30 – Unyakuo
Haya ni maneno matakatifu ya Mungu Mwenyezi.
Hatupendi maneno ya wanadamu.
Kwa mtu yeyote anayempenda Mungu... hivi ndivyo Mungu anasema kuhusu: Unyakuo.
Haya ni maneno matakatifu ya Mungu Mwenyezi.
Hatupendi maneno ya wanadamu.
Kwa mtu yeyote anayempenda Mungu... hivi ndivyo Mungu anasema kuhusu: Unyakuo.
“Mara baada ya dhiki ya siku zile, “ ‘jua litatiwa giza, nao mwezi hautatoa nuru yake; nazo nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu za anga zitatikisika.’ “Ndipo itakapotokea ishara ya Mwana wa Adamu angani na makabila yote ya dunia yataomboleza. Nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya angani, katika uwezo na utukufu mkuu. Naye atawatuma malaika zake kwa sauti kuu ya tarumbeta, nao watawakusanya wateule wake kutoka pande zote nne za dunia, kutoka mwisho mmoja wa mbingu hadi mwisho mwingine.
”Kwa maana Bwana mwenyewe atashuka toka mbinguni, akitoa amri kwa sauti kuu pamoja na sauti ya malaika mkuu na sauti ya tarumbeta ya Mungu, nao wale waliolala mauti wakiwa wanamwamini Kristo watafufuka kwanza. Baada ya hilo sisi tulio hai bado, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu ili kumlaki Bwana hewani, hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.
”Ndugu, kuhusu kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo na kukusanyika kwetu pamoja mbele zake, tunawasihi, msiyumbishwe kwa urahisi wala msitiwe wasiwasi na roho wala neno au barua inayosemekana kuwa imetoka kwetu, isemayo kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwako. Mtu ye yote na asiwadanganye kwa namna yo yote kwa maana siku ile haitakuja mpaka uasi utokee kwanza na yule mtu wa kuasi adhihirishwe, yule ambaye amehukumiwa kuangamizwa kabisa. Yeye atapingana na kujitukuza juu ya kila kitu kiitwacho Mungu au kinachoabudiwa, ili kujiweka juu katika Hekalu la Mungu, akijitangaza mwenyewe kuwa ndiye Mungu.
”Nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na wake, huo atakuponda kichwa, nawe utamgonga kisigino.”
”Ninajua kwamba Mkombozi wangu yu hai, naye kwamba mwishoni atasimama juu ya nchi. Nami baada ya ngozi yangu kuharibiwa, bado nikiwa na mwili huu nitamwona Mungu; mimi nitamwona kwa macho yangu mwenyewe: mimi, wala si mwingine. Tazama jinsi moyo wangu unavyomtamani sana!
”Katika siku za mwisho mlima wa Hekalu la BWANA utaimarishwa kama mlima mkuu miongoni mwa milima, utainuliwa juu kupita vilima na mataifa yote yatamiminika huko. Mataifa mengi yatakuja na kusema, “Njoni na tuupande mlima wa BWANA, kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo. Atatufundisha njia zake, ili tuweze kuenenda katika mapito yake.” Sheria itatoka Sayuni, neno la BWANA kutoka Yerusalemu. Atahukumu kati ya mataifa na ataamua magomvi ya mataifa mengi. Watafua panga zao kuwa majembe na mikuki yao kuwa miundu ya kukata matawi. Taifa halitainua upanga dhidi ya taifa jingine, wala hayatafanya mazoezi ya vita tena.
”Ingieni kwenye miamba, jificheni ardhini kutokana na utisho wa BWANA na utukufu wa enzi yake! Macho ya mtu mwenye majivuno yatanyenyekezwa na kiburi cha wanadamu kitashushwa, BWANA peke yake ndiye atakayetukuzwa siku hiyo. BWANA Mwenye Nguvu Zote anayo siku aliyoiweka akiba kwa wote wenye kujivuna na wenye kiburi, kwa wote wanaojikweza (nao watanyenyekezwa), kwa mierezi yote ya Lebanoni, iliyo mirefu sana, nayo mialoni yote ya Bashani, kwa milima yote mirefu na vilima vyote vilivyoinuka, kwa kila mnara ulio mrefu sana na kila ukuta wenye ngome, kwa kila meli ya biashara ya Tarshishi na kila chombo cha baharini cha fahari. Majivuno ya mwanadamu yatashushwa na kiburi cha wanadamu kitanyenyekezwa, BWANA peke yake ndiye atatukuzwa siku hiyo, nazo sanamu zitatoweka kabisa. Watu watakimbilia kwenye mapango ndani ya miamba na kwenye mahandaki ardhini kutokana na utisho wa BWANA na utukufu wa enzi yake, ainukapo kuitikisa dunia. Katika siku ile watu watawatupia panya na popo vinyago vyao vya fedha na vya dhahabu, walivyovitengeneza ili waviabudu. Watakimbilia kwenye mapango miambani na kwenye nyufa za miamba kutokana na utisho wa BWANA na utukufu wa enzi yake, ainukapo kuitikisa dunia.
”Bwana atausafisha uchafu wa wanawake wa Sayuni, atatakasa madoa ya damu kutoka Yerusalemu kwa Roho ya hukumu na Roho ya moto. Kisha BWANA ataumba juu ya Mlima wote wa Sayuni na juu ya wale wote wanaokusanyika hapo, wingu la moshi wakati wa mchana na kung'aa kwa miali ya moto wakati wa usiku, juu ya huo utukufu wote kutatanda kifuniko cha ulinzi.
”Kwa maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume, nao utawala utakuwa mabegani mwake. Naye ataitwa Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani. Kuongezeka kwa utawala wake na amani hakutakuwa na mwisho. Atatawala katika kiti cha enzi cha Daudi na juu ya ufalme wake, akiuthibitisha na kuutegemeza kwa haki na kwa adili, tangu wakati huo na hata milele. Wivu wa BWANA Mwenye Nguvu Zote utatimiza haya.
”Ombolezeni, kwa maana siku ya BWANA i karibu, itakuja kama uharibifu kutoka kwa Mwenyezi. Kwa sababu ya hili, mikono yote italegea, moyo wa kila mtu utayeyuka. Hofu itawakamata, uchungu na maumivu makali yatawashika, watajinyonganyonga kama mwanamke aliye na utungu wa kuzaa. Watatazamana kwa hofu kila mtu na mwenzake, nyuso zao zikiwa katika hali ya kuwaka kama moto. Tazameni, siku ya BWANA inakuja, siku katili, yenye ghadhabu na hasira kali, kuifanya nchi kuwa ukiwa na kuwaangamiza wenye dhambi waliomo ndani yake. Nyota za mbinguni na makundi ya nyota havitatoa mwanga wake. Jua linalochomoza litatiwa giza na mwezi hautatoa nuru yake. Nitauadhibu ulimwengu kwa ajili ya uovu wake, waovu kwa ajili ya dhambi zao. Nitakomesha majivuno ya wenye kiburi Na nitakishusha kiburi cha watu wakatili. Nitawafanya wanadamu kuwa adimu kuliko dhahabu safi, watakuwa wachache sana kuliko dhahabu ya Ofiri. Kwa hiyo nitazifanya mbingu zitetemeke, nayo dunia itatikisika kutoka mahali pake katika ghadhabu ya BWANA Mwenye Nguvu Zote, katika siku ya hasira yake iwakayo.
”yeye atameza mauti milele katika ushindi. BWANA Mwenyezi atafuta machozi katika nyuso zote, ataondoa aibu ya watu wake duniani kote. BWANA amesema hili.
”BWANA ameyakasirikia mataifa yote; ghadhabu yake ni juu ya majeshi yao yote. Atawaangamiza kabisa, atawatia mikononi mwa wachinjaji. Waliouawa watatupwa nje, maiti zao zitatoa uvundo, milima itatota kwa damu zao. Nyota zote za mbinguni zitayeyuka na anga litasokotwa kama kitabu, jeshi lote la angani litaanguka kama majani yaliyonyauka kutoka kwenye mzabibu, kama tini iliyonyauka kutoka kwenye mtini. Upanga wangu umekunywa na kushiba huko mbinguni, tazama, unashuka katika hukumu juu ya Edomu, wale watu ambao nimeshawahukumu, kuwaangamiza kabisa. Upanga wa BWANA umeoga katika damu, umefunikwa na mafuta ya nyama: damu ya kondoo na mbuzi, mafuta kutoka katika figo za kondoo waume. Kwa maana BWANA ana dhabihu huko Bosra na machinjo makuu huko Edomu. Nyati wataanguka pamoja nao, ndama waume na mafahali wakubwa. Nchi yao italowana kwa damu, nayo mavumbi yataloa mafuta ya nyama. Kwa sababu BWANA anayo siku ya kulipiza kisasi, mwaka wa malipo, siku ya kushindania shauri la Sayuni. Vijito vya Edomu vitageuka kuwa lami, mavumbi yake yatakuwa kiberiti kiunguzacho, nchi yake itakuwa lami iwakayo! Haitazimishwa usiku wala mchana, moshi wake utapaa juu milele. Kutoka kizazi hadi kizazi itakuwa ukiwa, hakuna mtu ye yote atakayepita huko tena.
”“Nigeukieni mimi nanyi mkaokolewe, enyi miisho yote ya dunia; kwa maana mimi ndimi Mungu, wala hapana mwingine. Nimeapa kwa nafsi yangu, kinywa changu kimenena katika uadilifu wote neno ambalo halitatanguka: Kila goti litapigwa mbele zangu, kwangu mimi kila ulimi utaapa.
”Ni mimi tangazaye mwisho tangu mwanzo, naam, tangu zamani za kale, mambo ambayo hayajatendeka. Ninasema: Kusudi langu ndilo litakalosimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote.
”Sikiliza! Walinzi wako wanapaza sauti zao, kwa pamoja wanapaza sauti zao kwa furaha. Wakati BWANA atakaporejea Sayuni, wataliona kwa macho yao wenyewe.
”“Tazama, nitaumba mbingu mpya na dunia mpya. Mambo ya zamani hayatakumbukwa, wala hayatakuja akilini.
”“Kama vile mbingu mpya na nchi mpya ninazozifanya zitakavyodumu mbele zangu,” asema BWANA, “ndivyo jina lenu na wazao wenu watakavyodumu.
”Tazama jinsi ile siku itakavyokuwa ya kutisha! Hakutakuwa na nyingine mfano wake. Utakuwa wakati wa dhiki kwa Yakobo, lakini ataokolewa kutoka katika hiyo.
”“ ‘Kwa kuwa hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Mimi mwenyewe nitawaulizia kondoo zangu na kuwatafuta. Kama vile mchungaji atafutavyo kundi lake lililotawanyika wakati akiwa pamoja nalo, hivyo ndivyo nitakavyowatafuta kondoo wangu. Nitawaokoa kutoka mahali pote walipokuwa wametawanyikia katika siku ya mawingu na giza nene. Nitawatoa katika mataifa na kuwakusanya kutoka nchi mbalimbali, nami nitawaleta katika nchi yao wenyewe. Nitawalisha kwenye milima ya Israeli, katika mabonde na mahali pote panapokalika katika nchi.
”Hivyo watabirie na uwaambie: ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Enyi watu wangu, nitayafunua makaburi yenu na kuwatoa ndani yake, nami nitawarudisha tena katika nchi ya Israeli. Ndipo ninyi watu wangu, mtakapojua kuwa Mimi ndimi BWANA, nitakapoyafunua makaburi yenu na kuwatoa humo.
”lakini yuko Mungu mbinguni afunuaye siri. Amemwonyesha Mfalme Nebukadneza kitakachotokea siku zijazo. Ndoto yako na maono yaliyopita akilini mwako ulipokuwa umelala kitandani mwako ni haya:
”“Ee mfalme, ulitazama na mbele yako ilisimama sanamu kubwa, kubwa mno kupita kiasi, sanamu inayong'aa inayotisha kwa kuonekana kwake. Kichwa cha ile sanamu kilikuwa kimetengenezwa kwa dhahabu safi, kifua chake na mikono yake vilikuwa vya fedha, tumbo lake na mapaja yake vilikuwa vya shaba, miguu yake ilikuwa ya chuma, kwa sehemu nyayo zake zilikuwa chuma na sehemu nyingine zilikuwa udongo wa mfinyanzi uliochomwa. Ulipokuwa unaangalia, jiwe lilikatwa, lakini si kwa mikono ya mwanadamu. Lile jiwe liliipiga ile sanamu kwenye nyayo zake za chuma na udongo wa mfinyanzi na kuivunja. Ndipo ile chuma, ule udongo wa mfinyanzi, ile shaba, ile fedha na ile dhahabu vikavunjika vipande vipande kwa wakati mmoja na kuwa kama makapi katika sakafu ya kupuria nafaka wakati wa kiangazi. Upepo ukavipeperusha bila kuacha hata alama. Lakini lile jiwe lililoipiga ile sanamu likawa mlima mkubwa mno na kuijaza dunia yote.
”“Hii ndiyo iliyokuwa ndoto, nasi sasa tutamfasiria mfalme. Ee mfalme, wewe ni mfalme wa wafalme. Mungu wa mbinguni amekupa wewe utawala, uweza, nguvu na utukufu, mikononi mwako amewaweka wanadamu, wanyama wa kondeni na ndege wa angani. Po pote waishipo amekufanya wewe kuwa mtawala juu yao wote. Wewe ndiye kile kichwa cha dhahabu. “Baada yako, ufalme mwingine utainuka, ulio dhaifu kuliko wako. Baadaye, utafuata ufalme wa tatu, ule wa shaba, utatawala juu ya dunia yote.
”Hatimaye, kutakuweko na ufalme wa nne, wenye nguvu kama chuma, kwa maana chuma huvunja na kupondaponda kila kitu, kama vile chuma ivunjavyo vitu vipande vipande, ndivyo ufalme huo utakavyopondaponda na kuvunjavunja nyingine zote. Kama vile ulivyoona kuwa kwa sehemu nyayo na vidole vilikuwa vya udongo wa mfinyanzi uliochomwa na kwa sehemu nyingine chuma, hivyo huu utakuwa ufalme uliogawanyikagawanyika, hata hivyo kutakuwa na baadhi zenye nguvu za chuma ndani yake, kama vile ulivyoona chuma imechanganywa na udongo wa mfinyanzi. Kama vile vidole vyake vya miguu vilikuwa kwa sehemu chuma na sehemu udongo wa mfinyanzi, hivyo ufalme huo kwa sehemu utakuwa na nguvu na kwa sehemu udhaifu. Kama vile ulivyoona chuma kikiwa kimechanganyikana na udongo wa mfinyanzi uliochomwa, ndivyo watu watakavyokuwa mchanganyiko wala hawatabaki kuwa wameungana tena kama vile chuma kisivyoweza kuchanganyikana na udongo wa mfinyanzi.
”“Katika siku za wafalme hao, Mungu wa mbinguni atauweka ufalme ambao kamwe hautaangamizwa, wala hautaachiwa taifa jingine. Utaziponda zile falme zote na kuzikomesha, bali wenyewe utadumu milele. Hii ndiyo maana ya maono ya jiwe lililochongwa kutoka mlimani, lakini si kwa mikono ya mwanadamu, lile jiwe ambalo lilivunja chuma, shaba, udongo wa mfinyanzi, fedha na dhahabu vipande vipande. “Mungu Mkuu amemwonyesha mfalme kile kitakachotokea wakati ujao. Ndoto hii ni ya kweli na tafsiri yake ni ya kuaminika.”
”Danieli akasema: “Katika maono yangu usiku nilitazama, mbele yangu kulikuwepo na upepo kutoka pande nne za mbinguni zikivuruga bahari kuu. Wanyama wakubwa wanne, kila mmoja tofauti na mwenzake, wakajitokeza kutoka baharini. “Mnyama wa kwanza alifanana na simba, naye alikuwa na mabawa kama ya tai. Nikatazama mpaka mabawa yake yalipong'olewa naye akainuliwa katika nchi akasimama kwa miguu miwili kama mwanadamu, naye akapewa moyo wa binadamu. “Hapo mbele yangu kulikuwa na mnyama wa pili, ambaye alionekana kama dubu. Upande wake mmoja ulikuwa umeinuka, alikuwa na mbavu tatu katika kinywa chake kati ya meno yake. Akaambiwa, ‘Amka, ule nyama mpaka ushibe!’ “Baada ya huyo, nilitazama, mbele yangu kulikuwa na mnyama mwingine, aliyefanana na chui. Juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama yale ya ndege. Mnyama huyu alikuwa na vichwa vinne, naye akapewa mamlaka ya kutawala. “Baada ya huyo, katika maono yangu usiku nilitazama, mbele yangu kulikuwa na mnyama wa nne, mwenye kutisha na kuogofya tena mwenye nguvu nyingi. Alikuwa na meno makubwa ya chuma, akapondaponda na kuangamiza wahanga wake na kukanyaga chini ya nyayo zake cho chote kilichosalia. Alikuwa tofauti na wanyama wote waliotangulia, naye alikuwa na pembe kumi. “Wakati nilipokuwa ninafikiri kuhusu pembe hizo, mbele yangu kulikuwa na pembe nyingine, ambayo ni ndogo, ikajitokeza miongoni mwa zile kumi, pembe tatu za mwanzoni ziling'olewa ili kuipa nafasi hiyo ndogo. Pembe hii ilikuwa na macho kama ya mwanadamu na mdomo ulionena kwa majivuno.
”“Nilipokuwa ninaendelea kutazama, “viti vya enzi vikawekwa, naye Mzee wa Siku akaketi. Mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, nywele za kichwa chake zilikuwa nyeupe kama sufu. Kiti chake cha enzi kilikuwa kinawaka kwa miali ya moto, nayo magurudumu yake yote yalikuwa yanawaka moto. Mto wa moto ulikuwa unatiririka, ukipita mbele yake. Maelfu elfu wakamhudumia, kumi elfu mara kumi elfu wakasimama mbele zake. Mahakama ikakaa ili kuhukumu na vitabu vikafunguliwa.
”“Kisha nikaendelea kutazama kwa sababu ya yale maneno ya majivuno yaliyosemwa na ile pembe. Nikaendelea kuangalia mpaka yule mnyama alipochinjwa na mwili wake ukaharibiwa na kutupwa katika ule moto unaowaka. (Wanyama wengine walikuwa wamevuliwa mamlaka yao, lakini waliruhusiwa kuishi kwa muda fulani.)
”“Katika maono yangu ya usiku nilitazama, mbele yangu nikamwona anayefanana na mwanadamu, akija pamoja na mawingu ya mbinguni. Akamkaribia huyo Mzee wa Siku na akaongozwa mbele zake. Akapewa mamlaka, utukufu na ufalme wenye nguvu, watu, kabila zote za mataifa na watu wa kila lugha wakamwabudu. Utawala wake ni utawala wa milele ambao hautapita, nao ufalme wake ni ule ambao kamwe hautaangamizwa.
