01 – Biblia Takatifu
Haya ni maneno matakatifu ya Mungu Mwenyezi.
Hatupendi maneno ya wanadamu.
Kwa mtu yeyote anayempenda Mungu... hivi ndivyo Mungu anasema kuhusu: Biblia Takatifu.
Haya ni maneno matakatifu ya Mungu Mwenyezi.
Hatupendi maneno ya wanadamu.
Kwa mtu yeyote anayempenda Mungu... hivi ndivyo Mungu anasema kuhusu: Biblia Takatifu.
Kila Andiko limevuviwa na Mungu na lafaa kwa mafundisho, kwa kuwaonya watu makosa yao, kuwaongoza na kuwafundisha katika haki
”Kwa maana, amin nawaambia, mpaka mbingu na dunia zitakapopita, hakuna hata herufi moja ndogo wala nukta itakayopotea kwa namna yo yote kutoka kwenye Torati mpaka kila kitu kiwe kimetimia.
”Yuko amhukumuye yeye anikataaye mimi na kutokuyapokea maneno yangu, yaani, yale maneno niliyosema yenyewe yatamhukumu siku ya mwisho.
”Mungu akaona ya kuwa nuru ni njema, ndipo Mungu akatenganisha nuru na giza.
”Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa porini ambao BWANA Mungu aliwafanya. Nyoka akamwambia mwanamke, “Ati kweli Mungu alisema, ‘Kamwe msile matunda ya mti wo wote wa bustanini’?”
”BWANA akaona jinsi ambavyo uovu wa mwanadamu umekuwa mkubwa duniani na ya kuwa kila mwelekeo wa mawazo ya moyo wake wakati wote ulikuwa mbaya tu.
”BWANA ni shujaa wa vita; BWANA ndilo jina lake.
”Mose alipokwenda na kuwaambia watu maneno yote na sheria zote za BWANA, wakaitikia kwa sauti moja, “Kila kitu alichosema BWANA tutakifanya.” Ndipo Mose akaandika kila kitu BWANA alichokuwa amesema. Akaamka kesho yake asubuhi na mapema na kujenga madhabahu chini ya mlima na kusimamisha nguzo kumi na mbili za mawe kuwakilisha makabila kumi na mawili ya Israeli.
”Mungu si mtu, hata aseme uongo, wala yeye si mwanadamu, hata ajute. Je, anasema, kisha asitende? Je, anaahidi, asitimize?
”Usiongeze wala usipunguze cho chote ninachowaamuru ninyi, ila myashike maagizo ya BWANA Mungu wenu ambayo nawapa.
”Tazama, nimewafundisha amri na sheria kama BWANA Mungu wangu alivyoniamuru mimi, ili mzifuate katika nchi mnayoiingia kuimiliki. Zishikeni kwa uangalifu, kwa kuwa hii itaonyesha hekima na ufahamu wenu kwa mataifa, ambayo yatasikia kuhusu amri zote hizi, nao watasema, “Hakika taifa hili kubwa ni watu wenye hekima na ufahamu.”
”Kumbuka siku uliyosimama mbele za BWANA Mungu wako kule Horebu, wakati aliponiambia, “Wakutanishe watu mbele yangu wasikie maneno yangu ili kwamba waweze kujifunza kuniheshimu kwa muda wote watakaoishi katika nchi, nao waweze kuwafundisha watoto wao maneno hayo.”
”Kwa kuwa BWANA Mungu wenu ni moto ulao, Mungu mwenye wivu.
”Hivyo iweni waangalifu kuyafanya yale BWANA Mungu wenu aliyowaagiza; msigeuke upande wa kuume wala wa kushoto.
”Mpende BWANA Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote na kwa nguvu zako zote. Amri hizi ninazokupa leo zitakuwa katika moyo wako. Wafundishe watoto wako kwa bidii. Nena kuhusu amri hizi uketipo nyumbani na wakati utembeapo njiani, ulalapo na uamkapo. Zifunge kama alama juu ya mkono wako, na uzifunge juu ya paji la uso wako. Ziandike kwenye miimo ya milango ya nyumba yako na juu ya malango yako.
”Alikudhili na kukufanya uone njaa kisha akulishe kwa mana, ambayo wewe wala baba zako hamkuijua, awafundishe kuwa mwanadamu hataishi kwa mkate tu bali kwa kila neno litokalo katika kinywa cha BWANA.
”Shikeni maagizo ya BWANA Mungu wenu mtembee katika njia zake na kumheshimu.
”Naye BWANA akaniambia, “Nimewaona watu hawa nao ni watu wenye shingo ngumu sana!
”Na sasa, Ee Israeli, BWANA Mungu wako anataka nini kwako ila kumcha BWANA Mungu wako, kwenda katika njia zake, kumpenda na kumtumikia BWANA Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote, na kuyashika maagizo ya BWANA na amri zake ninazokupa leo kwa mafanikio yako mwenyewe?
”Mpende BWANA Mungu wako na kushika masharti yake, amri zake, sheria zake na maagizo yake siku zote.
”Yawekeni haya maneno yangu katika mioyo yenu na akili zenu, yafungeni kama alama juu ya mikono yenu na kwenye paji za nyuso zenu. Wafundisheni watoto wenu, yazungumzeni wakati mketipo nyumbani na wakati mtembeapo njiani, wakati mlalapo na wakati mwamkapo. Yaandikeni juu ya miimo ya nyumba zenu na juu ya malango yenu,
”Tazama, leo ninaweka mbele yenu baraka na laana: baraka kama mtatii maagizo ya BWANA Mungu wenu, ambayo ninawapa leo; laana kama hamtatii maagizo ya BWANA Mungu wenu na kuacha njia ambayo ninawaamuru leo kwa kufuata miungu mingine, ambayo hamkuijua.
”Angalieni kwamba mnafanya yote niliyowaamuru; msiongeze kitu wala msipunguze kitu.
”Kama nabii, au yule anayetabiri kwa njia ya ndoto, akijitokeza miongoni mwenu na akawatangazia ishara ya miujiza na ajabu, ikiwa ishara au ajabu ya aliyozungumza ikatokea, naye akasema, “Na tufuate miungu mingine” (miungu ambayo hamjaifahamu) “na tuiabudu,” kamwe msiyasikilize maneno ya nabii wala mwota ndoto huyo. BWANA Mungu wenu anawajaribu kuangalia kama mnampenda kwa moyo wenu wote na kwa roho yenu yote. Ni BWANA Mungu wenu ambaye mnapaswa kumfuata tena ni yeye mnapaswa kumheshimu. Shikeni maagizo yake na kumtii, mtumikieni na kushikamana naye.
”Atakuwa na nakala hiyo, naye ataisoma siku zote za maisha yake ili kwamba ajifunze kumheshimu BWANA Mungu wake na kufuata kwa uangalifu maneno yote ya sheria hii na amri hizi,
”BWANA Mungu wako anakuagiza leo kufuata amri hizi na sheria; zishike kwa bidii kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote.
”“Alaaniwe mtu ambaye hatashika maneno haya ya sheria hii kwa kuyafanya.” Kisha watu wote watasema, “Amen!”
”Kama ukimtii BWANA Mungu wako kwa bidii na kufuata amri zake zote ninazokupa leo kwa bidii, BWANA Mungu wako atakuweka juu ya mataifa yote katika dunia.
”Hata hivyo, kama hutamtii BWANA Mungu wako na kuzishika kwa bidii amri zake zote na maagizo ninayokupa leo, laana hizi zote zitakuja juu yako na kukupata:
”Mambo ya siri ni ya BWANA Mungu wetu, bali yaliyofunuliwa ni yetu na watoto wetu milele, ili tuweze kuyafanya maneno yote ya sheria hii.
”kama ukimtii BWANA Mungu wako, na kuzishika amri zake na maagizo yake ambayo yameandikwa katika Kitabu hiki cha Sheria, na kumgeukia BWANA Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote.
”Leo ninaziita mbingu na nchi kama mashahidi dhidi yako kwamba nimeweka mbele yako uzima na mauti, baraka na laana. Basi sasa chagueni uzima, ili wewe na watoto wako mpate kuishi,
”Kusanya watu wote, wanaume, wanawake, watoto na wageni wanaoishi katika miji yenu, ili waweze kusikia na kujifunza kumcha BWANA Mungu wenu na kufuata kwa bidii maneno yote ya sheria hii.
”“Chukueni Kitabu hiki cha Sheria mkakiweke kando ya Sanduku la Agano la BWANA Mungu wenu. Hapo ndipo kitakapokaa kama shahidi dhidi yenu. Kwa kuwa ninajua jinsi mlivyo waasi na mlivyo na shingo ngumu. Kama mmekuwa mkiasi dhidi ya BWANA nikiwa bado niko hai na nikiwa pamoja nanyi, mtaasi mara ngapi baada ya kufa kwangu!
”Usiache Kitabu hiki cha Torati kiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, ili upate kuwa mwangalifu kufanya kila kitu sawasawa na yote yaliyoandikwa ndani yake. Ndipo utakapoifanikisha njia yako na kisha utastawi sana.
”Lakini hakikisheni mnamcha BWANA na kumtumikia kwa uaminifu kwa moyo wenu wote, tafakarini ni mambo gani makubwa aliyotenda kwa ajili yenu.
”Lakini Samweli akajibu: “Je, BWANA anafurahia sadaka za kuteketezwa na dhabihu kama vile kuitii sauti ya BWANA? Kutii ni bora zaidi kuliko dhabihu, nako kusikia ni bora kuliko mafuta ya kondoo dume. Kwa maana kuasi ni kama dhambi ya uaguzi, nao ukaidi ni kama uovu wa kuabudu sanamu. Kwa sababu umelikataa neno la BWANA, naye amekukataa wewe kuendelea kuwa mfalme.” Ndipo Sauli akamwambia Samweli, “Nimetenda dhambi. Nimevunja amri ya BWANA na maagizo yako. Niliwaogopa watu na kwa hiyo nikafanya walivyotaka.
”Kwa maana nimezishika njia za BWANA sijatenda ubaya nikamwacha Mungu wangu. Sheria zake zote zi mbele yangu, wala sijayaacha maagizo yake.
”Lakini hawakusikiliza, walikuwa na shingo ngumu kama baba zao, ambao hawakumtegemea BWANA Mungu wao.
”“Nendeni mkamwulize BWANA kwa ajili yangu na kwa ajili ya mabaki walioko Israeli na Yuda kuhusu haya yaliyoandikwa katika kitabu hiki ambacho kimeonekana hekaluni. Hasira ya BWANA ni kubwa mno ambayo imemwagwa juu yetu kwa sababu baba zetu hawakulishika neno la BWANA wala hawakutenda sawasawa na yale yote yaliyoandikwa katika Kitabu hiki.”
”Lakini waliwadhihaki wajumbe wa BWANA wakayadharau maneno yake na kuwacheka manabii wake mpaka ghadhabu ya BWANA ikawa kubwa dhidi ya watu wake na hakukuwa na namna ya kuituliza.
”Kwa maana Ezra alikuwa amejitoa kwa moyo wote kujifunza na kushika sheria ya BWANA na kuwafundisha watu wa Israeli amri na sheria zake.
