yote watakaosema kitu cho chote dhidi ya Mungu wa Shadraki, Meshaki na Abednego wakatwe vipande vipande na nyumba zao zifanywe kuwa malundo ya kokoto, kwa maana hakuna mungu mwingine awezaye kuokoa namna hii.” Kisha mfalme akawapandisha vyeo Shadraki, Meshaki na Abednego katika jimbo la Babeli.
”Mfalme Nebukadneza, Kwa kabila za watu, mataifa na watu wa kila lugha, wanaoishi katika ulimwengu wote: Amani na mafanikio yawe kwenu! Ni furaha yangu kuwaambia kuhusu ishara ya miujiza na maajabu ambayo Mungu Aliye Juu Sana amenifanyia. Tazama jinsi ishara zake zilivyo kuu, jinsi maajabu yake yalivyo na nguvu! Ufalme wake ni ufalme wa milele; enzi yake hudumu kutoka kizazi hadi kizazi.
”“ ‘Uamuzi huu umetangazwa na walinzi, hukumu hii imetangazwa na watakatifu, ili walio hai wajue kuwa Aliye Juu Sana ndiye anayetawala juu ya falme zote za wanadamu, naye humpa ye yote amtakaye na kumtawaza juu yake hata yeye aliye mnyonge sana miongoni mwa wanadamu.’
”Wewe utafukuzwa mbali na wanadamu, nawe utaishi pamoja na wanyama pori, utakula manyasi kama ng'ombe na kuloana kwa umande wa mbinguni. Nyakati saba zitapita juu yako, mpaka utakapokubali kuwa Yeye Aliye Juu Sana ndiye anayetawala juu ya falme za wanadamu, naye humtawaza ye yote amtakaye.
”Kwa hiyo, Ee mfalme, uwe radhi kupokea shauri langu: Acha dhambi zako kwa kutenda yaliyo haki, ukaache uovu wako uwe na huruma kwa walioonewa. Hivyo itawezekana baada ya hayo mafanikio yako yakaendelea.”
”Haya yote yalimpata Mfalme Nebukadneza. Miezi kumi na miwili baadaye, mfalme alipokuwa akitembea juu ya paa la jumba la kifalme la Babeli, alisema, “Je, huu si Babeli mji mkuu nilioujenga kama makao ya kifalme, kwa uwezo wangu mkubwa na kwa ajili ya utukufu wa enzi yangu?” Maneno hayo yalikuwa bado katika midomo yake wakati sauti ilipokuja kutoka mbinguni, ikisema, “Mfalme Nebukadneza, hiki ndicho kilichoamriwa kwa ajili yako: Mamlaka yako ya kifalme yameondolewa kutoka kwako. Utafukuzwa mbali na wanadamu ukaishi pamoja na wanyama pori, utakula manyasi kama ng'ombe. Nyakati saba zitapita juu yako, mpaka utakapokubali kuwa Yeye Aliye Juu Sana ndiye anayetawala juu ya falme za wanadamu, naye humtawaza ye yote amtakaye.” Papo hapo yale yaliyokuwa yamesemwa kuhusu Nebukadneza yakatimia. Alifukuzwa mbali na wanadamu, akala majani kama ng'ombe. Mwili wake uliloweshwa kwa umande wa mbinguni mpaka nywele zake zikakua kama manyoya ya tai na kucha zake kama makucha ya ndege.
”Mwisho wa huo wakati, mimi Nebukadneza, niliinua macho yangu kuelekea mbinguni, nazo fahamu zangu zikanirudia. Ndipo nikamsifu Yeye Aliye Juu Sana, nikamheshimu na kumhimidi yeye aishiye milele. Utawala wake ni utawala wa milele; ufalme wake hudumu kutoka kizazi na kizazi. Mataifa yote ya dunia yanahesabiwa kuwa si kitu. Hufanya kama atakavyo kwa majeshi ya mbinguni na kwa mataifa ya dunia. Hakuna anayeweza kuuzuia mkono wake au kumwambia, “Umefanya nini wewe?” Wakati huo huo fahamu zangu ziliponirudia, heshima yangu na fahari yangu nikarudishiwa kwa ajili ya utukufu wa ufalme wangu. Washauri wangu na wakuu wangu walikuja kunitafuta, nami nikarudishwa kwenye kiti changu cha ufalme hata nikawa mkuu kuliko mwanzoni. Basi mimi, Nebukadneza, humhimidi, humtukuza na kumsifu Mfalme wa mbinguni, kwa sababu kila kitu afanyacho ni haki na njia zake zote ni adili. Nao waendao kwa kiburi anaweza kuwashusha.
”Yuko mtu katika ufalme wako ambaye ana Roho ya Miungu Mitakatifu ndani yake. Wakati wa baba yako, mtu huyo alionekana kuwa na ufahamu, akili na hekima kama ile ya miungu. Mfalme Nebukadneza baba yako, yaani nasema mfalme baba yako, alimtuma kuwa mkuu wa waganga, wasihiri, wanajimu na waaguzi.
”“Ee mfalme, Mungu Aliye Juu Sana alimpa baba yako Nebukadneza utawala, ukuu, utukufu na fahari. Kwa sababu ya nafasi ya juu aliyompa baba yako, kabila zote za watu, mataifa na watu wa kila lugha walimhofu na kumwogopa. Wale ambao mfalme alitaka kuwaua, aliwaua, wale aliotaka kuwaacha hai, aliwaacha hai, wale aliotaka kuwapandisha cheo, aliwapandisha, aliotaka kuwashusha, aliwashusha. Lakini moyo wake ulipokuwa na majivuno na kuwa mgumu kwa kiburi, aliondolewa kutoka kwenye kiti chake cha utawala cha kifalme na kuvuliwa utukufu wake. Akafukuzwa mbali na wanadamu na kupewa akili ya mnyama, akaishi pamoja na punda-mwitu, akala majani kama ng'ombe, nao mwili wake ukaloweshwa kwa umande wa mbingu, mpaka alipotambua kwamba Mungu Aliye Juu Sana ndiye mtawala juu ya falme za wanadamu na kwamba humtawaza juu yao ye yote amtakaye.
”“Lakini wewe mwanawe, Ee Belshaza, hukujinyenyekeza, ingawa ulifahamu haya yote. Badala yake, umejiinua dhidi ya Bwana wa mbingu. Uliletewa vikombe vya Hekalu lake, nawe na wakuu wako, wake zako na masuria wako mlivitumia kwa kunywea mvinyo. Ukaisifu miungu ya fedha, ya dhahabu, ya shaba, ya chuma, ya miti na ya mawe, miungu ambayo haiwezi kuona au kusikia wala kufahamu. Lakini hukumheshimu Mungu ambaye anaushikilia uhai wako na njia zako zote mkononi mwake. Kwa hiyo ameutuma mkono ule ulioandika maneno. “Haya ndiyo maneno yaliyoandikwa: MENE, MENE, TEKELI NA PERESI “Hii ndiyo maana ya maneno haya: Mene: Mungu amezihesabu siku za utawala wako na kuukomesha. Tekeli: Wewe umepimwa katika mizani na umeonekana umepungua. Peresi: Ufalme wako umegawanywa na kupewa Wamedi na Waajemi.” Ndipo kwa amri ya Belshaza, Danieli akavikwa nguo za zambarau na mkufu wa dhahabu shingoni, tena akatangazwa kuwa mtawala wa tatu kutoka juu katika ufalme. Usiku ule ule Belshaza, mfalme wa Babeli akauawa, naye Dario Mmedi akashika ufalme akiwa na miaka sitini na miwili.
”Ilimpendeza Dario kuteua wakuu 120 kutawala katika ufalme wake wote, pamoja na wasimamizi watatu juu yao, ambao mmoja wao alikuwa Danieli. Wakuu walitoa hesabu kwa hao wasimamizi ili mfalme asipate hasara. Basi Danieli alijidhihirisha mwenyewe, miongoni mwa wasimamizi na wakuu kwa sifa zake za kipekee hata mfalme akapanga kumweka juu ya ufalme wote. Kwa hili, wakuu na wasimamizi wakajaribu kutafuta sababu za kumshitaki Danieli kuhusu usimamizi wake wa shughuli za serikali, lakini hawakuweza kufanikiwa. Hawakuweza kupata kosa kwake, kwa sababu alikuwa mwaminifu na wala hakupatikana na upotovu wala uzembe. Mwishoni watu hawa walisema, “Kamwe hatutapata msingi kwa ajili ya mashtaka dhidi ya mtu huyu Danieli isipokuwa kile kinachohusiana na sheria ya Mungu wake.” Basi wasimamizi na wakuu wakaingia kwa mfalme kama kikundi wakasema, “Ee Mfalme Dario, uishi milele! Wasimamizi wa kifalme, wasaidizi, wakuu, washauri na watawala wote wamekubaliana kwamba mfalme atoe sheria na kukazia amri kuwa ye yote atakayemwomba Mungu ye yote au mwanadamu katika muda huu wa siku thelathini zijazo, isipokuwa kwako wewe, Ee mfalme, atatupwa ndani ya tundu la simba. Sasa, Ee mfalme, toa amri na uiandike ili kwamba isiweze kubadilishwa, kwa kulingana na sheria za Wamedi na Waajemi, ambazo haziwezi kubatilishwa.” Hivyo Mfalme Dario akaiweka amri hiyo katika maandishi.
”Ikawa Danieli alipofahamu kuwa amri ile imetangazwa, alikwenda nyumbani kwenye chumba chake cha ghorofani ambako madirisha yalifunguka kuelekea Yerusalemu. Mara tatu kwa siku akapiga magoti na kuomba, akimshukuru Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya mwanzoni. Ndipo watu hawa wakamwendea kama kikundi na kumkuta Danieli anaomba na kumsihi Mungu kwa ajili ya msaada. Basi wakaenda kwa mfalme na kusema naye kuhusu amri ya kifalme: “Je, hukutangaza amri kwamba kwa muda huu wa siku thelathini zijazo mtu ye yote ambaye atamwomba mungu au mwanadamu ye yote isipokuwa wewe, Ee mfalme, angetupwa ndani ya tundu la simba?” Mfalme akajibu, “Amri ndivyo ilivyo, kulingana na sheria za Wamedi na Waajemi, ambazo haziwezi kutanguka.” Ndipo wakamwambia mfalme, “Danieli, ambaye ni mmoja wa watu wa uhamisho kutoka Yuda hakuheshimu, Ee mfalme, wala hajali amri uliyoiweka kwa maandishi. Angalia anaomba mara tatu kwa siku.” Wakati mfalme aliposikia hili, akahuzunishwa mno, akakusudia kumwokoa Danieli, naye akafanya kila jitihada ya kumwokoa hadi jua likatua. Ndipo wale watu wakamwendea mfalme kama kikundi na kumwambia, “Ee mfalme, kumbuka kwamba kulingana na sheria ya Wamedi na Waajemi hakuna amri wala sheria ambayo mfalme ameitoa inayoweza kubadilishwa.”
”Basi mfalme akatoa amri, nao wakamleta Danieli wakamtupa ndani ya tundu la simba. Mfalme akamwambia Danieli, “Mungu wako unayemtumikia daima na akuokoe!” Jiwe likaletwa na kuwekwa kwenye mdomo wa tundu, naye mfalme akalitia muhuri kwa pete yake mwenyewe pamoja na kwa pete za wakuu wake, ili kwamba hali ya Danieli isiweze kubadilishwa. Kisha mfalme akarudi kwenye jumba lake la kifalme na usiku kucha hakula chakula wala kutumia viburudisho alivyoletewa. Wala hakuweza kulala.