”‘Hao wanyama wakubwa wanne ni falme nne zitakazoinuka duniani. Lakini watakatifu wa Yeye Aliye Juu Sana watapokea ufalme na kuumiliki milele, naam, milele na milele.’
”“Kisha nilitaka kufahamu maana ya kweli ya mnyama yule wa nne, ambaye alikuwa tofauti na wale wengine wote tena wa kutisha mwenye meno ya chuma na makucha ya shaba, mnyama ambaye alipondaponda na kuangamiza wahanga wake na kukanyaga cho chote kilichosalia. Pia mimi nilitaka kujua kuhusu zile pembe kumi juu ya kichwa chake na pia kuhusu ile pembe nyingine iliyojitokeza, ambayo mbele yake zile tatu za mwanzoni zilianguka, ile pembe ambayo ilionekana kuvutia macho zaidi kuliko zile nyingine na ambayo ilikuwa na macho na kinywa kilichonena kwa majivuno. Nilipoendelea kutazama, pembe hii ilikuwa inapigana vita dhidi ya watakatifu na kuwashinda, mpaka huyo Mzee wa Siku alipokuja na kutamka hukumu kwa kuwapa ushindi watakatifu wa Yeye Aliye Juu Sana, na wakati ukawadia walipomiliki ufalme.
”“Alinipa maelezo haya: ‘Mnyama wa nne ni ufalme wa nne ambao utatokea duniani. Utakuwa tofauti na falme nyingine zote nao utaharibu dunia nzima, ukiikanyaga chini na kuipondaponda. Zile pembe kumi ni wafalme kumi watakaotokana na ufalme huu. Baada yao mfalme mwingine atainuka, ambaye atakuwa tofauti na wale waliotangulia, naye atawaangusha wafalme watatu. Atanena maneno kinyume cha Yeye Aliye Juu Sana na kuwaonea watakatifu wake, huku akijaribu kubadili sikukuu zao takatifu pamoja na sheria. Watakatifu watatiwa chini ya mamlaka yake kwa wakati, nyakati mbili, na nusu wakati. “ ‘Lakini ndipo mahakama itakapokaa kuhukumu, nayo mamlaka yake yataondolewa na kuangamizwa kabisa milele. Ndipo ufalme, mamlaka na ukuu wa falme chini ya mbingu yote utakabidhiwa kwa watakatifu, watu wa Yeye Aliye Juu Sana. Ufalme wake utakuwa ufalme wa milele, nao watawala wote watamwabudu na kumtii yeye.’
”Kutoka katika mojawapo ya zile pembe nne ambao ulianza ukiwa mdogo ukaongezeka nguvu kuelekea kusini na kuelekea mashariki na kuelekea Nchi ya Kupendeza. Pembe hiyo ikaendelea kukua hadi kufikia jeshi la mbinguni, nayo ikalitupa baadhi ya jeshi la vitu vya angani hapa chini duniani na kukanyaga juu yake. Pembe hiyo ikajikweza ili iwe kama Mkuu wa hilo jeshi, ikamwondolea dhabihu ya kila siku, napo mahali pake patakatifu pakashushwa chini. Kwa sababu ya uasi, jeshi la watakatifu na dhabihu za kila siku vikatiwa mikononi mwake. Ikafanikiwa katika kila kitu ilichofanya, nayo kweli ikatupwa chini. Kisha nikamsikia mtakatifu mmoja akizungumza na mtakatifu mwingine akamwambia, “Je, itachukua muda gani maono haya yatimie, yaani maono kuhusu dhabihu ya kila siku, uasi unaosababisha ukiwa, kutwaliwa kwa mahali patakatifu na jeshi litakalokanyagwa chini ya nyayo?” Akaniambia, “Itachukua siku 2,300, ndipo mahali patakatifu patawekwa wakfu tena.”
”Mimi Danieli nilipokuwa ninaangalia maono na kujaribu kuelewa, mbele yangu alisimama mmoja anayefanana na mwanadamu. Kisha nikasikia sauti ya mwanadamu kutoka mto Ulai ikiita, “Gabrieli, mwambie mtu huyu maana ya maono haya.” Alipokuwa akikaribia pale mahali nilipokuwa nimesimama, niliogopa nikaanguka kifudifudi, akaniambia, “Mwana wa mwanadamu, fahamu kuwa maono haya yanahusu siku za mwisho.” Alipokuwa akinena nami, nilikuwa katika usingizi mzito, huku nimelala kifudifudi. Ndipo aliponigusa na kuniinua nikasimama kwa miguu yangu. Akaniambia, “Nitakuambia yale yatakayotokea baadaye katika wakati wa ghadhabu, kwa sababu maono haya yanahusu wakati wa mwisho ulioamriwa.
”“Katika sehemu ya mwisho ya utawala wao, wakati waasi watakapokuwa waovu kabisa, atainuka mfalme mwenye uso mkali na stadi wa hila. Atakuwa na nguvu nyingi, lakini si kwa uwezo wake mwenyewe. Atasababisha uharibifu wa kutisha na atafanikiwa kwa cho chote anachofanya. Atawaangamiza watu maarufu na watu watakatifu. Atasababisha udanganyifu ustawi, naye atajihesabu mwenyewe kuwa bora. Wakati wajisikiapo kuwa wako salama, atawaangamiza wengi na kushindana na Mkuu wa wakuu. Lakini ataangamizwa, isipokuwa si kwa uwezo wa mwanadamu. “Maono kuhusu jioni na asubuhi ambayo umepewa ni kweli, lakini yatie muhuri maono haya, kwa maana yanahusu wakati mrefu ujao.”
”“Majuma sabini yameamuriwa kwa ajili ya watu wako na kwa ajili ya mji wako mtakatifu ili kumaliza makosa, kukomesha dhambi, kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, kuleta haki ya milele, kutia muhuri maono na unabii pia kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu sana. “Ujue na kuelewa hili: Tangu kutolewa kwa amri ya kuutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu mpaka kuja kwa Mpakwa mafuta, aliye mtawala, kutakuweko majuma saba na majuma sitini na mawili. Barabara zitajengwa tena pamoja na mahandaki, lakini katika wakati wa taabu. Baada ya majuma sitini na mawili Mpakwa mafuta atakatiliwa mbali wala hatabakia na kitu. Watu wa mtawala atakayekuja watauharibu mji pamoja na mahali patakatifu. Mwisho utakuja kama mafuriko: Vita vitaendelea mpaka mwisho, nao ukiwa umeamriwa. Mtawala huyo atathibitisha agano na watu wengi kwa juma moja. Katikati ya juma hilo atakomesha dhabihu na sadaka. Mahali pa dhabihu katika Hekalu atasimamisha chukizo la uharibifu, hadi mwisho ulioamuriwa utakapomiminwa juu yake yeye aletaye uharibifu.”
”Sasa nimekuja kukueleza mambo yatakayowatokea watu wako wakati ujao, kwa maana maono hayo yanahusu wakati ambao haujaja bado.”
”Wafalme hawa wawili, mioyo yao ikiwa imekusudia mabaya wataketi kwenye meza moja na kudanganyana wao kwa wao, lakini pasipo faida, kwa sababu bado mwisho utakuja katika wakati ulioamuriwa. Mfalme wa Kaskazini atarudi katika nchi yake na utajiri mwingi, lakini atakuwa ameukaza moyo wake kinyume na Agano takatifu. Atachukua hatua dhidi ya hilo agano na kisha atarudi katika nchi yake.
”“Katika wakati ulioamuriwa atavamia tena Kusini, lakini wakati huu matokeo yake yatakuwa tofauti na yale ya wakati wa kwanza. Meli za nchi ya Kitimu zitampinga, naye atavunjika moyo. Ndipo atageuka nyuma na kutoa wazi hasira yake dhidi ya Agano takatifu. Atarudi na kuonyesha fadhili kwa wale waliachao Agano takatifu. “Majeshi yake yenye silaha yatainuka ili kunajisi ngome ya Hekalu na kuondolea mbali sadaka ya kuteketezwa ya kila siku. Ndipo watalisimamisha chukizo la uharibifu lisababishalo ukiwa. Kwa udanganyifu atapotosha wale walionajisi Agano, lakini watu wanaomjua Mungu wao watampinga kwa uthabiti. “Wale wenye hekima watawafundisha wengi, ingawa kwa kitambo watauawa kwa upanga au kuchomwa moto, au kukamatwa na kufanywa mateka. Watakapoanguka, watapokea msaada kidogo, nao wengi ambao si waaminifu wataungana nao.
”Baadhi ya wenye hekima watajikwaa, ili kwamba waweze kusafishwa, kutakaswa na kufanywa wasio na waa mpaka wakati wa mwisho, kwa maana bado litakuja kwa wakati ulioamuriwa.
”“Mfalme atafanya apendavyo. Atajikweza na kujitukuza mwenyewe kujihesabu mwenye nguvu zaidi juu ya kila mungu naye atasema vitu ambavyo havijasikiwa dhidi ya Mungu wa miungu. Atafanikiwa hadi wakati wa ghadhabu utimie, kwa maana kile kilichokusudiwa lazima kitokee. Hataonyesha heshima kwa miungu ya baba zake au kwa yule aliyetamaniwa na wanawake, wala hatajali mungu ye yote, bali atajikweza mwenyewe juu yao wote. Badala ya kuwajali hao miungu, ataheshimu mungu wa ngome, mungu ambaye hakujulikana na baba zake, atamheshimu kwa dhahabu na fedha, kwa vito vya thamani na zawadi za thamani kubwa. Atashambulia ngome zenye nguvu mno kwa msaada wa mungu wa kigeni naye atawaheshimu sana wale watakaomkubali yeye. Atawafanya watawala juu ya watu wengi na atagawa nchi kwa kulipia.
”“Katika wakati wa mwisho mfalme wa Kusini atapigana naye vita, naye mfalme wa Kaskazini atamshambulia kwa magari ya vita na askari wapanda farasi na idadi kubwa ya meli. Atavamia nchi nyingi na kukumba nchi hizo kama mafuriko. Pia ataivamia Nchi ya Kupendeza. Nchi nyingi zitapinduliwa, bali Edomu, Moabu na viongozi wa Amoni wataokolewa kutoka katika mkono wake. Atapanua mamlaka yake juu ya nchi nyingi, Misri haitaepuka. Atamiliki hazina za dhahabu, fedha na utajiri wote wa Misri, pamoja na Walibya na Wakushi kwa kujisalimisha. Lakini taarifa kutoka mashariki na kaskazini zitamshtua, naye ataondoka kwa ghadhabu nyingi ili kuangamiza na kuharibu kabisa wengi. Atasimika mahema yake ya kifalme kati ya bahari na mlima mtakatifu wa kupendeza. Hata hivyo, atafikia mwisho wake, wala hakuna ye yote atakayemsaidia.
”“Katika wakati huo Mikaeli, mtawala mkuu ambaye huwalinda watu wako, atainuka. Kutakuwako wakati wa taabu ambao haujatokea tangu mwanzo wa mataifa hadi wakati huo. Lakini wakati huo, watu wako, kila mmoja ambaye jina lake litakutwa limeandikwa kwenye kitabu, ataokolewa. Watu wengi ambao wamelala kwenye mavumbi wataamka, baadhi yao kwa uzima wa milele, wengine kwenye aibu na kudharauliwa milele. Wale wenye hekima watang'aa kama mwanga wa mbingu, nao wale ambao huwaongoza wengi kutenda haki, watang'aa kama nyota milele na milele. Lakini wewe Danieli, yafunge na kuyatia muhuri maneno ya kitabu hiki mpaka wakati wa mwisho. Wengi watakwenda huku na huko na maarifa yataongezeka.”
”Ndipo mimi Danieli, nikaangalia, nako mbele yangu walisimama wengine wawili, mmoja katika ukingo huu wa mto na mwingine ukingo wa pili wa mto. Mmoja wao akasema na yule mtu aliyevaa nguo za kitani, aliyekuwa juu ya maji ya mto, “Je, itachukua muda gani kabla mambo haya ya kushangaza hayajatimizwa?” Kisha mtu yule aliyevaa nguo za kitani, aliyekuwa juu ya maji ya mto, akainua mkono wake wa kuume na mkono wake wa kushoto kuelekea mbinguni, nami nikamsikia akiapa kwa jina lake yeye aishiye milele, akisema, “Itakuwa wakati, nyakati mbili, na nusu wakati. Nguvu za watu watakatifu zitakapokuwa zimevunjwa kabisa, ndipo mambo haya yote yatakapotimizwa.”
”Nilisikia, lakini sikuelewa. Kwa hiyo nikauliza, “Bwana wangu, matokeo ya haya yote yatakuwa nini?” Akajibu, “Danieli, enenda zako, kwa sababu maneno haya yamefungwa na kutiwa muhuri mpaka wakati wa mwisho. Wengi watatakaswa na kuondolewa mawaa na kuwa safi, lakini waovu wataendelea kuwa waovu. Hakuna mmoja wa waovu atakayefahamu, lakini wale wenye hekima watafahamu.
”“Tangu wakati ule wa kukomeshwa dhabihu ya kila siku na kusimamishwa kwa chukizo la uharibifu kutakuweko siku 1,290. Amebarikiwa mtu yule atakayevumilia hadi kufikia mwisho wa hizo siku 1,335. “Kuhusu wewe, enenda zako mpaka mwisho. Utapumzika, nawe ndipo mwisho wa hizo siku utafufuka ili kuupokea urithi uliowekwa kwa ajili yako.”
”“Katika siku ile,” asema BWANA, “utaniita mimi ‘Mume wangu’; hutaniita tena mimi ‘Bwana wangu.’
”Pigeni tarumbeta katika Sayuni; pigeni mbiu katika mlima wangu mtakatifu. Wote waishio katika nchi na watetemeke, kwa kuwa siku ya BWANA inakuja. Iko karibu, siku ya giza na huzuni, siku ya mawingu na utusitusi. Kama mapambazuko yasambaavyo toka upande huu wa milima hata upande mwingine jeshi kubwa na lenye nguvu linakuja. Jambo kama hili halijakuwapo tangu zamani wala halitakuwapo tena kamwe kwa vizazi vijavyo. Mbele yao moto unateketeza, nyuma yao miali ya moto inawaka kwa nguvu. Mbele yao nchi iko kama bustani ya Edeni, nyuma yao ni jangwa lisilofaa: hakuna kitu kinachowaepuka. Wanaonekana kama farasi; wanakwenda mbio kama askari wapanda farasi. Wanatoa sauti kama magari ya vita, wanaporukaruka juu ya vilele vya milima, kama mlio wa miali ya moto ilayo mabua, kama jeshi kubwa lililojipanga kwa ajili ya vita. Wanapoonekana, mataifa yanakuwa katika maumivu makuu; kila uso unabadilika rangi. Wanashambulia kama wapiganaji wa vita; wanapanda kuta kama askari. Wote wanatembea katika safu, hawapotoshi safu zao. Hakuna anayemsukuma mwenzake; kila mmoja anakwenda mbele moja kwa moja. Wanapita katika vizuizi bila kuharibu safu zao. Wanaenda kasi kuingia mjini; wanakimbia ukutani. Wanaingia ndani ya nyumba; kwa kuingilia madirishani kama wevi. Mbele yao dunia inatikisika, anga linatetemeka, jua na mwezi vinatiwa giza, na nyota hazitoi mwanga wake tena. BWANA anatoa mshindo wa ngurumo mbele ya jeshi lake; majeshi yake hayana idadi, ni wenye nguvu nyingi wale ambao hutii agizo lake. Siku ya BWANA ni kuu, ni ya kutisha. Ni nani anayeweza kuistahimili?
”“Hata itakuwa, baada ya hayo, nitamimina Roho yangu juu ya wote wenye mwili. Wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono. Hata juu ya watumishi wangu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile nitamimina Roho yangu.
”Nami nitaonyesha maajabu katika mbingu na juu ya nchi, damu, moto na wimbi la moshi. Jua litageuzwa kuwa giza na mwezi kuwa damu kabla ya kuja siku ya BWANA iliyo kuu na ya kutisha. Na kila mmoja atakayeliitia jina la BWANA ataokolewa. Kwa maana juu ya Mlima Sayuni na katika Yerusalemu kutakuwako wokovu, kama BWANA alivyosema, miongoni mwa walionusurika ambao BWANA awaita.
”Tia mundu, kwa kuwa mavuno yamekomaa. Njoni, mkanyage zabibu, kwa kuwa shinikizo la kukamua zabibu limejaa na mapipa yanafurika: kwa kuwa uovu wao ni mkubwa!” Umati mkubwa, umati mkubwa katika bonde la uamuzi! Kwa kuwa siku ya BWANA ni karibu katika bonde la uamuzi. Jua na mwezi vitatiwa giza, na nyota hazitatoa mwanga wake tena. BWANA atanguruma kutoka Sayuni na mshindo wa ngurumo kutoka Yerusalemu; dunia na mbingu vitatikisika. Lakini BWANA atakuwa kimbilio la watu wake, ngome imara kwa ajili ya watu wa Israeli.
”“Ndipo mtakapojua kwamba Mimi, BWANA Mungu wenu, nakaa Sayuni, mlima wangu mtakatifu. Yerusalemu utakuwa mtakatifu; kamwe wageni hawataivamia tena. “Katika siku hiyo milima itadondosha divai mpya, na vilima vitatiririka maziwa; mabonde yote ya Yuda yatatiririka maji. Chemchemi itatiririka kutoka kwenye nyumba ya BWANA na kunywesha Bonde la Shitimu. Lakini Misri itakuwa ukiwa, Edomu itakuwa jangwa tupu, kwa sababu ya jeuri waliofanya kwa watu wa Yuda, ambao katika nchi yao walimwaga damu isiyo na hatia. Yuda itakaliwa na watu milele na Yerusalemu itadumu vizazi vyote. Hatia yao ya damu, ambayo sijasamehe, nitasamehe.” BWANA anakaa Sayuni!
”Katika siku za mwisho mlima wa Hekalu la BWANA utaimarishwa na kuwa mkuu kuliko milima yote; utainuliwa juu ya vilima na mataifa yatamiminika humo. Mataifa mengi yatakuja na kusema, “Njoni, twendeni mlimani kwa BWANA, kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo. Atatufundisha njia zake, ili tutembee katika mapito yake.” Sheria itatoka Sayuni, neno la BWANA litatoka Yerusalemu. Atahukumu kati ya mataifa mengi na ataamua migogoro ya mataifa yenye nguvu na yaliyo mbali. Watafua panga zao ziwe majembe ya kulimia na mikuki yao kuwa miundu ya kukatia matawi. Taifa halitachukua upanga dhidi ya taifa, wala hawatajifunza vita tena. Kila mtu ataketi chini ya mzabibu wake na chini ya mtini wake, wala hakuna mtu atakayewaogopesha, kwa kuwa BWANA Mwenye Nguvu Zote amesema.