”Kisha kila mmoja aliyetetemeshwa na maneno ya Mungu wa Israeli alikusanyika kunizunguka kwa sababu ya upotovu huu wa hao watu waliorudi kutoka utumwani. Nami niliketi pale nikishangaa mpaka wakati wa dhabihu ya jioni.
”Lakini humwambia Mungu, ‘Tuache sisi!’ Hatuna haja ya kufahamu njia zako.
”Sijaziacha amri zilizotoka midomoni mwake, bali nimeyathamini maneno ya kinywa chake kuliko chakula changu cha kila siku.
”Kisha BWANA akamjibu Ayubu kutoka katika upepo wa kisulisuli. Akasema: “Nani huyu atiaye mashauri yangu giza kwa maneno yasiyo na maarifa? Jikaze kama mwanaume, nami nitakuuliza swali, nawe unijibu. “Ulikuwa wapi nilipoweka misingi ya dunia? Niambie, kama unafahamu.
”Bali huifurahia sheria ya BWANA, naye huitafakari hiyo sheria mchana na usiku.
”Maneno ya BWANA ni safi, kama fedha iliyosafishwa katika tanuru, iliyosafishwa mara saba. Ee BWANA, utatuweka salama na kutulinda na kizazi hiki milele.
”Kwa maana nimezishika njia za BWANA, sijatenda ubaya nikamwacha Mungu wangu.
”Kuhusu Mungu, njia yake ni kamilifu, neno la BWANA ni kamili. Yeye ni ngao kwa wote wanaokimbilia kwake.
”Sheria ya BWANA ni kamilifu, ikihuisha nafsi. Shuhuda za BWANA ni za kuaminika, zikimpa mjinga hekima. Maagizo ya BWANA ni kamili, nayo hufurahisha moyo. Amri za BWANA huangaza, zatia nuru machoni. Kumcha BWANA ni utakatifu, nako kwadumu milele. Amri za BWANA ni za hakika, nazo zina haki. Ni za thamani kuliko dhahabu, kuliko dhahabu iliyo safi sana, ni tamu kuliko asali, kuliko asali kutoka kwenye sega. Kwa hizo mtumishi wako anaonywa, katika kuzishika kuna thawabu kubwa.
”kwa maana upendo wako uko mbele yangu daima, nami natembea siku zote katika kweli yako.
”Sauti ya BWANA ina nguvu; sauti ya BWANA ni tukufu.
”Ninaikabidhi roho yangu mikononi mwako, Ee BWANA unikomboe, wewe uliye Mungu wa kweli.
”Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; nitakushauri na kukuangalia. Usiwe kama farasi au nyumbu wasio na akili, ambao ni lazima waongozwe kwa lijamu na hatamu la sivyo hawatakukaribia.
”Dunia yote na imwogope BWANA, watu wote wa dunia wamche.
”Lakini mipango ya BWANA inasimama imara milele, makusudi ya moyo wake kwa vizazi vyote.
”Njoni, watoto wangu, mnisikilize, nitawafundisha kumcha BWANA.
”Ndipo niliposema, “Mimi hapa, nimekuja: imeandikwa kuhusu mimi katika gombo. Ee Mungu wangu, natamani kufanya mapenzi yako; sheria yako iko ndani ya moyo wangu.” Nimehubiri haki katika kusanyiko kubwa, sikufunga mdomo wangu, Ee BWANA, kama ujuavyo. Sikuficha haki yako moyoni mwangu; ninasema juu ya uaminifu wako na wokovu wako. Sikuficha upendo wako na kweli yako mbele ya kusanyiko kubwa.
”Lakini kwake mtu mwovu, Mungu asema: “Una haki gani kunena sheria zangu au kuchukua Agano langu midomoni mwako? Unachukia mafundisho yangu na kuyatupa maneno yangu nyuma yako.
”Ee Mungu, uniumbie moyo safi, uifanye upya roho ya uthabiti ndani yangu.
”Bwana alitangaza neno, waliolitangaza neno hilo walikuwa kundi kubwa:
”Hawakulishika Agano la Mungu na walikataa kuishi kwa sheria yake.
”“Lakini watu wangu hawakutaka kunisikiliza; Israeli hakutaka kunitii. Basi niliwaacha katika ukaidi wa mioyo yao wafuate mashauri yao wenyewe. “Laiti kama watu wangu wangalinisikiliza, kama Israeli wangalifuata njia zangu, ningaliwatiisha adui zao kwa haraka na kuugeuza mkono wangu dhidi ya watesi wao! Wale wanaomchukia BWANA wangalinywea mbele zake, na adhabu yao ingedumu milele.
”Ee BWANA, nifundishe njia yako, nami nitakwenda katika kweli yako; nipe moyo usiositasita, ili niweze kulicha jina lako.
”Katika kusanyiko la watakatifu Mungu huogopwa sana, anahofiwa kuliko wote wanaomzunguka.
”Alituma giza na nchi ikawa giza, kwani si walikuwa wameyaasi maneno yake?
”kwa sababu walikuwa wameasi dhidi ya maneno ya Mungu na kudharau shauri la Aliye Juu Sana. Aliwatumikisha kwa kazi ngumu; walijikwaa na hapakuwepo na ye yote wa kuwasaidia.
”Akalituma neno lake na kuwaponya, akawaokoa kutoka maangamizo.
”Kazi za mikono yake ni za uaminifu na haki, mausia yake yote ni ya kuaminika. Zinadumu milele na milele, zikifanyika kwa uaminifu na unyofu.
”Kumcha BWANA ndicho chanzo cha hekima, wote wanaozifuata amri zake wana busara. Sifa zake zadumu milele.
”Msifuni BWANA. Heri mtu yule amchaye BWANA, mtu yule apendezwaye sana na amri zake.
”Ni bora kumkimbilia BWANA kuliko kumtumainia mwanadamu. Ni bora kumkimbilia BWANA kuliko kuwatumainia wakuu.
”Heri wale walio waadilifu katika njia zao, wanaoenenda katika sheria ya BWANA.
”Hivyo mimi sitaaibishwa ninapozingatia juu ya amri zako zote.
”Jinsi gani kijana aifanye njia yake kuwa safi? Ni kwa kutii akilifuata neno lako.
”Ninakutafuta kwa moyo wangu wote, usiniache niende mbali na amri zako.
”Nimelificha neno lako moyoni mwangu ili nisikutende dhambi.
”Kwa midomo yangu nitasimulia sheria zote zinazotoka katika kinywa chako.
”Yafungue macho yangu nipate kuona mambo ya ajabu katika sheria yako.
”Nafsi yangu inataabika kwa shauku kubwa juu ya sheria zako wakati wote.
”Unawakemea wenye majivuno, waliolaaniwa waendao mbali na amri zako.
”Niepushe na njia za udanganyifu, kwa neema unifundishe sheria zako.
”Nimechagua njia ya kweli, nimekaza moyo wangu katika sheria zako.
”Nipe ufahamu, nami nitaishika sheria yako na kuitii kwa moyo wangu wote.
”Niitii amri yako siku zote, milele na milele.
”kwa kuwa ninazifurahia amri zako kwa sababu ninazipenda.
”Nimeshikwa sana na ghadhabu kwa ajili ya waovu, ambao wameacha sheria yako.
”Nitafanya haraka bila kuchelewa kuzitii amri zako.
”Ilikuwa vyema mimi kupata shida ili nipate kujifunza maagizo yako.
”Sheria inayotoka kinywani mwako ina thamani kubwa kwangu kuliko maelfu ya vipande vya fedha na dhahabu.
”Ee BWANA, neno lako ni la milele, linasimama imara mbinguni.
”Aha! Tazama, sheria yako naipenda mno ajabu. Ninaitafakari mchana kutwa.
”Tazama jinsi maneno yako yalivyo matamu kwangu, matamu kuliko asali katika kinywa changu!
”Ninapata ufahamu kutoka mausia yako, kwa hiyo ninachukia kila njia ya upotovu.
”Neno lako ni taa ya miguu yangu na mwanga katika njia yangu.
”Nimekusudia moyoni mwangu kuyafuata maagizo yako mpaka mwisho.
”Ondokeni kwangu, ninyi mtendao mabaya, ili niweze kushika amri za Mungu wangu!
”Unawakataa wote wanaoyaasi maagizo yako, kwa maana udanganyifu wao ni bure.
”Ee BWANA, wakati wako wa kutenda umewadia, kwa kuwa sheria yako inavunjwa.
”Chemchemi za machozi zinatiririka kutoka machoni pangu, kwa kuwa sheria yako haifuatwi.
”Jitihada yangu imenidhoofisha, kwa kuwa adui zangu wanayapuuza maneno yako.
”Ingawa ni mdogo na ninadharauliwa, sisahau mausia yako.
”Haki yako ni ya milele, na sheria yako ni kweli.
”Sikufumba macho yangu usiku kucha, ili niweze kutafakari juu ya ahadi zako.
”Maneno yako yote ni kweli, sheria zako zote za haki ni za milele.
”Watawala wamenitesa bila sababu, lakini moyo wangu unatetemeka kwa neno lako.
”Nafurahia ahadi zako kama mtu aliyepata mateka mengi.
”Ee BWANA, ninatamani wokovu wako, na sheria yako ni furaha yangu.
”Nitasujudu nikielekea Hekalu lako takatifu, nami nitalisifu jina lako kwa ajili ya upendo wako na uaminifu, kwa kuwa umelikuza jina lako na neno lako juu ya vitu vyote.
”Kumcha BWANA ndiyo chanzo cha maarifa, lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu.
”“Enyi wajinga, mtang'ang'ania ujinga wenu hadi lini? Mpaka lini wenye mizaha watafurahia mizaha na wapumbavu kuchukia maarifa?
”Kwa kuwa walichukia maarifa, wala hawakuchagua kumcha BWANA, kwa kuwa hawakukubali mashauri yangu, na kukataa maonyo yangu, watakula matunda ya njia zao, na watashibishwa matunda ya hila zao.
”kutega sikio lako kwenye hekima na kuweka moyo wako katika ufahamu, na kama ukiita busara na kuita kwa sauti ufahamu, na kama utaitafuta kama fedha na kuitafuta sana kama hazina iliyofichwa, ndipo utakapoelewa kumcha BWANA na kupata maarifa ya Mungu.
”Usiache kamwe upendo na uaminifu vitengane nawe; vifunge shingoni mwako, viandike katika ubao wa moyo wako.
”Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote wala usizitegemee akili zako mwenyewe;
”Pata hekima, pata ufahamu, usiyasahau maneno yangu wala usiyaache. Usimwache hekima naye atakuweka salama, mpende, naye atakulinda.
”Mwanangu, yasikilize kwa makini yale ninayokuambia, sikiliza kwa makini maneno yangu. Usiruhusu yaondoke machoni pako, yahifadhi ndani ya moyo wako,
”Macho yako na yatazame mbele, kaza macho yako moja kwa moja mbele yako. Sawazisha mapito ya miguu yako na njia zako zote ziwe zimethibitika. Usigeuke kulia wala kushoto, epusha mguu wako na ubaya.