”Mapema alfajiri mfalme akaondoka na kuharakisha kwenda kwenye tundu la simba. Wakati alipokaribia lile tundu, alimwita Danieli kwa sauti ya uchungu, “Danieli, mtumishi wa Mungu aliye hai, je, Mungu wako unayemtumikia daima, ameweza kukuokoa na simba hawa?” Danieli akajibu, “Ee mfalme, uishi milele! Mungu wangu alimtuma malaika wake, naye akafunga vinywa vya hawa simba. Hawajanidhuru, kwa sababu nilionekana sina hatia mbele zake. Wala kamwe sijafanya jambo lo lote baya mbele yako, Ee mfalme.” Mfalme akafurahi mno naye akatoa amri Danieli atolewe kwenye lile tundu. Danieli alipotolewa katika lile tundu, hakukutwa na jeraha lo lote, kwa sababu alikuwa amemtumaini Mungu wake.
”Kwa amri ya mfalme wale watu waliokuwa wamemshtaki Danieli kwa uongo waliletwa na kutupwa ndani ya lile tundu la simba, pamoja na wake zao na watoto wao. Nao kabla hawajafika chini kwenye sakafu ya lile tundu, simba wakawakamata na kusaga mifupa yao yote. Kisha Mfalme Dario akawaandikia kabila zote za watu, mataifa na watu wa kila lugha katika nchi yote: “Ninyi na mstawi sana! “Natoa amri hii kwamba katika kila sehemu ya ufalme wangu lazima watu wamwogope na kumheshimu Mungu wa Danieli. “Kwa maana yeye ni Mungu aliye hai naye hudumu milele, ufalme wake hautaangamizwa, nao utawala wake kamwe hauna mwisho. Huponya na kuokoa: hufanya ishara na maajabu mbinguni na duniani. Amemponya Danieli kutoka katika nguvu za simba.” Hivyo Danieli akastawi wakati wa utawala wa Dario na utawala wa Koreshi, Mwajemi.
”Akapewa mamlaka, utukufu na ufalme wenye nguvu, watu, kabila zote za mataifa na watu wa kila lugha wakamwabudu. Utawala wake ni utawala wa milele ambao hautapita, nao ufalme wake ni ule ambao kamwe hautaangamizwa.
”‘Hao wanyama wakubwa wanne ni falme nne zitakazoinuka duniani. Lakini watakatifu wa Yeye Aliye Juu Sana watapokea ufalme na kuumiliki milele, naam, milele na milele.’
”“Kisha nilitaka kufahamu maana ya kweli ya mnyama yule wa nne, ambaye alikuwa tofauti na wale wengine wote tena wa kutisha mwenye meno ya chuma na makucha ya shaba, mnyama ambaye alipondaponda na kuangamiza wahanga wake na kukanyaga cho chote kilichosalia. Pia mimi nilitaka kujua kuhusu zile pembe kumi juu ya kichwa chake na pia kuhusu ile pembe nyingine iliyojitokeza, ambayo mbele yake zile tatu za mwanzoni zilianguka, ile pembe ambayo ilionekana kuvutia macho zaidi kuliko zile nyingine na ambayo ilikuwa na macho na kinywa kilichonena kwa majivuno.
”“Alinipa maelezo haya: ‘Mnyama wa nne ni ufalme wa nne ambao utatokea duniani. Utakuwa tofauti na falme nyingine zote nao utaharibu dunia nzima, ukiikanyaga chini na kuipondaponda. Zile pembe kumi ni wafalme kumi watakaotokana na ufalme huu. Baada yao mfalme mwingine atainuka, ambaye atakuwa tofauti na wale waliotangulia, naye atawaangusha wafalme watatu.
”Atanena maneno kinyume cha Yeye Aliye Juu Sana na kuwaonea watakatifu wake, huku akijaribu kubadili sikukuu zao takatifu pamoja na sheria. Watakatifu watatiwa chini ya mamlaka yake kwa wakati, nyakati mbili, na nusu wakati. “ ‘Lakini ndipo mahakama itakapokaa kuhukumu, nayo mamlaka yake yataondolewa na kuangamizwa kabisa milele.
”Ndipo ufalme, mamlaka na ukuu wa falme chini ya mbingu yote utakabidhiwa kwa watakatifu, watu wa Yeye Aliye Juu Sana. Ufalme wake utakuwa ufalme wa milele, nao watawala wote watamwabudu na kumtii yeye.’
”Wafalme hawa wawili, mioyo yao ikiwa imekusudia mabaya wataketi kwenye meza moja na kudanganyana wao kwa wao, lakini pasipo faida, kwa sababu bado mwisho utakuja katika wakati ulioamuriwa.
”“Katika wakati huo Mikaeli, mtawala mkuu ambaye huwalinda watu wako, atainuka. Kutakuwako wakati wa taabu ambao haujatokea tangu mwanzo wa mataifa hadi wakati huo. Lakini wakati huo, watu wako, kila mmoja ambaye jina lake litakutwa limeandikwa kwenye kitabu, ataokolewa.
”Wanaweka Wafalme bila idhini yangu, wamechagua wakuu bila kibali changu. Kwa fedha zao na dhahabu wamejitengenezea sanamu kwa ajili ya maangamizi yao wenyewe.
”“Ee Israeli, Umeharibiwa, kwa sababu wewe u kinyume nami, kinyume na msaidizi wako. Yuko wapi mfalme wako, ili apate kukuokoa? Wako wapi watawala wako katika miji yako yote ambao ulisema kuwahusu, ‘Nipe mfalme na wakuu’? Hivyo katika hasira yangu nilikupa mfalme na katika ghadhabu yangu nilimwondoa.
”Watu wa Ninawi wakamwamini Mungu, wakatangaza kufunga, watu wote kuanzia mkubwa sana hadi yule mdogo kabisa, wakavaa nguo za gunia. Habari zilipomfikia mfalme wa Ninawi, aliondoka kwenye kiti chake cha enzi, akavua majoho yake ya kifalme, akajifunika nguo ya gunia kisha akaketi chini mavumbini. Ndipo akatoa tangazo katika Ninawi yote: “Kwa amri ya mfalme na wakuu wake: “Msiruhusu mtu ye yote au mnyama, makundi ya ng'ombe au wanyama wengine wafugwao, kuonja kitu cho chote, msiwaruhusu kula wala kunywa. Bali wanadamu na wanyama wafunikwe kwa nguo za gunia. Kila mmoja afanye hima kumwomba Mungu. Waziache njia zao mbaya na udhalimu ulio mikononi mwao.
”Kisha nikasema, “Sikilizeni enyi viongozi wa Yakobo, enyi watawala wa nyumba ya Israeli. Je, hampaswi kujua hukumu, ninyi mnaochukia mema na kupenda maovu; ninyi mnaowachuna watu wangu ngozi na kuondoa nyama kwenye mifupa yao; ninyi mnaokula nyama ya watu wangu, mnaowachuna ngozi na kuvunja mifupa yao vipande vipande; mnaowakatakata kama nyama ya kuwekwa kwenye sufuria na kama nyama ya kuwekwa kwenye chungu?”
”Sikieni hili, enyi viongozi wa nyumba ya Yakobo, enyi watawala wa nyumba ya Israeli, mnaodharau haki na kupotosha kila lililo sawa; mnaojenga Sayuni kwa kumwaga damu na Yerusalemu kwa uovu.
”Atahukumu kati ya mataifa mengi na ataamua migogoro ya mataifa yenye nguvu na yaliyo mbali. Watafua panga zao ziwe majembe ya kulimia na mikuki yao kuwa miundu ya kukatia matawi. Taifa halitachukua upanga dhidi ya taifa, wala hawatajifunza vita tena.
”“Lakini wewe, Bethlehemu Efrathi, ingawa u mdogo miongoni mwa koo za Yuda, kutoka kwako atatokea kwa ajili yangu yeye atakayekuwa mtawala katika Israeli, ambaye asili yake ni kutoka zamani, kutoka milele.”
”BWANA atakuwa mfalme juu ya dunia yote. Katika siku hiyo atakuwepo BWANA mmoja na jina lake litakuwa jina pekee.
”Kisha walionusurika katika mataifa yote ambayo yaliushambulia Yerusalemu watakuwa wakipanda Yerusalemu kila mwaka kumwabudu Mfalme, BWANA Mwenye Nguvu Zote na kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda. Ikiwa taifa lo lote la dunia hawatakwenda Yerusalemu kumwabudu Mfalme, BWANA Mwenye Nguvu Zote, mvua haitanyesha kwao. Ikiwa watu wa Misri nao hawatakwenda kushiriki, hawatapata mvua. BWANA ataleta juu yao tauni ile ambayo itawapiga mataifa yale ambayo hayatakwenda kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda. Hii itakuwa adhabu ya Misri na adhabu ya mataifa yote yale ambayo hayatakwenda Yerusalemu kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda.
”Baada ya Yesu kuzaliwa katika mji wa Bethlehemu huko Uyahudi, wakati wa utawala wa Mfalme Herode, wataalamu wa mambo ya nyota kutoka mashariki walifika Yerusalemu wakiuliza, “Yuko wapi huyo aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tumeona nyota yake ikitokea mashariki, nasi tumekuja kumwabudu.” Mfalme Herode aliposikia jambo hili aliingiwa na hofu sana pamoja na watu wote wa Yerusalemu. Herode akawaita pamoja makuhani wakuu na walimu wa sheria, akawauliza ni mahali gani ambapo Kristo angezaliwa. Nao wakamwambia, “Katika Uyahudi, kwa maana hivyo ndivyo ilivyoandikwa na nabii: “ ‘Nawe, Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, wewe si mdogo miongoni mwa watawala wa Yuda, kwa maana kutoka kwako atakuja mtawala atakayekuwa mchungaji wa watu wangu Israeli.’ ”
”Walipokwisha kwenda zao, malaika wa Bwana akamtokea Yosefu katika ndoto akamwambia, “Ondoka, mchukue mtoto na mama yake mkimbilie Misri. Kaeni huko mpaka nitakapowaambia, kwa maana Herode anataka kumtafuta huyu mtoto ili amuue.” Kisha Yosefu akaondoka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake wakati wa usiku, nao wakaenda Misri ambako walikaa mpaka Herode alipokufa. Hili lilikuwa, ili litimie lile lililonenwa na Bwana kwa kinywa cha nabii kusema, “Kutoka Misri nilimwita mwanangu.”
”Herode alipong'amua kwamba wale wataalamu wa nyota wamemshinda kwa akili, alikasirika sana, naye akatoa amri ya kuwaua watoto wote wa kiume wenye umri wa miaka miwili kurudi chini katika mji wa Bethlehemu na sehemu zote za jirani, kufuatana na ule muda alioambiwa na wale wataalamu wa nyota.
”Kwa mara nyingine, ibilisi akamchukua Yesu mpaka kwenye kilele cha mlima mrefu na kumwonyesha falme zote za dunia na fahari zake, kisha akamwambia, “Nitakupa hivi vyote kama ukinisujudia na kuniabudu.” Yesu akamwambia, “Ondoka mbele yangu, Shetani! Kwa maana imeandikwa, ‘Utamwabudu Bwana Mungu wako, nawe utamtumikia yeye peke yake.’ ”
”“Hakuna mtu ye yote awezaye kuwatumikia mabwana wawili, kwa kuwa ama atamchukia huyu na kumpenda yule mwingine, au atashikamana sana na huyu na kumdharau huyu mwingine. Ninyi hamwezi kumtumikia Mungu na Mali.