”“Siku kubwa ya BWANA iko karibu: iko karibu na inakuja haraka. Sikilizeni! Kilio katika siku ya BWANA kitakuwa kichungu, hata shujaa atapiga kelele. Siku ile ni siku ya ghadhabu, siku ya fadhaa na dhiki, siku ya uharibifu na ukiwa, siku ya giza na utusitusi, siku ya mawingu na giza nene, siku ya tarumbeta na mlio wa vita dhidi ya miji yenye ngome na dhidi ya minara mirefu. Nitawaletea watu dhiki, nao watatembea kama wasio na macho, kwa sababu wametenda dhambi dhidi ya BWANA. Damu yao itamwagwa kama vumbi na matumbo yao kama taka. Fedha yao wala dhahabu yao haitaweza kuwaokoa katika siku hiyo ya ghadhabu ya BWANA. Katika moto wa wivu wake dunia yote itateketezwa, kwa maana ataleta mwisho wa wote wanaoishi katika dunia ghafula.”
”BWANA anasema, “Kwa hiyo ningojee mimi, siku nitakayosimama kuteka nyara. Nimeamua kukusanya mataifa, kukusanya falme na kumimina ghadhabu yangu juu yao, hasira yangu kali yote. Dunia yote itateketezwa kwa moto wa wivu wa hasira yangu.
”“Ndipo nitatakasa midomo ya mataifa, kwamba wote waweze kuliitia jina la BWANA na kumtumikia kwa pamoja.
”“Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu Zote, ‘Baada ya muda kidogo kwa mara nyingine nitazitingisha mbingu na nchi, bahari na nchi kavu. Nitatikisa mataifa yote, nacho kile kinachotamaniwa na mataifa yote kitakuja, nami nitaujaza utukufu katika nyumba hii,’ asema BWANA Mwenye Nguvu Zote. ‘Fedha ni mali yangu na dhahabu ni mali yangu,’ asema BWANA Mwenye Nguvu Zote. ‘Utukufu wa nyumba hii ya sasa utakuwa mkubwa kuliko utukufu wa ile nyumba ya mwanzoni,’ asema BWANA Mwenye Nguvu Zote. ‘Na mahali hapa nitawapa amani,’ asema BWANA Mwenye Nguvu Zote.”
”Siku ya BWANA inakuja ambayo nyara zilizotekwa kwenu zitagawanywa miongoni mwenu. Nitayakusanya mataifa yote huko Yerusalemu kupigana dhidi yake, mji utatekwa, nyumba zitavamiwa na kuporwa na wanawake watanajisiwa. Nusu ya mji watakwenda uhamishoni, lakini watakaobaki hawataondolewa kutoka mjini. Kisha BWANA atatoka na kupigana dhidi ya watu wa yale mataifa, kama apiganavyo siku ya vita.
”Siku hiyo miguu yake itasimama juu ya Mlima wa Mizeituni, mashariki mwa Yerusalemu, nao Mlima wa Mizeituni utagawanyika mara mbili kuanzia mashariki hadi magharibi, ukifanya bonde kubwa, nusu ya mlima ukisogea kuelekea kaskazini na nusu kuelekea kusini. Nanyi mtakimbia kupitia katika bonde hilo la mlima wangu kwa kuwa litaenea hadi Aseli. Mtakimbia kama mlivyokimbia tetemeko la ardhi katika siku za Uzia mfalme wa Yuda. Kisha BWANA Mungu wangu atakuja na watakatifu wote pamoja naye. Siku hiyo hakutakuwepo nuru, baridi wala theluji. Itakuwa siku ya kipekee, isiyo na mchana wala usiku, siku ijulikanayo na BWANA. Jioni inapofika nuru itakuwepo. Siku hiyo, maji yaliyo hai yatatiririka kutoka Yerusalemu, nusu kwenda kwenye bahari ya mashariki na nusu kwenda kwenye bahari ya magharibi, wakati wa kiangazi na wakati wa masika.
”BWANA atakuwa mfalme juu ya dunia yote. Katika siku hiyo atakuwepo BWANA mmoja na jina lake litakuwa jina pekee.
”Nchi yote kuanzia Geba, kaskazini mwa Yuda, hadi Rimoni, kusini mwa Yerusalemu, itakuwa kama Araba. Lakini Yerusalemu utainuliwa juu na kubaki mahali pake, toka Lango la Benyamini hadi mahali pa Lango la Kwanza, mpaka kwenye Lango la Pembeni na kutoka Mnara wa Hananeli hadi kwenye mashinikizo ya divai ya mfalme. Utakaliwa na watu, kamwe hautaharibiwa tena, Yerusalemu utakaa salama. Hii ndiyo tauni ambayo BWANA atapiga nayo mataifa yote ambayo yalipigana dhidi ya Yerusalemu: Nyama ya miili yao itaoza wangali wamesimama kwa miguu yao, macho yao yataoza kwenye matundu yake na ndimi zao zitaoza vinywani mwao. Katika siku hiyo BWANA atawatia wanaume hofu kuu. Kila mwanaume atakamata mkono wa mwenzake nao watashambuliana. Yuda pia atapigana katika Yerusalemu. Utajiri wa mataifa yote yanayoizunguka Yerusalemu utakusanywa, wingi wa dhahabu, fedha na nguo. Tauni ya aina iyo hiyo itapiga farasi na nyumbu, ngamia na punda, nao wanyama wote walioko kwenye kambi za adui.
”Kisha walionusurika katika mataifa yote ambayo yaliushambulia Yerusalemu watakuwa wakipanda Yerusalemu kila mwaka kumwabudu Mfalme, BWANA Mwenye Nguvu Zote na kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda. Ikiwa taifa lo lote la dunia hawatakwenda Yerusalemu kumwabudu Mfalme, BWANA Mwenye Nguvu Zote, mvua haitanyesha kwao. Ikiwa watu wa Misri nao hawatakwenda kushiriki, hawatapata mvua. BWANA ataleta juu yao tauni ile ambayo itawapiga mataifa yale ambayo hayatakwenda kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda. Hii itakuwa adhabu ya Misri na adhabu ya mataifa yote yale ambayo hayatakwenda Yerusalemu kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda.
”Katika siku hiyo, kengele zilizofungwa kwenye farasi zitaandikwa maneno haya: TAKATIFU KWA BWANA, navyo vyungu vya kupikia katika nyumba ya BWANA vitakuwa kama bakuli takatifu mbele ya madhabahu. Kila chungu kilichoko Yerusalemu na Yuda kitakuwa kitakatifu kwa BWANA Mwenye Nguvu Zote na wote wanaokuja kutoa dhabihu watachukua baadhi ya vyungu hivyo na kupikia. Katika siku hiyo hatakuwepo tena mfanyabiashara katika nyumba ya BWANA Mwenye Nguvu Zote.
”Lakini ni nani atakayeweza kustahimili hiyo siku ya kuja kwake? Ni nani awezaye kusimama atakapotokea? Kwa kuwa atakuwa kama moto wa mfua fedha au kama sabuni ya afuaye nguo. Ataketi kama mfuaji na asafishaye fedha, atawatakasa Walawi, naye atawasafisha kama dhahabu na fedha. Kisha BWANA atakuwa na watu watakaoleta sadaka katika haki,
”Shamba ni ulimwengu na mbegu nzuri ni wana wa Ufalme. Magugu ni wana wa yule mwovu. Yule adui aliyepanda magugu ni ibilisi. Mavuno ni mwisho wa dunia, nao wavunaji ni malaika. “Kama vile magugu yang'olewavyo na kuchomwa motoni, ndivyo itakavyokuwa wakati wa mwisho wa dunia. Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika Ufalme wake kila kitu kinachosababisha dhambi na watenda maovu wote. Nao watawatupa katika tanuru la moto ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno. Ndipo wenye haki watang'aa kama jua katika Ufalme wa Baba yao. Yeye aliye na masikio, na asikie.
”“Tena, Ufalme wa Mbinguni ni kama wavu wa kuvua samaki uliotupwa baharini ukavua samaki wa kila aina. Ulipojaa, wavuvi wakavuta pwani, wakaketi na kukusanya samaki wazuri kuwaweka kwenye vyombo safi, lakini wale samaki wabaya wakawatupa. Hivi ndivyo itakavyokuwa wakati wa mwisho wa dunia. Malaika watakuja na kuwatenganisha watu waovu na watu wenye haki. Nao watawatupa hao waovu katika tanuru la moto ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.”
”Akawajibu akawaambia, “Ifikapo jioni, mnasema, ‘Hali ya hewa itakuwa nzuri, kwa kuwa anga ni nyekundu,’ nanyi wakati wa asubuhi mnasema, ‘Leo kutakuwa na dhoruba, kwa sababu anga ni nyekundu na mawingu yametanda.’ Mnajua jinsi ya kupambanua kule kuonekana kwa anga, lakini hamwezi kupambanua dalili za nyakati.
”Kwa maana Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake, naye ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. Nawaambia kweli, baadhi yenu hapa hawataonja mauti kabla ya kumwona Mwana wa Adamu akija katika Ufalme wake.”
”Yesu akawaambia, “Amin, amin nawaambia, wakati wa kufanywa upya vitu vyote, wakati Mwana wa Adamu atakapoketi kwenye kiti chake cha utukufu cha enzi, ninyi mliomfuata pia mtaketi katika viti vya enzi kumi na viwili, mkiyahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli.
”Yesu alipokuwa ameketi kwenye Mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamjia mahali pasipo na watu, wakamwuliza, “Tuambie, mambo haya yatatukia lini, nazo ni nini dalili za kuja kwako na za mwisho wa dunia?” Yesu akawajibu, “Angalieni, mtu asiwadanganye. Kwa maana wengi watakuja kwa Jina langu wakidai, ‘Mimi ndiye Kristo,’ nao watawadanganya wengi. Mtasikia habari za vita na matetesi ya vita, angalieni msitishike, kwa maana haya hayana budi kutukia, lakini ule mwisho bado. Taifa litainuka dhidi ya taifa na ufalme dhidi ya ufalme. Kutakuwa na njaa na matetemeko ya ardhi sehemu mbalimbali. Haya yote yatakuwa ndio mwanzo wa utungu.
”“Ndipo mtasalitiwa, ili mteswe na kuuawa, nanyi mtachukiwa na mataifa yote kwa ajili yangu. Wakati huo, wengi wataacha imani yao, nao watasalitiana kila mmoja na mwenzake na kuchukiana. Watatokea manabii wengi wa uongo, nao watawadanganya watu wengi. Kwa sababu ya kuongezeka kwa uovu upendo wa watu wengi utapoa, Lakini yule atakayevumilia hadi mwisho ndiye atakayeokoka. Injili ya Ufalme itahubiriwa ulimwenguni pote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote. Ndipo ule mwisho utakapokuja.
”“Hivyo mtakapoona lile ‘chukizo la uharibifu’ lililonenwa na nabii Danieli limesimama mahali patakatifu, asomaye na afahamu, basi wale walioko Uyahudi wakimbilie milimani. Ye yote aliyeko juu ya paa la nyumba asishuke ili kuchukua cho chote kutoka ndani ya nyumba. Yeye aliye shambani na asirudi nyumbani kwenda kuchukua vazi lake. Ole wa wenye mimba na wenye watoto wachanga siku hizo! Ombeni ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi au siku ya Sabato. Kwa maana wakati huo kutakuwa na dhiki kuu ambayo haijapata kuwako tangu mwanzo wa dunia mpaka sasa, wala haitakuwako tena. Kama siku hizo zisingelifupizwa, hakuna hata mtu mmoja ambaye angeliokoka, lakini kwa ajili ya wateule siku hizo zitafupizwa.
”Wakati huo kama mtu ye yote akiwaambia, ‘Tazama, huyu hapa ni Kristo! Au Kristo yuko kule!’ Msisadiki. Kwa maana watatokea makristo wa uongo na manabii wa uongo na kufanya ishara kubwa na miujiza mingi ili kuwapotosha, hata ikiwezekana wale wateule hasa. Angalieni, nimetangulia kuwaambia mapema. “Kwa hiyo mtu ye yote akiwaambia, ‘Yule kule nyikani,’ msiende huko. Au akisema, ‘Yuko kwenye chumba,’ msisadiki. Kwa maana kama vile umeme utokeavyo mashariki na kuonekana hata magharibi, ndivyo itakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. Kwa maana po pote ulipo mzoga, huko ndiko wakusanyikapo tai.
”“Mara baada ya dhiki ya siku zile, “ ‘jua litatiwa giza, nao mwezi hautatoa nuru yake; nazo nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu za anga zitatikisika.’ “Ndipo itakapotokea ishara ya Mwana wa Adamu angani na makabila yote ya dunia yataomboleza. Nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya angani, katika uwezo na utukufu mkuu. Naye atawatuma malaika zake kwa sauti kuu ya tarumbeta, nao watawakusanya wateule wake kutoka pande zote nne za dunia, kutoka mwisho mmoja wa mbingu hadi mwisho mwingine.
”“Jifunzeni kutokana na mtini. Matawi yake yanapoanza kuwa laini na kuchipua majani, fahamuni kwamba kiangazi kimekaribia. Hata hivyo, mwonapo mambo hayo, jueni kwamba yu karibu malangoni. Amin, amin nawaambia, kizazi hiki hakitapita hadi mambo haya yote yawe yametimia. Mbingu na dunia zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe. “Kwa habari ya siku ile na saa hakuna ajuaye, hata malaika mbinguni wala Mwana, ila Baba peke yake. Kama ilivyokuwa wakati wa Noa, ndivyo itakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. Kwa maana siku zile kabla ya gharika, watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, mpaka siku ile Noa alipoingia kwenye safina, nao hawakujua lo lote mpaka gharika ilipokuja ikawakumba wote. Hivyo ndivyo itakavyokuwa atakapokuja Mwana wa Adamu.
”Watu wawili watakuwa shambani, mmoja atatwaliwa, mwingine ataachwa. Wanawake wawili watakuwa wanasaga pamoja, mmoja atatwaliwa, mwingine ataachwa. “Kwa hiyo kesheni, kwa maana hamjui ni siku gani atakapokuja Bwana wenu. Lakini fahamuni hili kwamba: Kama mwenye nyumba angelijua ni wakati gani wa usiku ambao mwivi anakuja, angelikesha na asingeliiacha nyumba yake kuvunjwa. Kwa hiyo ninyi pia hamna budi kuwa tayari, kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja saa msiyotazamia.
”“Ni nani basi aliye mtumishi mwaminifu na mwenye busara ambaye bwana wake amemweka kusimamia watumishi wengine katika nyumba yake, ili awape chakula chao kwa wakati muafaka? Heri mtumishi yule ambaye bwana wake atakapokuja atamkuta akifanya hivyo. Amin, amin nawaambia, atamweka mtumishi huyo kuwa msimamizi wa mali yake yote. Lakini kama huyo mtumishi ni mwovu naye akasema moyoni mwake, ‘Bwana wangu atakawia muda mrefu,’ kisha akaanza kuwapiga watumishi wenzake na kula na kunywa pamoja na walevi, bwana wa mtumishi huyo atakuja siku ambayo mtumishi huyo hamtazamii na saa ile ambayo haijui. Atamkata huyo mtumishi vipande vipande na kumweka katika sehemu moja pamoja na wanafiki, mahali ambako kutakuwa ni kulia na kusaga meno.
”“Wakati huo, Ufalme wa Mbinguni utakuwa kama wanawali kumi waliochukua taa zao na kwenda kumlaki bwana arusi. Watano wao walikuwa wapumbavu na watano walikuwa wenye busara. Wale wapumbavu walichukua taa zao lakini hawakuchukua mafuta ya akiba, lakini wale wenye busara walichukua taa zao na mafuta ya akiba kwenye vyombo. Bwana arusi alipokawia kuja wale wanawali wote wakasinzia na kulala. “Usiku wa manane pakawa na kelele: ‘Tazameni, huyu hapa bwana arusi! Tokeni nje mkamlaki!’ “Ndipo wale wanawali wote wakaamka na kuzitengeneza taa zao. Wale wapumbavu wakawaambia wale wenye busara, ‘Tupatieni mafuta yenu kidogo, taa zetu zinazimika.’ “Lakini wale wenye busara wakawajibu, ‘Sivyo, hayatutoshi sisi na ninyi pia. Afadhali mwende kwa wauzao mkajinunulie mafuta yenu.’ “Nao walipokuwa wakienda kununua mafuta, bwana arusi akafika. Wale wanawali waliokuwa tayari, wakaingia ndani pamoja naye kwenye karamu ya arusi na mlango ukafungwa. “Baadaye wale wanawali wengine nao wakaja, wakaita, ‘Bwana! Bwana! Tufungulie mlango!’ “Lakini yeye bwana arusi akawajibu, ‘Amin, amin nawaambia, siwajui ninyi!’ “Kwa hiyo kesheni, kwa sababu hamjui siku wala saa.
”“Mwana wa Adamu atakapokuja katika utukufu wake na malaika wote watakatifu pamoja naye, ndipo atakapoketi juu ya kiti cha enzi cha utukufu wake. Mataifa yote watakusanyika mbele zake, naye atawatenga kama mchungaji anavyotenga kondoo na mbuzi. Atawaweka kondoo upande wake wa kuume na mbuzi upande wake wa kushoto.
”“Ndipo Mfalme atawaambia wale walioko upande wake wa kuume, ‘Njoni, ninyi mliobarikiwa na Baba yangu, urithini Ufalme ulioandaliwa kwa ajili yenu tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Kwa maana nilikuwa na njaa mkanipa chakula, nilikuwa na kiu mkaninywesha, nilikuwa mgeni mkanikaribisha, nilikuwa uchi mkanivika, nilikuwa mgonjwa mkanitunza, nami nilikuwa kifungoni mkaja kunitembelea.’ “Ndipo wale wenye haki watakapomjibu wakisema, ‘Bwana, ni lini tulikuona una njaa tukakulisha au ukiwa na kiu tukakunywesha? Lini tulikuona ukiwa mgeni tukakukaribisha au ukiwa uchi tukakuvika? Tena ni lini tulikuona ukiwa mgonjwa tukakutunza au ukiwa kifungoni tukakutembelea?’ “Naye Mfalme atawajibu, ‘Amin, amin ninawaambia, kwa jinsi mlivyomtendea mmojawapo wa hawa ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.’