”Kwa maana amri hizi ni taa, mafundisho haya ni mwanga na maonyo ya maadili ni njia ya uzima,
”Kumcha BWANA ni kuchukia uovu, ninachukia kiburi na majivuno, tabia mbaya na mazungumzo potovu.
”Usimkemee mwenye mzaha la sivyo atakuchukia; mkemee mwenye hekima naye atakupenda.
”“Kumcha BWANA ni mwanzo wa hekima na kumjua Mtakatifu ni ufahamu.
”Kumcha BWANA ni chemchemi ya uzima, ikimwepusha mtu na mitego ya mauti.
”Ni bora kiasi gani kupata hekima kuliko dhahabu, kuchagua ufahamu kuliko fedha!
”Usizungumze na mpumbavu, kwa maana atadhihaki hekima ya maneno yako.
”Kama mtu ye yote akikataa kusikia sheria, hata maombi yake ni chukizo.
”“Kila neno la Mungu ni kamilifu; yeye ni ngao kwa wale wanaomkimbilia. Usiongeze kwenye maneno yake, ama atakukemea na kukuthibitisha kuwa mwongo.
”Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa: Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.
”Kwa hiyo, kama ndimi za moto zirambavyo nyasi na kama vile majani makavu yazamavyo katika miali ya moto, ndivyo mizizi yao itakavyooza na maua yao yatakavyopeperushwa kama mavumbi; kwa kuwa wameikataa sheria ya BWANA Mwenye Nguvu Zote na kulisukumia mbali neno la Aliye Mtakatifu wa Israeli.
”Akasema, “Nenda ukawaambie watu hawa: “ ‘Mtaendelea daima kusikia, lakini kamwe hamtafahamu; mtaendelea daima kuona, lakini kamwe hamtatambua.’
”Kwa sheria na kwa ushuhuda! Kama hawatasema sawasawa na neno hili, hawana mwanga wa mapambazuko.
”Nenda sasa, liandike neno hili juu ya kibao kwa ajili yao, liandike kwenye kitabu, ili kwa ajili ya siku zijazo liweze kuwa shahidi milele. Hawa ni watu waasi, watoto wadanganyifu, watoto ambao hawataki kusikiliza mafundisho ya BWANA. Wanawaambia waonaji, “Msione maono tena!” Nako kwa manabii wanasema, “Msiendelee kutupatia maono ambayo ni ya kweli! Tuambieni mambo ya kupendeza, tabirini mambo ya uongo. Acheni njia hii, ondokeni katika mapito haya, nanyi acheni kutukabili pamoja na yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli!” Kwa hiyo, hili ndilo asemalo yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli: “Kwa sababu mmekataa ujumbe huu, mkategemea uonevu na kutumainia udanganyifu, dhambi hii itakuwa kwenu kama ukuta mrefu, wenye ufa na wenye kubetuka, ambao unaanguka ghafula, kwa mara moja.
”Majani hunyauka na maua huanguka, lakini neno la Mungu wetu lasimama milele.”
”Ni nani aliyeamini ujumbe wetu na mkono wa BWANA umefunuliwa kwa nani?
”“Kwa kuwa mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu,” asema BWANA. “Kama vile mbingu zilivyo juu kuliko dunia, ndivyo njia zangu zilivyo juu kuliko njia zenu na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.
”ndivyo lilivyo neno langu lile litokalo kinywani mwangu: Halitanirudia tupu, bali litatimiliza lile nililokusudia na litafanikiwa katika kusudi lile nililolituma.
”Utakapolia kwa kuhitaji msaada, sanamu zako ulizojikusanyia na zikuokoe! Upepo utazipeperusha zote, pumzi peke yake itazipeperusha, Lakini mtu atakayenifanya kimbilio lake, atairithi nchi na kuumiliki mlima wangu mtakatifu.”
”“Kwa habari yangu mimi, hili ni Agano langu nao,” asema BWANA. “Roho wangu, aliyeko juu yenu na maneno yangu ambayo nimeyaweka katika vinywa vyenu hayataondoka vinywani mwenu, wala kutoka vinywani mwa watoto wenu, wala kutoka vinywani mwa wazao wao kuanzia sasa na hata milele,” asema BWANA.
”Je, mkono wangu haukufanya vitu hivi vyote, hivyo vikapata kuwepo?” asema BWANA. “Mtu huyu ndiye ninayemthamini: yeye ambaye ni mnyenyekevu na mwenye roho yenye toba, atetemekaye asikiapo neno langu.
”hivyo, mimi pia nitachagua mapigo makali kwa ajili yao, nami nitaleta juu yao kile wanachokiogopa. Kwa maana nilipoita, hakuna ye yote aliyejibu, niliposema, hakuna ye yote aliyesikiliza. Walifanya maovu machoni pangu na kuchagua lile linalonichukiza.” Sikieni neno la BWANA, ninyi mtetemekao kwa neno lake, “Ndugu zenu wanaowachukia ninyi na kuwatenga ninyi kwa sababu ya Jina langu, wamesema, ‘BWANA na atukuzwe, ili tupate kuona furaha yenu!’ Hata sasa wataaibika.
”Ee BWANA, je, macho yako hayaitafuti kweli? Uliwapiga, lakini hawakusikia maumivu, uliwapondaponda lakini walikataa marudi. Walifanya nyuso zao kuwa ngumu kuliko jiwe nao walikataa kutubu. Ndipo nikasema, “Hawa ni maskini tu; wao ni wapumbavu, kwa maana hawaijui njia ya BWANA, sheria ya Mungu wao.
”Sikia Ee nchi: Ninaleta maafa juu ya watu hawa, matunda ya mipango yao, kwa sababu hawakusikiliza maneno yangu na wameikataa sheria yangu.
”lakini niliwapa amri hii nikisema: Mtanitii mimi, nami nitakuwa Mungu wenu nanyi mtakuwa watu wangu. Enendeni katika njia zote ninazowaamuru ili mpate kufanikiwa. Lakini hawakusikiliza wala kujali, badala yake, walifuata ukaidi wa mioyo yao miovu. Wakarudi nyuma badala ya kusonga mbele.
”Wenye hekima wataaibika, watafadhaika na kunaswa. Kwa kuwa wamelikataa neno la BWANA, hiyo hekima waliyo nayo ni ya namna gani?
”Lakini kama hamtasikiliza, nitalia sirini kwa ajili ya kiburi chenu; macho yangu yatalia kwa uchungu, yakitiririka machozi, kwa sababu kundi la kondoo na mbuzi la BWANA litachukuliwa mateka.
”Maneno yako yalipokuja, niliyala; yakawa shangwe yangu na furaha ya moyo wangu, kwa kuwa nimeitwa kwa jina lako, Ee BWANA Mungu Mwenye Nguvu Zote.
”Hili ndilo asemalo BWANA: “Amelaaniwa yeye amtegemeaye mwanadamu, ategemeaye mwenye mwili kwa ajili ya nguvu zake, ambaye moyo wake umemwacha BWANA.
”Hata hivyo hawakusikiliza wala kujali, walishupaza shingo zao na hawakutaka kusikia wala kukubali marudi.
”“Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Sikilizeni! Nitaleta juu ya mji huu pamoja na vijiji vinavyouzunguka kila maafa niliyosema dhidi yake, kwa sababu wamekuwa na shingo ngumu na hawakuyasikiliza maneno yangu.’ ”
”Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote asemalo: “Msisikilize wanachowatabiria manabii, wanawajaza matumaini ya uongo. Wanasema maono kutoka katika akili zao wenyewe, hayatoki katika kinywa cha BWANA.
”“Je, neno langu si kama moto,” asema BWANA, “na kama nyundo ivunjayo mwamba vipande vipande?
”Ingawa BWANA amewatuma watumishi wake wote hao manabii kwenu mara kwa mara, hamkusikiliza wala hamkujali.
”Waambie, ‘Hili ndilo asemalo BWANA: Ikiwa hamtanisikiliza na kuifuata sheria yangu ambayo nimeiweka mbele yenu, nanyi ikiwa hamtayasikiliza maneno ya watumishi wangu manabii, ambao nimewatuma kwenu tena na tena (ijapokuwa hamkuwasikiliza), ndipo nitaifanya nyumba hii kama Shilo na mji huu kuwa kitu cha kulaaniwa na mataifa yote ya dunia.’ ”
”Sasa tengenezeni njia zenu na matendo yenu na kumtii BWANA Mungu wenu. Ndipo BWANA atawahurumia na kuacha kuleta maafa aliyokuwa ameyatamka dhidi yenu.
”Naam, hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: “Msikubali manabii na wabashiri walioko miongoni mwenu wawadanganye. Msisikilize ndoto ambazo mmewatia moyo kuota. Wanawatabiria ninyi uongo kwa Jina langu. Sikuwatuma,” asema BWANA.
”“Wakati unakuja,” asema BWANA, “nitakapofanya Agano jipya na nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda. Halitafanana na Agano nililofanya na baba zao wakati nilipowashika mkono na kuwaongoza watoke Misri, kwa sababu walivunja Agano langu, ijapokuwa nilikuwa mume kwao,” asema BWANA. “Hili ndilo Agano nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya wakati ule,” asema BWANA. “Nitaweka sheria yangu ndani yao na kuiandika katika mioyo yao. Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Mtu hatamfundisha tena jirani yake, au mtu kumfundisha ndugu yake akisema, ‘Umjue BWANA Mungu,’ kwa sababu wote watanijua mimi, kuanzia aliye mdogo kabisa kwao hata aliye mkuu sana,” asema BWANA. “Kwa sababu nitausamehe uovu wao na sitazikumbuka dhambi zao tena.”
”“Lakini mnasema, ‘Njia ya Bwana si ya haki.’ Sikia, Ee nyumba ya Israeli: Njia yangu siyo iliyo ya haki? Je, si njia zenu ndizo ambazo si za haki?
”Watawafundisha watu wangu tofauti kati ya vitu vitakatifu na vitu vya kawaida na kuwaonyesha jinsi ya kupambanua kati ya vitu najisi na vitu safi.
”watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa, “Kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeacha kuijali sheria ya Mungu wako mimi nami sitawajali watoto wako.
”Ole wao, kwa sababu wamepotoka kutoka kwangu! Maangamizi ni yao kwa sababu wameniasi! Ninatamani kuwakomboa, lakini wanasema uongo dhidi yangu.
”“Siku zinakuja,” asema BWANA Mwenyezi, “wakati nitakapotuma njaa katika nchi yote: si njaa ya chakula wala kiu ya maji, lakini njaa ya kusikia maneno ya BWANA.
”“Lakini wakakataa kusikiliza, wakanipa kisogo kwa ukaidi na kuziba masikio yao. Wakaifanya mioyo yao migumu kama jiwe gumu na hawakuisikiliza sheria au maneno ambayo BWANA Mwenye Nguvu Zote aliyatuma kwa njia ya Roho wake kupitia manabii waliotangulia. Kwa hiyo BWANA Mwenye Nguvu Zote alikasirika sana. “ ‘Wakati nilipoita, hawakusikiliza, kwa hiyo walipoita, sikusikiliza,’ asema BWANA Mwenye Nguvu Zote.