”Kwa hiyo cho chote ambacho mnataka mtendewe na watu, ninyi nanyi watendeeni vivyo hivyo. Kwa kuwa hii ndiyo Torati na Manabii.
”“Jihadharini na wanadamu, kwa maana watawapeleka katika mabaraza yao na kuwapiga kwenye masinagogi yao, nanyi mtaburutwa mbele ya watawala na wafalme kwa ajili yangu, ili kuwa ushuhuda kwao na mbele ya watu Mataifa. Lakini watakapowapeleka humo, msisumbuke kufikirifikiri mtakalosema, kwa maana mtapewa la kusema wakati huo. Kwa sababu si ninyi mtakaokuwa mkinena, bali ni Roho wa Baba yenu atakayekuwa akinena kupitia kwenu.
”Wakiwatesa katika mji mmoja, kimbilieni mji mwingine. Amin, amin nawaambia, hamtamaliza miji yote ya Israeli kabla Mwana wa Adamu kuja.
”Wakati huo, Mfalme Herode aliyekuwa mtawala alisikia habari kuhusu sifa za Yesu, akawaambia watumishi wake, “Huyu ni Yohana Mbatizaji, amefufuka kutoka kwa wafu! Hiyo ndiyo sababu nguvu za kutenda miujiza zinafanya kazi ndani yake.”
”Herode alikuwa amemkamata Yohana akamfunga na kumweka gerezani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo, ndugu yake, kwa kuwa Yohana alikuwa amemwambia Herode kwamba, “Si halali kwako kuwa na huyo mwanamke.” Herode alitaka sana kumwua Yohana, lakini akaogopa watu kwa maana walimtambua kuwa ni nabii. Katika siku ya kuadhimisha sikukuu ya kuzaliwa kwa Herode, binti wa Herodia alicheza mbele ya watu waliohudhuria akamfurahisha sana Herode kiasi kwamba aliahidi kwa kiapo kumpa huyo binti lo lote atakaloomba. Yeye akiwa amefundishwa na mama yake, huyo binti akasema, “Nipatie kichwa cha Yohana Mbatizaji kwenye sinia.” Mfalme akasikitika, lakini kwa ajili ya kile kiapo alichoapa mbele ya wageni, akaamuru kwamba apatiwe ombi lake. Hivyo akaagiza Yohana Mbatizaji akatwe kichwa mle gerezani. Kichwa chake kikaletwa kwenye sinia, akapewa yule binti, naye akampelekea mama yake.
”Baada ya Yesu na wanafunzi wake kufika Kapernaumu, wakusanya kodi ya Hekalu wakamjia Petro na kumwuliza, “Je, Mwalimu wenu halipi kodi ya Hekalu?” Petro akajibu, “Ndiyo, yeye hulipa.” Petro aliporudi nyumbani, Yesu akawa wa kwanza kulizungumzia, akamwuliza, “Unaonaje Simoni? Wafalme wa dunia hupokea ushuru na kodi kutoka kwa nani? Je, ni kutoka kwa watoto wao au kutoka kwa watu wengine?” Petro akamjibu, “Kutoka kwa watu wengine.” Yesu akamwambia, “Kwa hiyo watoto wao wamesamehewa. Lakini ili tusije tukawaudhi, nenda baharini ukatupe ndoana. Mchukue samaki wa kwanza utakayemvua, fungua kinywa chake nawe utakuta humo fedha, ichukue ukalipe kodi yako na yangu.”
”Tuambie basi, wewe unaonaje? Ni halali kulipa kodi kwa Kaisari au la?” Lakini Yesu akijua makusudi yao mabaya akawaambia, “Enyi wanafiki, kwa nini mnajaribu kunitega? Nionyesheni hiyo sarafu inayotumika kwa kulipia kodi.” Wakamletea dinari. Naye akawauliza, “Sura hii na maandishi haya ni vya nani?” Wakamjibu, “Ni vya Kaisari.” Basi Yesu akawaambia, “Mpeni Kaisari kilicho cha Kaisari, naye Mungu mpeni kilicho cha Mungu.”
”Kwa sababu hii tazama nawapelekea manabii na wenye hekima na walimu. Baadhi yao mtawaua na kuwasulibisha, wengine mtawapiga mijeledi katika masinagogi yenu na wengine mtawafuatia kutoka mji mmoja hadi mji mwingine.
”Mtasikia habari za vita na matetesi ya vita, angalieni msitishike, kwa maana haya hayana budi kutukia, lakini ule mwisho bado. Taifa litainuka dhidi ya taifa na ufalme dhidi ya ufalme. Kutakuwa na njaa na matetemeko ya ardhi sehemu mbalimbali. Haya yote yatakuwa ndio mwanzo wa utungu. “Ndipo mtasalitiwa, ili mteswe na kuuawa, nanyi mtachukiwa na mataifa yote kwa ajili yangu.
”Basi viongozi wa wazee, makuhani na baraza lote wakatafuta ushahidi wa uongo dhidi ya Yesu ili wapate kumwua. Lakini hawakupata jambo lo lote, ingawa mashahidi wengi wa uongo walijitokeza. Hatimaye wakajitokeza mashahidi wawili wa uongo
”Kisha wakamtemea mate usoni na wengine wakampiga ngumi. Wengine walimpiga makofi na kusema, “Tutabirie, wewe Kristo! Ni nani aliyekupiga?”
”Wakati Yesu akiwa amesimama mbele ya mtawala, mtawala akamwuliza, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?” Yesu akasema, “Wewe wasema hivyo.” Lakini viongozi wa makuhani na wazee walipomshtaki, hakujibu neno. Ndipo Pilato akamwuliza, “Je, husikii ni mambo mangapi wanayokushtaki nayo?” Lakini Yesu hakumjibu hata kwa shtaka moja, kiasi kwamba mtawala alishangaa sana.
”Kisha askari wa mtawala wakampeleka Yesu kwenye Praitorio na wakakusanya kikosi kizima cha askari kumzunguka. Wakamvua nguo zake na kumvika vazi la rangi nyekundu, kisha wakasokota taji ya miiba wakaiweka kichwani pake. Wakamwekea fimbo katika mkono wake wa kuume, wakapiga magoti mbele zake na kumdhihaki wakisema “salamu, mfalme wa Wayahudi!” Wakamtemea mate, wakachukua ile fimbo wakampiga kichwani tena na tena. Baada ya kumdhihaki, wakamvua lile vazi, wakamvika tena nguo zake. Kisha wakampeleka ili kumsulibisha.
”Juu ya kichwa chake, kwenye msalaba, wakaandika shtaka lake: HUYU NI YESU, MFALME WA WAYAHUDI.
”“Aliwaokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa mwenyewe! Yeye ni Mfalme wa Israeli! Ashuke sasa kutoka msalabani, tutamwamini.
”Yesu akawajia na kusema, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
”Baada ya Yohana kukamatwa na kutiwa gerezani, Yesu aliingia Galilaya akaanza kuhubiri habari njema ya Mungu, akisema, “Wakati umewadia, Ufalme wa Mungu umekaribia. Tubuni na kuiamini Habari Njema.”
”Mfalme Herode akasikia habari hizi, kwa maana jina la Yesu lilikuwa limejulikana kila mahali. Watu wengine walikuwa wakisema, “Yohana Mbatizaji amefufuka kutoka kwa wafu ndiyo maana uwezo wa kutenda miujiza unafanya kazi ndani yake!” Wengine wakasema, “Yeye ni Eliya.” Nao wengine wakasema, “Yeye ni nabii, kama mmojawapo wa wale manabii wa zamani.” Lakini Herode aliposikia habari hizi, akasema, “Huyo ni Yohana Mbatizaji, niliyemkata kichwa, amefufuka!”
”Kwa kuwa Herode alikuwa ameagiza kwamba Yohana Mbatizaji akamatwe, afungwe na kutiwa gerezani. Alifanya hivi kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo ndugu yake, ambaye alikuwa amemwoa. Yohana alikuwa amemwambia Herode, “Si halali wewe kumwoa mke wa ndugu yako.” Kwa hiyo Herodia alikuwa amemwekea Yohana kinyongo akataka kumwua. Lakini hakuweza, kwa sababu Herode alimwogopa Yohana akijua kwamba ni mtu mwenye haki na mtakatifu, akawa anamlinda. Herode alifadhaika sana alipomsikia Yohana, lakini bado alipenda kumsikiliza. Mfalme Herode alifanya karamu kubwa, wakati wa sikukuu ya kuzaliwa kwake. Akawaalika maafisa wake wakuu, majemadari wa jeshi na watu mashuhuri wa Galilaya. Hatimaye Herodia alipata wasaa aliokuwa akiutafuta. Binti yake Herodia alipoingia na kucheza, akamfurahisha Herode pamoja na wageni wake walioalikwa chakulani. Mfalme Herode akamwambia yule binti, “Niombe kitu cho chote utakacho, nami nitakupa.” Tena akamwahidi kwa kiapo akamwambia, “Cho chote utakachoomba nitakupa, hata kama ni nusu ya ufalme wangu.” Yule binti akatoka nje akaenda kumwuliza mama yake, “Niombe nini?” Mama yake akajibu, “Omba kichwa cha Yohana Mbatizaji.” Yule binti akarudi haraka kwa mfalme akamwambia, “Nataka unipe sasa hivi kichwa cha Yohana Mbatizaji kwenye sinia.” Mfalme akasikitika sana, lakini kwa sababu alikuwa ameapa mbele ya wageni wake hakutaka kumkatalia. Mara mfalme akatuma askari mmojawapo wa walinzi wake kukileta kichwa cha Yohana. Akaenda na kumkata Yohana kichwa humo gerezani, akakileta kichwa chake kwenye sinia na kumpa yule msichana, naye yule msichana akampa mama yake.
”Wakamjia, wakamwambia, “Mwalimu, tunajua ya kuwa wewe ni mtu mwadilifu. Wewe huyumbishwi na wanadamu, kwa kuwa hujali kwamba wao ni nani. Lakini wewe hulifundisha neno la Mungu sawasawa na kweli. Je, ni haki kumlipa Kaisari kodi au la? Je, tulipe kodi au tusilipe?” Lakini Yesu alijua unafiki wao. Akawauliza “Mbona mnajaribu kunitega? Nileteeni hiyo dinari niione.” Wakamletea hiyo sarafu. Naye akawauliza, “Picha hii ni ya nani na maandishi haya ni ya nani?” Wakamjibu, “Ni ya Kaisari.” Ndipo Yesu akawaambia, “Mpeni Kaisari kilicho cha Kaisari, na kilicho cha Mungu mpeni Mungu.” Nao wakamstaajabia sana.
”Msikiapo habari za vita na uvumi wa vita, msiwe na hofu. Mambo haya hayana budi kutukia, lakini ule mwisho bado. Taifa litainuka dhidi ya taifa na ufalme dhidi ya ufalme. Kutakuwa na matetemeko sehemu mbalimbali na njaa. Huu ndio mwanzo wa utungu.
”“Lakini ninyi jihadharini. Kwa maana watawapeleka mahakamani na kuwapiga mijeledi katika masinagogi. Mtashtakiwa mbele ya watawala na wafalme kwa ajili yangu, ili kuwa ushuhuda kwao. Nayo habari njema lazima ihubiriwe kwanza kwa mataifa yote kabla ule mwisho haujawadia. Mtakapokamatwa na kushtakiwa, msisumbuke kuhusu mtakalosema. Semeni tu lo lote mtakalopewa wakati huo, kwa kuwa si ninyi msemao bali ni Roho Mtakatifu.