”“Kisha atawaambia wale walio upande wake wa kushoto, ‘Ondokeni kwangu, ninyi mliolaaniwa, nendeni kwenye moto wa milele ulioandaliwa kwa ajili ya ibilisi na malaika zake. Kwa maana nilikuwa na njaa hamkunipa chakula, nilikuwa na kiu hamkuninywesha, nilikuwa mgeni nanyi hamkunikaribisha, nilikuwa uchi hamkunivika, nilikuwa mgonjwa hamkunitunza na nilikuwa gerezani nanyi hamkuja kunitembelea.’ “Ndipo wao pia watajibu, ‘Bwana ni lini tulikuona ukiwa na njaa au kiu, au ukiwa mgeni au uchi, au ukiwa mgonjwa na kifungoni na hatukukuhudumia?’ “Naye atawajibu, ‘Amin, amin nawaambia, kwa jinsi ambavyo hamkumtendea mmojawapo wa hawa ndugu zangu walio wadogo, hamkunitendea mimi.’ “Ndipo hawa watakapoingia kwenye adhabu ya milele, lakini wale wenye haki wataingia katika uzima wa milele.”
”Yesu akajibu, “Wewe umenena. Lakini ninawaambia nyote, tangu sasa mtamwona Mwana wa Adamu akiwa ameketi mkono wa kuume wa Mwenye Nguvu, na akija juu ya mawingu ya mbinguni.”
”Mtu ye yote anayenionea aibu mimi na maneno yangu katika kizazi hiki cha uzinzi na cha dhambi, Mwana wa Adamu, atamwonea aibu wakati atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu.”
”Yesu akaendelea kuwaambia, “Amin, amin nawaambia, kuna watu waliosimama hapa ambao hawataonja mauti kabla ya kuuona Ufalme wa Mungu ukija katika nguvu.”
”“Tafadhali tuambie, mambo haya yatatukia lini? Nayo ni nini ishara ya wakati hayo yote yanapokaribia kutimia?” Yesu akawaambia: “Jihadharini mtu ye yote asiwadanganye. Wengi watakuja kwa Jina langu wakidai, ‘Mimi ndiye,’ nao watawadanganya wengi. Msikiapo habari za vita na uvumi wa vita, msiwe na hofu. Mambo haya hayana budi kutukia, lakini ule mwisho bado. Taifa litainuka dhidi ya taifa na ufalme dhidi ya ufalme. Kutakuwa na matetemeko sehemu mbalimbali na njaa. Huu ndio mwanzo wa utungu.
”“Lakini ninyi jihadharini. Kwa maana watawapeleka mahakamani na kuwapiga mijeledi katika masinagogi. Mtashtakiwa mbele ya watawala na wafalme kwa ajili yangu, ili kuwa ushuhuda kwao. Nayo habari njema lazima ihubiriwe kwanza kwa mataifa yote kabla ule mwisho haujawadia. Mtakapokamatwa na kushtakiwa, msisumbuke kuhusu mtakalosema. Semeni tu lo lote mtakalopewa wakati huo, kwa kuwa si ninyi msemao bali ni Roho Mtakatifu. “Ndugu atamsaliti ndugu yake ili auawe, baba atamsaliti mwanawe. Watoto watawaasi wazazi wao na kusababisha wauawe. Watu wote watawachukia kwa ajili ya Jina langu, lakini atakayevumilia hata mwisho ataokoka.
”“Mtakapoona chukizo la uharibifu limesimama mahali pasipolipasa (asomaye na afahamu), basi wale walioko Uyahudi na wakimbilie milimani. Yeye aliyeko juu ya dari ya nyumba asishuke au kuingia ndani ili kuchukua kitu cho chote. Aliye shambani asirudi nyumbani kuchukua vazi lake. Ole wao wenye mimba na wale wanaonyonyesha watoto siku hizo! Ombeni mambo haya yasitokee wakati wa baridi. Kwa maana siku hizo itakuwako dhiki kuu ambayo haijapata kuwako tangu mwanzo wa uumbaji, hapo Mungu alipoumba ulimwengu mpaka leo na wala haitakuwako tena kamwe. Kama Bwana asingelifupiza siku hizo, kamwe asingeliokoka mtu ye yote, lakini kwa ajili ya wateule, wale aliowachagua, amezifupiza siku hizo.
”Wakati huo mtu ye yote akiwaambia, ‘Tazama, Kristo huyu hapa!’ au, ‘Tazama, yuko kule,’ msiamini. Kwa maana watatokea makristo wa uongo na manabii wa uongo, nao watafanya ishara na maajabu ili kuwapotosha, ikiwezekana hata wale wateule. Hivyo jihadharini, nimekwisha kuwaambia mambo haya yote mapema kabla hayajatukia.
”“Lakini katika siku hizo, baada ya hiyo dhiki, “ ‘jua litatiwa giza na mwezi hautatoa nuru yake; nyota zitaanguka kutoka angani, nazo nguvu za anga zitatikisika.’ “Ndipo watu wote watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni kwa nguvu nyingi na utukufu. Naye atawatuma malaika zake wawakusanye wateule wake kutoka pande zote nne za dunia, kutoka miisho ya dunia hadi miisho ya mbingu.
”“Basi jifunzeni somo hili kutokana na mtini: Mara mwonapo matawi yake yakichipua na kutoa majani, mnajua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia. Vivyo hivyo, myaonapo mambo haya yakitukia, tambueni kwamba Kristo yu karibu malangoni. Amin, amin nawaambia, kizazi hiki hakitapita hadi mambo haya yote yametukia. Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe. “Lakini kwa habari ya siku ile na saa hakuna ye yote ajuaye, hata malaika walioko mbinguni wala Mwana hajui, ila Baba peke yake. Jihadharini! Kesheni! Kwa maana hamjui wakati ule utakapowadia. Ni kama mtu anayesafiri akiiacha nyumba yake na kuwaachia watumishi wake kuiangalia, kila mtu na kazi yake, kisha akamwambia yule bawabu aliye mlangoni akeshe. “Basi kesheni kwa sababu hamjui ni lini mwenye nyumba atakaporudi, iwapo ni jioni, au kwamba ni usiku wa manane, au alfajiri awikapo jogoo, au wakati wa mapambazuko. Kama akija ghafula, asije akawakuta mmelala. Lile ninalowaambia ninyi, nawaambia watu wote: ‘Kesheni!’ ”
”Yesu akajibu, “Mimi ndimi, nanyi mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa Mwenye Nguvu, akija na mawingu ya mbinguni.”
”Kama mtu ye yote akinionea aibu mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu atamwonea aibu mtu huyo atakapokuja katika utukufu wake na katika utukufu wa Baba na wa malaika watakatifu. Amin, amin nawaambia, wako baadhi ya watu waliosimama hapa ambao hawataonja mauti mpaka watakapouona Ufalme wa Mungu.”
”“Iweni tayari mkiwa mmevikwa kwa ajili ya huduma na taa zenu zikiwa zinawaka, kama watumishi wanaomngojea bwana wao arudi kutoka kwenye karamu ya arusi, ili ajapo na kugonga mlango waweze kumfungulia mara. Heri wale watumishi ambao bwana wao atakapokuja atawakuta wakiwa wanakesha. Amin, nawaambia, atajifunga mkanda wake na kuwaketisha ili wale, naye atakuja na kuwahudumia. Itakuwa heri kwa watumwa hao ikiwa bwana wao atakapokuja atawakuta wamekesha hata kama atakuja mnamo usiku wa manane, au karibu na mapambazuko. Lakini fahamuni jambo hili kwamba: Kama mwenye nyumba angalijua ni saa ipi mwivi atakapokuja, asingaliacha nyumba yake kuvunjwa. Ninyi nanyi imewapasa kuwa tayari saa zote, kwa maana Mwana wa Adamu atakuja saa ambayo hamumtarajii.”
”Itakuwa ni furaha kwa mtumishi yule ambaye bwana wake atakaporudi atamkuta akifanya hivyo. Amin nawaambia, atampa mamlaka juu ya vyote alivyo navyo. Lakini ikiwa yule mtumishi atawaza moyoni mwake, ‘Bwana wangu anakawia kurudi,’ akaanza kuwapiga wale watumishi wa kiume na wa kike na kula na kunywa na kulewa, bwana wake yule mtumwa atakuja siku asiyodhani na saa asiyoijua. Huyo bwana wake atamkata vipande vipande na kumwekea fungu lake pamoja na wale wasio waaminifu. “Yule mtumishi anayefahamu vyema mapenzi ya bwana wake na asijiandae wala kufanya kama apendavyo bwana wake, atapigwa kwa mapigo mengi.
”Pia Yesu akauambia ule umati wa watu, “Mwonapo wingu likitokea magharibi, mara mwasema, ‘Mvua itanyesha,’ nayo hunyesha. Nanyi mwonapo upepo wa kusini ukivuma, ninyi husema, ‘Kutakuwa na joto,’ na huwa hivyo. Enyi wanafiki! Mnajua jinsi ya kutambua kuonekana kwa dunia na anga. Inakuwaje basi kwamba mnashindwa kutambua wakati huu wa sasa?
”Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Wakati utafika ambapo mtatamani kuiona moja ya siku ya Mwana wa Adamu, lakini hamtaiona. Watu watawaambia, ‘Yule kule!’ Au, ‘Huyu hapa!’ Msiwakimbilie. Kwa maana Mwana wa Adamu katika siku yake atakuwa kama umeme wa radi, umulikao katika anga kuanzia mwisho mmoja hadi mwingine.
”Lakini kwanza itampasa kuteseka katika mambo mengi na kukataliwa na kizazi hiki. “Kama ilivyokuwa siku za Noa, ndivyo itakavyokuwa katika siku za Mwana wa Adamu. Wakati huo wa Noa watu walikuwa wakila, wakinywa, wakioa na kuolewa mpaka siku ile Noa alipoingia katika safina, gharika ikaja na kuwaangamiza wote. “Ndivyo ilivyokuwa katika siku za Loti: Watu walikuwa wakila na kunywa, wakinunua na kuuza, wakilima na kujenga. Lakini siku ile Loti alipoondoka Sodoma, ikanyesha mvua ya moto na kiberiti kutoka mbinguni ukawaangamiza wote. “Hivyo ndivyo itakavyokuwa siku ile Mwana wa Adamu atakapofunuliwa.
”Siku hiyo, mtu ye yote aliyeko kwenye dari ya nyumba yake, vitu vyake vikiwa ndani ya hiyo nyumba asishuke kuvichukua. Vivyo hivyo mtu aliyeko shambani asirudi nyumbani kuchukua cho chote. Mkumbukeni mke wa Loti! Mtu ye yote anayejaribu kuyaokoa maisha yake atayapoteza na ye yote atakayeyapoteza maisha yake atayaokoa.
”Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa wamelala kitanda kimoja, mmoja atachukuliwa, mwingine ataachwa. Wanawake wawili watakuwa wanasaga nafaka pamoja, mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa. Wanaume wawili watakuwa wanafanya kazi pamoja shambani, mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa.” Kisha wakamwuliza, “Haya yatatukia wapi Bwana?” Akawaambia, “Pale ulipo mzoga, ndipo tai watakapokusanyika.”
”Je, Mungu hatawatendea haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku? Je, atakawia kuwasaidia? Ninawaambia, atawapatia haki upesi. Lakini je, Mwana wa Adamu atakapokuja ataikuta imani duniani?”
”Kisha akawaambia: “Taifa litainuka dhidi ya taifa jingine na ufalme mmoja dhidi ya ufalme mwingine. Kutakuwa na matetemeko ya ardhi katika sehemu mbalimbali, njaa kali na magonjwa ya kuambukiza. Kutakuwa na matukio ya kutisha na ishara kuu kutoka mbinguni.
”“Lakini kabla yote hayajatokea, watawakamata ninyi na kuwatesa. Watawatia mikononi mwa wakuu wa masinagogi na kufungwa magerezani, nanyi mtapelekwa mbele ya wafalme na watawala kwa ajili ya Jina langu. Hii itawapa nafasi ya kushuhudia. Lakini msiwe na wasiwasi kwamba mtasema nini kabla ya mashtaka. Kwa maana nitawapa maneno na hekima ambayo hakuna hata adui yenu mmoja atakayeweza kushindana nayo wala kuipinga. Mtasalitiwa hata na wazazi, ndugu, jamaa na marafiki na baadhi yenu watawaua. Mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya Jina langu. Lakini hapatakuwa na unywele mmoja wa kichwa chenu utakaoangamia. Kwa kuvumilia mtaokoa roho zenu.
”“Mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, basi fahamuni kwamba kuharibiwa kwake kumekaribia. Wakati huo, wale walio Uyahudi wakimbilie milimani, walio mjini Yerusalemu watoke humo na wale walioko mashambani wasiingie mjini. Kwa sababu huu utakuwa ni wakati wa adhabu ili kutimiza yote yaliyoandikwa. Ole wao wenye mimba na watakaokuwa wananyonyesha katika siku hizo! Kutakuwa na dhiki kuu katika nchi na ghadhabu juu ya hawa watu Wataanguka kwa makali ya upanga, wengine watachukuliwa kuwa mateka katika mataifa yote, nao Yerusalemu utakanyagwa na watu Mataifa hadi muda wa hao watu Mataifa utimie.
”“Kutakuwa na ishara katika jua, mwezi na nyota. Hapa duniani, mataifa yatakuwa katika dhiki na fadhaa kutokana na ngurumo na misukosuko ya bahari. Watu watazimia roho kutokana na hofu kuu na kuyaona yale mambo yanayotokea duniani, kwa maana nguvu za vitu vya angani zitatikisika. Wakati huo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni pamoja na uweza na utukufu mkuu. Mambo haya yatakapoanza kutendeka, simameni na mkaviinue vichwa vyenu, kwa sababu ukombozi wenu umekaribia.”
”Akawaambia mfano huu: “Uangalieni mtini na miti mingine yote. Unapochipua majani, ninyi wenyewe mnaweza kuona na kutambua ya kuwa wakati wa kiangazi umekaribia. Vivyo hivyo, mnapoyaona mambo haya yakitukia, mwajua kwamba Ufalme wa Mungu umekaribia. “Amin, amin nawaambia, kizazi hiki hakitapita hadi mambo haya yote yatimie. Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.” “Jihadharini mioyo yenu isije ikalemewa na anasa, ulevi na fadhaa za maisha haya, nayo siku ile ikawakuta ninyi bila kutazamia kama vile mtego unasavyo. Kwa maana kama vile mtego unasavyo, ndivyo siku hiyo itakavyowapata wanadamu wote waishio katika uso wa dunia yote. Kesheni daima na mwombe ili mweze kuokoka na yale yote yatakayotokea na kusimama mbele ya Mwana wa Adamu.”
”Amin, amin nawaambia, saa yaja, nayo saa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, nao watakaoisikia watakuwa hai. Kama vile Baba alivyo na uzima ndani yake, vivyo hivyo amempa Mwana kuwa na uzima ndani yake. Naye amempa Mwanawe mamlaka ya kuhukumu kwa kuwa yeye ni Mwana wa Adamu. “Msishangae kusikia haya, kwa maana saa inakuja ambapo wale walio makaburini wataisikia sauti yake. Nao watatoka nje, wale waliotenda mema watafufuka wapate uzima na wale waliotenda maovu, watafufuka wahukumiwe.
”Nyumbani kwa Baba yangu kuna makao mengi. Kama sivyo, ningeliwaambia. Nakwenda kuwaandalia makao. Nami nikienda na kuwaandalia makao, nitarudi tena na kuwachukua mkae pamoja nami, ili mahali nilipo, nanyi mpate kuwepo.
”Baada ya kusema mambo haya, walipokuwa wanatazama, akachukuliwa juu mbinguni mbele ya macho yao na wingu likampokea wasimwone tena. Walipokuwa bado wakikaza macho yao kuelekea juu alipokuwa akienda zake Mbinguni, tazama ghafula, wanaume wawili waliovaa mavazi meupe wakasimama karibu nao, wakasema, “Enyi watu wa Galilaya, mbona mnasimama mkitazama juu angani? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda Mbinguni, atarudi tena jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake Mbinguni.”
”Nayahesabu mateso yetu ya wakati huu kuwa si kitu kulinganisha na utukufu utakaodhihirishwa kwetu. Kwa maana viumbe vyote vinangoja kwa shauku kudhihirishwa kwa watoto wa Mungu.
”Kwa kuwa imeandikwa: “ ‘Kama niishivyo,’ asema Bwana, ‘kila goti litapigwa mbele zangu, na kila ulimi utamkiri Mungu.’ ”
”Mungu wa amani atamponda Shetani chini ya miguu yenu upesi. Neema ya Bwana wetu Yesu iwe pamoja nanyi. Amen.
”Kama mtu ye yote akijenga juu ya msingi huu kwa kutumia dhahabu, fedha, mawe ya thamani, miti, majani au nyasi, kazi yake itaonekana kuwa ikoje, kwa kuwa siku ile itaidhihirisha kazi yake. Itadhihirishwa kwa moto, nao moto utapima ubora wa kazi ya kila mtu. Kama kile alichojenga kitabaki, atapokea thawabu. Kama kazi ya mtu itateketea, atapata hasara, ila yeye mwenyewe ataokolewa, lakini kama mtu aliyenusurika kwenye moto.
”Kwa hiyo msihukumu jambo lo lote kabla ya wakati wake, ngojeni mpaka Bwana atakapokuja. Yeye atayaleta nuruni mambo yale yaliyofichwa gizani na kuweka wazi nia za mioyo ya wanadamu. Wakati huo kila mmoja atapokea sifa anayostahili kutoka kwa Mungu.
”mkabidhini mtu huyu kwa Shetani, ili mwili wake uharibiwe, ili roho yake iokolewe katika siku ya Bwana. Majivuno yenu si mazuri. Je, hamjui ya kwamba chachu kidogo huchachusha donge zima la unga?
”Ndugu zangu nisemalo ni hili: nyama na damu haviwezi kuurithi Ufalme wa Mungu, wala kuharibika kurithi kutokuharibika. Sikilizeni, nawaambia siri: Sote hatutalala, lakini sote tutabadilishwa ghafula, kufumba na kufumbua, parapanda ya mwisho itakapolia. Kwa kuwa parapanda italia, nao wafu watafufuliwa na miili isiyoharibika, nasi tutabadilishwa.
”ili kwa Jina la Yesu, kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, vya duniani na vya chini ya nchi, na kila ulimi ukiri ya kwamba YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.
”Wakati Kristo atakapotokea yeye aliye uzima wenu ndipo nanyi mtakapotokea pamoja naye katika utukufu.
”na ili kumngojea Mwanawe kutoka mbinguni, ambaye Mungu alimfufua kutoka kwa wafu: yaani, Yesu, yeye aliyetuokoa kutoka katika ghadhabu inayokuja.
”Lakini ndugu, hatutaki msijue kuhusu wale waliolala mauti, ili msihuzunike kama watu wengine wasiokuwa na tumaini. Kwa kuwa tunaamini kwamba Yesu alikufa na kufufuka, hata hivyo, Mungu kwa njia ya Yesu atawafufua pamoja naye wale waliolala mauti katika yeye. Kulingana na neno la Bwana mwenyewe tunawaambia kwamba, sisi ambao bado tuko hai, tutakaobaki hadi kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wale waliolala mauti.