”Lakini Yesu akajibu, “Imeandikwa, ‘Mtu haishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.’ ”
”“Msidhani kwamba nimekuja kufuta Torati au Manabii, sikuja kuondoa bali kutimiza. Kwa maana, amin nawaambia, mpaka mbingu na dunia zitakapopita, hakuna hata herufi moja ndogo wala nukta itakayopotea kwa namna yo yote kutoka kwenye Torati mpaka kila kitu kiwe kimetimia. Kwa hiyo, ye yote atakayevunja mojawapo ya amri ndogo kuliko zote ya amri hizi, naye akawafundisha wengine kufanya hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika Ufalme wa Mbinguni, lakini ye yote azitendaye na kuzifundisha hizi amri ataitwa mkuu katika Ufalme wa Mbinguni.
”“Hakuna mtu ye yote awezaye kuwatumikia mabwana wawili, kwa kuwa ama atamchukia huyu na kumpenda yule mwingine, au atashikamana sana na huyu na kumdharau huyu mwingine. Ninyi hamwezi kumtumikia Mungu na Mali.
”“Ingieni kwa kupitia mlango mwembamba, kwa maana lango ni pana na njia ni pana ielekeayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa kupitia lango hilo. Lakini mlango ni mwembamba na njia ni finyu ielekeayo kwenye uzima, nao ni wachache tu waionao.
”“Si kila mtu aniambiaye, ‘Bwana, Bwana,’ atakayeingia katika Ufalme wa Mbinguni bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, ‘Bwana, Bwana, hatukutoa unabii kwa jina lako na kwa jina lako kutoa pepo wachafu na kufanya miujiza mingi?’ Ndipo nitakapowaambia wazi, ‘Sikuwajua kamwe. Ondokeni kwangu, ninyi watenda maovu!’
”“Kwa hiyo kila mtu ayasikiaye haya maneno yangu na kuyatenda, ni kama mtu mwenye busara aliyejenga nyumba yake kwenye mwamba. Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja na upepo ukavuma ukaipiga hiyo nyumba, lakini haikuanguka kwa sababu msingi wake ulikuwa kwenye mwamba. Naye kila anayesikia haya maneno yangu wala asiyatende, ni kama mtu mjinga aliyejenga nyumba yake kwenye mchanga. Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, nao upepo ukavuma ukaipiga hiyo nyumba, nayo ikaanguka kwa kishindo kikubwa.”
”Kama mtu ye yote hatawakaribisha ninyi, wala kusikiliza maneno yenu, kung'uteni mavumbi kutoka kwenye miguu yenu mtakapokuwa mnatoka kwenye nyumba hiyo au mji huo. Amin, amin nawaambia, miji ya Sodoma na Gomora itastahimili zaidi katika hukumu kuliko mji huo.
”“Kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, mimi nami nitamkiri yeye mbele za Baba yangu aliye mbinguni. Lakini ye yote atakayenikana mimi mbele ya watu, mimi nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni.”
”“Ye yote ampendaye baba yake au mama yake kuliko anavyonipenda mimi, hastahili kuwa wangu. Ye yote ampendaye mwanawe au binti yake kuliko anavyonipenda Mimi, hastahili kuwa wangu. Tena ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kunifuata, hastahili kuwa wangu. Ayang'ang'aniaye maisha yake atayapoteza, lakini yeye atakayeyatoa maisha yake kwa ajili yangu atayapata. “Mtu ye yote atakayewapokea ninyi atakuwa amenipokea mimi na ye yote atakayenipokea mimi atakuwa amempokea yeye aliyenituma.
”Akawajibu, “Ninyi mmepewa kuzifahamu siri za Ufalme wa Mbinguni, lakini wao sivyo.
”Hii ndiyo sababu nasema nao kwa mifano: “Ingawa wanatazama, hawaoni, wanasikiliza, lakini hawasikii wala hawaelewi. Kwao unatimia ule unabii wa Isaya aliposema: “ ‘Hakika mtasikiliza lakini hamtaelewa, na pia mtatazama lakini hamtaona. Kwa maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, hawasikii kwa masikio yao, na wamefumba macho yao. Wasije wakaona kwa macho yao, wakasikia kwa masikio yao, wakaelewa kwa mioyo yao, wakageuka, nami nikawaponya.’ Lakini heri macho yenu, kwa sababu yanaona na heri masikio yenu kwa sababu yanasikia. Amin, nawaambia, manabii wengi na wenye haki walitamani kuona yale mnayoyaona, nao hawakuyaona na kusikia yale mnayosikia lakini hawakuyasikia. “Sikilizeni basi maana ya ule mfano wa mpanzi: Mtu ye yote anaposikia neno la Ufalme, naye asilielewe, yule mwovu huja na kunyakua kile kilichopandwa moyoni mwake, hii ndiyo ile mbegu iliyopandwa kando ya njia. Ile mbegu iliyopandwa kwenye sehemu yenye mawe ni mtu yule ambaye hulisikia neno na mara hulipokea kwa furaha. Lakini kwa kuwa hana mizizi yenye kina ndani yake, lile neno hukaa kwa muda mfupi. Inapotokea dhiki au mateso kwa ajili ya hilo neno, yeye mara huchukizwa. Ile mbegu iliyopandwa katika miiba ni yule mtu alisikiaye neno, lakini masumbufu ya dunia na ushawishi wa mali hulisonga lile neno na kulifanya lisizae matunda. Lakini ile mbegu iliyopandwa kwenye udongo mzuri ni yule mtu ambaye hulisikia neno na kulielewa. Naye hakika hutoa matunda, akizaa mara mia, au mara sitini, au mara thelathini ya mbegu iliyopandwa.”
”Akawajibu, “Kila pando ambalo Baba yangu wa mbinguni hakulipanda, litang'olewa.
”Yesu akawajibu, “Mwapotoka kwa sababu hamjui maandiko wala uweza wa Mungu.
”Yesu akamjibu, “ ‘Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote.’ Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. Nayo ya pili ni kama hiyo, nayo ni hii: ‘Mpende jirani yako kama nafsi yako.’ Amri hizi mbili ndizo msingi wa Torati na manabii.”
”Injili ya Ufalme itahubiriwa ulimwenguni pote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote. Ndipo ule mwisho utakapokuja.
”Mbingu na dunia zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
”Yesu akawajia na kusema, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
”Baada ya Yohana kukamatwa na kutiwa gerezani, Yesu aliingia Galilaya akaanza kuhubiri habari njema ya Mungu, akisema, “Wakati umewadia, Ufalme wa Mungu umekaribia. Tubuni na kuiamini Habari Njema.”
”Naye akawaambia, “Ninyi mmepewa kujua siri ya Ufalme wa Mungu, lakini kwa wale walioko nje, kila kitu husemwa kwao kwa mifano ili, “ ‘daima waone lakini wasitambue, daima wasikie lakini wasielewe; wasije wakageuka, wakatubu na kusamehewa!’ ” Kisha Yesu akawauliza, “Hamwelewi maana ya mfano huu? Basi mtaelewaje mifano mingine? Yule mpanzi hupanda neno. Hawa ndio wale walio kando ya njia, ambako neno lilipandwa. Walisikiapo neno, Shetani huja mara na kulichukua lile neno lililopandwa ndani yao. Nazo hizi ni zile mbegu zilizoanguka kwenye udongo wenye miamba, wanapolisikia neno, mara hulipokea kwa furaha. Basi kwa kuwa hawana mizizi, hudumu kwa muda mfupi tu, kisha dhiki au mateso yanapoinuka kwa ajili ya lile neno, wao mara huiacha imani. Lakini wengine, kama mbegu iliyopandwa kwenye miiba, hulisikia lile neno, lakini masumbufu ya maisha haya, udanganyifu wa mali na tamaa ya mambo mengine huja na kulisonga lile neno na kulifanya lisizae. Wengine, kama mbegu iliyopandwa kwenye udongo mzuri, hulisikia lile neno, wakalipokea na kutoa mazao: Wengine thelathini, wengine sitini na wengine mara mia moja ya ile iliyopandwa.”
”Kwa kusikia hayo waliyosema, Yesu akamwambia huyo kiongozi wa sinagogi, “Usiogope. Amini tu.”
”Kwa njia hiyo ninyi mnabatilisha neno la Mungu kwa taratibu zenu mlizojiwekea. Nanyi mnafanya mambo mengi ya jinsi hiyo.”
”Ndipo akauita ule umati wa watu pamoja na wanafunzi wake, akasema, “Mtu ye yote akitaka kunifuata, ni lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake, anifuate. Kwa maana mtu ye yote anayetaka kuiokoa nafsi ataipoteza, lakini yeye ayapotezaye maisha yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili atayaokoa. Mtu atafaidiwa nini kama akiupata ulimwengu wote lakini akaipoteza nafsi yake? Au mtu atatoa nini apate tena maisha yake? Mtu ye yote anayenionea aibu mimi na maneno yangu katika kizazi hiki cha uzinzi na cha dhambi, Mwana wa Adamu, atamwonea aibu wakati atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu.”
”Yesu akawajibu, “Je, hampotoki kwa sababu hamjui maandiko wala uweza wa Mungu?
”Nayo habari njema lazima ihubiriwe kwanza kwa mataifa yote kabla ule mwisho haujawadia.
”Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
”Akawaambia, “Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Ye yote aaminiye na kubatizwa ataokoka. Lakini ye yote asiyeamini atahukumiwa.
”Kisha wanafunzi wake wakatoka, wakahubiri kila mahali, naye Bwana akatenda kazi pamoja nao na kulithibitisha neno lake kwa ishara zilizofuatana nalo.
”ili mawazo ya mioyo mingi yadhihirike na upanga utauchoma moyo wako.”
”Yesu akajibu akamwambia, “Imeandikwa: ‘Mtu haishi kwa mkate tu, bali kwa kila neno la Mungu.’ ”
”Wakashangazwa sana na mafundisho yake, maana maneno yake yalikuwa na mamlaka.
”“Kwa nini mnaniita, ‘Bwana, Bwana,’ nanyi hamfanyi ninayowaambia? Nitawaonyesha jinsi alivyo mtu yule anayekuja kwangu na kusikia maneno yangu na kuyatenda. Yeye ni kama mtu anayejenga nyumba, akachimba chini sana na kuweka msingi kwenye mwamba. Mafuriko yalipokuja, maji ya ghafula yakaipiga ile nyumba lakini haikutikisika, kwa sababu ilikuwa imejengwa vizuri juu ya mwamba. Lakini yeye ayasikiaye maneno yangu na asiyatende ni kama mtu aliyejenga nyumba juu ya mchanga bila kuweka msingi. Mafuriko yalipoikumba nyumba ile, ikaanguka mara na kubomoka kabisa.”