”Wakampeleka Yesu kwa Kuhani Mkuu, nao viongozi wa makuhani, wazee na walimu wa sheria wakakusanyika pamoja. Petro akamfuata kwa mbali, mpaka kwenye ua wa Kuhani Mkuu. Huko akaketi pamoja na walinzi, akiota moto. Viongozi wa makuhani na wajumbe wote wa Baraza walikuwa wanatafuta ushahidi dhidi ya Yesu ili wapate kumwua, lakini hawakupata. Wengi wakatoa ushahidi wa uongo dhidi yake, lakini maelezo yao hayakukubaliana.
”Kuhani Mkuu akararua mavazi yake, akasema, “Tuna haja gani tena ya mashahidi zaidi? Ninyi mmesikia hayo makufuru. Uamuzi wenu ni nini?” Wote wakamhukumu kwamba anastahili kifo. Kisha baadhi ya watu wakaanza kumtemea mate, wakamfunga kitambaa machoni, wakampiga kwa ngumi na kumwambia, “Tabiri ni nani aliyekupiga!” Walinzi wakamchukua na kumpiga makofi.
”Asubuhi na mapema, viongozi wa makuhani, pamoja na wazee, walimu wa sheria na Baraza lote, wakafikia uamuzi. Wakamfunga Yesu, wakamchukua na kumkabidhi kwa Pilato. Pilato akamwuliza, “Je, wewe ndiye Mfalme wa Wayahudi?” Yesu akajibu, “Wewe umesema.” Viongozi wa makuhani wakamshtaki kwa mambo mengi. Pilato akamwuliza tena, “Je, huna la kujibu? Tazama ni mashtaka mangapi wanayaleta juu yako.” Lakini Yesu hakuendelea kujibu, hivyo Pilato akashangaa.
”Pilato akawauliza, “Mnataka niwafungulie huyu Mfalme wa Wayahudi?”
”Pilato akawauliza tena, “Basi mnataka nifanye nini na huyu mtu mnayemwita Mfalme wa Wayahudi?” Wakapiga kelele wakisema, “Msulibishe!”
”Pilato akitaka kuuridhisha ule umati wa watu, akawafungulia Baraba, naye baada ya kuamuru Yesu achapwe mijeledi, akamtoa ili asulibishwe. Askari wakampeleka Yesu hadi kwenye ukumbi wa ndani wa jumba la kifalme, ndio Praitorio, wakakusanya kikosi kizima cha Askari. Wakamvalisha Yesu joho la zambarau, wakasokota taji ya miiba, wakamvisha kichwani. Wakaanza kumsalimu kwa dhihaka, “Salamu, Mfalme wa Wayahudi!” Wakampiga kwa fimbo ya mwanzi tena na tena kichwani na kumtemea mate. Wakapiga magoti mbele yake wakamsujudia kwa kumdhihaki. Walipokwisha kumdhihaki, wakamvua lile joho la zambarau, wakamvika zile nguo zake mwenyewe. Kisha wakamtoa nje ili wakamsulibishe.
”Tangazo likaandikwa la mashtaka dhidi yake lenye maneno haya: “MFALME WA WAYAHUDI.”
”Basi huyu Kristo, huyu Mfalme wa Wayahudi, ashuke sasa kutoka msalabani, ili tupate kuona na kuamini.” Wale waliosulibiwa pamoja naye pia wakamtukana.
”Yeye atakuwa mkuu, naye ataitwa Mwana wa Aliye Juu Sana. BWANA Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake. Ataimiliki nyumba ya Yakobo milele na ufalme wake hautakuwa na mwisho.”
”Siku zile Kaisari Augusto alitoa amri kwamba watu wote waandikishwe katika ulimwengu wa Kirumi. (Orodha hii ndiyo ya kwanza iliyofanyika wakati Krenio alipokuwa mtawala wa Shamu). Kila mtu alikwenda kuandikishwa katika mji wake alikozaliwa.
”Katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberio, Pontio Pilato akiwa mtawala wa Uyahudi, Herode akiwa mfalme wa Galilaya, Filipo ndugu yake akiwa mfalme wa Iturea na nchi ya Trakoniti na Lisania akiwa mfalme wa Abilene, Anasi na Kayafa wakiwa makuhani wakuu, ndipo neno la Mungu likamjia Yohana, mwana wa Zekaria huko nyikani.
”Lakini Yohana alipomkemea Mfalme Herode kuhusu uhusiano wake na Herodia mke wa ndugu yake na maovu mengine aliyokuwa amefanya, Herode akijumlisha haya yote, akamfunga Yohana gerezani.
”Basi Herode mtawala wa Galilaya akasikia habari za yote yaliyotendeka, naye akafadhaika kwa kuwa baadhi ya watu walikuwa wakisema Yohana Mbatizaji amefufuka. Wengine wakasema Eliya amewatokea, na wengine wakasema kwamba mmoja wa manabii wa kale amefufuka. Herode akasema, “Yohana nilimkata kichwa. Lakini ni nani basi huyu ambaye ninasikia habari zake kuhusu mambo kama haya?” Akatamani sana kumwona.
”Kwa sababu ya jambo hili, Mungu katika hekima yake alisema, ‘Tazama, nitatuma kwao manabii na mitume, nao watawaua baadhi yao na wengine watawatesa.’ Kwa hiyo kizazi hiki kitawajibika kwa ajili ya damu ile ya manabii iliyomwagwa tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu,
”Uwapo njiani na adui yako kwenda kwa hakimu, jitahidi kupatana naye mkiwa njiani. La sivyo, atakupeleka kwa hakimu, naye hakimu atakukabidhi kwa afisa, naye afisa atakutupa gerezani.
”“Hakuna mtumishi awezaye kuwatumikia mabwana wawili. Ama atamchukia mmoja na kumpenda mwingine au atamheshimu mmoja na kumdharau mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu pamoja na Mali.”
”“Akawajibu, ‘Nawaambia kwamba, kila aliye na kitu, ataongezewa, naye yule asiyetumia alicho nacho atanyang'anywa hata kile alicho nacho, lakini wale adui zangu ambao hawakutaka mimi niwe mfalme juu yao, waleteni hapa mkawaue mbele yangu.’ ”
”Je, ni halali sisi kumlipa Kaisari kodi au la?” Lakini Yesu akatambua hila yao, kwa hiyo akawaambia, “Kwa nini ninyi mnanijaribu? Nionyesheni dinari. Je, picha hii na maandishi haya yaliyoko juu yake ni ya nani?” Wakamjibu, “Ni ya Kaisari.” Akawaambia, “Basi mpeni Kaisari kilicho cha Kaisari na Mungu mpeni kilicho cha Mungu.”
”“Lakini kabla yote hayajatokea, watawakamata ninyi na kuwatesa. Watawatia mikononi mwa wakuu wa masinagogi na kufungwa magerezani, nanyi mtapelekwa mbele ya wafalme na watawala kwa ajili ya Jina langu.
”ili mpate kula na kunywa mezani pangu katika karamu ya ufalme wangu na kukaa katika viti vya enzi, mkihukumu makabila kumi na mawili ya Israeli.”
”Wale watu waliokuwa wanamlinda Yesu wakaanza kumdhihaki na kumpiga. Wakamfunga kitambaa machoni na kumwuliza, “Tabiri! Tuambie ni nani aliyekupiga?” Wakaendelea kumtukana kwa matusi mengi. Kulipopambazuka baraza la wazee wa watu, yaani viongozi wa makuhani na walimu wa sheria, wakakutana pamoja, naye Yesu akaletwa mbele yao. Wakamwambia, “Kama wewe ndiye Kristo, tuambie.” Yesu akawajibu, “Hata nikiwaambia hamtaamini.
”Nao wakaanza kumshtaki wakisema: “Tumemwona huyu mtu akipotosha taifa letu, akiwazuia watu wasilipe kodi kwa Kaisari na kujiita kuwa yeye ni Kristo, mfalme.” Basi Pilato akamwuliza Yesu, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?” Yesu akajibu, “Wewe wasema.” Pilato akawaambia viongozi wa makuhani na watu wote waliokuwapo, “Sioni sababu ya kutosha kumshtaki mtu huyu!”
”Askari nao wakaja, wakamdhihaki, wakamletea siki ili anywe. Nao wakamwambia, “Kama wewe ni Mfalme wa Wayahudi, jiokoe mwenyewe.” Kwenye msalaba juu ya kichwa chake, kulikuwa na maandishi haya: HUYU NDIYE MFALME WA WAYAHUDI. Maandishi haya yalikuwa yameandikwa kwa lugha ya Kiyunani, Kilatini na Kiebrania.
”Kwa kuwa sheria ilitolewa kwa mkono wa Mose, lakini neema na kweli imekuja kupitia Yesu Kristo.
”Nathanaeli akamwambia, “Mwalimu, wewe ni Mwana wa Mungu! Wewe ni Mfalme wa Israeli!”
”Basi palikuwa na mtu mmoja Farisayo, jina lake Nikodemo, mmoja wa Baraza la Wayahudi lililotawala. Huyu alimjia Yesu usiku akamwambia, “Rabi, tunajua kuwa wewe ni mwalimu uliyetumwa na Mungu, kwa maana hakuna mtu awezaye kufanya miujiza hii uifanyayo wewe, kama Mungu hayuko pamoja naye.” Yesu akamjibu, “Amin, amin nakuambia, mtu hawezi kuuona Ufalme wa Mungu asipozaliwa mara ya pili.”
”Kwa hiyo Wayahudi wakaanza kumsumbua, kwa sababu alikuwa anafanya mambo kama hayo siku ya Sabato.
”Yesu akijua kwamba walitaka kuja kumfanya awe mfalme wao, kwa nguvu, akajitenga nao akaenda milimani peke yake.
”Siku iliyofuata umati mkubwa uliokuwa umekuja kwenye Sikukuu walisikia kwamba Yesu angekuja Yerusalemu. Basi wakachukua matawi ya mitende wakatoka kwenda kumlaki, huku wakipaza sauti wakisema, “Hosana!” “Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana!” “Amebarikiwa Mfalme wa Israeli!”
”Kwa hiyo Pilato akaingia ndani akamwita Yesu, akamwuliza, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?” Yesu akamjibu, “Je, unauliza swali hili kutokana na mawazo yako mwenyewe au uliambiwa na watu kunihusu mimi?” Pilato akamjibu, “Mimi si Myahudi, ama sivyo? Taifa lako mwenyewe na viongozi wa makuhani wamekukabidhi kwangu. Umefanya kosa gani?” Yesu akajibu, “Ufalme wangu si wa ulimwengu huu. Ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu wafuasi wangu wangenipigania ili nisitiwe mikononi mwa Wayahudi. Lakini kama ilivyo ufalme wangu hautoki hapa ulimwenguni.” Pilato akamwuliza, “Kwa hiyo wewe ni mfalme?” Yesu akajibu, “Wewe wasema kwamba mimi ni mfalme. Kwa kusudi hili nilizaliwa na kwa ajili ya hili nilikuja ulimwenguni ili niishuhudie kweli. Mtu ye yote aliye wa kweli husikia sauti yangu.” Pilato akamwuliza Yesu, “Kweli ni nini?” Baada ya kusema haya Pilato akaenda nje tena akawaambia wale viongozi wa Wayahudi waliomshtaki Yesu, “Sioni kosa lo lote alilotenda mtu huyu. Lakini ninyi mna desturi yenu kwamba wakati wa Pasaka nimwachie huru mfungwa mmoja mnayemtaka. Je, mnataka niwafungulie huyu ‘Mfalme wa Wayahudi?’ ”
”Wakawa wanapanda pale alipo tena na tena, wakisema, “Salamu! Mfalme wa Wayahudi!” Huku wakimpiga makofi usoni.