”Kwa maana Bwana mwenyewe atashuka toka mbinguni, akitoa amri kwa sauti kuu pamoja na sauti ya malaika mkuu na sauti ya tarumbeta ya Mungu, nao wale waliolala mauti wakiwa wanamwamini Kristo watafufuka kwanza. Baada ya hilo sisi tulio hai bado, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu ili kumlaki Bwana hewani, hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.
”Basi, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira hatuna haja ya kuwaandikia, kwa kuwa mnajua vyema kwamba siku ya Bwana itakuja kama mwivi ajapo usiku. Wakati watu wanaposema, “Kuna amani na salama,” maangamizi huwajia ghafula kama vile utungu umjiavyo mwanamke mwenye mimba wala hawatatoroka. Bali ninyi, ndugu, hamko gizani hata kwamba siku ile iwakute ghafula kama mwivi.
”Kwa maana Mungu hakutuita ili tupate ghadhabu bali tupate wokovu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo. Yeye alikufa kwa ajili yetu ili kwamba kama tuko macho au tukiwa tumelala tupate kuishi pamoja naye.
”Ndiyo sababu miongoni mwa makanisa ya Mungu, tunajivuna kuhusu saburi yenu na imani mliyo nayo katika mateso yote na dhiki mnazostahimili. Haya yote ni uthibitisho kwamba hukumu ya Mungu ni ya haki na kwa sababu hiyo ninyi mtahesabiwa kwamba mnastahili Ufalme wa Mungu, ambao ninyi mnateswa kwa ajili yake. Mungu ni mwenye haki: yeye atawalipa mateso wale wawatesao ninyi na kuwapa ninyi mnaoteseka raha pamoja na sisi, wakati Bwana Yesu atakapodhihirishwa kutoka mbinguni katika mwali wa moto pamoja na malaika wake wenye nguvu. Atawaadhibu wale wasiomjua Mungu na ambao hawakuitii Injili ya Bwana wetu Yesu. Wataadhibiwa kwa uangamivu wa milele na kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa uweza wake, siku hiyo atakapokuja kutukuzwa katika watakatifu wake na kustaajabiwa miongoni mwa wote walioamini. Ninyi pia mtakuwa miongoni mwa hawa kwa sababu mliamini ushuhuda wetu kwenu.
”Ndugu, kuhusu kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo na kukusanyika kwetu pamoja mbele zake, tunawasihi, msiyumbishwe kwa urahisi wala msitiwe wasiwasi na roho wala neno au barua inayosemekana kuwa imetoka kwetu, isemayo kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwako. Mtu ye yote na asiwadanganye kwa namna yo yote kwa maana siku ile haitakuja mpaka uasi utokee kwanza na yule mtu wa kuasi adhihirishwe, yule ambaye amehukumiwa kuangamizwa kabisa. Yeye atapingana na kujitukuza juu ya kila kitu kiitwacho Mungu au kinachoabudiwa, ili kujiweka juu katika Hekalu la Mungu, akijitangaza mwenyewe kuwa ndiye Mungu.
”Je, hamkumbuki ya kwamba nilipokuwa pamoja nanyi niliwaambia mambo haya? Nanyi sasa mnajua kinachomzuia, ili kwamba apate kudhihirishwa wakati wake utakapowadia. Maana ile nguvu ya siri ya uasi tayari inatenda kazi, lakini yule anayeizuia ataendelea kufanya hivyo mpaka atakapoondolewa. Hapo ndipo yule mwasi atafunuliwa, ambaye Bwana Yesu atamteketeza kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kabisa kwa utukufu wa kuja kwake. Kuja kwa yule mwasi kutaonekana kana kwamba ni kutenda kazi kwake Shetani ambaye hutumia nguvu zote, ishara, maajabu ya uongo na kila aina ya udanganyifu kwa wale wanaoangamia kwa sababu walikataa kuipenda kweli wapate kuokolewa. Kwa sababu hii, Mungu ameruhusu watawaliwe na nguvu ya udanganyifu, ili waendelee kuamini uongo na hivyo wote wahukumiwe ambao hawakuamini ule ukweli bali wamefurahia uovu.
”uishike amri hii bila dosari wala lawama mpaka kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye Mungu atamleta kwa wakati wake mwenyewe, yeye ahimidiwaye, aliye peke yake Mtawala, Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana. Yeye peke yake hapatikani na mauti, ambaye anakaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa, ambaye hakuna mwanadamu aliyemwona wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye milele. Amen.
”Lakini yakupasa ufahamu jambo hili, kwamba siku za mwisho kutakuwa na nyakati za hatari. Kwa maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kumkufuru Mungu, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio watakatifu, wasio na upendo, wasiopenda kupatanishwa, wasingiziaji, wasiozuia tamaa zao, wakatili, wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi, waliojaa majivuno, wapendao anasa zaidi kuliko kumpenda Mungu. Wakiwa na mfano wa utauwa kwa nje lakini wakizikana nguvu za Mungu. Jiepushe na watu wa namna hiyo.
”Nakuagiza mbele za Mungu na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu watu walio hai na waliokufa wakati wa kuja kwake na ufalme wake kwamba: Uhubiri Neno, uwe tayari wakati ufaao na wakati usiofaa, karipia, kemea na kuonya kwa uvumilivu wote na kwa mafundisho mazuri. Maana wakati utakuja watu watakapokataa kuyakubali mafundisho yenye uzima, badala yake, ili kutimiza tamaa zao wenyewe, watajikusanyia idadi kubwa ya walimu wapate kuwaambia yale ambayo masikio yao yanayowasha yanatamani kuyasikia. Watakataa kusikiliza kweli na kuzigeukia hadithi za uongo. Kwa habari yako wewe, vumilia mateso, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiza wajibu wote wa huduma yako.
”Sasa nimewekewa taji ya haki ambayo Bwana, mwamuzi wa haki, atanitunukia siku ile, wala si mimi tu, bali pia wote ambao wamengoja kwa shauku kudhihirishwa kwake.
”tukilitazamia tumaini lenye baraka na ufunuo wa utukufu wa Mungu wetu Mkuu na Mwokozi wetu Yesu Kristo,
”Pia asema, “Hapo mwanzo, Ee Bwana, uliweka misingi ya dunia, nazo mbingu ni kazi ya mikono yako. Hizo zitaangamia, lakini wewe utadumu; zote zitachakaa kama vazi. Utazikung'utakung'uta kama joho, kama vazi zitachakaa. Bali wewe hubadiliki, wala miaka yako kamwe haitakoma.”
”Kwa hiyo, ilikuwa muhimu kwa nakala za vitu vile vya mbinguni vitakaswe kwa dhabihu hizi, lakini vitu halisi vya mbinguni vilihitaji dhabihu bora kuliko hizi. Kwa maana Kristo hakuingia kwenye patakatifu palipofanywa kwa mikono ya mwanadamu, ambao ni mfano wa kile kilicho halisi. Yeye aliingia mbinguni penyewe, ili sasa aonekane mbele za Mungu kwa ajili yetu. Wala hakuingia mbinguni ili apate kujitoa mwenyewe mara kwa mara, kama vile Kuhani Mkuu aingiavyo Patakatifu pa Patakatifu kila mwaka kwa damu ambayo si yake mwenyewe. Ingelikuwa hivyo, ingelimpasa Kristo kuteswa mara nyingi tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Lakini sasa ametokea mara moja tu katika mwisho wa nyakati aiondoe dhambi kwa kujitoa mwenyewe kuwa dhabihu. Kama vile mwanadamu alivyowekewa kufa mara moja tu na baada ya kufa akabili hukumu, vivyo hivyo Kristo alitolewa mara moja tu kuwa dhabihu ili azichukue dhambi za watu wengi, naye atakuja mara ya pili, si ili kuchukua dhambi, bali kuwaletea wokovu wale wanaomngoja kwa shauku.
”Wala tusiache kukutana pamoja, kama wengine walivyo na desturi ya kukutana, tuhimizane sisi kwa sisi kadiri tuonavyo Siku ile inakaribia.
”Wanawake walipokea watu wao waliokuwa wamekufa wakafufuliwa. Lakini wengine waliteswa, nao wakakataa kufunguliwa, ili wapate ufufuo ulio bora zaidi.
”Basi sikilizeni, ninyi matajiri, lieni na kuomboleza kwa ajili ya hali mbaya sana inayowajia. Utajiri wenu umeoza na mavazi yenu yameliwa na nondo. Dhahabu yenu na fedha yenu vimeliwa na kutu. Kutu yake itashuhudia dhidi yenu nayo itaila miili yenu kama vile moto. Mmejiwekea hazina kwa ajili ya siku za mwisho.
”Kwa hiyo, ndugu zangu, vumilieni hadi kuja kwake Bwana. Angalieni jinsi mkulima angojavyo ardhi itoe mavuno yake yaliyo ya thamani na jinsi anavyovumilia kwa ajili ya kupata mvua za kwanza na za mwisho. Ninyi nanyi vumilieni tena simameni imara, kwa sababu kuja kwa Bwana kumekaribia.
”Kwanza kabisa, ni lazima mfahamu ya kwamba siku za mwisho watakuja watu wenye dhihaka wakidhihaki na kuzifuata tamaa zao mbaya, wakisema, “Iko wapi ile ahadi ya kuja kwake? Tangu baba zetu walipokufa, kila kitu kinaendelea kama kilivyokuwa tangu mwanzo wa kuumbwa.” Wao kwa makusudi hupuuza ukweli huu, ya kwamba kwa neno la Mungu mbingu zilikuwepo tangu zamani nayo dunia ilifanyizwa kutoka ndani ya maji na kwa hayo maji, ulimwengu wa wakati ule uligharikishwa na kuangamia. Lakini kwa neno lilo hilo mbingu za sasa na dunia, zimewekwa akiba kwa ajili ya moto, zikihifadhiwa hadi siku ile ya hukumu na ya kuangamizwa kwa watu wasiomcha Mungu.
”Lakini wapenzi, msisahau neno hili, kwamba kwa Bwana, siku moja ni kama miaka elfu na miaka elfu ni kama siku moja. Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake kama watu wengine wanavyodhani kukawia. Yeye anawavumilia, maana hataki mtu ye yote aangamie, bali kila mmoja afikilie toba.
”Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi. Ndipo mbingu zitatoweka kwa kishindo kikuu na vitu vya asili vitateketezwa kwa moto, nayo dunia na kila kitu kilichomo ndani yake kitaunguzwa. Kwa kuwa vitu vyote vitaharibiwa namna hii, ninyi je, imewapasa kuwa watu wa namna gani? Inawapasa kuishi maisha matakatifu na ya kumcha Mungu, mkingojea na kuhimiza kuja kwa hiyo siku ya Mungu, ambayo siku hiyo mbingu zitachomwa moto na kutoweka na vitu vya asili vitayeyuka kwa moto. Lakini kufuatana na ahadi yake, sisi tunatazamia kwa furaha mbingu mpya na dunia mpya, ambayo haki hukaa ndani yake.
”Nao ulimwengu unapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu milele. Watoto wadogo, huu ni wakati wa mwisho! Kama mlivyosikia kwamba mpinga Kristo anakuja, hivyo basi wapinga Kristo wengi wamekwisha kuja. Kutokana na hili twajua kwamba huu ni wakati wa mwisho. Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu hasa. Kwa maana kama wangelikuwa wa kwetu, wangelikaa pamoja nasi, lakini kutoka kwao kulionyesha kwamba hakuna hata mmoja wao aliyekuwa wa kwetu.
”Wapenzi, msiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho mwone kama zimetoka kwa Mungu, kwa sababu manabii wengi wa uongo wametokea ulimwenguni. Hivi ndivyo mnavyoweza kutambua Roho wa Mungu: Kila roho inayokubali kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatoka kwa Mungu. Lakini kila roho ambayo haimkubali Yesu haitoki kwa Mungu. Hii ndiyo roho ya mpinga Kristo, ambayo mmesikia kwamba inakuja na sasa tayari iko ulimwenguni. Watoto wadogo, ninyi mmetokana na Mungu, nanyi mmewashinda kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika ulimwengu. Wao wanatokana na ulimwengu na kwa hiyo hunena yaliyo ya ulimwengu, hivyo ulimwengu huwasikiliza. Sisi twatokana na Mungu na ye yote anayemjua Mungu hutusikiliza, lakini asiyetokana na Mungu hatusikilizi. Hivi ndivyo tunavyoweza kutambua Roho wa Kweli na roho ya upotovu.
”Wadanganyifu wengi, wasiokubali kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili, wametokea ulimwenguni. Mtu wa namna hiyo ni mdanganyifu na mpinga Kristo. Jihadharini msije mkapoteza kile mlichokitenda, bali mpate kupewa thawabu kamilifu. Mtu ye yote asiyedumu katika mafundisho ya Kristo, bali akayaacha, yeye hana Mungu. Ye yote anayedumu katika mafundisho ana Baba na Mwana pia. Msimpokee mtu ye yote anayewajia ambaye hawaletei mafundisho haya, wala msimkaribishe nyumbani mwenu. Ye yote amkaribishaye mtu wa namna hiyo anashiriki katika matendo maovu ya mtu huyo.
”Enoki, mtu wa saba kuanzia Adamu alitoa unabii kuhusu watu hawa, akisema: “Tazama, Bwana anakuja pamoja na maelfu kwa maelfu ya watakatifu wake, ili kumhukumu kila mmoja na kuwapatiliza wote wasiomcha Mungu kwa matendo yao yote ya uasi waliyoyatenda, pamoja na maneno yote ya kuchukiza ambayo wenye dhambi wamesema dhidi yake.”
”Ufunuo wa Yesu Kristo aliopewa na Mungu ili awaonyeshe watumishi wake mambo ambayo ni lazima yatukie hivi karibuni. Alijulisha mambo haya kwa kumtuma malaika wake kwa Yohana mtumishi wake,
”Tazama! Anakuja na mawingu na kila jicho litamwona, hata wale waliomchoma mkuki; na mataifa yote ulimwenguni yataomboleza kwa sababu yake. Naam, ndivyo itakavyokuwa! Amen.
”Kwa kuwa umelishika neno la saburi yangu nitakulinda hata utoke katika saa ya kujaribiwa inayokuja ulimwenguni pote ili kuwajaribu wote wakaao duniani. “Ninakuja upesi. Shika sana ulicho nacho, ili mtu asije akaichukua taji yako. Yeye ashindaye nitamfanya kuwa nguzo katika Hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo kamwe. Nitaandika juu yake Jina la Mungu wangu na jina la mji wa Mungu wangu, yaani, Yerusalemu mpya, ambao unashuka kutoka mbinguni kwa Mungu wangu. Nami pia nitaandika juu yake Jina langu jipya.
”Nayajua matendo yako, ya kwamba wewe si baridi wala si moto. Afadhali ungelikuwa baridi au moto. Hivyo kwa kuwa u uvuguvugu, kwamba wewe si baridi wala si moto, nitakutapika utoke kinywani mwangu. Kwa maana unasema: ‘Mimi ni tajiri, nimejilimbikizia mali, wala sihitaji kitu cho chote.’ Lakini hutambui ya kwamba wewe ni mnyonge, wa kuhurumiwa, maskini, kipofu, tena uliye uchi. Kwa hiyo nakushauri ununue kutoka kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto ili upate kuwa tajiri na mavazi meupe ili uyavae, upate kuficha aibu ya uchi wako na mafuta ya kupaka macho yako ili upate kuona. “Wale niwapendao, ninawakemea na kuwaadibisha. Hivyo uwe na bidii ukatubu.
”Baada ya mambo hayo nilitazama, nami nikaona mbele yangu mlango ulio wazi mbinguni. Nayo ile sauti niliyokuwa nimeisikia hapo kwanza ikisema nami kama tarumbeta ikasema, “Njoo panda huku nami nitakuonyesha yale ambayo hayana budi kutokea baada ya haya.”
”Kisha nikaona katika mkono wake wa kuume yule aliyeketi kwenye kile kiti cha enzi, kitabu kilichoandikwa ndani na upande wa nyuma kikiwa kimefungwa kwa lakiri saba. Nami nikamwona malaika mwenye nguvu akitangaza kwa sauti kuu, akisema, “Ni nani anayestahili kuzivunja hizo lakiri na kukifungua hicho kitabu?” Lakini hapakuwa na ye yote mbinguni wala duniani au chini ya dunia aliyeweza kukifungua hicho kitabu wala hata kutazama ndani yake. Nikalia sana sana kwa sababu hakuonekana ye yote anayestahili kukifungua hicho kitabu wala kutazama ndani yake. Kisha, mmoja wa wale wazee akaniambia, “Usilie! Tazama, Simba wa kabila la Yuda, wa Uzao wa Daudi, ameshinda. Yeye ndiye anayeweza kukifungua hicho kitabu na kuvunja hizo lakiri zake saba.” Ndipo nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale viumbe wenye uhai wanne na miongoni mwa wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, akiwa kama amechinjwa. Alikuwa na pembe saba na macho saba, ambazo ndizo zile Roho saba za Mungu zilizotumwa duniani pote. Huyo Mwana-Kondoo akaja na kukitwaa kile kitabu kutoka kwenye mkono wa kuume wa yule aliyeketi kwenye kile kiti cha enzi. Alipokwisha kukitwaa kile kitabu, wale viumbe wenye uhai wanne pamoja na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele ya yule Mwana-Kondoo. Kila mmoja wao alikuwa na kinubi, nao walikuwa wameshika mabakuli ya dhahabu yaliyojaa uvumba, ambayo ni maombi ya watakatifu. Nao wakaimba wimbo mpya, wakisema: “Wewe unastahili kukitwaa kitabu na kuzivunja lakiri zake, kwa sababu ulichinjwa na kwa damu yako ukamnunulia Mungu watu kutoka katika kila kabila, kila lugha, kila jamaa na kila taifa. Wewe umewafanya hawa wawe ufalme na makuhani wa kumtumikia Mungu wetu, nao watatawala duniani.”
”Kisha nikatazama, nikasikia sauti za malaika wengi wakiwa wamekizunguka kile kiti cha enzi, pamoja na wale viumbe wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne, idadi yao ilikuwa kumi elfu mara kumi elfu na maelfu ya maelfu. Nao wakiimba kwa sauti kuu, wakisema: “Anastahili Mwana-Kondoo, yeye aliyechinjwa, kupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na sifa!” Kisha nikasikia kila kiumbe mbinguni na duniani, chini ya nchi na baharini na vyote vilivyomo ndani yake vikiimba: “Sifa na heshima na utukufu na uweza ni vyake yeye aketiye juu ya hicho kiti cha enzi na kwa Mwana-Kondoo, milele na milele!” Wale viumbe wenye uhai wanne wakasema, “Amen!” Nao wale wazee ishirini na wanne wakaanguka kifudifudi wakaabudu.