”Naye akasema, “Ninyi mmejaliwa kufahamu siri za Ufalme wa Mungu, lakini kwa wengine nazungumza kwa mifano, ili, “ ‘ingawa wanaona, wasione; ingawa wanasikia, wasielewe.’ “Maana ya mfano huu ni hii: Mbegu ni neno la Mungu. Zile zilizoanguka kando ya njia, ni wale ambao husikia neno na ibilisi huja na kuliondoa kutoka mioyoni mwao, ili wasije wakaamini na kuokoka. Zile za kwenye mwamba ni wale ambao hulipokea neno kwa furaha wanapolisikia, lakini hawana mizizi. Wanaamini kwa kitambo kidogo, lakini wakati wa kujaribiwa huiacha imani. Zile mbegu zilizoanguka kwenye miiba ni mfano wa wale wanaosikia, lakini wanapoendelea husongwa na masumbufu ya maisha haya, utajiri na anasa, nao hawakui. Lakini zile mbegu kwenye udongo mzuri ni mfano wa wale ambao hulisikia neno la Mungu na kulishika kwa moyo mnyofu na wa utii, nao kwa kuvumilia kwingi huzaa matunda.
”Yesu akamjibu, “Mama yangu na ndugu zangu ni wale wote wanaolisikia neno la Mungu na kulitii.”
”Kisha akawaambia wote, “Ye yote anayetaka kunifuata ni lazima ajikane mwenyewe, achukue msalaba wake kila siku na anifuate. Kwa maana ye yote atakayekuyaponya maisha yake atayapoteza, lakini ye yote atakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu atayaokoa. Je, itamfaidia nini mtu kuupata ulimwengu wote, lakini akayapoteza maisha yake? Kama mtu ye yote akinionea aibu mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu atamwonea aibu mtu huyo atakapokuja katika utukufu wake na katika utukufu wa Baba na wa malaika watakatifu.
”Yesu akamwambia mtu mwingine, “Nifuate.” Mtu huyo akamjibu, “Bwana, niache kwanza nikamzike baba yangu.” Yesu akamwambia, “Waache wafu wawazike wafu wao, bali wewe nenda ukautangaze Ufalme wa Mungu.” Mtu mwingine akamwambia, “Bwana, nitakufuata lakini naomba kwanza nikaage jamaa yangu.” Yesu akamwambia, “Mtu ye yote atiaye mkono wake kulima, kisha akatazama nyuma, hafai kwa Ufalme wa Mungu.”
”Yesu akajibu, “Wamebarikiwa zaidi wale wanaolisikia neno la Mungu na kulitii.”
”Mtu mmoja akamwuliza, “Bwana, ni watu wachache tu watakaookolewa?” Yesu akawaambia, “Jitahidini kuingia kwa kupitia mlango mwembamba, kwa maana, nawaambia, wengi watajaribu kuingia lakini hawataweza.
”“Mtu ye yote anayekuja kwangu hawezi kuwa mwanafunzi wangu kama hatanipenda mimi zaidi ya baba yake na mama yake, mke wake na watoto, ndugu zake na dada zake, naam, hata maisha yake mwenyewe. Ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kunifuata hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
”“Torati na manabii vilitumiwa mpaka kuja kwa Yohana Mbatizaji. Tangu wakati huo habari njema za Ufalme wa Mungu zinahubiriwa na kila mmoja hujiingiza kwa nguvu. Lakini ni rahisi zaidi mbingu na nchi kupita kuliko hata herufi moja kuondoka katika Sheria.
”“Abrahamu akamjibu, ‘Ndugu zako wana Mose na Manabii, wawasikilize hao.’ “Yule tajiri akasema, ‘Hapana, baba Abrahamu, lakini mtu kutoka kwa wafu akiwaendea, watatubu.’ “Abrahamu akamwambia, ‘Kama wasipowasikiliza Mose na manabii, hawataweza kushawishiwa hata kama atafufuka mtu kutoka kwa wafu.’ ”
”Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.”
”Yesu akawaambia, “Ninyi ni wajinga kiasi gani, nanyi ni wazito mioyoni mwenu kuamini mambo yote yaliyonenwa na manabii!
”Naye akianzia na Mose na manabii wote, akawafafanulia jinsi maandiko yalivyosema kumhusu yeye.
”Akawaambia, “Haya ndiyo yale niliyowaambia nilipokuwa bado niko pamoja nanyi, kwamba yote yaliyoandikwa kunihusu mimi katika Torati ya Mose, Manabii na Zaburi hayana budi kutimizwa.” Ndipo akafungua fahamu zao ili waweze kuyaelewa Maandiko.
”Hapo mwanzo alikuwako Neno, huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
”Kwa kuwa sheria ilitolewa kwa mkono wa Mose, lakini neema na kweli imekuja kupitia Yesu Kristo.
”Baada ya kufufuka kutoka kwa wafu, wanafunzi wake wakakumbuka yale aliyokuwa amesema. Ndipo wakayaamini Maandiko na yale maneno Yesu aliyokuwa amesema.
”Nimewaambia mambo ya duniani, nanyi hamkuniamini, mtaniaminije basi nitakapowaambia mambo ya mbinguni?
”“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Kwa maana Mungu hakumtuma Mwanawe kuuhukumu ulimwengu, bali kwa yeye ulimwengu upate kuokolewa. Ye yote amwaminiye hahukumiwi, lakini asiyeamini amekwisha kuhukumiwa, kwa sababu hakumwamini Mwana pekee wa Mungu.
”Yeye aliyetumwa na Mungu husema maneno ya Mungu, kwa kuwa Mungu humtoa Roho pasipo kipimo.
”Ye yote anayemwamini Mwana ana uzima wa milele, lakini yeye asiyemwamini Mwana hatauona uzima, bali ghadhabu ya Mungu itakuwa juu yake.”
”Mungu ni Roho na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.”
”“Amin, amin ninawaambia, ye yote anayesikia maneno yangu na kumwamini yeye aliyenituma, anao uzima wa milele, naye hatahukumiwa, bali amepita kutoka mautini, na kuingia uzimani. Amin, amin nawaambia, saa yaja, nayo saa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, nao watakaoisikia watakuwa hai.
”wala hamna neno lake ndani yenu, kwa sababu hamkumwamini yeye aliyetumwa naye. Ninyi mnachunguza Maandiko mkidhani ya kuwa ndani yake mna uzima wa milele, maandiko haya ndiyo yanayonishuhudia Mimi.
”Roho ndiye atiaye uzima, mwili haufai kitu. Maneno haya niliyowaambia ni Roho tena ni uzima.
”Niliwaambia kuwa mtakufa katika dhambi zenu, kwa maana msipoamini ya kwamba ‘Mimi Ndiye,’ mtakufa katika dhambi zenu.”
”Kisha Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, “Kama mkidumu katika maneno yangu, mtakuwa wanafunzi wangu kweli kweli. Ndipo mtaijua kweli nayo kweli itawaweka huru.”
”Kwa nini hamwelewi ninayowaambia? Ni kwa sababu hamwezi kusikia nisemacho. Ninyi ni watoto wa baba yenu ibilisi, nanyi mnataka kutimiza matakwa ya baba yenu. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo, wala hakushikana na kweli maana hamna kweli ndani yake. Asemapo uongo husema yaliyo yake mwenyewe kwa maana yeye ni mwongo na baba wa huo uongo. Lakini kwa sababu nimewaambia kweli hamkuniamini! Je, kuna ye yote miongoni mwenu awezaye kunithibitisha kuwa mwenye dhambi? Kama nawaambia yaliyo kweli, mbona hamniamini? Yeye atokaye kwa Mungu husikia kile Mungu asemacho. Sababu ya ninyi kutosikia ni kwa kuwa hamtokani na Mungu.”
”Amin, amin nawaambia, mtu ye yote akilitii neno langu hataona mauti milele.”
”Lakini hamwamini, kwa sababu ninyi si wa kundi la kondoo wangu. Kondoo wangu huisikia sauti yangu nami nawajua, nao hunifuata,
”Kama aliwaita ‘miungu,’ wale ambao neno la Mungu liliwafikia, nayo Maandiko hayawezi kutanguka.
”Mtu ye yote anayependa maisha yake atayapoteza, naye ayachukiaye maisha yake katika ulimwengu huu atayaokoa hata uzima wa milele. Mtu ye yote akinitumikia lazima anifuate, nami mahali nilipo ndipo mtumishi wangu atakapokuwa. Mtu akinitumikia, Baba yangu atamheshimu.
”Hata baada ya Yesu kufanya miujiza hii yote mbele yao, bado hawakumwamini. Hii ilikuwa ili kutimiza lile neno la nabii Isaya lililosema: “Bwana, ni nani aliyesadiki ujumbe wetu na mkono wa Bwana amefunuliwa nani?” Kwa hivyo hawakuamini, kwa sababu Isaya anasema mahali pengine: “Amewafanya vipofu na kuifanya mioyo yao kuwa migumu, ili wasiweze kuona kwa macho yao, wala kuelewa kwa mioyo yao, wasije wakageuka, nami nikawaponya.” Isaya alisema haya alipoona utukufu wa Yesu na kunena habari zake. Lakini wengi miongoni mwa viongozi wa Wayahudi walimwamini, lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakukiri waziwazi kwa maana waliogopa kufukuzwa katika masinagogi. Wao walipenda sifa za wanadamu kuliko sifa zitokazo kwa Mungu.
”Yuko amhukumuye yeye anikataaye mimi na kutokuyapokea maneno yangu, yaani, yale maneno niliyosema yenyewe yatamhukumu siku ya mwisho.
”Kwa maana sisemi kwa ajili yangu mwenyewe, bali Baba aliyenituma aliniamuru ni nini cha kusema na jinsi ya kukisema. Nami ninajua amri zake huongoza hadi kwenye uzima wa milele. Hivyo lo lote nisemalo, ndilo lile Baba aliloniambia niseme.”
”Yesu akawaambia, “Mimi ndimi njia na kweli na uzima. Mtu hawezi kuja kwa Baba isipokuwa kwa kupitia kwangu.
”“Kama mnanipenda, mtazishika amri zangu.
”Ye yote mwenye amri zangu na kuzishika ndiye anipendaye, naye anipendaye atapendwa na Baba yangu, nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.”
”Yesu akamjibu, “Mtu ye yote akinipenda atalishika neno langu na Baba yangu atampenda, nasi tutakuja kwake na kufanya makao yetu kwake. Mtu ye yote asiyenipenda hayashiki maneno yangu na maneno niliyowapa si yangu bali ni ya Baba aliyenituma.
”Ninyi mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni lo lote mtakalo, nanyi mtatendewa.
”Atakapokuja huyo Roho wa kweli atawaongoza awatie katika kweli yote. Yeye hatanena kwa ajili yake mwenyewe, bali atanena yale yote atakayosikia, naye atawaonyesha mambo yajayo.
”Nimewapa neno lako, nao ulimwengu umewachukia kwa kuwa wao si wa ulimwengu kama mimi nisivyo wa ulimwengu huu.
”Uwatakase kwa ile kweli, neno lako ndilo kweli.
”Pilato akamwuliza, “Kwa hiyo wewe ni mfalme?” Yesu akajibu, “Wewe wasema kwamba mimi ni mfalme. Kwa kusudi hili nilizaliwa na kwa ajili ya hili nilikuja ulimwenguni ili niishuhudie kweli. Mtu ye yote aliye wa kweli husikia sauti yangu.”
”Petro na wale mitume wengine wakajibu, “Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu.
”Ndipo Paulo na Barnaba wakawajibu kwa ujasiri, wakisema, “Ilitupasa kunena nanyi neno la Mungu kwanza. Lakini kwa kuwa mmelikataa, mkajihukumu wenyewe kuwa hamstahili uzima wa milele, sasa tunawageukia watu Mataifa.