”Pilato aliposikia haya, akaogopa zaidi. Akaingia tena ukumbini akamwuliza Yesu, “Wewe umetoka wapi?” Lakini Yesu hakumjibu. Pilato akamwambia, “Wewe unakataa kuongea na mimi? Hujui ya kuwa nina mamlaka ya kukuachia huru au kukusulibisha?” Ndipo Yesu akamwambia, “Wewe hungekuwa na mamlaka yo yote juu yangu kama hungepewa kutoka juu. Kwa hiyo yeye aliyenitia mikononi mwako ana hatia ya dhambi iliyo kubwa zaidi.” Tangu wakati huo, Pilato akajitahidi kutafuta njia ya kumfungua Yesu, lakini Wayahudi wakazidi kupiga kelele wakisema, “Ukimwachia huyu mtu, wewe si rafiki wa Kaisari. Mtu ye yote anayedai kuwa mfalme anampinga Kaisari.”
”Basi ilikuwa siku ya Maandalio ya Pasaka, yapata kama saa sita hivi. Pilato akawaambia Wayahudi, “Huyu hapa mfalme wenu!” Wao wakapiga kelele, “Mwondoe! Mwondoe! Msulibishe!” Pilato akawauliza, “Je, nimsulibishe mfalme wenu?” Wale viongozi wa makuhani wakamjibu, “Sisi hatuna mfalme mwingine ila Kaisari.”
”Pilato akaamuru tangazo liandikwe na liwekwe juu kwenye msalaba wa Yesu: “YESU WA NAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI.” Kwa kuwa mahali hapo aliposulibiwa palikuwa karibu na mjini, Wayahudi wengi walisoma maandishi haya yaliyokuwa yameandikwa kwa lugha za Kiebrania, Kiyunani na Kilatini. Viongozi wa makuhani wa Wayahudi wakapinga, wakamwambia Pilato, “Usiandike, ‘Mfalme wa Wayahudi,’ bali andika kwamba, mtu huyu alisema, ‘Mimi ni mfalme wa Wayahudi.’ ” Pilato akawajibu, “Nilichokwisha kuandika, nimeandika!”
”Kisha wakawaita tena ndani na kuwaamuru wasiseme wala kufundisha kamwe kwa hili jina la Yesu. Lakini Petro na Yohana wakajibu, “Amueni ninyi wenyewe iwapo ni haki mbele za Mungu kuwatii ninyi kuliko Mungu. Lakini sisi hatuwezi kuacha kusema yale tuliyoyaona na kuyasikia.” Baada ya vitisho vingi, wakawaacha waende zao. Hawakuona njia yo yote ya kuwaadhibu, kwa sababu ya watu, kwa kuwa watu wote walikuwa wakimsifu Mungu kwa kile kilichokuwa kimetukia.
”Mara Petro na Yohana walipoachiwa, walirudi kwa waumini wenzao wakawaeleza waliyoambiwa na makuhani wakuu na wazee. Watu hao waliposikia hayo, wakainua sauti zao wakamwomba Mungu kwa pamoja, wakisema, “Bwana Mwenyezi, uliyeumba mbingu na nchi na bahari, na vitu vyote vilivyomo. Wewe ulisema kwa Roho Mtakatifu kupitia kwa kinywa cha baba yetu Daudi, mtumishi wako, ukasema: “ ‘Mbona watu Mataifa wanaghadhibika, na kabila za watu zinawaza ubatili? Wafalme wa dunia wamejipanga na watawala wanakusanyika pamoja dhidi ya Bwana na dhidi ya Mpakwa Mafuta wake.’ Ni kweli Herode na Pontio Pilato pamoja na watu Mataifa na Waisraeli, walikusanyika katika mji huu dhidi ya mwanao mtakatifu Yesu uliyemtia mafuta. Wao wakafanya yale ambayo uweza wako na mapenzi yako yalikuwa yamekusudia yatokee tangu zamani. Sasa, Bwana angalia vitisho vyao na utuwezeshe sisi watumishi wako kulinena neno lako kwa ujasiri mkuu.
”Kisha Kuhani Mkuu na wenzake wote waliokuwa pamoja naye (ambao ni wa kundi la Masadukayo), wakiwa wamejawa na wivu, wakawakamata mitume na kuwatia gerezani.
”Lakini wakati wa usiku malaika wa Bwana akaja akafungua milango ya gereza akawatoa nje akawaambia, “Nendeni, mkasimame Hekaluni mkawaambie watu maneno yote ya uzima huu mpya.” Waliposikia haya wakaenda Hekaluni alfajiri wakaendelea kufundisha watu. Kuhani Mkuu na wale waliokuwa pamoja nao walipowasili, alikusanya baraza na wazee wote wa Israeli wakatuma wale mitume waletwe kutoka gerezani. Lakini wale walinzi wa Hekalu walipokwenda gerezani hawakuwakuta wale mitume mle. Kwa hiyo wakarudi na kutoa habari. Wakasema, “Tumekuta milango ya gereza imefungwa sawasawa na maaskari wa gereza wamesimama nje ya mlango, lakini tulipofungua milango hakuwepo mtu ye yote ndani.” Basi mkuu wa walinzi wa Hekalu, viongozi na makuhani waliposikia haya, wakafadhaika na kushangaa sana kwa ajili yao kwamba jambo hili litakuwaje. Ndipo mtu mmoja akaja akawaambia, “Tazameni watu wale mliowatia gerezani wako Hekaluni wakiwafundisha watu.” Ndipo yule mkuu wa walinzi wa Hekalu wakaenda pamoja na maaskari wakawaleta wale mitume, lakini bila ghasia kwa sababu waliogopa kupigwa mawe na watu. Wakiisha kuwaleta hao mitume wakawaamuru kusimama mbele ya baraza. Kuhani Mkuu akawahoji. “Tuliwaonya kwa nguvu msifundishe kwa jina hili, lakini ninyi mmeijaza Yerusalemu yote mafundisho yenu na tena mmekusudia kuleta damu ya mtu huyu juu yetu.” Petro na wale mitume wengine wakajibu, “Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu.
”Wale mitume walitoka nje ya baraza, wakiwa wamejaa furaha kwa sababu wamehesabiwa kustahili kupata aibu kwa ajili ya jina la Yesu.
”Ilikuwa wakati kama huu Mfalme Herode Agripa aliwakamata baadhi ya watu wa kanisa. Akaamuru Yakobo, ndugu yake Yohana, auawe kwa upanga. Alipoona jambo hilo limewapendeza Wayahudi, akaendelea, akamkamata pia Petro. Hii ilitokea wakati wa Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Baada ya kumkamata alimtia gerezani, chini ya ulinzi wa vikundi vinne vya askari, vyenye askari wanne kila kimoja. Herode alikuwa amekusudia kumtoa na kumfanyia mashtaka mbele ya watu baada ya Pasaka. Kwa hiyo Petro akawekwa gerezani, lakini kanisa lilikuwa likimwombea kwa Mungu kwa bidii.
”Usiku ule kabla ya siku ambayo Herode Agripa alikuwa amekusudia kumtoa na kumfanyia mashtaka, Petro alikuwa amelala kati ya askari wawili, akiwa amefungwa kwa minyororo miwili. Nao walinzi wa zamu walikuwa wakilinda penye lango la gereza. Ghafula malaika wa Bwana akatokea na nuru ikamulika mle ndani ya gereza. Yule malaika akampiga Petro ubavuni na kumwamsha, akisema, “Ondoka upesi!” Mara ile minyororo ikaanguka kutoka mikononi mwa Petro. Yule malaika akamwambia, “Vaa nguo zako na viatu vyako.” Petro akafanya hivyo. Kisha akamwambia, “Jifunge vazi lako na unifuate.” Petro alitoka mle gerezani akiwa amefuatana na yule malaika. Hakujua wakati huo kuwa yaliyokuwa yakitukia yalikuwa kweli. Alidhani kuwa anaona maono. Wakapita lindo la kwanza na la pili, ndipo wakafika kwenye lango la chuma linaloelekea mjini. Lango likawafungukia lenyewe, nao wakapita hapo wakatoka nje. Baada ya kutembea umbali wa mtaa mmoja, ghafula yule malaika akamwacha Petro. Ndipo Petro akarudiwa na fahamu, akasema, “Sasa ninajua bila shaka yo yote kuwa Bwana amemtuma malaika wake na kuniokoa kutoka katika makucha ya Herode Agripa na kutoka katika matazamio yote ya Wayahudi.” Mara Petro alipotambua hili alikwenda nyumbani kwa Maria, mama yake Yohana aliyeitwa pia Marko, ambako watu wengi walikuwa wamekutana kwa maombi. Petro alipobisha hodi kwenye lango la nje, mtumishi wa kike jina lake Roda, akaja kumfungulia. Alipoitambua sauti ya Petro, alifurahi mno akarudi bila kufungua na kuwaeleza kwamba, “Petro yuko langoni!” Wakamwambia yule mtumishi wa kike, “Umerukwa na akili.” Alipozidi kusisitiza kuwa ni kweli, wakasema, “Lazima awe ni malaika wake.” Lakini Petro aliendelea kugonga langoni, nao walipofungua lango na kumwona Petro, walistaajabu sana. Yeye akawaashiria kwa mkono wake wanyamaze kimya, akawaeleza jinsi Bwana alivyomtoa gerezani. Naye akaongeza kusema, “Waelezeni Yakobo na ndugu wengine habari hizi.” Kisha akaondoka akaenda sehemu nyingine.
”Kulipokucha kukawa na fadhaa kubwa miongoni mwa wale maaskari kuhusu yaliyomtukia Petro. Baada ya Herode kuamuru atafutwe kila mahali na bila kumpata, aliwahoji wale askari walinzi kisha akatoa amri wauawe. Basi Herode Agripa akatoka Uyahudi akaenda Kaisaria, akakaa huko kwa muda.
”Basi Herode Agripa alikuwa amekasirishwa sana na watu wa Tiro na Sidoni. Hivyo watu wa miji hiyo miwili wakaungana pamoja wakatafuta kukutana naye. Wakiisha kuungwa mkono na Blasto, mtumishi maalum wa Mfalme Herode Agripa aliyeaminika, wakaomba mapatano ya amani maana nchi zao zilitegemea nchi ya huyo mfalme kwa mahitaji yao ya chakula. Katika siku iliyochaguliwa Herode Agripa akavaa mavazi yake ya kifalme, akaketi kwenye kiti chake cha enzi na kuwahutubia watu. Watu waliokuwa wamekusanyika wakapiga kelele, wakisema, “Hii si sauti ya mwanadamu, bali ni ya Mungu.” Ghafula, kwa kuwa Herode Agripa hakumpa Mungu utukufu, malaika akampiga, akaliwa na chango akafa.
”Umati wa watu waliokuwepo wakajiunga katika kuwashambulia Paulo na Sila na wale mahakimu wakaamuru wavuliwe nguo zao na wachapwe viboko. Baada ya kuchapwa sana wakatupwa gerezani na kumwagiza mkuu wa gereza awalinde kikamilifu, kwa kufuata maelekezo haya, yule mkuu wa gereza akawaweka katika chumba cha ndani sana mle gerezani na akawafunga miguu yao kwa minyororo.