”Kisha nikaangalia wakati Mwana-Kondoo akivunja ile lakiri ya kwanza miongoni mwa zile saba. Ndipo nikasikia mmoja wa wale viumbe wenye uhai wanne akisema kwa sauti kama ya radi: “Njoo!” Nikatazama na hapo mbele yangu alikuwepo farasi mweupe! Yeye aliyempanda alikuwa na upinde, naye akapewa taji, akampanda akatoka akishinda, tena apate kushinda.
”Alipoivunja ile lakiri ya pili, nikamsikia yule kiumbe mwenye uhai wa pili akisema, “Njoo!” Ndipo akatokea farasi mwingine wa rangi nyekundu. Yeye aliyempanda akapewa uwezo wa kuondoa amani duniani na kuwafanya watu wauane. Yeye akapewa upanga mkubwa.
”Alipoivunja ile lakiri ya tatu, nikamsikia yule kiumbe wa tatu mwenye uhai akisema, “Njoo!” Nikatazama na mbele yangu alikuwepo farasi mweusi! Yeye aliyempanda alikuwa na mizani mkononi mwake. Ndipo nikasikia kile kilichokuwa kama sauti katikati ya wale viumbe wanne wenye uhai ikisema, “Kipimo kimoja cha ngano kwa mshahara wa kibarua wa siku moja. Vipimo vitatu vya shayiri kwa mshahara wa kibarua wa siku moja. Lakini usiharibu mafuta ya zeituni wala divai!”
”Alipovunja ile lakiri ya nne, nikasikia sauti ya yule kiumbe wa nne mwenye uhai ikisema, “Njoo!” Nikatazama na hapo mbele yangu alikuwepo farasi mwenye rangi ya kijivujivu! Yeye aliyempanda huyo farasi aliitwa Mauti, naye Kuzimu alikuwa akimfuata nyuma yake kwa karibu, nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya dunia, kuua kwa upanga, njaa, tauni na kwa wanyama wakali wa dunia.
”Alipoivunja ile lakiri ya tano, nikaona chini ya madhabahu, roho za wale waliochinjwa kwa ajili ya Neno la Mungu na kwa ajili ya ushuhuda walioutunza. Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, “Hata lini, Ee Bwana Mwenyezi, uliye Mtakatifu na Mwaminifu, hutawahukumu na kulipiza kisasi juu ya watu waishio duniani kwa ajili ya damu yetu?” Kisha kila mmoja wao akapewa joho jeupe na wakaambiwa wangoje kwa muda kidogo zaidi, mpaka idadi ya ndugu zao na watumishi wenzao watakaouawa kama wao walivyouawa, itakapotimia.
”Nikaangalia, naye alipokuwa akiivunja ile lakiri ya sita, pakatokea tetemeko kuu la nchi na jua likawa jeusi kama nguo ya gunia iliyotengenezwa kwa singa za mbuzi, mwezi wote ukawa mwekundu kama damu. Nyota zilizo angani zikaanguka ardhini kama vile matunda ya mtini yasiyokomaa yaangukavyo wakati mti wake unapotikiswa na upepo mkali. Anga ikatoweka kama vile karatasi isokotwavyo na kila mlima na kila kisiwa kikaondolewa mahali pake. Ndipo wafalme wa dunia, wakuu wote, majemadari, matajiri, wenye nguvu na kila mtu, mtumwa na mtu huru, wakajificha katika mapango na kwenye miamba ya milima. Wakaiita milima na miamba wakisema, “Tuangukieni, mkatufiche na uso wake yeye aketiye kwenye kiti cha enzi na mkatuepushe na ghadhabu ya Mwana-Kondoo! Kwa maana siku ile kuu ya ghadhabu yao imewadia. Je, ni nani awezaye kustahimili?”
”Baada ya hili nikaona malaika wanne wakiwa wamesimama katika pembe nne za dunia, wakizuia hizo pepo nne za dunia, ili kwamba pasiwe na upepo utakaovuma juu ya nchi au juu ya bahari au juu ya mti wo wote. Nikaona malaika mwingine akipanda kutoka maawio ya jua akiwa na muhuri wa Mungu aliye hai. Akawaita kwa sauti kubwa wale malaika wanne waliokuwa wamepewa mamlaka ya kuidhuru nchi na bahari, akisema, “Msiidhuru nchi wala bahari, wala miti, hadi tuwe tumetia muhuri kwenye vipaji vya nyuso za watumishi wa Mungu wetu.”
”Ndipo nikasikia idadi ya wale waliotiwa muhuri: yaani 144,000 kutoka katika makabila yote ya Israeli. Kutoka kabila la Yuda 12,000, kabila la Reubeni 12,000, kabila la Gadi 12,000, kabila la Asheri 12,000, kabila la Naftali 12,000, kabila la Manase 12,000, kabila la Simeoni 12,000, kabila la Lawi 12,000, kabila la Isakari 12,000, kabila la Zabuloni 12,000, kabila la Yosefu 12,000, na kabila la Benyamini 12,000.
”Baada ya hili nikatazama na hapo mbele yangu palikuwa na umati mkubwa wa watu ambao hakuna ye yote awezaye kuuhesabu, kutoka kila taifa, kila kabila, kila jamaa na kila lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi na mbele ya Mwana-Kondoo. Walikuwa wamevaa mavazi meupe na wakiwa wameshika matawi ya mitende mikononi mwao. Nao walikuwa wakipiga kelele kwa sauti kubwa wakisema: “Wokovu una Mungu wetu, yeye aketiye kwenye kiti cha enzi na Mwana-Kondoo!” Malaika wote walikuwa wamesimama kukizunguka kile kiti cha enzi na wale wazee ishirini na wanne na wale viumbe wanne wenye uhai. Wakaanguka kifudifudi mbele ya hicho kiti cha enzi na kumwabudu Mungu, wakisema: “Amen! Sifa na utukufu na hekima na shukrani na heshima na uweza na nguvu viwe kwa Mungu wetu milele na milele. Amen!” Kisha mmoja wa wale wazee ishirini na wanne akaniuliza, “Ni nani hawa waliovaa mavazi meupe, nao wametoka wapi?” Nikamjibu, “Bwana, wewe wajua.” Naye akasema, “Hawa ni wale waliotoka katika ile dhiki kuu, nao wamefua mavazi yao katika damu ya Mwana-Kondoo na kuyafanya meupe kabisa. Kwa hiyo, “Wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu na kumtumikia usiku na mchana katika Hekalu lake; naye aketiye katika kile kiti cha enzi atakaa pamoja nao na kuwalinda. Kamwe hawataona njaa wala kiu tena. Jua halitawapiga wala joto lo lote liunguzalo. Kwa maana Mwana-Kondoo aliyeko katikati ya kile kiti cha enzi atakuwa Mchungaji wao; naye atawaongoza kwenda kwenye chemchemi za maji yaliyo hai. Naye Mungu atafuta kila chozi kutoka katika macho yao.”
”Mwana-Kondoo alipoivunja ile lakiri ya saba, pakawa kimya mbinguni kwa muda wa nusu saa. Nami nikawaona wale malaika saba wanaosimama mbele za Mungu, nao wakapewa tarumbeta saba. Malaika mwingine aliyekuwa na chetezo cha dhahabu, akaja na kusimama mbele ya madhabahu. Akapewa uvumba mwingi ili autoe pamoja na maombi ya Watakatifu wote, juu ya ile madhabahu ya dhahabu iliyoko mbele ya kile kiti cha enzi. Ule moshi wa uvumba pamoja na yale maombi ya watakatifu, vikapanda juu mbele za Mungu, kutoka mkononi mwa huyo malaika. Kisha yule malaika akachukua kile chetezo, akakijaza moto kutoka kwenye ile madhabahu, akautupa juu ya dunia. Pakatokea sauti za radi, ngurumo, umeme wa radi na tetemeko la nchi. Basi wale malaika saba waliokuwa na zile tarumbeta saba wakajiandaa kuzipiga.
”Malaika wa kwanza akaipiga tarumbeta yake, pakatokea mvua ya mawe na moto uliochanganyika na damu, vikatupwa kwa nguvu juu ya nchi na theluthi ya dunia ikateketea, theluthi ya miti ikateketea na majani yote mabichi yakateketea.
”Malaika wa pili akaipiga tarumbeta yake na kitu kama mlima mkubwa unaowaka moto kikatupwa baharini. Theluthi ya bahari ikawa damu, theluthi ya viumbe vyenye uhai viishivyo baharini vikafa na theluthi ya meli zikaharibiwa.
”Malaika wa tatu akaipiga tarumbeta yake na nyota kubwa iliyokuwa ikiwaka kama taa, ikaanguka toka angani, ikaangukia theluthi ya mito na chemchemi za maji. Nyota hiyo inaitwa Uchungu. Theluthi ya maji yakawa machungu na watu wengi wakafa kutokana na maji hayo kwa maana yalikuwa machungu.
”Kisha malaika wa nne akaipiga tarumbeta yake na theluthi ya jua, theluthi ya mwezi na theluthi ya nyota, zikapigwa. Kwa hiyo theluthi moja ya mwanga ikawa giza. Theluthi ya mchana ikawa haina mwanga na pia theluthi ya usiku. Nilipokuwa tena nikitazama, nikamsikia tai mmoja akipiga kelele kwa sauti kuu wakati akiruka katikati ya mbingu, akisema, “Ole! Ole! Ole wa watu waishio duniani, kwa sababu ya tarumbeta ambazo malaika hao wengine watatu wanakaribia kuzipiga!”
”Malaika wa tano akaipiga tarumbeta yake, nami nikaona nyota iliyokuwa imeanguka toka angani hadi ardhini. Nyota hiyo ilipewa ufunguo wa lile Shimo lisilo na mwisho. Alipolifungua hilo Shimo lisilo na mwisho, moshi ukapanda kutoka humo kama moshi wa tanuru kubwa sana. Jua na anga vikatiwa giza na ule moshi uliotoka katika hilo shimo lisilokuwa na mwisho. Ndipo katika ule moshi wakatoka nzige wakaenda juu ya nchi, nao wakapewa nguvu kama zile za nge wa duniani. Wakaambiwa wasidhuru majani ya nchi, wala mmea wala mti wo wote, bali wawadhuru tu wale watu ambao hawana muhuri wa Mungu kwenye vipaji vya nyuso zao. Wakaruhusiwa kuwatesa kwa muda wa miezi mitano, lakini wasiwaue. Uchungu wa kuuma kwao ulikuwa kama ule wa mtu aumwapo na nge. Katika siku hizo watu watatafuta kifo lakini hawatakiona, watatamani kufa, lakini kifo kitawakimbia. Wale nzige walikuwa na umbo kama la farasi waliotayarishwa kwa ajili ya vita. Kwenye vichwa vyao kulikuwa na kitu kama taji za dhahabu na nyuso zao zilikuwa kama za binadamu. Walikuwa na nywele kama za wanawake na meno yao yalikuwa kama ya simba. Walikuwa na dirii kama za chuma na sauti za mabawa yao zilikuwa kama ngurumo za magari mengi ya farasi wanaokimbilia vitani. Walikuwa na mikia yenye miiba ya kuumia kama nge. Nguvu yao ya kutesa watu kwa huo muda wa miezi mitano ilikuwa katika hiyo mikia yao. Walikuwa na mfalme wao, ambaye ni malaika wa lile Shimo lisilo na mwisho, ambaye jina lake kwa Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kiyunani ni Apolioni. Ole ya kwanza imepita, bado nyingine mbili zinakuja.
”Malaika wa sita akaipiga tarumbeta yake, nami nikasikia sauti ikitoka katika zile pembe nne za madhabahu ya dhahabu iliyoko mbele za Mungu. Ile sauti ikamwambia yule malaika wa sita mwenye tarumbeta, “Wafungulie wale malaika wanne waliofungwa kwenye ule mto mkubwa Eufrati.” Basi wale malaika wanne wakafunguliwa ambao walikuwa wamewekwa tayari kwa ajili ya saa hiyo na siku hiyo na mwezi huo na mwaka huo ili wawaue theluthi ya wanadamu. Idadi ya majeshi wapanda farasi ilikuwa 200,000,000. Nilisikia idadi yao. Hivi ndivyo nilivyowaona hao farasi na wapanda farasi katika maono yangu: Wapanda farasi walivaa dirii vifuani zenye rangi ya moto na yakuti samawi na kiberiti. Vichwa vya hao farasi vilikuwa kama vichwa vya simba. Moto, moshi na kiberiti vilitoka vinywani mwao. Theluthi ya wanadamu wakauawa kwa maafa hayo matatu, yaani, huo moto, moshi na kiberiti, vilivyotoka kwenye vinywa vya hao farasi. Nguvu za hao farasi zilikuwa katika vinywa vyao na kwenye mikia yao, kwa sababu mikia yao ilikuwa kama nyoka, yenye vichwa ambayo waliitumia kudhuru. Wanadamu waliosalia, ambao hawakuuawa katika mapigo hayo, bado walikataa kutubia kazi za mikono yao na hawakuacha kuabudu mashetani na sanamu za dhahabu, za fedha, za shaba, za mawe na za miti, ambazo haziwezi kuona, kusikia wala kutembea. Wala hawakutubu na kuacha matendo yao ya uuaji, uchawi, uasherati wala wizi wao.
”Kisha nikamwona malaika mwingine mwenye nguvu akishuka kutoka mbinguni. Alikuwa amevikwa wingu na upinde wa mvua juu ya kichwa chake. Uso wake uling'aa kama jua na miguu yake ilikuwa kama nguzo za moto. Mkononi mwake alikuwa ameshika kitabu kidogo kilichokuwa kimefunguliwa. Akauweka mguu wake wa kuume juu ya bahari na mguu wake wa kushoto akauweka juu ya nchi kavu. Naye akapiga kelele kwa sauti kuu kama simba anayenguruma. Alipopiga kelele, zile radi saba zikatoa ngurumo zake. Nazo zile radi saba zilipotoa ngurumo, nilitaka kuanza kuandika, lakini nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, “Yatie muhuri hayo yaliyosemwa na hizo radi saba na usiyaandike.” Kisha yule malaika niliyekuwa nimemwona akiwa amesimama juu ya bahari na juu ya nchi kavu akainua mkono wake wa kuume kuelekea mbinguni. Naye akaapa kwa Jina la Mungu aishiye milele na milele, aliyeumba mbingu na vyote vilivyomo, dunia na vyote viijazavyo, pamoja na bahari na vyote vilivyomo ndani yake, akasema, “Hakuna kungoja tena! Lakini katika siku zile ambazo huyo malaika wa saba atakapokaribia kuipiga hiyo tarumbeta yake, siri ya Mungu itatimizwa, kama vile alivyowatangazia watumishi wake manabii.”
”Ndipo ile sauti niliyokuwa nimeisikia kutoka mbinguni ikasema nami tena ikaniambia, “Nenda, chukua kile kitabu kilichofunguliwa kilichoko mkononi mwa yule malaika aliyesimama juu ya bahari na juu ya nchi kavu.” Basi nikamwendea nikamwomba yule malaika anipe kile kitabu kidogo. Akaniambia, “Chukua na ukile. Kitakuwa kichungu tumboni mwako, lakini kinywani mwako kitakuwa kitamu kama asali.” Hivyo nikakichukua kile kitabu kidogo kutoka mkononi mwa yule malaika nikakila. Kilikuwa kitamu kama asali kinywani mwangu, lakini baada ya kukila, tumbo langu likatiwa uchungu. Kisha nikaambiwa, “Imekupasa kutoa unabii tena kuhusu makabila mengi, mataifa, lugha na wafalme.”
”Ndipo nikapewa mwanzi wa kupimia ulio kama fimbo, nikaambiwa, “Nenda ukapime Hekalu la Mungu pamoja na madhabahu, nawe uwahesabu wale waabuduo humo. Lakini usiupime ua wa nje wa Hekalu, uache, kwa sababu ua huo wamepewa watu Mataifa. Hao wataukanyagakanyaga mji mtakatifu kwa muda wa miezi arobaini na miwili. Nami nitawapa mashahidi wangu wawili uwezo, nao watoe unabii kwa muda wa siku 1,260, wakiwa wamevaa nguo za gunia.” Hawa ndio ile mizeituni miwili na vile vinara viwili vya taa visimamavyo mbele za Bwana Mungu wa dunia yote. Kama mtu ye yote akitaka kuwadhuru, moto hutoka vinywani mwao na kuwateketeza adui zao. Hivi ndivyo impasavyo kufa mtu ye yote atakayetaka kuwadhuru. Watu hawa wanao uwezo wa kufunga anga ili mvua isinyeshe wakati wote watakapokuwa wanatoa unabii wao. Nao watakuwa na uwezo wa kuyabadili maji kuwa damu na kuipiga dunia kwa kila aina ya mapigo mara kwa mara kama watakavyo.
”Basi watakapokuwa wamemaliza ushuhuda wao, yule mnyama atokaye katika lile Shimo lisilo na mwisho atapigana nao vita, atawashinda na kuwaua. Maiti zao zitabaki katika barabara ya mji mkubwa, ambao kwa fumbo unaitwa Sodoma na Misri, ambapo pia Bwana wao alisulibiwa. Kwa muda wa siku tatu na nusu, watu wa kila kabila, jamaa, lugha na taifa wataziangalia hizo maiti zao na hawataruhusu wazikwe. Watu waishio duniani watazitazama kwa furaha maiti za hao manabii wawili na kushangilia kwa kupeana zawadi kwa sababu hao manabii waliwatesa watu waishio duniani.
”Lakini baada ya zile siku tatu na nusu, pumzi ya uhai kutoka kwa Mungu ikawaingia, nao wakasimama kwa miguu yao na wote waliowaona wakaingiwa na hofu kuu. Kisha wale manabii wawili wakasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikiwaambia, “Njoni huku juu!” Nao wakapaa mbinguni katika wingu, wakati adui zao wakiwa wanawatazama. Saa iyo hiyo, kukatokea tetemeko kubwa la nchi na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka. Watu elfu saba wakauawa katika tetemeko hilo, nao walionusurika wakaogopa sana, wakamtukuza Mungu wa mbinguni. Ole ya pili imekwisha kupita, tazama ole ya tatu inakuja upesi.
”Yule malaika wa saba akaipiga tarumbeta yake, pakawa na sauti kubwa mbinguni iliyosema: “Ufalme wa ulimwengu umekuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atatawala milele na milele.” Nao wale wazee ishirini na wanne, waliokuwa wameketi mbele za Mungu, kwenye viti vyao vya enzi wakaanguka kifudifudi wakamwabudu Mungu, wakisema: “Tunakushukuru, BWANA Mungu Mwenyezi, uliyeko na uliyekuwako, kwa kuwa umetwaa uweza wako mkuu na ukaanza kutawala. Mataifa walikasirika kwa kuwa wakati wa ghadhabu Yako umewadia. Wakati umewadia wa kuwahukumu waliokufa na kuwapa thawabu watumishi wako manabii na watakatifu wako pamoja na wale wote wanaoliheshimu Jina Lako, wakubwa kwa wadogo: na kuwaangamiza wale wanaoiangamiza dunia.” Ndipo Hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa na Sanduku la Agano lake likaonekana humo ndani. Kukatokea mianga ya umeme wa radi, ngurumo, sauti za radi, tetemeko la nchi na mvua kubwa ya mawe.