”Hawa Wayahudi wa Beroya walikuwa waungwana zaidi kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa waliupokea ule ujumbe kwa shauku kubwa na kuyachunguza Maandiko kila siku ili kuona kama yale Paulo aliyosema yalikuwa kweli.
”Lakini baadhi yao kwa ukaidi walipokataa kuamini na kukashifu ujumbe wake mbele ya umati wa watu, Paulo aliachana nao, akawachukua wanafunzi na kuhojiana nao kila siku katika darasa la mtu mmoja aitwaye Tirano.
”Najua kwamba baada mimi kuondoka, mbwa mwitu wakali watakuja katikati yenu ambao hawatalihurumia kundi. Hata kutoka miongoni mwenu wenyewe watainuka watu na kuupotosha ukweli ili wawavute wanafunzi wawafuate. Hivyo jilindeni! Kumbukeni kwamba kwa miaka mitatu sikuacha kamwe kuwaonya, kila mmoja kwa machozi usiku na mchana.
”“ ‘Nenda kwa watu hawa na useme, “Kweli mtasikiliza lakini kamwe hamtaelewa; kweli mtatazama, lakini hamtaona.” Kwa kuwa mioyo ya watu hawa imekuwa migumu, na masikio yao ni mazito kusikia, nao wamefumba macho yao. Wasije wakaona kwa macho yao, na kusikiliza kwa masikio yao, wakaelewa kwa mioyo yao na kugeuka, nami nikawaponya.’
”Paulo, mtumishi wa Kristo Yesu, aliyeitwa kuwa mtume na kutengwa kwa ajili ya Injili ya Mungu, Injili ambayo Mungu alitangulia kuiahidi kwa vinywa vya manabii wake katika maandiko matakatifu,
”Mimi siionei haya Injili ya Kristo kwa maana ni uweza wa Mungu uletao wokovu kwa kila aaminiye, kwanza kwa Myahudi na kwa Myunani pia. Kwa maana katika Injili haki itokayo kwa Mungu imedhihirishwa, haki ile iliyo kwa njia ya imani hadi imani. Kama ilivyoandikwa: “Mwenye haki ataishi kwa imani.” Ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni dhidi ya uasi wote na uovu wa wanadamu ambao huipinga kweli kwa uovu wao, kwa maana yote yanayoweza kujulikana kumhusu Mungu ni dhahiri kwao, kwa sababu Mungu mwenyewe ameliweka wazi kwao. Kwa maana tangu kuumbwa kwa ulimwengu, asili ya Mungu asiyeonekana kwa macho, yaani, uweza wake wa milele na asili yake ya Uungu, umeonekana waziwazi ukitambuliwa kutokana na yale aliyoyafanya ili wanadamu wasiwe na udhuru. Kwa maana ingawa walimjua Mungu, hawakumtukuza yeye kama ndiye Mungu wala hawakumshukuru, bali fikira zao zimekuwa batili na mioyo yao ya ujinga ikatiwa giza. Ingawa wakijidai kuwa wenye hekima, wakawa wajinga
”Basi kuna faida gani kuwa Myahudi? Au kuna thamani gani katika tohara? Kuna faida kubwa kwa kila namna, kwanza kabisa, Wayahudi wamekabidhiwa lile Neno halisi la Mungu. Ingekuwaje kama wengine hawakuwa na imani? Je, kutokuamini kwao kungebatilisha uaminifu wa Mungu? La hasha! Mungu na aonekane mwenye haki na kila mwanadamu kuwa mwongo, kama ilivyoandikwa: “Ili uweze kujulikana kuwa na haki katika maneno yako, nawe ukashinde katika hukumu.”
”Kama ilivyoandikwa: “Hakuna mwenye haki, hakuna hata mmoja. Hakuna hata mmoja mwenye ufahamu, hakuna hata mmoja amtafutaye Mungu.
”Je, basi ni kwamba tunaibatilisha sheria kwa imani hii? La, hasha! Badala yake tunaithibitisha sheria.
”Lakini sasa, kwa kufia kile kilichokuwa kimetufunga kwanza, tumewekwa huru kutoka katika sheria ili tutumike katika njia mpya ya Roho, wala si katika njia ya zamani ya sheria iliyoandikwa.
”Hivyo basi, sheria yenyewe ni takatifu na amri ni takatifu na ya haki, tena ni njema.
”Ashukuriwe Mungu kwa njia ya Yesu Kristo Bwana wetu! Hivyo basi, mimi mwenyewe kwa akili zangu ni mtumwa wa sheria ya Mungu, lakini katika asili ya dhambi ni mtumwa wa sheria ya dhambi.
”Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui na Mungu, kwa maana haiitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii.
”Nao watahubirije wasipopelekwa? Kama ilivyaoandikwa, “Ni mizuri mno miguu ya hao wanaohubiri Injili ya amani na kuleta habari ya mema!” Lakini si wote waliotii Habari Njema. Kwa maana Isaya asema, “Bwana, ni nani aliyeamini ujumbe wetu?” Basi, imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la Kristo.
”kama ilivyoandikwa: “Mungu aliwapa bumbuazi la mioyo, macho ili wasiweze kuona na masikio ili wasiweze kusikia, hadi leo.”
”Kwa maana kila kitu kilichoandikwa zamani, kiliandikwa kutufundisha, ili kwamba kwa saburi na faraja tunayopata katika Maandiko tuwe na tumaini.
”Ndugu zangu, nawasihi mjihadhari na kujiepusha na wale watu waletao matengano na kuweka vikwazo mbele yenu dhidi ya mafundisho mliyojifunza. Kwa maana watu kama hao hawamtumikii Bwana Kristo, bali wanatumikia tamaa zao wenyewe. Kwa kutumia maneno laini na ya kubembeleza, hupotosha mioyo ya watu wajinga.
”Kwa maana ujumbe wa msalaba kwa wale wanaopotea ni upuzi, lakini kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.
”Lakini miongoni mwa watu waliokomaa twanena hekima, wala si hekima ya ulimwengu huu au ya watawala wa dunia hii wanaobatilika. Sisi tunanena hekima ya Mungu ambayo ni siri, tena iliyofichika kwa wanadamu, ambayo Mungu aliikusudia kabla ya ulimwengu kuwepo, kwa ajili ya utukufu wetu.
”Haya ndiyo tusemayo, si kwa maneno tuliyofundishwa kwa hekima ya wanadamu bali kwa maneno tuliyofundishwa na Roho, tukifafanua kweli za kiroho kwa wale watu wa kiroho. Mtu ambaye hana Roho wa Mungu hawezi kupokea mambo yatokayo kwa Roho wa Mungu, kwa kuwa ni upuzi kwake, naye hawezi kuyaelewa kwa sababu hayo yanaeleweka tu kwa jinsi ya rohoni. Mtu wa kiroho hutambua mambo yote, lakini yeye mwenyewe hatambuliwi na mtu ye yote.
”Kutahiriwa au kutokutahiriwa si kitu. Lakini kuzitii amri za Mungu ndilo jambo muhimu.
”Basi ndugu zangu nataka niwakumbushe kuhusu Injili niliyowahubiria, mkaipokea na ambayo katika hiyo mmesimama. Kwa Injili hii mnaokolewa mkishikilia kwa uthabiti neno nililowahubiria ninyi. La sivyo, mmeamini katika ubatili.
”Kama mtu ye yote hampendi Bwana Yesu Kristo, na alaaniwe. Bwana wetu, njoo!
”Kwa maana sisi kwa Mungu ni harufu nzuri ya manukato ya Kristo miongoni mwa wale wanaookolewa na kwa wale wanaopotea, sisi kwa wale wanaopotea ni harufu ya mauti iletayo mauti, lakini kwa wale wanaookolewa sisi ni harufu nzuri iletayo uzima. Ni nani awezaye mambo hayo?
”Yeye ndiye aliyetuwezesha sisi kuwa wahudumu wa Agano Jipya: si wa andiko, bali wa Roho; kwa kuwa andiko huua bali Roho hutia uzima. Basi ikiwa ile huduma iliyoleta mauti, ile iliyoandikwa kwa herufi juu ya jiwe ilikuja kwa utukufu hata Waisraeli wakawa hawawezi kuutazama uso wa Mose kwa sababu ya ule utukufu wake, ingawa ulikuwa ni wa kufifia, je, huduma ya Roho haitakuwa na utukufu zaidi? Ikiwa huduma ile iwahukumuyo wanadamu ina utukufu, je, haitakuwa ya utukufu zaidi ile huduma iletayo haki?
”Tumekataa mambo ya siri na ya aibu, wala hatufuati njia za udanganyifu, tukichanganya Neno la Mungu na uongo. Kinyume cha hayo, tunadhihirisha kweli waziwazi na kujitambulisha wenyewe kwenye dhamiri ya kila mtu mbele za Mungu. Hata nayo Injili yetu kama imetiwa utaji, ni kwa wale tu wanaopotea. Kwa habari yao, mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, ili wasione nuru ya Injili ya utukufu wa Kristo, aliye sura ya Mungu.
”Lakini nina hofu kuwa, kama vile Eva alivyodanganywa kwa ujanja wa yule nyoka, mawazo yenu yasije yakapotoshwa, mkauacha unyofu na usafi wa upendo wenu kwa Kristo.
”Watu kama hao ni mitume wa uongo, ni wafanyakazi wadanganyifu, wanaojigeuza waonekane kama mitume wa Kristo. Wala hii si ajabu, kwa kuwa hata Shetani mwenyewe hujigeuza aonekane kama malaika wa nuru.
”Kwa maana hatuwezi kufanya lo lote kinyume na kweli, bali kuithibitisha kweli tu.
”Nashangaa kwamba mnamwacha upesi hivyo yeye aliyewaita kwa neema ya Kristo na kuifuata injili nyingine, ambayo kwa kweli si injili kamwe, ila kwa dhahiri kuna watu wanaowachanganya na wanaotaka kuipotosha Injili ya Kristo. Lakini hata ikiwa sisi au malaika atokaye mbinguni akihubiri injili nyingine tofauti na ile tuliyowahubiria sisi, basi mtu huyo alaaniwe milele! Kama vile tulivyokwisha kusema kabla, sasa nasema tena, ikiwa mtu ye yote atawahubiria injili kinyume na ile mliyoipokea na alaaniwe milele!
”hatukukubaliana nao hata dakika moja, ili kwamba ukweli wa Injili ubaki nanyi.
”Kwa maana wote wanaotumainia matendo ya sheria, wako chini ya laana, kwa kuwa imeandikwa, “Amelaaniwa mtu yule asiyeshika na kutii mambo yote yaliyoandikwa katika Kitabu cha Sheria.”
”Kristo alitukomboa kutoka katika laana ya sheria kwa kufanyika laana kwa ajili yetu, kwa maana imeandikwa, “Amelaaniwa yeye aangikwaye juu ya mti.” Alitukomboa ili kwamba baraka aliyopewa Abrahamu ipate kuwafikia watu Mataifa kwa njia ya Kristo Yesu, ili kwa imani tupate kupokea ile ahadi ya Roho.