”Ilipokaribia usiku wa manane, Paulo na Sila walikuwa wakiomba na kuimba nyimbo za kumsifu Mungu, nao wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. Ghafula pakatokea tetemeko kubwa la ardhi, hata msingi wa gereza ukatikisika. Mara milango ya gereza ikafunguka na ile minyororo iliyowafunga kila mmoja ikafunguka. Yule mkuu wa gereza alipoamka na kuona milango ya gereza iko wazi, akachomoa upanga wake akataka kujiua, akidhani ya kuwa wafungwa wote wametoroka. Lakini Paulo akapiga kelele kwa sauti kubwa, akasema, “Usijidhuru kwa maana sisi sote tuko hapa!” Yule askari wa gereza akaagiza taa ziletwe, akaingia ndani ya kile chumba cha gereza, akapiga magoti akitetemeka mbele ya Paulo na Sila. Kisha akawaleta nje akisema, “Bwana zangu, nifanye nini ili nipate kuokoka?”
”Kulipopambazuka wale mahakimu wakawatuma maafisa wao kwa mkuu wa gereza wakiwa na agizo linalosema, “Wafungue wale watu, waache waende zao.” Mkuu wa gereza akamwambia Paulo “Mahakimu wameagiza niwaache huru, kwa hiyo tokeni.” Lakini Paulo akawaambia wale maafisa, “Wametupiga hadharani bila kutufanyia mashtaka na kutuhoji, nao wakatutupa gerezani, hata ingawa sisi ni raia wa Rumi. Nao sasa wanataka kututoa gerezani kwa siri? Hapana! Wao na waje wenyewe watutoe humu gerezani.” Wale maafisa wakarudi na kuwaambia wale mahakimu maneno haya, wakaogopa sana walipofahamu kuwa Paulo na Sila ni raia wa Rumi. Kwa hiyo wakaja wakawaomba msamaha, wakawatoa gerezani, wakawaomba waondoke katika ule mji. Baada ya Paulo na Sila kutoka gerezani walikwenda nyumbani kwa Lidia, ambapo walikutana na wale ndugu walioamini, wakawatia moyo, ndipo wakaondoka.
”Lakini walipowakosa wakamburuta Yasoni na ndugu wengine mbele ya maafisa wa mji, wakipiga kelele: “Watu hawa ni wale walioupindua ulimwengu wamekuja huku nako, naye Yasoni amewakaribisha nyumbani mwake. Hawa wote wanaasi amri za Kaisari wakisema yuko mfalme mwingine aitwaye Yesu.” Waliposikia haya, ule umati wa watu na maafisa wa mji wakaongeza ghasia.
”Kutoka kwa mtu mmoja, yeye aliumba mataifa yote ya wanadamu ili waikalie dunia yote, naye akaweka nyakati za kuishi.
”yule jemadari akaamuru Paulo aingizwe kwenye ngome. Akaelekeza kwamba achapwe viboko na aulizwe ili kujua kwa nini watu walikuwa wanampigia kelele namna hiyo. Lakini walipokwisha kumfunga kwa kamba za ngozi ili wamchape viboko, Paulo akamwambia kiongozi wa maaskari aliyekuwa amesimama pale karibu naye, “Je, ni halali kwenu kwa mujibu wa sheria kumchapa mtu ambaye ni raia wa Rumi hata kabla hajapatikana na hatia?” Yule askari aliposikia maneno haya, alimwendea yule jemadari na kumwambia, “Unataka kufanya nini? Kwa maana huyu mtu ni raia wa Rumi.” Yule jemadari akaja akamwuliza Paulo, “Niambie, wewe ni raia wa Rumi?” Paulo akajibu, “Naam, hakika ndiyo.” Ndipo yule jemadari akasema, “Mimi ilinigharimu kiasi kikubwa cha fedha kupata uraia wangu.” Paulo akasema “Lakini mimi ni raia wa Rumi kwa kuzaliwa.” Mara wale waliokuwa wanataka kumhoji wakajiondoa haraka na yule jemadari akaingiwa na hofu, alipotambua ya kuwa amemfunga Paulo, ambaye ni raia wa Rumi kwa minyororo. Kesho yake, kwa kuwa yule Jemadari alitaka kujua hakika kwa nini Paulo alikuwa anashutumiwa na Wayahudi, alimfungua na kuwaagiza viongozi wa makuhani na baraza lote likutane. Kisha akamleta Paulo akamsimamisha mbele yao.
”Paulo akawakazia macho wale wajumbe wa baraza, akasema, “Ndugu zangu, nimetimiza wajibu wangu kwa Mungu kwa dhamiri safi kabisa hadi leo.” Kwa ajili ya jambo hili Kuhani Mkuu Anania akaamuru wale waliokuwa karibu na Paulo wampige kofi kinywani. Ndipo Paulo akamwambia, “Mungu atakupiga wewe, ewe ukuta uliopakwa chokaa! Wewe umeketi hapo ili kunihukumu kwa mujibu wa sheria, lakini wewe mwenyewe unakiuka sheria kwa kuamuru kwamba nipigwe kinyume cha sheria!” Wale watu waliokuwa wamesimama karibu na Paulo wakamwambia, “Je, wewe wathubutu kumtukana Kuhani Mkuu wa Mungu?” Paulo akajibu, “Ndugu zangu, sikujua kwamba yeye alikuwa Kuhani Mkuu. Kwa maana imeandikwa, ‘Usimnenee mabaya kiongozi wa watu wako.’ ”
”Paulo alipotambua ya kuwa baadhi yao walikuwa Masadukayo na wengine ni Mafarisayo, akapaza sauti kwenye baraza, “Ndugu zangu, mimi ni Farisayo, mwana Farisayo. Hapa nimeshtakiwa kuhusu tumaini langu katika ufufuo wa wafu.” Aliposema haya, farakano likaanza kati ya Mafarisayo na Masadukayo na baraza lote likagawanyika. (Kwa maana Masadukayo wanasema kwamba hakuna ufufuo, wala hakuna malaika au roho, lakini Mafarisayo wanaamini haya yote.) Kukawa na ghasia kubwa, nao baadhi ya walimu wa sheria ambao ni Mafarisayo, wakasimama wakapinga kwa nguvu wakisema, “Hatuoni kosa lo lote la mtu huyu! Huenda ikawa roho au malaika amezungumza naye” Ugomvi ukawa mkubwa kiasi kwamba yule jemadari akahofu kuwa wangemrarua Paulo vipande vipande, akaamuru vikosi vya askari vishuke na kumwondoa Paulo katikati yao kwa nguvu na kumleta ndani ya ngome ya jeshi.
”Baada ya Festo kukaa miongoni mwao kwa karibu siku nane au kumi, akashuka kwenda Kaisaria na siku iliyofuata akaitisha mahakama, akaketi penye kiti chake cha hukumu, akaamuru Paulo aletwe mbele yake. Paulo alipotokea, wale Wayahudi waliokuwa wametelemka toka Yerusalemu wakasimama wakiwa wamemzunguka, wakileta mashtaka mengi mazito dhidi yake ambayo hawakuweza kuyathibitisha. Ndipo Paulo akajitetea, akasema, “Mimi sikufanya jambo lo lote kinyume cha sheria ya Wayahudi au dhidi ya Hekalu au kinyume cha Kaisari.” Festo, akitaka kuwapendeza Wayahudi, akamwuliza Paulo, “Je, ungependa kwenda Yerusalemu na kukabili mashtaka mbele yangu huko?” Paulo akasema, “Mimi sasa nimesimama mbele ya mahakama ya Kaisari, ambako ndiko ninakostahili kushtakiwa. Kama vile wewe mwenyewe ujuavyo vyema kabisa sijawatendea Wayahudi kosa lo lote. Basi kama mimi nina hatia ya kutenda kosa lo lote linalostahili kifo, sikatai kufa. Lakini kama mashtaka yaliyoletwa dhidi yangu na hawa Wayahudi si kweli, hakuna ye yote aliye na haki ya kunikabidhi mikononi mwao. Naomba rufaa kwa Kaisari!” Baada ya Festo kufanya shauri pamoja na baraza lake, akatangaza, “Wewe umeomba rufaa kwa Kaisari, nako kwa Kaisari utakwenda!”
”Kwa kuwa sikujua jinsi ya kupeleleza jambo hili, nilimwuliza kama angependa kwenda Yerusalemu na kuhojiwa huko kuhusu mashtaka haya. Lakini Paulo alipoomba afadhiliwe ili rufaa yake isikilizwe na Mfalme Agusto, nilimwamuru alindwe mpaka nitakapoweza kumpeleka kwa Kaisari.”
”Lakini Paulo akajibu, “Mimi sijarukwa na akili, mtukufu sana Festo, bali nanena kweli nikiwa na akili zangu timamu. Naam, Mfalme anajua kuhusu mambo haya yote, nami nasema naye kwa uhuru. Kwa sababu nina hakika kwamba hakuna hata mojawapo ya mambo haya asilolijua, kwa kuwa hayakufanyika mafichoni. Mfalme Agripa, je, unaamini manabii? Najua kuwa unaamini.” Agripa akamwambia Paulo, “Je, unanishawishi kwa haraka namna hii niwe Mkristo?” Paulo akasema, “Ikiwa ni kwa haraka au la, namwomba Mungu, si wewe peke yako bali pia wale wote wanaonisikiliza leo, wawe kama mimi nilivyo, isipokuwa minyororo hii.” Baada ya kusema hayo, mfalme akainuka pamoja na mtawala na Bernike na wale waliokuwa wameketi pamoja nao. Wakati walipokuwa wakiondoka, wakaambiana “Mtu huyu hafanyi jambo lo lote linalostahili kufa au kufungwa.” Agripa akamwambia Festo, “Mtu huyu angeweza kuachwa huru kama hangekuwa amekata rufaa kwa Kaisari.”
”Jana usiku, malaika wa Mungu yule ambaye mimi ni wake na ambaye ninamwabudu alisimama karibu nami, naye akasema, ‘Paulo usiogope, kwa kuwa ni lazima usimame mbele ya Kaisari, naye Mungu amewapa usalama wote wanaosafiri pamoja nawe.
”Tulipofika Rumi, Paulo aliruhusiwa kuishi peke yake akiwa na askari wa kumlinda. Siku tatu baadaye Paulo akawaita pamoja viongozi wa Kiyahudi. Walipokwisha kukusanyika akawaambia, “Ndugu zangu, ingawa sikufanya jambo lo lote dhidi ya watu wetu au dhidi ya desturi za baba zetu, lakini nilikamatwa huko Yerusalemu nikakabidhiwa kwa Warumi. Wao walipokwisha kunihoji, wakataka kuniachia huru kwa sababu hawakuona kosa lo lote nililolifanya linalostahili adhabu ya kifo. Lakini Wayahudi walipopinga uamuzi huo, nililazimika kukata rufaa kwa Kaisari, ingawa sikuwa na lalamiko lo lote juu ya taifa langu.