”Kukaonekana ishara kuu mbinguni: Palikuwa na mwanamke aliyevikwa jua na mwezi ukiwa chini ya miguu yake na taji ya nyota kumi na mbili ilikuwa kichwani mwake. Alikuwa na mimba naye akilia kwa uchungu kwa kuwa alikuwa anakaribia kuzaa. Kisha ishara nyingine ikaonekana mbinguni: Likaonekana joka kubwa jekundu lenye vichwa saba na pembe kumi na taji saba katika vichwa vyake. Mkia wake ukakokota theluthi ya nyota zote angani na kuziangusha katika nchi. Ndipo lile joka likasimama mbele ya yule mwanamke aliyekuwa karibu kuzaa ili lipate kumla huyo mtoto mara tu atakapozaliwa. Yule mwanamke akazaa mtoto mwanamume, atakayeyatawala mataifa yote kwa fimbo yake ya utawala ya chuma. Lakini huyo mtoto akanyakuliwa na kupelekwa kwa Mungu kwenye kiti chake cha enzi. Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambako Mungu alikuwa amemtayarishia mahali ili apate kutunzwa huko kwa muda wa siku 1,260.
”Basi palikuwa na vita mbinguni: Mikaeli na malaika zake wakapigana na hilo joka, nalo joka pamoja na malaika zake likapigana nao. Lakini joka na malaika zake wakashindwa na hapakuwa tena na nafasi kwa ajili yao mbinguni. Lile joka kuu likatupwa chini, yule nyoka wa zamani aitwaye ibilisi au Shetani, aupotoshaye ulimwenguni wote. Akatupwa chini duniani, yeye pamoja na malaika zake. Kisha nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema: “Sasa Wokovu na uweza na Ufalme wa Mungu wetu umekuja na mamlaka ya Kristo wake. Kwa kuwa ametupwa chini mshtaki wa ndugu zetu, anayewashtaki mbele za Mungu usiku na mchana. Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo na kwa neno la ushuhuda wao. Wala wao hawakuyapenda maisha yao hata kufa. Kwa hiyo, furahini ninyi mbingu na wote wakaao humo! Lakini ole wenu nchi na bahari, kwa maana huyo Shetani ameshuka kwenu, akiwa amejaa ghadhabu, kwa sababu anajua ya kuwa muda wake ni mfupi!”
”Lile joka lilipoona kuwa limetupwa chini duniani, lilimfuatilia yule mwanamke aliyekuwa amezaa mtoto mwanamume. Lakini huyo mwanamke akapewa mabawa mawili ya tai mkubwa, kusudi aweze kuruka mpaka mahali palipotayarishwa kwa ajili yake huko nyikani, ambako atatunzwa kwa wakati na nyakati na nusu, wakati ambako yule joka hawezi kufika. Ndipo lile joka likamwaga maji kama mto kutoka kinywani mwake, ili kumfikia huyo mwanamke na kumkumba kama mafuriko. Lakini nchi ikamsaidia huyo mwanamke kwa kufungua kinywa na kuumeza huo mto ambao huyo joka alikuwa ameutoa kinywani mwake. Kisha lile joka likapatwa na hasira kali kwa ajili ya huyo mwanamke, likaondoka ili kupigana vita na watoto waliosalia wa huyo mwanamke, yaani, wale wanaozitii amri za Mungu na kuushika ushuhuda wa Yesu Kristo. Lile joka likasimama kwenye mchanga wa bahari.
”Yule joka akajikita katika mchanga ulioko ufuoni mwa bahari. Nami nikamwona mnyama akitoka ndani ya bahari. Mnyama huyo alikuwa na pembe kumi na vichwa saba, akiwa na taji kumi kwenye hizo pembe zake na juu ya kila kichwa kulikuwa na jina la kukufuru. Mnyama yule niliyemwona alikuwa kama chui, miguu yake ilikuwa kama ya dubu na kichwa chake kama cha simba. Lile joka likampa huyo mnyama nguvu zake, kiti chake cha enzi na mamlaka makubwa. Kimojawapo ya vichwa vya huyo mnyama kilikuwa kama kilichokwisha kupata jeraha la mauti, lakini jeraha hilo la mauti likapona. Ulimwengu wote ukashangaa ukamfuata huyo mnyama. Watu wakaliabudu lile joka kwa sababu lilikuwa limempa huyo mnyama mamlaka yake, pia wakamwabudu huyo mnyama na kuuliza, “Ni nani aliye kama huyu mnyama? Ni nani awezaye kupigana vita naye?” Huyo mnyama akapewa kusema maneno ya kujisifu na kukufuru na kutumia mamlaka yake kwa muda wa miezi arobaini na miwili. Akafungua kinywa chake ili kumkufuru Mungu, akilitukana Jina lake na mahali aishipo na wale wakaao mbinguni.
”Pia akaruhusiwa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda. Akapewa uwezo juu ya watu wa kila kabila, jamaa, lugha na taifa. Nao watu wote waishio duniani watamwabudu huyo mnyama, yaani, wale wote ambao majina yao hayakuandikwa kwenye kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo aliyechinjwa tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Yeye aliye na sikio na asikie. Ikiwa mtu ni wa kuchukuliwa mateka, atachukuliwa mateka. Ikiwa mtu ni wa kuuawa kwa upanga, atauawa kwa upanga. Hapa ndipo penye wito kwa ajili ya saburi na imani ya watakatifu.
”Kisha nikamwona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika dunia. Alikuwa na pembe mbili kama mwana-kondoo, lakini akanena kama joka. Akatumia mamlaka yote ya yule mnyama wa kwanza kwa niaba yake, naye akawafanya wote wakaao duniani kumwabudu yule mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona. Naye akafanya ishara kuu na za ajabu, hata kusababisha moto kushuka toka mbinguni kuja duniani watu wakiona waziwazi. Kwa sababu ya zile ishara alizokuwa amepewa uwezo wa kufanya kwa niaba ya yule mnyama wa kwanza, akawadanganya wakaao duniani. Akawaamuru wasimamishe sanamu kwa heshima ya yule mnyama aliyekuwa amejeruhiwa kwa upanga lakini akaishi. Akapewa uwezo wa kuipa pumzi ile sanamu ya yule mnyama wa kwanza, ili iweze kusema na kuwasababisha wale wote waliokataa kuiabudu hiyo sanamu kuuawa.
”Pia alimlazimisha kila mmoja, mdogo na mkubwa, tajiri na maskini, mtu huru na mtumwa, atiwe chapa kwenye mkono wake wa kuume au kwenye kipaji chake cha uso, ili kwamba mtu ye yote asiweze kununua wala kuuza isipokuwa amekuwa na hiyo chapa, ambayo ni jina la huyo mnyama au tarakimu za jina lake. Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na ufahamu na ahesabu tarakimu za huyo mnyama, kwa maana ni tarakimu za kibinadamu. Tarakimu zake ni 666.
”Kisha nikatazama na hapo mbele yangu alikuwepo Mwana-Kondoo, akiwa amesimama juu ya Mlima Sayuni. Pamoja naye walikuwa wale 144,000 wenye Jina la Mwana-Kondoo na Jina la Baba yake likiwa limeandikwa kwenye vipaji vya nyuso zao. Nami nikasikia sauti kutoka mbinguni kama sauti ya maji mengi yaendayo kasi na sauti kama ngurumo ya radi. Sauti hiyo niliyoisikia ilikuwa kama sauti ya wapiga vinubi wakipiga vinubi vyao. Nao wakaimba wimbo mpya mbele ya hicho kiti cha enzi na mbele ya wale viumbe wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne. Hakuna mtu ye yote aliyeweza kujifunza wimbo huo isipokuwa hao 144,000 waliokuwa wamekombolewa kutoka duniani. Hawa ndio wale ambao hawakujitia unajisi kwa wanawake, kwa kuwa wao ni mabikira. Wao humfuata Mwana-Kondoo kila aendako. Hawa wamekombolewa kutoka miongoni mwa wanadamu wakawa malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo. Vinywani mwao hapakuonekana uongo, wala hawakuwa na hatia yo yote.
”Kisha nikamwona malaika mwingine akiruka juu angani, naye alikuwa na Injili ya milele ya kuwatangazia wale waishio duniani, yaani, kwa kila taifa, kabila, lugha na jamaa. Akasema kwa sauti kubwa, “Mcheni Mungu na kumpa utukufu, kwa maana saa ya hukumu yake imewadia. Mwabuduni yeye aliyeziumba mbingu, dunia, bahari na chemchemi za maji.” Malaika wa pili akafuata akisema, “Ameanguka! Ameanguka Babeli aliye mkuu, yeye aliyeyafanya mataifa yote kulewa kwa mvinyo wa ghadhabu ya uasherati wake.”
”Malaika wa tatu akawafuata hao wawili akisema kwa sauti kubwa, “Kama mtu ye yote anamwabudu huyo mnyama na sanamu yake na kutiwa chapa yake kwenye kipaji chake cha uso au kwenye mkono wake, yeye naye, atakunywa mvinyo wa hasira kali ya Mungu ambayo imemiminwa katika kikombe cha ghadhabu yake pasipo kuchanganywa na maji. Naye atateswa kwa moto uwakao na kiberiti mbele ya malaika watakatifu na mbele za Mwana-Kondoo. Nao moshi wa mateso yao hupanda juu milele na milele. Hakuna mapumziko, mchana wala usiku, kwa wale wamwabuduo huyo mnyama na sanamu yake, au kwa ye yote anayepokea chapa ya jina lake.” Hapa ndipo penye subira na uvumilivu wa watakatifu, yaani, wale wanaozishika amri za Mungu na kudumu kuwa waaminifu kwa Yesu.
”Kisha nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, “Andika: Wamebarikiwa wale wafao katika Bwana tangu sasa.” “Naam,” asema Roho, “watapumzika kutoka katika taabu zao, kwa kuwa matendo yao yatawafuata.”
”Nikatazama, hapo mbele yangu palikuwa na wingu jeupe, na aliyekuwa ameketi juu ya hilo wingu alikuwa “kama Mwana wa Adamu” mwenye taji ya dhahabu kichwani mwake na mundu mkali mkononi mwake. Kisha malaika mwingine akaja kutoka Hekaluni naye akamwita kwa sauti kubwa yule aliyekuwa ameketi juu ya lile wingu akasema, “Chukua mundu wako ukavune kwa kuwa wakati wa mavuno umewadia, kwa maana mavuno ya dunia yamekomaa.” Hivyo yule aliyekuwa ameketi juu ya lile wingu akauzungusha mundu wake duniani, nayo dunia ikavunwa.
”Malaika mwingine akatoka katika Hekalu lililoko mbinguni, naye pia alikuwa na mundu mkali. Kisha malaika mwingine, aliyekuwa na mamlaka juu ya moto, akatoka kwenye madhabahu, naye akamwita yule malaika mwenye mundu mkali kwa sauti kubwa, akisema, “Chukua mundu wako mkali ukakusanye vichala vya mizabibu ya dunia, maana zabibu zake zimeiva.” Hivyo yule malaika akauzungusha mundu wake duniani na kukusanya vichala vya zabibu za dunia na kuzitupa kwenye shinikizo kubwa la ghadhabu ya Mungu. Lile shinikizo likakanyagwa nje ya mji, nayo damu ikatiririka kama mafuriko kutoka katika hilo shinikizo kufikia kimo cha hatamu za farasi, kwa umbali wa maili 200.
”Ndipo nikaona ishara nyingine kubwa ya ajabu mbinguni, malaika saba wenye yale mapigo saba ya mwisho, kwa sababu kwa mapigo hayo ghadhabu ya Mungu ilikuwa imekamilika.
”Nikaona kile kilichoonekana kama bahari ya kioo iliyochanganyikana na moto. Kando ya hiyo bahari, walikuwa wamesimama wale watu waliomshinda yule mnyama na sanamu yake pamoja na tarakimu ya jina lake. Mikononi mwao walikuwa wameshika vinubi walivyopewa na Mungu. Nao wakaimba wimbo wa Mose, mtumishi wa Mungu na wimbo wa Mwana-Kondoo wakisema: “BWANA Mungu Mwenyezi, matendo yako ni makuu na ya ajabu. Njia zako wewe ni za haki na za kweli Mfalme wa nyakati zote! Ni nani ambaye hatakuogopa wewe Bwana na kulitukuza jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako ndiwe mtakatifu. Mataifa yote yatakuja na kuabudu mbele zako, kwa kuwa matendo yako ya haki yamedhihirishwa.”
”Baada ya haya nikatazama, nalo Hekalu la hema la Ushuhuda lilikuwa limefunguliwa mbinguni. Ndani ya lile Hekalu wakatoka malaika saba wakiwa na mapigo saba. Walikuwa wamevaa nguo safi za kitani ing'aayo na kufungwa mikanda ya dhahabu vifuani mwao. Ndipo mmoja wa wale wenye uhai wanne akawapa wale malaika saba mabakuli saba ya dhahabu yaliyojaa ghadhabu ya Mungu, yeye aishiye milele na milele. Nalo lile Hekalu lilijawa na moshi uliotokana na utukufu wa Mungu na uweza wake, wala hakuna ye yote aliyeweza kuingia mle Hekaluni mpaka yale mapigo saba ya wale malaika saba yalipomalizika.
”Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka mle Hekaluni ikiwaambia wale malaika saba, “Nendeni, mkayamwage duniani hayo mabakuli saba ya ghadhabu ya Mungu.”
”Malaika wa kwanza akaenda akalimwaga hilo bakuli lake juu ya nchi. Majipu mabaya yenye maumivu makali yakawapata wale watu wote waliokuwa na chapa ya yule mnyama na walioabudu sanamu yake.
”Malaika wa pili akalimwaga bakuli lake baharini, nayo ikabadilika kuwa damu kama ya mtu aliyekufa na kila kiumbe hai kilichokuwa ndani ya bahari kikafa.
”Malaika wa tatu akalimwaga bakuli lake katika mito na chemchemi za maji, nazo zikawa damu. Ndipo nikamsikia malaika msimamizi wa maji akisema: “Wewe una haki katika hukumu hizi ulizotoa, wewe uliyeko, uliyekuwako, uliye Mtakatifu, kwa sababu umehukumu hivyo; kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu wako na manabii wako, nawe umewapa damu wanywe kama walivyostahili.” Nikasikia madhabahu ikiitikia, “Naam, BWANA Mungu Mwenyezi, hukumu zako ni kweli na haki.”
”Malaika wa nne akamimina bakuli lake kwenye jua, nalo likapewa nguvu za kuwaunguza watu kwa moto. Watu wakaunguzwa na hilo joto kali, wakalaani Jina la Mungu, aliyekuwa na uwezo juu ya mapigo haya, tena wakakataa kutubu na kumtukuza Mungu.
”Malaika wa tano akamimina bakuli lake kwenye kiti cha enzi cha yule mnyama, nao ufalme wake ukagubikwa na giza. Watu wakatafuna ndimi zao kwa ajili ya maumivu wakamlaani Mungu wa mbinguni kwa sababu ya maumivu na majeraha yao, wala hawakutubu kwa ajili ya matendo yao maovu.
”Malaika wa sita akamimina bakuli lake kwenye mto mkubwa Eufrati, maji yake yakakauka ili kutayarisha njia kwa ajili ya wafalme watokao Mashariki.
”Kisha nikaona roho wachafu watatu waliofanana na vyura wakitoka katika kinywa cha lile joka na katika kinywa cha yule mnyama na katika kinywa cha yule nabii wa uongo. Hizo ndizo roho za pepo wachafu zitendazo miujiza. Nazo huwaendea wafalme wa ulimwengu wote na kuwakusanya tayari kwa ajili ya vita katika siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi. “Tazama, naja kama mwivi! Amebarikiwa yeye akeshaye na kuziweka tayari nguo zake ili asiende uchi na kuonekana aibu yake.” Ndipo wakawakusanya wafalme pamoja mahali paitwapo Armagedoni kwa Kiebrania.
”Malaika wa saba akamimina bakuli lake angani na sauti kubwa ikatoka mle Hekaluni katika kile kiti cha enzi, ikisema, “Imekwisha kuwa!” Kukawa na mianga ya umeme wa radi, ngurumo, radi na tetemeko kubwa la ardhi. Hapajawa kamwe na tetemeko la ardhi kama hilo tangu mwanadamu awepo duniani, hivyo lilikuwa tetemeko kubwa ajabu. Ule mji mkubwa ukagawanyika katika sehemu tatu, nayo miji ya mataifa ikaanguka. Mungu akaukumbuka Babeli ule uliokuwa mkuu na kuupa kikombe cha hasira na ghadhabu yake. Kila kisiwa kikatoweka wala milima haikuonekana. Mvua kubwa ya mawe, mawe yenye uzito wa talanta moja yakaanguka kutoka mbinguni, yakawaangukia wanadamu. Nao wanadamu wakamlaani Mungu kwa ajili ya hayo mapigo ya mvua ya mawe, kwa sababu pigo hilo lilikuwa la kutisha.
”Mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na yale mabakuli saba akaja akaniambia, “Njoo, nitakuonyesha adhabu ya yule kahaba mkuu, aketiye juu ya maji mengi. Yule ambaye wafalme wa dunia walizini naye na watu wakaao duniani walilewa kwa mvinyo wa uzinzi wake.” Kisha yule malaika akanichukua katika Roho akanipeleka nyikani. Huko nikamwona mwanamke mmoja ameketi juu ya mnyama mwekundu aliyejaa majina ya kumkufuru Mungu mwili mzima. Mnyama huyo alikuwa na vichwa saba na pembe kumi. Huyo mwanamke alikuwa amevaa mavazi ya rangi ya zambarau na nyekundu, akimetameta kwa dhahabu, vito vya thamani na lulu. Mkononi mwake alikuwa ameshika kikombe cha dhahabu kilichojaa mambo ya machukizo na uchafu wa uzinzi wake. Kwenye kipaji chake cha uso palikuwa pameandikwa jina: “SIRI, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA DUNIA.” Nikaona kuwa huyo mwanamke alikuwa amelewa kwa damu ya watakatifu, yaani, damu ya wale watu waliouawa kwa ushuhuda wa Yesu. Nilipomwona huyo mwanamke, nilistaajabu sana. Ndipo yule malaika akaniambia, “Kwa nini unastaajabu? Nitakufafanulia siri ya huyo mwanamke na huyo mnyama aliyempanda, mwenye vichwa saba na pembe kumi.