”Ahadi zilinenwa kwa Abrahamu na kwa mzao wake. Maandiko hayasemi “kwa wazao,” likimaanisha watu wengi, bali “kwa mzao wako,” yaani mtu mmoja, ndiye Kristo.
”Hivyo, sheria ilikuwa kiongozi kutufikisha kwa Kristo, ili tupate kuhesabiwa haki kwa imani.
”Je, sasa nimekuwa adui yenu kwa kuwaambia kweli?
”Nazidi kumwomba Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awajalieni ninyi roho ya hekima na ya ufunuo, ili mpate kumjua zaidi. Ninaomba pia kwamba macho ya mioyo yenu yatiwe nuru ili mpate kujua tumaini mliloitiwa, utajiri wa urithi wa utukufu wake kwa watakatifu
”Ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwatupwa huku na huku na kuchukuliwa na kila upepo wa mafundisho kwa hila za watu, kwa ujanja, kwa kufuata njia zao za udanganyifu.
”kusudi alifanye takatifu, akilitakasa kwa kuliosha kwa maji katika Neno lake,
”Vaeni chapeo ya wokovu na mchukue upanga wa Roho, ambao ni Neno la Mungu.
”Haya ndiyo maombi yangu kwamba upendo wenu uongezeke zaidi na zaidi katika maarifa na ufahamu wote, ili mpate kutambua yale yaliyo mema, mkawe safi, wasio na hatia hadi siku ya Kristo,
”Mkilishika neno la uzima, ili nipate kuona fahari siku ya Kristo kwamba sikupiga mbio wala kujitaabisha bure.
”mradi tu kwamba mnaendelea kuwa waaminifu, mkiwa mmefanywa imara na thabiti katika imani, pasipo kuliacha tumaini lililoahidiwa na Injili. Hii ndiyo ile Injili mliyoisikia ambayo imehubiriwa kwa kila kiumbe chini ya mbingu na ambayo mimi Paulo, nimekuwa mtumwa wake.
”Angalieni mtu ye yote asiwafanye ninyi mateka kwa elimu batili na madanganyo matupu yanayotegemea mapokeo ya wanadamu na mafundisho ya ulimwengu ambayo siyo ya Kristo.
”Pia tuombeeni na sisi ili Mungu atufungulie mlango wa kunena, ili tupate kuitangaza siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake pia mimi nimefungwa.
”Nanyi mkawa wafuasi wetu na wa Bwana, ingawa mlipata mateso mengi, mlilipokea lile Neno kwa furaha katika Roho Mtakatifu.
”kama vile mjuavyo, tulikuwa tumeteswa na kutukanwa huko Filipi, lakini hata hivyo, kwa msaada wa Mungu wetu, tulikuwa na ujasiri wa kuwaambia Injili ya Mungu ingawa kulikuwa na upinzani mkubwa.
”Nasi pia tunamshukuru Mungu bila kukoma kwa sababu mlipolipokea neno la Mungu mlilosikia kutoka kwetu, hamkulipokea kama neno la wanadamu, bali mlilipokea kama lilivyo hasa, neno la Mungu, litendalo kazi ndani yenu ninyi mnaoamini.
”na kuwapa ninyi mnaoteseka raha pamoja na sisi, wakati Bwana Yesu atakapodhihirishwa kutoka mbinguni katika mwali wa moto pamoja na malaika wake wenye nguvu. Atawaadhibu wale wasiomjua Mungu na ambao hawakuitii Injili ya Bwana wetu Yesu. Wataadhibiwa kwa uangamivu wa milele na kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa uweza wake,
”Hapo ndipo yule mwasi atafunuliwa, ambaye Bwana Yesu atamteketeza kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kabisa kwa utukufu wa kuja kwake. Kuja kwa yule mwasi kutaonekana kana kwamba ni kutenda kazi kwake Shetani ambaye hutumia nguvu zote, ishara, maajabu ya uongo na kila aina ya udanganyifu kwa wale wanaoangamia kwa sababu walikataa kuipenda kweli wapate kuokolewa. Kwa sababu hii, Mungu ameruhusu watawaliwe na nguvu ya udanganyifu, ili waendelee kuamini uongo na hivyo wote wahukumiwe ambao hawakuamini ule ukweli bali wamefurahia uovu.
”Tunajua kwamba sheria ni njema ikiwa inatumika kwa halali kama ilivyokusudiwa. Lakini tunajua ya kuwa sheria si kwa ajili ya wenye haki, bali kwa ajili ya wavunja sheria na waasi, kwa ajili ya wasiomcha Mungu na wenye dhambi, wasio watakatifu na wanaokufuru, kwa wale wawauao baba zao au mama zao, kwa wauaji, kwa wazinzi na wahanithi, wauza watu na kwa waongo na waapao kwa uongo, na kwa cho chote kingine kilicho kinyume na mafundisho ya kweli, ambayo yanakubaliana na Injili ya utukufu wa Mungu anayehimidiwa, ambayo mimi Paulo nimewekea amana.
”Jambo hili ni jema tena linapendeza machoni pa Mungu Mwokozi wetu anayetaka watu wote waokolewe na wafikie kuijua kweli.
”kama nikikawia, utajua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, ambayo ndiyo kanisa la Mungu aliye hai, lililo nguzo na msingi wa kweli.
”Roho asema waziwazi kwamba katika siku za mwisho baadhi ya watu wataiacha imani na kufuata roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani.
”Kama ukiwakumbusha ndugu mambo haya, utakuwa mtumishi mwema wa Kristo Yesu, uliyelelewa katika kweli ya imani na yale mafundisho mazuri uliyoyafuata.
”Fanya bidii kusoma Maandiko hadharani, kuhubiri na kufundisha, mpaka nitakapokuja.
”Jilinde sana nafsi yako na mafundisho yako. Dumu katika hayo, kwa maana kwa kufanya hivyo utajiokoa wewe mwenyewe pamoja na wale wanaokusikia.
”Kwa hiyo usione haya kushuhudia kuhusu Bwana wetu, wala usinionee haya mimi niliye mfungwa kwa ajili yake. Bali uishiriki pamoja nami taabu ya Injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu,
”Kama tukistahimili, pia tutatawala pamoja naye. Kama tukimkana yeye, naye atatukana sisi.
”Jitahidi kujionyesha kwa Mungu kuwa umekubaliwa naye, mtenda kazi asiye na sababu ya kuona aibu, ukilitumia kwa usahihi neno la kweli.
”Tena haimpasi mtumishi wa Bwana kuwa mgomvi, bali inampasa awe mwema kwa kila mtu, awezaye kufundisha, tena mvumilivu. Inampasa kuwaonya kwa upole wale wanaopingana naye, kwa matumaini kwamba Mungu atawajalia kutubu na kuijua kweli,
”Wakijifunza siku zote lakini kamwe wasiweze kufikia ujuzi wa kweli.
”na jinsi ambavyo tangu utoto umeyajua Maandiko matakatifu, ambayo yanaweza kukuhekimisha upate wokovu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu. Kila Andiko limevuviwa na Mungu na lafaa kwa mafundisho, kwa kuwaonya watu makosa yao, kuwaongoza na kuwafundisha katika haki ili mtu wa Mungu awe amekamilishwa, ili apate kutenda kila kazi njema.
”Uhubiri Neno, uwe tayari wakati ufaao na wakati usiofaa, karipia, kemea na kuonya kwa uvumilivu wote na kwa mafundisho mazuri. Maana wakati utakuja watu watakapokataa kuyakubali mafundisho yenye uzima, badala yake, ili kutimiza tamaa zao wenyewe, watajikusanyia idadi kubwa ya walimu wapate kuwaambia yale ambayo masikio yao yanayowasha yanatamani kuyasikia. Watakataa kusikiliza kweli na kuzigeukia hadithi za uongo.
”Inampasa alishike kwa uthabiti lile neno la imani kama lilivyofundishwa, kusudi aweze kuwafundisha wengine kwa mafundisho manyofu na kuwakanusha wale wanaopingana nayo.
”Ushuhuda huu ni kweli. Kwa hiyo, uwakemee kwa ukali wapate kuwa wazima katika imani,
”Lakini kwa habari yako wewe, inakupasa kufundisha kulingana na mafundisho yenye uzima.
”Kwa hiyo, imetupasa kuwa waangalifu sana kuhusu kile tulichosikia, ili tusije tukakiacha. Kwa kuwa ujumbe ulionenwa na malaika ulikuwa imara na kila uasi na kutokutii kulipata adhabu ya haki, je, sisi tutapaje kupona kama tusipojali wokovu mkuu namna hii? Wokovu huu, ambao mwanzo ulitangazwa na Bwana, kisha ulithibitishwa kwetu na wale waliomsikia.
”Kwa hiyo, kama Roho Mtakatifu asemavyo: “Leo, kama mkiisikia sauti yake, msifanye mioyo yenu migumu, kama mlivyofanya katika uasi, wakati ule wa kujaribiwa jangwani, pale baba zenu waliponijaribu na kunipima ingawa kwa miaka arobaini walikuwa wameona matendo yangu. Hiyo ndiyo sababu nilikikasirikia kizazi kile, nami nikasema, ‘Siku zote mioyo yao hupotoka, nao hawajazijua njia zangu.’ Hivyo nikaapa kwa hasira yangu, ‘Kamwe hawataingia rahani mwangu.’ ” Ndugu zangu, angalieni, asiwepo miongoni mwenu mtu mwenye moyo mwovu usioamini, unaojitenga na Mungu aliye hai.
”Kwa maana sisi pia tumesikia Injili iliyohubiriwa kwetu, kama nao walivyosikia, lakini ujumbe ule waliousikia haukuwa na maana kwao, kwa sababu wale waliousikia hawakuuchanganya na imani. Sasa sisi ambao tumeamini tunaingia katika ile raha, kama vile Mungu alivyosema, “Hivyo natangaza kwa kiapo katika hasira yangu, ‘Kamwe hawataingia rahani mwangu.’ ” Lakini kazi yake ilikamilika tangu kuumbwa kwa ulimwengu.
”Kwa maana Neno la Mungu li hai tena lina nguvu tena lina makali kuliko upanga uwao wote wenye makali kuwili, tena linachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, viungo na mafuta yaliyo ndani yake, tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. Wala hakuna kiumbe cho chote kilichofichika machoni pa Mungu. Kila kitu kimefunuliwa na kiko wazi machoni pake yeye ambaye kwake ni lazima tutatoa hesabu.
”Kwa kuwa ni vigumu kuwarejeza tena katika toba wale ambao wakati fulani walishapata nuru, ambao walishaonja kipawa cha mbinguni, ambao wamekwisha kushiriki katika Roho Mtakatifu, wale ambao wameonja uzuri wa Neno la Mungu na nguvu za wakati ujao, kisha wakaanguka, kwa kuwa kwa nafsi zao wanamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili na kumdhalilisha hadharani.
”Baada ya siku zile, hili ndilo Agano nitakalofanya na nyumba ya Israeli, asema Bwana. Nitaweka sheria zangu katika nia zao na kuziandika katika mioyo yao. Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
”“Hili ndilo Agano nitakalofanya nao baada ya siku hizo, asema Bwana. Nitaziweka sheria zangu mioyoni mwao, na kuziandika katika nia zao.”