”Kila mtu na atii mamlaka inayotawala, kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu, nazo mamlaka zilizopo zimewekwa na Mungu. Kwa hiyo yeye anayeasi dhidi ya mamlaka inayotawala anaasi dhidi ya kile kilichowekwa na Mungu, nao wale wafanyao hivyo watajiletea hukumu juu yao wenyewe. Kwa kuwa watawala hawawatishi watu wale wanaotenda mema bali wale wanaotenda mabaya. Je, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Basi tenda lile lililo jema naye atakusifu. Kwa maana mwenye mamlaka ni mtumishi wa Mungu kwa ajili ya mema. Lakini kama ukitenda mabaya, basi ogopa, kwa kuwa hauinui upanga bila sababu. Yeye ni mtumishi wa Mungu, mjumbe wa Mungu wa kutekeleza adhabu juu ya watenda mabaya. Kwa hiyo ni lazima kutii wenye mamlaka, si kwa sababu ya kuogopa adhabu iwezayo kutolewa, bali pia kwa ajili ya dhamiri. Kwa sababu hii mnalipa kodi, kwa maana watawala ni watumishi wa Mungu, ambao hutumia muda wao wote kutawala. Mlipeni kila mtu kile mnachodaiwa. Kama mnadaiwa kodi lipeni kodi, kama ni ushuru, lipeni ushuru, astahiliye hofu, mhofu, astahiliye heshima, mheshimu.
”Lakini miongoni mwa watu waliokomaa twanena hekima, wala si hekima ya ulimwengu huu au ya watawala wa dunia hii wanaobatilika. Sisi tunanena hekima ya Mungu ambayo ni siri, tena iliyofichika kwa wanadamu, ambayo Mungu aliikusudia kabla ya ulimwengu kuwepo, kwa ajili ya utukufu wetu. Hakuna hata mtawala mmoja wa nyakati zetu aliyeelewa jambo hili. Kwa maana kama wangelielewa, wasingemsulibisha Bwana wa utukufu.
”“Vitu vyote ni halali kwangu”: lakini si vitu vyote vyenye faida. “Vitu vyote ni halali kwangu”: lakini sitatawaliwa na kitu cho chote.
”“Vitu vyote ni halali,” lakini si vitu vyote vilivyo na faida. “Vitu vyote ni halali,” lakini si vyote vinavyojenga.
”Ndipo mwisho utafika, wakati atakapomkabidhi Mungu Baba Ufalme, akiisha angamiza kila utawala na kila mamlaka na nguvu. Kwa maana lazima Kristo atawale mpaka awe amewaweka adui zake wote chini ya miguu yake.
”Wala hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume wala mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu. Nanyi mkiwa ni mali ya Kristo, basi ninyi ni wa uzao wa Abrahamu na warithi sawasawa na ile ahadi.
”Lakini maandiko yasemaje? “Mwondoe mwanamke mtumwa pamoja na mwanawe, kwa sababu mwana wa mtumwa kamwe hatarithi pamoja na mwana wa aliye huru.” Kwa hiyo ndugu zangu, sisi si watoto wa mwanamke mtumwa, bali wa yule aliye huru.
”Kristo alitupa uhuru, akataka tubaki huru. Hivyo simameni imara wala msikubali tena kulemewa na kongwa la utumwa.
”Kwa maana sheria yote hukamilika katika amri moja: “Mpende jirani yako kama nafsi yako.”
”Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole na kiasi. Katika mambo kama haya hakuna sheria.
”juu sana kuliko falme zote na mamlaka, enzi na milki na juu ya kila jina litajwalo, si katika ulimwengu huu tu, bali na katika ule ujao pia. Naye Mungu ameweka vitu vyote viwe chini ya miguu yake na amemfanya yeye awe kichwa cha vitu vyote kwa ajili ya Kanisa,
”kumbukeni kwamba wakati ule mlikuwa hamna Kristo, mkiwa mmtengwa kutoka katika jumuiya ya watu wa Mungu, yaani, Israeli mkiwa wageni katika yale maagano ya ahadi, mliishi duniani mkiwa hamna tumaini wala Mungu.
”Hivyo basi, ninyi sasa si wageni tena wala wapitaji, bali mmekuwa wenyeji pamoja na watakatifu na pia jamaa wa nyumbani mwake Mungu.
”Kwa maana kushindana kwetu si juu ya nyama na damu, bali dhidi ya falme, mamlaka, dhidi ya wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
”Kwa hiyo, Mungu alimtukuza juu sana na kumpa Jina lililo kuu kuliko kila jina, ili kwa Jina la Yesu, kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, vya duniani na vya chini ya nchi, na kila ulimi ukiri ya kwamba YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.
”Lakini uenyeji wetu uko mbinguni. Nasi tunamngoja kwa shauku Mwokozi kutoka huko, yaani, Bwana Yesu Kristo,
”Kwa yeye vitu vyote vilivyoko mbinguni na juu ya nchi viliumbwa, vile vitu vinavyoonekana na vile visivyoonekana, kama ni viti vya enzi au falme, au wenye mamlaka au watawala, vitu vyote viliumbwa na yeye na kwa ajili yake.
”Angalieni mtu ye yote asiwafanye ninyi mateka kwa elimu batili na madanganyo matupu yanayotegemea mapokeo ya wanadamu na mafundisho ya ulimwengu ambayo siyo ya Kristo.
”Tunajua kwamba sheria ni njema ikiwa inatumika kwa halali kama ilivyokusudiwa. Lakini tunajua ya kuwa sheria si kwa ajili ya wenye haki, bali kwa ajili ya wavunja sheria na waasi, kwa ajili ya wasiomcha Mungu na wenye dhambi, wasio watakatifu na wanaokufuru, kwa wale wawauao baba zao au mama zao, kwa wauaji, kwa wazinzi na wahanithi, wauza watu na kwa waongo na waapao kwa uongo, na kwa cho chote kingine kilicho kinyume na mafundisho ya kweli,
”Basi, Mfalme wa milele, asiye na mwisho, asiyeonekana, aliye Mungu pekee, apewe heshima na utukufu milele na milele. Amen.
”Awali ya yote, nasihi, kwanza kabisa, naagiza kwamba dua, sala, maombezi na shukrani zifanyike kwa ajili ya watu wote: kwa ajili ya wafalme na wale wote wenye mamlaka, ili tupate kuishi kwa amani na utulivu, katika uchaji wote wa Mungu na utakatifu.
”ambaye Mungu atamleta kwa wakati wake mwenyewe, yeye ahimidiwaye, aliye peke yake Mtawala, Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana.
”Kama tukistahimili, pia tutatawala pamoja naye. Kama tukimkana yeye, naye atatukana sisi.
”Wakumbushe watu kuwanyenyekea watawala na kuwatii wenye mamlaka, wawe tayari kutenda kila lililo jema. Wasimnenee mtu ye yote mabaya, wasiwe wagomvi, bali wawe wapole, wakionyesha unyenyekevu kwa watu wote.
”Lakini kwa habari za Mwana asema, “Kiti chako cha enzi, Ee Mungu, kitadumu milele na milele, nayo haki itakuwa fimbo ya utawala ya ufalme wako.
”Basi jambo tunalotaka kulisema ni hili: Tunaye Kuhani Mkuu ambaye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni, yeye ahudumuye katika patakatifu, pa hema la kweli lililowekwa na Bwana, wala si mwanadamu.
”Wengine walidhihakiwa na kupigwa, hata walifungwa minyororo na kutiwa gerezani. Walipigwa kwa mawe, walipasuliwa vipande viwili kwa msumeno, waliuawa kwa upanga, walizungukazunguka wakiwa wamevaa ngozi za kondoo na mbuzi, wakiwa maskini, waliteswa na kutendwa mabaya, watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao. Walizunguka majangwani na milimani, katika mapango na katika mahandaki ardhini.
”Watiini viongozi wenu na kujinyenyekeza chini ya mamlaka yao. Kwa maana wao wanakesha kwa ajili yenu kama watu watakaopaswa kutoa hesabu. Watiini ili kwamba wafanye kazi yao kwa furaha, wala si kama mzigo, maana hiyo haitakuwa na faida kwenu.
”Lakini ninyi ni taifa teule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu la Mungu, mlioitwa ili kutangaza sifa zake yeye aliyewaita kutoka gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu.
”Wapenzi, ninawasihi, mkiwa kama wageni na wapitaji hapa ulimwenguni, epukeni tamaa mbaya za mwili ambazo hupigana vita na roho zenu. Mwe na mwenendo mzuri mbele ya watu wasiomjua Mungu, ili kama wanawasema kuwa ninyi ni watenda mabaya, wayaone matendo yenu mema wamtukuze Mungu siku atakapokuja kuhukumu. Tiini kila mamlaka iliyowekwa na wanadamu kwa ajili ya Bwana: Mfalme akiwa ndiye aliye na mamlaka ya juu zaidi, pamoja na maafisa aliowaweka. Kwa kuwa mfalme amewatuma ili kuwaadhibu wale wanaokosa na kuwasifu wale watendao mema. Kwa maana ni mapenzi ya Mungu kwamba kwa kutenda mema mnyamazishe maneno ya kijinga ya watu wapumbavu. Ishini kama watu huru, lakini msitumie uhuru wenu kama kisingizio cha kutenda uovu, bali ishini kama watumishi wa Mungu. Mheshimuni kila mtu. Wapendeni jamaa ya waaminio. Mcheni Mungu. Mpeni heshima mfalme. Ninyi watumwa, watiini mabwana zenu kwa heshima yote, si wale mabwana walio wema na wapole peke yao, bali pia wale walio wakali.
”kama aliihukumu miji ya Sodoma na Gomora kwa kuiteketeza kwa moto ikawa majivu na kuifanya kuwa kielelezo kwa yale yatakayowapata wale wasiomcha Mungu na kama alimwokoa Loti, mtu mwenye haki, ambaye alihuzunishwa na maisha machafu ya watu wapotovu (kwa sababu yale matendo mapotovu aliyoyaona na kuyasikia huyo mtu mwenye haki alipoishi miongoni mwao yalimhuzunisha siku baada ya siku),
”Hii ni hakika hasa kwa wale wanaofuata tamaa mbaya za mwili na kudharau mamlaka. Kwa ushupavu na kwa kiburi watu hawa hawaogopi kunena mabaya dhidi ya viumbe vya mbinguni, lakini hata malaika, ingawa wana nguvu na uwezo zaidi, hawaleti mashtaka dhidi ya viumbe kama hao mbele za Bwana.
”Kila mtu atendaye dhambi afanya uasi, kwa kuwa dhambi ni uasi.
”Vivyo hivyo, hawa waotao ndoto huutia mwili unajisi, hukataa kuwa chini ya mamlaka na kunena mabaya juu ya wenye mamlaka.
”Yohana, kwa makanisa saba yaliyoko Asia: Neema na amani iwe kwenu kutoka kwake yeye aliyeko, aliyekuwako na atakayekuja na kutoka kwa wale Roho saba walioko mbele ya kiti chake cha enzi na kutoka kwa Yesu Kristo ambaye ni shahidi mwaminifu, aliye mzaliwa wa kwanza kutoka kwa wafu, ambaye yeye ndiye mtawala wa wafalme wa dunia. Kwake yeye anayetupenda na ambaye ametuweka huru kutoka katika dhambi zetu kwa damu yake, akatufanya sisi kuwa ufalme na makuhani, tumtumikie Mungu wake ambaye ni Baba yake. Utukufu na uwezo vina yeye milele na milele! Amen.
”“Yeye ashindaye nitampa haki ya kuketi pamoja nami kwenye kiti changu cha enzi, kama vile mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu kwenye kiti chake cha enzi.