”Huyo mnyama, ambaye ulimwona, wakati fulani alikuwepo, lakini sasa hayupo, naye atapanda kutoka katika lile Shimo lisilo na mwisho na kwenda kwenye maangamizo yake. Watu waishio duniani ambao majina yao hayakuandikwa kwenye kitabu cha uzima tangu kuumbwa kwa ulimwengu watastaajabu kumwona huyo mnyama, kwa maana alikuwepo, wakati fulani na sasa hayupo, lakini atakuja. “Hapa ndipo penye akili pamoja na hekima. Vile vichwa saba ni vilima saba ambavyo huyo mwanamke amevikalia. Pia hivyo vichwa saba ni wafalme saba ambao miongoni mwao watano wamekwisha kuanguka, mwingine hajaja bado, lakini atakapokuja, atalazimika kukaa kwa muda mfupi. Yule mnyama aliyekuwepo wakati fulani na ambaye sasa hayupo, yeye ni mfalme wa nane. Ni miongoni mwa wale saba, naye anakwenda kwenye maangamizi yake. “Zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme kumi ambao bado hawajapokea ufalme, lakini ambao watapokea mamlaka kuwa wafalme kwa saa moja pamoja na yule mnyama. Hawa wana nia moja, nao watamwachia yule mnyama nguvu zao na mamlaka yao.
”Watafanya vita na Mwana-Kondoo, lakini Mwana-Kondoo atawashinda kwa sababu yeye ni Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme. Yeye atakuwa pamoja na watu wake walioitwa ambao ni wateule wake na wafuasi wake waaminifu.” Kisha yule malaika akaniambia, “Yale maji uliyoyaona, yule kahaba akiwa ameketi juu yake ni jamaa za watu, makutano, mataifa na lugha. Zile pembe kumi ulizoziona, pamoja na huyo mnyama, watamchukia huyo kahaba, watamfilisi na kumwacha uchi, watamla nyama yake na kumteketeza kwa moto. Kwa maana Mungu ataweka mioyoni mwao kutimiza kusudi lake kwa kukubali kumpa yule mnyama mamlaka yao ya utawala mpaka maneno ya Mungu yatakapotimia. Yule mwanamke uliyemwona ni ule mji mkubwa unaotawala juu ya wafalme wa dunia.”
”Baada ya haya nikaona malaika mwingine akishuka kutoka mbinguni, akiwa na mamlaka makuu na dunia ikamulikiwa na mng'ao wake. Naye akalia kwa nguvu kwa sauti kubwa, akisema: “Umeanguka! Umeanguka Babeli uliye Mkuu! Umekuwa makao ya mashetani na makazi ya kila pepo mchafu, makazi ya kila ndege na kila mnyama achukizaye. Kwa maana mataifa yote yamekunywa mvinyo wa uasherati wake. Nao wafalme wa dunia wamefanya uzinzi naye, nao wafanya biashara wa dunia wametajirika kutokana na wingi wa utajiri wake.”
”Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni ikisema: “Tokeni katikati yake, enyi watu wangu, ili msije mkashiriki dhambi zake, ili msije mkapatwa na pigo lake lo lote; kwa kuwa dhambi zake zimerundikana hadi mbinguni, naye Mungu ameukumbuka uhalifu wake. Mtendee kama yeye alivyotenda; umlipe mara mbili kwa ajili ya yale aliyotenda. Katika kikombe chake mchanganyie mara mbili ya kile alichochanganya. Mpatie mateso na huzuni nyingi sawa na utukufu na anasa alizojipatia. Kwa kuwa moyoni mwake hujivuna, akisema, ‘Mimi ninatawala kama malkia; mimi si mjane, wala sitaona huzuni kamwe.’ Kwa hiyo mapigo yatampata kwa siku moja: mauti, maombolezo na njaa. Naye atateketezwa kwa moto, kwa maana amhukumuye ni BWANA Mungu Mwenyezi.
”“Wafalme wa dunia waliozini naye na kushiriki anasa zake watakapoona moshi wa kuungua kwake, watamlilia na kumwombolezea. Watasimama mbali na kulia kwa hofu kutokana na mateso yake na kusema: “ ‘Ole! Ole Ee mji mkubwa, Ee Babeli mji wenye nguvu! Hukumu yako imekuja katika saa moja!’ “Wafanyabiashara wa dunia watalia na kuomboleza kwa sababu hakuna anunuaye bidhaa zao tena: Bidhaa za dhahabu, za fedha, za vito vya thamani na vya lulu, kitani safi, nguo za rangi ya zambarau, hariri, nguo nyekundu, aina zote za miti ya manukato, vifaa vyote vya pembe za ndovu, vifaa vyote vya miti yenye thamani kuliko yote, shaba nyeusi, chuma na marmar, mdalasini, vikolezi, uvumba, manemane, uvumba wenye harufu nzuri, divai, mafuta ya zeituni, unga mzuri na ngano, ng'ombe na kondoo, farasi na magari, watumwa, pia na roho za wanadamu. “Watasema, ‘Yale matunda ambayo roho yako iliyatamani yamekoma. Utajiri wako wote na fahari yako vimetoweka, wala haviwezi kupatikana tena kamwe!’ Wale wafanyabiashara waliotajirika kwa bidhaa hizo kutoka kwake watasimama mbali naye kwa hofu ya mateso yanayompata. Watalia na kuomboleza wakipiga kelele wakisema: “ ‘Ole! Ole, Ee, mji mkubwa, uliyekuwa umevikwa mavazi ya kitani safi, ya rangi ya zambarau na nyekundu, ukimetameta kwa dhahabu, vito vya thamani na lulu! Katika muda wa saa moja utajiri wote mkubwa kama huu umeangamia!’ “Kila nahodha, mabaharia wote wasafirio baharini na wote wapatao kipato chao kutokana na bahari, watasimama mbali naye. Watakapoona moshi wa kuungua kwake watalia wakisema, ‘Je, kulipata kuwako mji mkubwa kama huu?’ Nao watajirushia mavumbi vichwani mwao, huku wakilia na kuomboleza, wakisema: “ ‘Ole! Ole, Ee mji mkubwa, mji ambao wote wenye meli baharini walitajirika kwa kupitia mali zake! Katika saa moja tu ameangamizwa! Furahia kwa ajili yake, Ee mbingu! Furahini watakatifu, mitume na manabii! Kwa kuwa Mungu amemhukumu kwa vile alivyowatendea ninyi.’ ” Kisha malaika mmoja mwenye nguvu akainua jiwe kubwa kama la kusagia akalitupa baharini akisema: “Hivyo ndivyo mji mkubwa Babeli utakavyotupwa chini kwa nguvu wala hautaonekana tena. Nyimbo za wapiga vinubi na waimbaji, wapiga filimbi na sauti za wapiga tarumbeta kamwe hazitasikika tena ndani yako. Ndani yako kamwe hataonekana tena fundi mwenye ujuzi wa aina yo yote. Wala sauti ya jiwe la kusagia kamwe haitasikika tena.
”Mwanga wa taa hautaangaza ndani yako tena. Sauti ya bwana arusi na bibi arusi kamwe haitasikiwa ndani yako tena. Wafanyabiashara wako walikuwa watu maarufu wa dunia. Mataifa yote yalipotoshwa kwa uchawi wako. Ndani yake ilionekana damu ya manabii na ya watakatifu na wote waliouawa duniani.”
”Baada ya haya nikasikia sauti kama ya umati mkubwa mbinguni wakipiga kelele wakisema: “Haleluya! Wokovu na utukufu na uweza ni vya Mungu wetu, kwa maana hukumu zake ni za kweli na za haki. Amemhukumu yule kahaba mkuu aliyeuharibu ulimwengu kwa uzinzi wake. Mungu amemlipiza kisasi kwa ajili ya damu ya watumishi wake.” Wakasema tena kwa nguvu: “Haleluya! Moshi wake huyo kahaba unapanda juu milele na milele.” Wale wazee ishirini na wanne pamoja na wale viumbe wenye uhai wanne wakaanguka kifudifudi, wakamwabudu Mungu, aliyekuwa ameketi kwenye kile kiti cha enzi. Wakasema kwa sauti kuu: “Amen, Haleluya!” Kisha sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi, ikisema: “Msifuni Mungu wetu, ninyi watumishi wake wote, ninyi nyote mnaomcha, wadogo kwa wakubwa!” Kisha nikasikia sauti kama ya umati mkubwa, kama sauti ya maji mengi yaendayo kasi na kama ngurumo kubwa ya radi wakipiga kelele wakisema: “Haleluya! Kwa maana BWANA Mungu wetu Mwenyezi anatawala.
”Tufurahi, tushangilie na kumpa utukufu! Kwa maana arusi ya Mwana-Kondoo imewadia na bibi arusi wake amejiweka tayari. Akapewa kitani safi, nyeupe inayong'aa, ili avae.” (Hiyo kitani safi inawakilisha matendo ya haki ya watakatifu.) Ndipo malaika akaniambia, “Andika: ‘Wamebarikiwa wale walioalikwa kwenye karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo!’ ” Naye akaongeza kusema, “Haya ndiyo maneno ya kweli ya Mungu.” Ndipo nikaanguka kifudifudi miguuni pake ili kumwabudu, lakini yeye akaniambia, “Usifanye hivyo! Mimi pia ni mtumishi mwenzako pamoja na ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Mwabudu Mungu! Maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii.”
”Kisha nikaona mbingu imefunguka na hapo mbele yangu akiwepo farasi mweupe, ambaye yeye aliyempanda huyo farasi aliitwa Mwaminifu na Kweli. Yeye huhukumu kwa haki na kufanya vita. Macho yake ni kama miali ya moto na juu ya kichwa chake kuna taji nyingi. Alikuwa na jina lililoandikwa ambalo hakuna mtu ye yote anayelijua isipokuwa yeye mwenyewe. Alikuwa amevaa joho lililochovywa kwenye damu na Jina lake ni “Neno la Mungu.” Majeshi ya mbinguni walikuwa wakimfuata, wakiwa wamepanda farasi weupe, hali wamevaa mavazi ya kitani nzuri, nyeupe safi. Kinywani mwake hutoka upanga mkali ambao kwa huo atayaangusha mataifa. “Atayatawala kwa fimbo yake ya utawala ya chuma.” Atalikanyaga shinikizo la mvinyo wa ghadhabu ya Mungu Mwenyezi. Kwenye joho lake na paja lake liliandikwa jina hili: MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA.
”Nami nikamwona malaika amesimama ndani kwenye jua, akaita ndege wote warukao angani kwa sauti kuu, “Njoni, kusanyikeni kwa ajili ya karamu kubwa ya Mungu, ili mpate kula nyama ya wafalme na ya majemadari, ya mashujaa, ya farasi na ya wapanda farasi, nyama ya wanadamu, wote walio huru na watumwa, wadogo na wakubwa.”
”Kisha nikamwona yule mnyama na wafalme wa dunia pamoja na majeshi yao wakiwa wamekusanyika pamoja ili kufanya vita dhidi ya yule aliyempanda huyo farasi mweupe pamoja na jeshi lake. Lakini yule mnyama akakamatwa pamoja na huyo nabii wa uongo ambaye alikuwa amefanya ishara kwa niaba ya huyo mnyama, ambaye kwa ishara hizi aliwadanganya wale waliopokea chapa ya huyo mnyama na kuiabudu sanamu yake. Hawa wawili wakatupwa wakiwa hai ndani ya ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti. Wale waliosalia waliuawa kwa upanga uliotoka kinywani mwa yule aliyekuwa amempanda huyo farasi mweupe, nao ndege wote wakajishibisha kwa nyama yao.
”Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, akiwa ameshika ufunguo wa lile Shimo lisilo na mwisho na mnyororo mkubwa mkononi mwake. Akalishika lile joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ndiye ibilisi na Shetani, naye akamfunga kwa muda wa miaka 1,000. Akamtupa katika lile Shimo lisilo na mwisho, akamfunga humo na kulitia lakiri, ili kumzuia asiendelee kudanganya mataifa mpaka hiyo miaka 1,000 itimie. Baada ya hayo lazima afunguliwe kwa muda mfupi.
”Kisha nikaona viti vya enzi vilivyokuwa vimekaliwa na hao waliopewa mamlaka ya kuhukumu. Nami nikaona roho za wale waliokatwa vichwa kwa sababu ya ushuhuda wa Yesu na kwa sababu ya neno la Mungu. Hawakuwa wamemsujudia huyo mnyama wala sanamu yake wala hawakupokea ile chapa yake kwenye vipaji vya nyuso zao au kwenye mikono yao. Wakawa hai na kutawala pamoja na Kristo miaka 1,000. (Wafu waliosalia hawakufufuka mpaka ilipotimia hiyo miaka 1,000.) Huu ndio ufufuo wa kwanza. Waliobarikiwa na walio watakatifu ni wale walio na sehemu katika ufufuo wa kwanza. Hao mauti ya pili haina nguvu juu yao, bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye kwa muda wa miaka 1,000.
”Hiyo miaka 1,000 itakapotimia, Shetani atafunguliwa kutoka kifungoni mwake, naye atatoka ili kuyadanganya mataifa yaliyopo katika pembe nne za dunia, yaani, Gogu na Magogu apate kuwakusanya tayari kwa vita. Idadi yao ni kama mchanga ulioko Pwani. Nao walitembea katika eneo lote la dunia, wakaizunguka kambi ya watakatifu na ule mji unaopendwa. Lakini moto ukashuka kutoka mbinguni na kuwateketeza.
”Naye ibilisi aliyewadanganya akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti walikokuwa wametupwa yule mnyama na yule nabii wa uongo. Watateswa humo mchana na usiku, milele na milele.
”Kisha nikaona kiti kikubwa cheupe cha enzi pamoja na yeye aliyeketi juu yake. Dunia na mbingu zikaukimbia uso wake wala mahali pao hapakuonekana. Nami nikawaona wafu wakubwa na wadogo, wakiwa wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi na vitabu vikafunguliwa. Pia kitabu kingine kikafunguliwa ambacho ni cha uzima. Hao wafu wakahukumiwa sawasawa na matendo yao kama yalivyoandikwa ndani ya hivyo vitabu. Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake, nayo mauti na kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Kila mtu akahukumiwa kulingana na yale aliyotenda. Kisha Mauti na Kuzimu zikatupwa katika ziwa la moto. Hii ndio Mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. Iwapo mtu jina lake halikuonekana katika kile kitabu cha uzima, alitupwa ndani ya lile ziwa la moto.
”Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya, kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza vimekwisha kupita, wala hapakuwepo na bahari tena. Nikaona Mji Mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, ukiwa umeandaliwa kama bibi arusi aliyepambwa kwa ajili ya mumewe.
”Nami nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, “Sasa makao ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atakaa pamoja nao. Yeye atakuwa Mungu wao nao watakuwa watu wake, naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. Atafuta kila chozi, kutoka katika macho yao. Mauti haitakuwepo tena, wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu, kwa maana mambo ya kwanza yamekwisha kupita.” Naye yule aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi akasema, “Tazama, nayafanya mambo yote kuwa mapya!” Kisha akasema, “Andika haya, maana maneno haya ni ya kuaminika tena ni kweli.” Akaniambia, “Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Yeye aonaye kiu nitampa kunywa kutoka katika chemchemi ya maji ya uzima bila gharama yo yote. Yeye atakayeshinda atayarithi haya yote, Nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu. Lakini waoga, wasioamini, wachafu, wauaji, wazinzi, wachawi, waabudu sanamu, pamoja na waongo wote, mahali pao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.” Mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na yale mabakuli saba ya hayo mapigo saba ya mwisho akaja akaniambia, “Njoo, nami nitakuonyesha bibi arusi, yaani, mke wa Mwana-Kondoo.”
”Naye akanichukua katika Roho hadi kwenye mlima mkubwa na mrefu, akanionyesha ule Mji Mtakatifu, Yerusalemu, likishuka kutoka mbinguni kwa Mungu. Ulikuwa uking'aa kwa utukufu wa Mungu kama kito chenye thamani sana, kama yaspi, safi kama kioo. Ulikuwa na ukuta mkubwa, mrefu wenye malango kumi na mawili, pakiwa na malaika kumi na wawili kwenye hayo malango. Kwenye malango hayo yaliandikwa majina ya yale makabila kumi na mawili ya Israeli. Kulikuwa na malango matatu upande wa mashariki, matatu upande wa kaskazini, matatu upande wa kusini na matatu upande wa magharibi. Ukuta wa huo mji ulikuwa na misingi kumi na miwili na juu yake yaliandikwa majina ya wale mitume kumi na wawili wa Mwana-Kondoo. Huyo malaika aliyesema nami alikuwa na ufito wa dhahabu wa kupimia huo mji, malango yake na kuta zake. Mji huo ulikuwa mraba, urefu wake ulikuwa sawa na upana wake. Akaupima huo mji kwa huo ufito akakuta una kama kilomita 2,400; urefu wake na upana wake na kwenda juu kwake vilikuwa sawa. Akaupima ukuta wake, ulikuwa na unene wa dhiraa 144 kwa kipimo cha kibinadamu ambacho huyo malaika alikuwa akikitumia. Ukuta huo ulijengwa kwa yaspi hali mji wenyewe ulijengwa kwa dhahabu safi, iking'aa kama kioo. Misingi ya kuta za mji huo zilipambwa kwa kila aina ya kito cha thamani. Msingi wa kwanza ulikuwa wa yaspi, wa pili yakuti samawi, wa tatu kalkedoni, wa nne zumaridi, wa tano sardoniki, wa sita akiki, wa saba krisolitho, wa nane zabarajadi, wa tisa yakuti manjano, wa kumi krisopraso, wa kumi na moja hiakintho, wa kumi na mbili amethisto. Yale malango kumi na mbili yalikuwa ni lulu kumi na mbili, kila lango lilikuwa limetengenezwa kwa lulu moja. Barabara za mji huo zilikuwa za dhahabu safi ing'aayo kama kioo.
”Sikuona Hekalu ndani ya huo mji kwa sababu BWANA Mungu Mwenyezi na Mwana-Kondoo ndio Hekalu lake. Ule mji hauhitaji jua wala mwezi kuuangazia, kwa sababu utukufu wa Mungu ndio nuru yake na Mwana-Kondoo ndiye taa yake. Mataifa yatatembea yakiangaziwa na nuru yake na wafalme wa duniani wataleta fahari yao ndani yake. Malango yake hayatafungwa kamwe, kwa maana hakutakuwa na usiku humo. Utukufu na heshima za mataifa zitaletwa humo. Lakini kitu kichafu hakitaingia humo kamwe, wala mtu ye yote atendaye mambo ya aibu au ya udanganyifu. Bali watakaoingia humo ni wale tu ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.
”“Tazama, naja upesi! Thawabu yangu i mkononi mwangu, nami nitampa kila mtu sawasawa na alivyotenda.
”