”Kama tukiendelea kutenda dhambi kwa makusudi baada ya kupokea ufahamu wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi. Lakini kinachobaki ni kungoja kwa hofu hukumu ya moto uwakao utakaowaangamiza adui za Mungu. Ye yote aliyeikataa sheria ya Mose alikufa pasipo huruma kwa ushahidi wa watu wawili au watatu. Je, mnadhani ni adhabu kali kiasi gani anayostahili kupewa mtu aliyemkanyaga Mwana wa Mungu chini ya nyayo zake, yeye aliyeifanya damu ya Agano iliyomtakasa kuwa kitu najisi na kumtendea maovu Roho wa neema?
”Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, kwa maana ye yote anayemjia Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko na ya kuwa huwapa thawabu wale wamtafutao kwa bidii.
”Angalieni, msije mkamkataa yeye anenaye. Ikiwa wao hawakuepuka adhabu walipomkataa yeye aliyewaonya hapa duniani, sisi je, tutaokokaje tusipomsikiliza yeye anayetuonya kutoka mbinguni?
”kwa kuwa “Mungu wetu ni moto ulao.”
”Kama mtu ye yote miongoni mwenu amepungukiwa na hekima na amwombe Mungu, yeye awapaye watu wote kwa ukarimu wala hana kinyongo, naye atapewa.
”Kwa hiyo, ondoleeni mbali uchafu wote na uovu ambao umezidi kuwa mwingi, mkalipokee kwa unyenyekevu lile Neno lililopandwa ndani yenu ambalo laweza kuokoa nafsi zenu. Basi iweni watendaji wa Neno wala msiwe wasikiaji tu, huku mkijidanganya nafsi zenu. Kwa maana kama mtu ni msikiaji tu wa Neno wala hatendi kile linachosema, yeye ni kama mtu ajitazamaye uso wake kwenye kioo na baada ya kujiona alivyo, huenda zake na mara husahau jinsi alivyo.
”Ninyi wanaume na wanawake wazinzi, hamjui ya kwamba urafiki na dunia ni uadui na Mungu? Kwa hiyo mtu ye yote anayetaka kuwa rafiki wa dunia hufanyika adui wa Mungu. Au mwadhani kwamba Andiko lasema bure kuwa, huyo Roho ambaye Mungu amemweka ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu? Lakini yeye hutupatia neema zaidi. Hii ndiyo sababu Andiko husema: “Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.” Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, ninyi wenye dhambi na kuisafisha mioyo yenu, ninyi wenye nia mbili. Huzunikeni, ombolezeni na kulia. Kicheko chenu na kigeuzwe kuwa kuomboleza na furaha yenu kuwa huzuni. Jinyenyekezeni mbele za Bwana, naye atawainua.
”Basi kwa kuwa mmejitakasa nafsi zenu kwa kuitii ile kweli kwa njia ya Roho kwa kuwapenda ndugu zenu kwa upendo wa kweli, pendaneni kwa dhati kutoka moyoni. Kwa maana mmezaliwa upya, si kwa mbegu ile iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika, kwa neno la Mungu lililo hai na linalodumu hata milele. Maana, “Watu wote ni kama majani, na utukufu wao ni kama ua la shambani; majani hunyauka na ua lake hupukutika, lakini neno la Mungu ladumu milele.” Hili ndilo neno lililohubiriwa kwenu.
”Kama watoto wachanga, waliozaliwa sasa, yatamanini maziwa ya kiroho yasiyochanganywa na kitu kingine cho chote, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu,
”Kwenu ninyi mnaoamini, yeye ni wa thamani. Lakini kwao wasioamini, “Jiwe lile walilolikataa waashi limekuwa Jiwe Kuu la pembeni,” tena, “Jiwe lenye kuwafanya watu wajikwae, mwamba wa kuwafanya waanguke.” Wanajikwaa kwa sababu hawakulitii lile neno: kama walivyowekewa tangu zamani.
”Kwa maana wakati umewadia wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu. Basi kama ikianza kwetu sisi, mwisho wa hao wasiotii Injili ya Mungu utakuwaje?
”Sisi wenyewe tuliisikia sauti hii ambayo ilitoka mbinguni, wakati tulipokuwa pamoja naye kwenye ule mlima mtakatifu. Nasi tunalo pia neno la hakika zaidi la unabii, ambalo mtafanya vyema mkiliangalia kwa bidii, kama vile nuru inayong'aa gizani, hadi kupambazuka na nyota ya asubuhi itokee mioyoni mwenu. Awali ya yote, yawapasa mjue kwamba hakuna unabii katika Maandiko uliofasiriwa kama alivyopenda nabii mwenyewe. Kwa maana unabii haukuja kamwe kwa mapenzi ya mwanadamu, bali watu walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
”Lakini pia waliinuka manabii wa uongo miongoni mwa watu, kama vile watakavyokuwako walimu wa uongo miongoni mwenu, ambao kwa siri, wataingiza mafundisho yasiyopatana na kweli hata kumkana Bwana wa pekee aliyewanunua na kujiletea juu yao maangamizi ya haraka. Hata hivyo, wengi watafuata njia zao za ufisadi ambao kwa ajili yao njia ya kweli itatukanwa. Nao katika tamaa zao mbaya, watajipatia faida kwenu kwa maneno ya madanganyo waliyotunga wenyewe. Lakini hukumu imekwisha kutangazwa dhidi yao tangu zamani, ambayo haikawii wala uangamivu wao haujalala usingizi.
”Huandika vivyo hivyo katika nyaraka zake zote akizungumzia ndani yake mambo haya. Katika nyaraka zake kuna mambo mengine ambayo ni vigumu kuyaelewa, ambayo watu wajinga na wasio thabiti huyapotosha kwa maangamizi yao wenyewe, kama wapotoshavyo pia Maandiko mengine. Basi, ninyi wapenzi, kwa kuwa mmekwisha kujua mambo haya, jilindeni msije mkachukuliwa na kosa la watu hao waasi na kuanguka kutoka kwenye uthabiti wenu.
”Basi katika hili twajua ya kuwa tumemjua kama tunazishika amri zake. Mtu ye yote asemaye kuwa, “Ninamjua” lakini hazishiki amri zake, ni mwongo, wala ndani ya mtu huyo hamna kweli. Lakini kama mtu ye yote analitii neno lake, upendo wa Mungu umekamilika ndani yake kweli kweli. Katika hili twajua kuwa tumo ndani yake. Ye yote anayesema anakaa ndani yake hana budi kuenenda kama Yesu alivyoenenda.
”Wapenzi, msiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho mwone kama zimetoka kwa Mungu, kwa sababu manabii wengi wa uongo wametokea ulimwenguni.
”Sisi twatokana na Mungu na ye yote anayemjua Mungu hutusikiliza, lakini asiyetokana na Mungu hatusikilizi. Hivi ndivyo tunavyoweza kutambua Roho wa Kweli na roho ya upotovu.
”Hivi ndivyo tunavyojua kwamba tunawapenda watoto wa Mungu, kwa kumpenda Mungu na kuzitii amri zake.
”Kila mtu amwaminiye Mwana wa Mungu anao huu ushuhuda moyoni mwake. Kila mtu asiyemwamini Mungu amemfanya yeye kuwa mwongo, kwa sababu hakuamini ushuhuda Mungu alioutoa kuhusu Mwanawe.
”Hili ndilo pendo, kwamba tuenende sawasawa na amri zake. Hii ndiyo amri yake kama vile mlivyosikia tangu mwanzo, kwamba mwenende katika upendo.
”Mtu ye yote asiyedumu katika mafundisho ya Kristo, bali akayaacha, yeye hana Mungu. Ye yote anayedumu katika mafundisho ana Baba na Mwana pia. Msimpokee mtu ye yote anayewajia ambaye hawaletei mafundisho haya, wala msimkaribishe nyumbani mwenu. Ye yote amkaribishaye mtu wa namna hiyo anashiriki katika matendo maovu ya mtu huyo.
”Ingawa mmekwisha kujua haya yote, nataka niwakumbushe kuwa Bwana akiisha kuwaokoa watu wake kutoka Misri, baadaye aliwaangamiza wale ambao hawakuamini.
”Katika mkono wake wa kuume alishikilia nyota saba na kinywani mwake ulitoka upanga wenye makali kuwili. Uso wake kama jua kali linalong'aa kwa nguvu zake zote.
”Nayajua matendo yako, bidii yako na saburi yako. Najua kuwa huwezi kuvumiliana na watu waovu na ya kwamba umewajaribu wale wanaojifanya kuwa mitume na kumbe sio, nawe umewatambua kuwa ni waongo.
”Basi tubuni! Ama sivyo, nitakuja kwako upesi na kupigana na watu hao kwa upanga wa kinywa changu.
”Hivyo kwa kuwa u uvuguvugu, kwamba wewe si baridi wala si moto, nitakutapika utoke kinywani mwangu. Kwa maana unasema: ‘Mimi ni tajiri, nimejilimbikizia mali, wala sihitaji kitu cho chote.’ Lakini hutambui ya kwamba wewe ni mnyonge, wa kuhurumiwa, maskini, kipofu, tena uliye uchi.
”Kisha lile joka likapatwa na hasira kali kwa ajili ya huyo mwanamke, likaondoka ili kupigana vita na watoto waliosalia wa huyo mwanamke, yaani, wale wanaozitii amri za Mungu na kuushika ushuhuda wa Yesu Kristo. Lile joka likasimama kwenye mchanga wa bahari.
”Kisha nikamwona malaika mwingine akiruka juu angani, naye alikuwa na Injili ya milele ya kuwatangazia wale waishio duniani, yaani, kwa kila taifa, kabila, lugha na jamaa. Akasema kwa sauti kubwa, “Mcheni Mungu na kumpa utukufu, kwa maana saa ya hukumu yake imewadia. Mwabuduni yeye aliyeziumba mbingu, dunia, bahari na chemchemi za maji.”
”Ni nani ambaye hatakuogopa wewe Bwana na kulitukuza jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako ndiwe mtakatifu. Mataifa yote yatakuja na kuabudu mbele zako, kwa kuwa matendo yako ya haki yamedhihirishwa.”
”Macho yake ni kama miali ya moto na juu ya kichwa chake kuna taji nyingi. Alikuwa na jina lililoandikwa ambalo hakuna mtu ye yote anayelijua isipokuwa yeye mwenyewe. Alikuwa amevaa joho lililochovywa kwenye damu na Jina lake ni “Neno la Mungu.”
”Kinywani mwake hutoka upanga mkali ambao kwa huo atayaangusha mataifa. “Atayatawala kwa fimbo yake ya utawala ya chuma.” Atalikanyaga shinikizo la mvinyo wa ghadhabu ya Mungu Mwenyezi.
”Wale waliosalia waliuawa kwa upanga uliotoka kinywani mwa yule aliyekuwa amempanda huyo farasi mweupe, nao ndege wote wakajishibisha kwa nyama yao.
”Namwonya kila mtu asikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki: Mtu ye yote akiongeza humo cho chote, Mungu atamwongezea mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. Kama mtu ye yote akipunguza humo cho chote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.
”