”Ghafula nilikuwa katika Roho, hapo mbele yangu kilikuwapo kiti cha enzi mbinguni, kikiwa kimekaliwa na mtu mmoja. Yeye aliyekuwa amekikalia alikuwa anaonekana kama yaspi na akiki. Kukizunguka kile kiti cha enzi palikuwa na upinde wa mvua ulioonekana kama zumaridi. Pia kukizunguka hicho kiti cha enzi palikuwa na viti ishirini na vinne na juu ya hivyo viti walikuwa wameketi wazee ishirini na wanne, waliovaa majoho meupe, wakiwa na taji za dhahabu vichwani mwao. Kwenye kile kiti cha enzi palikuwa panatoka miali ya umeme wa radi, ngurumo na sauti za radi. Mbele ya hicho kiti cha enzi, palikuwa na taa saba zilizokuwa zinawaka. Hizi ndizo Roho saba za Mungu. Pia mbele ya hicho kiti cha enzi palikuwa na kile kilichoonekana kama bahari ya kioo, iliyokuwa angavu kama jiwe lisilo na rangi yo yote ling'aalo sana. Katikati, kukizunguka kile kiti cha enzi, kulikuwa na viumbe wanne wenye uhai, wakiwa wamejawa na macho mbele na nyuma.
”Kila mara viumbe hao wenye uhai wanne walipomtukuza, kumheshimu na kumshukuru yeye aliyeketi kwenye kile kiti cha enzi, tena aishiye milele na milele, wale wazee ishirini na wanne huanguka mbele zake yeye aliyeketi kwenye kile kiti cha enzi na kumwabudu yeye aliye hai milele na milele. Wao huziweka taji zao mbele ya hicho kiti cha enzi, wakisema:
”Wewe umewafanya hawa wawe ufalme na makuhani wa kumtumikia Mungu wetu, nao watatawala duniani.” Kisha nikatazama, nikasikia sauti za malaika wengi wakiwa wamekizunguka kile kiti cha enzi, pamoja na wale viumbe wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne, idadi yao ilikuwa kumi elfu mara kumi elfu na maelfu ya maelfu. Nao wakiimba kwa sauti kuu, wakisema: “Anastahili Mwana-Kondoo, yeye aliyechinjwa, kupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na sifa!” Kisha nikasikia kila kiumbe mbinguni na duniani, chini ya nchi na baharini na vyote vilivyomo ndani yake vikiimba: “Sifa na heshima na utukufu na uweza ni vyake yeye aketiye juu ya hicho kiti cha enzi na kwa Mwana-Kondoo, milele na milele!”
”Baada ya hili nikatazama na hapo mbele yangu palikuwa na umati mkubwa wa watu ambao hakuna ye yote awezaye kuuhesabu, kutoka kila taifa, kila kabila, kila jamaa na kila lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi na mbele ya Mwana-Kondoo. Walikuwa wamevaa mavazi meupe na wakiwa wameshika matawi ya mitende mikononi mwao. Nao walikuwa wakipiga kelele kwa sauti kubwa wakisema: “Wokovu una Mungu wetu, yeye aketiye kwenye kiti cha enzi na Mwana-Kondoo!” Malaika wote walikuwa wamesimama kukizunguka kile kiti cha enzi na wale wazee ishirini na wanne na wale viumbe wanne wenye uhai. Wakaanguka kifudifudi mbele ya hicho kiti cha enzi na kumwabudu Mungu,
”Kwa hiyo, “Wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu na kumtumikia usiku na mchana katika Hekalu lake; naye aketiye katika kile kiti cha enzi atakaa pamoja nao na kuwalinda.
”Yule malaika wa saba akaipiga tarumbeta yake, pakawa na sauti kubwa mbinguni iliyosema: “Ufalme wa ulimwengu umekuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atatawala milele na milele.” Nao wale wazee ishirini na wanne, waliokuwa wameketi mbele za Mungu, kwenye viti vyao vya enzi wakaanguka kifudifudi wakamwabudu Mungu, wakisema: “Tunakushukuru, BWANA Mungu Mwenyezi, uliyeko na uliyekuwako, kwa kuwa umetwaa uweza wako mkuu na ukaanza kutawala. Mataifa walikasirika kwa kuwa wakati wa ghadhabu Yako umewadia. Wakati umewadia wa kuwahukumu waliokufa na kuwapa thawabu watumishi wako manabii na watakatifu wako pamoja na wale wote wanaoliheshimu Jina Lako, wakubwa kwa wadogo: na kuwaangamiza wale wanaoiangamiza dunia.”
”Yule joka akajikita katika mchanga ulioko ufuoni mwa bahari. Nami nikamwona mnyama akitoka ndani ya bahari. Mnyama huyo alikuwa na pembe kumi na vichwa saba, akiwa na taji kumi kwenye hizo pembe zake na juu ya kila kichwa kulikuwa na jina la kukufuru. Mnyama yule niliyemwona alikuwa kama chui, miguu yake ilikuwa kama ya dubu na kichwa chake kama cha simba. Lile joka likampa huyo mnyama nguvu zake, kiti chake cha enzi na mamlaka makubwa.
”Malaika wa pili akafuata akisema, “Ameanguka! Ameanguka Babeli aliye mkuu, yeye aliyeyafanya mataifa yote kulewa kwa mvinyo wa ghadhabu ya uasherati wake.”
”Ule mji mkubwa ukagawanyika katika sehemu tatu, nayo miji ya mataifa ikaanguka. Mungu akaukumbuka Babeli ule uliokuwa mkuu na kuupa kikombe cha hasira na ghadhabu yake. Kila kisiwa kikatoweka wala milima haikuonekana.
”Mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na yale mabakuli saba akaja akaniambia, “Njoo, nitakuonyesha adhabu ya yule kahaba mkuu, aketiye juu ya maji mengi. Yule ambaye wafalme wa dunia walizini naye na watu wakaao duniani walilewa kwa mvinyo wa uzinzi wake.”
”“Hapa ndipo penye akili pamoja na hekima. Vile vichwa saba ni vilima saba ambavyo huyo mwanamke amevikalia. Pia hivyo vichwa saba ni wafalme saba ambao miongoni mwao watano wamekwisha kuanguka, mwingine hajaja bado, lakini atakapokuja, atalazimika kukaa kwa muda mfupi. Yule mnyama aliyekuwepo wakati fulani na ambaye sasa hayupo, yeye ni mfalme wa nane. Ni miongoni mwa wale saba, naye anakwenda kwenye maangamizi yake. “Zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme kumi ambao bado hawajapokea ufalme, lakini ambao watapokea mamlaka kuwa wafalme kwa saa moja pamoja na yule mnyama. Hawa wana nia moja, nao watamwachia yule mnyama nguvu zao na mamlaka yao.
”Watafanya vita na Mwana-Kondoo, lakini Mwana-Kondoo atawashinda kwa sababu yeye ni Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme. Yeye atakuwa pamoja na watu wake walioitwa ambao ni wateule wake na wafuasi wake waaminifu.” Kisha yule malaika akaniambia, “Yale maji uliyoyaona, yule kahaba akiwa ameketi juu yake ni jamaa za watu, makutano, mataifa na lugha. Zile pembe kumi ulizoziona, pamoja na huyo mnyama, watamchukia huyo kahaba, watamfilisi na kumwacha uchi, watamla nyama yake na kumteketeza kwa moto. Kwa maana Mungu ataweka mioyoni mwao kutimiza kusudi lake kwa kukubali kumpa yule mnyama mamlaka yao ya utawala mpaka maneno ya Mungu yatakapotimia. Yule mwanamke uliyemwona ni ule mji mkubwa unaotawala juu ya wafalme wa dunia.”
”Naye akalia kwa nguvu kwa sauti kubwa, akisema: “Umeanguka! Umeanguka Babeli uliye Mkuu! Umekuwa makao ya mashetani na makazi ya kila pepo mchafu, makazi ya kila ndege na kila mnyama achukizaye. Kwa maana mataifa yote yamekunywa mvinyo wa uasherati wake. Nao wafalme wa dunia wamefanya uzinzi naye, nao wafanya biashara wa dunia wametajirika kutokana na wingi wa utajiri wake.”
”“Wafalme wa dunia waliozini naye na kushiriki anasa zake watakapoona moshi wa kuungua kwake, watamlilia na kumwombolezea. Watasimama mbali na kulia kwa hofu kutokana na mateso yake na kusema: “ ‘Ole! Ole Ee mji mkubwa, Ee Babeli mji wenye nguvu! Hukumu yako imekuja katika saa moja!’
”Kisha malaika mmoja mwenye nguvu akainua jiwe kubwa kama la kusagia akalitupa baharini akisema: “Hivyo ndivyo mji mkubwa Babeli utakavyotupwa chini kwa nguvu wala hautaonekana tena.
”Kinywani mwake hutoka upanga mkali ambao kwa huo atayaangusha mataifa. “Atayatawala kwa fimbo yake ya utawala ya chuma.” Atalikanyaga shinikizo la mvinyo wa ghadhabu ya Mungu Mwenyezi.
”Kwenye joho lake na paja lake liliandikwa jina hili: MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA.
”Nami nikamwona malaika amesimama ndani kwenye jua, akaita ndege wote warukao angani kwa sauti kuu, “Njoni, kusanyikeni kwa ajili ya karamu kubwa ya Mungu, ili mpate kula nyama ya wafalme na ya majemadari, ya mashujaa, ya farasi na ya wapanda farasi, nyama ya wanadamu, wote walio huru na watumwa, wadogo na wakubwa.” Kisha nikamwona yule mnyama na wafalme wa dunia pamoja na majeshi yao wakiwa wamekusanyika pamoja ili kufanya vita dhidi ya yule aliyempanda huyo farasi mweupe pamoja na jeshi lake.
”Waliobarikiwa na walio watakatifu ni wale walio na sehemu katika ufufuo wa kwanza. Hao mauti ya pili haina nguvu juu yao, bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye kwa muda wa miaka 1,000.
”Kisha nikaona kiti kikubwa cheupe cha enzi pamoja na yeye aliyeketi juu yake. Dunia na mbingu zikaukimbia uso wake wala mahali pao hapakuonekana. Nami nikawaona wafu wakubwa na wadogo, wakiwa wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi na vitabu vikafunguliwa. Pia kitabu kingine kikafunguliwa ambacho ni cha uzima. Hao wafu wakahukumiwa sawasawa na matendo yao kama yalivyoandikwa ndani ya hivyo vitabu. Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake, nayo mauti na kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Kila mtu akahukumiwa kulingana na yale aliyotenda.
”Naye yule aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi akasema, “Tazama, nayafanya mambo yote kuwa mapya!” Kisha akasema, “Andika haya, maana maneno haya ni ya kuaminika tena ni kweli.” Akaniambia, “Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Yeye aonaye kiu nitampa kunywa kutoka katika chemchemi ya maji ya uzima bila gharama yo yote.
”Kisha yule malaika akanionyesha mto wa maji ya uzima, maangavu kama kioo yakitiririka kutoka kwenye kile kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo, kupitia katikati ya barabara kuu ya huo mji. Kwenye kila upande wa huo mto kulikuwa na mti wa uzima utoao matunda ya aina kumi na mbili, ukizaa matunda yake kila mwezi. Nayo majani ya mti huo ni kwa ajili ya uponyaji wa mataifa. Katika mji huo hakutakuwa tena na kitu cho chote kilicholaaniwa, bali kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo kitakuwamo humo na watumishi wake watamtumikia, nao watamwona uso wake na Jina lake litakuwa kwenye vipaji vya nyuso zao. Usiku hautakuwako tena, wala hawatahitaji mwanga wa taa au wa jua, kwa maana BWANA Mungu atakuwa nuru yao, nao watatawala milele na milele.
”